Aliyoyasema Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wakati Akipokea Gawio la Serikali Kutoka Kampuni ya Twiga Minerals na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Tarehe 13 oktoba, 2020

Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta, Dar es salaam.

# Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kuweza kutukutanisha katika tukio hili muhimu la Serikali kukabidhiwa gawio kutoka Kampuni ya Twiga Minerals na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

# Ndugu zangu Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa madini, ikiwa ni pamoja na Dhahabu, Almasi, Shaba, Chuma, Makaa ya mawe, Uranium, Chumvi, Rubi, Helium, Tin, Titanium, Tangstan nk.

Viongozi kutoka kampuni ya Twiga Minerals kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philipo Mpango (wa pili toka kushoto) wakati wa hafla ya kupokea gawio toka kampuni hiyo Oktoba 13,2020 Jijini Dar es salaam.

# Karibu madini yote yaliyopo duniani, asilimia kubwa  utayakuta Tanzania.

# Pia tuna gesi, Ethanol, Methanol, Noble gas/stable gas(helium) madini yanayopatikana nchi tatu tu duniani na Tanzania yapo.

# Kuna dalili ya uwepo wa mafuta na sasa utafiti unafanywa katika mbuga za Wembele ambako kuna dalili zote zinazoonesha uwepo wa mafuta pamoja na maeneo ya Zanzibar.

# Hiyo ndiyo Tanzania, kwa hiyo Tanzania utajiri tunao.

# Pia Tanzania tumebarikiwa  kuwa na madini ya thamani ambayo yanapatikana Tanzania pekee, madini ya Tanzanite

# Ndugu  zangu zimefanyika juhudi mbalimbali katika kusimamia rasilimali zilizoko nchini.

# Sote tunakumbuka marekebisho ya Sheria ya Madini yaliyofanyika mwaka 2017, na kutungwa Sheria mbili mpya yaani Sheria ya utajiri wa Rasilimali ya 2017 na Sheria ya majadiliano ya Masharti hasi ya mikataba ya mwaka 2017.

#  Matokeo ya majadiliano hayo ni pamoja na kuanzishwa kwa kampuni ya 

Kampuni ya Twiga Minerals.

#  Matokeo ya sheria hizo ni pamoja na Serikali kuwa na umiliki wa asilimia 16 na kampuni ya Barrick kumiliki asilimia 84 kwa kila uwekezaji wa migodi ya uchimbaji mkubwa wa madini.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) John Bina akizungumza na wadau wa Madini kwenye hafla ya Serikali kupokea gawio Jijini Dar es salaam Oktoba 13,2020

# Aidha, tulikubaliana kuwa faida itakayokuwa ikipatikana kutokana na uwekezaji huo serikali na kampuni ya Barrick watagawana 50/50.

# Hii ndiyo sababu leo hii tupo hapa kushuhudia gawio hili ambalo ni matunda ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali yetu ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na hisa ya asilimia 16 katika Kampuni za Uchimbaji Mkubwa wa Madini

# Napenda kuwashukuru Barrick kwa kukubali kufanya.mazungumzo na serikali yaliyochukua takribani miaka 2

# Wapo watu waliobeza sana juhudi hizi za Serikali hawakujua serikali inataka nini? Gawio hili la shilingi bilioni 100 litapeleka watoto wetu kusoma elimu bure, tutanunua madawa, tutatengeneza barabara, tutatengeneza na kujenga hospitali zetu, tutatoa huduma za kila aina kwa watanzania na ndio maana nasema Barrick asante sana

# Naomba mfikishe ujumbe kwa viongozi wenu kwamba makubaliano haya yanaleta impact kwa Watanzania wa hali ya chini.

# Naishukuru timu ya mazungumzo chini ya Prof.  Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya nje kwa kazi kubwa waliyoifanya na kufikia maamuzi haya mazuri.

# Makubaliano yaliyofikia yametokana na ujasiri wa team hii iliyokuwa ikijadiliana na Barrick maana haikuwa kazi rahisi.

This image has an empty alt attribute; its file name is 222.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza wakati wa hafla ya kupokea gawio toka kampuni ya Twiga Minerals na STAMICO iliyofanyika Oktoba 13,2020 Jijini Dar es salaam.

# Ninaomba Mkurugenzi Mkuu na wawakilishi kutoka Twiga Minerals mrudi mkafanye mahesabu vizuri najua kuna fedha huko mkazilete mkishirikiana na Wizara ya fedha ili kuleta ziweze kutumika kuboresha maisha ya wanyonge

# Ndugu zangu, pamoja na kufanya mazungumzo na Barrick tumeimarisha Shirika letu la Taifa la Madini (STAMICO) lililoanzishwa mwaka 1972 linajiendesha kwa faida tumebadilisha Sheria. Shirika la Taifa la Madini (Stamico) tangu lianzishwe lilikuwa linasuasua na kwenye mwaka 1997 ilikuwa lifutwe kutokana na kutokuwa na faida.

#Shirika limewezeshwa kuwa na mitambo ya kisasa ya kufanya uchorongaji ili kubaini uwepo wa madini na hivi karibuni tumenunua mitambo mingine mitatu yenye teknolojia ya kisasa zaidi iliyogharimu takribani Shilingi bilioni 5.347 na kulifanya Shirika liwe na jumla ya mitambo 7 ya uchorongaji

# Kwa mara ya kwanza kupitia migodi yao ya Kabulo Kiwira na Buhema Stamico imeweza kutoa gawio la shilingi bilioni 1.1

# Stamico kwa sasa inakamilisha ujenzi wa kusafisha dhahabu (gold refinery)

# Hii ndiyo Tanzania ninayotaka kuiona, Tanzania ya matajiri na ndio maana natoa wito kwa wote oportunity ni yetu, mambo ya kujifichaficha yamepitwa na wakati  pata leseni iwe ni halali nenda ukachimbe nitafurahi nikienda mikoani nakuta mgodi wa Kakobe nk. Hakuna ubaya.

# Tanzania pawe ni mahali pa kutengeneza pesa kwasababu Mungu ametupa mali cha kuzingatia ni hizo pesa kuleta manufaa kwa watanzania na hivyo ndio tutakuwa tunaijenga nchi yetu

# Tumeimarisha Taasisi yetu ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na hivyo kuweza kufanikisha kupata ithibati ya kimataifa ya uchunguzi wa madini ya uchunguzi wa sampuli za dhahabu kwa njia ya tanuru yenye namba SIO1725 ya mwezi Oktoba, 2019j

# Tumeboresha mazingira ya biashara ya madini kwa kuanzisha masoko 37 na vituo vidogo 38 vya uuzaji madini katika maeneo yenye madini nchini, nawapa hongera sana Wizara na Wakuu wa Mikoa yote nchini

# Pia tutafungua bandari ya Kalema, sababu kuna dhahabu nyingi, na sisi tutapokea dhahabu kutoka nje ili zije ziuzwe hapa.

# Ukiritimba unatuchelewesha, nakuagiza Waziri wa Madini kutatua matatizo yaliyopo kigoma.

Sehemu ya Wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere katika hafla ya Serikali kupokea gawio toka kwa kampuni ya Twiga Minerals na STAMICO iliyofanyika Oktoba 13, Jijini Dar es salaam

# Tumeendelea kuboresha mazingira ya wachimbaji wadogo wa madini na Jumla ya maeneo 23 yalitengwa na kugawiwa kwa wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali nchini ambapo jumla ya leseni 801 zilitolewa.

#Tumeongeza makusanyo yatokanayo na Sekta ya Madini kutoka bilioni 194 mwaka 2015/2016 hadi bilioni 528 mwaka 2019/2020, kazi nzuri kwa Tume ya Madini na usimamizi wa Wizara ya Madini.

# Tumeimarisha udhibiti wa utoroshaji wa madini ikiwa ni pamoja na kujenga ukuta wa Mirerani na sasa mchango wa madini ya Tanzanite umeongezeka kutoka shilingi milioni 238 kwa miaka miwili ya 2016 na 2017 kabla ya kujenga ukuta hadi shilingi bilioni 3.587 kwa miaka miwili ya 2018 na 2019 baada ya kujengwa kwa ukuta.

# Aidha, nyote ni mashahidi kuwa tumeanza kupata mabilionea watanzania ambao ni wachimbaji wadogo kwa mfano  Saniniu Laizer.

#Tumefuta baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa kero kwa wachimbaji wadogo yaani Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kodi ya zuio (Witholding tax) ambazo zina jumla ya asilimia 23 na kubakiza mrabaha, ada ya ukaguzi na tozo ya ushuru wa huduma (Service levy) zenye jumla ya asilimia 7.3 tu. Aidha, tulifuta kodi na tozo zingine 11 kwa wazalishaji wa chumvi

# Taasisi zinazohusika na mazingira simamieni kampuni katika kusimamia ulipwaji wa rehabilitation bond kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link