Aliyoyasema Waziri wa Madini Doto Biteko wakati wa Hafla ya Upokeaji wa Gawio kwa Serikali Oktoba 13, 2020

Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta, Dar es salaam.

 # Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha hapa tukiwa na afya njema. Pia, nichukue nafasi hii kukushukuru kwa kutenga muda wako na kuja kuhudhuria katika hafla hii. Aidha, nakupongeza wewe binafsi na Serikali yako ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuwa mbeba maono na kutupa miongozo na maelekezo katika usimamizi wa Sekta ya Madini. Sekta ya madini imebadilika sana na aliyeifanya sekta hii kubadilika ni wewe Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wakati wa Hafla ya Upokeaji Gawio kwa Serikali Oktoba 13, 2020 iliyofanyika Jijini Dar es salaam.

# Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yaliyofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilifanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123 na kutunga Sheria mpya mbili: Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusu Usimamizi wa Maliasili na Raslimali za nchi na Sheria ya Raslimali na Maliasili za Nchi (Mapitio ya Mikataba yenye Vifungu Kandamizi).

# Kufuatia marekebisho hayo ya sheria na usimamizi imara wa Sekta ya Madini, mafanikio mbalimbali yamepatikana. Mafanikio hayo ni pamoja na

# Kuongezeka kwa mapato ya Serikali kutoka shilingi bilioni 168 Mwaka wa Fedha 2014/15, hadi shilingi bilioni 528 kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

# Wizara ilifanikiwa kuvuka lengo la makusanyo la Shilingi bilioni 470 la Mwaka wa Fedha 2019/2020 zilizopangwa na Serikali na kuweza kukusanya Shilingi bilioni 528.24 sawa na asilimia 112.4.

# Kufuatia Sheria ya Local Content, Tumeshuhudia kuwa, huduma zote zinazopatikana nchini zimeendelea kununuliwa hapahapa nchini ikiwa ni pamoja na vyakula, vipuli, huduma za kibenki na masoko ya hisa, jambo hili linasaidia kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza wakati wa upokeaji gawio katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es salaam Oktoba 13, 2020.

# Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo ili wanufaike zaidi na madini yao kwa kutenga maeneo mengi zaidi na kuendelea kuweka mazingira bora ya biashara yao..

#Mchango wa Sekta kwenye Pato la Taifa (GDP) umeendelea kuongezeka kutoka 4.3 Mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 Mwaka 2019. Lengo la Serikali ni kufikia asilimia 10 Mwaka 2025.

# Wizara ya Madini kama msimamizi mkuu wa dira hiyo tutatekeleza kwa vitendo mipango mizuri tuliyojiwekea pamoja na maelekezo yako mazuri.

# Usimamizi wa sekta umeimarishwa hasa kuzuia vitendo vya utoroshaji madini kwenda nje ya nchi pamoja na kuweka mazingira mazuri na bora kwa wafanyabiashara wote wadogo na wakubwa kwa kufungua ofisi katika kila mkoa na kuweka afisa ambaye ataangalia maslahi ya Serikali katika kila mgodi mkubwa, mgodi wa kati pamoja na mipaka yote ikiwemo Viwanja vya ndege na bandari.

# Tumeendelea kusisitiza ujenzi wa viwanda vya kuyeyusha na kusafisha madini hapa nchini. Lengo ni kuhakikisha kuwa, madini yote yanachakatwa hapa nchini ili kuongeza ajira na usimamizi wa rasilimali zetu.

# Hadi ninavyoongea, tumeshatoa leseni za uyeyushaji madini (smelter) tano na usafishaji madini (refinery) nne.

Picha ya baadhi ya washiriki katika hafla ya Serikali wa upokeaji gawio iliyofanyika Jijini Dar es salaam Oktoba 13,2020.

# Refinery kubwa na ya kisasa inaendelea kujengwa Jijini Mwanza na Kampuni ya Mwanza Precious Metals Refinery Company Limited chini ya STAMICO. Kiwanda hiki kinatarajiwa kuanza kazi ifikapo Desemba 2020.

# Kukamilika kwa kiwanda hicho kutaiwezesha  Serikali  kupata theluthi moja ya mrabaha kwa mfumo wa madini yaliyosafishwa badala ya fedha kama ilivyozoeleka hivyo kuifanya nchi kuwa na akiba ya dhahabu katika Benki Kuu.

# Kukamilika kwa ujenzi wa ukuta kuzunguka machimbo ya Tanzanite, pamoja na kuimarisha usimamizi, kuzuia utoroshaji, kuwapatia wachimbaji tathimini halisi na bei ya madini yao imepelekea upatikanaji wa madini ya Tanzanite kilogramu 20.7 yaliyo katika vipande 3 vyenye uzito mkubwa kuwahi kuripotiwa yenye thamani ya shilingi bilioni 12.6. Katika kipindi cha nyuma madini haya yangetoroshwa. 

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link