Aliyozungumza Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya Kuhusu Madini ya Nickel katika Kipindi cha Morning Trumpet cha Azam Tv Tarehe 20 Januari, 2021

Mradi wa kuchimba Madini ya Nickeli upo Kaskazini Magharibi mwa Tanzania katika eneo la Kabanga lililopo Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Mradi huo  uligunduliwa kutokana na utafiti uliofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ifadhilli wa UNDP kuanzia Mwaka 1976 hadi 1979.

Utafiti huo ulibainisha  kuwepo kwa madini ya Nikeli katika mwamba unaoanzia eneo la  Msongati Burundi kufika hadi eneo la Kabanga nchini Tanzania. Eneo la Kabanga lilionekana kuwa na hifadhi na mkusanyiko mkubwa wa madini ya Nikeli na yenye ubora kuliko madini yote ya Nikeli yanayopatikana ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Eneo la Kabanga pia lina mkusanyiko wa madini ya Shaba (Cu), Cobalt (Co), Dhahabu (Ag) na Platinum.

Madini ya Nikeli yana matumizi mengi ikiwa ni pamoja na kutengeneza vyuma vya pua (Stainlless Steel Alloys), vyuma vya pua vingine vigumu zaidi vinavyotumika kwenye injini za ndege na maroketi, utengenezaji wa betri na vifaa vya kielektroniko pamoja na kupakwa kwenye vifaa mbalimbali ili kuviimarisha na kuvizuia kupata kutu.

Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengine yenye madini ya Nikeli. Maeneo hayo ni pamoja na Wanangola, Zanzui na Nyakisasa katika Wilaya ya Kahama; Kapalagulu, Mto Wakemba, Tambwa na Mto malambo Mkoani Kigoma.

Pia katika maeneo ya Ntaka Hill Nachingwea Lindi, Dutwa Simiyu na Haneti Dodoma.

Kampuni mbalimbali zimeendesha tafiti eneo la Kabanga ili kubaini na kuthibitisha kuwa madini hayo yanaweza kuchimbwa kibiashara.

Kampuni ya LZ Nickel Limited (LZL) ilijitokeza kuanzisha mazungumzo na Serikali Mwezi Agosti, 2020. LZL ni kampuni iliyosajiliwa Uingereza lakini yenye wamiliki kutoka nchi za Uingereza, Marekani na Australia

Ili kuingia katika mazungumzo hayo Serikali ilitoa masharti ya msingi ambayo utekelezaji wake uwe ndiyo masharti ya kuwezesha mazungumzo kuendelea.

LZN ilikubaliana na masharti ya msingi ya Serikali na hivyo  kuwezesha kuanza kwa majadiliano kuhusu uendelezaji uchimbaji wa madini ya Nikeli na uanzishwaji wa kiwanda cha usafishaji/uchenjuaji kitakachojengwa katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

Timu ya Serikali  ya Majadiliano kwa kushirikiana na Timu ya LZN tayari imekamilisha Usajili wa Kampuni ya ubia ya Tembo Nickel Corporation Limited, na Usajili wa kampuni tanzu ya Tembo Nickel  Refining Company Limited

Mradi wa Nikeli unategemewa kuinufaisha nchi kwa namna mbalimbali ikiwemo  Kuanzisha na kuendeleza uchimbaji wa madini ya Nikeli na madini mwambata (Cu, Co, PGM, na Au) nchini na kukuza ya madini hayo

Kufanikisha uanzishwaji wa vinu vya kuchenjua madini ya metali mbalimbali hadi kufikia viwango vya mwisho.

Kuendeleza biashara, uchumi, na maisha bora kwa wilaya ya Kahama na wananchi kwa ujumla

Kuanza kwa matumizi mbadala ya miundombinu iliyokuwa inatumika kwenye kuendeshea mgodi

Ongezeko la ajira (migodini na kwenye mitambo ya uchenjuaji madini)

Ongezeko la mapato ya Serikali na wananchi kwa ujumla.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA MADINI

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link