Posts by madini

Jarida la Nchi Yetu: Tolea Maalum la Wizara ya Madini, Mei 2019

Uongozi wa Wizara ya Madini unampongeza kwa dhati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali anayoiongoza, ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ameimarisha na kusisitizia usimamizi wa rasilimali za Taifa hususani madini ili kunufaisha Taifa kwa ujumla.

Katika kipindi cha uongozi wake, Wizara imefanikiwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini, Miongozo na Kanuni za Sekta ya Madini ili kuhakikisha rasilimali hii inawanufaisha Watanzania na kuongeza mapato ya Serikali na kuongeza ukusanyaji wa maduhuli na hii imeonesha wazi nia ya Wizara ya Madini kutekeleza kwa vitendo maono ya Mhe. Rais kuwa “Rasilimali ya Madini Iwanufaishe Watanzania.”

Tunawiwa kwa namna ulivyosaidia sisi kufika hapa. Hatuna cha kukulipa isipokuwa kukuahidi kazi zaidi na uadilifu zaidi. Na kwa sababu hiyo basi, tunalitoa toleo hili maalum kuwa ni shukrani kwako na tunakuombea afya njema na nguvu zaidi katika kuendelea kuliongoza Taifa letu.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Nafasi za kazi-Wakaguzi wasaidizi wa madini ujenzi na viwandani

UTANGULIZI

Tume ya Madini ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Madini yenye jukumu la kusimamia shughuli za Madini nchini. Lengo kuu la Tume ni kuboresha usimamizi na udhibiti katika ukaguzi wa uzalishaji na biashara ya madini. Pia,Tume ina jukumu la kuhakikisha Sera, Sheria, Kanuni na taratibu zinazoongoza shughuli za Madini zinafuatwa ipasavyo ili kuongeza pato la Taifa kutoka katika sekta ya Madini.

Baadhi ya majukumu ya Tume ya Madini:-

 1. Kusimamia na kuratibu kikamilifu utekelezaji wa sheria na kanuni za Madini;
 2. Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi biashara ya Madini ili kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye pato la Taifa;
 3. Kusimamia utafutaji na uchimbaji endelevu wa rasilimali madini;
 4. Kutoa, kusitisha na kufuta leseni pamoja na vibali kulingana na Sheria,Kanuni za Madini;
 5. Kuchambua na kuthaminisha madini yaliyozalishwa na migodi mikubwa ,ya kati na midogo ili kuwezesha ukusanyaji wa mrabaha stahiki;
 6. Kufuatilia na kuzuia utoroshaji /magendo ya madini, na ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na vyombo na Mamlaka nyingine husika za Serikali; na
 7. Kuandaa na kutoa bei elekezi za Madini mbalimbali kutokana na bei za soko za hapa nchini na za kimataifa.

NAFASI ZA KAZI

Tume ya Madini inawatangazia watanzania wote wenye sifa kuomba kazi za Mkataba, (Vibarua) katika Ofisi za Afisa Madini Wakazi katika Mikoa ifuatayo ili kujaza nafasi wazi: Mkoa wa Dares Salaam nafasi (4 ); Katavi nafasi (2); Geita nafasi (3); Dodoma nafasi (3); Kagera nafasi (2);Kahama nafasi (2); Kigoma nafasi (2); Kilimanjaro nafasi (3); Lindi nafasi (2); Mara nafasi (3); Manyara nafasi (2); Mbeya nafasi (2); Mirerani nafasi (3); Morogoro nafasi (2); Rukwa nafasi (3); Tanga ,nafasi (2), Tabora nafasi (2), Chunya nafasi (3); Singida nafasi (3); Simiyu nafasi (2); Shinyanga nafasi (2); Ruvuma nafasi (2); Mwanza nafasi (3); Mtwara nafasi (2); na Arusha nafasi (2).

Sifa za Mwombaji

i. Mwombaji awe amehitimu na kufaulu elimu ya kidato cha Nne; ii. Mwenye Cheti kutoka Chuo cha Madini; au

iii. Cheti cha uhasibu au ugavi kutoka chuo chochote kinachotambulika na Serikali; na

iv. Umri usiozidi miaka 45.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Hotuba ya Mhe. Doto Biteko (Mb.), Waziri wa Madini akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/20

UTANGULIZI

1.  Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, ambayo imechambua bajeti ya Wizara ya Madini, naomba sasa Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa Mwaka 2018/19 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake kwa Mwaka 2019/20.

2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuijalia nchi yetu amani na utulivu na kutuwezesha kushiriki katika mkutano huu wa 15 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, kwa unyenyekevu namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kwa mara ya kwanza nikiwa Waziri wa Madini na kwamba ni mara yangu ya kwanza kuwasilisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara.

3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nitumie fursa hii pia kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Madini, Wizara ambayo ikisimamiwa 2 vizuri na kuwa na ufanisi itatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Aidha, nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuipa kipaumbele Sekta hii ya Madini kwa miongozo, maelekezo na maagizo mbalimbali anayoyatoa. Napenda kumuahidi Mheshimiwa Rais, Bunge lako Tukufu pamoja na Watanzania wote kwamba mimi pamoja na viongozi wenzangu na wafanyakazi wote wa Wizara ya Madini tutafanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu mkubwa kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyotujalia ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na manufaa kwa Watanzania na kuchangia ipasavyo katika Pato la Taifa.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, azindua Soko la Madini Chunya

Na Greyson Mwase, Chunya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amezindua Soko la Madini Chunya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Wilaya ya Chunya kuhakikisha imekamilisha na kuzindua soko la madini ndani ya kipindi cha siku saba. Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 27 Aprili, 2019 wilayani Chunya katika mkutano wake na wachimbaji na wachenjuaji wa madini.

Uzinduzi huo ulishirikisha Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi,  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi, Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Anthony Tarimo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Migodi kutoka Wizara ya Madini, Ali Ali.

Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, wawakilishi wa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Msanjila alisema kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Akielezea mafanikio ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi  wa rasilimali za madini, Profesa Msanjila alisema kuwa,  ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wananufahika na rasilimali za madini, Serikali ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Nchi  Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili Namba 5 ya Mwaka 2017; Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Namba 6 ya mwaka 2017 pamoja na kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123.

Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa, kuwekwa kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 kutaondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.

Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila aliwataka  wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini  kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali  za Serikali katika kutekeleza majukumu  yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali  inayotolewa na Serikali.

Akielezea manufaa ya soko jipya la madini Chunya, Profesa Msanjila alisema soko litaziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa Soko la Madini Chunya kutawezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.

Profesa Msanjila aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa  vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa  vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

“Soko hili litaondoa  uwezekano wa wanunuzi  wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya  kuwa na madini wakati hawana, nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu” alisema Profesa Msanjila.

Katika hatua nyingine Profesa Msanjila aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Chunya, wafanyabiashara wa madini kwa kuhakikisha Soko la Madini Chunya limezinduliwa ndani ya muda uliopangwa.

Wakati huo huo akizungumzia hali ya uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa, hadi kufikia sasa masoko matano ya madini yameshafunguliwa katika mikoa ya Geita, Singida, Kahama, Arusha – Namanga na Chunya.

Aliongeza kuwa masoko mengine ya madini yanatarajiwa kufunguliwa kabla ya tarehe 05 Mei, 2019 ikiwa ni pamoja na Soko la Madini ya Dhahabu na Vito vya Thamani Ruvuma, Soko la Madini Shinyanga, Soko la Madini Dodoma na Soko la Madini Mbeya.

Profesa Kikula alitaja masoko mengine ambayo yanatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kuwa ni pamoja na Soko la Madini ya Bati (tin) na Soko la Madini ya Dhahabu Handeni.

Alisisitiza kuwa mikoa mingine ipo katika  hatua za mwisho kukamilisha vigezo mbalimbali vikiwemo vya kiusalama na miundombinu.

Read more

Biteko akutana na Viongozi Waandamizi wa Wizara na Tume ya Madini

Na Issa Mtuwa, Dodoma

Waziri wa madini Doto Biteko amewataka wafanyakazi wa wizara ya madini pamoja na taasisi zake kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao kwa wakati ili kufikia malengo ya wizara hiyo.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akisisitiza jambo wakati kikao cha kazi na viongo waandamizi wa wizara ya Madini na Tume ya Madini. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kulia kwake Katibu Mkuu wizara ya Madini Prof. Msanjila.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na viongozi waandamizi wa wizara ya madini na tume ya madini. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine amezungumzia juu utekelezaji wa maagizo anayoyatoa na usimamizi wa utekeleza wa maagizo yake. Ameongeza kuwa anawategemea sana viongozi hao na wafanyakazi wote katika kufanikisha kazi na malengo ya wizara hiyo.

Ametolea mfano wa maagizo aliyowahi kuyatoa ni pamoja na ufutwaji wa leseni zisizo hai ndani ya siku 7 na zingine siku 30 na lile linalo husu mgodi wa North Mara kuhusu utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi ambapo alitoa pia siku 30 kuhakikisha maji hayo yanadhibitiwa.

Amewaambia viongozi hao kuwa akishatoa maagizo, kazi ya kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo ni kazi yao. Amemshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wa Tume Prof. Idris Kikula na tume yake kwa kazi nzuri wanayoifanya na ziara zake mikoani zimekuwa na tija.

Biteko amesisitiza kuwa anatambua mchango wa watumishi wote wa wizara yake hivyo amewaomba kuongeza bidii  na kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakizingatia weledi na uadilifu.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na Makamishna. Kwa upande wa tume ya madini waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume Prof. Kikula, Mtendaji mkuu wa tume ya madini Prof. Shukrani Manya, Mkurugenzi wa Leseni Mhandisi Yahya Samamba, Mkurugenzi wa Biashara Dkt. Venance Bahati.

Read more

Nyongo kupokea ujumbe wa watu kumi kutoka China

Nuru Mwasampeta na Tito Mselem

Naibu Waziri wa Madini, Stansilaus Nyongo jana tarehe 28 April, 2019 amepokea ujumbe ulioongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China waliofika kwa ajili ya kujadili maeneo ya kushirikiana katika sekta ya madini baina ya nchi hizo mbili yaani Tanzania na China.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha majadiliano baina ya nchi hizo mbili, Nyongo aliwahakikishia wageni hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mazingira mazuri ya kuwekeza nchini kupitia sekta ya Madini na kuwataka kutosita kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea fursa zilizopo na kuwekeza nchini Tanzania.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (Mbele Kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili wa China Dkt, Zhong Ziran (Kulia) pamoja na wajumbe walioambatana nao katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere Jana.

Nyongo amewadhihirishia wageni hao uwepo wa sera na sheria  zisizokandamiza upande wowote baina ya wawekezaji, wananchi na Serikali na hivo kuzifanya pande zote kunufaika na rasilimali na uwekezaji unaofanyika katika sekta ya madini.

Aidha, Nyongo amebainisha kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China ni wa muda mrefu ikiwa ni takribani miaka 50 na kufika kwa ujumbe huo kunabainisha wazi kuwa  urafiki na ukaribu baina ya nchi hizo hauna mashaka.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya mkutano huo, Nyongo alisema wataalamu kutoka China wamekuja kuunganisha nguvu ya pamoja na watanzania ili kuweza kusaidiana katika kufanya tafiti za kina katika kujua kiasi cha madini yaliyopo, namna nzuri ya kuvuna madini hayo pamoja na namna ya kuyaongezea thamani madini yaliyopo nchini kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.

Pia, Nyongo amebainisha kuwa China ipo tayari kuleta wataalamu katika masuala ya madini watakaojikita katika kufanya shughuli za uchimbaji wa madini.

Naibu Waziri Nyongo amebainisha kuwa ujio wa ujumbe kutoka China utasaidia kuweka makubaliano ya pamoja baina ya Taasisi ya Utafiti na Jiolojia Tanzania na Taasisi ya Jiolojia na utafiti ya nchini China katika kusimamia masuala ya utafiti wa madini katika maeneo ambayo hayajafikiwa.

Zaidi ya hayo Nyongo amewadhihirishia wageni hao uwepo wa mazingira mazuri na rafiki ya uwekezaji yanayotokana na uwepo wa sera na sheria zisizokandamiza upande wowote baina ya wawekezaji na Serikali na kuwataka kutosita kuja kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti na Jiolojia nchini Bi Yourghbert Myumbilwa amesema ushirikiano huo utaleta manufaa makubwa kwani uzoefu wa China katika masuala ya utafiti ni mkubwa hivyo itawawezesha watumishi wa taasisi hiyo kupata uelewa mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.

Akizungumzia ujio wa ujumbe wake nchini, Naibu Waziri wa Maliasili wa China Dkt. Zhong Ziran amesema ni kuweza kujadili na kukubaliana juu ya maeneo ya kushirikiana baina ya Tanzania na China kupitia maliasili madini inayopatikana nchini.

Ushirikiano huu baina ya Taasisi ya Utafiti na Jiolojia nchini na Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia nchini China ni matokeo ya kikao kilichofanyika mwezi Desemba, 2018 baina ya aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki na Waziri wa Maliasili wa China kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Maliasili nchini China ambapo Mhe. Kairuki alishiriki kongamano la uwekezaji lililofanyika  nchini humo na kuibua fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini.

Read more

Wachimbaji watelekeza Madini na pikipiki kukimbia msafara wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

Na Issa Mtuwa, Gairo

Wachimbaji wa Madini ya Rubi wilaya ya Gairo kata ya Iyombe kijiji cha Kirama, wamekimbia na kutelekeza Madini ya viwandani aina ya Rubi Nut, Pikipiki na vifaa mbalimbali vya kuchimbia baada ya kuona msafara wa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambae pia ni Mkuu wa Wilaya (DC) ya Gairo Seriel Shaid Mchembe waliokuwa wanatembelea mgodi huo kuona shuguli za uchimbaji kwa lengo la kwenda kutatua kero zinazowakabili.

Msafara wa Tume ya Madini na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwa kwenye eneo la mgodi Kijiji cha Kirama walipotembelea kukagua shuguli za uchimbaji katika eneo hilo wa mbele ni Athumani anae uongoza msafara kwenda kuonyesha anapochimba Sadick Athuan baada ya kukimbia

Msafara wa mwenyekiti wa Tume ya madini akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Machiyeke na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ulianza majira ya saa tatu asubuhi kuelekea  kwenye eneo la mgodi.

Wakiwa njiani msafara huo ulikubwa na changamoto baada ya gari ya Polisi iliyokuwa inaongoza msafara huo kukwama kwenye maji katikati ya mto kwa muda wa saa moja kitendo kilichopelekea kuchelewa kufika kwenye eneo la mgodi.

Hata hivyo mara baada ya kufika kwenye nyumba ya mchimbaji mmoja alie tambuliwa kwa jina la Sadick Athuman maarufa kwa jina la (Saadam) alikutwa kijana mmoja aliejitambulisha kwa jina la Athumani mkazi wa Gairo mjini akilinda mahali apo ndipo mkuu wa Wilaya na vyombo vyake vya ulinzi na Mwenyekiti wa Tume na Kamishna waliingia ndani na kufanya msako na kukuta madini aina ya Rubi Nut yakiwa kwenye mifuko, Pikipiki moja na vifaa mbalimbali vya kuchimbia.

Alipo ulizwa bwana Athumani, nani anae miliki madini hayo, alisema ni madini ya bwana Saadam. Alipo ulizwa yeye anafanya nini alisema yeye ni kibarua tuu na mwenyewe Saadam yupo mgodini anaendelea na uchimbaji ndipo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akamuamuru Athumani kwenda nae mpaka anakochimba bwana Saadam na mara baada ya kufika eneo la mgodi wachimbaji wote wakakimbia na kuelekea vichakani akiwemo bwa Saadam huku vifaa vya uchimbaji vikiwa vimetelekezwa sambamba na madini yale ya kwenye mfuko na pikipiki.

Kufuatia kitendo hicho mwenyekiti wa tume ya Madini Prof. Kikula amesikitishwa na kitendo hicho ambacho kinaashiria uchimbaji wa mgodi huo unafanyika bila kufuata sheria.

Kutokana na hali hiyoo, mwenyekiti wa tume amemuagiza afisa Madini Mkazi mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija kufuatilia uhalali wa eneo hilo (Leseni na Codinates) na mwenendo mzima wa uchimbaji wake, endapo eneo hilo litakuwa na leseni mmiliki wake alipe maduhuli yote anayotakiwa kulipa tangu alipoanza na kama eneo hilo halijakatiwa leseni mgodi huo ufungwe mara moja na shuguli za uchimbaji zisitishwe mara moja.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Kikula wa pili kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya gairo ikiongozwa na mwenyekiti wake Siriel Shaid Mchembe wa tatu kushoto na wa kwanza kulia ni Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke wakionyesha baadhi ya vifaa ikiwemo pikipiki iliyo telekezwa na mchimbaji wa madini Sadick Athuman maarufu kwa jina la Saadam alie kimbia baada ya kuona msafara wa tume ya Madini.

Aidha, amesikitishwa na wachimbaji na wawekezaji katika eneo hilo kushindwa kusaidia shuguli za maendelo ya kijiji kinacho zunguka migodi hiyo ambapo ofisi yake haikumridhisha mwenyekiti wa tume.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Gairo amesikitishwa na wachimbaji hao kwa kukiuka sheria zinazo ongoza shuguli za uchimbaji madini, amesema amekuwa akiwahimizi mara kadhaa wachimbaji wote wilayani humo kuzingatia na kufuata taratibu kabla hawajanza kazi za uchimbaji ikiwemo kukata leseni na kulipa maduhuli ya serikali.

Kufuatia kwa tukio hilo Mchembe amepiga marufuku kwa mtu yeyote katika wilaya ya Gairo kufanya shuguli za madini bila kuwa na kibali kutoka tume ya madini.

Wakati huo huo Mchembe amemuagiza Kamanda wa Polisi wilaya ya Gairo Lugano Piter Mwakisunga kuhakikisha anamkamata Sadick Athumani ndani ya siku saba na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Wakiwa kwenye mgodi wa eneo la mwekezaji wa kampuni ya Mofar Holdings (T) Ltd Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Machiyeke amemsisitiza mwekezaji huyo kuzingatia taratibu na sheria katika hatua ya kuajiri wafanyakazi na vibarua na manunuzi ya bidhaa kama muongozo unavyo sema.

Dkt. Machiyeke amesema, sheria inasisitiza kutoa kipaumbele kwa wananchi waozunguka mgodi na taifa kwa nafasi kubwa kabla ya kufikiria nje ya eneo hilo na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini na Kamishna walikuwa wanahitimisha ziara yao ya siku tano katika mkoa wa Morogoro baada ya kutembelea wilaya ya Morogoro mjini, Ulanga, Mvomero na Gairo ambapo ujumbe wake mkubwa kwa wafanyakazi wa tume na wachimbaji madini ulikuwa ni uadilifu katika kazi zaona kuepuka rushwa

Read more

Tunataka kurahisisha mazingira biashara ya madini-Biteko

 • Naibu Waziri Nyongo ataka Soko la Madini Arusha kuanzishwa haraka

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema Serikali kupitia Wizara yake inalenga kurahisisha Mazingira ya Biashara ya Madini ikiwemo kuwalea wachimbaji na kuwataka wafanyabiashara na wachimbaji kuhakikisha wanajisimamia wenyewe kwa manufaa yao na Taifa.

Waziri wa Madini Doto Biteko na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel wakati akizungumza jambo katika kikao hicho. Wengine wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini David Mulabwa na mmoja wa wajumbe wa chama hicho, Abe Latif.

Waziri Biteko ameyasema hayo alipokutana na viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Sam Mollel ofisini kwake jijini Dodoma Aprili 10, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu biashara ya madini nchini.

Amekitaka chama hicho kuendelea kushirikiana na wizara kwa lengo la kusukuma mbele Sekta ya Madini ikiwemo kuhakikisha biashara ya madini inafanyika katika mazingira yenye kuzinufaisha pande zote na kuwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanachama wao wanafuata taratibu wanapofanya biashara ya madini.

Awali, kabla ya kujibu hoja zilizowasilishwa na chama hicho, Waziri Biteko amekipongeza  chama  hicho kwa kuwa kimekuwa kikitoa njia mbadala pindi kinapowasilisha changamoto na kero  zake badala ya kuishia kulalamika na kuongeza, “wizara inaona fahari kwa hilo na tunayachukulia kwa umuhimu maoni yenu,”.

Akizungumzia suala la kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya zuio ambayo imeondolewa kwenye uchimbaji mdogo, Waziri Biteko amekitaka Chama hicho kutoa nafasi kwa serikali kufuatilia suala hilo. Waziri Biteko ameleeza hilo kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel ambaye ameeleza kuwa, katika mkoa wa Arusha, kodi hiyo bado inatozwa licha ya serikali kuiondoa.

Aidha, Waziri Biteko ametolea ufafanuzi wa changamoto kadhaa zilizowasilishwa na Mwenyekiti Sam Mollel kwa niaba ya chama hicho ikiwemo. Kuhusu bei elekezi, Waziri Biteko  amesema wizara itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha suala hilo linakuwa shirikishi. Waziri Biteko amesema hilo baada ya TAMIDA kutoa pongezi kwa serikali kwa kutoa nafasi kwa wadau kukaa pamoja na serikali kujadili suala la bei elekezi ambapo Mwenyekiti huyo amemweleza Waziri Biteko kuwa, katika hilo, serikali na wadau wameanza vizuri.

Akitolea ufafanuzi kuhusu suala la kurejesha maonesho ya madini jijini Arusha, Waziri Biteko amesema suala la maonesho ya madini kufanyika arusha inawezekana lakini si kwa madini ya Tanzanite, na kuongeza kuwa, serikali imedhamiria kufanya shughuli zote zinazohusu madini hayo ndani ya ukuta unaozunguka machimbo ya mirerani lakini pia ikilenga kuubadilisha  mji wa  mirerani ufanane na madini hayo.

Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara ya Madini Tanzania (Tamida) wakifuatilia mkutano wao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko , Naibu Waziri na Viongozi wa Wizara.

Aidha, Waziri Biteko amezungumzia suala la kuongeza wataalam wa kuthamini madini ya Tanzanite Mirerani na kueleza kuwa, kutokana na unyeti na umuhimu wa suala hilo, tayari serikali imeanza kulifanyia kazi ili kuhakikisha inaongeza idadi ya wataalam kuwezesha shughuli za uthamini Mirerani, kufanyika kwa wakati. Ufafanuzi huo umetolewa baada ya Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel kuwasilisha changamoto ya kuwepo na  upungufu wa wataalam hao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza katika kikao hicho, ametaka kuanzishwa haraka kwa soko la Madini jijini Arusha na kueleza kuwa, kwa upande wa wizara itahakikisha inashirikiana na serikali ya mkoa kuhakikisha soko hilo linaanzishwa haraka. Naibu Waziri Nyongo amesema hayo akijibu hoja ya Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel ambaye ameleeza katika kikao hicho kuwa, Chama hicho kinaunga mkono Serikali kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini na kuitaka serikali ione umuhimu wa kuanzisha soko La madini la madini mkoani arusha kuwezesha biashara ya madini ya vito kufanyika kwa urahisi.

Kuhusu vibali vya Wataalam wa masuala ya ukataji na unga’rishaji wa madini kutoka nje ya nchi, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, ni kweli kwamba serikali inawahitaji wataalam hao kwa kuwa pia watawezesha kutoa ujuzi huo kwa wataalam wa ndani ili kuhamasisha viwanda vya ukataji madini na kuongeza, “ serikali inaangalia namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika kwa sababu pia tunataka watu wetu wanufaike na utaalam huo”,.

Pia, ameongeza kuwa, kutokana na kulichukulia suala la uongezaji thamani madini kwa umuhimu, inakitegemea kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kwa ajili ya kuzalisha wataalam na kukitaka chama hicho kusaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika kituo hicho kwa kuwa hivi sasa idadi bado ni ndogo.

Kikao hicho cha Waziri na TAMIDA ni cha kwanza tangu kuteuliwa kwa Waziri wa Madini Doto Biteko kuiongoza wizara husika.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Viongozi Waandamizi kutoka wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Read more

Agizo la Waziri halijadiliwi, ni kutekeleza–Prof. Kikula

Na Issa Mtuwa, Ulanga Morogoro

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewataka  Watumishi wa tume hiyo ofisi ya Morogoro na Ulanga kutambua kwamba agizo la Waziri linalowataka kufuta leseni zisizofuata utaratibu wa kisheria sio la kujadili bali ni kutekeleza.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa pili kushoto akiwa katika eneo la wachimbaji wadogo Ipanko wilayani Ulanga akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija alipotembelea kujionea namna shuguli za uchimbaji zinavyofanyika. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki.

Prof. Kikula ameyasema hayo Aprili 10, 2019 wilayani Ulanga wakati akizungumza na watumishi wa tume hiyo wakati wa ziara yake.

Taarifa iliyosomwa kwake na Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge Ulanga, Tandu Jilabi inaonyesha kuwa wilaya ya Ulanga ina leseni za wachimbaji wadogo 221 kati ya hizo ni leseni 9 tu ndio zinazofanya kazi huku leseni za uchimbaji wa kati zikiwa 5 na leseni za utafiti wa madini 13.

Kufuatia hali hiyo, Afisa Migodi Mkazi ofisi ya Mahenge ameiomba tume ya madini kufuta leseni zisizofanya kazi ili wapewe wenye uhitaji ili waweze kuziendeleza. Kufuatia ombi hilo, Mwenyekiti wa tume amesema jukumu la kuzifuta leseni hizo ni la kwake pamoja na Afisa Madini Mkazi Morogoro na halina mjadala kwakuwa muongozo wa utekeleza wa suala hilo ulishatolewa na waziri wa Madini.

“Suala la leseni zisizofanya kazi sio la kujadili, hili ni agizo la Waziri na kazi yetu ni kutekeleza na wenye kuzifuta ni ninyi, fuateni taratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria katika kuzifuta na sio kuzifuta lazima wote waliozishikilia leseni hizo kwa muda wote walipe fidia na wasipo fanya hivyo taratibu za kisheria zifuatwe kwani katika kipindi hicho chote serikali imekosa mapato yake. Kuanzia leo pitieni leseni zote na ifikapo Juni 30 mwaka huu leseni zote zisizo hai ziwe zimefutwa”, amesema Prof. Kikula.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa tume amekutana na kuzungumza mwakilishi wa mwekezaji wa kampuni ya TanzGraphite (T) Ltd ambae ni Meneja Uhusiano wa Jamii na kuzungumzia kuhusu mgogoro uliopo baina ya mwekezaji huyo na baadhi ya wananchi wanaotakiwa kufanyiwa tathimini ili kupisha shuguli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Prof. Kikula ameonyesha kusikitishwa na mgogoro huo ambao amesema ni wa muda mrefu sasa na unachelewesha maendeleo ya watu na kuikosesha serikali mapato.

Ameongeza kimsingi wananchi wanapaswa kuelewa kuwa “right surface” (haki ya kumiliki vitu vilivyo juu ya ardhi) inampa mwananchi haki  ya kulipwa fidia ya mali zilizo juu ya ardhi anayo miliki lakini watambue kuwa kuna “resource right” (haki ya kumiliki raslimali zilizo chini ya ardhi) ikiwemo madini ambayo mmiliki wake ni serikali, ndio maana inapohitaji raslimali hizo humuondoa na kumfidia mliliki wa mali za juu ya ardhi, hivyo wananchi wanapo ng’ang’ania wanatakiwa walitambue hilo.

Pia, amesema kuwa, kwa mpango ulioanishwa na mwekezaji huyo unaonyesha manufaa kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo (CSR) ambapo amebainisha kuwa mwekezaji ameahidi kuwalipa fidia, kuwajengea nyumba za kisasa wale wote walio ndani ya eneo.

Mambo mengine ni pamoja na kuwapatia chakula kwa muda wa miaka miwili wakiwa kwenye makazi mapya watakayo jengewa na kila kaya kusomesha mtoto mmoja kwenye vyuo vya veta na wakihitimu wataajiriwa na mgodi ili waweze kupata kipato cha kusaidia na kuendeleza kaya zao.

Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Macheyeki kushoto akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mara baada ya kuzunguka na kukagua eneo la wachimbaji lililopo Iponka eneo ambalo awali lilifungiwa kufanya shuguli za uchimbaji.

Pamoja na hayo, mwekezaji huyo amemweleza mwenyekiti wa tume kuwa tayari wameshakubaliana kujengaa kituo cha afya, matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule, kujenga shule na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali. Hata hivyo hakusita kuonyesha kusikitishwa kwake na watu wachache wanaogoma kuondoka kupisha shuguli za uchimbaji huku kila kitu ikiwemo mtaji wa shuguli hizo ukiwa tayari.

Katika mgogoro huo, kaya 347 zinatakiwa kuondoka kupisha mwekezaji huyo na kati ya hizo kaya 62 ndio zinazo goma kuondoka ili mwekezaji aanze kazi ya uchimbaji. Mwenyekiti amesikitishwa na hali hiyo na na kuuomba uongozi wa mkoa na wilaya kuzungumza na kaya hizo sambamba na Baba Askofu aliyeko ndani ya eneo hilo ili mradi huo uanze kwani ni wa muda mrefu na serikali inakosa mapato.

Amesema kwa sasa anaziachia juhudi za serikali ya mkoa na wilaya katika kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Mapema mwenyekiti alikutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya ambapo amemshukuru kwa ushirikiano anao utoa kwa viongozi na wafanyakazi wa tume ya madini wilaya ya Ulanga.

Amesisitiza suala la uadilifu kwa wafanyakazi wa tume na amesema hilo litakuwa jambo la kwanza kulisema kila aendapo sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.  Aidha, amesema kipimo kikubwa cha kila mkuu wa kituo cha tume ya madini kitakuwa ni ukusanyaji wa maduhuli ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 tume ilipangiwa kukusanya Bilioni 310 na mwaka wa fedha ujao tume imepangiwa kukusanya Bilioni 467.

Upande wake, Kamishna wa tume hiyo Dkt. Athanas Macheyeki amewakumbusha na kuwasisitiza watumishi wa tume na wachimbaji wa madini kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji na ulipaji wa tozo na stahiki zote za serikali kwa wakati.

Amesema kwa kufanya hivyo raslimali za madini zitakuwa na tija kwa taifa kama anavyo sisitiza Rais John Pombe Magufuli kuwa anataka raslimali za madini ziwanufaishe watanzania wote na namna za kuwanufaisha ni kulipa stahiki za serikali zinazo tokana na madini ili zikatumike kujenga uchumi wa taifa.

Prof. Kikula na Dkt. Macheyeki wanaendelea na ziara yao mkoani Morogoro kukagua shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali ambapo leo walitembelea eneo la wachimbaaji wadogo ipanko wilayani ulanga.

Read more

Kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Mwakitolyo Wananchi watakiwa kumpisha mwekezaji kuchimba dhahabu

Na Greyson Mwase, Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo kilichopo Wilayani Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga kumpisha mwekezaji  ambaye ni  mgodi wa uchimbaji wa kati wa madini ya dhahabu wa kampuni ya  Hanan Afro Asia Geo Engineering (T) Limited kutoka China  kuendelea na maandalizi ya uchimbaji wa madini ya dhahabu, kwa kuwa ndiye aliyewekeza katika kijiji husika kwa kufuata sheria na kanuni zake.

Kutoka kushoto mbele, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Jasinta Mboneko na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakinukuu kero mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo kilichopo Wilayani Shinyanga Vijijini mkoani Shinyanga (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.

Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo hilo mapema leo tarehe 03 Aprili, 2019 katika mkutano wake wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa wa Shinyanga yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Jasinta Mboneko, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Kamando, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba, Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa, wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa, kumekuwepo na mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo na mwekezaji kutoka nchini China ambaye ni  kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering Co. Limited ambapo malalamiko yaliwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Kahama Machi 10, 2018 ambapo alielezwa kuhusu unyanyasaji  uliofanywa wakati wa zoezi la uthamini na ulipaji wa fidia kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kupisha uanzishwaji wa mgodi wa uchimbaji wa kati wa madini ya dhahabu.

Aliendelea kusema kuwa katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli Machi 11, 2018 aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alitembelea eneo la Mwakitolyo linalolalamikiwa kwa lengo la kufanya mkutano na kusikiliza malalamiko ya wananchi ambapo baada ya kusikiliza malalamiko hayo aliahidi kwenda kufanyia kazi malalamiko yao na kuwapa mrejesho.

Aliendelea kueleza kuwa, iliundwa timu maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi kulingana na hadidu rejea iliyokuwa imepewa ambayo iliitaka timu kukutana na viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi wilaya, kuainisha majina ya wananchi waliolipwa na ambao hawajalipwa fidia, vigezo vilivyotumika wakati wa uthaminishaji na ulipaji wa fidia pamoja na mapendekezo mbalimbali.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo kilichopo Wilayani Shinyanga Vijijini mkoani Shinyanga akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.

Nyongo aliendelea kufafanua kuwa, mara baada ya timu kumaliza kazi yake, ilibainika kuwa mwekezaji alilipa kiasi cha shilingi bilioni 1.63  kama fidia kwa wananchi waliokuwa katika eneo husika hivyo zoezi kukamilika kwa asilimia 99.6.

Alisisitiza kuwa pamoja na wananchi takribani 375 kulipwa fidia bado ilionekana kuwa wananchi wengi waliolipwa fidia sio wanakijiji wa Mwakitolyo na kuongeza kuwa wananchi 40 tu ndio walioonekana wamiliki halali wa mashamba pamoja na makazi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliitaka Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kuharakisha upatikanaji wa maeneo mapya kwa ajili ya wanananchi 40 ambao ni wamiliki halali wa makazi na mashamba katika kijiji cha Mwakitolyo ili mwekezaji aweze kuanza shughuli za uchimbaji mara moja.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo alimtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering Co. Limited kuhakikisha anadumisha mahusiano na wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo na kumtaka kuhakikisha anashiriki katika uboreshaji wa huduma za jamii kama vile afya, elimu, barabara kama Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake inavyofafanua.

Wakati huo huo Nyongo aliwataka wananchi kumpa ushirikiano mwekezaji ili kufaidi matunda ya uwekezaji  kwenye kijiji chao ikiwa ni pamoja na ajira kwa wazawa, utoaji wa huduma za vyakula, biashara, huduma za jamii hivyo kupaisha uchumi wa kijiji hicho.

Aliendelea kusema kuwa, madini ni mali ya watanzania wote, hivyo baada ya uwekezaji kuanza kampuni hiyo italipa kodi mbalimbali kwenye halmashauri na Serikali kuu hivyo kuboresha sekta nyingine kama vile miundombinu, afya, elimu n.k.

Naye Mbunge wa Solwa, Ahmed Salum akizungumza katika mkutano huo mbali na kumpongeza Naibu Waziri Nyongo kwa kutatua mgogoro huo, aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii huku wakilinda amani ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering Co. Limited, Zhang Jiangho mbali na kuishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kutatua mgogoro huo  uliodumu kwa muda mrefu, aliahidi kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mwakitolyo kwa kuboresha  huduma za jamii na kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

Read more

Waziri Biteko awasimamisha kazi Maafisa Madini Ofisi ya Madini Chunya

Na Tito Mselem, Chunya 

Waziri wa Madini Doto Biteko amewasimamisha kazi Maafisa Madini wote wa Ofisi ya Madini Chunya Mkoani Mbeya na kuteua Wajiolojia watakaokaimu nafasi hizo wakati wizara ikitafuta Maafisa wengine waaminifu watakaofanya kazi hizo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kugundua wizi mkubwa wa madini ya dhahabu unaofanywa na maafisa hao wakishilikiana na wamiliki wa kampuni ya uchenjuaji wa dhahabu.

Baadhi ya Viongozi waandamizi wa Wizara ya Madini na Viongozi wengine wa Wilaya ya Chunya wakisikiliza maelezo ya namna wizi unavyofanyika katika mitambo ya kuchenjua dhahabu.

Akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo wadogo pamoja na wamiliki wa makampuni ya uchenjuaji wa dhahabu Waziri Biteko, amesema udanganyifu unaofanywa na Maafisa hao wa Madini pamoja wenye  kampuni hizo za uchenjuaji ni mkubwa na  hahuitaji msamaha hata kidogo.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana katika sekta hii ya Madini ninawapenda sana wachimbaji ila nasikitika sana kwa wachimbaji na wenye makampuni ya uchenjuaji kutokuwa waaminifu,” amesisitiza Waziri Biteko.

Ameongeza kuwa, Maafisa wa madini hao ndiyo wanaotoa mianya ya wizi wa dhahabu unaofanyika kwenye kampuni zaa uchenjuaji wa dhahabu  wilayani humo.

Aidha, katika ziara hiyo Biteko ameifunga kampuni ya   Ntorah Gold Company Ltd inayohusika na uchenjuaji wa dhahabu wilayani  humo baada ya kutoa taarifa za udanganyifu kwa serikali.

Pia, Waziri Biteko ameongeza kwamba, Wilaya ya  Chunya ndiyo sehemu pekee Tanzania inayoongoza kwa wizi wa dhahabu na kutoa taarifa za uongo za kampuni za uchenjuaji wa dhahabu ikifuatiwa na wilaya ya Kahama iliyopo Mkoani Shinyanga.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjla, amesema serikali imeondoa kodi zote kwa wachimbaji wadogo zilizokuwa zikilalamikiwa na wachimbaji pamoja na kampuni za uchenjuaji wa dhahabu lakini bado wizi unafanyika tena kwa kiwango kikubwa.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amikiri kwamba hana elimu ya madini hivyo imekuwa vigumu kwake kudhibiti wizi huo   lakini anaamini wizi na udanganyifu upo tena kwa kiwango kikubwa.

“kiukweli sina elimu ya madini hasa kwenye upande wa uchenjuaji wa dhahabu, naamini kuna wizi mkubwa wa madini haya ya dhahabu na taarifa zisizo na ukweli”amesema  Chalamila.

Read more

KfW IPEX-Bank Mandated for Epanko Graphite Project

Kibaran Resources Limited (ASX:KNL) is pleased to report that it has signed a new agreement with German KfW IPEX-Bank for debt funding of the Epanko Graphite Project.

The agreement reappoints KfW IPEX-Bank to arrange senior debt funding for the Epanko Graphite Project in Tanzania (“Epanko” or the “Project”) after a hiatus of 18 months, during which many discussions have been held with the Tanzanian Ministry of Minerals, Mining Commission and the Bank of Tanzania concerning the regulatory changes introduced in July 2017 that have impacted on mineral project debt financings in the country, and is a reflection of the improved investment outlook in Tanzania.

As recently reported (refer ASX announcement Tanzania and Germany to Forge Closer Economic Relationship on 26 March 2019) the mining investment climate in Tanzania continues to improve and there is increasing confidence among international banks that the remaining regulatory aspects impeding new mine financing arrangements will be satisfactorily resolved.

Epanko is development ready with the Company having invested over $35 million to date in order to prepare the Project for construction and operation, including:

 • Completion of a bankable feasibility study;
 • Exhaustive due diligence by KfW IPEX-Bank appointed Independent Technical Engineers SRK Consulting on all technical and financial aspects of the Project as well as social, environmental and safety aspects to IFC Performance Standards and World Bank Group Environmental, Health and Safety Guidelines;
 • Sales and offtake agreements for graphite production in Germany with ThyssenKrupp and EGT and in Asia with Japanese group Sojitz Corporation; and
 • Mining Licence and environmental approvals in place.

>>Read More>>

 

Read more

Wizara itaendelea kuanzisha masoko ya madini-Biteko

Imeelezwa kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kusimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Madini katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za Uanzishwaji wa masoko hayo.

Waziri wa Madini Doto Biteko ameysema hayo Machi 31, 2019 wakati akifunga Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati zenye uhusiano na Sekta ya Madini.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati nyingine wakifuatilia uwasilishaji wa mada uliotolewa na Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Taasisi zake.

Semina hiyo ililenga kutoa elimu na kujenga uelewa wa pamoja kwa wabunge hao kuhusu sekta ya madini ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini, mafanikio na changamoto ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO), elimu kuhusu majanga ya asili (hasa matetemeko ya ardhi), ukaguzi migodini, biashara ya madini na shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Uwazi na uwajibikaji katika Rasiimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia.

Waziri Biteko aliongeza kuwa, Wizara itaendelea kuwaelea wadau wa madini huku akiwataka kubadilika na kutenda matendo yenye manufaa kwa pande mbili na kuwaomba wabunge hao kushirikiana na serikali katika kutoa elimu kwa wadau wa madini ili waweze kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa.

Pia, alisema serikali itaendelea kufanya kaguzi migodini kwa lengo la kuhakikisha wachimbaji wanachimba kwa usalama na kueleza kuwa, wizara imeomba kibali cha kuongeza maeneo mengine ya ukaguzi wa madini na kusema,“ tumepanga kuongeza vituo vingine 85”.

Aidha, alizungumzia maeneo yenye wizi wa dhahabu katika maeneo ya kuchanjua madini hayo na kuyataja kuwa ni Kahama na Chunya na kuwataka wahusika kuzingatia sheria.

Akizungumzia suala la kupunguza zaidi kodi kwa uchimbaji mdogo wa madini, alisema serikali haitapunguza tena kodi hizo kwa sasa mpaka hapo itakapoona manufaa yake.

Ikumbukwe kuwa, baada ya mkutano wa Kisekta uliofanyika Januari 22 mwaka huu chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa madini baada ya wadau hao kuwasilisha kero zao kubwa ikiwa kodi, serikali ilifanya mabadiliko na kuondoa kodi kwenye uchimbaji mdogo wa madini kwa kuwafutia kodi ya ongezeko la thamani yaani VAT  (18%) na  kodi ya zuio( withholding tax).

Mbali na wajumbe wa kamati, wengine walioshiriki semina hiyo ni Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Watendaji na Wataalam kutoka wizara na taasisi zake.

Read more

Naibu Waziri Nyongo afunga mitambo yote ya kuchenjulia madini Kahama

Na Greyson Mwase, Kahama

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefunga mitambo yote ya kuchenjulia madini ya dhahabu Wilayani Kahama baada ya kubaini udanganyifu mkubwa kwenye uchenjuaji wa madini.

Naibu Waziri Nyongo amechukua hatua hiyo kwenye ziara yake aliyoifanya mapema leo tarehe 31 Machi, 2019 Wilayani Kahama yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Kamishna Msaidizi, Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini,  Ali Saidi Ali, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian, wataalam kutoka Tume ya Madini, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.

Akiwa katika ziara hiyo, alifanya ziara ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group inayomilikiwa na  Theogenes Zacharia pamoja na mwenzake aliyejulikana kwa jina la  Antidius na kubaini kampuni hiyo imekuwa ikiwaibia wateja wake kupitia mfumo wa uchenjuaji wa madini ya dhahabu.

Akiwa ameambatana na msafara wake mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo alioneshwa na wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini waliopewa kazi maalum ya kuchunguza mfumo wa uchenjuaji wa dhahabu wa kampuni hiyo, sehemu ya mabomba ya mfumo iliyoharibiwa kwa makusudi kwa lengo la kunasa kiasi cha dhahabu kabla ya kufikishwa katika chombo maalum cha kupokelea kwa ajili ya mteja.

Kutoka kushoto Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakishuhudia kaboni ikichomwa ili kupata dhahabu katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group tarehe 31 Machi, 2019.

Alisema kuwa, kiasi cha kaboni iliyokuwa na dhahabu iliyokamatwa ilipelekwa kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kubaini kiasi cha adhabu kilichokuwa kimeibiwa na kusisitiza kuwa baada ya kuchenjuliwa kiasi cha gramu 102 kiligundulika kutaka kuibwa.

Katika hatua nyingine mbali na kufunga mitambo ya kuchenjua madini ya dhahabu katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya ya Kahama kuhakikisha watuhumiwa wote wa kampuni ya Ng’ana Group wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama na uchunguzi kuanza mara moja.

Katika hatua nyingine, Nyongo alisema kuwa maafisa madini wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama wataanza kufungua mtambo mmoja mmoja wa kuchenjua madini ya dhahabu mara baada ya kujiridhisha na uendeshaji wake.

Awali akielezea siri ya wizi unaofanywa na kampuni ya  Ng’ana Group, mmoja wa wateja kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya  Joseph Magunila & Partners, aliyepeleka kaboni kwa ajili ya kuchenjuliwa ili kupata madini ya dhahabu, Wema Shibitali alisema kuwa, wakati zoezi la uchanjuaji likiendelea alishangaa kupata kiasi kidogo cha dhahabu tofauti na kaboni iliyokuwa imewekwa.

Alisimulia kuwa aliomba maafisa kutoka vyombo vya dola kufungua mfumo ili kubaini kama kuna madini yamebaki na kuongeza kuwa mara baada ya mfumo kufunguliwa walibaini kiasi kikubwa cha kaboni kilichokuwa kimebaki kwenye mfumo.

Aidha Shabitali aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kuwa wamekuwa wakiibiwa na wachenjuaji wa madini ya dhahabu kwa muda mrefu.

Wakati huo huo akizungumza katika msafara huo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha mbali na kumpogeza Naibu Waziri Nyongo kwa kutembelea Wilaya yake na kushughulikia changamoto mbalimbali kwenye Sekta ya Madini, alisema kuwa ziara hiyo imewapa mwanga zaidi wa mbinu zinazotumiwa na wachenjuaji wa madini na kusisitiza kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu zaidi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Aliwataka wachimbaji na wachenjuaji wa madini nchini kuunga juhudi zinazofanywa na Rais wa Awamu ya Tano pamoja na Serikali yake, Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kuwa waaminifu kwenye ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali.

Read more

Naibu Waziri Nyongo abaini udanganyifu madini Kahama

Aelekeza soko la madini kuanzishwa mara moja………

Na Greyson Mwase, Kahama

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameelekeza soko la madini katika mkoa wa kimadini wa Kahama ikiwa ni pamoja na maeneo mengine ya Chunya, Musoma, Singida kuanzishwa mara moja ili kudhibiti utoroshwaji wa madini unaopelekea Serikali kukosa mapato yake.

Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo leo tarehe 31 Machi, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika mjini Kahama. Wengine waliokuwepo katika mkutano huo ni pamoja na Kamishna Msaidizi, Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini,  Ali Saidi Ali, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama, Andrea Fabian pamoja na wataalam kutoka Tume ya Madini.

Alisema kuwa, mara baada ya kufanya ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Kahama, alibaini kumekuwepo na udanganyifu mkubwa katika shughuli za uchenjuaji wa madini huku akitolea mfano wa kampuni ya Busami inayojihusisha na uchenjuaji wa madini ya dhahabu.

Alisisitiza kuwa, alibaini kumekuwepo na udanganyifu kwenye uzito na kiwango halisi cha dhahabu kwenye madini yaliyopatikana hali inayopelekea Serikali kukosa mapato yake stahiki.

“Kwa mfano katika mtambo wa kuchenjua dhahabu unaomilikiwa na kampuni ya Busami tumebaini kuna udanganyifu kwenye uchenjuaji, jana baada ya kufika na kuona namna uchenjuaji wa madini unavyofanyika na kuelekeza wataalam wa madini kuchenjua upya mchanga uliokuwepo kwenye maji yaliyohifadhiwa, tulibaini kuna madini,” alisema Nyongo

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo alisimamisha shughuli za uchenjuaji katika kampuni ya Busami na kutaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mmiliki wake.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Nyongo alielekeza wamiliki wote wa mitambo  ya kuchenjulia madini ya dhahabu nchini kuhakikisha wanakuwa na mizani na mashine maalum za kupimia madini ya dhahabu zilizoidhinishwa na Wakala wa Vipimo Tanzania, na biashara ya madini kufanyika katika masoko ya madini yaliyoanzishwa na kusisitiza kuwa lazima madini yajulikane yanapopelekwa na Ofisi za Madini Nchini kuhakikisha zinatuza kumbukumbu sahihi.

Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo aliagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya kufuatilia iwapo hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya kampuni inayojihusisha na uchenjuaji wa madini ya dhahabu Wilayani Kahama ya Jema baada ya kukamatwa ikifanya udanganyifu hivi karibuni.

Read more

Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Nyongo soko la madini kufunguliwa Kahama

Na Greyson Mwase, Kahama

Ofisi ya Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa Kimadini wa Kahama inatarajia kuanzisha soko la madini mapema ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Kutoka kulia Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wakisikiliza kero za wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu (hawapo pichani) kupitia mkutano maalum uliofanyika Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliyoifanya mapema leo tarehe 30 Machi, 2019 katika Wilaya ya Kahama lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya dhahabu, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Nyongo aliambatana na Kamishna Msaidizi- Uendelezaji Migodi na Madini wa Wizara ya Madini, Ali Said Ali wataalam kutoka Tume ya Madini pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Mara baada ya kufanya ziara katika baadhi  ya mitambo ya kuchenjua dhahabu, Nyongo alifanya kikao na wamiliki wa mitambo hiyo na kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuzitatua.

Mara baada ya kusikiliza kero husika ikiwa ni pamoja na ya kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, Naibu Waziri Nyongo alimwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama,  Adrea Fabian kuhakikisha sehemu ya ofisi yake inatumika kama soko la madini ya dhahabu ambapo wauzaji na wanunuzi watakuwa wanafanya biashara huku serikali ikipata mapato yake, kauli ambayo ilipokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa madini ya dhahabu.

Aliendelea kusema kuwa kutokuwepo kwa soko la madini katika Wilaya ya Kahama, kunachochea utoroshwaji wa madini ya dhahabu kwakuwa inakuwa vigumu kwa wauzaji wa madini hayo kusafiri umbali mrefu hadi Geita kwa ajili ya kwenda kuuza madini hayo.

“Hapa tunataka kuhakikisha biashara ya madini inafanyika hapa hapa ili kuwarahisishia wafanyabiashara wa madini ya dhahabu huku Serikali ikipata mapato yake,” alisisitiza Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliutaka uongozi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Kahama kushirikisha mamlaka nyingine za Serikali kama vile Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mabenki na soko kuanza mara moja.

Aidha, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wamiliki wa mitambo ya kuchenjua dhahabu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kulinda rasilimali za madini kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wamiliki wa mitambo ya kuchenjulia dhahabu walioshiriki katika kikao hicho mbali na kumpongeza Naibu Waziri Nyongo wamesema kuwa uwepo wa soko hilo utawarahisishia sana biashara ya madini kutokana na kuepukana na matapeli huku serikali ikipata mapato yake stahiki.

Walisema kabla ya uamuzi huo wamekuwa wakisafirisha madini hadi Geita kwa ajili ya kuuza hali inayopelekea baadhi yao kuuza kwa watu wasio waaminifu.

Read more

Hatukunufaika na madini, haikuwa ajenda ya Kitaifa–Spika Ndugai

Na Asteria Muhozya,

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugani, amesema awali, Taifa halikunufaika na rasilimali madini kwa kuwa sekta hiyo haikuwa ajenda ya Kitaifa.

Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalam wa Wizara ya Madini.

“Madini yaliachwa kwa wabunge ambao rasilimali hiyo inapatikana kwenye maeneo yao, haikuwa ajenda ya taifa, wengine walizungumzia zaidi masuala yanayowagusa kama korosho, pamba na mambo mengine, nashukuru tumefanya mabadiliko na sasa matokeo yameanza kuonekana,” amesema Spika Ndugai.

Amesema  kwa mwelekeo wa sasa, serikali imefika mahali ambapo manufaa ya rasilimali hiyo yameanza kuonekana kutokana na  mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kumpongeza kutokana na namna anavyohakikisha rasilimali madini inalinufaisha taifa, na kuongeza, “kilio cha watanzania cha kutokunufaika na madini kimepata mwenyewe, Rais Magufuli amefanya uthubutu”.

Spika Ndugai ameyasema hayo Machi 30, 2019, wakati akifungua Semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati nyingine za bunge wanaohudhuria semina ya siku mbili jijini Dodoma, iliyoandaliwa na Wizara ya Madini kwa lengo la kutoa elimu ili kupata uelewa wa sekta ya madini.

Amesema, awali, ikijulikana kama Wizara ya Nishati na Madini ilikuwa ni kazi hata kwa bunge hilo kupitisha Bajeti ya wizara hiyo kutokana na kwamba, sekta zote mbili nishati na madini   hazikuwa zikilinufaisha taifa na kusema, “ kulikuwa na kutokuridhika na sekta zote na hususan madini, kama taifa tulikuwa hatupati haki yetu tuliyoistahili”.

Kufuatia hali hiyo, Spika Ndugai amewataka Wabunge  na wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli  kwa kuwa  mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa utasaidia kusogeza mbele maendeleo ya taifa na watu wake.

Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalam wa Wizara ya Madini.

Aidha, amewaasa viongozi wote waliobeba dhamana ya kusimamia sekta husika kuhakikisha wanaichukulia dhamana waliyopewa kwa uzito wa kipekee  ili kuliwezesha taifa kufanana na nchi nyingine ambazo zimeendelea kutokana na rasilimali madini.

Pia, amepongeza mabadiliko yanayofanywa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na kueleza kwamba anafurahi kusikia STAMICO mpya tofauti na ilivyokuwa awali.

Akizungumzia Kamati mbili zilizoundwa na bunge kuchunguza biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi, amesema kuwa, kamati hizo zilifanya kazi nzuri na kwamba  bunge litaendelea kuishauri serikali  ili kuhakikisha sekta  ya madini inazidi kuchangia zaidi katika uchumi wa taifa.

Ameongeza kuwa, ripoti hizo zilipokelewa vizuri na serikali na kwamba juhudi zilizochukuliwa zimewezesha uanzishwaji wa masoko ya madini huku STAMICO ikifanya mabadiliko makubwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza katika semina hiyo, amesema  sekta ya madini ni muhimu kwa uchumi wa taifa la Tanzania na kueleza kuwa, mchango wa taifa umeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kueleza kuwa, mwaka 2017, sekta hiyo ilichangia asilimia 4.8 kwenye pato la taifa ikilinganishwa na asilimia 4.0 mwaka 2015.

Akizungumzia ukuaji wa sekta hiyo amesema umeongeza kwa kasi kutoka asilimia 9.0 mwaka 2015 kufikia 17.5 mwaka 2017, na kusema mafanikio hayo yametokana na juhudi za serikali kuhakikisha sekta hiyo inachangia zaidi  ili kufikia lengo la asilimia 10 ya mchango wake ifikapo mwaka 2025.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Madini, Wenyeviti wa Bodi ya Taasisi chini ya wizara na Wataalam kutoka wizarani na taasisi zake wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Semina iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya wabunge wa kamati nyingine (hayupo pichani).

Akizungumzia marekebisho ya Sheria ya Madini yaliyofanywa mwaka 2017,  na usimamizi wa Rasilimali Madini, amesema umewezesha ongezeko la makusanyo ya maduhuli yatokanayo na shughuli za madini kutoka Shilingi bilioni 194 iliyotarajiwa kukusanywa mwaka 2017/18 hadi shilingi bilioni 301.29 sawa na asilimia 154.999 ya lengo la makusanyo kwa mwaka huo.

“Mhe. Spika, mwenendo wa ukusanyaji maduhuli kwenye sekta hii kwa mwaka 2018/19 ni wa kuridhisha ambapo hadi Februari kiasi cha shilingi 218,650,392 kimekusanywa hii ikiwa ni sawa na asilimia 105.6,” amesema Waziri Biteko.

Ameeleza kuwa, miongoni mwa sababu zilizopelekea mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa mrabaha  kwa baadhi ya madini, kuanzisha kodi  mpya  ya ukaguzi ya asilimia 1; kuimarisha udhibiti wa utoroshaji wa madini; na kwa kushirikiana na wananchi  na vyombo vya ulinzi na usalama na kuzuia usafirishaji wa madini ghafi ya nje ya nchi ili  viwanda vya kusafishia na kuongeza ubora wa madini vijengwe  nchini.

Akizungumzia usimamizi wa shughuli za madini ya Tanzanite baada ya kukamilika kwa ukuta unaozunguka machimbo ya tanzanite Mirerani amesema udhibiti wa madini hayo umeimarika  na kusababisha kuongezeka kwa ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na madini hayo

Ameongeza kuwa, kufuatia juhudi hizo, ukusanyaji wa maduhuli kutokana na uzalishaji wa tanzanite kwa wachimbaji wa Wadogo na Kati uliongezeka hadi kufikia shilingi 1,436, 427, 228.99 kwa mwaka  2018, ikilinganishwa na  shilingi 71,861,970 kwa mwaka 2016.

“Uzalishaji umeongezeka kutoka migodi midogo na ya kati hadi kufikia kilo 781.204 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na kilo 147.7  zilizoripotiwa  kwa mwaka 2017 na kilo 164.6 za mwaka 2016,” amesema Waziri Biteko.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula, ameishukuru Wizara kwa kuandaa semina hiyo kwa wabunge na kueleza kuwa, kamati hiyo itaendelea kupata uelewa kuhusu sekta ya madini.

Mbali na wabunge, wengine wanaoshiriki semina hiyo ni Wenyeviti wa Bodi za taasisi za zilizo chini ya wizara, Wataalam kutoka wizarani na taasisi zake.

Read more

Waziri Mkuu atembelea Mji wa Serikali

Na Greyson Mwase, 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewapongeza wakandarasi kwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma.

Ametoa pongezi hizo leo tarehe 27 Machi, 2019 mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo na kuonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali wakati wakimsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye jengo la Wizara ya Madini kabla ya kuanza kwa ukaguzi kwenye jengo hilo.

“Nimefurahishwa sana na wakandarasi waliochukua zabuni za kujenga majengo ya ofisi hizi, hivyo ninawaomba Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) watoe vyeti kwenye majengo ambayo yamekamilika kwa asilimia mia ili waanze kutumia majengo hayo kama ilivyokusudiwa,” alisema Majaliwa.

Katika  hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa  hakuridhishwa  na ubora  wa milango iliyopachikwa kwenye jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Jengo la Wizara ya Fedha na kuagiza milango hiyo kubadilishwa.

Pia, Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka umeme mkubwa katika eneo hilo kwa wakati ili majengo yakamilike kwa asilimia mia na kufikia azma ya Serikali ya kuhamia katika mji wa Serikali baada ya ofisi hizo kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Mgufuli.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha, Philip Mpango, amesema mradi wa ujenzi wa nyumba hizo umezalisha ajira kubwa kwa vijana kutokana na kuajiri takribani watu 1141 walioshiriki katika ujenzi huo.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini,   Naibu Waziri wa  Madini, Stanslaus Nyongo, amesema jengo la Wizara limekamilika kwa asilimia 99, na kubainisha kuwa, mkandarasi yupo katika hatua za mwisho ili aweze kukabidhi jengo hilo.

Read more

Kituo cha Madini na Jiosayansi Kunduchi, kinavyowanufaisha Watanzania

Na Nuru Mwasampeta,

TAARIFA za kijiolojia zinaonesha kuwa, Afrika ni bara lenye utajiri mkubwa wa rasilimali madini huku sehemu kubwa ya madini hayo yakiwa bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji.

Aidha, rasilimali za madini zilizopo barani Afrika hususani Tanzania, taarifa za kijiolojia zinadokeza kuwa yanaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa na kijamii ikiwa kila mmoja aliyepewa jukumu la kuwajibika katika sekta ya madini atatumia utaalamu wake, weledi na ufanisi ili kupata matokeo chanya.

Ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kwa kutambua utajiri mkubwa wa madini tuliyonayo hapa nchini yakiwemo ya tanzanite, almasi,dhahabu, chuma au vito ameendelea kutoa hamasa kwa viongozi wenye mamlaka ya kuyasimamia madini kuongeza ubunifu na usimamizi wenye tija.

Kwa kutambua umuhimu wa madini katika kuharakisha maendeleo ya nchi, Wizara ya Madini kupitia viongozi wake kila kukicha wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali ili kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya nchi kuleta tija kubwa kwenye sekta ya uchimbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta kwa matokeo makubwa.

WAZIRI NYONGO

Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, ameshiriki katika kikao cha 39 cha kutathmini utendaji wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika (AMGC)) katika kutekeleza maazimio ya nchi wanachama kilichofanyika nchini Sudani Februari 18, mwaka huu.

Neno jiosayansi linamaanisha sayansi inayohusu Dunia ikihusisha masuala yote yanayohusisha elimu ya miamba kama vile utafutaji wa madini, uchimbaji, uchenjuaji pamoja na biashara ya madini.

Hivyo, AMGC ni kituo kinachoratibu masuala hayo kwa nchi mwanachama wa umoja huo katika Bara la Afrika.

Kituo hicho kilichoanzishwa na Kamisheni inayohusu masuala ya Kiuchumi katika Umoja wa Afrika (UNECA) kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli zote zinazohusu sekta ya madini chini ya Mwamvuli wa Dira ya Afrika kuhusu Madini (AMV) ili kupelekea maendeleo endelevu kwa nchi wanachama pasipo kuathiri mazingira.

Umoja huo ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1977 ukijulikana kama Southern and Eastern African Mineral Centre (SEAMIC) ambapo shughuli zake zilikuwa zikifanyika katika jengo la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) jijini Dodoma, kabla ya kuhamia katika ofisi zilizopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Gharama za ujenzi wa ofisi za kituo hicho zilitokana na michango ya nchi wanachama.

Aidha, kituo hicho kinafanya shughuli mbalimbali za madini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kukata na kuchenjua madini, kukata madini na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na madini, uchambuzi na huduma za ushauri katika maeneo tofautitofauti ya kimadini, pamoja na tafiti juu ya madhara yatokanayo na kemikali za kuchenjulia madini kwa mazingira.

Kabla ya mkutano uliowahusisha mawaziri wenye dhamana na sekta ya madini, kulitanguliwa na mikutano mingine miwili iliyohusisha Bodi ya Wakurugenzi wa kituo hiki ni kikao kidogo zaidi wakiwa ni wasimamizi wa karibu wa kituo kikao cha pili kinawahusisha watendaji wakuu katika wizara zenye dhamana ya madini, ambacho baada ya kikao waliwasilisha taarifa za kikao katika mkutano wa Baraza la Mawaziri la nchi wanachama kwa ajili ya kutolea maamuzi.

Kuhudhuria katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Madini Nyongo amesema, amejifunza namna sekta ya madini nchini Sudan ulivyojipanga katika kuikwamua Sudan kiuchumi kutokana na rasilimani madini.

Ameendelea kueleza kuwa, nchi ya Sudan inazalisha madini ya dhahabu kwa wingi kwa kiasi cha tani 107 ukilinganisha na Tanzania inayofikisha kiasi cha takriban tani 50 kwa mwaka.

Nyongo anaeleza kuwa, kiasi cha tani 107 cha dhahabu kilichozalishwa nchini Sudan mwaka uliopita kiliuzwa nje ya nchi ambapo asilimia 90 ya madini hayo yalichimbwa na kuuzwa kutoka kwa wachimbaji wadogo.

Waziri Nyongo amekiri kuwa, sekta ya uchimbaji mdogo inao uwezo mkubwa wa kuchangia katika pato la Taifa tofauti na fikra za wengi zilivyo.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia uwajibikaji wa migodi katika kutoa huduma na unufaikaji wa wazawa, Torence Ngole amesema uwepo wa kituo hicho kwa Watanzania una manufaa makubwa kwa Watanzania hususani wachimbaji wadogo katika kujipatia ujuzi.

Lakini pia kituo hicho kina maabara kubwa inayotumika katika kuchunguza madini na kuyabainisha ambapo wachimbaji wanaweza kupeleka madini yao na kuwa na uhakika zaidi wa mali waliyonayo.

Katika kupunguza migogoro katika kanda ya maziwa makuu kama vile Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi zenye migogoro na vita, Ngole amebainisha uwepo wa mashine maalumu inayoyafanya uchunguzi wa madini na kubaini madini hayo yanachimbwa nchi gani.

Amesema, ikibainika kuwa madini husika yanapatikana katika nchi zenye vita basi hayapewi kibali cha kuweza kuyauza na hivyo kuyanyima sifa ya kuuzika.

Hiyo ni moja kati ya mbinu ya kuleta amani na kupunguza kasi ya mauaji miongoni mwa nchi katika Bara la Afrika.

Pamoja na kuiwakilisha nchi katika kikao hicho cha mwaka, Ngole amesema alipata fursa ya kutembelea maonesho ya madini yanayoandaliwa na wizara yenye dhamana na madini nchini Sudan na kujifunza mambo muhimu ambayo nchi yetu ikiyafanya itasaidia katika kukuza sekta ya madini.

Amesema, kuwepo kwa maonesho ya madini kunafungua ukurasa kwa wachimbaji na wauzaji wa madini kukutana na kushirikishana uzoefu katika masuala yanayohusiana na sekta ya madini.

Swali unaweza kujiuliza je? Umoja wa kusimamia sekta ya madini Afrika una umuhimu gani?.

Akifafanua swali hilo, Ngole anasema, wakati wa uumbaji wa nchi/dunia mipaka ya kikanda na kijiografia havikuwepo, kutokana na hilo mipaka hiyo haizuii miamba ya madini iliyopo Tanzania inapofika baina ya mpaka wa nchi na nchi kukoma na kutokuendelea, kutokana na ukweli huo ushirikiano huo utazifanya nchi mwanachama kufanya shughuli za uchimbaji kwa namna zinazofanana na kutumia uzoefu wa nchi jirani kutambua uwepo wa madini katika nchi nyingine.

Ameongeza kuwa, katika kufanya tafiti za madini kuna ramani za madini zinatengenezwa, endapo kutakuwa na ushirikiano ramani hizo zitaandaliwa kwa vigezo vinavyofanana hivyo utangazaji wa sekta ya madini kufanana kwa nchi zote mwanachama.

Ameendelea kueleza kuwa, tafiti za pamoja zinasaidia sana katika kugundua aina mbalimbali za madini yaliyopo kwenye nchi wanachama kutokana na kufanya tafiti kwa pamoja na kubainisha kuwa mipaka ya kijiolojia iko tofauti na mipaka ya kijografia.

Pia ushirikiano unasaidia kupunguza changamoto ya utoroshwaji wa madini na kubainisha kuwa kutokuwepo na ushirikiano na mbinu za kuwafanya watoroshaji wa madini kukaguliwa katika mipaka ya nchi, nchi mwanachama hazitanufaika na madini yanayochimbwa kwani hayatalipiwa tozo zinazotakiwa na Serikali.

Katika hatua nyingine, inabainishwa kuwa, ushirikino ukiwepo baina ya nchi wanachama nchi hizo zitakuwa na sera zinazofanana kusimamia sekta ya madini.

Hii itatokana na mijadala wanayoifanya ya kubaini na kuchangia uzoefu katika kuendesha sekta, wawekezaji watashindwa kukimbia kimbilia, kwani sera zinafanana za nchi hizo zinafanana na kuamua kuwekeza mahali walipoanzia.

UMOJA UNAVYOJIENDESHA

Uendeshwaji wa kituo hicho unategemea michango ya nchi wanachama kwa asilimnia 60 ambapo kila nchi mwanachama anatakiwa kuchangia kiasi cha sh.milioni 150 (zaidi ya dola za Kimarekani 62,000) kwa mwaka na asilimia 40 zinatokana na kipato kitokanacho na ada za huduma zinazotolewa na kituo hicho.

KILICHOJADILIWA

Aidha, katika kikao hicho, kilijadili tathmini ya utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na kikao cha maamuzi cha mwaka uliotangulia ili kujiridhisha na mwenendo wa kituo hicho na kubaini changamoto zinazopelekea maagizo hayo kutokutekelezwa.

UMUHIMU WA KITUO

Kwanza kabisa kituo cha umoja huo kipo nchini Tanzania katika Jiji la Dar es Salaam. Uwepo wa kituo hicho ni heshima kubwa taifa limepewa na kuaminiwa na nchi wanachama.

Umuhimu wa kwanza unaotokana na kituo ni elimu inayotolewa katika kituo hicho kwa wachimbaji wadogo wa madini, hivyo Watanzania wengi kunufaika.

Wachimbaji wanafundishwa namna ya kukata madini, kuyaongezea thamani kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na madini pamoja na njia bora za uchenjuaji wa madini.

Pili kituo kinatoa huduma za kimaabara, hivyo mtu yeyote mwenye madini na anataka kutambua madini yake anaweza kupata huduma hiyo katika kituo hicho.

Vikao vya utendaji wa kituo vinakaliwa kila mwaka sawasawa na utaratibu uliowekwa na nchi wanachama.

Read more

Wizara ya Madini yaieleza Kamati ya Bunge utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/19

 • YATAJA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA
 • TUME YA MADINI YAPONGEZWA

Wizara ya Madini na Taasisi zake leo Machi 25, imewasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, kwa  kipindi  cha kuanzia  mwezi Julai 2018 hadi Februari, 2019.

Akiwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa ya utekelezaji wa Wizara, Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila pamoja na mambo mengine, ameelezea Mafanikio ya utekelezaji  wa bajeti kuwa ni pamoja na wizara kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli kwa asilimia 5.6 kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Februari 2019. Lengo la makusanyo kwa kipindi kinachorejewa lilikuwa shilingi 207,065,336,001 ambapo makusanyo halisi yamekuwa shilingi 218,650,392,234.

Pia, amesema Serikali imeondoa kodi kwenye uchimbaji mdogo kwa kuwafutia kodi ya ongezeko la thamani (VAT 18), na kodi ya zuio (Withholding tax  asilimia 5).

Pia, amesema kuzinduliwa kwa Soko la Madini katika mkoa wa  Geita ni juhudi za kuhakikisha uwepo wa masoko ya madini na bei inayoridhisha kwa wachimbaji wa madini hususan wachimbaji wadogo ili kudhibiti uuzaji holela na utoroshaji madini hayo.

“Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alizindua rasmi soko hilo tarehe 17 Machi, 2019,” amesema Prof. Msanjila.

Vilevile, ameeleza kwamba, kufuatia Kongamano lililofanyika nchini China lililojulikana kama China Tanzania Mining Forum, kampuni tatu zimewasilisha maombi ya miradi ya ubia (JV) kati ya watanzania na wageni Ofisi ya TIC Kanda ya Kati kwa ajili ya kupatiwa Cheti cha Vivutio vya Uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda vya kuchataka madini ya Graphite. Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza zaidi ya Dola za Marekani milioni 30 na kuzalisha ajira mpya 600 itakapokamilika.

Naye, Waziri wa Madini Waziri wa Madini Doto Biteko, akizungumza katika kikao hicho, ameishukuru Kamati hiyo kwa kuendelea kuisimamia na kuishauri vizuri na kueleza kwamba, Dira Kuu ya wizara ni kuongeza mchango kwenye uchumi wa nchi unaotokana na rasilimali madini.

Pia, Waziri Biteko ameiomba Kamati hiyo kuendelea kuishauri wizara ikiwemo kuikosoa kwa lengo la kuwezesha kuongeza tija zaidi kwenye sekta ya madini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula, amepongeza  jitihada zilizofanywa na wizara hususan kwa kuwezesha mkutano wa Kisekta baina ya serikali na wadau wa madini uliofanyika Januari 22 mwaka huu chini ya Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri wa Muungano  wa Tanzania Dkt. John Magufuli na kueleza kwamba, mkutano huo ulifungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya Serikali na wadau na hivyo kuutaka ushirikiano huo kuendelezwa ili uwezeshe kuendeleza sekta ya madini nchini.

Amesema matarajio ya Rais Magufuli kwenye sekta ya madini ni makubwa na hivyo kutaka jitihada zaidi kufanyika ili kukidhi maratajio hayo.

Aidha, wakichangia hoja kwa nyakati tofauti, wajumbe wa Kamati hiyo wameipongeza Tume ya Madini kwa ukusanyaji maduhuli na kwa utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo ukaguzi migodini.

Read more

Biteko azitaka Taasisi za Madini kufikiri kibiashara

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini Doto Biteko amezitaka taasisi zilicho chini ya Wizara kufikiri kibiashara ikiwemo kutafuta njia zitakazowezesha sekta ya madini kuchangia zaidi katika pato la taifa.

Waziri wa Madini Doto Biteko katikati akipitia jambo wakati wa kikao kazi cha kupitia na kujadili Mpango Mkakati na Mkakati wa Kibiashara wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC). Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kushoto ni Katibu Mkuu, Prof. Simon Msanjila.

Waziri Biteko ameyasema hayo Machi 23, jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha kupitia na kujadili Mpango Mkakati na Mkakati wa Kibiashara wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) iliyoandaliwa na Wataalam Elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Aidha, amezitaka taasisi hizo kuhama katika mtindo wa kutegemea ruzuku ya serikali badala yake zijiendeshe kibiashara na kuwataka watendaji wa wizara na taasisi kuhakikisha wanafanya mageuzi yatakayowezesha sekta hiyo kuchangia zaidi sambamba na kasi yake ya ukuaji kiuchumi.

“ Serikali kwa upande wake imeshafanya mageuzi makubwa. Tunataka Idara, kitengo na taasisi zifanye mageuzi. Tuwe na taasisi ambayo mfanyakazi anaweza kueleza amefanya nini kipya,” amesisitiza Waziri Biteko.

Pia, ameongeza kuwa, ukataji madini ni suala ambalo linalopaswa kuchukuliwa kwa uzito wa kipekee kutokana na umuhimu wake katika biashara ya madini na hususan kipindi hiki ambacho serikali inasisitiza shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika nchini ikiwemo kuhamasisha ujenzi wa viwanda hivyo.

Vilevile, amewataka washiriki wa kikao hicho kuwasilisha mawazo chanya yatakayosaidia kuboresha mkakati huo utakopelekea uboreshaji wa kituo cha TGC.

Aidha, amewataka watendaji wa Kituo cha TGC kuhakikisha wanakitangaza kituo hicho ikiwemo kuwafanya wachimbaji wadogo wa madini kuwa marafiki wa kituo hicho.

Kwa upande wake, Naibu wa Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, amesema serikali iliona umuhimu wa Kituo cha TGC hali ambayo imepelekea kuandaliwa kwa mikakati hiyo na kueleza kuwa uwepo wake unapaswa kutoa mabadiliko katika kituo hicho na hususan katika eneo la uongezaji thamani madini.

Waziri wa Madini Doto Biteko akieleza jambo wakati akifungua kikao kazi cha kupitia na kujadili Mpango Mkakati na Mkakati wa Kibiashara wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC). Wengine ni watendaji wa Wizara na Taasisi.

Ameongeza kuwa, uongezaji thamani madini ni jambo ambalo serikali inaliangalia kwa umuhimu wake na kueleza kuwa ni miongoni mwa mambo  yaliyopelekea kufanyika kwa mabadiliko katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na 2017 ili taifa liweze kunufaika zaidi .

Ameeleza masuala mengine yaliyopelekea serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya madini ni pamoja na kutaka kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na madini, serikali kushiriki katika uchumi wa madini na kumiliki hisa, kushirikisha jamii katika miradi ya madini na kampuni za madini kushirikiana  na jamii.

Aidha, amewashukuru wataalam washauri Prof. Beatus Kundi na Prof. Marcellina Chijoriga kutokana na ushauri wao walioutoa kwa wizara wakati wa kupitia Mikakati hiyo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara yaMadini, Prof. Simon Msanjila amewataka watendaji wa Wizara kuhakikisha kila mmoja anaangalia eneo linalomhusu katika kituo hicho na kulifanyia kazi kikamilifu ili kufikia lengo linalotarajiwa .

Wizara ya Madini iliona umuhimu wa kukiimarisha Kituo cha TGC ili kijiendeshe kibiashara kutokana na fursa zilizopo katika sekta ya madini hususan kwenye ukataji wa madini. Pia, kutokana na fursa zilizopo katika ukataji wa madini ya vito na jimolojia kwa ujumla, wizara iliona TGC inaweza kujiendesha kibiashara na hivyo kuongeza mapato kwa serikali.

Kazi ya kuandaa Mikakati hiyo imetekelezwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) na  kuandaliwa na Wataalam Elekezi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na kupitiwa kikamilifu na Prof. Beatus Kundi na Prof. Marcellina Chijoriga kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Watendaji kutoka Wizarani na taasisi zake.

Read more

Viongozi Waandamizi Madini watembelea jengo la Wizara, Ihumwa

 • Waziri Biteko asema wizara iko tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa
 • Mkandarasi aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku Tano

Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Machi 23, wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Waziri wa Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara

Akizungumza baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara.

Vilevile, Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na wajeta wake.

Pia, amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana na msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa wakati.

Aidha,  amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara imepanga kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti ya aina mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri ya kuvutia.

Naye, Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi cha siku Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika hatua nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila.

Akizungumzia mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa kifedha.

Pia, ameeleza kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini ya mable ambayo yamepatikana kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo   Hamisi Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani ya siku tano zijazo, jengo hilo litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.

Read more

Taarifa ya uanzishaji masoko ya madini iliyosomwa na Prof. Simon Msanjila kwenye uzinduzi wa soko la dhahabu mkoani Geita

Mh. Kassim Majaliwa MajaliwaWaziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mheshimiwa Dotto M. Biteko (Mb.), Waziri wa Madini,

Mh. Dkt Medadi Kalemani, Waziri wa Nishati,

Waheshimiwa Manaibu Mawaziri Mliopo,

Mh. Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Geita,

Waheshimiwa wakuu wa mikoa mliopo,

Ndugu Denis Bandisa, Katibu Tawala Mkoa wa Geita,

Waheshimiwa wakuu wa Wilaya,

Prof. Idris Kikula, Mwenyekiti wa Tume ya Madini,

Prof. Shukrani Manya, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini,

Katibu Tawala wa Wilaya,

Wakurugenzi wa Wilaya,

Watendaji wa Wizara na Tume ya Madini

Wawakilishi wa wachimbaji Madini

Wanahabari

Wageni waalikwa

Mabibi na Mabwana.

 

HABARI ZA MCHANA

 

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia kukutana hapa leo, katika uzinduzi wa soko la Madini ya dhahabu mjini Geita. Naomba pia nikushukuru wewe mwenyewe kwa kukubali kuja huku Geita kutufungulia soko hili la kwanza la aina yake, soko la dhahabu. Naomba pia uniruhusu niwashukuru sana wananchi wote wa mkoa wa Geita chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa mwitikio wao wa haraka na chanya katika kujenga soko hili na hata leo tunawaona hapa wakiwa wamefika kwa wingi kushuhudia soko lao likizinduliwa. Naomba pia niwashukuru wengine wote waliokubali mwaliko wetu na kusafiri kokote walikotokea na kufika hapa kuungana nasi katika tukio hili muhimu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,

Tarehe 22/01/2019, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,alifungua na kushiriki mkutano Mkuu wa Kisekta wa wachimbaji wadogo uliolenga kusikiliza kero na changamoto zinazoikabili sekta hii ya madini hasa kwa wachimbaji wadogo.  Kupitia mkutano huo, Mh. Rais alipokea kero mbalimbali za wachimbaji wadogo, na kutoa maelekezo ya namna ya kuziondoa kero hizo. Moja ya kero iliyoainishwa na Wachimbaji wadogo, ni ukosefu wa masoko ya uhakika na rasmi ya Madini katika maeneo mbalimbali wanayofanyia shughuli zao za uchimbaji. Wadau hawa walieleza kuwa, ukosefu wa masoko rasmi na ya uhakika ndio sababu kubwa inayowafanya watoroshe madini na kuuza katika masoko yasiyo rasmi.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Hotuba ya Mhe. Kassim M. Majaliwa (MB.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akizindua soko la madini ya dhahabu mkoani Geita

SALAMU

Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (Mb.), Waziri wa Madini;

Mheshimiwa Mhandisi Robert Luhumbi, Mkuu wa Mkoa wa Geita;

Prof. Simon Msanjila, Katibu Mkuu Wizara ya Madini;

Ndugu Denis Bandisa, Katibu Tawala Mkoa wa Geita;

Prof. Idris Kikula, Mwenyekiti wa Tume ya Madini;

Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya;

Makatibu Tawala wa Wilaya;

Wakurugenzi wa Wilaya;

Watendaji wa Wizara na Tume ya Madini;

Wawakilishi wa wachimbaji Madini;

Wanahabari;

Wageni Waalikwa;

Mabibi na Mabwana;

 

Habari za Asubuhi

 

SHUKRANI NA PONGEZI

Ndugu wananchi,

Nianze kwa kuushukuru Uongozi wa Mkoa wa Geita, Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa kunialika kuwa mgeni rasmi katika shughuli hii ya uzinduzi wa Soko la Madini ya Dhahabu la Mkoa wa Geita.

Pokeeni salamu kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi wetu hao wanawasalimu na kuwapongeza kwa kazi nzuri hususan katika kutekeleza kwa wakati maelekezo, mipango na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.

Niupongeze uongozi wa Mkoa kwa kutekeleza kwa haraka kuanzisha soko mara baada ya agizo lilolotolewa na Mheshimiwa Rais siku ya tarehe 22.01.2019.

MCHANGO WA SERIKALI KATIKA UKUAJI WA SEKTA YA MADINI

Ndugu Wananchi,

Tangu iingie madarakani, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kujipambanua kuhusu dhamira yake ya kuhakikisha sekta ya madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa pato la taifa. Aidha, Serikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020 ambayo yanaitaka Serikali kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha kupunguza au kukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji madini kwenda nje ya nchi na biashara haramu ya madini nchini.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Majaliwa atoa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa kukamilisha masoko ya madini

Nuru Mwasampeta na Greyson Mwase, Geita 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi mitatu kwa wakuu wa mikoa hususan mikoa yenye utajiri mwingi wa madini ya metali na vito nchini kuhakikisha wanakamilisha na kufungua masoko ya madini ili kuwawezesha wachimbaji na wafanyabiashara ya madini kuwa na soko la uhakika la madini hayo.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.

Majaliwa alitoa  agizo hilo kwenye uzinduzi wa Soko la Madini la Geita tarehe 17 Machi, 2019 uliofanyika katika viwanja vya Soko Kuu mkoani Geita na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa kiserikali ikiwa ni pamoja na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.

Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula, watendaji kutoka Tume ya Madini, Wakuu wa Mikoa, wabunge, madiwani, viongozi wa dini, waandishi wa habari pamoja na wananchi kutoka katika mkoa wa Geita pamoja na mikoa ya  jirani.

Alisema kuwa, uanzishwaji wa masoko ya madini ni  sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa tarehe 22 Januari, 2019 kwenye mkutano wake na wachimbaji wa madini nchini uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

“Ninawataka wakuu wa mikoa kuhakikisha agizo hili linatekelezwa kabla ya mwaka wa fedha kumalizika Juni 30, 2019,” alisema Majaliwa.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwanufaisha watanzania wote, Serikali kupitia Wizara ya Madini ilianza kwa kuboresha Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Simon Msanjila akitoa taarifa ya uzalishaji wa madini nchini kwenye uzinduzi huo.

Aliongeza kuwa, serikali imeamua kuondoa tozo mbalimbali zilizokuwa mzigo kwa wachimbaji wa madini uli uchimbaji wao uwe na faida kubwa na kuwawezesha kulipa kodi mbalimbali za Serikali.

Alisema kuwa, kufutwa kwa kodi na tozo mbalimbali kutapunguza kwa kiwango kikubwa utoroshwaji wa madini nje ya nchi na Serikali kujipatia pato kubwa linalotokana na shughuli za madini nchini.

Akielezea umuhimu wa masoko ya madini, Majaliwa alieleza kuwa mbali na kupunguza utoroshwaji wa madini, hakutakuwepo na dhuluma kwa wachimbaji wadogo wa madini kwani watakuwa na sehemu yenye uhakika ya kuuzia madini hayo kulingana na bei elekezi iliyotolewa na Serikali.

Aliendelea kueleza kuwa, soko la madini  litarahisisha huduma za uuzaji na ununuzi wa madini ambapo huduma zote zitatolewa ndani ya jengo moja hivyo kuokoa muda wa wauzaji na wanunuzi wa madini.

Katika hatua nyingine, Majaliwa alitoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa, atakayekamatwa anatorosha madini atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha.

Pia aliwataka viongozi na watendaji wa Serikali kusimamia kwa weledi, uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali  kuhusu sekta ya madini kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi wa Soko la Madini la Geita kufanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa tarehe 17 Machi, 2019.

Aidha, aliitaka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine za Serikali  zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini kuheshimu mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

“Wizara ya Madini, ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahususi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya soko hilo ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini,” alisisitiza Majaliwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya  sekta ya madini ambapo utekelezaji  wa dhamira hiyo unakwenda sambamba na kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa sekta ya madini nchini.

Read more

Tutaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini-Mwenyekiti wa Kamati

Na Issa Mtuwa, Songea

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mariam Ditopile Mzuzuri amesema kamati yake inaipongeza na itaendelea kuiunga mkono Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Meneja wa Kanda ya Ujenzi SUMA JKT, Meja Atupele Mwamfup akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kituo na kutafsiri michoro mbalimbali ya jengo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu Wizara ya Madini Issa Nchasi, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Makamu Mwenyekiti Mhe. Mriam Mzuzuri na wajumbe wengine.

Akiongea na waandishi wa habari mbele ya kamati yake Machi 13, 2019 mjini songea baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha umahiri (Centre of excellence) kwa mkoa wa ruvuma, Mzuzuri amesema kamati yake inaridhishwa na kazi za Wizara ya Madini na wataendelea kuiunga mkono (support) hasa swala la wachimbaji wadogo.

“Tunawapongeza sana Wizara ya Madini, mnafanya kazi nzuri na sisi kama kamati niseme tutaendelea kuwaunga mkono (support) hasa hili la wachimbaji wadogo” alisema Mzuzuri.

Naibu Wziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo ameiambia kamati kuwa wizara yake imejipanga katika kukamilisha ujenzi wa vituo vyote vya umairi kikiwemo cha Songea kwa kuzingatia ubora. Amesema ujenzi wa vituo vyote unakwenda vizuri, hata hivyo kituo cha songea kilichelewa ujenzi wake tofauti na vituo vingine kwa sababu mbalimbali ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa kokoto tatizo ambalo lilisha tatuliwa na kwa sasa ujenzi unaendelea kwa kasi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imekusudia kukamilisha ujenzi wa kituo hiki na vingine kwa wakati na kama nilivyo tangulia kusema zile changamoto zimesha tatuliwa na tuaendelea vizuri. Naishukuru kamati yako kwa kutuunga mkono na ushauri wote uliotolewa tutauzingatia.” Alisema Nyongo.

Nae Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Prof. Riziki Shemdoe akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo amewambia wajumbe wa kamati kuwa ni kweli kuna kipindi mkoa wa Ruvuma ulikumbwa na changamoto za upatikanaji wa kokoto na miradi mingi ya serikali ilisimama kutokana na kuwa na kampuni moja tu ya uzalishaji wa kokoto mkoa nzima, mara baada ya mitambo yake kuharibika na uzalishaji kusimama upatikanaji wa kokoto ulikuwa ni tatiizo.

Kituo cha Umahiri Songea ni miongoni mwa vituo mbalimbali vinavyo jengwa hapa nchini katika maeneo mbalimbali kama vile, kituo cha Bukoba, Simiyu, Tanga, Chuya kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo kujifunza na kupata uelewa wa masuala mbalimbali madini.

Read more

Waziri Kairuki amkabidhi rasmi Wizara Biteko

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki amemkabidhi rasmi Majukumu ya Uwaziri wa Wizara ya Madini, Waziri Doto Biteko katika kikao kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Waziri Kairuki amemshukuru Waziri Biteko kwa ushirikiano aliompatia kwa kipindi chote alichokuwa Waziri wa wizara hiyo na kueleza kwamba, kabla ya makabidhiano hayo, wamepata wasaa wa kupitia kwa pamoja majukumu na vipaumbele vya wizara ikiwemo maeneo muhimu yanayotakiwa kupewa msukumo.

Naye, Waziri Biteko, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, amemshukuru Waziri Kairuki na kumwelezea kuwa ni Waziri aliyekuwa mwalimu mzuri kwake kwa kipindi chote alichokuwa Naibu Waziri.

Ameongeza, Waziri Kairuki hakuwahi kumnyima nafasi ya kujifunza ikiwemo kumtuma kutekeleza majukumu mbalimbali nafasi ambayo ilimkomaza.

“ Waziri hakuwahi kuninyima fursa, alinituma popote na nitaendelea kuhitaji ushauri wake katika kutekeleza majukumu yangu,” amesisitiza Biteko.

Makabidhiano hayo yamefanyika Machi 12, ofisini kwa Waziri Biteko Jijini Dodoma.

Waziri Biteko aliteuliwa Januari 8, 2019 kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Waziri Biteko alichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Read more

Acacia yazungumza na Serikali kunusuru Mgodi usifungwe

Na Issa Mtuwa, Dodoma

Uongozi wa Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wa North Mara umezungumza na Serikali kuelezea hatua zilizochukuliwa hadi sasa kudhibiti maji yenye sumu ikiwa ni wiki moja tu ipite tangu Waziri wa Madini Doto Biteko, atangaze kufunga shuguli za mgodi huo endapo utashindwa kudhibiti maji ya sumu yanayotiririka kwenye makazi ya watu, ifike Machi 30 mwaka huu.

Tamko hilo la serikali limeifanya kampuni ya Acacia kuchukua hatua za haraka za kudhibiti maji hayo ili kukwepa rungu la serikali la kuufunga mgodi huo.  Machi 12, uongozi wa Acacia North Mara ulikutana na Waziri Biteko ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kueleza hatua iliyofikiwa ya kutekeleza agizo la serikali.

Uongozi wa kampuni hiyo ukizungumza katika kikao hicho, ulieleza kuwa, tayari mgodi huo umechukua hatua za haraka tangu kutolewa kwa agizo na kwamba hadi sasa suala la kudhibiti maji yenye sumu limeshetekelezwa na hakuna maji yanayotiririka kuelekea kwenye makazi ya watu.

Aidha, ulimweleza kuwa, pamoja na kudhibiti maji hayo kupitia bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu yajulikanayo kitaalam kama “topesumu” (Tailings Storage Facility- TSF) mgodi umeanza kuchukuwa hatua za kujenga TSF mpya.

“Mhe. Waziri tumekuja kutoa mrejesho wa utekelezaji wa agizo lako, tunafurahi kukuambia kuwa tumetekeleza agizo hilo na kwa sasa hakuna maji yanayotiririka. Pamoja na hatua hiyo mgodi umeanza mchakato wa ujenzi wa bwawa jipya (TSF) la kuhifadhia topesumu,” walieleza.

Aidha, ulimweleza Waziri Biteko kuhusu hujuma za uharibifu wa miundombinu ya bomba la maji yenye sumu unaofanywa kwa maksudi na wakazi wanaozunguka mgodi ili kufifisha juhudi zao za kudhibiti maji hayo wakiwa na lengo la kuufanya mgodi uonekane haujachukuwa hatua kudhibiti jambo hilo, ambapo walionesha picha mbalimbali ya namna bomba lilivyo pasuliwa ili maji yatiririke kuelekeka kwa wananchi.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko alieleza kuwa, amepokea taarifa ya kampuni husika na kuwapongeza kwa hatua zilizochukuliwa na kusema kuwa, ukweli wa jambo hilo atauthibitisha mara baada ya kupata ripoti ya wataalam watakaokwenda kuhakikisha kuhusu utekelezaji wa agizo hilo na kuongeza,“katika hili sitanii juu ya kuufunga mgodi ikiwa utashindwa kudhibiti tope sumu,”.

“Naomba nirudie tena katika hili sitanii, sitabadilisha msimamo wangu kama serikali na utaendelea kubaki pale pale dawa pekee ni kutekelezwa kwa agizo hilo. Lakini niseme ukweli, nasikitishwa sana na kitendo hiki cha wananchi kupasua bomba, kwa hili sikubaliani nao na siwaungi mkono.

Pia, aliongeza kuwa, atawasiliana na Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuona namna ya kudhibiti hali hiyo ili wale watakao bainika wachukuliwe hatua.

Waziri Biteko alilitoa agizo hilo   Machi 6, alipoutembelea mgodi huo hapo kwa ziara ya kikazi  pamoja na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime.

Read more

Kamati ya Bunge yaipongeza Wizara ya Madini

Na Issa Mtuwa, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Madini kwa utekelezaji wa Ujenzi wa Jengo la Taaluma la chuo cha Madini Dodoma (MRI) na Ujenzi wa Jengo la Ofisi za Wizara ya Madini lilipo eneo la Mji wa Serikali Ihumwa, Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Danstan Kitandula wa kwanza kushoto akisikiliza maelezo ya ujenzi wa jengo la taaluma la chuo cha Madini (MRI) kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Fredrick Mangasini wa kwanza kulia na wapili yake ni Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteo.

Hayo yamesemwa  Machi 13, 2019 na Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa kikao cha majumuhisho kilichofanyika kwenye jengo la wizara ya Madini Ihumwa, mara baada ya kukagua majengo yote mawili na kupewa taarifa ya ujenzi wake.

Wakiwa kwenye jengo la taaluma la chuo cha madini, wajumbe wamepongeza na kuridhishwa na  hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kupongeza SUMA JKT  kujenge jengo hilo.

Jengo la Taaluma ni la ghorofa tatu lenye ofisi, vyumba vya kufundishia na ukumbi wa mikutano. Ujenzi huo utagharimu jumla ya shilingi 2, 863, 161, 369.00 hadi kukamilika kwake  na unatekelezwa chini ya chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Raslimali Madini (SMMRP) kwa mkopo kutoka Benki ya  Dunia.

Akizungumzia ujenzi wa jengo la Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amewaeleza wajumbe wa kamati kuwa, ujenzi huo ulianza tarehe 4/12/2018 na ulitakiwa kukamilika tarehe 31/01/2019, hata hivyo mkandarasi hakuweza kukamilisha ndani ya muda huo kutokana na sababu mbalimbali. Prof. Msanjila ameongeza kuwa, kwa kuzingatia ushauri wa msimamizi wa ujenzi huo, walifikia makubaliano ya kumuongezea muda mkandarasi hadi kufikia tarehe 28/02/2019.

Prof. Msanjila ameongeza kuwa, mpaka sasa ujenzi huo umefikia asilimia 80 na mwezi ujao wizara itakuwa tayari kuhamia. Amesema ujenzi huo umegharimu Jumla ya shilingi Milioni 975,360,028.10 zitatumika katika ujenzi huo.

Naye, Waziri wa Madini Doto Biteko ameiambia kamati kuwa, mkandarasi wa ujenzi huo, alipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha ujenzi wake ili wafanyakazi wa Wizara hiyo waanze kulitumia. Waziri emeleza kuwa wizara inaridhishwa na kasi ya mkandarasi katika ujenzi huo.

Biteko ameongeza kuwa, wizara imedhamiria kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kuthibitisha hilo wizara imemteuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Raslimaliwatu, Nsajigwa Kabigi ambae yupo muda wote wote eneo la ujenzi.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na viongozi wa Wizara ya Madini wakiwa kwenye kikao cha majumuisho baada ya kutembelea miradi

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dunstan Kitandula amesema pamoja na wabunge kuipongeza wizara kwa kazi nzuri, ameishauri wizara na mkandarasi wa ujenzi huo, Mzinga Holdings Company kujielekeza kwenye manunuzi ya vifaa vinavyopatikana hapa nchini.

Wakichangia wajumbe wa kamati hiyo, Joseph Musukuma na Ally Keissy wakichangia wakati wa majumuhisho waliipongeza wizara na mkandarasi, hata hivyo, walishangaa muda waliopewa na hatua iliyofikia, msukuma alisema ni kazi ya kupongeza na  wameeleza pamoja na mkandarasi kutokamilisha kazi yake kwa wakati bado utendaji wake wa kazi unaridhisha na kasi  yake inaonekana.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo aliwaambia wajumbe wa kamati kuwa, ujenzi wa jengo hilo la wizara unafanana ramani na wizara nyingine ikiwemo kiasi cha fedha zilizotolewa na serikali zote zikiwa na kiwango cha shilingi Bilioni moja.

Amesema muda uliotolewa ulilenga kutimiza azma ya wizara kuhamia eneo hilo kwa wakati. Aliwashukuru wajumbe kwa ushauri wao na  kueleza kwamba kama wizara watauzingatia.

Read more

Waziri Biteko azitaka nchi za Maziwa Makuu kudhibiti rasilimali ardhi

Na Issa Mtuwa Dodoma

Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu zimetakiwa kushikamana kuunganisha nguvu katika kulinda na kusimamia matumizi ya raslimali ardhi ikiwemo madini ili kunufaisha nchi hizo.

Mjumbe kutoka Burundi Gerard Nayuburundi akiwasilisha mada kwenye mkutano wa kimataifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu kwenye Hotel ya Morena Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua mkutano wa Kimataifa    wa nchi Wanachama wa Maziwa Makuu (International Conference on the Great Lakes Region – ICGLR) unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11-12 Machi 2019 katika Hotel ya Morena jijini Dodoma.

Biteko amezitaka nchi hizo kuunganisha nguvu ya pamoja katika kudhibiti raslimali ardhi ikiwemo madini na kujiwekea utaratibu utakao dhibiti shughuli za uzalishaji na biashara ya madini ili raslimali hizo zinufaishe mataifa yao na zisitumike vibaya.

“Unganisheni nguvu kwa pamoja, wekeni utaratibu utakao wafanya nchi wanachama kunufaika na raslimali ardhi/madini. Jitahidini kuhakikisha raslimali hizo hazitumiki vibaya kama ilivyo kubaliwa kwenye itifaki, hivyo lazima kuwe na utaratibu na sheria kwa kila nchi namna ya kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini,” amesema Biteko.

Naye, Mtaalam kutoka Wizara ya Madini, Mhandisi Assah Mwakilembe amesema Mkutano huo unalenga kujadili na kupitia mfumo wa udhibitisho wa mnyororo wa madini kwa lengo la kudhibiti uzalishaji na biashara ya madini katika nchi za maziwa makuu kufuatia kuwepo tetesi zilizo kuwa zinahusisha raslimali ardhi (Madini) na ufadhili wa vita katika nchi za aaziwa makuu. (Region Certification Manual)

Akizungumza mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu marekebisho ya Sheria Madini ya Mwaka 2017 Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Madini, Edwin Igenge amesema kwa upande wa Tanzania, imetekeleza itifaki ya pamoja ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu kama ilivyo kubaliwa.

Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akiongea na wajumbe wa mkutano wa kimataaifa wa nchi wanachama wa Maziwa Makuu jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa, utekelezaji wa itifaki kwa Tanzania ni pamoja na marekebisho ya sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yaliyopelekea kuundwa kwa Tume ya Madini ambapo shuguli zote za usimamizi wa raslimali madini zimepewa Tume ya Madini ambapo kabla ya hapo shuguli hizo zilikuwa chini ya Kamishna wa Madini.

Igenge amesema kuanzishwa kwa itifaki katika nchi za maziwa makuu kulitokana na tetesi za uwepo wa matumizi mabaya ya raslimali ardhi ikiwemo madini ambapo kipato cha raslimali hizo inasadikika kuwa zilikuwa zinatumika kufadhili shuguli za za kivita katika nchi za maziwa makuu, hivyo kupelekea kuanzishwa kwa itifaki ya pamoja kwa lengo la kudhibiti.

Mkutano huo wa kimataaifa unahudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania, Burundi, Rwanda na wawakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretariati ya nchi wanachama wa Maziwa Makuu. Kwa upande wa  Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Madini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Shirikisho la Wachimbaji Tanzania (FEMATA), Chama cha Wanunuzi  na Wauzaji wa  Madini Tanzania  (TAMIDA), Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa  Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST).

Katika mkutano huo, Waziri Biteko aliambatana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini Mhandisi Daivid Mulabwa, Mkurugenzi wa Sheria kutoka Wizara ya Madini Edwin Igenge na baadhi ya maafisa kutoka wizara ya Madini.

Read more

Waziri Biteko ateta na wenye nia ya kuwekeza nchini

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.

Kamishna wa Madini David Mulabwa akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.

Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.

Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.

Read more

Nyongo abainisha changamoto zinazoikabili sekta ya madini

Na Nuru Mwasampeta,

Licha ya kwamba Wizara ya Madini kuwa miongoni mwa wizara nyeti katika kufikia uchumi wa viwanda, inakutana na changamoto nyingi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo hilo Tarehe 9 Machi, 2019.

Naibu Waziri Nyongo alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na utoroshwaji wa Madini unaosababisha Taifa kutokupata kodi stahiki, uwepo wa mikataba isiyolinufaisha Taifa, hali mbaya ya wachimbaji wadogo na hali ya wachimbaji kufanya shughuli zao bila kuzingatia suala zima la usalama.

Pamoja na changamoto hizo, Naibu Waziri Nyongo alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilifanyia marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 mnamo mwaka 2017.

“Mimi pamoja na uongozi wote wa wizara ya Madini tumepewa dhamana kusimamia sheria hiyo ili Madini yaliyopo nchini yanufaishe Taifa na watu wake”, alisema Nyongo.

Awali kabla ya mkutano huo, Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Read more

Nyongo akagua miradi ya maendeleo jimboni Kwake Maswa

Na Nuru Mwasampeta,

Katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na utekelezaji wa ahadi za chama kwa wananchi, Naibu Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Stanslaus Nyongo leo amekagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo lake.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kulia) akiambatana na wajumbe wa Chama na mhandisi wa barabara akikagua ujenzi wa Barabara ya km 1.5 ikiwa ni moja ya ahadi za chama

Nyongo alitembelea mradi wa ujenzi wa shule unaoendelea katika kata ya Nyalikungu na kuagiza shule hiyo ya  msingi ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwezi huu ili kuwapa nafuu wanafunzi wanaotembea mwendo mrefu kutafuta elimu.

Aidha, Nyongo ameelekeza mwenge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakapopita katika wilaya ya Maswa, ndipo shule hiyo ifunguliwe rasmi ili kuruhusu masuala mengine ya kimaendeleo kutekelezwa.

Mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika eneo hilo, Nyongo alielekea katika kijiji cha  ambako alikagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ambao haukuwa wakuridhisha aidha, alitembelea hospitali ya Wilaya ya Maswa kujionea eneo lililopendekezwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ambalo mchakato wa ujenzi na upatikanaji wa pesa umekamilika.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo katika eneo hilo la shule, Diwani wa Kata ya Nyalikungu, Joseph Bundara, alisema ni kutokuwa na barabara, huduma ya maji, umeme pamoja na ombi lakujengewa nyumba ya mwalimu ili kuishi karibu na mazingira ya shule.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa shule iliyopo katika kata hiyo ya Nyalikungu Katibu wa CCM wilaya ya Maswa Mwl. Mathius Filagisa alimtaka Diwani wa kata hiyo kuhakikisha wakati wa ziara za viongozi wa juu wa Chama na CCM viongozi wote na watendaji wote wa Serikali wawepo katika ziara na mikutano   ili kujibu hoja zitakazoibuka wakati wa mikutano hiyo.

Tunatekeleza Ilani ya CCM kuleta makaimu kwenye ziara za waheshimiwa haifai mjitahidi mwaunge mkono viongozi wenu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao wawapo majimboni” alikazia.

Read more

Serikali yakasirishwa na tabia ya uongozi wa mgodi

Na Issa Mtuwa, Tarime

Waziri wa madini Mhe. Doto Biteko ameonyesha kukerwa na tabia zinazofanywa na uongozi wa juu wa mgodi wa Acacia North Mara kwa serikali  kwa kushindwa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyo andaliwa baina ya pande hizo mbili, licha ya baadhi ya vikao kuongozwa na Waziri wa Madini lakini viongozi wa juu wa mgodi ambao ndio wafanya maamuzi na watekelezaji wa maagizo ya serikali wamekuwa wakishindwa kuhudhuria.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko wa tatu kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa TSF kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Kigoma Malima.

Biteko amesema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara jana Machi 5, 2019 katika kijiji cha Nyamongo  wilayani Tarime ikiwa  ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi kwenye migodi ya North Mara na Buhemba. Biteko amesema anakerwa na tabia za uongozi wa mgodi huo kwa kushindwa kuhudhuria mara kwa mara mikutano mbalimbali ya ndani na ile ya hadhara badala yake wamekuwa wakituma wawakilishi.

“Kuanzia leo, haki ya mungu, haki ya mungu, haki ya mungu, mimi Waziri wa Madini leo ni siku ya mwisho kukaa na hawa wawakilishi kwenye vikao, hasa kama hivi vinavyo husu hatima ya maisha ya watu alafu wafanya maamuzi hawahudhurii. Niwambie ukweli nasikitishwa sana na tabia hii. Hawa walipo sio saizi yangu, kama ni hawa hata mimi ningewaleta maafisa wa wizara tena wale wanaolingana na hawa.

Wanataka wawepo hadi afike Rais…!? nendeni mkawambie kwenye ngazi ya Wizara mimi ndio wamwisho katika kufanya maamuzi, kama mimi nipo kwa nini wao wasiwepoo…!? nyinyi mliokuja hapa nendeni mkawaambie hii ni mara ya mwisho wasifikiri serikali hii wanaweza kuiweka mfukoni, haikubaliki, hii tabia lazima ifike mwisho” alisema Biteko huku akisikitika sana.

Amesema kwa ujumla hafurahishwi na namna mambo yanavyokwenda mgodini hapo ukilinganisha na migodi mingine. Mgodi wa North Mara umezungukwa na matatizo mengi sana yakiwemo ya malipo yafidiaza wananchi, utiririshaji wa maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya wananchi.

Read more

Biteko-Maisha ya watu yanathamani kubwa kuliko shughuli za Mgodi

Na Issa Mtuwa, Tarime

Serikali imesema itaufunga mgodi wa North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya kuhifadhia maji (topesumu) (Tailings Storage Facility -TSF) ya mgodi huo kuelekea kwenye makazi ya watu.

Hayo yamesemwa leo machi 5, 2019 na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa topesumu (TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na baadae na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyamongo wilaya ya Tarime kuzungumzia hatima ya malipo ya fidia za wananchi waliohamishwa kupisha shuguli  za mgodi.

Biteko amesema serikali hairidhishwi na namna mgodi wa North Mara kwa jinsi wanavyo zingatia swala la utunzaji wa maji yenye sumu kwenye (TSF) zao. Amesema serikali inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja, na kwamba maisha ya mtu mmoja ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.

“Naomba niseme ukweli, tena kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya Dkt. John Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu chochote. Thamani yamaisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko kinachochibwa hapa. Nitoe rai kwa mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu, hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo, nitafunga mgodi mpaka pale mtakapo tekeleza jambo hili” alisema Biteko.

Kwa upande wa uongozi wa mgodi umesema, utatekeleza agizo hilo na kwamba juhudi za kudhibiti topesumu kuelekea kwenye makazi ya watu limepewa kipaumbele na kwamba ndani ya muda huo litakuwa limekamilika.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna wa Madini Mha. David Mlabwa na Afisa Madini mkoa wa Mara Mha. Nyaisara Mgaya, wengine ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara wakiongwa na mwenyekiti wake ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Mara bwana Adam Kigoma Malima.

Ziara hiyo inafuatia vikao mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala mbalimbali yanoyo husu mgodi huo likiwemo swala la udhibiti wa maji yenye sumu (topesumu) yanayo lalamikiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi huo, kikao cha kwanza kilifanyika Januari 19, chini ya makatibu wakuu wa wizara saba ((Madini, Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi, TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji)) ambapo serikali ilitoa miezi nane kutekeleza maagizo yaliyopewa.

Read more

Wanawake Wizara za Madini, Nishati, GST waadhimisha siku yao na wenye Mahitaji Maalum

Na Nuru Mwasampeta,

Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Wanawake kutoka Wizara za Madini, Nishati na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), leo Machi 5, wamefanya Matendo ya Huruma kwa kuwatembelea watu wenye mahitaji maalum na kutoa mahitaji mbalimbali ya kijamii.

Wawakilishi wa wanawake kutoka Wizara za Madini, Nishati na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wakiwa njiani kuelekea katika vituo vya watu wenye mahitaji maalumu katika Kata ya Buigiri, Halmashauri ya Chamwino, Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Vituo vilivyotembelewa na wanawake hao ni Shule ya watoto wasioona na kituo cha watu wazima wasioona vilivyopo katika Kata ya Buigiri, Halmashauri ya Chamwino jijini Dodoma kwa lengo la kujumuika pamoja kabla ya kilele cha maadhimisho hayo ambayo hufanyika tarehe 8 Machi, kila mwaka.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo mara baada ya kuwasili katika shule ya watoto wasioona, Afisa Utumishi kutoka Wizara ya Madini  anayeshughulikia masuala ya wanawake Remida Ibrahim, amesema kutokana na wanawake kuguswa  zaidi na masuala ya kijamii ndio  sababu  iliyopekea  ujumbe huo  kufika kituoni hapo kwa  ajili ya kutoa mahitaji mbalimbali ili yaweze kuwasaidia watoto hao.

Remida amewaasa wanafunzi hao ambao asilimia tisini na tano wana ulemavu wa kutokuona kusoma kwa bidii ili kujikwamua  na maisha yao ya baadaye na kuwataka kuelewa kuwa Serikali inatambua uwepo wao na kwamba iko bega kwa bega katika kuhakikisha inachangia katika kutoa elimu bora.

Wanawake Watumishi wa Wizara za Nishati na Madini katika picha ya pamoja walipojumuika na watu wenye mahitaji maalumu ikiwa ni moja kati ya matukio katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Historia Mputa, ameushukuru ujumbe wa wanawake kutoka katika makundi hayo kwa kutoa kipaumbele kwao na kuamua kutembelea kituo hicho na kueleza, “vituo vya watoto wenye mahitaji maalum ni vingi sana lakini mmeona vema kututembelea mahala hapa tunashukuru sana”, amesisitiza.

Baada ya kukamilisha shughuli ya kukabidhi zawadi katika kituo hicho, ujumbe hao ulihamia katika kituo cha wasioona watu wazima ambapo   walipata fursa ya kusikia historia fupi ya kituo na kusikiliza kero mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na baadaye kukabidhi bidhaa zitakazosaidia katika kupata mahitaji kwa siku kadhaa.

Akizungumzia uanzishwaji wa kituo hicho, Mwenyekiti Msaidizi wa kituo hicho Yusuph Matando, amesema kituo hicho kilianzishwa mnamo mwaka 1992 na Mwalimu Keneth D. Mwanampalila na kufadhiliwa na Kendall Lee wa nchini Uingereza kwa lengo la kuwasaidia watu wasioona kujipatia mahitaji yao kwa shughuli za kilimo cha mbogamboga badala ya watu hao kuombaomba mtaani.

Yusuph amebainisha changamoto  zilizopo kituoni hapo kuwa ni hicho kuwa ni pamoja  kutokufikiwa na huduma ya umeme ,ugumu katika upatikanaji wa mbegu, uhaba wa mipira ya maji kwa ajili ya kumwagilia bustani zao pamoja na maji yanayopatikana katika kisima hicho kutokutosheleza mahitaji ya kijiji.

Siku ya wanawake duaniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka ikilenga kusisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuelimisha kuhusu jitihada zinazofanywa na serikali na taasisi zisizo za serikali katika kuwaendeleza wanawake na kuhamasisha utekelezaji wa Sera na mipango ya Serikali yenye lengo la kudumisha amani, usawa na maendeleo.

Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Mwaka 2019 ni “ Badili fikra, fikiria usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu’’.

Read more

Biteko ahimiza wana Bukombe kuchapa kazi na kuchukia umaskini

Na Issa Mtuwa Bukombe

Kazi kubwa ya kiongozi yeyote aliepewa dhamana, ana wajibu wa kuhahikisha anabadilisha maisha ya watu kwa kushugulikia matatizo na kero zao kwenye eneo alilopewa, na ndio maana Rais Magufuli kila kukicha anawaza juu ya changamoto za Watanzania na anawahiza viongozi wote kushugulikia matatizo ya Watanzania.

Akiongea na Wananchi wa vijiji mbalimbali katika kata ya Ushirombo na Bugelenga wilaya ya Bukombe katika muendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Geita, jana Machi 2, 2019, Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema “dhana” ya kushugulika na matatizo ya watanzania katika wizara yake na wananchi wa jimbo lake kwa ujumla ndiyo inayomfikisha kila mara kwenye maeneo mbalimbali nchini kushugulikia matatizo yao ikiwemo Bukombe.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akizungumza na Wananchi wakiwemo Wachimbaji wadogo wa Madini katika kijiji cha Busonjo kata ya Busonjo wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita.

Akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mkange kata ya Bugelenga, Biteko amewambia wananchi hawanabudi kuuchukia umaskini kwa kujishugulisha na kufanya kazi kwa bidii. Amesema hata yeye wanae muona leo, ni mtu alietokana na familia maskini na ndio maana hata kipindi akisoma walikuwa wakimuita “Doto Maziwa”, kwa kuwa sehemu kubwa ya gharama za masomo yake ilitokana kwa kuuza mazima hivyo kila familia ijitume kufanya kazi kwa kutumia fursa zilizopo.

“Ndugu zangu, ngoja niwaambie ukweli, nimetembea nchi nyingi sana, kuna nchi zina watu masikini zaidi kuliko hata sisi, mi niwaombe kama wewe huna ulemavu wa kukufanya ushindwe kufanya kazi ndugu zangu tuchapeni kazi, tuibadilishe Bukombe yetu” alisema Biteko.

Biteko amewaambia wananchi kuwa hataona fahari kama matatizo ya Watanzania katika sekta ya madini na wananchi wake wa Bukombe wanaendela kuwa na changamoto na hazipatiwi majawabu. Amesema kama ambavyo ameweka mkazo katika kuondoa kila aina ya kero kwenye sekta ya madini ndivyo hivyo hivyo anahakikisha anaondoa kero za wananchi wa Bukombe katika sekta Afya, Elimu, Miundombinu, Maendeleo ya jamii, vijana, wanawake na walemavu.

Katika ziara yake Biteko amekagua shuguli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuweka jiwe na msingi katika majengo ya zahanati, kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za waalimu, kukagua madaraja na miundombinu ya barabara katika kuhakikisha ilani ya  chama cha Mapinduzi inatekelezwa.

Read more

Biteko asema ufahari wa kiongozi uwe kwenye kuwatumikia Wananchi

Na Issa Mtuwa, Bukombe

Waziri wa Madini ambae pia ni Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko amesema viongozi wa serikali wajibu wao mkubwa ni kuwatumikia wananchi, dhamana yao ya madaraka kama haina msaada kwa wananchi haina maana, yeye kama waziri na mbunge kama shida na matatizo ya wanchi wa Bukombe na sekta nzima ya madini atashindwa kuzitatua  haina maana ya uwepo wake na ndio maana anaumiza kichwa kila siku kuhakiksha sekta ya Madini inaleta tija kwa taifa huku pia wananchi wa Bukombe wanaozungukwa na Madini ya dhahabu pia wananufaika.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiongea kwenye kikao cha ndani na viongozi waandamizi wa Wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu wilayani humo.

Biteko ameyasema hayo leo tarehe 02/03/2019 akihutubia wananchi kwa nyakati tofauti tofauti wilaya ya Bukombe katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa geita ambapo pamoja na mambo mengine anasikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi na zinazo husu sekta ya madini.

“Rais Pombe Joseph Magufuli amekuwa akituambia mara kwa mara  nendeni mkawahudumie Watanzania muwaondolee kero, ule mfumo wa watu wakiwa ofisini anakuwa Boss Magufuli hataki mfumo huoo, anataka mabosi wawe wananchii, wananchi wasikilizwe kama wana jambo litatuliwe na kama haliwezekani waambiwe ukweli sio kudanganya” amesema Biteko.

Amesema Bukombe inautajiri wa madini ya dhahabu na endapo kila mmoja atajishugulisha katika kutafuta kwa kutumia fursa zilizopo maisha ya wana Bukombe yataboreka, ametoa wito kwa vijana, akina mama na kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi ajishugulishe.

Aidha, ameongeza kwa kusema wajibu alionao kama Waziri wa Madini ni kuhakikisha kodi na malipo mbalimbali yanayohusiana na madini yanalipwa tena kwa wakati, na jamii zinazo zunguka migodi zinachangia maendeleo ya wananchi hao kama sheria inavyo wataka.

‘Msiwakamue sana hawa wawekezaji kwa sababu wanatumia fedha nyingi katika kuwekeza, sio kila shida ya kijiji, kata au wilaya mnakimbilia kwa mwekezaji wa mgodi hapaaaaaa….! lakini sizui kuwaomba msaada lakini kuwe na kipimo yale ya kisheria waacheni watekeleze ili wasipo timiza mimi nitawabana” aliongeza Biteko.

Read more

Prof. Msanjila ashikilia msimamo wa serikali kuhusu mgodi wa North Mara

Na Issa Mtuwa, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Madini imesema bado imeshikilia msimamo wake kuhusu muda uliotolewa kwa Mgodi wa North Mara kutekeleza maagizo ya serikali yaliyotolewa kwenye kikao cha Januari 9, 2019 kuhusu Bwawa la kuhifadhi topesumu (Tailings Storage Facility -TSF).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila Februari 26, 2019 wakati akizungumza katika mahojiano maalum ofisini kwake Jijini Dodoma, mara baada ya kufungua kikao cha pamoja baina ya wajumbe kutoka serikalini na wajumbe kutoka Mgodi wa North Mara waliokutana kujadili kuhusu hatua zilizofikwa na Mgodi katika kutekeleza maagizo hayo.

Amesema serikali haitoongeza muda zaidi ya ule uliotolewa katika kikao cha awali, na kusema kuwa msimamo wa serikali utabaki kuwa hivyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila mwenye tai katikati kushoto akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho wakati akichangia.

“Ndugu zangu katika kikao hiki kilenge kutoa majibu ya utekelezaji wa maagizo ya serikali kama yalivyowasilishwa kwenye kikao cha Januari 9, 2019, ni kwa kiasi gani mmetekeleza maagizo hayo,” alisema Prof. Msanjila.

Serikali kupitia kikao chake cha Januari 9, 2019 chini ya Makatibu Wakuu wa wizara saba (Madini, Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi, TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji) kilitoa maagizo mbalimbali yakiwemo: Kujenga TFS mpya na Kukarabati TFS iliyopo kwa aajili ya kudhibiti mtiririko wa topesumu, maagizo ambayo mgodi ulipewa kuyatekeleza kwa muda wa miezi Nane (8) kuanzia Januari 9, 2019.

Akiongoza wakati wa mjadala wa uwasilishaji wa mada mbalimbali wa kikao hicho, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Prof. Hudson Nkotaga aliwataka North Mara kueleza namna gani wametekeleza maagizo ya serikali kwa lengo la kupata mrejesho wa utekelezaji.

Kuhusu utekelezaji wa maagizo hayo, Meneja Usalama, Afya na Mazingira Reuben Ngusaru, kutoka mgodi wa North Mara amesema mgodi umeanza kutekeleza maagizo hayo na bado wanaendelea kutekeleza maagizo hayo na hata kikao cha tarehe 26 Februari ikiwa ni moja mkakati wa kutekeleza maagizo hayo kwa ufanisi.

Akizungumzia kuhusu hatua zilizochukuliwa na mgodi kudhibiti uvujaji unaoendelea kwenye (TSF) mpaka kufikia siku ya kikao cha Februari 26, mambo yaliyotekelezwa ni pamoja na: Kuondoa mawe na kusafisha mtaro uliopo upande wa Kaskazini mwa TSF. Kuvukiza (evaporation) maji yaliyotokana na uchenjuaji wa mawe yanayotengeneza tindikali asili (PAF Rock) (leachate water) badala ya kuyapeleka yote kwenye TSF na Programu zote zilizokuwepo za kupunguza maji katika TSF bado zinaendelea.

Aidha, kuhusu utekelezaji uliofikiwa katika kutekeleza agizo la Serikali la kujenga TSF mpya (Construction of a new TSF) Reuben amesema mpaka kufika tarehe 26 Februari, mgodi umefanya utambuzi wa eneo linalofaa kwa ajili ya ujenzi wa TSF mpya (Site Identification) nau sanifu wa awali (Conceptual design) ambapo usanifu wa awali umefanyika na ujenzi wa TSF mpya unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani milioni 45 za tope sumu (tailings) kavu kwa kadirio la ongezeko la tani 8200 kwa siku.

Maagizo ya serikali kwa mgodi wa North Mara yalitokana na ukaguzi uliofanywa na serikali kwenye mgodi huo uliohusisha timu kutoka ofisi mbalimbali za serikali zikiwemo, NEMC, Mkemia Mkuu wa Serikali, Wizara ya Madini, na Wizara ya Afya, uliopelekea kutolewa kwa maagizo yaliyolenga kudhibiti uharibifu wa mazingira uliokuwa unafanywa na mgodi.

Read more

Leseni za migodi mikubwa kutolewa karibuni

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Madini inakamilisha taratibu za utoaji wa Leseni kwa Migodi Mikubwa ambazo hazijawahi kutolewa nchini, huku migodi hiyo ikitarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof.Simon Msanjila akimsikiliza mmoja wa Viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipokutana na viongozi wa Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi ofisini kwake, jijini Dodoma.

Viongozi hao walikutana na Prof. Msanjila Februari 26, kwa lengo la kujitambulisha, kuelewa shughuli za serikali upande wa sekta ya madini, kupata uelewa kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Madini na namna pande hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kuendeleza sekta husika.

Prof. Msanjila aliwakaribisha viongozi hao kwenye sekta ya madini huku akiwataka kuzishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini hususani katika shughuli za uongezaji thamani madini na kueleza kuwa, suala hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo serikali inayapa kipaumbele ikiwemo ujenzi wa vinu vya kusafisha na kuyeyusha madini.

Akizungumzia Sheria Mpya ya Madini ya Mwaka 2017, Prof. Msanjila amesema hakuna tatizo lolote katika utekelezaji wa sheria na kueleza kuwa, serikali kupitia wizara ya madini inapokea wawekezaji wengi wenye utayari na nia ya kuwekeza nchini huku utekelezaji wa sheria hiyo ukiwa si kikwazo na kuongeza kwamba, “hakuna mahali ambapo serikali inatengeneza sheria kwa ajili ya kumkandamiza mfanya biashara”.

“Hakuna tatizo lolote kwenye sheria ya madini. Hata wageni huwa tunakaa nao tunawaelimisha na wanatuelewa vizuri.  Kama kuna dosari ni vitu ambavyo tunaweza kuvirekebisha na tayari tumekwishakufanya hivyo kwa baadhi ya maeneo,” alisema Prof. Msanjila.

Mmoja wa viongozi wa jumuiya Jumuiya ya Watendaji Wakuu wa Taasisi Binafsi, Francis Nanai ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, akizungumza jambo.

Aidha, katika kikao hicho Prof. Msanjila alitoa ushauri kwa viongozi hao kujitangaza zaidi kuhusu kazi zao huku akiwataka kutafuta wasaa kwa ajili ya pande hizo mbili kukutana ili wizara iweze kutoa elimu zaidi kwa Jumuiya hiyo kuhusu sekta ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji zilizopo.

Pia, Prof. Msanjila alisema kuwa suala la kuaminiana linaweza kujengwa huku akiwataka watanzania kuwa wazalendo na namna wanavyotumia fedha za umma. Prof. Msanjila alizungumzia jambo hilo baada ya mmoja wa viongozi hao kueleza kuwa, bado kuna hali ya kutokuaminiana baina ya serikali na taasisi binafsi.

Kwa upande wake, mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo, Francis Nanai ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited amemweleza Prof. Msanjila kuwa, kama viongozi wa umoja huo, wamezipokea changamoto zilizotolewa kwao na Prof. Msanjila ikiwemo ushauri wa kukutana na wizara kwa lengo la kupata ufafanuzi na elimu  zaidi  kuhusu sekta ya madini.

Read more

Prof. Msanjila aongoza wadau kujadili rasimu Kanuni Uanzishwaji wa Masoko ya Madini nchini

Na Nuru Mwasampeta,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila ameongoza kikao kilicholenga kupokea maoni juu rasimu ya kanuni za uanzishwaji wa masoko ya madini nchini.

Washiriki wa kikao cha kutoa na kupokea maoni juu ya rasimu ya uanzishwaji wa kanuni za masoko ya madini nchini wakisubiri kuanza rasmi kwa kikao hicho.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara kimewakutanisha, Makamishna Wasaidizi wa Wizara, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) John Bina, viongozi wa shirikisho hilo pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo kutoka mikoa ya kimadini nchini.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa kikao, Prof. Msanjila alisema maoni ya wajumbe hao ni muhimu kwa watanzania na taifa kwa ujumla katika kuboresha kanuni hizo.

Aidha, Msanjila amebainisha kuwa, wadau wengine wamekwisha kutoa maoni yao katika makundi tofauti tofauti na pia maoni mengine yanaendelea kupokelewa kwa njia ya maandishi na kuwataka maoni hayo yakamilishwe ndani ya kipindi cha wiki moja.

Kabla ya kupokea maoni hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara, Edwin Igenge aliwasilisha rasimu ya kanuni hizo ili kutoa uelewa wa kile wanachopaswa kuchangia katika kutoa maoni yao.

Akiwasilisha rasimu hiyo, Igenge alisema hii ni sheria ndogo inayotokana na sheria mama ya madini. “Kanuni hizo zinatungwa kwa mujibu wa kifungu cha 27 (C) kifungu kidogo cha pili pamoja na kifungu cha 129 cha sheria ya madini,” amesema Igenge.

Aidha, amesema mahala patakapo kuwa na soko la madini kutakuwa na huduma zote zinazotakiwa ili kurahisisha ubadilishwaji wa fedha na  madini kama vile mabenki, ofisi za mamlaka ya Mapato (TRA), ofisi za masuala ya ulinzi na usalama, pamoja na ofisi mbalimbali za serikali.

Igenge amesema baada ya kukamilika na kupitishwa kwa kanuni hizo zitatafsiriwa na kupatikana katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wote kuelewa kanuni na mwongozo wa masoko ya madini.

Wajumbe wa mkutano wa kutoa na kupokea maoni juu ya rasimu ya uanzishwaji wa kanuni za masoko ya madini nchini wakifuatilia mada.

Akizungumzia baadhi ya vipengele vilivyopo katika rasimu hiyo, Igenge alisema sehemu ya kwanza inahusika na utangulizi yenye vifungu 3 cha kwanza ni jina la kanuni ambapo litaitwa ‘Kanuni za masoko za mwaka 2019’, pili ni maelezo ya wapi kanuni hizo zitatumika na kuratibiwa na kipengele cha mwisho kitatoa tafsiri ya maneno mbalimbali yanayotumika ndani ya kanuni hizo.

Sehemu ya pili ya kanuni inahusika na uanzishwaji wa masoko yenyewe, ambapo masoko yataanzishwa katika maeneo yenye tawala za mikoa na kuipa maelekezo Tume ya Madini kuhakikisha wanashirikiana na tawala za mikoa katika kuanzisha masoko hayo.

Aidha, alielezea msingi wa kwanza ni msingi wa uwazi, msingi wa matangazo ili watu waweze kujua madini yanauzwa na kununuliwa wapi, msingi wa haki ambao utazuia manunuzi haramu ya madini, lakini pia msingi wa mwendelezo ikiwa na maana masoko hayo kuwa ni masoko ya kudumu na si ya msimu.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Wachimbaji wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, ameiomba serikali kuyafanyia kazi maoni yaliyotolewa na wawakilishi wa wachimbaji wadogo ili kupata kitu kitakachokubalika na jamii nzima ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini.

Aidha, alikiri kufurahishwa na ufafanuzi uliotolewa katika kila kipengele cha rasimu ya kanuni za uanzishwaji wa masoko ya madini na kukiri kwamba wanaamini kuwa serikali ina nia njema na wananchi wake.

Read more

Wachimbaji madini watakiwa kuwa na mpango wa ufungaji Mgodi

Na Greyson Mwase, Pwani 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amewataka wachimbaji wa madini  ya ujenzi  aina ya kokoto katika mkoa wa Pwani kuwa na Mpango wa Ufungaji Mgodi utakaotumika kama mwongozo wa kuhakikisha mazingira yanaachwa yakiwa katika hali salama mara baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) pamoja na Kamishna-Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki (katikati) wakiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na mgodi unaomilikiwa na Sisti Mganga uliopo katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani tarehe 21 Februari, 2019 ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya kokoto, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji. Kushoto ni mmiliki wa mgodi huo, Sisti Mganga.

Profesa Kikula aliyasema hayo leo tarehe 21 Februari, 2019 katika nyakati tofauti alipofanya ziara yake katika migodi  inayojishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ujenzi aina ya kokoto iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani yenye lengo la kutembelea wachimbaji wa madini hayo pamoja na kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Profesa Kikula katika ziara hiyo akiwa ameambatana na Kamishna – Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, wataalam kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma, Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi wa Lugoba pamoja na waandishi wa habari, Profesa Kikula alitembelea migodi ya Sisti Mganga, Gulf Concrete Company Limited na  Yaate Company Limited iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo.

Akizungumza katika nyakati tofauti mara baada ya kutembelea migodi hiyo, Profesa Kikula aliwataka wamiliki wa migodi kuhakikisha wanakuwa na mipango ya ufungaji migodi mapema badala ya kusubiri mpaka shughuli za uchimbaji madini zinapomalizika hivyo kufanya zoezi la ufungaji wa migodi kuwa gumu huku wakiacha mazingira yakiwa hatarishi.

“Ninapenda kuwakumbusha kuwa suala la kuwa na Mpango wa Ufungaji wa Migodi ni la lazima kulingana na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake, hivyo ninawataka kuhakikisha mnakuwa na mpango ili kuhakikisha mashimo hayaachwi wazi,” alisema Profesa Kikula.

Awali akiwa katika mgodi unaomilikiwa na Sisti Mganga Profesa Kikula  alielezwa mafanikio ya mgodi huo ikiwa ni pamoja na  kokoto za mgodi huo kutumika katika ujenzi wa daraja la Mto Wami uliopo mkoani Pwani,  reli ya kisasa ya standard gauge na utengenezaji wa marumaru kwa ajili ya soko la ndani ya nchi.

Katika hatua nyingine Mganga alitaja changamoto zinazoukumba mgodi huo kuwa ni pamoja na tozo kubwa kutoka katika halmashauri na tozo nyingine zinazotozwa na kijiji cha Kihangaiko  pasipo kuwa na risiti pamoja na ukosefu wa vifaa vya kisasa.

Profesa Kikula alisema kuwa, suala la tozo litafanyiwa kazi kwa kuliwasilisha mamlaka za juu kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kusisitiza kuwa nia ya Serikali kupitia Tume ya Madini, ni kuhakikisha wachimbaji wa madini hususan wadogo wanafanya kazi katika mazingira mazuri yenye faida kubwa huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini pasipo vikwazo vyovyote.

Mmoja wa watendaji wa mgodi wa kuzalisha kokoto wa Gulf Concrete Company Limited, ulipo katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani, Ramesh Annlahamadu (kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati) mara alipofanya ziara kwenye mgodi huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya kokoto, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji tarehe 21 Februari, 2019. Kulia mbele ni Kamishna – Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki.

Wakati huo huo, akiwa katika mgodi wa uzalishaji wa kokoto wa Gulf  Concrete Limited Profesa Kikula alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa mgodi huo kuhakikisha wanarekebisha kasoro ya mazingira kwa kuhakikisha vumbi linalotoka wakati wa shughuli za uchimbaji wa kokoto halisambai kwani linaathiri wananchi  wa vijiji vya jirani katika mgodi huo.

Alisema ni vyema wakazingatia Sheria ya Mazingira kwani vumbi mbali na kuathiri wananchi wanaoishi katika vijiji vya jirani linaweza kuathiri wafanyakazi wa mgodi huo.

Aidha, alituaka mgodi huo kuendelea kuhakikisha unatoa huduma kwa jamii inayozunguka mgodi huo na kutumia huduma za ndani ya nchi kama vile bidhaa pamoja na ajira kwa wazawa.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula akiwa katika mgodi wa kuzalisha kokoto wa Yaate Co. Limited, mbali na kuupongeza mgodi kwa kuaminiwa na kupewa kazi ya kusambaza kokoto kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge unaotelekezwa na kampuni ya Yapi  Merkezi na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii inayouzunguka mgodi huo pamoja na ajira, aliutaka mgodi huo kuendelea kununua bidhaa/huduma kutoka kwa wananchi.

“Kutoa huduma bora kwa wananchi wanaozunguka mgodi kunaboresha mahusiano na kupunguza migogoro ya mara kwa mara inayoweza kujitokeza.

Awali akielezea mafanikio ya mgodi, Mkurugenzi Mtendaji wa Yaate Co. Limited, Eugen Mikongoti alisema  mradi umenufaisha watanzania wengi kwa kuchangia maendeleo ikiwa ni pamoja na ulipaji  wa zaidi ya shilingi bilioni 1.31 ambazo zimelipwa kama ushuru wa madini  kati ya kipindi cha mwezi Juni, 2018 hadi Januari, 2019 na shilingi milioni 338.8 zilizolipwa kama mrabaha.

Alieleza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na utoaji wa fursa za ajira kwa watanzania hususan vijana wanaozunguka mgodi na kuziwezesha kampuni zinazomilikiwa na wazawa kushiriki katika miradi mikubwa  hivyo kuzijengea uwezo wa kitaalam na kupata fursa.

Mikongoti alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuwezesha maendeleo ya wanachi wanoishi karibu na mgodi kupitia huduma za jamii ambapo mpaka  sasa mgodi huo  unaendelea na ujenzi wa nyumba za watumishi na kuhudumia wananchi katika zahanati iliyopo mgodini.

Katika hatua nyingine Mikongoti alipongeza kazi kubwa zinazofanywa na Tume ya Madini chini ya Mwenyekiti wake Profesa Kikula ikiwa ni pamoja na kuwatembelea, kuwapa elimu na kutatua changamoto mbalimbali.

Read more

EoI-Consultancy Services for Carrying Out Scoping of Tanzania Extractive Industries Performance and Production of TEITI Report for the Fiscal Year 2016/17 and 2017/18

1. The Government of the United Republic of Tanzania through the Ministry of Minerals (MoM) has received financial support to meet eligible payments for Provision of Consultancy Services for Carrying out Scoping of Tanzania Extractive Industries performance and Production of TEITI report for the Fiscal Years 2016/17 and 2017/18. The reports will cover reconciliation of payments from extractive industries and revenue received by the Government during the period of July 1, 2016 to June 30, 2017 and July 1, 2017 to June 30, 2018.

2. Tanzania joined EITI in February 2009 with an objective of promoting transparency and accountability in its natural resources. The process in Tanzania is lead by a Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Committee consisting of civil society organizations, government agencies and extractive companies. In October 2017 EITI Board declared Tanzania as having achieved meaningful progress with EITI standard. EITI meaningful progress means that the country has made significant progress for annual disclosure and reconciliation of all revenues from its extractive sector, helping citizens to see how much their country receives from oil, gas and mining companies. Tanzania under the TEITI Committee has produced eight (8) TEITI reports since it joined EITI in February 2009. The last report covering the fiscal year 2015/16 was published in April 2018.

>>Read More>>

 

Read more

Waziri Biteko ataka Jengo la kituo cha pamoja cha biashara kukamilika ifikapo Aprili mwaka huu

 • ASEMA ATAKAYEKAMATWA NA TANZANITE MARUFUKU KUINGIA TENA NDANI  YA UKUTA.
 • ATAKA MINADA YA TANZANITE ILIYOSIMAMISHWA SASA IANZE.
 • SUMA JKT msitucheleweshe,

ifikapo Aprili mwaka huu jengo liwe limekamilika. Jengo hili la Kituo cha Pamoja cha Biashara ya Madini litajengwa na SUMA JKT kwa gharama ya shilingi 1,148, 259,500.

 • Tunafunga CCTV camera kuzunguka ukuta. Lengo la uwekaji wa mitambo hii ni kuimarisha ulinzi kwa ajili ya rasilimali na watu  waliomo na wanaoingia ndani ya ukuta. Tunataka tukiwa Dar es Salaam na Dodoma tuwaone. Rai yangu kwenu ni kila mtu awe mlinzi wa rasilimali madini na kwa upande wafanyabiashara wapende kununua katika mkondo sahihi madini yao ili kuepuka usumbufu.

  Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatilia jambo baada ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Pamoja Cha Biashara, eneo la Mirerani. Wengine wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula. Kulia ni mwanzo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila.

 • Tarehe 30 Januari 2019 nilisaini Kanuni za Mirerani Controlled Area. Nakuagiza Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Kamati ianze kazi tuanze kusimamia Kanuni hizi.
 • Tumekuja kumkabidhi mkandarasi site  hakuna kulala mpaka madini yalinufaishe taifa.
 • Mkandarasi wa CCTV nakukabidhi kazi hii nataka ufanye kazi yenye ubora na kumaliza ndani ya Mkataba tuliokubaliana bila kuongeza hata sekunde.
 • Tulieni tunakuja na utaratibu wa mashine. Wizi ni lazima  tuutoe kwenye fikra zenu.
 • Wakati ukuta huu unajengwa  kulikuwa na siasa nyingi. Wapo waliouita jela lakini leo mapato yameongezeka mnalipa kodi vizuri. Tunakwenda kuondoa vikwazo kwenye biashara ya madini. Mtalipa mrabaha usiozidi asilimia 7. Deni limebaki kwenu.
 • Suala kujengwa ukuta lilikuwepo tangu mwaka 2002 lakini haukujengwa. Ametokea mzalendo Rais Magufuli tumejenga. Asingekuwa yeye ingebaki hadithi nyingine.
 • Nitawashangaa sana baada ya jitihada hizi tunazozifanya mapato yakishuka. Mkuu wa Mkoa wasimamieni hawa  huku mkiwalea.
 • Jengo la biashara ya madini limejengwa mahususi ili kurahisisha uthaminishaji wa madini pindi yanapovunwa hapa ndani.Ma broker tumewajengea nyumba hii hapa tuheshimu taratibu.
 • Jengo hili la biashara na uthaminishaji litatumika kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo na wenye madini ili kuweza kufanya biashara sehemu salama na  kwa uwazi. Kama alivyosema Katibu Mkuu, jengo hili limegharimu shilingi milioni 85.
 • Tanzania Tumegeuka kuwa darasa kwa jirani zetu  na nchi nyingine kutokana na namna tunavyosimamia Sekta ya madini. Watu wa mataifa wanakuja kujifunza lakini pia Tunapata mialiko mingi kutoka nchi mbalimbali ili tuwaeleze namna tunavyosimamia rasilimali hii.
 • Tutumie madini yetu kubadilisha maisha yetu. Tunataka siku moja watoto wa Simanjiro wasome kwenye shule nzuri, watumie barabara nzuri, akina mama wapate huduma za afya sehemu nzuri. Haya ndiyo mambo tunayoyataka. Siasa nyingine siyo agenda ya watanzania.
 • Tanzania ni nchi ya 3 Afrika kwa kuzalisha dhahabu, ya pili Afrka kwa madini ya vito na ya 18 duniani kwa kuzalisha dhahabu lakini utajiri huu wa madini na maisha ya watanzania havifanani.
 • Minada ya Tanzanite iliyosimamishwa sasa ianze.

  Waziri wa Madini Doto Biteko akizindua Jengo la Biashara na Uthaminishaji wa Madini, Mirerani. Wengine wanaoshuhudia ni Viongozi mbalimbali wa Mkoa, Wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

 • Chama Cha MAREMA unganeni,tukigundua hamna msaada tutawaacha.
 • Hatutaki kukwamishana,tunataka kusimamia sekta..Wachimbaji acheni majungu, toeni taarifa za kweli.
 • Hatutawatoza fedha nyingi lakini mtatuonesha vitambulisho. Natoa maelekezo kuanzia leo tozo za kiingilio zitatozwa kwa wale wanaofanya kazi. Ndani ya mgodi watalipa shilingi elfu 50,000 kwa mwaka, Mabroker watalipa shilingi elfu 30,000 kwa mwaka na wana Appolo, wafanyabiashara wadogo kama wachekechaji, mama lishe watalipa shilingi 20,000 kwa mwaka.
 • Naomba Wizara ya Kazi kupitia Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi  ( WCF) na  Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuja kujifunza na kutengeneza muundo ambao unaendana na aina ya kundi hili ili kuweza kulihudumia kundi hili la wachimbaji wadogo wa madini.
 • Katika mkutano wa wadau wa tarehe 22 Januari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  pamoja na mambo mengine alisisitiza kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara ya Madini Tanzania na pia kuimairisha usalama. Tuliagizwa kiualisia kuanza mara moja kuweka mifumo ya kidigitali kuzunguka ukuta.

ALIYOYASEMA MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI

 • Mkoa wa Manyara ni mkoa mkubwa wenye Tanzanite ambayo haipo  popote duniani. Unapokuwa Mkuu wa Mkoa kama huu lazima uweze kudhibiti Tanzanite. Nataka nikamwambie Mhe. Waziri  tuna madini mengi zaidi ya Tanzanite.
 • Kwenye madini lazima nibanane na wewe. Nisipodhibiti sina cha kumwambia Mhe. Rais. Tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha kodi zinapatikana. Babati tuna rubi ya kutosha. Nataka nikwambie ifanye Babati kuwa Makao Makuu ya Madini nchi nzima.
 • Waziri kazi yetu ni kusimamia mnayoyapitisha juu ili yasipotoshwe na yatekelezwe kwa Mujibu wa Sheria.
 • Rais alituelekeza tupitie na kukubaliana kuweka mazingira mazuri ya kuboresha Tanzania kupitia sekta hii. Tulikaa kujadili mabadiliko makubwa. Nina hakika mabadiliko makubwa yanakuja.
 • Waziri tumeshakubaliana na wadau hawa mambo mengi. Tunataka kuona mengi kutoka kwao.
 • Ni matarajio yangu kuwa shughuli nyingi zitafanyika ndani ya jengo la Kituo cha Biashara.
 • Nakipongeza Chama Cha Marema kwa kufanya kazi nzuri. Ukipingana na Serikali hakuna unachoweza kufanya. Hakuna aliye juu ya serikali.

ALIYOYASEMA MWENYEKITI WA  KAMATI YA KUDUMU YA  BUNGE YA NISHATI NA MADINI, DUSTAN KITANDULA

 • Rais ameonesha uungwana, mpira uko kwenu. Hisani pekee kwake ni ninyi kulipa kwa kuonesha kwa vitendo. Yale yaliyokuwa yakiwakwaza yameondoka, mlipe kodi.
 • Tumewaona mkiwa katika maandamano ya kumuunga mkono Rais. Kikao cha Januari 22 kilionesha dhamira ya Rais na aliahidi kutekeleza  kero zenu ndani ya kipindi kifupi. Tuliletewa miswada kufanya mabadiliko.
 • Nampongeza Rais kwa kuondoa vikwazo kwa wachimbaji wadogo. Serikali imedhamiria kuhakikisha sekta hii inalinufaisha taifa.

ALIYOYASEMA MBUNGE WA SIMANJIRO JAMES OLLE  MILLYA

 • Kuwepo kwa ukuta huu hakumaanishi hakuna majirani. Kwa mujibu wa Sheria na  taratibu zake  nakuomba  Mhe  Waziri migodi hii isaidie jamii. Wanaofanya uchimbaji wakumbuke vijiji vya jirani.
 • Baada  ya kujengwa ukuta bado wanapanga mistari mirefu. Wanaongia ndani wakaguliwe mapema.
 • Bado kuna changamoto kwako Mhe. Waziri na  Katibu Mkuu ikiwezekana muwaletee maji.

ALIYOYASEMA MWENYEKITI WA MAREMA, JUSTIN NYARI

 • Rais ameweka alama ambayo haitapotea, alama ambayo itakumbukwa kwa vizazi na vizazi.
 • Ujenzi wa kituo cha pamoja cha biashara ni  mwanzo mzuri kwetu na mkoa wetu na nchi yetu, wachimbaji wako tayari kushirikiana na serikali.
Read more

Wadau wa Tanzanite Mirerani waandamana kumpongeza Rais Magufuli

 • NI KUFUATIA KUPUNGUZA KODI ZA MADINI NA KUSIKILIZA KERO ZAO 
 • WAAHIDI KULIPA KODI

Maandamamo hayo yaliyofanyika Februari 16, yalihusisha wadau wote wa madini ya Tanzanite wanaofanya shughuli za uchimbaji ndani ya ukuta wakiwemo wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa, yakilenga kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kupunguza kodi za madini, kusisitiza suala la uanzishwaji wa masoko ya madini na  mwongozo wa uongezaji thamani madini.

 • ALIYOYASEMA MKUU WA MKOA WA MANYARA, ALEXANDER MNYETI

Mhe. Rais ametuagiza mlipe kodi kwa hiari. Msipofanya hivyo mtalipa kwa nguvu. Lipeni kodi.

 • Nimepokea maandamano yenu na tutaandaa barua Maalum kwenda kwa Mhe. Rais kufikisha salam zenu.
 • Mnajua safari ya tulikotoka, tulipofika na tunaweza kutengeneza njia nzuri ya tunakotaka kufika. MAREMA inakwenda vizuri.
 • Mirerani acheni umbeya, kuna uongo mwingi, punguzeni uongo taarifa zenu zinatupotosha.
 • Mnajichonganisha wenyewe na serikali. Waajiri mnawatelekeza wafanyakazi wenu wakiugua wanakuwa mzigo wa serikali.

ALIYOYASEMA MWENYEKITI WA MAREMA, MKOA WA MANYARA, JUSTIN NYARI

 • Maandamano haya yanalenga kutoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kuondo kodi ambazo hazikuwa rafiki kwa wachimbaji.Tunampongeza Mhe. Rais kwa  kupeleka bungeni Muswada kwa hati ya dharura, ujenzi wa masoko  ya madini na mwongozo wa uongezaji thamani madini.
 • Wachimbaji wako tayari  kushirikiana na serikali kukuza uchumi kupitia sekta ya madini.

ALIYOYASEMA MBUNGE WA SIMANJIRO, JAMES OLLE MILLYA

Tunampongeza Rais kwa kuondoa VAT ya asilimia 18 kwenye sekta. Ameacha asilimia 7 tu huu ni upendo wa pekee.

Baada ya Januari 22 Mkuu wa Mkoa aliitisha kikao Januari 25 na migodi yote imeanza kufanya kazi na matunda yameanza kuonekana.

ALIYOYASEMA MKUU WA WILAYA YA SIMANJIRO, MHANDISI ZEPHANIA CHAULA

 • Kama Mhe. Rais amewaheshimu na ninyi mumheshimu, heshima hiyo ni kulipa kodi.

ALIYOYASEMA MWAKILISHI WA TANZANITE AFRIKA KWA NIABA YA WACHIMBAJI WA KATI, WILFRED MUSHI

 • Tunampongeza Mhe.Rais, kwa mara ya kwanza ameondoa kero za wachimbaji wa  Kati ambazo hazipishani sana na wachimbaji wadogo.
 • Nuru ya Tanzanite imenga’rishwa, Mirerani sasa inakwenda kutengeneza  tanzanite mpya.

ALIYOYASEMA MWAKILISHI WA TANZANITE ONE, FEISAL SHABHAI

 • Tunampongeza Rais Magufuli kwa kutambua uwepo wetu, kusikiliza kilio chetu na kuondoa changamoto zetu.
 • Tunatambua maendeleo yanayotarajiwa kutokana na rasilimali hii ambayo lengo ni kuwanufaisha watanzania na vizazi vijavyo viweze kuishi katika mazingira salama.

ALIYOYASEMA MWAKILISHI WA TAMIDA, HUSSEIN GONGA 

 • Tulikuwa na tashwishi kubwa juu ya kufanya biashara ya madini. Mhe Rais alisikia kilio cha wachimbaji na dealers.
 • Hawezi kuwepo mnunuzi bila mchimbaji, tulikuwa na changamoto ya kusafirisha madini ghafi.
 • Rais Magufuli ameondoa kodi ya VAT ya asilimia 18, ilikuwa kero kubwa.
 • Rais hajapoteza, mafanikio  atayaona tunamhakikishia. Biashara ya madini  sasa inakuwa nzuri.

ALIYOYASEMA MWAKILISHI WA BROKER,

 • Tunampongeza Rais kwa suala la ujenzi wa masoko ya madini nchi nzima, serikali itakusanya kodi ya kutosha.
 • Niwaombe Ma broker, kufanya uthamini wa madini, sitamwombea radhi broker yoyote atakayevunja sheria.

ALIYOYASEMA MWAKILISHI WA WANA APOLLO

 • Tunampongeza Rais Magufuli kwa kututambua wana Appolo na kutupa nafasi ya kuwasilisha kero zetu. Tunaahidi kushirikiana katika nyaja zote. Wana Appolo ndiyo wachimbaji wa tanzanite.
 • Tunayo sababu ya kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Manyara, leo wana Appolo tunapewa vipaza sauti. Kwa muda mrefu wana Appolo hawakuwa na sehemu ya kuzungumza
Read more

Watumishi Wizara ya Madini watakiwa kutoa huduma stahiki kwa wadau wake

Na Nuru Mwasampeta,

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka watumishi wa wizara kuhakikisha wanatoa huduma stahiki kwa watanzania ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu

Aidha, amewataka watumishi hao, kila mmoja kulingana na majukumu yake  kujipima utendaji wake binafsi kabla ya kungoja vipimo vilivyopo kwa kuzingatia miongozo na taratibu za Utumishi wa Umma.

Naibu Waziri Nyongo, ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua Mkutano wa Wafanyakazi wa Wizara kwa niaba ya Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyekuwa katika utekelezaji wa majukumu mengine ya kitaifa.

Aidha, Nyongo amewaeleza watumishi hao kuwa wanao wajibu wa kuzingatia dhana nzima ya kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa manufaa ya Taifa na watanzania kwa ujumla.

Pamoja na rai ya kila mtumishi kujipima utendaji wake, Nyongo amewakumbusha kuzingatia matumizi ya Opras katika kutekeleza na kujipima namna kila mmoja anavyotekeleza majukumu yake. Amesema Opras ni hitaji la kisheria kila mmoja hanabudi kulizingatia.

“Wote tnafahamu kuwa ipo miongozo mbalimbali inayotumika katika utendaji wetu wa kila siku hivyo ni rai yangu kuwa tuizingatie ili kutoa huduma stahiki kwa watanzania kwa ufanisi na viwango vinavyotakiwa.” Alisisitiza .

Aidha, Nyongo alieleza wajibu wa Wizara kwa kuzingatia miongozo iliyopo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kazi yatakayowawezesha watumishi wake kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Pamoja na hilo, alikazia suala la kuwaendeleza watumishi, kuwajengea uwezo katika kazi zao pamoja na kushughulikia na kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.

Zaidi ya hapo, Nyongo alisisitiza suala la kuimarisha mawasiliano baina ya watumishi wa wizara lakini pia mawasiliano baina ya wizara na taasisi zilizo chini ya wizara na wadau wote wa sekta ya madini ili kuongeza ufanisi hatimaye kuongeza tija katika utendaji wa wizara.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu

Kuhusu kuzingatia suala la afya za watumishi, Nyongo ameipongeza wizara kwa kuratibu mara kwa mara suala la upimaji wa afya kwa hiari kwa watumishi wake na kutoa rai kwa kila mmoja kutumia fursa hiyo na kujitokeza kupima afya zao kwa hiari.

Akihitimisha hotuba yake,  Nyongo amewasihi  watumishi wa wizara kuongeza juhudi na kuelekeza fikra zao katika kupelekea serikali ya viwanda kutokana na ukweli kwamba sekta ya madini ni mojawapo ya nguzo ya uchumi wa viwanda na kuwa itasaidia katika kuifikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati ifikapo 2025.

Kutokana na uwepo wa wastaafu katika mkutano huo, Nyongo alitumia fursa hiyo kuwapongeza sana wastaafu watano walijumuika katika mkutano na hafla fupi ya kuwaaga na kuwatakia maisha mema katika hatua nyingine ya maisha.

Kwa uande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Nsajigwa Kabigi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila alisema mkutano huo umelenga katika kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji ya wizara ili kupata mwelekeo wa namna bora ya kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu na shughuli za kila siku za wizara pamoja na kubadilishana mawazo, kufurahi pamoja na kuwaaga wastaafu.

Read more

Kampuni ya Jervois yaonesha nia kuwekeza Kabanga

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Nikel- Colbat, Kabanga.

Baadhi ya Wataalam wa Wizara ya Madini wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Madini na wawakilishi wa kampuni ya Jervois Mining Limited.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu kufuatwa kwa Sheria na taratibu kwa wenye nia ya kuwekeza katika Sekta ya Madini na kueleza kuwa, kwa upande wa Wizara, inafanya jitihada za kuondoa urasimu kwenye uwekezaji katika sekta husika.

“ Tunataka mwekezaji mwenye nia anapoonesha dhamira ya kuwekeza baada ya taratibu zote kukamilika basi aanze mara moja,” amesema Waziri Biteko.

Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo Balozi Mstaafu Andrew Mcalister, amesema kuwa, nchi ya Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat kutokana na ubora wake na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini ikiwemo uwazi.

Mbali na Waziri Biteko, wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na wataalam wengine wa wizara.

Read more

Nyongo ataka Watumishi Madini kuepuka rushwa

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Naibu wa Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka watumishi wa Wizara ya Madini kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwemo kuzuia rushwa katika sehemu zao za kazi kwani suala hilo linasababisha migogoro kwenye sekta ya madini.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika tarehe 13 Februari, 2019.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo Februari 13 wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi la wizara na kuongeza kuwa, serikali inafuatilia mienendo ya watumishi wa sekta husika.

Alisema kuwa, wako watumishi wanaomiliki leseni kwa dhuluma suala ambalo pia limechangia kuwepo kwa migogoro mingi kwenye sekta na kueleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli anasisitiza suala la kuzingatia maadili katika utumishi wa umma na hususan katika sekta ya madini.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo alilitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha linajiendesha kwa faida na kusisitiza kuwa Serikali inataka gawio.

Aidha, aliutaka uongozi wa STAMICO kuzingatia maslahi ya watumishi kwa kutoa motisha mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa shirika kwa ujumla.

Akizungumzia mafanikio makubwa katika Sekta ya Madini, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ni pamoja na mabadiliko ya Sheria ya Madini na kusisitiza kuwa kwa Afrika Tanzania imekuwa mfano kama nchi bora inayosimamia vyema rasilimali za madini.

“Sifa bora kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini zisitufanye tubweteke bali tuendelee kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu huku tukizingatia maadili ya kazi,” alisema Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini Sanslaus Nyongo na Viongozi Waandamizi wa Wizara pamoja na Viongozi wa TUGHE Taifa na TUGHE Tawi la Wizara ya Madini, wakiimba wimbo Maalum wa kuhamasisha Umoja wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.

Nyongo aliendelea kusema kuwa, kama moja ya mikakati ya kutoa motisha kwa watumishi, uongozi wa Wizara unatakiwa kutoa fursa mbalimbali kwa watumishi ikiwa ni pamoja na mafunzo.

Wakati huo huo, akizungumza kwa niaba ya watumishi, Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Madini, Joyce Manyama alisema kuwa watumishi kupitia chama chao watafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Wizara ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na viwanda vingi vya uongezaji thamani madini ili kufikia malengo ya Serikali kupitia mchango wa Sekta ya Madini kwenye ukuaji wa Pato la Taifa.

Aidha, Manyama alichukua fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Shirika la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Nchini (FEMATA), wachimbaji wadogo kwa kuitisha mkutano uliofanyika hivi karibuni baina yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli

Vilevile, aliishukuru Wizara kwa kuanzisha mfumo mpya wa utunzaji wa kumbukumbu za Wizara unaojulikana kama Electronic Filing Management System ambao utaboresha utunzaji wa kumbukumbu na kurahisisha upatikanaji wake pindi zinapohitajika.

Pia, aliiomba Wizara kuendelea kusimamia zoezi la upandishwaji wa vyeo ili watumishi waweze kupandishwa vyeo kulingana na sifa wanazokuwa nazo.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema kuwa Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kazi ili kila mtumishi afanye kazi kwa ubunifu zaidi.

Aliongeza kuwa, kwa sasa Wizara inafanya vizuri ambapo Sekta ya Madini imekua kwa asilimia 18 huku mchango wa sekta kwa fedha za kigeni ikiwa ya tatu nyuma ya Kilimo na Utalii na kueleza kwamba, pamoja na mafanikio hayo, bado kuna rushwa na kukosekana uadilifu.

Read more

Biteko ameitaka bodi ya STAMICO kuhakikisha inachangia pato la taifa kabla ya mwezi Juni, 2019

Na Nuru Mwasampeta,

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuhakikisha kuwa sekta ya Madini kupitia shirika hilo inaongeza mchango wake kwa pato la taifa kwa kulipa mrabaha na kodi mbalimbali za serikali na kuongeza wigo wa ajira za watanzania kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi katika kuendesha shirika hilo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza jambo kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Stamico na Menejimenti ya Shirika hilo wakati wa hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Stamico zilizopo maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 12 February, 2019.

Biteko alisema anautambua wazi umuhimu wa Bodi hiyo katika kufanya maamuzi, kupitia Sheria na sera zinazohusiana na uendeshaji wa shirika hilo na ndio maana uundwaji wa bodi hiyo ulipewa kipaumbele mara tu baada ya yeye kuteuliwa kushika wadhifa huo wa Waziri wa Madini.

Ameendelea kwa kusema, uteuzi wao haukuwa rahisi na ulizingatia uwezo na uzoefu wa wajumbe katika kutekeleza majukumu ya Bodi pamoja na uzalendo walionao kwa taifa na kuwasihi kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wazuri wa shirika hilo kwa manufaa ya Taifa.

Alisema, kigezo kikubwa kilichotumika katika uteuzi huo ni kuangalia ubunifu wa mtu mmoja mmoja, mahali anakofanyia kazi au alipofanyia kazi, “ninyi katika ofisi mlizopita mliacha mambo makubwa Imani yetu wizara ni kuwa mtatumia ubunifu huo katika kusimamia na kubadilisha taswira ya shirika letu”. Alisisitiza.

Alikiri kuwa Serikali imewaamini na kuwapa mamlaka ya kusimamia Shirika hilo tunaamini mnaweza ndio maana katika wengi mliteuliwa  ninyi.

Akibainisha majukumu ya Bodi hiyo, Biteko alisema ni pamoja na Kuisimamia Menejimenti ya Shirika katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku kwa mujibu wa Sheria.

Kusimamia sera ya Shirika na kuanzisha mifumo ya udhibiti katika utekelezaji wa Sera hizo, Kupitia na kuidhinisha miundo ya Maendeleo ya Watumishi wa Shirika, kupitia na kuidhinisha mishahara na marupurupu ya watumishi wa shirika pamoja na kuanzisha mfumo mzuri wa kutoa gawio kwa wana hisa wa Shirika.

Mkurgenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi akijitambulisha kabla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Biteko alilipongeza shirika kwa hatua nzuri waliyoifikia katika kutekeleza baadhi ya miradi ikiwa ni pamoja na uchimbwaji na uuzwaji wa makaa ya mawe wa Kabulo, kuanza uchenjuaji wa mabaki ya mchanga wa dhahabu katika eneo la mradi wa dhahabu wa Buhemba, kuzalisha na kuuza kokoto Ubena Zomozi, kuimarisha usimamizi wa miradi ya ubia ya TanzaniteOne na Buckreef na kampuni tanzu ya STAMIGOLD, na kuratibu shughuli za kuwaendeleza wachimbaji wadogo.

Biteko alikiri kuwa Serikali imechoshwa na kupata hasara kupitia katika shirika hilo, na kusema badala ya miradi inayoanzishwa katika shirika hilo kuzalisha faida inazalisha madeni na kuliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya pesa.

Akitoa mfano wa watu wawili waliokwenda vitani, mmoja akiwa na moyo wa vita bila silaha na mwingine akiwa na silaha bila moyo wa kupigana Biteko alisema ni dhahiri yule mwenye moyo wa vita atashinda na kuitaka bodi hiyo kuiga mfano huo katika kutekeleza majukumu yake.

Aliendelea kusisitiza kuwa Serikali anaamini wajumbe wa bodi hiyo wanao moyo wa kupigana vita bila kubeba silaha na kuwasihi kuanzia hapohapokutekeleza majukumu yake, “anzeni hivyo mlivyo, ipeni Serikali sababu ya kuishawishi serikali kuleta pesa”. Alisisitiza.

Serikali ya awamu ya tano inafanya vitu vilivyoshindikana, Vilee vitu ambavyo watu wanasema haviwezekani ndivyo vinavyofanyika nasi tunaamini mmeteuliwa ili kurekebisha madhaifu ya Stamico yaliyoshindikana kwa muda mrefu, wakurekebisha na kulifanya shirika la Stamico kuwa bora ni ninyi bodi pamoja na  menejimenti ya shirika.

Aidha, ameitaka bodi hiyo kumtafuta popote pale mtu yeyote wanayedhani anaweza kulisaidia Shirika kuzalisha faida na vile vile amewataka kumpeleka mtu yeyote mwenye cheo chochote anayelirudisha shirika hilo nyuma ili atafutiwe kazi nyingine ya kufanya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa, Mej. Gen (Mstaafu) Michael Isamuyo akizugumza jambo mara baada ya Waziri wa Madini Doto Biteko kuzindua rasmi bodi hiyo na kuipa meno kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya Shirika.

“Haiwezekani shirika kutoka kuundwa kwake mwaka 1972 halijawahi kutoa gawio, haiwezekani lipo kwa ajili ya nini? Lakini watu wakizunguka wanalipwa posho lakini mwenye mali hapati kitu”. Biteko aling’aka.

Aidha, Biteko aliwataka wanabodi hao kubadilisha wimbo wa lawama unaosbabaishwa na shirika hilo na kuimba wimbo wa sifa, amekiri kutaka matokeo na sio stori. Alisema kwa namna anavyowafahamu wajumbe hao wa bodi wakishindwa kulibadilisha shirika hilo kwa awamu hii yeye binafsi atakuwa wa kwanza kuomba shirika hilo lifutwe.

Aliwataka wajumbe hao wa bodi kuifanya Stamico kuwa eneo la mataifa mengine kujifunzia namna bora ya kuendesha mashirika ya umma ikiwa ni pamoja na kuwaacha kufanya maamuzi yao kama shirika.

Alimuhakikishia Mwenyekiti wa bodi hiyo kuifanyia kazi changamoto ya uhaba wa wafanyakazi unaolikabili shirika mara tu baada ya kuurekebisha muundo wa uongozi wa shirika hilo aliokiri kuwa na vyeo vingi kulioko uwezo na uzalishaji wa shirika.

Aliitaka bodi hiyo kuhakikisha inabadilisha fikra na taswira ya shirika kwa kubadilisha namna ya kufikiri kwa watendaji wake ili wafikiri kibiashara zaidi na si kimishahara.

Alisisitiza kuwa anataka aibu ya Stamico ya miaka mingi iondolewe sasa na kama sio sasa basi sasa hivi, na kuwataka kutoa taarifa wakati wowote wanapoona wanakwama katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha, Biteko aliitaka bodi hiyo kwenda kufuatilia suala la hisa za kampuni ya Tanzania Gemstone Industries Ltd (TGI) iliyosajiliwa mnamo mwaka 1969 ikiwa ni kampuni Tanzu ya Stamico na kutoliingizia faida yeyote shirika licha ya uzalishaji kufanyika na kuwa na umiliki wa hisa za kampuni ya Mundarara Mining Ltd kwa asilimia 50.

Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa wizara haitaingilia masuala ya shirika lakini jicho lake litakuwa Stamico kutokana na kwamba kushindwa kwa shirika ni kushindwa kwa wizara na kushindwa kwa wizara ni kushindwa kwa Waziri kitu ambacho hatakikubali.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa Bodi ya Stamico na Menejimenti ya shirika wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mej. Gen (Mstaafu) Michael Isamuyo alitoa shukrani zake kwa uteuzi uliofanywa wa kumpatia fursa ya kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo ambapo alieleza kuwa aliyeteuliwa mwezi Disemba Tarehe 6 na baadaye kuteuliwa kwa wajumbe wengine wa bodi ambao amekiri watafanya kazi kubwa kwa shirika na taifa.

Alikiri kuwa wajumbe wa bodi wametoka katika maeneo mbalimbali wakiwa na ujuzi na uzoefu tofauti tofauti ambao wakikaa pamoja katika kutekeleza majukumu watafanya kitu kikubwa na kusababisha mabadiliko makubwa kwenye Shirika kubwa la Taifa la madini.

Amekiri kuwa masuala yote waliyoagizwa watatekeleza kama walivyoelekezwa “Majukumu yetu tunayafahamu lakini haya majukumu ni muongozo tu, naamini tutatumia uwezo wetu, tutatumia akili zetu, uzoefu tulionao katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi kuhakikisha kwamba zile changamoto ambazo zipo na zitakazoendelea kujitokeza tunazigeuza kuwa fursa na tunazitatua”. Alisisitiza.

Amesema katika ameneo yote changamoto hazikosekani, lakini kufanya kazi kwa mazoea ndiko kunakorudisha nyuma mafanikio “huu mfumo wa kufanya kazi kwa mazoea bila ubunifu wowote utaturudisha nyuma alisema na haya ndiyo masuala uliyotushauri” amekiri kuwa bodi yake ina utashi huo na watahakikisha kuwa wanakuwa na ubunifu wa hali ya juu na kuifanya Stamico kujikwamua kutoka mahali walipo.

Akijibu hoja ya kuwa na moyo wa vita kabla ya kupata silaha, Isamuyo alisema yapo matatizo mengi kwa shirika ikiwa ni pamoja na suala la uhaba wa mitaji pamoja na wafanyakazi, na kuiri kuwa kutokana na moyo wa vita walionano changamoto hizo zitageuzwa na kuwa fursa.

Akitolea mfano ujenzi wa nyumba zenye vioo zilivyowafanya wezi kuichukulia ujenzi huwa kama fursa kwa kuwarahisishia kuingia  ndani ndani ya nyumba bila shida lakini pia hiyo kuwa ni fursa kwa wajenzi na wafanyabiashara kuzalisha kuzalisha nondo na kujengea ili kuwapa wezi kazi ya kufanya pindi wanapotaka kuvamia majengo ya watu kwa lengo la kuwaibia. Isamuyo ameahidi kugeuza changamoto za Stamico kuwa fursa na kulipeleka shirika mbele.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini a Taifa, Kanali Sylvester Ghuliku Akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo jijini Dodoma.

Amemuhakikishia Waziri wa Madini kuwa bodi hiyo haitashindwa kazi, “Hatutashindwa kwa sababu hamkushindwa kututeua, mlikuwa na majina mengi yenye sifa zinazofanana na zetu lakini hamkushindwa kututeua na kwa sababu ninyi hamkushindwa kututeua na sisi hatutashindwa kuhakikisha kwamba tunasonga mbele katika kutekeleza majukumu ya shirika” alisisitiza .

Amekiri kwamba kabla ya kuomba silaha ya mizinga sehemu yeyote tutahakikisha kwamba silaha ndogo zitafanya kazi na kuhakikisha adui anapigwa, amesema watumishi waliopo lazima wahakikishe kuwa wanafanya kazi na kuliletea shirika faida bila kutegemea mtu kutoka eneo lingine. Alisema waajiliwa wengine wakipatikana waje kuongeza nguvu lakini si kwa sababu waliopo wameshindwa kazi.

Kuhusu Mikataba isiyokuwa na tija, Isamuyo amewataka wanasheria kuhakikisha mikataba inayoingiwa sasa hivi inazalisha faida tofauti na ilivyokuwa awali.

Kuhusu agizo la kuhakikisha shirika linatoa gawio kwa serikali, Isamuyo amesema agizo hilo limetolewa kwa mwanajeshi, hilo ni agizo na litatekelezwa vizuri sana na kuahidi kufuatilia suala la kushughulikia hisa za kampuni ya Tanzania Gemstone Industries Ltd(TGI) ambayo ni kampni tanzu ya Stamico itashughulikiwa ipasavyo.

Ameiomba serikali kushughulikia changamoto za msingi na masuala mengine yanayopaswa kutatuliwa na wizara kufanyiwa maamuzi mapema ikiwa ni pamoja na suala la ajira mpya na kukiri kuwa shirika ni la kibiashara hivyo kila dakika inayopotea inazalisha hasara kwa shirika.

Uzinduzi wa Bodi hiyo ulishirikisha viongozi wote waandamizi wa wizara ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliyewataka Bodi hiyo kwenda kufanya kazi na kuithibitisha Imani ya serikali kwao, Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi.

Read more

Mlolongo wa kodi sekta ya madini kuondolewa-Biteko

Na Samwel Mtuwa, Mwanza 

Mchakato wa kuondoa Mlolongo wa Kodi na Tozo kwa wachimbaji Wadogo wa Madini upo katika hatua za mwisho na ndani ya muda mfupi ujao, baadhi ya kodi na tozo hizo zitafutwa katika Sekta ya Madini.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na baadhi ya Watendaji Waandamizi wa Wizara na Wadau wa warsha hiyo, mara baada ya kuifungua.

Hayo yamesemwa Februari 11, 2019 na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifungua Warsha kuhusu namna ya kuanzisha masoko ya madini nchini inayofanyika Jijini Mwanza.

Warsha hiyo inayolenga katika kutoa elimu ya namna ya kuanzisha masoko ya madini imeanza leo na itafanyika kwa siku mbili hadi Februari 12, 2019 ikiwashirikisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo.

Waziri Doto ameeleza, warsha hiyo ni muhimu kwa wizara  nan  nchi kwa ujuml kutokana na  lengo ililojiwekea wizara hivi sasa ya kuhakikisha mchango wa sekta ya madini kwenye Uchumi na maisha ya wananchi unaongezeka.

Ameongeza kuwa, ana imani kwamba kwa kuondoa baadhi ya tozo na kodi kwa wachimbaji wadogo zitawezesha kuziba mianya ya utoroshaji wa madini na hivyo kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa.

Waziri Biteko amefafanua kuwa, Mchakato wa kuandaa Kanuni za Masoko ya madini umezingatia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujifunza kutoka nchi zenye masoko ya madini.

Ameeleza kuwa, Halmashauri zinaowajibu wa kuendelea kuwajenga, kuwalea, na kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa sababu mazao yao ndio yanayotegemewa kuuzwa katika masoko hayo.

Ametaka njia pekee ya kujibu na kutolea ufanunuzi wa taarifa potofu ni kutumia maelekezo yaliyopo katika sheria ya Madini ya 2010 na Marekebisho yake ya 2017.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na baadhi ya Watendaji Waandamizi wa Wizara na Wadau wa warsha hiyo, mara baada ya kuifungua.

“Pamoja na changamoto zilizopo kwenye usimamizi wa  sekta ya Madini nchini namshukuru Mungu kwani rasilimali hizi hazijageuka kuwa balaa,” amesema Biteko.

Katika hatua nyingne, amesema kuwa, Maafisa madini watakaokuwa kikwazo katika uanzishwaji wa masoko ya madini watachukuliwa hatua za kisheria.

Wadau katika warsha hiyo ni kutoka Mikoa ya Mwanza Dodoma, Arusha, Geita, Shinyanga, Mara, Manyara, Kagera, Tabora, Singida, Mbeya, Morogoro,na Ruvuma.

Warsha hiyo imeandaliwa na wizara ya Madini kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.

Read more

Naibu Waziri Nyongo afungua warsha kujadili mpango ufungaji migodi

Na Nuru Mwasampeta, Dodoma

Kufuatia kutokuwepo kwa mwongozo wa ufungaji wa migodi pindi shughuli za uchimbaji zinapofikia kikomo, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeandaa rasimu ya mwongozo ambayo inajadiliwa na wadau kutoka Taasisi za Kiserikali na wadau mbalimbali wa madini zikiwemo makampuni za uchimbaji kutoka Chamber of Mine.

Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Dr. Abdurahman Mwanga akiwasilisha rasimu ya ufungaji wa migodi kwa wadau waliojumuika kwa lengo la kuiboresha.

Akifungua warsha ya kujadili rasimu hiyo, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amewataka washiriki na waalikwa wote kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa ili kuuboresha mwongozo huo.

Amesema, mwongozo huo utawasaidia wawekezaji watakaokuwa na nia ya kuwekeza nchini kujua taratibu na namna wanavyopaswa kufanya pindi wanapoandaa mpango wao wa kufunga mgodi ambao kwa mujibu wa taratibu, unapaswa kuwasilishwa serikalini kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji nchini.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 206 ya Sheria ya Madini ya 2010 kama ilivyorekebishwa mwaka 2107, kila mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini wa kati na mkubwa anatakiwa kuandaa mpango wa ufungaji migodi na kuwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa leseni ambaye ataandaa mkutano wa kamati ya kitaifa ya ufungaji migodi ambayo hupitia, kuujadili na kupitisha mpango huo.

Naibu Waziri Nyongo ameongeza kuwa, Mpango huo wa ufungaji wa migodi unaeleza kwa kina namna migodi itakavyofungwa na kurudisha eneo katika hali inayoweza kufaa kwa matumizi mengine.

Aidha, amesema kuwa, mipango hiyo huelezea namna wamiliki wa migodi watakavyowawezesha wafanyakazi pamoja na jamii inayozunguka eneo la migodi waliokuwa wakifanya kazi katika migodi hiyo pindi migodi hiyo inapofungwa.

Amesema mwongozo huo utaweka wazi namna bora ya kuandaa mpango wa kufunga mgodi pamoja na kuhifadhi mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Madini na Sheria nyingine zinavyoelekeza.

Naibu Waziri, Nyongo amesema anatarajia mpango huo uendane na mazingira ya Tanzania na mwongozo ikiwemo kuhakikisha kuwa unajali vizazi na vizazi vitakavyofuata baada ya madini kuisha na kusema “Lazima tujue kwamba kuna vizazi vitakavyokuja baadaye, madini tunayo ni rasilimali yetu, lakini lazima tujue kuna vizazi vingine vinakuja,”

Kamishna Msaidizi wa migodi na Maendeleo ya Madini Ali S. Ali akijitambulisha kabla ya ufunguzi wa warsha ya maandalizi ya mwongozo wa ufungaji wa migodi unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa, uchimbaji unaendana na uharibifu wa mazingira, lakini ni lazima kuwaza namna ambavyo vizazi vinavyokuja vitakavyoishi.

Amebainisha kuwa, hatua hiyo ni muhimu ambayo kama taifa linategemea kikao hicho kiwe na manufaa kwa taifa la leo na vizazi vijavyo.

Akizungumza na washiriki wa warsha hiyo inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ufundi (Veta) kwa siku mbili, Nyongo ameupongeza uongozi wa Tume ya Madini kwa hatua nzuri waliyoifikia katika kuandaa mwongozo huo.

Aidha, nyongo amesema Tume ya Madini kwa kushirikiana na Wizara ya Madini kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), iliandaa rasimu ya kwanza ya mwongozo wa huo ambao unajadiliwa na wajumbe hao ili wamekutana ili kupata mwongozo unaokubalika kwa taifa.

Aidha, Nyongo ameeleza kuwa, maoni yaliyotolewa na wadau kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa Mkutano wa kisekta uliofanyika mwezi Januari, yanafanyiwa kazi na hivyo kuahidi kuwa wadau wa madini na taifa watapata mrejesho wa kile kilichowasilishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Dkt. Abdurahman Mwanga amesema katika nchi mbalimbali duniani suala la ufungaji wa migodi limekuwa ni gumu, hivyo, mwongozo unaoandaliwa utaonesha nini hasa kinapaswa kufanyika mara baada ya mgodi kufungwa.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Neoroika, Honest Mrema, ulioko katika mkoa wa Songwe unaomilikiwa na Shanta mining, amesema rasimu hiyo ni nzuri na imetoa nafasi nzuri kwa wadau kukaa meza moja na watendaji wa serikali kujadili changamoto zinazowakabili kuhakikisha wanapochimba wanapata kile wanachotarajia.

Wadau mbalimbali wa madini walioshiriki katika warsha ya maandalizi ya mwongozo wa ufungaji wa migodi unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Dr. Abdurahman Mwanga akiwasilisha rasimu hiyo tayari kwa majadiliano.

Aidha, amebainisha kuwa, madini ni rasilimali, na pindi yanapochimbwa kuna uharibifu unatokea hivyo katika uharibifu kurudisha mazingira katika hali yake ya kawaida ni kuifanyia ardhi hivyo masuala muhimu.

Akielezea umuhimu wa maandalizi ya mwongozo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini (TAWOMA), Eunice Negele, amesema rasimu inayojadiliwa itaisaidia jamii pamoja na vizazi vijavyo kwa kuwa, itawafanya wawekezaji kuhakikisha wanaiacha ardhi yenye kufaa kwa matumizi mengine tofauti na uchimbaji.

Read more

Wizara yakutana na Kampuni zinazokusudiwa kujenga vinu vya kuyeyusha, kusafisha madini

Na Asteria Muhozya,

Katika jitihada za kuhamasisha shughuli za Uongezaji Thamani Madini Nchini, kuanzia tarehe 6 hadi 7 Februari, 2019, Wizara ya Madini ilikutana na baadhi ya Kampuni zinazokusudiwa kujenga Vinu vya Kuchenjua, Kuyeyusha na Kusafisha Madini nchini.

Lengo la wizara kukutana na kampuni hizo ilikuwa ni kuangalia uwezo wa kifedha, teknolojia na Utayari wao. Kampuni hizo ni kutoka Ndani na Nje ya Nchi.

Serikali inahamasisha shughuli za uongezaji Thamani madini kufanyika nchini ili kuongeza pato, ajira na uhuishaji wa teknolojia kwa wazawa.

Read more

Waziri Biteko akutana na Watumishi Tume ya Madini

Na Greyson Mwase,

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019 amekutana na watendaji na watumishi wa Tume ya Madini katika makao makuu ya Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akisikiliza mapendekezo mbalimbali yaliyokuwa yanawasilishwa na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani)

Kikao hicho  kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa  Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi na  Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.

Wengine ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi wa  Tume ya Madini.

Katika kikao hicho Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha kamati tendaji kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha maombi mbalimbali ya leseni za madini na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.

Read more

Biteko apangua hoja hofu ya wadau kuwekeza nchini

Na Nuru Mwasampeta,

Waziri wa Madini, Doto Biteko amewatoa hofu Wawekezaji wa Nje na kueleza kuwa, Mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2017, hayana lengo la kuwakandamiza isipokuwa yamelenga katika kuifanya rasilimali madini kuwanufaisha wote, wawekezaji na watanzania.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akiagana na Balozi wa Canada nchini mara baada ya kumaliza kikao baina yao. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Aliyasema hayo Januari 4, 2019 katika kikao baina yake na Balozi wa Canada nchini Pamela O’Donnel, ambacho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal.

Akielezea lengo la kuonana na uongozi wa juu wa Wizara, Balozi O’Donnel alisema amefika ili kupata uelewa wa mabadiliko mbalimbali yaliyotokea katika sekta ya madini pamoja na maeneo mengine ili kuwatoa hofu wawekezaji kutoka katika taifa lake wanaopenda kuwekeza nchini.

Pamoja na nia yake ya kupata ufumbuzi kwa masuala ya Sheria ya Madini, Balozi O’Donnel alihoji kuhusu masuala mengine ikiwemo utawala wa kisheria, mikataba ya madini, kodi na tozo mbalimbali pamoja na upatikanaji wa vibali vya kufanya kazi nchini kwa wananchi kutoka nchini Canada.

Akijibu hoja hizo, Waziri Biteko aliwataka wawekezaji kutoka nchini Canada kutokuwa na wasiwasi kwa mabadiliko hayo na kuwataka kutembelea ofisi ya madini ili kupata ufafanuzi wa jambo lolote lenye utata katika kufanikisha nia njema ya kuwekeza nchini. “Tupo kwa ajili yao, wasisite kupata ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu sekta ya madini,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa, mataifa mbalimbali duniani yanafanya mabadiliko katika masuala mbalimbali na kueleza kuwa, si vibaya kwa Tanzania kufanya mabadiliko kwa jambo lolote ambalo lina manufaa kwa taifa.

Waziri Biteko alieleza kuwa, madini ni rasilimali inayokwisha, hivyo ni muhimu madini yanapochimbwa yawaletee faida watanzania  na pindi  yatakapokwisha wajivunie rasilimali madini iliyokuwepo kutokana na maendeleo yaliyoletwa na Madini hayo kama vile barabara bora, shule, ujenzi wa vituo vya Afya na masuala mengine ya maendeleo.

“Sheria ya awali ilikuwa hainufaishi taifa na watanzania ndio maana mabadiliko yanafanyika.Mabadiliko ni kitu kizuri, tunahitaji rafiki atakayesababisha mabadiliko kutokea hivyo hawana haja ya kuogopa, tunawakaribisha kuwekeza” alisisitiza Biteko.

Akifafanua zaidi, Biteko alieleza kuwa, mabadiliko ya sheria ya madini yamekuwa yakifanyika kulingana na sera inayoongoza. Alieleza kuwa tangu kutungwa kwa sheria ya madini mwaka 1998 mabadiliko yamefanyika kwa awamu mbili yaani mwaka 2010 na mwaka 2017 lengo likiwa ni moja tu, rasilimali madini iweze kulinufaisha taifa na Watanzania.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto), akizungumza jambo wakati wa kikao na Balozi wa Canada nchini Pamela O’Donnel (wa pili kutoka kushoto).

Aidha, alibainisha kuwa mabadiliko ya kisheria yanayotokea katika sekta ya madini yanapitia mchakato wa kutosha kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta na hayatokei kwa ghafla kama inavyozungumzwa.

Waziri Biteko alisema serikali imekusudia kuziwezesha benki za ndani kukua na hivyo kuwataka wawekezaji kutunza fedha zao katika benki za ndani na endapo wawekezaji watataka kutunza fedha zao katika benki za nje watumie benki zenye usajili nchini Tanzania.

Kuhusiana na suala la upatikanaji wa vibali kwa wataalamu wa kigeni kufanya kazi nchini, Biteko alifafanua  kuwa, Serikali haizuii wataalamu kutoka nje kufanya kazi nchini isipokuwa kuwepo uwazi na uwajibikaji na Serikali ikijiridhisha na  kubaini kuwa nchini hakuna mtaalamu wa kufanya kazi fulani serikali haitasita kutoa kibali kwa watu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi nchini.

Kwa upande wa utawala wa kisheria, Biteko alikiri kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaongoza nchi kwa Sheria na taratibu bila kuchagua wala kubagua.

Biteko alitanabaisha kuwa kutokana na ukweli kwamba wapo watu ambao wamejikita katika kuamini mitazamo hasi na hawataki ukweli ni suala gumu kubadili mitazamo yao, na kueleza kuwa, itakuwa rahisi kwa wale watakaokubali ukweli na kubadili mitazamo hasi waliyonayo juu ya serikali ili kwenda sambamba.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alisema, wawekezaji ni wadau muhimu wa maendeleo na hakuna taifa lolote lililo tayari kuwakatisha tamaa wadau wa maendeleo.

Aidha, alibainisha mambo manne yaliyopelekea Sheria ya Madini kufanyiwa marekebisho ili kukidhi matakwa ya taifa na watu wake kwa ujumla na kusema kuwa mambo hayo ni pamoja na kuongeza mapato kwa taifa kwa kuongeza mrabaha wa madini ya vito na almasi kutoka asilimia 5 mpaka asilimia 6.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango (Kulia), katikati ni Katibu wa Waziri Kungulu Masakala wakifuatilia hoja kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Pamela O’Donnel (Hayupo pichani)

Alisema, suala lingine ni uongezaji thamani wa rasilimali madini inayopatikana nchini ili inaposafirishwa nje ya nchi iwe ya viwango vyenye ubora mkubwa na hivyo kusaidia kuongeza mapato kwa taifa. Aidha, amebainsha kuwa kuna baadhi ya madini kama ya graphite yanayoongezwa thamani kwa asilimia 90 na kusafirishwa nje ya nchi kuongezewa ubora zaidi.

Akifafanua hilo, Nyongo alisema ili kulipelekea taifa kuwa na viwanda vya kutosha, serikali imefanya mabadiliko hayo ili kupata wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata madini nchini ili yasafirishwe yakiwa katika viwango bora na kupelekea ongezeko la fedha za kigeni nchini.

Pia, Naibu Waziri Nyongo alizungumzia suala la uwajibikaji wa wawekezaji kwa jamii ya kitanzania na kusema kuwa, ili kuwafanya wawekezaji kuwatumia wazawa katika kufanikisha shughuli za uchimbaji na biashara ya madini, Sheria mpya imeweka wazi masuala mbalimbali yanayopaswa kufanywa na wazawa na manunuzi ya baadhi ya mahitaji kufanyika ndani ya nchi na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na kuajili wazawa.

Mwisho Naibu Waziri Nyongo alizungumzia suala la kuzuia wawekezaji kumiliki leseni wasizozifanyia kazi. Alisema  kuwa, wapo  baadhi ya wawekezaji wamekuwa wakitumia leseni za madini  kuombea mikopo katika taasisi za kifedha nje ya nchi na baada ya kupata mikopo hiyo wamekuwa  wakiendesha shughuli zao nje ya Tanzania.

Alibainisha kuwa, ili kuwabana wawekezaji hao sheria imekuja ikiweka wazi muda maalum wa mmiliki wa leseni kumiliki leseni hiyo vinginevyo maeneo yanarudishwa serikalini ili kutoa fursa kwa watu wenye nia ya kufanya kazi kuendelea na kazi.

Read more

Katibu Mkuu Madini amsimamisha kazi Afisa Dodoma

Na Asteria Muhozya,                                                                    

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amemsimamisha kazi Fundi Sanifu wa Madini, Asheni Daudi wa Ofisi ya Madini Dodoma baada ya kuagizwa na Waziri wa Madini Doto Biteko.

Waziri wa Madini Doto Biteko akitafakari jambo wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika eneo ambalo shughuli za uuzaji wa madini zinafanyika bila kuwa na leseni. Mbele ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila. Wengine ni Maafisa wa Wizara.

Hatua hiyo ilifikiwa Januari 30, 2019, baada ya Waziri Biteko akiongozana na Katibu Mkuu na Wataalam wengine wa wizara vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, kufanya ziara ya kushtukiza katika Kiwanda cha Kuchenjua madini ya Dhahabu cha   Umoja kilichopo eneo la Viwanda la Kizota (Industrial Area) na kubaini mapungufu makubwa katika utendaji kazi wa wataalamu hususan uandaaji wa tarifa za uzalishaji wa madini.

Akizungumza katika eneo hilo, Waziri Biteko alisema wizara ilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu mienendo inayoendelea katika eneo hilo ambapo wahusika ambao ni Maafisa Madini wamekuwa hawatoi taarifa halisi za uzito na ubora wa dhahabu zinazozalishwa baada ya kuchenjuliwa, hivyo, serikali kukosa mapato stahiki.

Waziri Biteko aliongeza kuwa, tayari anayo majina yote ya wanaofanya michezo ya ujanja ujanja kwenye viwanda vya kuchenjua dhahabu, huku akieleza kuwa, hatua madhubuti zitachukuliwa kwa wote wanaofanya vitendo hivyo na kuongeza kwamba, zoezi hilo litakuwa endelevu kwa lengo la kuwabaini wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwataka maafisa madini kuwa makini.

Aidha, alimwagiza Kamishna wa Madini kufanya kaguzi katika viwanda vyote vya kuchenjua dhahabu kwa lengo la kubaini utendaji wa kazi wa viwanda hivyo, ikiwemo taarifa za uzalishaji zinazotolewa na kusema “Lazima tufike mahali tuheshimu taratibu, madini haya ni mali ya nchi”, alisisitiza Biteko.

Wakati huo huo, Waziri Biteko alimtaka Afisa Madini Mkoa wa Dodoma kujitathmini kutokana na mambo yanavyokwenda katika eneo lake la kazi na kumtaka kuwasilisha kwa Kamishna wa Madini na kwa Waziri wa Madini taarifa za uzalishaji madini ya dhahabu kwa kipindi cha miezi sita.

Waziri wa Madini Doto Biteko akieleza jambo wakati akimhoji Munuzi wa Madini Matondo Michembe (wa pili kulia) ambaye alikutwa akifanya shughuli hizo bila kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila.

Pia, katika ziara yake, Waziri Biteko alibaini mnunuzi wa madini ya dhahabu katika eneo la Kizota aliyefahamika kwa jina la Matondo Michembe ambaye anafanya shughuli hizo bila kuwa na leseni ya biashara ya madini hayo. Hivyo, alimwagiza Michembe kuwasilisha taarifa za utendaji wake kwa Kamishna wa Madini na Waziri wa Madini hususan  soko analouzia madini  hayo ya dhahabu.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila alieleza kuwa, kiutaratibu ilikuwa lazima taarifa za uzalishaji na kiasi kilichozalishwa kujazwa katika vitabu maalum ndani ya kiwanda hicho lakini jambo hilo halikufanyika kama inavyotakiwa.

Aliongeza kuwa, Afisa huyo amesimamishwa ili kupisha uchunguzi na endapo itabainika, taratibu za kiutumishi zitachukuliwa.

Read more

Waziri wa Madini Doto Biteko akutana na Mwenyekiti wa TEITI Jijini Dodoma

Na Rhoda James,

Waziri wa Madini Doto Biteko, Januari 29, 2019, alikutana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI), Ludovick Utouh, ofisini kwake Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu ya TEITI nchini.

Read more

Nafasi za mafunzo ya uongezaji thamani madini TGC

Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kilicho chini ya Wizara ya Madini kinatangaza nafasi za mafunzo ya muda mfupi (Short Course) katika fani za ukataji na usanifu wa madini ya vito (Lapidary training course) , Utambuzi wa madini ya vito (Gem Identification), usonara (Introduction to jewelry) pamoja na mafunzo ya muda mrefu ya diploma in Gem & Jewellery Technology. Mafunzo hayo yatatolewa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ambacho kipo Jijini Arusha katika barabara ya Themi-Njiro mkabala na Ofisi ya Madini Arusha.

Fomu ya maombi/Application form

>>Soma Zaidi>>

Read more

Wachimbaji wadogo kutunukiwa Vyeti vya Uhifadhi wa Mazingira

Na Nuru Mwasampeta,

Waziri wa Madini, Doto Biteko amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga, ofisini kwake jijini Dodoma.

Biteko ameshukuru Dkt. Mafwenga kwa kuonesha nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata cheti cha mazingira baada ya kubainisha njia bora za kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata uelewa juu ya uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Januari 28, 2019, Dkt. Mafwenga amesema kutokana na mwamko mkubwa iliyonayo Serikali wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kukua na kufanikiwa katika sekta ya uchimbaji mdogo wa madini, Nemc itajikita katika kuhakikisha inashirikiana na wizara katika kuhamasisha na kuelimisha wachimbaji wadogo juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.

Aidha, amebainisha kuwa, kutokana na vigezo vya awali ambavyo viliwafanya wachimbaji wadogo kutokupewa cheti cha mazingira zitaboreshwa na kuwawezesha kupata cheti hicho.

Amesema, wachimbaji wadogo watapaswa kusajili miradi yao katika Ofisi za Kanda za Baraza la Hifadi la Mazingira  ambao watakagua miradi hiyo na baada ya kujiridhisha watawapatia vyeti hivyo.

Read more

Biteko awataka Maafisa madini kuepuka tuhuma za rushwa, urasimu

Na Nuru Mwasampeta,

Waziri wa Madini Doto Biteko, amewataka Maafisa Madini wa mikoa kuepuka tuhuma za rushwa na urasimu na kubainisha kuwa, hatamfumbia macho Mtumishi yeyote atakayebainika kutekeleza majukumu yake kinyume na Sheria.

Aidha, amewataka maafisa hao kuwabaini na kuwatambua wachimbaji wadogo waliopo katika maeneo yao ya kazi.

Biteko aliwaeleza maafisa hao kuwa wizara haita mfumbia macho mtumishi yeyote asiyetekeleza majukumu yake na kukiri kuwa ni vema kufanya kazi na watu wachache kuliko kufanya kazi na mamia ya watu wasiokidhi mahitaji na kasi ya wizara katika kutekeleza majukumu yao.

Biteko alitoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki alipofanya mkutano baina yake, Katibu Mkuu wa Wizara, Prof. Simon Msanjila, Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na maafisa Madini wa Mikoa. Mkutano huo uliolenga  kutoa msisitizo katika kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji na wafanyabiashara wa madini katika maeneo yao ya kazi.

“Tunao wachimbaji wadogo wengi, wengi sana. Walio rasmi na wasio rasmi. Mwenye wajibu wa kuwatambua wachimbaji hao ni ninyi. Lazima sasa hivi mkatengeneze data base kwenye mikoa yenu ili kujua  akina nani wanajihusisha na shughuli za uchimbaji mdogo ili tutakapotaka  kuwasaidia wachimbaji wadogo misaada hiyo itolewe kwa wahusika kuliko kubahatisha,” alisisitiza Biteko.

Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kikao baina ya uongozi wa wizara na Maafisa Madini wa Mikoa kilichofanyika katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam

“Tunataka kuanzisha soko la madini, na Serikali itatoa nafuu (incentive) kwa wachimbaji wadogo,  nafuu kwenye kodi, nafuu kwenye ushuru,  sasa hawa wachimbaji wadogo watakaonufaika na punguzo hilo lazima tuwajue ni akina nani, lazima tuwe pro- active katika utendaji wetu wa kila siku” alikazia.

Aidha, Waziri Biteko aliwataka Maafisa hao kwenda kutekeleza na kusimamia  Sheria  na kukataa kila aina ya maelekezo yanayotolewa kwao  ambayo yanayokiuka sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.

Biteko aliongeza kwa kuwataka Maafisa madini wa mikoa kuhakikisha wanafanya kazi na kulifanya jina la Wizara ya Madini linakuwa zuri kuliko kuonekana kama watu wasiokuwa na mwelekeo wa kiutendaji.

Biteko alibainisha kuwa mpaka sasa wizara imehamisha watumishi 57 makao makuu ya wizara ambao wizara imejiridhisha kuwa utendaji kazi wao hauridhishi na kwamba zoezi hilo litaendelea kwa lengo la kuimarisha utendaji wizarani.

Zaidi ya hayo, Biteko aliwataka Maafisa Madini hao kuhakikisha kuwa wanashirikiana na kamati za ulinzi na usalama za mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuwataka kuwajibika kwao kwani ni wawakilishi wa Rais na wanasimamia shughuli za Serikali.

Aliongeza kuwa, wakuu wa wilaya ni wasimamizi wa Serikali katika maeneo hayo, ni wawakilishi wa Rais katika wilaya na mikoa hiyo ni wasimamizi wa kazi zote za serikali ikiwepo ya madini hivyo hawana budi kushirikiana nao.

Biteko aliwataka maafisa Madini hao kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo ziwe ni za kibajeti au vifaa  ili waweze kusaidiwa na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao na kuwaagiza kumtumia Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Simon. Msanjila katika kutatua changamoto hizo.

Akizungumzia suala la uanzishwaji wa vituo vya madini katika mikoa. Biteko alisema, Kanuni za kusimamia vituo hivyo zimekwisha andaliwa na zitasainiwa wakati wowote na kuwataka maafisa hao kutambua kuwa wao ni watu muhimu katika kusimamia vituo hivyo.

Biteko alisema anatamani ndani ya miezi sita sekta ya madini ibadilike, mtu akija aone kuna maendeleo, aliwasihi kuhama kwenye majina ya kuitwa wala rushwa, tuhame kuitwa warasimu tuhame kwenye sifa za watu wanaosimamia masuala ya madini pamoja na kujihusisha na shughuli za uchimbaji jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Akihitimisha kikao hicho, Biteko aliwataka maafisa hao kuhakikisha mapendekezo yote yaliyotolewa katika mkutano wa kisekta kila mtu katika mkoa wake akayafanyie kazi. Pia  aliwaagiza kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi wa wizara kwa nyakati tofauti ikiwa ni pamoja na yale yaliyotolewa na aliyekuwa Waziri wa Madini,  Angellah Kairuki pamoja na  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani  Manya alieleza kufurahishwa na kukiri kwenda kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na kiongozi wa wizara hiyo.

Read more

Waziri Biteko aanza kutatua mgogoro kati ya Mzee Mchata, Kampuni ya Mantra

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo Januari 28, amekutana na Mzee Eric Mchata na Kampuni ya madini ya Uranium ya Mantra Tanzania kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo baina ya pande hizo mbili.

Kikao hicho, kinafuatia malalamiko yaliyowasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Januari 22 na  Mzee Mchata wakati wa mkutano wa Kisekta ulioshirikisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Wakati akisikiliza kero za wachimbaji na wadau wa madini walioshiriki kikao hicho, Rais Magufuli alipokea kero ya Mzee Mchata aliyemweleza kwamba amekuwa na mgogoro na kampuni hiyo kwa kipindi cha takribani miaka 12 na bado hajapata suluhu.

Akijibu kero iliyowasilishwa na Mzee Mchata, Rais Magufuli aliitaka Wizara ya Madini kuhakikisha mgogoro huo unafikia mwisho.

Read more

Taarifa kwa Umma-Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) tarehe 18/01/2019. Kufuatia uteuzi huo Waziri wa Madini Mh. Doto Mashaka Biteko, kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1)(b)(c)(d) na (e) ya Kanuni ya The Mining (Geological Survey), amewateua wajumbe wa Bodi ya GST kama ifuatavyo:

 1. Abdulkarim Hamisi Mruma
 2. Emanuel Mpawe Tutuba
 3. Bibi Bertha Ricky Sambo
 4. Shukrani Manya
 5. David R. Mulabwa
 6. Bibi Monica Otaru

>>Soma Zaidi>>

Read more

Waziri Mkuu Majaliwa ataka kanuni za uanzishwaji masoko ya madini kukamilishwa haraka

 • Aitaka Wizara ya Madini kutoa Mwongozo wa Usafirishaji Madini Nje.
 • Waziri Biteko asema, Rasimu ya Kwanza imekamilika,
 • Asisitiza Masoko yaanze mwezi Februari

 Asteria Muhozya na Samwel Mtuwa, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Madini kuharakisha ukamilishaji wa Kanuni za Uanzishwaji Masoko ya Madini nchini, ikiwemo kuhakikisha masoko hayo yaanza haraka.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Januari 26, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mawaziri kutoka wizara mbalimbali, Wakuu wa Mikoa yote nchini, Wizara ya madini, Makatibu Tawala wa Mikoa, Taasisi mbalimbali zikiwemo Tume ya Madini, Benki Kuu ya Tanzania na Kituo cha Uwekezaji Nchini, (TIC).

Amesema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliyayotoa Januari 22 wakati akifungua Mkutano wa Kisekta uliowashirikisha wachimbaji na wadau wa madini nchini ambapo Rais Magufuli alisisitiza juu ya kuanzishwa kwa masoko ya madini.

Aidha, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kikao hicho na kusema kwamba, kimelenga katika kujenga uelewa wa pamoja kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Madini wa Mikoa kuhusu kanuni na namna ya kuendesha Masoko hayo.

Akisisitiza kuhusu usimamizi wa masoko ya madini, Waziri Mkuu amesema kuwa, Wakuu wa Mikoa kwa kushirikiana na Maafisa Madini ndiyo watakuwa wasimamizi wakuu wa masoko hayo  na kuongeza kuwa, katika ngazi ya Wilaya, masoko hayo yatasimamiwa na wakuu wa wilaya na kueleza “kwenye wilaya msimamizi ni mkuu wa wilaya, wakuu wa wilaya mkaripoti kwa wakuu wa mikoa wawasaidie,”.

Pia, ametaka pindi kanuni hizo zitakapokamilika kuzifikisha kwa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya na  katika maeneo yote yenye machimbo wakiwemo wachimbaji na Wafanyabiashara ikilenga kuwezesha wadau hao kufikiwa na kanuni hizo na kuwa na uelewa wa kutosha na hatimaye ziweze kusimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana  na Tume ya Madini.

Katika kuhakikisha kwamba masoko hayo yanaendeshwa  kwa usalama, ameitaka mikoa kuhakikisha kunakuwa na na hali ya ulinzi na usalama kwenye maeneo hayo ili  kuwahakikishia wafanyabiashara, wachimbaji na wananchi kwa ujumla usalama wa kutosha wakati wa kuuza madini hayo katika masoko yatakayoanzishwa.

Akizungumzia mwongozo wa usafirishaji madini nje ya nchi, ameitaka  wizara  ya madini kutoa mwongozo huo mapema na kueleza kuwa, baada ya serikali kutafakati kwa kina, imetoa mwongozo wa kusafirisha baadhi ya madini nje ya nchi na hivyo kuitaka wizara kutoa mwongozo huo kwa Wakuu wa Mikoa yote nchini.

 Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa, tayari rasimu ya kwanza ya Kanuni hizo imekamilika na kueleza kuwa, kikao kazi kinalenga jambo ambalo halikuwahi kufanyika tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru na hivyo kuwataka wakuu wa mikoa kulifanya kuwa jambo linalowahusu wote.

Amesema kwa sasa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hawana maeneo maalum wanayoweza kufanyia biashara  ya madini  hali ambayo inachangia kuwepo utoroshaji wa madini na hivyo kuikosesha serikali mapato.

Ameongeza, ili  kukabiliana na changamoto ya masoko ya madini, Wizara iliunda kamati iliyojumuisha wajumbe kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali zikiwemo Ofisi ya Rais Ikulu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Benki  Kuu na Tume ya Madini.

Amesema kuwa, Kamati hiyo iliundwa ili kuandaa rasimu ya Kanuni za kuanzisha na kusimamia Masoko ya Madini Nchini na kuongeza kuwa katika kuandaa kanuni hizo, jina la Kanuni linalondekezwa The Mining (Mineral and Gem House) Regulations, 2019,” amesema Waziri Biteko.

Ameongeza kuwa, Marekebisho ya sheria yaliyofanyika mwaka 2017 katika sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yalilenga kulinda maslahi ya taifa na kuhakikisha sekta ya madini inachangia ipasavyo katika kukuza na kuimarisha mchango wa sekta katika pato la Taifa na kuongeza kwamba, si kweli kwamba marekebisho hayo yamefukuza wawekezaji bali yameongeza idadi ya wanaotaka kuwekeza katika sekta ya madini.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha masoko ya madini yanaanza mara moja wakati kanuni hizo zinaendelea kuboreshwa na kusisitiza wakuu hao wahakikishe yaanza ifikapo mwezi Februari mwaka huu.

“Lazima Wakuu wa Mikoa tuanze. Wakuu wa Mikoa tutaanza na Kanuni hizi, hizi. Tutaendelea kuziboresha lakini lazima tuanze. Na kanuni hizi zikipita, lazima kila anayehusika atafanya biashara kupitia kanuni hizi,” amesisitiza Waziri Biteko.

Halikadhalika, amewataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanazipitia kanuni hizo kwa lengo la kufanya maboresho na kutoa mapendekezo yatakayowezesha kuwa na kanuni zitakazowezesha taifa kunufaika na rasilimali hiyo na kuongeza, “ hizi kanuni zikiwa mbovu itakuwa yetu wote,”.

Pia, amewaomba Wakuu wa Mikoa, Maafisa Tawala wa Mikoa, Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa na Wadau kwa ujumla kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kutimiza ndoto za muda mrefu za Wachimbaji wadogo Wafanyabiashara wa Madini, Wadau na Watanzania wote kwa ujumla za kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia zaidi katika taifa na inalinufaisha.

Naye, Waziri , Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo amesema kuwa, Waziri Biteko ameanza vizuri na  kueleza kuwa,  kikao hicho kitasaidia kupata mambo mbalimbali yatakayosaidia katika uanzishwaji wa masoko hayo na kueleza kuwa, timu yake ya mikoa iko tayari.

“Mhe. Waziri nimefurahi sana namna wakuu wa mikoa walivyozungumza wakati wa majadiliano ya kuboresha Kanuni hizi. Tunakwenda kuona namna ya kuanzisha masoko haya,”.

Aidha, amewataka wakuu wa mikoa kulichukulia jambo hilo kama matarajio ya Rais Magufuli anavyotaka kuona kwamba madini yanalinufaisha taifa.

Read more

Waziri Biteko amaliza mgogoro kati ya Kampuni ya BEAL na MTL

Na Rhoda James

Waziri wa Madini, Doto Biteko amemaliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Barrick Exploration Africa Limited (BEAL) na Megagems Tanzania Limited (MTL) uliodumu kwa muda mrefu.

MTL ambaye ni mlalamikiji alikuwa anadai kulipwa kiasi cha Dola za Marekani 10,000 na Kampuni ya BEAL.

Akisuluhisha mgogoro huo Waziri Biteko ameitaka Kampuni ya BEAL kumlipa mlalamikaji kwa kuwa vibali vyote vinaonesha kuwa anastahili kulipwa.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 25 Januari, 2019 jijini Dodoma katika Ofisi ya Waziri wa Madini, Doto Biteko.

Read more

STAMICO sasa imefanya kitu-Kamati ya Bunge

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeonesha kuwatia moyo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini baada ya kuwasilisha taarifa yake kwa kamati hiyo iliyoonesha kuwepo mafanikio kutokana na kuendeleza mgodi wake wa Kiwira, kuendeleza uchimbaji na uuzaji makaa ya mawe kupitia mgodi wake wa Kabulo na uzalishaji dhahabu katika mgodi wa STAMIGOLD.

Wakichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kuendeleza migodi ya Kiwira, Stamigold, Buhemba na Backreef, na taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha nusu mwaka 2018/19, kuanzia mwezi Julai hadi Desemba, 2018, wajumbe hao wamesifu jitihada zinazofanywa na shirika hilo kwa kufufua mgodi wake wa Kiwira na uzalishaji unaofanywa Stamigold na Kabulo na kueleza kuwa, hivi sasa kuna mambo yanafanyika na yanakamilika.

Pamoja na mafanikio hayo, kamati imeitaka wizara kuendelea kuzifanyia kazi changamoto za uchimbaji mdogo wa madini nchini huku ikitakiwa kufanyia kazi ushauri uliotokana na mkutano wa Kisekta kati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na wadau wa madini uliofanyika Januari 22, 2019.

Aidha, wameitaka wizara kutumia mkutano huo kupanga mipango itakayowezesha Tanzania Ijayo kunufaika na rasilimali madini ikiwemo kuhakikisha inawawezesha wachimbaji wadogo kukua kutoka uchimbaji mdogo, kwenda wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

Vilevile, wajumbe wa kamati wameishauri wizara kulifanyia kazi suala la mitobozano huku ikitakiwa kuweka mazingira mazuri ya kuepusha ajali za wachimbaji wadogo migodini.

Akitoa taarifa kwa kamati hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Deusdedith Magala, amesema kuwa, katika kipindi cha nusu mwaka wa utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/19, kuanzia mwezi Julai hadi Disemba, 2018, mgodi wa Kabulo umezalisha tani 4,052 na kuuza tani 1,302 za makaa yenye thamani ya shilingi 96.2 milioni ambapo kutokana na mauzo hayo, serikali imepokea mrabaha na ada ya ukaguzi wa shilingi 8,062,961.31 na ushuru wa huduma shilingi 738,597.94.

Magala ameeleza kuwa, mgodi wa STAMIGOLD umezalisha wakia 7581.55 za dhahabu na wakia 1,014.33 za madini ya fedha yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 21.3, na kuongeza kwamba, mauzo hayo yameuwezesha mgodi huo kulipa mrabaha wa shilingi bilioni 1.27 katika kipindi hicho.

Akitaja mafanikio mengine, Magala amesema kuwa, shirika hilo limekamilisha ukarabati wa kinu cha kusagia makaa ya mawe kwa lengo la kuongeza thamani ya makaa yanayochimbwa katika mgodi wa Kabulo ili kukidhi mahitaji ya soko.

Aidha, amesema ukarabati mwingine ni pamoja na matengenezo ya njia za kusafirisha makaa ya mawe ikiwemo reli na mikanda; matengenezo ya mashine za kusaga na kuchekecha makaa, uhunzi na uchongaji vipoli na kusema kuwa, ukarabati huo ulitumia gharama ya shilingi 31,471,010.

“Mhe. Mwenyekiti vilevile, shirika linaendelea na tathmini ya kufufua mgodi wa chini wa Kiwira ili nao ujumuishwe katika uzalishaji wa makaa,” amesema Magala.

Akitoa ufafanuzi kuhusu akiba ya uwepo wa makaa ya makaa katika mgodi wa Kiwira, Magala amesema kuwa, unakadiriwa kuwa na wastani wa tani milioni 35.14 za mashapo ya makaa, ambapo kati ya mashapo hayo, yaliyothibitishwa yanafikia tani milioni 22.14 na mashapo yanayoweza kuvunwa kwa faida yanafikia tani milioni 14.64.

Akieleza mikakati ya shirika hilo, Magala amesema kuwa, ni pamoja na kutafuta mbia wa kuendeleza mradi wa visusu vya dhahabu wa Buhemba, kutafuta mkandarasi wa uchimbaji ili kutekeleza sehemu ya uchimbaji wa kokoto katika mradi wa Ubena Zomozi, kuendelea kutafuta mkandarasi mwingine wa uchimbaji ili aweze kuongeza uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kabulo na kuendelea kufuatilia vibali vya kuajiri kutoka mamlaka ya ajira za utumishi wa Umma ili kuongeza nguvu kazi ya shirika.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumzia mafanikio ya mgodi wa Stamigold amesema kwamba mgodi huo unafufuka tofauti na ilivyokuwa awali ambapo sasa unazalisha ikiwemo kulipa madai ya wafanyakazi.

Akizungumzia changamoto ya mitobozano, amesema kuwa, wizara inashirikiana na mamlaka za mikoa na wilaya kuhakikisha inatatua migogoro hiyo na kuongeza kuwa, wizara inafanya jitihada za kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwa endapo wataendelezwa, watawezesha kuwepo na mapato ya uhakika kwa serikali kutokana na idadi yao nchini.

Wizara ya Madini na taasisi zake ilianza kukutana na Kamati hiyo kuanzia Januari 21 hadi 23, ambapo taarifa ya utekelezaji kwa wizara na taasisi zake kwa kipindi cha Nusu Mwaka, (2018/19) ziliwasilishwa kwa kamati hiyo.

Read more

Aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli wakati akifungua mkutano wa Kisekta Januari 22, 2019

 • Zile asilimia 1, 5, 6, 18 na nyingine zilizokuwa zinatozwa kwa kitu kimoja kwa kweli haziwezi kukubalika.
 • Bado hatujafikia tunakotaka kwenda. Lengo ni kufikia asilimia 10. Hivi sasa tunachangia asilimia 4.8 bado tuna safari ndefu ya kufikia malengo. Tunayo nafasi ya kufikia asilimia 10. Watanzania tuna wajibu wa kusukuma mbele uzalendo wetu. Usipolipa kodi unawaumiza watanzania, watoto na wajukuu wetu.
 • Uzalishaji kutoka kwa wachimbaji na mapato umeongezeka kidogo. Nawapongeza kidogo Wizara na wadau kwa mafanikio haya yaliyopatikana.
 • Bei ya Almasi soko la nje ni Dola 5,000, soko la Maganzo ni dola 4,000. Serikali inaambiwa ni dola 2,000.
 • Ifike mahali sisi wachimbaji tujiulize kwa nini tunawadhulumu watanzania? Uzalendo umepungua Tanzania.
 • Niliagiza Kamera zifungwe Mirerani. Mpaka sasa hazijafungwa Naagiza ndani ya mwezi mzima kamera ziwe zimefungwa. Zisipofungwa mjiandae kuondoka.
 • Tunashindwa kusimamia utekelezaji wa Mikataba. Wito kwa Wizara na Mamlaka kusimamia mikataba na kufanya kaguzi za mara kwa mara.
 • Tatizo hata TRA hawajachangamka. Nakwambia Kamishna General waambie watu wako wachangamke.
 • Toeni michango yenu, tangulizeni uzalendo kwa maslahi ya Taifa. Sina tatizo lolote mkijadiliana kwa maslahi ya taifa.
 • Tatizo la Wizara ya Madini hawataki kufanya maamuzi. Tuwe na tabia ya kuamua. Kama umepewa wizara amua, kama umepewa mkoa amua.
 • Tunataka ninyi mtupe hotuba siyo sisi tutoe hotuba. Nataka mzungumze kwa uwazi.
 • Nimesikia changamoto za Mabenki kwamba wachimbaji wanahamahama. Kwa kuwa nimekuja kusikia changamoto, nina Imani Waziri atasema changamoto zilizopo.
 • Mumkabidhi hayo mliyokubaliana. Muwape mawaziri wangu wayafanyie kazi. Mimi mniletee
 • Maeneo yote ya madini ambayo hayaendelezwi yarudishwe serikalini.

MASWALI YALIYOULIZWA NA MHE. RAIS WAKATI WA MKUTANO WA KISEKTA

 • Kwa nini katika ripoti ya Benki ya Dunia hatuongozi kuuza madini? Kwanini madini yanatoroshwa na kwanini TRA hawakusanyi kodi?
 • Kwanini Tanzania tunaongoza kwa kuzalisha Afrika Mashariki laini kwanini hatuongozi kwenye mauzo?
 • Kwanini Makamishna wanalipwa mishahara na madini yanatoroshwa?
 • Je Wakuu wa Mikoa wanasimamiaje?
 • Kwanini madini ya Bati yanachimbwa, hayauzwi yanatoroshwa nchi jirani?
 • Kwanini pamoja na kujengwa ukuta Mirerani madini yanatoroshwa?
 • Kwanini hatuna masoko ya madini kama dhahabu wakati Mawaziri wapo, Makatibu Wakuu wapo?
 • Tumeshindwa kitu gani kuwa na Smelters?
 • Center za kuuza Madini ni muhimu. Wataalamu wetu mmeshindwaje kujenga center za Madini?

ALIYOYASEMA WAZIRI WA MADINI DOTO BITEKO

 • Changamoto walizozieleza ni za kweli. Kikao hiki ni cha mashauriano. Tunataka tufungue ukurasa mpya. Wakati wote Mhe. Rais anatuambia tuwahudumie nyie, tuwafuate. Nawaomba wachimbaji, wafanyabiashara tushirikiane.
 • Hivi ninavyoongea tayari tumeunda Timu ya Wataalam wanajadili kanuni za Masoko haya. Tunakuja na utaratibu utakaowezesha kufanya biashara.
 • Sasa saa yakutembea imekwisha, tutakimbia.
 • Hakuna dawa ya uaminifu kama kupenda nchi yako. Tuipende nchi yetu, tuithamini nchi yetu.

ALIYOYASEMA RAIS WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WACHIMBAJI TANZANIA (FEMATA) JOHN BINA

 • Rais umewapa wachimbaji heshima kubwa. Kitu hiki hakiwajawahi kutokea. Hata mimi leo nakaa High table.
 • Tunashukuru umesaidia kufuta tozo za kodi kwenye madini ya chumvi.
 • Umeimarisha uhusiano kati ya wachimbaji na serikali katika ngazo zote.
 • Tanzania hakuna masoko rasmi. Yaliyopo siyo rasmi ikiwemo kukosekana kwa bei elekezi.
 • Umejenga ukuta Mirerani ili Tanzanite itunufaishe wote.
 • Wachimbaji wadogo wa madini wako milioni 6. Tukichukua wachimbaji milioni moja ambao watauza gramu 5 kwa siku ina maana tutapata tani 5 za dhahabu kwa mwaka. Kwa idadi hiyo, serikali itapata kodi nyingi kutoka kwa wachimbaji wadogo

MAPENDEKEZO YA FEMATA

 • Kuwepo na Benki ya Madini (Mineral Bank) ifanye kazi chini ya BoT.
 • Mwongozo wa kiwango gani cha madini kilichochakatwa kwa ajili ya kusafirishwa nje utolewe.
 • Tanzanite ipewe utambulisho ili ijulikane inapotoka itakapouzwa popote duniani
 • Serikali iharakishe kuanzisha soko la kuuzwa madini nchini.
 • Tunaomba asilimia 0.3 ikatwe kwa Mujibu wa Sheria siyo kwa kukadiria
 • Tunaomba kutengwa maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
 • GST na STAMICO waongezewe nguvu ili kutambua mashapo ya almasi.
 • Tunaomba serikali ipeleke umeme migodini.
 • Serikali itoe vitambulisho kwa wachimbaji. Hii itasaidia ulipaji wa kodi.
 • Tunaomba kuanzishwa kwa Siku ya Madini. Tunapendekeza iwe tarehe 5 Julai kumuenzi Mhe. Rais kwa mabadiliko ya Sheria ya Madini. Siku hiyo iitwe Magufuli Day.

ALIYOYASEMA NAIBU GAVANA WA BoT, BENARD KIBESE

 • Mashirikiano baina ya BoT, Tume ya Madini na Wizara ya Madini katika kuanzisha Mineral Center. Mpaka sasa BoT wanaandaa Kanuni za kuhifadhi madini ya vito na dhahabu .
 • BoT itanunua refine gold ikiwa mmoja wa wanunuzi wa dhahabu.

ALIYOSEMA MWENYEKITI WA   UMOJA WA MABENKI TANZANIA, ABDULMAJID NSEKELE

 • Benki zinashindwa kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo kutokana na ukosefu wa leseni na wengine kukodisha hivyo kushindwa kutambua uhalali wao.
 • Wachimbaji wadogo wanashindwa kufanya upembuzi yakinifu wa mapato yao ambayo husaidia benki kufanya tathmini.
 • Kuwepo kwa teknolojia duni kwa wachimbaji wadogo.
 • Kukosekana kwa mshikamano baina ya wachimbaji. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

Read more

Kamati ya Bunge yaipongeza Wizara ukusanyaji maduhuli

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara ya Madini kwa ukusanyaji maduhuli ambapo katika kipindi cha nusu Mwaka wa Fedha 2018/19, cha kuanzia mwezi Julai hadi 31 Disemba, 2018, ilikusanya shilingi 167,742,947,332 kati ya shilingi 310,598,007,000 iliyopangiwa.

Akiwasilisha taarifa kwa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, amesema kuwa, shilingi 310,320,0004,000 zilipangwa kukusanywa kupitia Tume ya Madini, na shilingi 278,003, 000 katika Makao Makuu ya Wizara na Chuo cha Madini Dodoma.

“ Mhe. Mwenyekiti, hivyo lengo la makusanyo kwa kipindi cha nusu mwaka Julai hadi Disemba 2018 ni shilingi 155,299,003,500. Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2018, wizara ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 167,742,947,332 sawa na asilimia 108.01 ya lengo,” amesema Kamishna Mulabwa.

Akizungumzia juhudi za wizara katika kuvutia uwekezaji katika sekta ya madini, amesema wizara iliandaa kongamano la kutangaza fursa za uwekezaji katika sekta ya madini nchini lililojulikana kama China Tanzania mining Forum lililenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini, ikiwemo kutafuta soko la madini hayo nchini China na kuangalia fursa za ushirikiano kati ya Wizara ya madini Tanzania na Wizara ya maliasili ya China.

“ Mhe. Mwenyekiti kongamano hilo pia lilitumika kuwakutanisha wachimbaji wa Tanzania na watengenezaji wa mitambo mbalimbali ambayo hutumika kwenye shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini,”amesema Kamishna Mulabwa.

Kamishna Mulabwa ameongeza kuwa, katika kongamano hilo jumla ya wachimbaji wadogo 40 na wakubwa 4 kutoka Tanzania walishiriki kongamano hilo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijibu hoja za Kamati kuhusu suala la ukusanyaji wa maduhuli amesema bado Wizara haijaridhika na kiwango kilichokusanywa na kuongeza kuwa, kama wizara katika mipango yake yenyewe ya ndani, imepanga kukusanya zaidi ya kiwango cha bilioni 310 iliyopangiwa.

“ Mhe. Mwenyekiti sisi wenyewe ndani tumejiwekea malengo yetu ya kukusanya zaidi ya kiasi tulichopangiwa. Tunajiongeza tuongeze kiwango hicho sisi wenyewe.  Tunafanya hivyo ili mwakani hata kama tutaongezewa kiwango basi tuwe tayari tumekwisha jipanga,” amesisitiza Naibu Waziri Nyongo.

Akizungumzia udhibiti wa madini, amesema kuwa, Wizara inaendelea za jitihada na kudhibiti utoroshaji madini ambapo kwa upande wa madini ya tanzanite udhibiti unaendelea na kusema kuwa, kwa sasa madini hayo yanapita katika mfumo unaoeleweka.

“Kesho Januari 22, tutakuwa na mkutano wa Kisekta, watakuja wachimbaji na wafanyabiashara naamini watamweleza Mhe. Rais kero zao na tutasikia. “Lakini pia tumewaalika wakuu wa Mikoa ambayo shughuli za madini zinafanyika, tunataka kuweka mazingira mazuri kwa sekta.

Kuhusu changamoto za masoko ya madini, amesema wizara inataka kuhakikisha kwamba biashara ya madini inakuwa wazi na halali huku ikijipanga kukusanya zaidi kodi za serikali na kuongeza kuwa, wizara inajipanga kuweka mfumo mzuri wa soko la madini jambo ambalo litazinufaisha pande zote.

“ Mhe. Rais anataka tununue tuweke reserve. Lakini pia Serikali ikinunua kwa bei ya soko, hata wachimbaji watafurahi,” amesema Nyongo.

Akizungumzia suala la uhifadhi wa mazingira amesema kuwa wizara imeweka utaratibu wa pindi wawekezaji wanapoanzisha mgodi ni lazima waweke mpango wa namna watakavyofunga migodi huku suala la uhifadhi wa mazingira likipewa umuhimu wake.

Ameongeza kuwa, wizara inaweka mkazo kwa migodi kueleza mpango wa ufungaji migodi ambao utaacha mazingira yakiwa salama.

Wakizungumza katika kikao hicho kwa nyakati tofauti, wajumbe wa Kamati hiyo, licha ya kuipongeza wizara kwa ukusanyaji wa maduhuli, wameitaka wizara kuweka mikakati madhubuti katika suala uongezaji thamani madini kutokana na zuio la usafirishaji madini ghafi nje ya nchi.

Aidha, wajumbe hao wameitaka Wizara kuendelea kukiimarisha Kituo chake cha Jimolojia Tanzania (TGC) ili kuweza kutoa wataalam wa kutosha katika tasnia hiyo ya uongezaji tthamani madini.

Read more

Maafisa madini watakiwa kutobagua Migodi

Na Asteria Muhozya, Mbinga

Maafisa Madini nchini wametakiwa kutobagua migodi midogo kwa kuelekeza nguvu kwenye migodi mikubwa  tu  huku wakisisitizwa kutatua migogoro kwenye maeneo yao ya kazi na kuelezwa kuwa,  watakaobainika wakibagua migodi hiyo na kutotatua migogoro wataondolewa  kwenye nafasi zao.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisamiliana na baadhi ya wachimbaji wa madini ya Sapphire katika kijiji cha Masuguru mara baada ya kuwasili kijijini hap wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo

Hayo yalibainishwa Januari 17 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati  akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini aina ya Sapphire wakati wa  ziara yake katika kijiji cha Masuguru, Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara hiyo ikilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini wilayani humo pamoja na kusikiliza kero za wachimbaji katika migodi hiyo,  ambapo wachimbaji waliwasilisha kero za kutaka kutengewa maeneo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji, bei elekezi za madini  ikiwemo kuunganishwa na  huduma ya umeme kwenye migodi yao.

Akizungumza kijijini hapo, alimtaka Afisa Madini mkoa wa Ruvuma hukakikisha anaishughulikia kero hiyo na kuitatua  mara moja na kuongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano anataka wachimbaji nchini wachimbe madini, hivyo,  maafisa madini   kote nchini wahakikishe wanashughulikia kero katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kusuluhisha migogoro.

“Sisi ni matajiri, tumebarikiwa madini ya vito. Wachimbaji chimbeni lakini mchimbe katika maeneo yaliyoruhusiwa kuchimbwa”.alisisitiza.

Alisema kuwa, kama mgogoro ni mkubwa wapo viongozi wa vyama vya wachimbaji wahakikishe kuwa  wanafikisha migororo hiyo na kusema “tuleteeni na sisi lakini  usipoishughulikia migogoro hiyo tutakuondoa.

Aliongeza kwamba, serikali inalenga katika kuwatoa wachimbaji wadogo kutoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa  kati na hatimaye mkubwa na ndiyo sababu inaendelea na ujenzi wa vituo vya umahiri  katika maeneo mbalimbali nchini ikilenga katika kutoa elimu ya uchimbaji bora, uchenjuaji bora, biashara ya madini na ujasiliamali ili kuhakikisha kwamba wachimbaji wadogo wanakua.

Aliongeza kuwa,  elimu  ya ujasiliamali ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa itawaandaa kuwa na uchimbaji endelevu na wenye tija.

Sehemu ya Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Saphire wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe Maalum kwa Naibu Waziri Stanslaus Nyongo baada ya kuwasili katika kijiji cha Masuguru Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Akijibu ombi la ruzuku,  aliwataka wachimbaji wadogo kujiunga katika vikundi vidogo vidogo  ili iwe rahisi kwa wachimbaji hao kufikiwa  ikiwemo kupatiwa huduma za leseni, elimu, vifaa, kuwamilikisha, kuwapatia mikopo na  kuwafuatilia  jambo ambalo litapelekea wafanye kazi kwa urahisi na kwa kulipa kodi za serikali na  wao kubaki na kipato  kitakachowezesha maisha bora.

Alisema uwepo wa mazingira mazuri migodini utasaidia vijana kufanya kazi na hivyo kuwa na taifa lenye watu wanaofanya kazi.  Aliwataka maafisa madini wote kuhakikisha wanashughulikia migogoro ya wachimbaji wadogo na kueleza kwamba, endapo serikali itakuta migogogoro ya wachimbaji wadogo  katika maeneo yao wataondolewa.

Aliongeza kwamba, wizara imejipanga na tayari kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya wachimbaji  na kuwasisisitiza kuhakikisha wanauza madini  wanayoyachimba katika maeneo rasmi.

Akizungumzia suala la broker, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni ya kufanya shughuli hizo ikiwemo vifaa vya kupimia madini na kuwataka kulipa kodi. Pia, aliwatahadharisha wachimbaji wanaoshirikiana na broker wasiokuwa  na leseni   kuacha kwani kwa kufanya hivyo ni kwamba  kwamba wote wanaliibia taifa.” Maafisa madini hakikisheni mnawajua ma broker wote  na wawe na leseni na walipe kodi, “ alisisitiza Nyongo.

Akijibu ombi la  ruzuku lililowasilishwa  kwake,  alisema fedha za ruzuku zilizokuwa zikitolewa awali  hazikuwafikia walengwa wote  na kueleza kuwa, wapo waliopata ruzuku hizo lakini hawakuwa wachimbaji na kuongeza kwamba, hivi sasa wizara inaangalia namna bora ya kuwasaidia wachimbaji.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Ruvuma  Abraham  Nkya alisema kuwa, mkoa huo tayari umetenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kwamba watashirikiana na wachimbaji hao ili  suala hilo liweze kuwasilishwa Tume ya Madini kwa  ajili ya hatua zaidi.

Awali , kiongozi wa wachimbaji   aliwasilisha ombi kwa Naibu Waziri   la wachimbaji kupatiwa  ruzuku. Alisema mkoa huo umebarikiwa madini ya ujenzi, nishati, viwanda    huku eneo la Masuguru likibariwa madini ya Sapphire. Alisema eneo hilo liliombwa kwa ajjili ya uchimbaji mdogo lakini mpaka  sasa bado halijatengwa.

Pia, alisema ipo changamoto ya kukosekana elimu kwa watendaji vijijini ambao wamesababisha mgizo mkubwa wa kodi kwa wachimbaji.

Read more

Madini kufanya mazungumzo barabara mgodi wa Makaa, Ngaka

Na Asteria Muhozya, Mbinga

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema Wizara yake itafanya mazungumzo na  Mamlaka zinazohusika na masuala  ya barabara ili kuweka mazingira bora ya miundombinu hiyo  kwa lengo la  kuwezesha biashara ya makaa ya mawe na shughuli za uzalishaji makaa hayo kufanyika kwa ufanisi zaidi katika mgodi wa makaa ya mawe  Ngaka, uliopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akiongozwa na Meneja wa mgodi wa Makaa ya Mawe TANCOAL, David Kamenya (aliyenyoosha mikono) kutembelea maeneo ambapo uchimbaji wa makaa hayo unafanywa katika machibo yaliyopo Wilayni Mbinga mkoa wa Ruvuma.

Alisema mgodi huo wa Ngaka chini ya kampuni ya TANCOAL ndiyo taswira ya uzalishaji makaa ya mawe nchini hivyo, serikali haina budi kuweka mazingira bora yatakayowezesha kupunguza gharama za uendeshaji jambo ambalo litapunguza gharama kwa walaji wa nje na ndani ikizingatiwa kuwa, ni kampuni ya Kimataifa kutokana na kuhudumia wateja kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda nchi na nyingine.

Kauli ya Naibu Waziri Nyongo inafuatia changamoto ya barabara iliyowasilishwa kwake na Meneja Mgodi wa TANCOAL Mhandisi David Kamenya, ambaye alimweleza Naibu Waziri kuwa, ukosefu wa miundombinu imara ikiwemo madaraja imechangia shughuli za upakiaji makaa hayo kutokuzidi tani 20 kwa kila gari jambo ambalo linapelekea kuwepo na foleni kubwa  kutokana na uhitaji wa makaa hayo.

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara mgodini hapo Januari 17 ikilenga kukagua shughuli za madini mkoani Ruvuma pamoja na kuangalia changamoto mbalimbali ambazo mgodi huo unakabiliana nazo katika utekelezaji wa shughuli zake.

Pamoja na kuridhia ombi hilo, Naibu Waziri aliitaka kampuni hiyo kuongeza kasi ya uzalishaji kutokana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika soko la nje na ndani na kuitaka kutobweteka huku ikitakiwa kuboresha huduma inazotoa ikiwemo kuongeza vifaa vya kazi.

“Nimeona changamoto ya barabara. Kama serikali ni lazima tuifanyie kazi changamoto hii ili kuwezesha uzalishaji zaidi wa makaa. Sisi tutaendelea kutoa leseni kwa wazalishaji wengine ili kuweka ushindani, hivyo msibeweteke, tunahitaji sana makaa haya kwa uchumi wa taifa letu kwa kuwa tunayo hazina ya kutosha ya rasilimali hii,” alisema Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akieleza jambo baada ya kutembelea eneo ambalo shughuli za upakiaji makaa ya mawe zinafanywa na mgodi wa TANCOAL kwa ajili ya makaa hayo kusafirishwa maenezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa, kufuatia serikali kuweka zuio la uingizaji makaa kutoka nje, ni lazima kuweka mazingira bora ya uzalishaji wa madini hayo ikiwemo kuwezesha biashara hiyo   na kuutaja mgodi wa makaa ya mawe wa Kabulo unaomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwa ni eneo jingine ambalo miundombinu ya barabara ni lazima iboreshwe kuwezesha  ufanisi zaidi wa shughuli za uzalishaji madini hayo.

Alisema kuwa, ili serikali iendelee kupata mrabaha zaidi kutokana na rasilimali hiyo suala hilo lazima lichukuliwe kwa uzito ili kuongeza mapato zaidi.

Aidha, akijibu ombi la kampuni hiyo kutaka kurudishiwa eneo ambalo lilitolewa kwa ajili ya Kiwanda cha Dangote na Rais John Magufuli, kwa kuwa bado haijanza kuchimba mpaka sasa, Naibu Waziri Nyongo alizitaka pande zote ikiwemo wizara na kampuni hizo kukutana Januari 22 mara baada ya kikao cha wadau wa sekta ya madini ili kujadili suala hilo ili hatimaye shughuli za uzalishaji zianze katika eneo hilo.

Mbali na hilo, kampuni hiyo ilimwomba Naibu Waziri kuwezesha upatikanaji  wa leseni mbili zilizoombwa na kampuni hiyo ikilenga kutumia makaa hayo kuzalisha umeme  kwa ajili ya matumizi ya mgodi. Naibu Waziri aliahidi kuwa, kupitia Tume ya Madini, suala hilo litakuwa limekamilika ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliitaka Halmashauri ya Mbinga kubuni miradi kwa ajili ya vijana na wanawake yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya majumbani na kuachana na matumizi ya mkaa kwa kuwa umekuwa ukisababisha uharibifu wa mazingira.

Wakati huo huo, akizungumzia suala la Mrabaha wa serikali  wa asilimia 3, alisema usilipwe kwa bei ya maeneo ya uchimbaji   bali ulipwe kwa bei ya sokoni. Hivyo, aliwataka wazalishaji wote na Maafisa wa Tume ya Madini kuhakikisha wanatoza bei ya sokoni na siyo ya uzalishaji.

Sughuli za upakiaji Mkaa ya Mawe zikiendelea katika Mgodi wa TANCOALtayari kwa ajili ya kusafirishwa maeneo mbalimbali.

Kwa upande wake, Meneja wa  mgodi  Mhandisi  David  Kamenya akizungumzia ubora wa makaa hayo, alisema kuwa, Makaa ya Ngaka yana ubora wa kimataifa  na ndiyo sababu imepelekea kupata wateja wengi kutoka nchi mbalimbali na kuongeza kwamba makaa hayo yana uwezo wa kufanya matumizi mbalimbali na kuongeza kuwa, kwa siku kampuni hiyo inapakia idadi ya magari yapatayo 100.

AKizungumzia malengo ya baaaye, alisema kuwa, idadi ya mashine ndani ya siku chache zinatarajiwa kuongezwa na kwamba kampuni imelenga kuzalisha hadi tani 5,000 kwa siku kutoka 3,000 za sasa.

Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana na akina mama, alisema kuwa, tayari kipo kikundi cha wakina Mama cha Mbarawala ambacho kimewezeshwa na  mgodi huo kwa kupatiwa mafunzo  ya namna ya kuandaa makaa hayo maalum kwa matumizi ya majumbani na kuongeza kuwa, hivi karibuni kikundi hicho kimepata  Cheti cha ubora kutoka shirika la Viwango nchini (TBS) jambo ambalo litawezesha kikundi hicho kuuza  makaa yake kwa ajili ya matumizi ya majumbani na hivyo kupunguza matumizi ya mkaa unaotokana na kukatwa miti.

Pia, Mhandisi Kamenya alimweleza Naibu Waziri Nyongo kuwa, mbali na kupatiwa mafunzo kikundi hicho pia kimepatiwa mashine ambayo inauwezo wa kuzalisha tani mbili za makaa hayo kwa saa.

Akishukuru kwa niaba ya kikundi, Meneja Usimamizi wa Mbarawala, Joyce Haule alisema kuwa,  wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwawezesha na  kwamba kikundi kinalenga kuzalisha tani 10 kwa siku na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari kimepata wateja kutoka maeneo mbalimbali zikiwemo nchi za Rwanda ambao  awali walitaka kwanza kikundi hicho  kuwa na cheti cha ubora wa makaa hayo.

Baadhi ya magari yakisubiri kupakia makaa ya mawe tayari kwa kusafirishwa maeneo mbalimbali ndani nan je ya nchi,

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Cosmas Ishenyi alimweleza Naibu Waziri kuwa, kama Wilaya itahakikisha kuwa, inashirikiana na mamlaka zinazohusika kuweka mazingira bora ya kuwezesha mundombinu bora ya barabaraba  ili TANCOAL iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi.

Katika hatua nyingine, akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Prof. Riziki Shemdoe, ofisini kwake Januari 18, Naibu Waziri alimweleza Prof. Shemdoe umuhimu wa kuwezesha miundombinu ya barabra kuelekea katika mgodi huo wa Ngaka.

Pia, Naibu Waziri alimweleza Prof. Riziki kuhusu mipango ya Serikali ya kuwa na vituo kwa ajili ya biashara ya madini na umuhimu wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hizo. “ Tunataka kuwa na utaratibu wa kuwa na maeneo ya kuuza na kununua madini ili kuwa na  utaratibu maalumu,” aliongeza

Kwa upande wake, Prof. Shemdoe alimwomba Naibu Waziri kusaidia upatikanaji wa wawekezaji kwa ajili ya viwanda vya kuchenjua dhahabu mkoani humo na kukumbushia suala la uchimbaji madini katika Mto Muhuwesi.

TANCOAL ni kampuni yenye ubia na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) ambapo serikali inamiliki hisa kwa asilimia 30.

Read more

Waziri Biteko, Prof. Msanjila wautaka mgodi wa North Mara kutii mamlaka za Serikali

Na Nuru Mwasampeta

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameutaka uongozi wa mgodi wa North Mara kutii Mamlaka ya Serikali kwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na mamlaka za Serikali nchini.

Waziri wa Madini, Doto Biteko, akiwasomea viongozi wa north Mara baadhi ya taarifa alizonazo juu ya masuala ya tathmini za fidia ya ardhi zilizofanywa namatokeo yake pamoja na kile wanachopaswa kuwa wamekitekeleza mpaka siku ya kikao hicho tarehe 17 Januari, 2019

Biteko alitoa kauli hiyo Jana tarehe 17 mwezi Januari katika kikao kilichoanza kwa utulivu mkubwa lakini kadri dakika zilivyokuwa zikisonga mbele kiligeuka kichungu na kuwapelekea wajumbe kutoka mgodi wa North Mara na Bulyanhulu kuridhia kuanza kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka mgodi huo ambao wamekaa kwa muda mrefu pasipo kulipwa fidia zao.

Katika kikao hicho, Waziri wa Madini, Doto Biteko, alianza kwa kuwahoji viongozi wa mgodi wa North Mara na Bulyankulu juu ya  changamoto kubwa iliyopo katika eneo lao ambapo bila kusita walikiri wazi kuwa ni suala la malipo ya fidia ya ardhi kwa wananchi wanaouzunguka mgodi huo.

Akizungumzia ukiukwaji katika kutekeleza maagizo ya Serikali Waziri Biteko aliwaeleza wajumbe hao kuwa ili kuonesha wanatii mamlaka ya Serikali walipaswa kuwa wamechukua hatua kadhaa katika kuelekea kutatua changamoto hiyo.

Biteko alionesha kusikitishwa na mwitikio unaooneshwa na wawekezaji hao ambao kutoka kikao cha mwisho kilipokaa na kuafikiana kuanza kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo ni miezi minne na hakuna chochote kilichofanyika.

“Hatuwezi kuwa tunakaa, tunafikia maamuzi ninyi mnayapinga, ni nani yupo juu ya Serikali” Waziri Biteko alihoji. “Mnajua suala la ardhi ni kubwa sana, mnajua ni maelekezo ya Rais, sasa Rais ameagiza halafu hakitokei kitu! Mimi sielewi kabisa. Afadhali watu wangeanza kulipwa unaweza sema sasa hatua za malipo zinafanyika lakini kuko kimya”aling’aka.

Akizungumzia chanzo cha mgogoro kuchukua muda mrefu Biteko alisema ni tathmini iliyofanyika kwa mara ya pili  kupelekea kiasi cha fidia mgodi unaopaswa kuwalipa wananchi kuongezeka kutoka bilioni 1.6 hadi kufikia  bilioni 12.

Akifafanua hilo mara baada ya kuzungumza na mthaminishaji Mkuu wa Serikali (jina halikupatikana) kwa njia ya simu, Biteko alisema ameelezwa kwamba tathmini inayofuatwa ni ile iliyofanyika kwa mara ya pili maana hiyo ndiyo current na kukazia kuwa hawawezi kufuata ya awali kutokana na kwamba muda wa kuwalipa fidia hizo ulipaswa kutokuzidi miezi sita tangu tathmini kufanyika.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akipiga simu kwa Mthamini Mkuu wa Serikali (jina halikupatikana mapema) kuhoji juu ya kile viongozi wa North Mara wanadai kuwa changamoto katika kutekeleza suala la ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo.

Ilielezwa kwamba, mara baada ya tathmini kufanywa kwa ajili ya malipo ya fidia, haipaswi kuzidi miezi sita na baada tu ya tathmini kufanyika; walipaswa kutoa tangazo ili kusimamisha uendelezaji wa maeneo ili kutokuongeza uwekezaji utakaopelekea wananchi kulipwa zaidi.

Biteko alieleza kuwa wananchi wanaomiliki maeneo hayo wakiendelea kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao baada ya miezi sita kutoka tathmini ilipofanyika ni dhahiri kuwa gharama ya kumlipa fidia mwananchi huyo itaongezeka tu.

Aidha, Biteko aliwaeleza wajumbe hao kuwa uongozi wa mgodi huo hawazifuati mamlaka husika katika kutatua changamoto hiyo na kubainisha kuwa mgogoro huo hautatatuliwa na wizara ya Madini isipokuwa ni watu wenye mamlaka na masuala ya ardhi.

Akijibu hoja ya mmoja kati ya wajumbe kutoka North Mara aliyejaribu kueleza kuwa kiongozi mkuu wa masuala ya kisheria katika mgodi huo anayeishi nchini Uingereza ni sharti aelezwe pindi maamuzi na maagizo yeyote yanapopokelewa katika mgodi ili kufanya maamuzi yanayokidhi matakwa ya mgodi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila alihoji endapo north Mara ipo juu ya Serikali?

Prof. Msanjila aliendelea kwa kusema haiwezekani mtu asiyekuwa na maamuzi katika mgodi kushiriki katika vikao vinavyojadili na kutoa maamuzi halafu mtu asiyeshiriki katika vikao hivyo akapinga maamuzi hayo.

“Yaani Waziri atoe maamuzi halafu mtu aliyeko Uingereza ayapinge that is totally subbodination maamuzi  ya mwisho yakishafanywa na Serikali hakuna serikali nyingine au kampuni yoyote ile iyapinge! Maamuzi yanayotolewa Tanzania hayawezi kwenda kujadiliwa London sio Sheria hiyo, ndio maana kampuni lazima iwe imesajiliwa Brella, kwa hiyo mambo ya kusema mshauri yupo London, South Africa No”. Alikazia Msanjila.

Msaidizi wa Waziri Kungulu Masakala ( wa Kwanza Kushoto), Wawakilishi kutoka Tume ya Madini, na Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Sera na Mipango Glads Qambaita wakiwa katika kikao baina ya Wizara chini ya Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) na uongozi wa mgodi wa North Mara.

Don’t talk about London or South Africa tunapoongelea masuala ya Tanzania tunaongea  kwa sheria za Tanzania we have nothing to do with London hiyo ni yao” alisisitiza.

Msanjila aliwakumbusha makubaliano waliyoafikiana katika vikao vya nyuma kuwa yaliyowataka wajumbe wa vikao vya maamuzi wasiokuwa na nguvu ya kufanya nakutekeleza makubaliano ya kikao wasishiriki katika vikao hivyo ili kuepuka kupotezeana muda.

Huyu ni waziri, anamwakilisha Rais, hamuwezi kwenda kuomba ushauri London kwa maagizo yaliyotolewa na waziri, hiyo si sheria. Prof. Msanjila Alikazia.

Baada ya mahjiano makali na yaliyochukua muda mrefu kikao kilifikia muafaka na ujumbe kutoka North Mara kukiri kuwa kutokana ukweli kwamba baadhi ya wananchi waliofanyiwa tathmini malipo yao hayana shida watakwenda na kuanza kufanya taratibu za malipo.

Walikiri kuwa mara baada ya kufika katika vituo vyao vya kazi watakwenda kuendelea na taratibu za malipo ili kuonesha uungwana na kuionesha Serikali na jamii kuwa wamechukua hatua kwa makubaliano yaliyoafikiwa na viongozi wakuu wa nchi.

Aidha, walikiri kuwa wamejifunza kitu kutokana na kikao hicho na kukiri wanaendelea kujifunza kwani wameona madhara makubwa katika kuchelewesha malipo hayo na kuipelekea kampuni hasara kwa kulipa zaidi ya mara mbile ya kile walichotakiwa kulipa awali.

Zaidi ya hapo, wamejifunza juu ya uhalisia wa kisheria upande wa  tathmini ya ardhi kuwa huwa  hai kwa kipindi cha miezi sita na ikizidi hapo inafanyika tathmini nyingine lakini pia wamejifunza juu ya taratibu na sheria za kusitisha shughuli za maendeleo kwa wananchi kwa kutangaza kusimamisha shughuli za maendeleo katika maeneo yaliyofanyiwa tathmini kwa kipindi cha miezi sita na pia kulipa fidia kwa wakati ili wananchi wakajiendeleze katika maeneo mengine watakayohamia.

Aidha, Bi Jane Reuben- Lekashingo alisema kuwa si lengo lao kupinga maamuzi ya serikali ila wanachelewa kutokana na taratibu za kiutendaji wanaazopaswa kuzifuata  ili kukidhi matakwa na taratibu  za kampuni katika kutekeleza majukumu yao na kukiri kuwa sasa watasimamia sheria za nchi na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa katika vikao vya maamuzi.

Read more

Madini kuweka msukumo miradi ya Liganga, Mchuchuma

Na Asteria Muhozya, Ludewa

Wizara ya Madini imesema itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kuweka msukumo ili kuhakikisha  kwamba miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na ule wa Chuma Linganga inaanza kutekelezwa.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akitoka katika Ofisi za Wilaya ya Ludewa tayari kwa ziara ya kutembelea katika mgodi wa Liganga kwa ajili ya kujionea changamoto za utekelezaji wa mradi huo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere.

Kauli hiyo ilitolewa Januari 16 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za madini mkoani Njombe  na kuona namna ya kutatua changamoto  zinazohusu Wizara ya Madini   katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Alisema miradi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo Taifa linatarajiwa kunufaika kwa kiasi kikubwa, hivyo kutokana na umuhimu wake, wizara ya madini itashirikiana na wizara hiyo kuhakikisha hatua zaidi zinapigwa ili hatimaye miradi hiyo ianze kutekelezwa kwa kuwa imechukua muda mrefu.

Aliongeza kuwa, ni miradi mikubwa ambayo taifa linatarajiwa kunufaika nayo  kupitia ajira  na kuongeza pato la nchi huku akiyataja madini ya chuma kuwa  moja ya malighafi muhimu kwa uchumi  wa Tanzania ya viwanda  na kusema kuwa, kama taifa, linautolea macho mradi huo na kwamba serikali imedhamiria kuutekeleza.

Aliongeza kwamba, katika Serikali ya Awamu ya Tano, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anayo imani kubwa  kuwa  miradi hiyo itaanza huku  serikali ikitegemea  kupeleka  maendeleo  kwa wananchi kupitia miradi husika.

“Wizara yetu ndiyo inatoa leseni za madini na tayari tulishatoa leseni ya Makaa ya mawe mchuchuma kwa hiyo nimefika kuangalia changamoto ambazo ziko upande wa wizara yetu kuweza kuzitatua ili tutoke hapa. Miradi hii tumeisikia miaka mingi ni wakati sasa tunataka ianze.” alisisitiza Nyongo.

Aliongeza kuwa, ikiwa wizara ndiyo inatoa leseni za madini,  inaowajibu wa kujua yule aliyepewa leseni kama anaifanyia kazi na kuongeza, “Sisi tuliotoa leseni lazima tuangalie tuliyempa leseni amekwama wapi  lakini pia tujue  miradi hii inaanza lini? Makaa ya mawe na chuma vyote vinahitajika kwa taifa. Tunatambua makaa ya mawe ni madini ambayo yana tija kwa uchumi kwa nchi,” alisema Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiangalia makaa ya katika mgodi wa Liganga alipoutembelea hivi karibuni. Naibu Waziri alifanya ziara hiyo kwa lengo la kujua changamoto za utekelezaji wa mradi huo. Anayemweleza jambo ni Mtalaam kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mhandisi Paschal Malesa.

Akifafanua zaidi kuhusu miradi hiyo alisema kuwa, mradi wa Makaa ya Mawe unatarajiwa kuzalisha umeme ambao mbali ya kuuza kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), umeme huo unatarajia kutumika katika kuzalisha madini ya Chuma Liganga.

“Mpango ni Liganga kutumia megawati 250 kwa shughuli zake za kuzalisha chuma na megawati 350 zitauzwa Tanesco kuzalisha umeme,” aliongeza.

Akifafanua sababu za kuchelewa kwa miradi hiyo, alisema ni kutokana na changamoto za kimkataba ambazo bado ziko katika majadiliano katika ngazi za juu na kuitaja baadhi ya mikataba hiyo kuwa ni  kuwa ni pamoja na mikataba ya upunguzaji wa kodi.

Aliongeza kuwa, wizara ya madini ikiwa ni wizara ambayo inasimamia Sheria ya Madini, imelenga kuhakikisha kwamba miradi hiyo mikubwa inaanza ili hatimaye iweze kuwanufaisha watanzania na taifa.

Akielezea suala la fidia kwa wananchi waliopisha miradi hiyo, alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ludewa kwa kutenganisha suala la miradi hiyo na fidia  ambapo alisema kwamba taratibu za juu zikikamilika, wananchi watalipwa fidia  na hivyo kuwataka kuwa na subira na kuwa tayari kupisha utekelezaji wa miradi hiyo.

Awali,  Mkuu wa Mkoa wa Njombe , Christopher Ole Sendeka alimweleza waziri umuhimu wa wizara ya madini kujielekeza  kwenye kupata taarifa halisi kuhusu tafiti zilizofanyika awali kuhusu  akiba iliyopo ya madini ya chuma  Liganga na Makaa ya Mawe mchuchuma.

Aidha, aliongeza kuwa, mbali na chuma na makaa ya mawe mkoa huo unayo madini mbalimbali ikiwemo dhahabu ambayo bado haijachimbwa kwa kiasi kikubwa.

Miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na Chuma Liganga, inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda Group Ltd, ya China.

Pia, akiwa mkoani humo, Naibu Waziri alitembelea mgodi wa Kokoko Kokoto wa Nyakamtwe Quary, ambapo alitoa changamoto kwa mmiliki wa mgodi huo kuongeza kasi ya uzalishaji na kuwa wabunifu kutumia fursa  za miradi mikubwa ya ujenzi  inayotekelezwa na serikali ikiwemo ya ujenzi wa reli ili kokoto hizo ziweze kutumika.

Read more

Wachimbaji madini Suguta wapata leseni

 • Watoa pongezi kwa Mwenyekiti Tume ya Madini

Na Greyson Mwase, Dodoma

Kikundi cha wachimbaji wadogo wanaojishughulisha na  uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika machimbo ya Suguta yaliyopo katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, kijulikanacho kwa jina la “Hapa Kazi Tu” kimepongeza Tume ya Madini kwa kutatua mgogoro uliokuwepo kwa muda mrefu pamoja na kuwapatia leseni.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Jonas Mwano (kulia) akimkabidhi leseni ya madini Mwenyekiti wa Kikundi cha wachimbaji wadogo wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika machimbo ya Suguta yaliyopo katika Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, kijulikanacho kwa jina la “Hapa Kazi Tu”, Elisha Cheti (kushoto)

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 16 Januari, 2019 katika makabidhiano ya leseni ya uchimbaji wa madini hayo katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma zilizopo jijini Dodoma.

Kutatuliwa kwa mgogoro kati ya kikundi hicho na wananchi wa kijiji cha Suguta ni matokeo ya ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula aliyoifanya mapema Septemba 05, 2018 katika machimbo hayo na kukuta kikundi hicho kikiendesha shughuli za uchimbaji wa madini pasipo kusajiliwa na kutokuwa na leseni ya uchimbaji wa madini.

Mara baada ya kufanya ziara katika eneo husika Profesa Kikula alielekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini wa Mkoa wa Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa  Dodoma, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius John Ndejembi kuhakikisha kikundi cha wachimbaji hao kinasajiliwa na kupatiwa leseni ndani ya muda mfupi.

Aidha, Profesa Kikula alimwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini wa Mkoa wa Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto kuhakikisha mgogoro uliokuwepo kati ya kikundi hicho na wananchi wa kijiji cha Suguta unamalizika.

Akitoa shukrani hizo kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha “Hapa Kazi Tu” Elisha Cheti alisema kuwa ziara ya Profesa Kikula ilipelekea kuongezeka kwa kasi ya usajili wa kikundi na hatimaye wakafanikiwa kuomba leseni ya kuchimba madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma.

Alisema mara baada ya kupata leseni pamoja na barua ya utambulisho wanatarajia kuanza shughuli za uchimbaji madini na kulipa kodi na tozo mbalimbali Serikalini.

Naye  Mwenyekiti wa DOREMA, Kulwa Mkalimoto mbali na kuipongeza na kuishukuru Tume ya Madini kwa utoaji wa leseni amekitaka kikundi kilichopewa leseni kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini kwa kufuata sheria na kanuni za madini huku kikihakikisha hakuna uharibifu wowote wa mazingira.

Naye Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Jonas Mwano akizungumza wakati wa makabidhiano hayo alifafanua kuwa, maombi ya leseni ya uchimbaji wa madini ya kikundi husika yalipitishwa kupitia kikao cha Kamati ya Ufundi ya Tume kilichokaa tarehe 22 Novemba, 2018.

Mwano alitoa wito kwa wachimbaji wadogo wasio rasmi kuunda vikundi, kusajili na kuomba leseni na kusisitiza kuwa ofisi yake itahakikisha leseni za madini zinatolewa kwa kasi ili waweze kuchimba pasipo kusumbuliwa huku wakilipa kodi na tozo mbalimbali Serikalini.

“Sisi kama Tume, tunaamini wachimbaji wadogo wana mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa sekta ya madini; tunaunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli za kuhakikisha watanzania wote wananufaika na rasilimali za madini,” alisisitiza Mwano.

Read more

Waziri Biteko akutana na kampuni ya Tanzaplus

Na Greyson Mwase,

Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 16 Januari, 2019 amekutana na kampuni  inayojishughulisha na uyeyushaji wa madini ya bati katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ya Tanzaplus katika Ofisi za Wizara ya Madini zilizopo jijini Dodoma.  Kikao chake  pia kilishirikisha Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Mhandisi Migodi Mkuu kutoka Tume ya Madini, Conrad Mtui pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Madini. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kampuni ya Tanzaplus Minerals kwa kushirikiana na kampuni nyingine ya AIMGROUP kutambulisha teknolojia ya mfumo wa usimamizi wa uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa madini. Waziri Biteko aliitaka kampuni ya Tanzaplus kuendelea kufanya utafiti zaidi juu ya mfumo husika kwa kushirikisha wadau mbalimbali  kabla ya kuwasilisha pendekezo lake Serikalini.

Read more

Biteko akutana na wawekezaji mradi wa uchimbaji wa uranium

Na Nuru Mwasampeta, Dodoma

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka  kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini  ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One  kutokusita kuwasiliana naye pindi wanapokutana na changamoto katika utekelezaji wa  mradi wao.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akisalimiana na Mkurugezni Mkuu wa kampuni ya Uranium One Holdings N.V, Vladimir Hlavinka mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick Kibodya.

Aliyasema hayo jana  tarehe 15 Januari, 2019 katika kikao chake na watendaji wa kampuni hiyo kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma.

Aidha, Biteko alisema kuwa maombi yote ya leseni kubwa za uchimbaji wa madini zinawasilishwa katika baraza la Mawaziri ili kuweza kuridhiwa baada ya wawekezaji kuonesha nia na kuwasilisha maombi ya leseni hizo.

Biteko alikiri kuwa anao uelewa wa kile kinachoendelea katika uwekezaji huo kutokana na ushirikishwaji alioupata kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki kupitia vikao mbalimbali alivyoshiriki.

Akizungumzia lengo la ujio wao katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium One, Frederick Kibodya alisema ni kuelezea maendeleo waliyofikia katika uwekezaji huo pamoja na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Madini.

Alisema, uteuzi huo umelenga katika kukuza sekta ya madini ikiwa ni pamoja na mradi wa uchimbaji wa madini ya uranium, “Tunaimani kubwa kwako na tunamshukuru Mungu kwa kukupa nafasi hii” alisema Kibodya.

Akizungumzia uwekezaji uliofanyika mpaka sasa katika mradi huo alisema ni kiasi cha dola za kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) kutoka mradi ulipoanza mwaka 2009.

Akizungumzia manufaa ya mradi huo  Kibodya alisema ni pamoja na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Alisema madini hayo yakichimbwa yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolijia mpya nchini.

Waziri wa Madini, Doto Biteko akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mantra, Fredrick Kibodya akichangia mada katika kikao baina ya wizara na kampuni ya Uranium One Holdings N.V ofisini kwa waziri jijini Dodoma

Mradi utasaidia katika kuongeza ajira nchini. Aliendelea kufafanua kuwa kwa kipindi cha ujenzi wa mradi wanatarajia kuajiri watanzania 1600 kwa kipindi cha miezi kumi na nane.

Aidha, alibainisha kuwa kutakuwepo na uzalishaji wa ajila zisiso rasmi kiasi cha watu 4500 wakati wa ujenzi na 2300 pindi uzalishaji utakapoanza.

Alisema, mradi utasaidia katika kuhamisha utaalamu kutoka kwa wawekezaji kwenda kwa wazawa na mradi umelenga katika kutoa elimu ya ajira na utaalamu kwa wazawa.

Pia Kibodya alisema, mradi unatarajia kuliingizia taifa pato la kiasi cha dola za kimarekani milioni 220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho  kitakuwa kikibadilika kadri uzalishaji unavyoongezeka.

Mradi wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Mbia wa kampuni ya Mantra anayejulikana kama Rosatom.

Read more

Naibu Waziri Nyongo aamuru kukamatwa wamiliki Mgodi wa Nyakavangala

Na Asteria Muhozya, Iringa

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameamuru kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala unaomilikiwa na  Thomas Masuka and Partners  kufuatia wamiliki hao kutofautiana juu ya taarifa  waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha wa serikali.

Sehemu ya wachimbaji wadogo wakifuatilia mkutano baina yao na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo. (Hayupo pichani)

Aidha, Naibu waziri amewataka wamiliki hao kutoa maelezo ya kina kuhusu ni lini watalipa kodi zote wanazodaiwa na serikali baada ya kuonekana kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya shilingi milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi.

Katika ziara yake mkoani humo, Naibu Waziri alisema kuwa pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

Pia, amemtaka Afisa Madini kutoa maelekezo ya kina kuhusu suala zima la ulipwaji wa kodi na mrabaha wa serikali, huku akiagiza zoezi hilo pia limuhusishe Afisa Msimamizi wa madini aliyekuwepo katika kipindi ambacho fedha hizo hazikulipwa.

“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu  Waziri.

Wakati akizungumza na wachimbaji katika mkutano wa hadhara, amewataka wachimbaji hao kuchimba kwa kuzingatia usalama  huku akisisitiza suala la kufuata sheria na taratibu  huku akiwataka kutoa taarifa za  uhakika kwa wale wote wanaokikuka sheria ikiwemo watoroshaji wa madini huku akisisitiza  utoaji  taarifa hizo usiwe wa majungu.

Akitolea ufafanuzi suala la fedha za mrabaha, amesema fedha hizo hazipaswi kuelekezwa katika masuala mengine na wamiliki wa migodi ikiwemo kutumiwa katika huduma za jamii badala yake  zinapaswa kulipwa serikalini.

Afisa Madini anayesimamia Mikoa ya Iringa na Njombe Wilfred Machumu akieleza jambo wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na wamiliki wa mgodi wa Thomas Masuka and Partners. Kulia ni Naibu Waziri Nyongo. Nayefuatia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela aliwataka wamiliki hao kukaa chini na kukubaliana namna ya kulipa kiasi cha fedha ambacho wanadaiwa na serikali huku akimtaka Afisa kutoka Halmashauri anayehusika na masuala ya usimamizi wa fedha kuhakikisha kwamba fedha ambazo mgodi huo ulipaswa kuzilipa kama mrabaha zinapatikana.

Mgodi huo wa Nyakavangala unamilikiwa na Thomas Masuka kwa ushirikiano na wawekezaji wengine wazawa wapatao 20. Wakati akiagiza kukamatwa kwao, wamiliki 8 kati ya 20 ndiyo walikuwa wamehudhuria kikao kati yake na wamiliki hao.

Naibu Waziri Nyongo alitoa agizo hilo Januari 15 wakat akihitimisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.

Read more

Naibu Waziri aagiza wanunuzi haramu wa dhahabu Ulata kukamatwa

Kufuatia kukaidi Wito wa kuonana na Naibu Waziri wa Madini  Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela kutokana na kufanya ununuzi haramu wa madini ya dhahabu ikiwemo kufadhili uchimbaji haramu, Naibu Waziri Nyongo amevitaka vyombo vya  Ulinzi na Usalama mkoani Iringa kuwakamata Mansoor  Almasi na Jacob Mwapinga iwapo watashindwa kuripoti wenyewe katika Mamlaka zinazohusika.

Naibu Waziri wa Madini Stansaus Nyongo akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua mgodi wa Nyakavangala. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo la kukamatwa wahusika hao baada ya kukiuka agizo la kuonana na viongozi hao  kwa hiari ambapo walielekezwa kuonana na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa  Januari 15.

Pia, kabla ya wito wa Naibu Waziri, awali, wahusika hao walitakiwa kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa wakiwemo Maafisa Madini kwa ajili ya kuupatia suluhisho mgogoro huo katika mgodi wa dhahabu wa Ulata, kijiji cha Ulata wilaya ya Iringa unaomilikiwa na Ibrahimu Msigwa.

Naibu Waziri Nyongo alibaini kuwa Mansoor na Mwapinga wanafanya ununuzi wa madini  kinyume cha Sheria  ikiwemo kufadhili  shughuli za uchimbaji katika mgodi ambao siyo wamiliki wake.

Pia, Naibu Waziri ameelekeza baada ya  wahusika hao kukamatwa wanatakiwa kutoa maelezo  kueleza ni lini watalipa kodi wanazodaiwa na serikali  baada ya kufanya shughuli hizo bila kulipa kodi.

Akizungumza  katika mkutano wa hadhara na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo aliwaeleza kuwa, Serikali inamtambua Ibrahimu Msigwa kama mmiliki halali baada ya kuwa na vibali vya kumiliki leseni ya mgodi huo na hivyo kutoa wito wa kuonana na pande zote ili kuhakikisha  kuwa anatoa suluhisho la mgogoro uliopo baina ya Msigwa, Mansoor, Mwapinga na wachimbaji.

Akihitimisha ziara yake mkoani Iringa Januari 15, Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi katika migodi  ya Ulata na  Nyakavangala.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimwonesha jambo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua migodi ya Nyakavangala.

Amesema wamiliki wa leseni wanaotumia mrabaha kwa ajili ya kufanya masuala mengine ya kijamii wanakiuka taratibu na kueleza kuwa, fedha za kufanyia shughuli za maendeleo zinapaswa kutoka katika fedha za Uwajibikaji kwa jamii ambazo halmashauri zinapanga kupitia Baraza la Madiwani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema wahisika  Mwapinga na Almasi wana kiburi na kwamba waliitwa kwa ajili ya kuongea ili ku[ata fursa ya kujieleza na a kueleza ni lini watalipa mrabaha  lakini wamekaidi hivyo kinachofuatia ni wahusika kukamatwa.

Naibu Waziri Nyongo alifanya ziaea katka mgodi wa Ulata Janauri 14 akilenga kukagua shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo ikiwemo kutatua mgogoro uliokuwep katika mgodi huo baina ya mmiliki halali Ibrahimu Msingwa, wanunuzi  haramu  wa madini hayo Mansoor Almasi na Jacob Mwapinga.

Read more

Nyongo ataka wanaomiliki migodi kwa kuvamia wasimame mara moja

Na Asteria Muhozya, Iringa

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wanaomiliki migodi kwa kuvamia maeneo bila kuwa na leseni, wasimame mara moja.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiteta jambo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa, Hashim Komba wakati akiondoka katika eneo la mgodi wa Ulata kijiji cha Ulata Wilaya ya Iringa, mara baada ya kuzungumza na wachimbaji wadogo na kutatua mgogoro uliokuwepo mgodini hapo.

Naibu Waziri Nyongo ametoa kauli hiyo katika  mgodi wa Ulata kijiji cha Ulata wilayani Iringa , wakati wa ziara yake iliyolenga  kukagua shughuli za uchimbaji madini ikiwemo kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wadogo.

Aidha, kauli ya Naibu Waziri inafuatia mgogoro uliopo katika mgodi huo kati ya  mwenye leseni ya kumiliki mgodi huo Ibrahim Msigwa , wachimbaji wadogo wanaochimba katika eneo hilo na  Mansoor Almasi anayetajwa kuwa mmiliki mwingine na mnunuzi wa madini  ya dhahabu yanayochimbwa mgodini hapo ambaye kwa mujibu wa taratibu,  hana  vibali  vinavyomruhusu kufanya shughuli hizo.

Akilenga kutatua na kuumaliza mgogoro uliopo mgodini hapo, Naibu Waziri amemtaka Mansoor Almas, kufika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa ifikapo Januari 15, na endapo atakiuka agizo hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Sisi kama serikali ambao ndiyo tunatoa vibali tunamtambua bwana Msigwa kuwa ndiye mmiliki halali. Nataka kuonana na huyu Mansour na yoyote anayedharau serikali tutakula nae sahani moja,” alisisitiza Naibu Waziri.

Naibu Waziri alisema lengo la kutaka Mansour kufika wilayani hapo ni kutaka kusikia kutoka pande zote ili  mgogoro huo uweze kutatuliwa na kufika mwisho jambo ambalo litawezesha  shughuli za uchimbaji katika eneo husika kuendelea vizuri  ili pande zote yaani serikali na wachimbaji wanufaike.

Akifafanua kuhusu suala la shughuli za uchimbaji, Naibu Waziri amesisitiza kuwa, ili kuwa mchimbaji halali ni lazima kuwa na kibali kutoka serikalini na kuongeza kwamba, ni vigumu kuomba kwenye leseni ya mtu mwingine.

Pia, amewataka wachimbaji wadogo kutoshirikiana na wale wote wanaopindisha  utekelezaji wa sheria na taratibu katika shughuli za uchimbaji madini na badala yake washirikiane na wale wenye vibali vya umiliki  kutoka serikalini.

Afisa Madini Mkoa wa Iringa na Njombe Mhandisi Wilfred Machumu akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri na wachimbaji katika mgodi wa Ulata, kijiji cha Ulata. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Iringa, Hashim Komba.

Pia, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wale wote wasiokuwa na uwezo wa kuchimba kuingia mikataba na wachimbaji wengine wenye uwezo ili kuwezesha lengo la kumiliki leseni kutimia kwa kuhakikisha kwamba zinafanyiwa kazi. “ unaweza kuingia mkataba na mchimbaji  wengine wakiwemo wa kati

“ Nataka muelewe kwamba, mnaochimba mnachimba kwa niaba ya watanzania kwa sababu watanzania ambao siyo wachimbaji. Hawa wanafaidika kutokana na kodi na mrabaha unaolipwa kutokana na shughuli zenu, kwa kuwa fedha hizo zinatumika katika kutoa huduma nyingine,” alisema Nyongo.

Awali, wachimbaji hao waliwasilisha kero kwa Naibu Waziri kuhusu mgogoro wa umiliki wa mgodi huo umesababisha shughuli za uchimbaji mgodini hapo kuwa mgumu suala ambalo linasababisha ugumu wa kupata kipato cha kujikimu na kuendesha familia zao.

Wachimbaji wao walimshukuru Naibu Waziri kwa kufika kwake mgodini hapo  ambapo walipata fursa ya kueleza kero ikiwemo  suala la bei elekezi ya madini hayo ambalo walimlalamikia kuwa, wamekuwa wakiwauzia wanunuzi wa  madini hayo akiwemo Mansoor Almasi na Ibrahim Msigwa kwa kiasi cha shilingi 45,000 kwa gramu moja jambo ambalo Naibu Waziri ameeleza kuwa, atakapoonana na wahusika hao atawaeleza kuhusu suala hilo.

Akitoa utetezi wake kwa Naibu Waziri kuhusu kero zilizowasilishwa dhidi yake na wachimbaji hao, Msigwa amesema mazingira mabaya mgodini hapo yaliyowasilishwa na wachimbaji yanatokana na kuwepo kwa kesi mahakamani jambo ambalo linamfanya ashindwe kuendelea na shughuli za uchimbaji kama inavyompasa.

Wakati huo, huo,  katika kikao na uongozi wa Mkoa wa Iringa, Katibu Tawala wa Mkoa huo Happines Seneda, alimweleza Naibu Waziri kuhusu umuhimu wa kuwa na Afisa Madini wa Mkoa huo badala ya kutegemea AFisa Madini wa Mkoa wa Njombe jambo ambalo ameeleza kwamba, uwepo wake mkoani humo utaongeza ufanisi katika ufuatiliaji wa shughuli za madini.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri Stanslaus Nyongo alimweleza  Katibu Tawala huyo kuwa, Wizara imelenga kuhakikisha kwamba kila Mkoa unakuwa na Afisa Madini baada ya kuondolewa kwa Makamishna wa Madini wa Kanda kufuatia Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Maboresho yake ya Mwaka 2017.

Naibu Waziri Nyongo alitembelea mgodi huo Januari 14, 2019.

Read more

Waziri Biteko aanza kazi

 • Awataka watumishi kufanyia kazi maagizo ya Rais Magufuli
 • Amshukuru Waziri Kairuki kuwa, amemfundisha Mengi
 • Aitaka STAMICO kuanza kutoa gawio kwa Serikali

 Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Menejimenti ya Wizara ya Madini, Taasisi zake pamoja na Wenyeviti wa Tume ya Madini na Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), jijini Dodoma, katika kikao ambacho pia kimejadili namna ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa wakati akimwapisha Waziri Biteko kushika wadhifa huo Januari 9, 2019.

Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi wakifuatilia kikao hicho

Biteko amewataka watumishi  wa Wizara na Taasisi zake ambao hawayajayasikiliza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhakikisha kuwa wanayasikiliza ili kuweka uelewa wa pamoja na kushirikiana katika kutekeleza majukumu  ya wizara kwa lengo la kuhakikisha kwamba sekta ya madini inaimarika.

“ Tuliulizwa dhahabu inauzwa wapi? Basi tusisubiri tena Rais atuulize inauzwa wapi,” amesisitiza Biteko.

Aidha, amesisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa pamoja miongoni mwa watumishi wa wizara katika utekelezaji wa majukumu hayo na kusisitiza kuhusu mabadiliko yanayoonekana kupitia sekta ya madini ikiwemo kufanya kazi na kuongeza kuwa, “ Kinachotuunganisha mahali hapa ni kazi na wala si dini ama jambo lingine,”.

Ameongeza kuwa, kiu kubwa ya Rais Magufuli ni kuona kuwa watanzania wote wananufaika na rasilimali madini huku akisisitiza kuwa, kiu yake binafsi ni kuona taswira nzuri inajengeka kuhusu sekta hiyo ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na kuongeza kuwa, matokeo bado hayaonekani.

“Vipaji mlivyonavyo mvitumie vizuri vitoe matokeo yanayoonekana. Fanyeni kazi ambazo zitaacha matokeo yatakayo dumu. Natamani ningezungumza na watumishi wote ili kila mmoja aelewe kile ninachosema,” amesisistiza Biteko.

Vilevile, amewataka watendaji kuchukua hatua badala ya kutumia muda mrefu kutafuta miongozo wakati wanapotekeleza majukumu jambo ambalo linachelewesha utekelezaji wa majukumu. “ Unasubiri mwongozo gani ilhali unayo Sheria ya Madini?amehoji Waziri Biteko.

Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi wakifuatilia kikao hicho

Pia, amechukua fursa hiyo kumshukuru aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki na kueleza kuwa, ni kiongozi ambaye amemfundisha mambo mengi.

“ Namshukuru sana dada yangu, rafiki yangu Angellah. Alinipokea vizuri sana. Hakuna ushirikiano nilioukosa kwake. Amenifundisha mengi ikiwemo kukaa kwenye kikao na kujadili mambo kwa kina,” amesema Biteko.

Pamoja na hayo, Biteko ametumia fursa hiyo kumshukuru Naibu Waziri Nyongo kwa kuwa naye pamoja katika kipindi chote ambacho alikuwa Naibu Waziri katika wizara ya madini.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko ameitaka STAMICO kuhakikisha kuwa, inaanza kutoa gawio kwa Serikali na ikiwezana, jambo hilo lifanyike kabla ya mwaka ujao wa fedha.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, awali akizungumza katika kikao hicho, amewataka watumishi ambao hawakupata fursa ya kusikia maagizo ya Rais Magufuli kufanya hivyo ili kila mmoja asimame kwa lengo moja.

“ Hatukusemwa vizuri. Nchi nzima imesikia na dunia imesikia. Tukiendelea hivi, hatutavumiliwa,” amesisitiza Nyongo.

Pia, ameitaka Tume ya Madini kuhakikisha inazingatia na kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli ikiwemo kutekeleza wajibu wao.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kwamba, kikao hicho ni cha kwanza na Waziri Mpya ikiwemo Mjumbe wa Bodi ya STAMICO na kuongeza kuwa, kinalenga kutoa utambulisho rasmi wa Waziri Mpya wa Madini na kusikia maelekezo ya Waziri Biteko kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo amemweleza Waziri Biteko kuwa, anayapokea majukumu yote yaliyo mbele yake ya kuhakikisha kwamba shirika hilo linatekeleza majukumu yaliyo mbele yake.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Januari, 2019.

Read more

Waziri Biteko apokelewa na Watumishi madini

Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta,

Waziri wa Madini Doto Biteko amewasili Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kupokelewa na Watumishi wa Wizara ya Madini na baadhi ya Taasisi zake.

Watumishi wa Wizara ya Madini wakimkaribisha Waziri wa Madini Doto Biteko katika wizara hiyo mara baada ya kuwasili kutoka kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Sambamba ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Biteko aliteuliwa kuwa Waziri wa Madini Januari 8 baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi.

Akizungumza na watumishi hao, amewataka kujipanga na kushirikiana pamoja na viongozi wa wizara na kuongeza kuwa, wao kama viongozi wanawategemea sana watumishi kuweza kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

“Mimi sio mgeni ni mwenyeji, wote tunafahamiana.  Nawashuru kwa kutupokea mimi na mwenzangu Nyongo. Ninyi ndiyo wenye wizara sisi hatuwezi kuwa hapa kama ninyi hamjatupa ushirikiano,” amesema Biteko.

Ameongeza kuwa, anataka kuona watumishi wa wizara hiyo wakiwa na furaha na kufanya kazi kwa furaha katika kutekeleza wajibu na majukumu ya wizara husika na kueleza kuwa, “Nataka nione wafanyakazi wanafurahi kufanya kazi. Kuna mtu unaweza kumlazimisha kufika kazini lakini si kufanya kazi,” amesema.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema mabadiliko yaliyotokea ni kwa ajili ya kuongeza ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu ya wizara na kuongeza kuwa, Rais Dkt. Magufuli wakati akimwapisha Waziri Biteko Januari 9, alitoa maagizo kwa viongozi hao, ambao wao waliyapokea kwa niaba ya watumishi wote wa wizara na taasisi zake.

Awali, Waziri Biteko alikuwa ni Naibu Waziri katika wizara hiyo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Waziri Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Read more

Biteko aapishwa kuwa Waziri wa Madini

Na Asteria Muhozya,

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ameapishwa leo Januari 9 kuwa Waziri wa Madini katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Biteko aliteuliwa Januari 8 kushika wadhifa huo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kufanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa wizara na taasisi.

Waziri Biteko anachukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji.

Read more

Biteko awaeleza watanzania kuwa Serikali ina macho

 • Aeleza itafika kokote madini yanakochimbwa pasipo vibali halali

Na Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewaeleza watanzania wasiofuata Sheria katika utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini kuwa Serikali inaona na itafika popote madini yanapochibwa pasipo vibali halali vya kufanya shughuli hiyo.

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Madini Prof. Simon Msanjila wakitoka katika jengo la ofisi za mwekezaji wa hifadhi za wanyamapori ya Makao, Mwiba Limited kuelekea eneo linalosadikiwa kuendesha shughuli za Uchimbaji hifadhini humo.

Biteko ameyasema hayo mwishoni mwa wiki, Tarehe 5 mwezi Januari, 2019 alipofanya ziara ya kukagua eneo ambako shughuli za uchimbaji wa madini ya shaba ulifanywa pasipo kibali na kubaini viashiria vya uchimbaji katika hifadhi ya Wanyama pori ya Makao iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Biteko alisema kumekuwa na viashiria vya kuwepo kwa watu wasiokuwa waaminifu na kujiingiza katika shughuli ya uchimbaji pasipokuwa na vibali jambo ambalo halikubaliki na halitavumilika. “Sisi madini yanatuuma, tukisikia kuna watu wanachimba tutafika mahali popote kujua madini hayo yanachimbwa na kupelekwa wapi” Biteko alikazia.

Aliendelea kwa kusema, huu mchezo ulifanyika sana na sasa nimekuja kuwaambia hautajirudia tena. Endapo mtu yeyote anataka kuchimba madini ya yoyote ikiwa ni pamoja na madini ya ujenzi kama vile mchanga wa kutengenezea barabara sharti afike katika ofisi zetu za madini aeleze nia na eneo analotakiwa kutengeneza barabara na wahusika watamuonesha eneo la kuchimba mchanga kwa utaratibu wa kisheria kwa matumizi hayo si kujiamlia tu.

Biteko alisisitiza kuwa lengo la ziara hiyo si kutoa kibali kwa watu kuchimba katika hifadhi  hiyo. “Sisi hatujaja kupromote watu wachimbe bali tumekuja kwa sababu watu wanachimba pasipo taratibu.

Alibainisha kuwa ili mtu yeyote apate kibali cha kuchimba katika hifadhi hiyo sharti apate kibali kutoka mamlaka kuu nne ambazo ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji kwa sababu katika hifadhi hiyo kuna vyanzo vya maji, Mamlaka ya Mazingira (NEMC)pamoja na Wizara ya Madini.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza Biteko aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila aliyeelezea sheria na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili mtu yeyote kuweza kujihusisha na shughuli za Madini.

Pori kwa pori mbugani, Prof. Simon Msanjila akiongoza wajumbe walioambatana kujiridhisha, kukagua pamoja na kutoa kauli ya serikali kwa wafanya biashara wa madini wanaojihusisha na biashara hiyo kinyume na taratibu na sheria ya nchi, Nyuma yake mwenye suti ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani

Aidha, Profesa Msanjila aliwataka watanzania kujua kuwa rasilimali madini zinazopatikana nchini ni kwa manufaa ya watanzania wote hivyo ni lazima wafuate utaratibu ili mapato yatokanayo na tozo mbalimbali kutokana na utafiti, uchimbaji na biashara ya madini ziwanufaishe watanzania wote. “Lazima niwaambie haya madini ni ya watanzania wote” alikazia.

Akizungumzia chanzo cha taarifa ya kuwepo kwa uchimbaji katika hifadhi hiyo Leons Welenseile (Mjiolojia) alisema mnamo mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alifanya ziara iliyolenga kutatua mgogoro baina ya kampuni ya inayomiliki leseni ya uwindaji wanyamapori katika hifadhi hiyo Mwiba Holdings Limited na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo baada ya wananchi kutoridhishwa na kile walichokuwa wakikipata kutoka kwa mwekezaji huyo.

Walipokuwa njiani kutoka katika kusuluhisha mgogoro huo ndipo wataalamu wa madini katika mkoa huo walikutana na loli lililobeba mchanga pasipokuwa na vibali halali vya kufanya uchimbaji huo nakubaini kuwa  shughuli hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni hiyo ya mwiba kwa lengo la kukarabati barabara katika hifadhi hiyo pasipo kujua kuwa walipaswa kuwa na leseni ya kuchimba mchanga huo na kupigiwa hesabu iliyopelekea kulipa mrabaha wa milioni 50 baada ya kukiri kufanya shughuli hiyo kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt. Joseph Eliaza Chilongani alikiri kutokuwa na taarifa za uchimbaji huo na kuwataka wataalamu na maafisa madini katika eneo lake kutoa taarifa pindi masuala ya ukiukwaji wa taratibu na sheria za nchi yanapotokea katika eneo lake ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto hizo.

Read more

Watumishi Madini waungana na wenzao kumpongeza Rais Magufuli kwa kutumika kikokotoo cha zamani

Na Asteria Muhozya,

Watumishi wa Wizara ya Madini wameungana na watumishi wengine nchini kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  kwa uamuzi wake wa kutangaza  kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.

Wafanyakazi wa Madini wakishiriki maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania uamuzi wake wa kutangaza kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.

Watumishi hao wameungana katika maandamano ya amani yaliyoanzia katika Ofisi za Bunge na kupokelewa na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika Bustani  za Nyerere Square, jijini Dodoma.

Akizungumza na watumishi kutoka sekta mbalimbali, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi katika hatua zote za majadiliano ya suala hilo hadi pale pande zote zitakaporidhika.

Ameongeza kuwa, maombi  yaliyowasilishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA)  yameanza kufanyiwa kazi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi.

Akizungumzia ombi  la mishahara mipya ya wafanyakazi amesema Tume ya Mishahara na Motisha inaendelea kulifanyia kazi suala hilo na pindi litakapokamilika, taarifa itatolewa.

Kuhusu madeni ya watumishi amesema serikali inaendelea kulipa madeni hayo ikiwemo malimbikizo mbalimbali ya watumishi.

Kuhusu kupandishwa madaraja, amesema  tayari Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza kushughulikia suala  hilo ambapo tayari utekelezaji umekwisha anza kwa baadhi ya sekta na kuongeza kwamba serikali itaharakisha suala hilo ili wenye sifa wapate madaraja mapya.

Aidha, amesisitiza kwamba serikali iko pamoja na watumishi wote na haitowaangusha na kuwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa weledi.

Wafanyakazi wa Madini wakishiriki maandamano ya kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania uamuzi wake wa kutangaza kutumika kwa kikokotoo cha zamani cha mafao ya Wastaafu.

” Tuendelee kujituma. Kazi zinazofanyika zinaonekana. Hata utoaji huduma unaendelea vizuri. Uko umoja wa wafanyakazi unaonekana na watumishi wanawahudumia wananchi,” amesema Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine ameendelea kusisitiza suala la kutowahamisha watumishi bila kulipwa fedha za uhamisho.

Awali, akisoma hotuba ya Wafanyakazi,  Katibu Mkuu wa TUCTA  amemweleza Waziri Mkuu kuwa  bado kiwango cha mishahara wanayolipwa watumishi hakitoshi na kuongeza kuwa bado wafanyakazi wanabeba mzigo wa kodi ya mapato hususan wale wenye viwango vya juu vya madaraja.

Aidha, amemweleza Waziri Mkuu  kuwa viongozi waache kunyanyasa wafanyakazi na pindi wanapoondolewa kwenye utumishi waondolewe taratibu za kazi.

Mwisho ameiomba serikali kufanya uchunguzi wa matumizi ya mifuko hiyo.

Read more

Matinga: Utafiti kuongeza tija na uzalishaji wa madini kwa wachimbaji wadogo

Na Priscus Benard, Mpanda Katavi

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amewataka wachimbaji wadogo kuachana na  kutafuta na kuchimba madini kimazoea badala yake  wafuate njia ya kisayansi katika kutafuta, kuchimba na kuchenjua madini katika maeneo yao ili kuongeza tija, pato lao na Taifa kwa ujumla.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokbeth Myumbilwa akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Aliyasema hayo Disemba 4  wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo eneo la D reef na Kapanda Mkaoni Katavi,  na kuongeza kuwa, masuala ya madini ni ya kisayansi na hivyo  kuwataka wachimbaji wadogo kuondoa dhana mbaya iliyojengeka kwa baadhi yao kuwa ukitaka kufanikiwa katika kuchimba madini unatakiwa uende kwa waganga wa jadi.

Mafunzo hayo kwa wachimbaji wadogo, yanafuatia utafiti wa kina wa jiosayansi uliofanywa na wataalam kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)  kwa kushirikiana na wataalam kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Aliongeza kuwa, utafiti huo umefanyika kufuatia nia na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano  inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanaondokana na uchimbaji usio na tija na kwenda kwenye uchimbaji utakaoongeza kiwango cha uzalishaji na hivyo kuongeza kipato kwa wachimbaji na kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.

“Baada ya kutumia taarifa za utafiti huu ni matumaini yangu kuwa kipato chenu na mapato yatokanayo na uchimbaji mdogo wa madini kwa ujumla yataongezeka,” alisema  Matinga.

Pia, Matinga aliwataka wachimbaji wadogo kuwa wazalendo katika kulipa kodi ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli katika kuliletea taifa maendeleo makubwa zaidi.

“Miradi ya maendeleo inahohitaji fedha ni mingi ukianzia elimu bure, mradi wa reli ya kisasa, bwawa la kuzalisha umeme na mengine mengi,” alisisitiza Matinga.

Wachimbaji wadogo wa madini mkoani Katavi wakifuatilia mafunzo,

Awali, akitoa taarifa ya mazfunzo hayo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokbeth Myumbilwa alisema utafiti wa kina ulifanyika kwa lengo la  kubaini uwepo na kiasi cha madini, mwelekeo wa miamba, ubora na tabia za mbale katika maeneo ya D-reef, Kapanda na Ibindi Mkoani Katavi.

Myumbilwa alibainisha kuwa matokeo ya utafiti huo yanaonesha uwepo wa mbale za dhahabu kiasi cha tani 4,394,162 zenye wakia 45,773.40 (kilo 1,423.71) za dhahabu katika eneo la D-reef na tani 452,215 zenye wakia 1,831.92 (kilo 56.98) za dhahabu katika eneo la Kapanda.

“Matokeo haya ni kwa maeneo ya D-reef na Kapanda yenye ukubwa wa jumla ya kilomita za mraba 0.06 yaliyofanyiwa uchorongaji,” alisema Myumbilwa.

Pia, alieleza kuwa, wataalamu wa GST wapo Mpanda kwa ajili ya kutoa mafunzo (mrejesho) juu ya matokeo ya utafiti huo. “Kuna watu walifikiri hatutarudi tena lakini niwahakikishie Serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nanyi ndiyo maana tumerudi hapa kuwapa mafunzo baada ya kukamilika utafiti uliofanyika tokea 2016,” alisema Myumbilwa.

Vilevile, alisema kuwa, kupitia mafunzo hayo yatatoa msukumo katika kuboresha utafutaji, uchenjuaji na uchimbaji salama na hatimaye kuongeza tija na kipato cha wachimbaji wadogo.

“Wachimbaji wadogo wanapoteza fedha zao na muda mwingi kwa sababu nyingi ikiwa ni pamoja na kuchimba kwa kubahatisha na kutokujua njia bora za unjenjuaji madini na hivyo kupelekea madini yao mengi kupotea kupitia mabaki,” alisisitiza.

Mnamo Mwaka 2016 Serikali ilitenga kiasi cha dola za kimarekani 3,703,630 kwa ajili ya utafiti wa kina wa jiosayansi chini ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ili kuboresha maisha ya mchimbaji mdogo na kutatua changamoto zinazomkabili ikiwa ni pamoja na uzalishaji mdogo na uchimbaji usiozingatia usalama na afya kwa mchimbaji.

Read more

Biteko akalipia ajali maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini

Na Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Ametanabaisha kuwa akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu kuliko mgodi wote, ‘kuliko mtanzania mmoja afe ni bora huo mgodi usiwepo’.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) alipofika ofisini kwake kuelezea uwepo wake katika wilaya hiyo.

Aliyasema hayo leo tarehe 04 mwezi Januari alipokuwa akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara inayoendelea kwa siku mbili.

Biteko alibainisha kuwa, Buhemba ni eneo linaloongoza kwa ajali kwenye migodi, huu mgodi ulifungwa na toka umefunguliwa kuna vifo vya wachimbaji kumi na mbili na majeruhi 20, Serikali haiwezi ikakubali hali hiyo iendelee “Mimi nakwambia mwenyekiti sitakubali hali hii iendelee mimi mwenyewe nitakuja kuufunga tena mgodi huu kama hali hiyo itaendelea hatuwezi kupoteza maisha ya watanzania” Biteko alisisitiza.

Biteko aliongeza kwa kusema, Serikali haiko tayari kuona kuwa watu wanaendelea kufa ndio maana imeamua kufika na kuandaa mafunzo  kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili  waweze kufundishwa namna bora za uchimbaji salama na wenye tija.

Biteko alisema mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya, na mazingira ya uchimbaji katika mkoa huu wa Mara.

Akiwapongeza wananchi na wachimbaji wadogo wa madini Buhemba, Biteko alisema kumetokea ugonjwa mmoja kwa watanzania wa kukwamisha mradi wa Serikali,  wananchi wanaanza vurugu na kudai fidia lengo ikiwa ni kukwamisha tu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa watanzania lakini Buhemba mmeonesha ushirikiano mkubwa kutoka mwanzo mpaka mwisho wa utafiti.

Aidha, Biteko alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano anaoufanya katika kusimamia shughuli za uchimbaji wa madini. Amesema mara nyingi wachimbaji wadogo wanakuwa kama watoto yatima lakini si kwa hapa Buhemba. Hawana mlezi, wanajiendesha wenyewe na wakati mwingine mamlaka za serikali zinajitokeza pindi matatizo yanapotokea lakini Mkuu wa wilaya amekuwa bega kwa bega.

Baadhi ya Wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao yenye lengo la kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa Madini yanayoendelea katika wilaya ya Butiama mjini Buhemba mkoani Mara.

Aidha, Biteko aliwasihi wachimbaji wadogo wa Buhemba kuchangia kwa ukamilifu katika pato la taifa. Alisema wakati wote ukikutana na kesi ya utoroshwaji wa madini mhusika mkuu anakuwa ni mchimbaji mdogo. Aliendelea kwa kuwaeleza wachimbaji hao kuwa wamepata Rais ambaye anawapenda, anawajali anawadhamini, Rais anayependa  wachimbaji wadogo wahame kutoka kwenye daraja la chini na kuwa watanzania wanaofurahia maisha kwenye nchi yao  kwa kuthaminiwa na kuheshimiwa, “nilidhani zawadi pekee ambayo mngeipa Serikali na Rais wetu DKt ni nyie kusimamiana mkalipa kodi vizuri, mhame kwenye mfumo wa kukwepa kodi na kutorosha madini”. Biteko alisisitiza

Pamoja na hayo Biteko alibainisha kuwa, katika mkoa wa Mara wilaya inayoongoza kwa kulipa kodi ni wilaya ya Butihama, alisema kiasi cha milioni 57 za kitanzania zimelipwa kwa mwezi jana, hata hivyo aliwahimiza wachimbaji hao  kufanya zaidi ili kuipa serikali wajibu mkubwa wa kuwahudumia.

“Ninapima mapenzi ya Rais Kwenu, halafu ninapima kile mnachochangia ninyi kwenye pato la Taifa haviendani” Mimi nilidhani mtu anayekupenda nawewe unamlipa kwa kumpenda zaidi. Rais wetu anawapenda wachimbaji wadogo hataki mtangetange, mpeni sababu ya kuendelea kuwapenda, mpeni sababu ya kuendelea kuwahudumia, siku mtu akiwagusa Rais awateteee kutokana na kodi zenu”

Naomba sana muwe wazalendo, muwe waaminifu, ili mchango wenu katika sekta hii uweze kuonekana na kutumika katika maeneo mengine nchini. Ili Serikali iweze kuhudumia maeneo mengine kama vile elimu, afya, usafirishaji na mambo mengine ni kutoka katika kodi. Simamianeni ninyi kwa ninyi, onyanenyi ninyi kwa nini bora mtu mbaya bora ake nje ya sekta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Mara (MAREMA) Dave Bita alitoa shukrani zake za dhati kwa serikali kwa kutupa jicho kwa wachimbaji wadogo kwa lengo la  kuwawezesha kuwa na uchimbaji wenye tija. Aliishukuru Serikali kwa kujipanga kuwajengea kituo cha mafunzo kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha masuala ya utafutaji na uchimbaji wa madini.

Ameishkuru Serikali kwa kuwasilisha taarifa ya utafiti ulioanza mwezi Oktoba 2016 kwa wachimbaji wa Butiama matokeo yatakayowapelekea kunufaika na uchimbaji wao.

Aidha, Dave amewataka wachimbaji wadogo kutengeneza mazingira ya kukubali kuwalipa posho viongozi wanaowasimamia katika shughuli zao vinginevyo wataendelea kugombana na viongozi hao siku kwa siku na hata kupelekea migogoro. Amesema wachimbaji wadogo hawako tayari kuwalipa viongozi wanaowasimamia katika maeneo ya uchimbaji.

Aidha, amewasihi wachimbaji wadogo kutumia mafunzo yanayotolewa kwa manufaa ameomba watoe ushirikiano kwa voiongozi watakaowachagua pamoja na kuwasihi kukitumia kwa manufaa kituo cha mafunzo kinachojengwa na serikali kwa ajili yao.

Read more

Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa wazalendo kwa Taifa

Na Nuru Mwasampeta

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuwa wazalendo na waaminifu kwa nchi kwa kulipa kodi stahiki zinazotokana na biashara ya madini wanayoifanya.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Umma. Pamoja na wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo yanayotolewa na wizara ili kuboresha utendaji wao.

Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa mchango wa wachimbaji wadogo katika pato la taifa ni mdogo ilihali asilimia 96 ya shughuli za uchimbaji zinafanywa na wachimbaji wadogo na asilimia nne tu zimeshikwa na wachimbaji wakubwa na ndio wanachangia Zaidi katika ukuaji wa pato la taifa.

Biteko amebainisha kuwa hayo ni matokeo ya ukwepaji wa baadhi ya wachimbaji wadogo katika kulipa kodi stahiki zitokanazo na uchimbaji wa madini.

Ameyasema hayo leo tarehe 2 Januari, 2019 wakati akifungua  rasmi mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Katente mkoani Geita.

Akifungua mafunzo hayo, Biteko amesema, mnamo mwaka 2016 Serikali ilitenga kiasi cha dola za kimarekani 3,703,630 kwa ajili ya utafiti wa kina wa jiosayansi chini ya mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ili kuboresha maisha ya mchimbaji mdogo na kutatua changamoto zinazomkabili ikiwa ni pamoja na uzalishaji mdogo na uchimbaji usiozingatia usalama na afya kwa mchimbaji.

Biteko alibainisha kuwa kazi ya utafiti katika mji wa Katente umekamilika kama inavyoshuhudiwa kupitia mafunzo yanayotolewa kwa wachimbaji wadogo wa eneo hilo yatakayosaidia kupunguza upotevu wa muda, uharibifu wa mazingira, upotevu wa mitaji pamoja na upotevu wa madini ya dhahabu yanayotokana na uelewa wa namna ya kufanya kazi hiyo.

Aidha, Biteko alibainisha kuwa, Baada ya matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa ushirika baina ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na  Shirika la Madini la Taifa (Stamico) na kubaini changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo katika kukua kiuchumi.

Wachimbaji wadogo wa madini katika mji wa Katente wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya uchimbaji wa madini yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Madini

Kutokana na changamoto zilizobainishwa na utafiti huo, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeanza kujenga madarasa na kufunga mitambo kwa ajili ya mafunzo Zaidi na kubainisha kuwa eneo la Katente ni moja kati ya maeneo ambayo mafunzo hayo yatatolewa.

Pamoja na kupewa mafunzo hayo, Biteko amewataka wachimbaji hao kuunda vikundi na kufanya shughuli zao ndani ya vikundi ili kuirahisishia Serikali kuwatambua na kuwapa huduma stahiki zitakazowawezesha kuboresha kazi zao pamoja na afya zao.

Akizungumzia jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo; Biteko alisema ni pamoja na kuendelea kutenga maeneo maalaum kwa ajili ya wachimbaji wadogo, kutoa ruzuku, kurahisisha utoaji wa leseni, pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kuwapa wachimbaji wadogo uelewa katika shughuli ya uchimbaji.

Utafiti huo ulifanyika kufuatia nia na adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Rais Dr. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanaondokana na uchimbaji usio na tija na kwenda kwenye uchimbaji utakaoongeza kiasi cha uzalishaji na baadaye kuongeza kipato kwa wachimbaji wadogo na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Huduma za Jioloji kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Maruvuko Msechu alisema mafunzo yanayofunguliwa ni matokeo ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano yenye lengo la kuhakikisha watanzania wanafaidika na uwepo wa madini nchini ili kujiondoa katika lundo la umaskini kwa kuongeza kipato na kuimarisha sekta mtambuka za uchumi.

Msechu alisema, Utafiti huo ulifanyika katika maeneo ya Ngazo, Kereza, na Katente wilayani Bukombe ukihusisha matumizi ya taaluma ya jiolojia, jiofizikia, na jiokemia ukihusisha uchukuaji wa sampuli mbalimbali za udongo na miamba.

Msechu aliongeza kwa kusema kuwa matokeo ya utafiti huo yalipelekea kufanyika kwa utafiti wa kina katika eneo la Katente, utafiti ulioanza rasmi tarehe 28 mwezi Oktoba, 2016 ambao ulipelekea jumla ya chorongo 19 za DD na 24 za RC kuchorongwa na kukusanya jumla ya sampuli 2821.

Aidha aliushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, Mkuu wa Wilaya pamoja na kamati ya ulinzi ya wilaya ya Bukombe kwa ushirikiano waliouonesha kipindi chote cha kufanya utafiti huo.

Read more

Nishati waunga mkono jitihada za Rais kuwezesha wachimbaji madini wadogo

 • Naibu Waziri Biteko apongeza wachimbaji kuunganishwa na huduma umeme

Na Veronica Simba, Geita

Wizara ya Nishati inatekeleza mkakati wa kuwaunganishia umeme wa uhakika wachimbaji wadogo wa madini kote nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufulu kuiwezesha sekta hiyo izalishe kwa tija kwa manufaa yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (katikati), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (kushoto), walipowasili kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo Chato Geita, Januari 2, 2019.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Msafiri Mtemi.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu, kinachomilikiwa na kampuni ya Padalu, kijijini Lumasa, Chato; Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo, Dkt Medard Kalemani, alisema serikali imefunga transfoma tano zenye uwezo wa KVA 400 hadi 1,000 ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wa Geita kuzalisha kwa tija.

“Umeme huu mkubwa utawawezesha wachimbaji kuchimba ,kuchenjua na kuongeza thamani dhahabu yao ili kuiongezea thamani, iwapatie faida na waweze kulipa kodi na mrabaha serikalini,” alisema.

Akieleza zaidi, Waziri Kalemani alisema yako maeneo mkoani humo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo lakini akabainisha kuwa utaratibu wa kufunga transfoma nyingine tano zenye uwezo uleule, unafanyika ili kuyafikia maeneo ya wachimbaji yaliyosalia ikiwemo Mbogwe na Nyakafuru.

Aidha, alifafanua kuwa, umeme uliounganishwa kwa ajili ya kiwanda hicho cha kuchenjua dhahabu, utawanufaisha pia wananchi wa maeneo jirani ambao wataanza kuunganishiwa huduma hiyo kuanzia wiki ijayo.

Waziri pia alitumia fursa hiyo kufafanua kuhusu gharama za umeme katika maeneo ya vijijini ambapo alibainisha kuwa serikali imedhamiria wananchi wa vijijini watozwe shilingi 27,000 tu kwa ajili ya huduma ya kuunganishiwa umeme.

“Wananchi maeneo yote ya vijijini nchi nzima, gharama za kuunganishiwa umeme ni shilingi 27,000 tu. Msikubali kutozwa zaidi. Iwe ni umeme wa REA au wa TANESCO, gharama ni hiyo na siyo zaidi,” alisisitiza Waziri.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alipongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Wizara ya Nishati katika kuhakikisha wachimbaji madini wadogo nchini wanakuwa na uchimbaji wenye tija kwa kuwapelekea huduma ya umeme.

Awali, uongozi wa kiwanda hicho cha uchenjuaji dhahabu ulieleza kuwa, ujenzi wake ulifanyika kufuatia agizo la Rais Magufuli la kuwataka wachimbaji kuyaongeza thamani madini yao hapa nchini kabla ya kusafirisha nje ya nchi.

Read more

Doto Biteko atoa maagizo mazito kwa wachimbaji kokoto Dodoma

Na Nuru Mwasampeta

Kufuatia ziara ya Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  aliyoifanya hivi karibuni katika eneo la Ihumwa ambako ujenzi wa Mji wa Serikali unaendelea  na kubaini uhaba wa kokoto katika ujenzi huo,  leo Disemba 30, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Anthony Mavunde wamefanya ziara ya kushtukiza kwenye maeneo yanayochimba kokoto hizo na kubaini madudu.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko, akitoa tamko la Serikali kwa wachimbaji wa kokoto alipofanya ziara kujionea kinachoendelea katika machimbo hayo baada ya kubainika uhaba wa kokoto katika eneo la ujenzi wa ofisi za Serikali Ihumwa jijini Dodoma.

Naibu Mawaziri hao wamebaini machimbo ya kokoto yakiwa yamefungwa kwa madai kuwa wafanyakazi wako likizo, zikiwemo mashine za kusagia mawe hayo zikiwa  zimeharibika kwa takribani miezi mitatu na hivyo kupelekea uzalishaji kusimama.

Akizungumza katika eneo hilo la machimbo, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amesema anashangazwa kuona kuwa watumishi katika mgodi wa kokoto wanakwenda likizo wakati mahitaji ya kokoto ni makubwa  na soko la  uhakika.

“Mmechukua  zabuni  kwa ajili ya kusambaza kokoto kutoka kwa   Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),na  kampuni ya MZINGA wenye uhitaji mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea halafu mnadai mko likizo,?” amehoji Biteko.

Akizungumza  kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd , Biteko amemtaka  mkurugenzi huyo aliyefahamika kwa jina la Joel Mchovu kuhakikisha kuwa, ifikapo  Januari 2, 2019 kokoto ziwe zimezalishwa na kusambazwa kwa wahitaji kama walivyokubaliana ili ujenzi uendelee kwa kasi iliyokusudiwa.

Aidha, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa juhudi na weledi mkubwa ili kuzalisha kiasi kinachotosheleza mahitaji vinginevyo oda zitahamishwa na kupewa kampuni za zinazozalisha kokoto zilizopo Chalinze ambazo zinaonesha  uwezo mkubwa katika uzalishaji wa kokoto.

“Mfahamu kwamba endapo tutatoa oda kwa watu wa Chalinze maana halisi ya ujenzi wa mji wa Serikali kwa watu wa Dodoma haitakuwepo kwani hamtanufaika na ujenzi huu,” amesisitiza Biteko.

Biteko amewataka wananchi wa Dodoma kutambua kuwa, ujenzi wa mji wa Dodoma ni fursa kwao ya kuweza kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao binafsi hivyo, wanapaswa kuwajibika ili kupata manufaa hayo. “Fursa kubwa imepatikana na soko la uhakika lipo nitawashangaa kuona kuwa mnapoteza fursa hii,” amesisitiza.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika machimbo ya kokoto ya kampuni ya Laroy Aggregate Co. Ltd, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthon Mavunde na kushoto ni msaidizi wake Kungulu K. Masakala

Naye, Fundi wa Mitambo ya kuchoronga mawe katika mgodi wa WADI, Gao Peng, amesema kuwa, kampuni hiyo iko katika hatua za kutengeneza mashine iliyoharibika ili kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa kokoto hizo na kueleza kwamba mashine hiyo imeharibika kwa takribani kipindi cha  miezi mitatu sasa na hivyo kufanya uzalishaji wa kokoto hizo kusimama.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde, amesema anajisikia vibaya kuona kazi katika maeneo ya machimbo hazifanyiki na kuwataka wananchi wanaofanya shughuli hizo kuongeza nguvu, weledi na ufanisi ili  waweze kunufaika.

“Dodoma tumejaliwa kuwa na mawe mengi ya kuzalisha kokoto na madini mengine ya ujenzi, mahitaji ni makubwa kutokana na kasi ya ujenzi iliyopo lakini bado wana Dodoma mmelala,” amesema Mavunde.

Kwa upande wake, Afisa Madini wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Jonas Mwano amekiri kuwepo kwa leseni hai za uchimbaji wa madini ya kokoto 75 katika mji wa Chigongwe na leseni 66 zimekwisha tolewa kwa waliowasilisha maombi ya leseni hizo na hivyo kuwataka wamiliki wa leseni hizo kuhakikisha wanazifanyia kazi leseni zao vinginevyo zitagawiwa kwa watu wengine.

Aidha, Mwano amekiri kuwa, awali wamiliki wengi wa leseni za madini ya kokoto walikuwa hawazalishi vya kutosha kwa madai kuwa soko lilikuwa adimu lakini sasa soko ni la uhakika na hivyo kuwataka wazalishe kokoto za kutosha ili kutoiangusha Serikali.

Pia, Mhandisi Mwano ameahidi kutembelea maeneo ya uchimbaji wa kokoto kila siku kufuatia maagizo ya Naibu Waziri Doto Biteko ili kuhakikisha kazi ya uzalishaji wa kokoto hizo unaridhisha na kutosheleza mahitaji ya ujenzi katika jiji la Dodoma.

Read more

Miaka mitatu ya Dkt. Magufuli ilivyoboresha sekta ya madini

Na Asteria Muhozya

Ni takriban Miaka Mitatu sasa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aingie madarakani kuliongoza Taifa la Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015, Serikali anayoiongoza imefanya mabadiliko makubwa kwenye Sekta ya Madini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa rasilimali madini zinawanufaisha zaidi Watanzania.

Wanafunzi wa Shule za Sekondari jijini Arusha wakiangalia Madini ya Tanzanite wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito na Usonara ya Arusha (AGF) yaliyofanyika Mwezi Mei,2017.

Katika hatua za awali za kutekeleza mabadiliko hayo, Rais Magufuli Mwaka 2017, alianzisha Wizara mpya ya Madini baada ya kutenganishwa kwa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini kupitia Hati ya Majukumu (Instrument) Na.144 ya tarehe 22 Aprili, 2016 na Marekebisho yake ya tarehe 7 Oktoba, 2017.

Wizara hii ya Madini inaongozwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Naibu Mawaziri wawili, Stanslaus Nyongo na Doto Biteko pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila.

Mbali na uundwaji wa wizara hii mpya, yamefanyika mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, utungwaji wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za nchi wa Mwaka 2017, na Sheria ya Mamlaka ya nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili za nchi wa Mwaka 2017.

Utungwaji wa Sheria hizo mpya na mabadiliko ya Sheria ya Madini na Kanuni zake kumeboresha ulipaji wa mrabaha wa Serikali kutoka asilimia nne (4) na kuwa asilimia sita (6) ya bei ya madini ghafi kwa madini ya metali na vito na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi wa madini ya kiasi cha asilimia moja (1).

Mabadiliko haya pia yanaiwezesha Serikali kuwa na umiliki wa asilimia zisizopungua 16 za hisa huru kwenye Migodi mikubwa na ya kati, kodi ya zuio ya asilimia tano ya thamani ghafi ya madini imeanzishwa kwa wachimbaji wadogo.

Akizungumza katika kipindi Maalum cha TUNATEKELEZA, Waziri wa Madini Angellah Kairuki anasema, Serikali imeweza kufanya majadiliano na wamiliki wa migodi ya ACACIA na TANZANITE ONE ambapo majadiliano hayo yameleta matokeo chanya kwa Acacia kukubali kuilipa Serikali kiasi cha Dola za Marekani Milioni 300.

Katika maelezo yake, Waziri Kairuki anaongeza kuwa, baada ya majadiliano na Kampuni ya Tanzanite One wamekubali kulipa fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali. “Tume maalum iliyoundwa na Rais inaendelea na majadiliano na makampuni yote makubwa yenye Mikataba na Serikali. Serikali ya Awamu ya Tano, imedhamiria kuhakikisha rasilimali za madini zinasimimiwa ipasavyo ili ziweze kuchangia kwa ufanisi katika uchumi wa Taifa na ustawi wa Watanzania,” anasema Waziri Kairuki.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia bidhaa za mapambo zilizotokana na madini yanayopatikana nchini baada ya kuongezwa thamani.

Aidha, Kairuki anaeleza kuwa, Mabadiliko ya Sheria yamewezesha na kuzuia usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi ili madini yaongezewe thamani hapa nchini. Aidha, Waziri Kairuki anasisitiza, mabadiliko hayo yanaifanya migodi ilazimike kutumia bidhaa na huduma za ndani ya nchi na kutoa uwezo wa usimamizi kisheria wa Sekta ya Madini kutakakoleta ufanisi mkubwa.

Akisisitiza suala hili katika moja ya mikutano yake na wadau wa sekta ya madini nchini, Waziri Angellah Kairuki anasema Serikali imeweka ZUIO la kusafirisha madini ghafi nje ya nchi ikiwa na lengo la kuyaongezea thamani kabla ya kuyasafirisha. Katika kulisimamia hilo, anasema, Serikali kupitia Wizara ya Madini inaandaa Muswada wa Sheria ya uongezaji Thamani Madini, ili kuwezesha shughuli za Uongezaji Thamani madini kufanyika kwa kuzingatia Sheria na kusimamia vyema shughuli za uongezaji thamani madini nchini.

“Dhamira ya Serikali ni kujenga na kuendeleza Viwanda vya ndani, kuongeza Mapato ya Serikali kutoka Sekta ya Madini, na kurekebisha mapungufu yaliojitokeza katika utekelezaji wa Sheria zilizopo katika shughuli za uongezaji thamani madini hususani kwenye eneo la masonara,” anasisitiza Waziri Kairuki.

Waziri Kairuki anaongeza kwamba, Wizara inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani madini na kuendelea kutoa leseni za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini ya metali. Pia, anafafanua kuwa, jumla ya maombi 27 ya uwekezaji kwenye smelters na refineries (ujenzi wa vinu (viwanda) vya uchenjuaji kwa ajili ya kusafisha na kuongeza thamani madini ya metali) yaliwasilishwa na uchambuzi unaendelea kufanyika ili kupata mwekezaji atakayekidhi vigezo.

Akizungumzia ukuaji wa Sekta ya madini katika Awamu hii anasema, Sekta ya Madini ilikua kwa asilimia 17.5 Mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 9.1 Mwaka 2015. Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa uliongezeka na kufikia asilimia 4.8 Mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 4.0 Mwaka 2015.

Waziri Kairuki anasisitiza kuwa, Wizara imevuka malengo ya makusanyo ya maduhuli iliyopewa  mwaka 2017/18 ya Shilingi bilioni 194.66 na kuweza kukusanya Shilingi bilioni 298 sawa na asilimia 153.09.

Pia anaongeza, kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji wa Sekta ya Madini kumetokana na kuimarishwa kwa udhibiti wa biashara haramu na utoroshwaji wa madini; kuimarishwa kwa ukaguzi na usimamizi katika sehemu za uzalishaji, biashara ya madini; na usafirishaji wa madini nje ya nchi; kuongezeka kwa viwango vya mrabaha na kuanzishwa kwa ada ya ukaguzi wa madini kufuatia marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yaliyofanyika Mwaka 2017 na Kanuni zake.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza mmoja wa Wachimbaji wa Madini ya Bati katika moja ya ziara zake za kukagua shughuli za uchimbaji madini, Kyerwa mkoani Kagera.

Akizungumzia uundwaji wa Tume ya Madini, ambayo ni zao la Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka, 2010, baada ya kufutwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (Tanzania Mineral Audit Agency –TMAA), Waziri Kairuki anasema kuundwa kwa Tume ya Madini, kumepelekea  usimamizi  wa karibu zaidi wa maeneo yenye uchimbaji wa madini. Aidha, uwepo wa ofisi za madini katika mikoa mbalimbali nchini unarahisisha ushughulikiaji wa maombi ya leseni, kupunguza migogoro na kuongeza makusanyo ya mrabaha.

“Pia, Tume imesimamia shughuli za uchimbaji ndani ya ukuta wa Mererani ili kudhibiti utoroshwaji wa Madini ya Tanzanites na madini mengine ili kuimarisha ukusanywaji wa kodi za Serikali,” anasema Waziri Kairuki.

Akizungumza katika Mkutano baina ya Waziri Kairuki na Wafanyabiashara wa Madini ya Tanzanite jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA) Sam Mollel anasema ukuta uliojengwa kuzunguka migodi ya Tanzanite Mirerani umeongeza Imani kubwa kwa walaji wa madini hayo zikiwemo nchi za Marekani na Ulaya huku akisisitiza kuwa, ukuta wa Mirerani umedhibiti ajira za watoto migodini na kuondoa wizi wa vifaa migodini.

Haya ni baadhi tu ya mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Sekta ya Madini. Kwa hakika watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na Serikali ambazo zinalenga kuhakikisha kwamba rasilimali madini zinalinufaisha taifa na watanzania wote.

Aidha, katika kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia zaidi katika pato la Taifa na ukuaji wa uchumi, Waziri Kairuki anasema katika kipindi cha miaka mitano ijayo, lengo la wizara ni kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia zaidi katika pato la Taifa ili hadi ifikapo mwaka 2025 sekta husika iweze kuchangia hadi kufikia asilimia kumi (10%).

Read more

Prof. Msanjila awataka STAMICO kuutangaza mtambo wa kuchoronga miamba

Na Nuru Mwasampeta

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutumia mtambo wa kuchoronga miamba kwa ufanisi ili kuliletea tija Taifa pamoja na  shirika hilo kutokana na  kipato kitakachotokana na uwepo wa mtambo huo.

Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Nsajigwa Kabigi, akieleza jambo kuhusu mtambo huo mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (mwenye tai) na wajumbe walioshiriki katika tukio hilo.

Ameyasema hayo leo Desemba 24, 2018 wakati wa hafla fupi ya kuukabidhi rasmi mtambo huo kwa STAMICO kwa ajili ya kuanza kuutumia.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Prof. Msanjila amesema, ununuzi wa mtambo huo ni uwekezaji mkubwa ambao Serikali imeufanya kwa shirika la Stamico hivyo, halina kuutumia vyema ili uweze kuleta tija.

Akizungumzia gharama za mtambo huo, Prof. Msanjila amesema umegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja na laki tatu(USD 1.3) ambazo yeye kama Mtendaji Mkuu wa wizara anaona kuwa na deni kubwa kwake, na hivyo kuahidi kuusimamia ipasavyo ili kuhakikisha mtambo huo unazalisha faida na kuwa chachu ya kuweza kununua mitambo mingine  kama hiyo ili kukuza sekta ya madini nchini.

Aidha, amelitaka Shirika hilo kujitangaza vema ili wananchi na hususn wadau wa madini wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini kufahamu uwepo wa mtambo huo ili uweze kutumika hata kwa kampuni binafsi ili kujiongezea kipato lakini pia kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. “Kwa zabuni nilizozisikia mpaka sasa mtambo huu utazalisha pesa za kutosha” amesema Msanjila.

Mbali na kukabidhi mtambo huo, Prof. Msanjila ameitaka Stamico kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya mtambo huo kila robo ya mwaka ili kuweza kufanya tathmini endapo mtambo unatumika kwa faida.

Pia, ameliagiza shirika hilo kuhakikisha kuwa, mtambo huo unawezesha manunuzi ya mtambo mwingine mpya kila mwaka ili ndani ya miaka mitano shirika liweze kumiliki mitambo mitano na kurahisisha utekelezaji wa shughuli za uchimbaji na utafutaji wa madini.

Akizungumzia ubora wa mtambo huo, Mkurugenzi wa Kampuni  ya Geo field Tanzania Ltd Denis Dillip ambaye ndiye mnunuzi wa mtambo huo amesema, mtambo huo ni wa kisasa na unatumika katika kuchimba aina tatu za miamba lakini pia unaweza kutumika katika kuchimba visima vya maji.

Aidha, Denis ameishukuru Serikali kwa wazo la kununua mtambo huo na kukiri kuwa, utawasaidia wchimbaji wadogo katika kuendeleza kazi zao za uchimbaji na utafutaji wa madini.

Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali na Utawala, Nsajigwa Kabigi mara baada ya kuwasili katika ofisi za STAMICO kwa ajili ya makabidhiano ya mtambo wa kuchoronga miamba. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Sylvester Ghuliku.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kanali Sylvester Ghuliku amekiri kuwa mtambo huo ni talanta waliyopewa na serikali na kuahidi kutoifukia na badala yake watahakikisha unatumika kwa faida na kuhakikisha unazalisha faida kwa serikali.

“Dola za kimarekani milioni 1.3 mlizotuamini na kutukabidhi ni pesa nyingi sana, na hamjatukabidhi ili zikae kwenye makabati, tutahakikisha tunautumia mtambo huu kwa weledi mkubwa ili uweze kuleta tija, ni imani yangu kuwa mtambo huu utanufaisha si Stamico pekee bali pia wachimbaji wadogo, wa kati, wakubwa na sekta nzima ya madini nchini,” amesema Ghuliku.

Ameongeza kuwa, mtambo huo unahitajika sana katika kufanikisha shughuli za utafutaji wa madini, hivyo atahakikisha katika kipindi cha mwaka mmoja stamico inazalisha ipasavyo kupitia mtambo huo na hivyo kuwezesha manunuzi ya mtambo mwingine wa aina hiyo.

Read more

Profesa Kikula aongoza kikao cha kazi Tume ya Madini

Na Greyson Mwase, Dodoma

Leo tarehe 21 Desemba, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameongoza kikao cha kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilishirikisha makamishna wa Tume ambao ni Mtendaji  Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Nchini (FEMATA), Haroun Kinega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dorothy Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka na  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.

Wengine ni Dkt. Athanas Macheyeki, Profesa Abdulkarim Mruma Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji wa Tume ya Madini.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Tume na Mpango Mkakati wa Tume wa miaka mitano (2019/20 -2023/2024). Katika kikao hicho kati ya masuala yaliyokubaliwa ni pamoja na leseni ambazo hazifanyiwi kazi kufutwa na tathmini ya kina kufanyika kwa waombaji wa leseni ili kubaini kama wanakidhi vigezo kama vile uwezo wa kifedha na utaalam.

Read more

Prof. Msanjila akutana na ujumbe wa Serikali ya India

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amekutana na Ujumbe wa Serikali kutoka nchini India pamoja na Kampuni ya National Mineral Development Corporation (NMDC) jijini Dodoma, katika kikao ambacho pia kimeshirikisha watendaji kutoka Wizarani, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini.

Sehemu ya ujumbe kutoka Serikali ya India na Kampuni ya NMDC pamoja na watendaji wa wizara wakifuatilia kikao hicho.

Ujumbe huo umefika wizarani kwa lengo la kuonana na uongozi wa Wizara kwa ajili ya kufanya majadiliano juu ya nia yao ya kufanya uwekezaji kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na kupata maeneo mapya ya uchimbaji. Awali kampuni hiyo ilikutana na Shirika la STAMICO na kufanya majadiliano kuona ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana katika utekelezaji wa malengo yao kupitia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini nchini.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 18, Katibu Mkuu Prof. Msanjila amewakaribisha na kuwapongeza kwa nia yao ya kufanya uwekezaji nchini na kuueleza ujumbe huo kuwa, kampuni ya NMDC inayo fursa ya kuchagua kuwekeza ikiwa kama kampuni inayojitegemea ama kwa kuingia ubia na Shirika la Madini la Taifa la (STAMICO).

Aidha, ameuleza ujumbe huo kuwa, wizara inazo taasisi ambazo zinasimamia masuala yanayohusu leseni na shughuli za utafiti na kuusisitiza kujadiliana na Kamishna wa Madini, Mkurugenzi wa Sheria na Tume ya Madini kwa ajili ya kupata taratibu zinazotakiwa kisheria kuhusu masuala ya leseni na mahitaji mengine wanayotakiwa kutekeleza kabla ya kuwasilisha mpango huo kwenye ofisi yake. Aidha, aliutaka ujumbe huo kujadiliana na GST kwa masuala yanayohusu shughuli za utafiti wa madini.

Pia, Prof. Msanjila ameishauri kampuni husika kukata leseni ya utafiti kwanza ili kufanya utafiti katika maeneo waliyoyakatia leseni na kuwasilisha taarifa hizo katika ofisi ya GST ndipo waendelee na utaratibu wa kupata leseni ya uchimbaji. Vilevile, ameutaka ujumbe huo kuwa tayari kuwasiliana na wizara pindi unapohitaji kupata ufafanuzi wa masuala yote ya yanayohusu uwekezaji katika sekta husika.

Kampuni ya NMDC inajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma na iko chini ya Wizara inayoshughulikia madini ya chuma ya India.  Pia kampuni hiyo pia inajishughulisha na utafiti wa madini mbalimbali kama vile madini ya chuma, shaba, phosphate, nk. katika nchi mbalimbali na barani Afrika.

Read more

Mgodi wa Wachimbaji Wadogo Mahenge Wafunguliwa

 • Ni baada ya kufungwa kwa miezi Mitano
 • Biteko azidua Ofisi ya Madini Ulanga

Na Rhoda James, Mahenge

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameufungua mgodi wa Wachimbaji Wadogo wa Mahenge baada ya kufungwa kwa takribani miezi Mitano tangu   Julai 10, 2018.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akikata utepe kuashiria uziduzi wa Ofisi ya Madini Wilayani Ulanga katika Mji wa Mahenge uliofanyika tarehe 14 Desemba, 2018.

Mgodi huo wa madini ya Vito aina ya Spino uliopo Wilayani Ulanga ulisimamishwa kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchimbaji wa madini ikiwemo  kutolipa kodi za Serikali.

Akizungumza katika mkutano kati yake na wachimbaji Biteko alisema kuwa, Sekta ya Madini haipo kwa ajili ya kufunga migodi, na kuongeza kuwa, hakuna mchimbaji yeyote atakayeruhusiwa kuchimba katika eneo hilo hadi pale atakapokuwa amelipa madeni yake angalau ya awamu ya kwanza.

Pia, alisema kuwa, ikiwa kuna mchimbaji ambaye atakiuka taratibu za uchimbaji, atachukuliwa hatua za kisheria  na si kwa kufungiwa mgodi tu bali atapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

“Nyie ni wadau muhimu katika sekta ya maendeleo, na mkilipa kodi, ikaonekana imefanya nini, hata wawekezaji hawatakwepa kulipa kodi,” alisema Biteko.

Aliwataka Wachimbaji Wadogo wa Mahenge kubadilika na kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kusema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano haitaki rushwa hususan kwenye Sekta ya Madini.

Aidha, pamoja na kufuungua mgodi huo, Biteko pia alizidua Ofisi ya Afisa  Madini Mkazi wa Mahenge, ikiwa ni mojawapo ya mahitaji ya awali ili shughuli za uchimbaji madini katika Mji wa Mahenge ziende  kama inavyotakiwa.

Pia, Biteko alimtaka Afisa Mkazi wa Mahenge, Tandu Jirabi kuhakikisha leseni za dealers zinasainiwa ili  pamoja na kutoa utaratibu kwa wadau hao kuhusu namna ambavyo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kabla ya  kupatiwa leseni.

Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga akiwahutubia wananchi pamoja na wachimbaji wadogo wa madini (hawapo pichani) wilayani Ulanga katika mji wa Mahenge, wakati wa ziara ya Naibu Waziri Biteko.

“Mzawa lazima awe na mashinetano na mwekezaji kuwa na mashine 30,” alisema Biteko.

Aidha, Biteko alitoa wito kwa viongozi wa Halmashauri ya Mahenge kuhakikisha kuwa fedha zinazolipwa kama kodi zinatumika ipasavyo katika kuwezesha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo kujenga Zahanati, Shule, Barabara na kadhalika.

Kwa Upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mahenge Goodluck Mlinga alimshukuru Naibu Waziri Biteko kwa kufugua mgodi huo wa wachimbaji wadogo na kuwataka wananchi wa Mahenge kufuata taratibu zinazotakiwa ili kuepusha usubufu kama huo uliojitokeza hapo awali.

Mlinga alisisitiza kuwa, kodi inayolipwa na Wachimbaji Wadogo lazima itekeleze majukumu yaliyopangwa na kumwakikishia Naibu Waziri kuwa wachimbaji watalipa kodi kwa kishindo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema kuwa Rais Magufuli anataka kila mwananchi afaidike na rasilimali za madini, hivyo, kuwataka wananchi na Wachimbaji wote wa Mahenge  kufuata taratibu zilizopo ili kila mmoja wao afaidike na rasilimali hiyo.

Read more

Nyongo aitaka Tume ya Madini kuchunguza chanzo cha mgogoro wa wachimbaji madini, Kilwa

Na Greyson Mwase, Kilwa

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameitaka Tume ya Madini kufanya uchunguzi kuhusu mgogoro kati ya kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya Kizimbani inayomilikiwa na Seleman Mohamed na wananchi wa kijiji cha Hotel Tatu kilichopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wazalishaji wa madini ya chumvi mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Desemba, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho wakati wa utatuzi wa mgogoro huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua shughuli za madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Alisema kuwa, baada ya kusikiliza pande zote mbili imeonekana kuna haja ya  Tume ya Madini kufanya uchunguzi ili kubaini namna utoaji wa leseni ya uchimbaji wa madini ya jasi kwa kampuni ya Kizimbani ulivyofanyika kabla ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni za madini.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini haitasita kuwaondoa maafisa madini wakazi wa mikoa watakaobainika kuwa ndio chanzo cha migogoro kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini.

“Kama Serikali tunataka kuhakikisha leseni za utafiti na uchimbaji wa madini zinatolewa kwa kufuata sheria na kanuni za madini bila kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote, aidha hatutasita kumwondoa afisa madini mkazi yeyote atakayebainika kuwa chanzo cha migogoro kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini,” alisema Naibu Waziri Nyongo huku akishangiliwa na wananchi.

Awali wakielezea mgogoro huo kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema kuwa walikuwa na mgogoro wa muda mrefu kati yao na Seleman Mohamed aliyedai kuwa mmiliki halali wa eneo husika hali iliyopelekea mgogoro kuwasilishwa kwenye Ofisi ya Madini Mtwara, ambapo  mtaalam kutoka ofisi hiyo alifika kwa ajili ya kuchukua alama za eneo husika kwa ajili ya kwenda kuhakiki umiliki wa eneo husika.

Waliendelea kusema kuwa, walifika katika Ofisi hiyo baada ya siku mbili na kuelezwa kuwa eneo hilo lilishaombewa leseni na kutolewa kwa mmiliki wa kampuni ya Kizimbani, Seleman Mohamed.

Walisema kuwa tangu kuzuka kwa mgogoro huo mwaka 2013, wamekwenda katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Mkoa pasipo mafanikio yoyote na kusisitiza kuwa wanahitaji eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji kwenye shughuli za uchimbaji wa madini ya jasi kwa kutumia mwekezaji na  kujipatia kipato pamoja na kulipa kodi Serikalini.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Hoteli Tatu kilichopo Wilayani Kilwa Mkoani Lindi wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya kijiji hicho na mmiliki wa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya Kizimbani, Seleman Mohamed.

Kwa upande wake mmiliki wa leseni hiyo, Seleman Mohamed alidai kuwa aliomba leseni kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kupatiwa leseni yake.

Wakati huo huo akizungumza katika nyakati tofauti kupitia mikutano na wazalishaji wa chumvi iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na katika eneo la Kilwa Masoko Wilayani Kilwa mkoani Lindi, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini inatambua mchango wa wazalishaji wa chumvi hususan katika mkoa wa Lindi kwenye Sekta ya Madini hivyo imeweka mikakati mbalimbali ya kuwasaidia.

Alieleza mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuondoa tozo mbalimbali tisa kisheria zilizokuwa zinatozwa na halmashauri ili uzalishaji wao uwe na tija na kuinua uchumi wa mkoa wa Lindi.

Alieleza kuwa mikakati mingine kuwa, ni pamoja na kuendelea kushughulikia changamoto zilizopo kwenye uzalishaji chumvi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi mara baada ya kupata eneo na fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini. (SMMRP) uliopo chini ya Wizara ya Madini.

Aliendelea kusema kuwa mahitaji ya chumvi nchini ni takribani tani laki tatu na nusu kwa mwaka ambapo asilimia 70 ya chumvi inaagizwa kutoka nje ya nchi  na kusisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga katika uboreshaji wa uzalishaji wa chumvi nchini.

“Kama Wizara ya Madini tunataka ifike mahali tuzalishe chumvi bora ya kutosha na kuuza ya ziada nje ya nchi na kujiingizia fedha za kigeni,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliwataka wazalishaji wa chumvi hao kufuata sheria na kanuni za madini.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wazalishaji wa chumvi mkoani Lindi waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na tozo zilizoondolewa kisheria kwenye madini ya chumvi kuendelea kutozwa na halmashauri, ukosefu wa mitaji pamoja na masoko.

Changamoto nyingine ni pamoja na miundombinu duni kwenye maeneo yenye uzalishaji wa chumvi, madini joto yanayotumika kwenye uzalishaji wa chumvi kuuzwa kwa gharama kubwa na kutotambuliwa katika halmashauri na taasisi  nyingine za kifedha.

Read more

Wachimbaji madini Namungo waomba vifaa

Na Greyson Mwase, Ruangwa

Wananchi katika kijiji cha Namungo kilichopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuwapatia vifaa bora ili kuboresha  uchimbaji wa madini na kuchangia kwenye pato la taifa kupitia Sekta ya Madini.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akifafanua jambo alipofanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Namungo uliopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali. Katikati ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari.

Wameyasema hayo leo  tarehe 14 Desemba, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanywa katika kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya  ziara ya siku mbili ya  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo mkoani Lindi yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake, Dickson Baltazary ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu alisema kuwa, wamekuwa wakichimba madini kwa kutumia zana duni hali inayowasababishia kushindwa kufikia malengo yao kwenye uzalishaji.

Baltazary aliongeza kuwa, iwapo watapata fedha kupitia mikopo na ruzuku Serikalini kupitia Wizara ya Madini wataweza kufanya shughuli zao za uchimbaji wa madini kwa ufanisi na kuchangia zaidi kwenye mapato ya Serikali.

Akizungumza na wachimbaji hao mara baada ya kupokea kero mbalimbali, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia wachimbaji wadogo ambapo mpaka sasa maeneo yameanza kutengwa kwa ajili ya uchimbaji madini.

Aliendelea kusema kuwa Serikali inaangalia utaratibu mzuri utakaowawezesha kupata ruzuku.

Wakati huohuo, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangurugai Wilayani Ruangwa mkoani Lindi Naibu Waziri Nyongo aliwataka wananchi kuunga mkono uwekezaji wa uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) unaotarajiwa kufanya na kampuni ya utafiti wa madini hayo ya Chilalo Graphite Mine.

Aidha, aliwapongeza wananchi hao kwa kuunga mkono uwekezaji huo kwa kuwa na subira wakati wa tathmini iliyofanywa miaka miwili iliyopita na kuitaka kampuni ya Chilolo kurudia tathmini kwani thamani ya mali imebadilika.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nangurugai kilichopo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Akielezea manufaa ya mradi huo, Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na ajira 480 kutolewa wakati wa ujenzi wa mgodi na ajira 250 kutolewa mara baada ya uendeshaji wa mgodi kuanza.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kukua kwa uchumi wa Wilaya ya Ruangwa kutokana na ongezeko la mapato yatokanayo na uzalishaji wa madini hayo.

“Madini ya kinywe yana soko kubwa duniani  kutokana na kampuni nyingi kutumia madini hayo katika utengenezaji wa betri za magari, ni vyema mkachangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi,” alifafanua Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliutaka mgodi huo kuhakikisha unatoa ajira kwa wananchi wenye sifa wanaozunguka karibu na mgodi kabla ya kufikiria kuajiri wageni kutoka katika mikoa mingine.

Read more

Waziri Kairuki, Waziri wa Maliasili China wafanya mazungumzo

Beijing, China

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Waziri wa Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China LU Hao Desemba 11 walifanya mazungumzo Beijing, nchini China wakati Tanzania ikishiriki katika Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini humo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimkabidhi Waziri wa Maliasili wa Jamhuri ya Watu wa China LU Hao, zawadi ya picha inayoonesha wanyama mbalimbali wanaopatikana nchini

Waziri wa Maliasili ndiye anayesimamia masuala ya Madini nchini China.

Kufuatia mazungumzo hayo, Waziri wa Maliasili wa China aliona kuwa maombi  yaliyowasilishwa na Waziri Kairuki ni ya msingi hivyo, nchi hizo zimekubaliana kuwa na  Kundi la Pamoja  la  Kazi  kati  ya wizara hizo  mbili ambalo  litapitia na kuchambua maeneo ya ushirikiano na baadaye  nchi husika zitasainiana Mkataba wa Makubaliano.

Aidha, nchi hizo zimekubaliana kukuza ushirikiano katika maeneo ya utafiti, mafunzo na uwekezaji katika sekta ya madini.

Wizara ya Madini ilishiriki Jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini tarehe 10 Desemba, mwaka huu Beijing nchini China. Jukwaa hilo liliandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya madini nchini.

Read more

Maafisa madini watakiwa kuwa wabunifu, ukusanyaji maduhuli

Na Greyson Mwase, Lindi

Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini wametakiwa kuongeza ubunifu kwenye  ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo lililowekwa na Serikali hivyo Sekta ya Madini kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa kokoto ya Drumax Construction kwa kushirikiana na kampuni inayomilikiwa na Said Seif iliyopo katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, George Tayyar (kulia) akielezea changamoto za kampuni yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) mara alipofanya ziara kwenye machimbo hayo.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 13 Desemba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kwenye kikao chake na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi iliyopo Wilayani Nachingwea mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kwenye mkoa huo, yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali.

Naibu Waziri Nyongo aliyekuwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Mhango alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa sekta nyingine kutokana na makusanyo ya kodi mbalimbali za madini.

“Ninawaagiza maafisa madini wakazi kuhakikisha wanafikia lengo lililowekwa na Serikali kwenye ukusanyaji wa kodi mbalimbali zitokanazo na Sekta ya Madini kwa kuwa wabunifu, na tupo tayari kusaidia pale itakapowezekana,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliwataka maafisa madini kujiridhisha na maeneo yanayoombewa leseni kabla ya kutoa leseni  ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wamiliki wa leseni na wananchi wanaozunguka maeneo ya uchimbaji.

Wakati huohuo akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini  imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya madini na kusisitiza kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili waweze kuzalisha zaidi na Serikali kupata mapato yake stahiki.

Aidha, Naibu Waziri alifanya ziara katika machimbo ya kokoto yanayomilikiwa na kampuni za Drumax Construction na Said Seff na  kiwanda cha kutengeneza vyombo vya ibada kwa kutumia madini ya mawe kinachomilikiwa na Shirika la Benedictine Abbey katika Wilaya ya Masasi na kuwahakikishia watendaji wake kuwa Serikali imejipanga katika kutatua changamoto zinazowakabili ili uwekezaji wao uwe na manufaa, hivyo kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Read more

Halmashauri msitoze kodi zilizofutwa kwenye madini ya chumvi-Nyongo

Na Greyson Mwase, Mtwara

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amezitaka halmashauri zote nchini kutokutoza kodi zilizofutwa kwenye madini ya chumvi ili wazalishaji wa madini hayo waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri na kulipa kodi stahiki serikalini.

Mkuu wa Gereza la Kiwanda Chumvi lililopo katika Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, SP Mohamed Mkangumbe (katikati) akionesha moja ya mashamba ya chumvi kwenye ziara hiyo.

Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo leo Desemba 12, 2018 kwenye mkutano wake na wazalishaji wa madini ya chumvi kutoka katika Chama cha Wazalishaji wa Madini katika Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA) kilichofanyika kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara mjini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Madini iliamua kufuta baadhi ya kodi walizokuwa wanatozwa wazalishaji  wa madini ya chumvi ambazo zilikuwa ni mzigo kwao na kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea.

“Ninaziagiza halmashauri zote nchini kutoza kodi kwa kuzingatia sheria zilizopo huku zikihakikisha kodi zilizofutwa kisheria hazitozwi tena.” Alisema Naibu Waziri Nyongo.

Akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kuwasaidia wazalishaji wa madini ya chumvi katika mkoa wa Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na  kuangalia namna ya uanzishwaji wa kiwanda cha chumvi katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuongeza ubora na thamani ya madini ya chumvi.

Katika hatua nyingine akizungumza na kikundi cha Umoja wa Vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya mchanga katika eneo la Ziwani lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara, mbali na kupongeza kikundi hicho kwa kazi nzuri Naibu Waziri Nyongo aliomba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kuendelea kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapa mikopo ya fedha ili waweze kuzalisha zaidi.

Aidha, aliwataka wakandarasi wanaopewa zabuni za ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja na majengo kununua mchanga na tofali kutoka katika vikundi vya wachimbaji wa mchanga katika mkoa wa Mtwara ambao wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria  kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akikagua madini ya chumvi katika ghala la kuhifadhi madini hayo kwenye shamba la chumvi linalomilikiwa na Jeshi la Magereza la Kiwanda Chumvi lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara.

Pia aliagiza Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuwapa ushauri wa kitaalam wachimbaji wa madini ya mchanga ili kufanya uchimbaji uwe wenye tija na kuzingatia sheria na kanuni za madini zilizopo.

Wakati huohuo Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara katika shamba la chumvi linalomilikiwa na jeshi la magereza la Kiwanda Chumvi lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara na kupongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri.

Read more

Naibu Waziri Biteko autaka Mgodi wa MMC kuwalipa fidia wananchi

 • Awataka Wachimbaji kuifahamisha Serikali Mikataba wanayoingia

Na Rhoda James, Morogoro

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ameutaka Mgodi wa MMC kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vya Mtukule na Mangae Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro waliopisha mgodi huo kufanya shughuli za uchimbaji lakini hawakuwahi kulipwa fidia zao.

Wafanyakazi wa Mgodi wa MMC wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao kati yao ili kujua utendaji kazi wao katika mgodi wa MMC uliopo mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Doto Biteko alitoa agizo hilo Desemba 10, 2018 alipotembelea Mgodi wa MMC kwa lengo la kukagua shughuli zinazoendelea mgodini hapo pamoja na kwamba mgodi husika uliagizwa kusimamisha shughuli hizo hadi hapo utakapowalipa fidia wananchi wanaodai haki zao.

Biteko alieleza kuwa, tangu Mgodi huu uanze kazi umekuwa ukiendelea na shughuli za uchimbaji pasipo kuwalipa fidia wananchi wanaouzunguka na hivyo, kuuagiza kuwalipa kwanza wananchi ndipo uendelee na shughuli zake.

“Lipeni kwanza fidia na kama uwekezaji wenu ni halali mtaendelea. MMC hakikisheni wananchi wote wanalipwa haki zao na siyo  shilingi Laki Tano niliyoambiwa kwamba wamelipwa,” alisisitiza Biteko.

Vilevile, Naibu Waziri Biteko alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally kufanya uchambuzi ili kujua wananchi wenye haki ya kulipwa ikiwemo kujua ikiwa ardhi hiyo inamilikiwa na wananchi hao ama mgodi, kujua kiasi cha fidia ambacho kila mmoja anatakiwa kulipwa. “Kama uwekezaji ni wa haki, wananchi wapishe uwekezaji huo,” aliongeza Biteko.

Aliongeza kuwa, maendeleo hayawezi kupatikana ikiwa mgodi na wananchi hawaelewani na hivyo kutoa wito kwa wawekezaji kupitia hatua mbalimbali kabla ya kuwekeza ikiwemo kujitambulisha katika ngazi za Serikali ya Kijiji hadi ya Wilaya.

“Na ili Mgodi upate adhabu ni  lazima shughuli zake za uchimbaji zisimame hadi hapo watakapokuwa wamewalipa wananchi fidia yao, alisema Naibu Madini Biteko.

Pia, alimtaka Mkuu huyo wa Wilaya kushirikiana na  Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Tanzania (TARURA) kulifanyia kazi tatizo la barabara linalowakabili wananchi hao kufuatia hatua ya mgodi huo kubadili matumizi ya barabara iliyokuwa ikitumiwa awali na wananchi hao. Tunataka tuondoe ubabaishaji na uongouongo kwenye Sekta ya Madini,” aliongeza

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally (kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko wakikagua uwekezaji uliofanywa na Mgodi wa MMC mkoani Morogoro.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Madini Biteko ametoa wito kwa Watanzania wote hususan wachimbaji wadogo kuhakikisha kuwa Serikali inatambua mikataba yao wanayoingia na wawekezaji

Biteko alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa watanzania hawanyonywi na vile vile wawekezaji hawaingii mikataba ambayo sio sahihi jambo litasaidia serikali kutolaumiwa.

“Sisi watanzania tusiwaingize wawekezaji kwenye migogoro. Madhara  yanasababisha  nchi ya Tanzania kuonekana kwamba inawanyanyasa wawekezaji.Fuateni sheria zilizopo,” alisema Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally alihaidi kuwa atayafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa atayasimamia kuhakikisha kuwa kila mwananchi analipwa haki yake.

Read more

Mwenyekiti Tume ya Madini, atatua mgogoro sugu wa madini, Nzega

Na Greyson Mwase, Nzega

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 06 Desemba 2018 ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya vikundi viwili vilivyokuwa vinajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Mwamikola lililopo Wilayani Nzega mkoani Tabora.

Mmiliki wa eneo lililopo katika kijiji cha Mwamikola kilichopo katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Rashid Kavula ( kushoto) pamoja na Katibu wa Kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu kilichokuwa kinaendesha shughuli zake za madini katika eneo hilo cha Mwaguguli Mining Society, Nyansaho Sumar (kulia) wakishikana mikono kama ishara ya kumaliza mgogoro baina yao kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika kijiji hicho.

Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha Mwaguguli Mining Society na kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society ambapo mgogoro wao ulitokana na mwingiliano wa maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini.

Profesa Kikula aliyekuwa Wilayani Nzega kwa ajili ya kutatua mgogoro huo aliambatana na watendaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki, Meneja wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Zephania Maduhu na Mwanasheria kutoka Tume ya Madini, Hadija Ramadhani.

Wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni pamoja na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Mayigi Makolobela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Onesmo Kisoka, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.

Mara baada ya kufanya mazungumzo na pande zote mbili kwa pamoja, Profesa Kikula alitoa maelekezo kulingana na sheria ya madini  kwa kusema kuwa maombi ya kikundi cha Mwaguguli Mining Society hayakustahili kupewa leseni  kwa kuwa yameombwa  kabla ya leseni iliyokuwepo kumaliza muda wake kinyume na Kifungu cha 15(2) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017.

Profesa Kikula aliongeza kuwa ombi la kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society linastahili kupewa leseni kwa vile liliombwa baada ya leseni ya awali  kumaliza muda wake na kuongeza kuwa, baada ya maombi ya kikundi cha Mwaguguli Mining Society kukataliwa kupewa leseni, kulingana na Sheria ya Madini kikundi husika kinaweza kuomba tena eneo  ambalo haliingiliani na eneo la ombi la Mwamikola Gold Mining Society.

Awali akielezea historia ya mgogoro huo, Profesa Kikula alisema kuwa mgogoro huo uliopo katika kijiji cha Mwamikola, Kata ya Mwangoye Wilayani Nzega mkoani Tabora ulitokana na mwingiliano wa maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini.

Alisema maombi ya vikundi hivyo kwa ajili ya uchimbaji wa madini yaliombwa katika eneo la leseni  ya utafutaji wa madini ya kampuni ya Resolute Tanzania Limited iliyotolewa Machi 14, 2014 na kumaliza muda wake Julai 13, 2018.

Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki (kulia) akifafanua jambo kwa wachimbaji wa madini katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Mwamikola kilichopo Wilayani Nzega mkoani Tabora. Katikati ni Meneja wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Zephania Maduhu

Aliendelea kusema kuwa eneo linaloombewa leseni lilivamiwa na wachimbaji wadogo  mwezi Januari, 2017 na kuongeza kuwa Tume ya Madini ilisimamisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo mapema Agosti mwaka huu kufuatia kuibuka kwa mgogoro  baada ya kikundi cha Mwaguguli Mining Society kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao.

Aliendelea kueleza kuwa Septemba 13 mwaka huu, Tume ya Madini ilituma wataalam wake kufanya ukaguzi katika eneo la mgogoro na kuonekana kuwa mgogoro husika ulitokana na wachimbaji waliovamia eneo hilo kugawanyika na kuunda vikundi viwili ambavyo vimeomba leseni ndogo ya uchimbaji wa madini.

Profesa Kikula aliendelea kufafanua kuwa, kikundi cha Mwaguguli Mining Society kiliwasilisha maombi yake ya leseni  tatu za  uchimbaji mdogo wa madini  Julai 13, 2018 huku kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society kikiwasilisha maombi ya leseni ya uchimbaji mdogo wa madini katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora katika eneo lililokuwa linachimbwa wakati wa uvamizi Agosti 06, 2018.

Alisisitiza kuwa ilionekana sehemu ya eneo la maombi ya kikundi cha Mwaguguli Mining Society inaingiliana na eneo la ombi la kikundi cha Mwamikola Gold Mining.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula alisema Serikali kupitia Tume ya Madini ipo tayari kusaidia vikundi vyote katika maombi mapya ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini kwa haraka ili waweze kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini na kujipatia kipato huku Serikali ikipata mapato yake stahiki.

Alimwagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Mayigi Makolobela kuhakikisha anasaidia kwa haraka vikundi husika katika upatikanaji wa leseni mpya za uchimbaji mdogo wa madini ili waendelee na shughuli za uchimbaji wa madini na kukuza uchumi wao uliokuwa umesimama kutokana na usitishwaji wa shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo husika kutokana na mgogoro.

Meneja wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Zephania Maduhu (kulia) na Mwanasheria wa Tume hiyo, Hadija Ramadhan (kushoto) wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa ziara ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Wakizungumza katika nyakati tofauti mara baada ya maamuzi kutolewa na Serikali kupitia Tume ya Madini, viongozi wa vikundi husika waliipongeza Tume ya Madini kwa utatuzi wa mgogoro kwa kuwa walikuwa wameathirika kiuchumi mara baada ya shughuli za uchimbaji wa madini kusimamishwa kutokana na mgogoro husika.

Naye Mfadhili wa kikundi cha Mwaguguli Mining Society, Shukrani Chacha mbali na kuridhika na kupongeza uamuzi uliotolewa na Tume ya Madini aliomba wachimbaji kutoka katika kikundi cha Mwamikola Mining Society kuzika tofauti zao na kuanza upya ushirikiano ili kila kikundi kinufaike na rasilimali za madini.

Aliongeza kuwa mgogoro uliodumu kwa kipindi kirefu haukuwa na tija kwenye uzalishaji badala yake ulipelekea uchumi katika kijiji cha Mwamikola kudorora na kusisitiza kuwa anaamini mara baada ya kuanza upya kwa shughuli za uchimbaji wa madini uchumi utakua kwa kasi.

Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society, Princh Kissoro aliongeza kuwa utatuzi wa mgogoro umewapa ari mpya ya kufanya shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo husika mara baada ya kupata leseni mpya za uchimbaji mdogo wa madini.

Wakati huo huo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Mayigi Makolobela alisema kuwa atahakikisha vikundi husika vinawasilisha maombi yao upya na kupatiwa leseni ndani ya muda mfupi ili waendelee na uchimbaji wa madini.

Makolobela aliwataka wachimbaji wadogo katika mkoa wa Tabora kuomba leseni kwa kufuata sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa ofisi yake ipo tayari kutoa ushirikiano muda wowote kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Read more

Jengo la Wizara ya Madini kukamilika ifikapo Januari 4,2019

Na Rhoda James, Dodoma

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameagiza Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd kukamilisha ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini ifikapo Januari 4 mwaka 2019.

Ametoa agizo hilo jana tarehe 4 Desemba, 2018 alipofanya ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa ofisi za Wizara lililopo Ihumwa Jijini Dodoma akiambatana na viongozi wengine waandamizi wa wizara.

Muonekano wa eneo la ujenzi wa Jengo la Wizara ya Madini.

Kairuki alibainisha kuwa baada ya sikukuu za mwisho wa mwaka, viongozi wote watatakiwa kuhamia katika eneo hilo kutokana na ukweli kuwa ifikapo Januari 4 jengo hilo litakuwa limekamilika.

Aidha, Waziri Kairuki ameshauri kuwa wakati wanaendelea na maandalizi mengine waendelee na manunuzi ya vifaa, na vifaa hivyo lazima viwe vya viwango ikiwezekana watumie dealers ambao ni wakubwa na wa uhakika.

Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa Wizara, Anthony Tarimo alisema kuwa pesa kwa ajili ya ujenzi huo ipo, wao wanachohitaji ni kujua mkataba ukoje na guarantee ili pesa kwa ajili ya ujenzi huo itolewe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Issa Nchasi ameeleza kuwa wamejiandaa kikamilifu ili kusimamia ujenzi wa Jengo hilo na atateua watu ambao watafutilia kwa ukaribu shughuli za kila siku za ujenzi wa Jengo hilo.

Vile vile, Mwakilishi wa Kampuni ya Mzinga Holding Co. Ltd, Mhandisi Hagai Mziray amesema wataanza maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Madini mapema tarehe 5 Decemba, 2018 na watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi kwa wakati.

Mziray ameongeza kuwa Kampuni yao inao uzoefu wa kutosha katika masuala ya ujenzi kwani wamejihusisha na ujenzi wa majengo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Manispa ya jiji Dodoma, Hosipitali ya Makole, Hosipital ya Mkoa wa Morogoro pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

Kwa sasa Wizara ya Madini inatumia Ofisi za Wakala wa Jiologia Tanzania (GST) zilizopo Mjini Dodoma.

Read more

Mgodi wa Kiwira waanza kuchenjua makaa ya mawe

Na Asteria Muhozya, Kiwira

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema ipo fursa kubwa katika Migodi ya Kiwira na Kabulo inayomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na tayari Serikali kupitia shirika hilo, imeanza kufufua baadhi ya mitambo  mgodini hapo ikiwemo ya kuchakata madini hayo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia vumbi linalotokana na shughuli za uchimbaji wa makaa katika eneo la Kabulo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli a uchimbaji makaa ya mawe na Shirika la Madini la Taifa, (STAMICO)

Waziri Kairuki aliyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea katika migodi hiyo mwishoni mwa wiki na kuchukua fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa Kiwira kutokana na  uzalendo waliouonesha kuhakikisha kwamba mgodi huo unafanya kazi tena.

Aliongeza kwamba, migodi ya Kiwira na Kabulo ni migodi inayotegemeana   hivyo serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba machimbo ya chini katika mgodi  wa Kiwira yananza uzalishaji na ikiwezekana kufikia mwakani uzalishaji kupitia machimbo hayo ufanyike kwa asilimia 100.

Akizungumzia madai ya wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira, alisema tayari madeni hayo yamekwishaanza kulipwa kila uzalishaji unapofanyika na kuongeza, “ madeni ya watumishi yataendelea kulipwa kila wakati uzalishaji unapofanyika hivi ndivyo tulivyokubaliana’’.

Aidha, Waziri Kairuki alimtaka  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, kuona namna ya kutoa motisha kwa wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira hususan wale wanaokaribia kustaafu ikiwa ni ishara ya kuthamini michango yao kwa kutumikia mgodi huo kwa uzalendo na moyo wa kujitolea.

Wakati huohuo, akizungumza katika eneo la machimbo ya Kabulo, alisema kuwa, mgodi huo ulisimama kwa kipindi kirefu hivyo jitihada za serikali ni kuhakikisha kwamba unaanza tena kufanya kazi ili kuleta tija kwa taifa ikiwemo serikali kupata mapato.

Aliongeza kuwa,  wizara  inafanya mashauriano na Wizara ya Nishati ili kuna namna ambavyo makaa ya mawe katika machimbo ya Kiwira na Kabulo yanaweza kutumika kuzalisha umeme  utakaoingizwa  katika gridi ya taifa  na kueleza, “tutakapokuwa tayari tutaanza kuzalisha megawati 200,”.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira

Akizungumzia hali ya uzalishaji  alisema kwamba,  katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba,2018, mgodi wa Kabulo umezalisha tani  Laki Mbili na mbili elfu  ambazo ni mara mbili ya kile kilichozalishwa mwaka jana na kuongeza kwamba,  tayari tani elfu 37 zimesafirishwa nje ya nchi.

Aidha, alisema mkakati  wa wizara ni kuongeza matumizi ya makaa ya mawe  na kuutaja mkakati wa kutumia makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya majumbani ili kuwezesha matumizi ya makaa ya mawe kutumika majumbani badala ya mkaa ambao unaharibu misitu.

“Tunaishukuru kampuni ya SMG kuingia kandarasi na STAMICO katika kuchimba madini haya Kabulo,” alisema Kairuki.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Madini la Taifa ((STAMICO), Kanali Mhandisi Syvester Ghuliku, alisema kuwa shirika hilo limefanya ukarabati wa mtambo wa kuchenjua makaa ya mawe katika mgodi wa Kiwira ambao umegharimu shilingi milioni 30 pamoja na kufanya ukarabati wa maabara na kununua vifaa ambavyo vimegharimu shilingi milioni 12 na kuongeza kuwa, hayo yote yamefanyika ili  kuweka thamani ya madini hayo.

Akizungumzia mipango ya shirika alileza kwamba ni kuendelea kuboresha miundombinu ya mgodi huo kadri uzalishaji unapofanyika likilenga kuhakikisha kwamba mgodi huo unarejesha uzalishaji wake kama ilivyokuwa awali.

Akizungumzia  hali ya uzalishaji katika machimbo ya  Kabulo alisema wateja wa makaa hayo wamekuwa ni viwanda vya saruji , viwanda  vya uzalishaji , nchi za  Kenya na Rwanda na kuongeza kuwa, wateja zaidi wanatarajia kuongezeka kadri uzalishaji unavyoendelea na kuongeza.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO), Kanali Mhandisi Syvester Ghuliku wakati wa wa ziara yake alipotembelea mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira.

Akizungumzia manufaa kwa wananchi wa Kabulo alisema wananchi wanaozunguka migodi hiyo wamenufaika kwa kupata ajira ndogo ndogo na pia wanatarajia kunufaika pale mradi wa makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi ya majumbani utakapoanza.

Aidha, alisema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ileje inanufaika kutokana na kuwepo kwa mgodi wa Kabulo kutokana na tozo zinazolipwa.

Naye, Meneja uzalishaji  na Msimamizi wa Migodi ya Kiwira na Kabulo  Peter Maha, alieleza kuwa, mgodi huo unatarajia kuongeza   uzalishaji  wa makaa ya mawe  ikiwemo kuongezeka kwa  idadi ya wateja  wakiwemo wateja wa zamani ambao walikuwa wakipata makaa hayo kutoka mgodi huo na  kuongeza “ Hata  viwanda vipya sasa vitakuwa na uhakika wa nishati kutokana na makaa tunayoyazalisha hapa,”

Nao, wafanyakazi wa mgodi wa Kiwira wakizungumza katika kikao baina yao na Waziri Kairuki, waliitaka serikali kuhakikisha inaufufua mgodi huo kutokana na  manufaa yake kwa taifa na hususan katika kipindi hiki ambacho kipaumbele cha serikali ni kuwa na Tanzania ya Viwanda na kuongeza, yapo manufaa makubwa kwa taifa kupitia madini ya makaa ya mawe ikiwa mgodi huo utarejesha shughuli zake za uzalishaji kama ilivyokuwa hapo awali.

Pia, waliitaka wizara isaidie kuhakikisha kwamba inakifufua kituo za zamani   cha kuzalisha  umeme mgodini hapo  wakati ikijipanga kujenga kituo kipya kutokana na kwamba, endapo nishati hiyo itazalishwa moja kwa moja mgodini hapo itasaidia kupunguza gharama za uzalishaji.

Read more

Waziri Kairuki ataka kaguzi za mara kwa mara Migodini

Na Asteria Muhozya, Chunya

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amewataka Maafisa Madini nchini kuhakikisha wanafanya kaguzi za mara kwa mara katika maeneo ya wachimbji wadogo ikiwemo kutoa elimu ya uchimbaji, masuala ya afya na usalama kazini ili kuongeza tija katika shughuli hizo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia ramani ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya litakavyokuwa mara baada ya kukamilika kwake. Jengo hilo linajengwa na Mkandarasi SUMAJKT.

Waziri Kairuki aliyasema hayo Novemba 27, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Chunya kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT.

Alisema, wachimbaji wadogo wanatakiwa kulelelewa ili watoke katika uchimbaji mdogo wa madini kwenda uchimbaji wa  Kati na hatimaye kuwa wachimbaji  wakubwa, na kueleza kuwa, ili kufikia azma hiyo  elimu ya mara kwa mara kwa wachimbaji ni muhimu  ikatolewa  kwani itawezesha serikali kupata mapato kutokana na kufuata uchimbaji sahihi.

Pia, aliwataka Maafisa hao kuhakikisha kuwa wanatatua migogoro katika maeneo yao kwani suala hilo litawezesha uzalishaji zaidi na kupelekea serikali kunufaika na shughuli hizo, ikiwemo ongezeko la ajira na ustawi wa jamii.

Vilevile, Waziri Kairuki alieleza kuwa, pamoja na kwamba katika Mwaka wa Fedha 2018/19 wizara yake imepangiwa kukusanya shilingi bilioni 310, lakini kama anataka makusanyo hayo yafikie shilingi bilioni 500 na kuongeza kwamba, Maafisa madini watapimwa kutokana na ukusanyo huo wa maduhuli.

“Sisi tumepangiwa kukusanya shilingi bilioni 310. Lakini na mimi nataka makusanyo hayo yafikie shilingi bilioni 500 na nitawapima maafisa madini kwa ukusanyaji wa maduhuli,” alisema Waziri Kairuki.

Katika hatua nyingine, amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha kwamba zinashaurina na Wizara ya madini katika masuala yote yanayohusu kodi za madini kabla ya kuyatolea maamuzi kwa kuwa, isipofanyika  hivyo inachangia taasisi za serikali kukinzana katika utoaji wa maamuzi.

Alisema, wizara inaandaa utaratibu wa kukutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali   na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI ili kulijadili suala la  kodi katika sekta ya madini.

Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Chunya likiwa katika maendeleo ya ujenzi wake.

Akizungumzia umuhimu wa Kituo cha Umahiri, alisema kuwa, kitawezesha wachimbaji kujua taratibu zinazotakiwa katika  utekelezaji wa majukumu yao katika sekta ya madini na kwamba, wizara inaangalia uwekezano wa kuwa na vituo hivyo katika kila mikoa ikiwemo ofisi za kisasa na vituo vya mafunzo ili kuwezesha  kuwepo na tija zaidi katika sekta ya madini.

“Tumeanza na vituo vya mahiri lakini upo umuhimu wa maafisa wetu kuwa na nyumba za kuishi lakini  pia kuhakikisha kwamba maafisa wetu hawakai katika eneo moja kwa kipindi kirefu,” alisema.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi Wilaya ya Chunya Athumani Kwariko alimweleza Waziri Kairuki kuwa, leseni nyingi wilayani humo hazifanyiwi kazi kutokana na wamiliki wake kukosa mitaji na uwepo wa migogoro.  Hata hivyo amesema kuwa, tayari ofisi hiyo imewasiliana  na  wamiliki hao ili kuhakikisha kwamba wanaziendeleza leseni hizo.

Akizungumzia madini yanayopatikana  wilayani humo  hiyo  aliyataja kuwa ni  pamoja na   ya  dhdhabu, chuma,  bati, ulanga, chokaa na kokoto na mchanga.

Naye, Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Mkoa wa Mbeya Leonard Manyesha akielezea umuhimu wa kituo hicho alisema kwamba kitawawezesha  kupata maelekezo ya kitaalam kuhusu uchimbaji na hivyo kuwawezesha kupata mazao bora ya dhahabu na yenye tija.

Aidha, alipongeza kwa hatua ya serkali ya kutaka kuhamasisha Mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishaji wa masoko ya madini na kueleza kuwa, uwepo wa masoko hayo utasaidia tatizo la wachimbaji kuficha mapato kuisha.

Read more

Serikali haijaruhusu uchimbaji madini Mto Muhuwesi-Kairuki

Na Asteria Muhozya, Songea

Serikali imesema haijaruhusu uchimbaji wa Madini katika Mto Muhuwesi na kwamba tayari Wizara ya Madini ilikwishakutoa maelekezo  yapatayo matano ambayo wahusika wanatakiwa kuyafanyia kazi ili itoe  maamuzi.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mdeme (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Songea Ploliti Mgema wakijadiliana jambo wakati Waziri Kairuki alipomtembelea Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake.

Hayo yalielezwa na  Waziri wa Madini Angellah Kairuki  wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea, wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina  Mndeme ambaye   alimwomba Waziri asimamishe uchimbaji huo na kwamba tayari  Mkoa  umezuia  shughuli hizo kuendelea  kwa kuwa  ndiyo chanzo cha maji mkoani humo na kwamba, alifanya hivyo ili kulinda miundombinu ya barabara.

Waziri Kairuki alimweleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa, wizara ilitoa maelekezo kwa  wahusika kwamba wanatakiwa  kuwasilisha barua ya ridhaa ya Waziri wa Maji, ridhaa ya Wakala wa Barabara nchini (TANROAD), ridhaa ya Bodi ya Bonde la Mto Ruvuma/Pwani na Kusini ili wizara ijiridhishe kabla ya kutoa maamuzi.

“ Tunataka tujiridhishe na approval kutoka katika maeneo hayo na vikipatikana vyote, nitafanya uamuzi. Kwa sasa ipo ridhaa ya bodi ya bonde la mto Ruvuma,” alisisitiza Waziri Kairuki

Pia, akifafanua  kuhusu kusimama kwa shughuli za uchimbaji wa madini ya Uranium unaofanywa na Kampuni ya  Mantra Tanzania Limited, waziri Kairuki  alisema  kuwa,  kampuni hiyo iliomba kusisitisha shughuli zake  kwa kipindi cha miaka mitano kutokana na bei ya madini hayo kushuka katika soko la dunia na kwamba , suala hilo bado linafanyiwa kazi kitaalam na kiuchumi hivyo, bado serikali haijatoa majibu kuhusu suala husika.

Kuhusu  upatikanaji wa masoko kwa wachimbaji wa madini, Waziri Kairuki  alieleza kuwa,   tayari  serikali imepanga kuanzisha masoko ya madini  katika maeneo mbalimbali nchini, na hivyo  kutoa rai kwa  Wakuu wa Mikoa nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uanzishwaji wa masoko hayo. Waziri Kairuki  alitoa ufafanuzi kwa  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina ambaye alitaka kujua ni namna gani serikali inawasaidia wachimbaji wadogo kupata masoko ya kuuzia madini madini yao.

Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Umahiri Songea.

“Mhe. Waziri Mkoa wetu umejaliwa kuwa na madini ya aina mbalimbali na madini haya yamekuwa ni kichocheo cha uchumi. Sasa, bado wachimbaji wetu wanapata changamoto ya masoko kwa ajili ya kuuza madini yao,” alisema Mkuu wa Mkoa Mndeme.

Akizungumzia  ujenzi wa Vituo vya Umahiri, Waziri Kairuki alisema, ujenzi wa vituo vya umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali nchini vinagharimu takribani  Bilioni 11 ambao ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Aliongeza kuwa,   Songea ni eneo  ambalo serikali inaliangalia kwa ajili ya  kuanzisha shughuli za ukataji na uongezaji thamani madini.

Alisema kuwa, serikali iliona umuhimu wa kuwepo na vituo hivyo kutokana na wananchi  wengi kutamani kuingia katika shughuli za uchimbaji  lakini bado  uchimbaji wao umekuwa si salama na wenye tija hivyo, uwepo wa kituo hicho utawezesha kutoa elimu ya uchimbaji sahihi na wenye tija.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Christina Mndeme akizungumzia uwepo wa kituo hicho alisema, kukamilika kwa kituo hicho kutawezesha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika mkoani humo, kupanua wigo wa shughuli za uchimbaji na wachimbaji kuchimba kwa faida.

Aliongeza kwamba, wachimbaji watapata taarifa sahihi wa mahali gani wauze madini yao  na pia uwepo wake  utawezesha kutangaza aina ya madini yanayopatikana mkoani huo.

Vilevile, alisema kuwa, kituo hicho kitawezesha kupunguza migogoro kati ya wachimbaji wadogo na wakubwa kwani kitawezesha kupata taarifa sahihi za wapi wachimbe madini.

Naye, Afisa Madini Mkoa wa Ruvuma Abraham Nkya alisema kuwa, ujenzi wa kituo hicho utawezesha kurahisisha upatikanaji wa takwimu za madini za mkoa huo, wachimbaji kupata elimu ya utaalamu wa uchenjuaji bora wa madini, elimu ya ujasiliamali wa shughuli za madini, afya na usalama mahali pa kazi.

Pia, aliongeza kuwa, uwepo wa kituo hicho chenye nafasi kubwa, kitaweza kuwahudumia wachimbaji wengi zaidi.

Waziri Kairuki alitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Songea Novemba 26.

Read more

Biteko atembelea wachimbaji wadogo Mbogwe, Geita

Na Greyson Mwase,

Leo tarehe 26 Novemba, 2018 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amefanya ziara katika machimbo ya  dhahabu ya wachimbaji wadogo yaliyopo wilayani Mbogwe mkoani Geita lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali  zinazowakabili wachimbaji wadogo. Katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Martha Mkupasi, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe, Augustino Masele, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahali, na Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Geita, Christopher Kadeo.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akimsikiliza mmoja wa wachimbaji wa madini ya dhahabu katika machimbo ya Nyakafulu yaliyopo wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Wengine ni pamoja na  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda, Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Mhandisi Frederick Mwanjisi, Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbogwe pamoja na waandishi wa habari.

Mara baada ya kukamilisha ziara yake katika migodi ya kuchenjua dhahabu ya Isanja Badugu, na Magimi Gold Partners iliyopo katika eneo la Buluhe wilayani Mbogwe mkoani Geita, Naibu Waziri Biteko alielekeza migodi husika kuhakikisha inahifadhi nyaraka zote mgodini kama sheria ya madini inavyotaka.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko alifanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Nyakafulu uliopo Wilayani Mbogwe Mkoani Geita unaomilikiwa na  kikundi cha Isanja Badugu na kufanya mkutano wa hadhara ulioshirikisha wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli  za uchimbaji madini katika eneo la mgodi huo na kutatua kero zao hapo hapo.

Mara baada ya kusikiliza na kutatua  kero mbalimbali zilizowasilishwa na wachimbaji wadogo hao, Naibu Waziri Biteko alitoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya  Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha inafanya uchunguzi dhidi wizi uliofanywa na  mmoja wa viongozi wa kikundi cha Isanja Badugu na kuchukua hatua za kisheria, wachimbaji wadogo kuhakikisha wanalipa kodi za madini Serikalini,  wamiliki wa machimbo kuhakikisha hawawanyanyasi wachimbaji wadogo na kufanya nao kazi kwa mikataba na wamiliki wa machimbo kuhakikisha hawatoi rushwa.

Kero zilizowasilishwa na wachimbaji wadogo hao awali ni pamoja na  baadhi ya wachimbaji wa madini kufanya kazi pasipokuwa na mikataba rasmi, ukosefu wa nishati ya umeme kwa ajili ya kuendeshea mitambo na baadhi ya wachimbaji wadogo kutokulipwa mara baada ya kusimamishwa kazi.

Read more

Naibu Waziri Biteko atembelea Mgodi wa Buzwagi

Na Greyson Mwase

Leo tarehe 25 Novemba, 2018 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amefanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali  zinazoukabili mgodi huo. Katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko aliambatana na  Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,  Anderson Msumba, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama, Timothy Ndaya,  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Mhandisi Abdulrahman Milandu, Afisa Mgodi Mkazi wa Mkoa wa Kahama, Modest Tarimo, Mkaguzi wa Migodi kutoka Tume ya Madini Mhandisi Frederick Mwanjisi,wataalam kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

Sehemu ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi uliopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Mara baada ya  kufanya ziara na kupokea taarifa ya hatua za kufunga mgodi wa Buzwagi, Naibu Waziri Biteko alitoa  maagizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na:- mgodi kuwasilisha upya mpango wa ufungaji wa shughuli zake kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini ili aweze kuwasilisha kwenye Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji wa Migodi  kwa ajili ya kuidhinishwa ili  utekelezaji wake uanze mara moja, pawepo na utaratibu wa kupitia upya kiwango cha fedha    zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa mazingira (rehabilitation bond) na kuweka mkakati wa kuhakikisha kuwa shughuli za kiuchumi za wakazi wanaozunguka mgodi huo haziathiriki na ufungaji wa mgodi husika.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kufuata sheria na kanuni za ufungaji wa mgodi kwa wakati na kuepuka kufanya kazi kwa zimamoto.

Meneja Mkuu wa Migodi ya Dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu, Benedict Buzunzu alisema kama mgodi wamepokea maelekezo na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.

Read more

Biteko atatua mgogoro sugu madini

 • Ni baada ya kruhusu wananchi kijiji cha Mhandu kuendelea na  uchimbaji dhahabu

Na Greyson Mwase, Shinyanga

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameruhusu wananchi  wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuendelea na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la utafiti wa madini hayo lililokuwa linamilikiwa na Menan Sanga kwa kushirikiana na kampuni ya  Lion Town.

Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara.

Biteko aliyasema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wananchi  wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa  huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wachimbaji wa madini.

Katika ziara hiyo, Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Wataalam kutoka Wizara ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

Biteko alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini  haiwezi kuruhusu mwekezaji kumiliki eneo pasipo kuliendeleza, kutokulipa kodi inayohitajika Serikalini  huku wananchi wenye nia ya kuchimba katika eneo husika wakiendelea kuteseka.

Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja marekebisho ya Sheria ya Madini inayotambua madini kama rasilimali za watanzania wote.

“Madini ni mali ya watanzania wote, na sisi kama Serikali tumejipanga katika kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kwa kiasi kikubwa katika umiliki wa rasilimali za madini, hivyo ninawaomba endeleeni kufanya kazi ya uchimbaji katika eneo hili wakati taratibu nyingine zikiwa zinaendelea,” alisema Biteko huku akishangiliwa na wananchi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini waliopo katika eneo hilo pamoja na kuwapatia leseni za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini ili wawe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa sekta ya madini.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo jinsi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinavyofanyika chini ya ardhi katika eneo la Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu.

Pia alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga kuandaa orodha ya wachimbaji wote wa madini pamoja na taarifa za uzalishaji wa madini  yanayozalishwa na wachimbaji wa madini ikiwa  ni pamoja na kodi mbalimbali wanazolipa Serikalini.

Aliwataka wachimbaji wadogo hao kufuata sheria na kanuni za madini ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali zinazohitajika Serikalini na kusisitiza kuwa, Serikali haitasita kufuta leseni za madini pale watakapokiuka sheria na kanuni za madini.

Awali wakizungumza katika nyakati tofauti wananchi  wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga walisema kuwa awali eneo hilo lilikuwa likimilikwa kampuni ya Lion Town tangu mwaka 1989 kabla ya kukabidhiwa kwa Menan Sanga ambaye amekuwa  haendelezi uchimbaji katika eneo hilo  huku akiwafukuza wananchi ambao wamekuwa wakichimba madini ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hao Innocent Deus alisema kuwa wachimbaji wadogo wa madini wanaochimba madini katika eneo hilo wamekuwa wakitishiwa maisha ikiwa ni pamoja na kupigwa mara kwa mara na walinzi waliowekwa na mmiliki wa eneo  hilo Menan Sanga

Deus alisema awali kikundi kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo kijulikanacho kwa jina la BMS kiliundwa na kuomba leseni ya uchimbaji wa madini katika Wizara ya Madini kupitia ofisi yake iliyopo mkoani Shinyanga lakini walishangaa kuambiwa kuwa leseni husika imeshaombwa na kutolewa kwa Menan Manga.

Aliomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuwapatia sehemu ya eneo hilo kwa ajili ya kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini huku taratibu nyingine zikiendelea ikiwa ni pamoja na urasimishaji na utoaji wa leseni ili waweze kuchangia kwenye pato la Taifa.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Naye Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mbali na kutoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Madini kwa kutatua mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu aliiomba Wizara ya Madini  kuwapatia maeneo yenye  madini kwa ajili ya uchimbaji hususan katika eneo husika kwa kuwa madini ni tegemeo pekee kwenye uchumi wao.

Alisema kuwa, wananchi wengi wanaishi katika maisha magumu huku wakiwa na rasilimali za madini ya kutosha ambazo zikitumiwa kikamilifu zinaweza kuwanufaisha na kuimarisha huduma nyingine za jamii kama vile miundombinu ya barabara, umeme na maji.

Wakati huohuo, Naibu Waziri Biteko alifanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulioko katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga  lengo likiwa ni kuona shughuli za uchimbaji madini na kufuatilia  utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki tarehe 24 Aprili, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Biteko aliutaka mgodi huo kuhakikisha unamaliza mgogoro kati yake na wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa mchanga wa marudio ambao ni mali ya wananchi  wanaozunguka mgodi huo waliouacha wakati wakipisha shughuli za uchimbaji kwa mgodi huo kwa kufuata sheria na taratibu.

Aidha, aliutaka mgodi kuandika barua kwenda Tume ya Madini kwa ajili ya kuomba mwongozo  wa namna ya kutoa mchanga wa marudio na kuwakabidhi wananchi ambao ndio wamiliki wa awali wa mchanga huo wakati wakiendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Aidha, Naibu Waziri Biteko  alikerwa na kitendo cha mgodi huo kutokulipa kodi ya mapato kwa takribani miaka 19 na kuendesha shughuli zake kwa kusuasua  kwa kisingizio cha kuwa mgodi umeamua kupunguza gharama za uendeshaji.

“Haiwezekani kama mgodi mnaamua kupunguza gharama za uzalishaji pasipo kushirikisha Serikali huku mkibadilisha umiliki wa leseni ya baruti wa kampuni nyingine na ni jambo ambalo halikubaliki kabisa,” alisisitiza Biteko.

Alielekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Sinyanga kuangalia iwapo kuna taratibu zimekiukwa ili taratibu za kisheria zichukuliwe.

Read more

Waziri Kairuki aahidi kusaidia uendelezaji madini ya nikel na chumvi Simiyu

Na Asteria Muhozya, Bariadi

Waziri wa Madini Angellah Kairuki  ametembelea Kituo cha Umahiri cha Bariadi ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho na kumhaidi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka kuwa,

Wizara  ya Madini itaangalia namna ya kuusaidia mkoa huo katika uendelezaji wa madini ya Nikel na chumvi yanayopatikana mkoani humo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiangalia matofali yanayotumika kujenga Kituo cha Umahiri cha Bariadi, alipokitembelea kituo hicho ili kukagua maendeleo ya ujenzi wake. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.

Pia, Waziri Kairuki ametoa pongezi kwa Mkandarasi SUMAJKT anayejenga kituo hicho  kwa kazi iliyofanyika na kumtaka mkandarasi huyo kuzingatia muda wa kukamilisha ujenzi na ubora wake.

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa kuridhia kuondoa tozo 9 kati ya 16 zilizokuwa zikitozwa na Taasisi mbalimbali  za serikali  katika Sekta ya Madini.

Amesema uwepo wa kituo hicho mkoani humo, utawezesha wachimbaji wadogo  wa madini kuchimba kwa tija.

Pia, ametoa rai kwa wananchi walio tayari kuwekeza katika Sekta ya Madini kuwekeza mkoani humo pamoja na maeneo mengine nchini.

Vilevile, amewataka wale wenye leseni za madini kutoshikilia leseni hizo bila  kuziendeleza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka, ameishukuru Wizara kwa kuuchagua mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa ambayo vituo hivyo vya umahiri vinajengwa.

Amesema  kuwa, uwepo wa kituo hicho utawezesha wachimbaji kupata mafunzo ya uchimbaji bora wenye tija  ikiwemo kupata mahali sahihi ambapo shughuli za uendelezaji Sekta ya Madini utafanyika.

Aidha, ameleeza pia, kituo hicho kitatumika kama sehemu ya kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa sahihi ikiwemo  taarifa kuhusu bei elekezi ambazo wizara kupitia Tume ya Madini imekua ikitoa kila mwezi.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka wakimsikiliza Mkandarasi SUMAJKT (hayupo) akieleza maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Simiyu. Waziri Kairuki alitembelea kituoni hapo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo husika.

Vituo vya Umahiri vinajengwa na mkandarasi kampuni ya SUMAJKT maeneo mbalimbali nchini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) kupitia Mkopo wa Benki ya Dunia.

Vituo hivyo vya umahiri vinalenga kutoa mafunzo ya jiolojia katika utafiti, mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.

Pia, vinalenga katka kutoa mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo, mafunzo ya usalama na afya sehemu za kazi na mafunzo bora za utunzaji wa mazingira kwenye migodi ya wachimbaji.

Mbali na Bariadi, kituo kama hicho kinachojengwa Bukoba, Mara, Chunya, Handeni, Songea, na Chuo Cha Madini Dodoma.

Wakati huo huo, Waziri Kairuki jana alitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Handeni. Akiwa kituoni hapo, Waziri Kairuki alisema wizara inaendelea kuweka jitihada kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia zaidi katika pato la taifa  na hivyo kuwataka watumishi katika sekta husika kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa weledi na kuongeza kuwa,“ mjue kuwa kosa moja mtakalofanya katika sekta hii, linawakosesha watanzania wote manufaa.

Aliongeza kuwa, hatosita kumwondoa afisa yoyote atakayekwamisha  kazi ya serikali na watanzania na kueleza kuwa, bado analikumbushia suala hilo kwa kuwa ni wajibu wake na kusema kuwa, ni vema watumishi katika sekta ya madini kuongeza nguvu  katika utendaji kazi na kuhakikisha kuwamba wanatoa kipaumbele kwa rasilimali hiyo ya madini.

“Mwaka huu tumewekewa malengo ya kukusanya shilingi bilioni  310, natamani tufike makusanyo ya shilingi bilioni 500. Nitawapima Maafisa Maadini kwa hayo. Sitasita kuchukua hatua kwa wanaolegalega,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Pia, alizungumzia kuhusu wamiliki wa leseni na kueleza kuwa, wote wanaomikili leseni hizo wanapaswa kuziendeleza badala ya kuzihodhi bila kuzifanyia kazi na kusema kuwa “ lengo letu ni kuhakikisha kwamba leseni zinachangia  katika upatikanaji wa mapato,” alisema Kairuki.

Sehemu ya jengo la Kituo cha Umahiri Bariadi katika hatua zake za ujenzi.

Aidha, alieleza kwamba, Serikali kupitia Wizara ya madini inaandaa Jukwaa la uwekezaji kati ya nchi ya China na Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika mwezi Disemba na hivyo kutoa wito kwa wadau wa sekta ya madini kuchangamkia fursa hiyo.

Pia, aliendelea kusisitiza kuhusu wadau wa sekta ya madini kufuata sheria na kuzingatia taratibu zilizopo wakati wa utekelezaji wa shughuli zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, alisema kuwa, uwepo wa kituo hicho katika wilaya hiyo kutakuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi wilyani humo na hivyo kutoa wito kwa wale wenye ni ya kufanya biashara ya madini wilayani humo kutosita kufanya hivyo.

Alisema Wilaya hiyo itasimamia kwa karibu maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kutokana na manufaa yake kwa wilaya hiyo na kueleza kuwa, wilaya hiyo ni mzalishaji mkubwa wa madini ya viwandani hivyo uwepo wa kituo hicho kitahamasisha wawekezaji zaidi kuwekeza wilayani humo.

Mwisho alimtaka Mkandarasi SUMAJKT kuharakisha ujenzi huo kabla ya msimu wa mvua na kumwomba Waziri Kairuki kuhakikisha  kusaidia upatikanaji wa haraka wa fedha za ujenzi.

Read more

Taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu North Mara Community Trust Fund, tarehe 21 Novemba 2018

Ndugu waandisha wa habari kama mnavyofahamu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika ziara yake mkoani Mara mnamo tarehe 04 hadi 08 Septemba 2018 pamoja na mambo mengine alielekeza kufanyika uchunguzi wa Mfuko wa North Mara Community Trust Fund baada ya baadhi wa wananchi wa Nyamongo wilayani Tarime kulalamika juu ya jamii kutofaidika na mfuko huo na badala yake unafaidisha watu wachache.

Ndugu waandishi wa habari, kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Wizara ya Madini imebaini mambo yafuatayo;

 1. Kati ya mwaka 1990 hadi 1995, Vijiji vya Nyangoto, Kerende, Kewanja, Genkuru na Nyamwaga viliwahi kumiliki leseni tano za uchimbaji (CTs). Mwaka 1996, Vijiji hivyo vilibadili leseni hizo kwa hiari na kuwa leseni ya utafiti PL 370/96 na kisha kuihamishia kwa Kampuni ya East Africa Gold Mining Ltd (EAGM) na kisha kubadilishwa na kuwa leseni ya uchimbaji wa kati (ML 17/96).>>Soma Zaidi>>
Read more

Waziri Kairuki aagiza RITA kuvunja bodi ya uongozi wa mfuko wa udhamini wa North Mara

Na Asteria Muhozya, Mara

Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa  kusimamia  uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri  wa usimamizi  wa Mfuko huo ambao utakuwa na  manufaa kwa Taifa .

Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuruhusu fedha za Keng’anya Enterprises Ltd (KEL) kuendelea kulipwa  hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo, huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.

“Kwa kuwa Keng’anya Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,” alisisitiza Kairuki.

Waziri Kairuki  alitoa  maagizo hayo Novemba 21, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye alielekeza kufanyika uchunguzi wa Mfuko wa North Mara Community Trust  Fund, baada  ya baadhi ya wananchi wa Nyamongo Wilayani  Tarime kulalamika juu ya jamii kutofaidika na mfuko huo na badala yake kunufaisha baadhi ya watu wachache.

Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kufanyika kwa uchunguzi wa mfuko huo wakati wa ziara yake Mkoani Mara tarehe 4 hadi 8 Septemba, 2018. 

Mbali na agizo la kuuvunja uongozi wa mfuko, Waziri Kairuki aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria wajumbe wa bodi ya wadhamini, menejimenti ya mfuko na yeyote atakayethbitika kujihusisha na ufujaji na matumizi mabaya ya fedha za mfuko.

Pia, aliiagiza serikali ya Mkoa kukaa na wamiliki wote wa leseni zilizopo ndani ya Mgodi ambao wanalipwa mrabaha wa asilimia 1 kuangalia mfumo bora ili nao wachangie kwenye mfuko sehemu ya fedha wanazopokea kwa ajili ya maendeleo ya vijiji vnavyozunguka Mgodi wa North Mara.

Vilevile, aliigiza TAKUKURU kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wote watakaobainika kufanya ufujaji na ubadhirifu wa fedha za umma shilingi 214,000,000.

Maagizo ya Waziri Kairuki yanatokana na yaliyobainika katika kamati iliyoundwa na Wizara ya Madini baada ya kutolewa maelekezo ya kuchunguzwa kwa mfuko huo na Rais Magufuli.

Waziri Kairuki alisema miongoni  mwa mambo iliyoyabaini  kamati hiyo ni pamoja na Kampuni Tanzu ya North Mara Commercial Business Ltd tarehe 20 Aprili, kutoa kiasi cha shilingi milioni 214,000,000 kwenda kwa DAS Tarime kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha miwa, ambapo katika taarifa yake, Waziri Kairuki alisema kuwa, fedha hizo zilitokana na maombi yaliyowasilishwa na  Mkuu wa wilaya ya Tarime, ambazo hata hivyo, hazikuzingatia utaratibu wa fedha za umma na manunuzi.

“Kampuni Tanzu ilifunguliwa mwaka 2017 ambayo wana hisa wake ni North Mara Community Trust Fund asilimia 99 na Bw., Robin Motengi Marwa asilimia 1,” alisema Kairuki

Aliongeza kuwa, pia ilibainika kuwa, wajumbe wa bodi  ya wadhamini wamekuwa wakikopeshwa  fedha za mfuko kinyume na malengo ya uanzishwaji wa mfuko huo.

Pia, kamati hiyo ilibaini kwamba, kati ya Mwaka 1990 hadi 1998, vijiji vya Nyangoto, Karende, Kewanja, Genkuru na Nyamwanga viliwahi kumiliki leseni tano za uchimbaji (CTs). Mwaka 1996, vijiji hivyo vilibadili leseni hizo kwa hiari yao na kuwa leseni ya utafiti PL 370/96 na kisha kuihamishia kwenye Kampuni ya East African Gold Mining Ltd (EAGM) na kisha kubadilishwa kuwa leseni ya uchimbaji wa kati (ML 17/96).

Halikadhalika, Waziri Kairuki alisema kamati ilibaini kuwa,  North Mara Community Trust Fund ilianzishwa kwa makubaliano kati ya Mgodi  na kampuni ya KEL ya Mwaka 2004. Mfuko huo ulisajiliwa Mwaka 2013 na kuanza kazi Mwaka 2015. Aliongeza kuwa, wachangiaji pekee wa Mfulo huo ni KEL na Mgodi kwa kiwango cha sawa cha asilimia 0.1 ya uzalishaji katika eneo la KEL.

“Mfuko huo unaendeshwa na wajumbe wa bodi inayoundwa na pande zote tatu yaani Mgodi, KEL na vijiji, bodi inatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watano.

Akizungumza kuhusu malengo ya kuundwa mfuko huo, alisema kamati ilibaini kwamba mfuko ulianzishwa kwa lengo l kutafuta shughuli zenye manufaa kwa jamii, kuhamasisha, kusaidia na kuwezesha program na shughuli kwenye maeneo ya elimu, mafunzo, afya, uwezo kilimo , maji na kupunguza umaskini kwa ujumla kadri ya wadhamini watakavyoona inafaa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, alisema kazi hiyo ilifanyika kwa kipidi cha miezi miwili na hivyo kumshukuru waziri na wote walioshiriki kukamilika  maagizo hayp hayo ya kufanyika uchunguzi, yaliyotolewa na Rais Magufuli.

Read more

Vituo vya Umahiri kuchochea shughuli za uongezaji thamani madini nchini-Kairuki

 • Asema baada ya Lwamgasa kituo kingine cha mfano kujengwa

Imeelezwa kuwa, vituo vya Umahiri vinavyojegwa maeneo mbalimbali nchini vinatarajiwa kuwa kichocheo cha shughuli za uongezaji thamani madini nchini kwa kuwa, vinatarajia kutoa mafunzo ya uchimbaji bora wa madini ikiwemo uongezaji thamani madini, ukataji na ung’arishaji madini.

Hayo yamebainishwa Novemba 20 na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Musoma kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT na kusimamiwa na kampuni ya Sky Architects.

Katika ziara hiyo, Waziri Kairuki ameambatana na Naibu  Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, Andrew Eriyo pamoja na Watendaji wa  Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara na uongozi wa Mkoa wa Mara.

Waziri Kairuki ameeleza kwamba, serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa shughuli za uongezaji thamani madini zinafanyika nchini badala ya kusafirisha madini yakiwa ghafi na kuongeza kuwa,  uwepo wa vituo husika utaongeza shughuli  hizo kufanyika nchini kwa kuwa vitatoa elimu  ambayo itawezesha wachimbaji kufanya uchimbaji wenye tija.

Pia, amesema serikali itaendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika nchini ikiwemo kuhakikisha kwamba inajenga  maeneo mengi zaidi ya vituo hivyo.

Vilevile, amezungumzia kituo cha mfano cha Lwamgasa kinachojengwa mkoani Geita, na kueleza kuwa, serikali inaangalia uwezekano wa kuwa na kituo kama hicho katika maeneo mengine na kuongeza, “tunaangalia sehemu nyingine baada ya kuwa na kituo cha mfano cha Lwamgasa huenda tukajenga kituo kama hicho hapa Musoma”.

Kituo cha Lwamgasa ni moja ya vituo ambavyo vinalenga katika kutoa mafunzo kwa  vitendo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kuhusu uchimbaji wenye tija ikiwemo uchenjuaji bora pasipo kutumikia kemikali.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya tarehe 29 Oktoba,  kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wizara ilieleza kuwa kazi ya ujenzi wa mgodi wa Lwamgasa na usimikaji mitambo ya uchenjuaji katika kituo  hicho imekamilika kwa asilimia 80.

Akiwa kituoni hapo, Waziri Kairuki ameendelea kusisitiza kuhusu kuzingatia muda wa kukamilisha ujenzi huo ikiwemo kuzingatia ubora na viwango vya ujenzi vinavyotakiwa.

Pia, ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa ushirikiano inaoonesha katika kufuatilia ujenzi huo na kuutaka kuendelea kushirikiana na wizara ili kuhakikisha kwamba azma ya kituo hicho inafikiwa.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Mara, Mgaya Nyaisara  amesema kuwa, kituo kitatoa mafunzo ya namna ya uandaa sampuli za madini, namna ya kusafisha madini pia kutakuwa na mashine za kupima madini ya aina mbalimbali.

Naye w Mkandarasi SUMAJKT, katika taarifa iliyosomwa na Meja Onesmo Njau, amesema kuwa, kampuni hiyo itahakikisha inakamilisha ujenzi wa kituo hicho katika muda uliopangwa kimkataba na kueleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho unaogharimu shilingi bilioni 1.2 ikijumuisha jengo la ofisi ya madini na kituo cha umahiri umefikia asilimia 35.

Vituo vya umahiri vinajengwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) kwa Benki wa Dunia.

Read more

Hakuna Krismasi, Mwaka Mpya vituo vya umahiri visipokamilika-Kairuki

 • Awatoa wasiwasi wachimbaji wa Bati Kyerwa

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amemtaka Mkandarasi Kampuni ya SUMAJKT kuzingatia muda uliopangwa wa  kukamilisha ujenzi wa vituo vya Umahiri vinavyojengwa  na kampuni hiyo maeneo mbalimbali nchini na endapo itashindwa kukamilisha kwa wakati asahau habari ya kusheherekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Waziri Kairuki aliyasema  hayo Novemba 19, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umahiri cha Bukoba ambacho ni miongoni mwa vituo vinavyojengwa na serikali ambapo pamoja na mambo mengine, vinalenga kutoa mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.

Pamoja na kupogeza hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo cha Bukoba, Waziri Kairuki ameitaka kampuni hiyo kuzingatia ubora ili kuwezesha majengo hayo kutumiwa na kizazi cha sasa na vizazi vijavyo ili kuendelezaji sekta ya madini nchini.

Waziri Kairuki alisema kuwa, ujenzi wa vituo hiyo umepangwa kukamilika ifikapo disemba 22 mwaka huu  na  shughuli zote za ujenzi zinatakiwa kukamilika ifikapo Januari 15, 2019.

Akizungumza katika ziara hiyo, Meneja wa Opereshi ya SUMAJKT Kapteni Fabian Bubelwa alisema kuwa, ujenzi wa kituo cha Bukoba utagharimu shilingi bilioni 1.8 na kilipangwa kukamilika ndani ya  kipindi cha miezi 6 kama ilivyokubalika katika Mkataba  na kuongeza kuwa, hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 35.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, alimwahidi Waziri Kairuki kufuatilia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo kutokana na thamani yake na manufaa yake kwa mkoa huo na kuongeza kuwa, mkoa huo unakionea fahari kituo hicho.

Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki akizungumza  kwa nyakati tofauti  ikiwemo na Wamiliki wa Kampuni TanzaPlus  inayolenga kufanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya bati wilayani Kyerwa , na wachimbaji wa madini ya bati katika kijiji cha Nyaruzumbura, amewataka wadau hao kuwa wavumilivu wakati serikali ikikamilisha taratibu za kupata Mkataba wa  Hatimiliki ya madini  hayo ili yaweze kutambulika katika eneo na nchi yanayotoka kutokana na upekee wa madini hayo ikiwemo mahitaji yake katika soko la dunia.

Waziri Kairuki alisema zipo fursa nyingi zinakuja kutokana na uwekezaji wa madini hayo na kueleza kwamba, wapo wawekezaji wa kampuni za TanzaPlus ambao walikuwa na changamoto ya leseni lakini sasa tatizo hilo halipo tena.

“TanzaPlus na ATM wanatarajia kununua kiasi kikubwa cha madini ya bati kutoka kwenu kwa hivyo muwe wavumilivu fursa zipo. Na wanasema wanahitaji kiasi kikubwa sana huenda hata kiasi mnachochimba kisiwatosheleze, alisema Kairuki.

Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza Meneja na mmiliki wa kiwanda cha TanzaPlus Minerals Salim Mhando ambaye pia ni Diaspora kwa jitihada zake za kuanzisha kiwanda cha uchenjuaji wa madini ya bati nchini na kueleza kuwa, kitakuwa kiwanda cha kwanza cha uchenjuaji wa madini ya bati nchini.

Mbali na kiwanda hicho, Wilaya ya Kyerwa pia inatarajiwa  kuwa na kiwanda kingine cha uchenjuaji wa madini ya bati cha ATM ambacho kinatarajiwa kuanza shughuli zake ifikapo mwezi Machi mwaka 2019 ilihali kiwanda cha TanzaPlus Minerals kinatarajiwa kuanza shughuli za uchenjuaji mwezi Januari mwaka ujao.

Akizungumzia kuhusu manufaa ya madini hayo, amewataka wamiliki hao kuzingatia na kufuata bei elekezi zinazotolewa na Serikali na kueleza kuwa tayari wizara kupitia Tume ya Madini imeanza kutoa bei elekezi za madini suala ambalo  wadau wa madini wanatakiwa kulizingatia.

Vilevile, Waziri Kairuki aliendelea kusisitiza kuhusu  zuio la kusafirisha madini ghafi nje ya nchi kabla ya kuongezwa thamani  na kueleza kwamba, uongezaji thamani madini nchini unalenga katika kuwanufaisha wachimbaji na taifa ikiwemo kuhamasisha viwanda   vya ndani.

Pia, aliwaeleza wachimbaji hao kuwa,  pale ambapo shughuli za uzalishaji wa madini hayo zitakapokaa vizuri wanapaswa kuzingatia ulipaji wa tozo mbalimbali za serikali ikiwemo kuzingatia sheria na taratibu zote zinazotakiwa katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

Aliongeza kuwa, bado wachimbaji wadogo wanachangia asilimia ndogo katika ulipaji kodi ikilinganishwa na uwekezaji wao pamoja na shughuli za uchimbaji wanazofanya.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkoa wa Kagera, Lucas Mlekwa  akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyaruzumbura uzalishaji wa madini ya bati, alisema kuwa kuna jumla ya leseni za uchimbaji mdogo madini hayo 250 zilizopo Wilayani Kyerwa ambapo leseni 120 ndiyo zina uzalishaji kwa sasa na wa kusuasua.

Baada ya kukagua maendeleo ya kituo cha Bukoba, katika ziara yake, waziri Kairuki anaendelea na ukaguzi wa vituo vingine kikiwemo cha Musoma, Bariadi, Handeni, Songea, Chunya, Mpanda na Songea

Vituo vya Umahiri vinajengwa na mkandarasi kampuni ya SUMAJKT maeneo mbalimbali nchini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) na vinalenga kutoa mafunzo ya jiolojia katika utafiti, mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.

Halikadhlika vinalenga katka kutoa mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo, mafunzi ya usalama na afya sehemu za kazi na mafunzo bora za utunzaji wa mazingira kwenye migodi ya wachimbaji.

Read more

Taarifa za utafiti wa madini zitolewe kwa wananchi-Biteko

Na Greyson Mwase, Singida

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida kuhakikisha unatoa taarifa za tafiti zake zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ili wachimbaji wadogo waweze kuzitumia katika kubaini madini yaliyopo na kuanza kuchimba kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

Naibu Waziri Biteko alitoa agizo hilo leo tarehe 19 Novemba 2018 kwenye mkutano wa hadhara na wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika tarafa ya Mang’onyi wilayani Ikungi mkoani Singida kama sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wa madini.

Aliongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira bora ya uchimbaji  wa madini kwa wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa mbalimbali  za utafiti zilizofanywa na Wakala wa Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na kampuni za utafiti wa madini lengo  likiwa  ni  kuhakikisha kuwa uchimbaji wao unakuwa wa uhakika na sio wa kubahatisha.

Akielezea maboresho mengine yaliyofanywa katika sekta ya madini, Biteko alisema Serikali imeboresha  Sheria ya Madini inayotambua madini kama mali ya watanzania  yanayosimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeweka mkakati wa kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini wasio rasmi na kuwapatia  leseni za madini ili uchimbaji wao ulete tija kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuunda vikundi na kupewa leseni ili waanze kuchimba   na kulipa kodi serikalini.

“Sisi kama Serikali kupitia Wizara ya Madini lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaweka mazingira bora kwa wachimbaji wadogo wa madini ili uchimbaji uongeze kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia kodi na tozo mbalimbali,” alisema Biteko.

Wakati huohuo Biteko aliwataka wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Shanta kutokuharibu miundombinu  ya maji iliyowekwa ili iweze kunufaisha wananchi wote.

Awali wakiwasilisha kero mbalimbali wakazi hao waliiomba Wizara ya Madini kuwapatia maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa madini ili waweze kujiingizia kipato na kulipa kodi serikalini.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo wa madini katika tarafa ya Mang’onyi iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Consolata Joseph alisema kuwa uchimbaji wao  umekuwa ni wa kubahatisha na hata kuvamia maeneo yenye leseni kubwa ya madini inayomilikiwa na Kampuni ya Dhahabu ya Shanta.

Aliongeza kuwa, kama wachimbaji wadogo wapo tayari kulipa kodi stahiki serikalini mara baada ya kupatiwa maeneo na kuanza kuendesha shughuli za uchimbaji wa madini.

Awali akizungumza katika ziara hiyo, Meneja Mkuu  wa Mgodi wa Dhahabu wa Shanta uliopo wilayani Ikungi mkoani Singida, Philbert Rweyemamu alisema mgodi umeshaanza kutoa fidia na kuongeza kuwa mpaka sasa umeshatoa shilingi bilioni 2.6 pamoja na ujenzi wa makazi mbadala ambapo mpaka sasa wameshajenga nyumba sita.

Aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu, mgodi unatarajia kukamilisha ujenzi wa nyumba nyingine sita na kufanya idadi ya nyumba kuwa 12 kama sehemu ya kuhakikisha wananchi wanaolipwa fidia wanaishi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia changamoto za mgodi wake, Rweyemamu alieleza kuwa ni pamoja na wachimbaji wadogo haramu kuvamia eneo la mgodi  na kuchimba madini, miundombinu kuhujumiwa na baadhi ya wananchi kugomea fidia inayotolewa na kampuni hiyo.

Read more

Kamati ya ushiriki wa Watanzania katika sekta ya madini yafanya kikao cha kazi

Na Greyson Mwase,

Leo tarehe 16 Novemba, 2018 Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini  (Local Content) imekutana kwenye Ofisi za Tume ya  Madini zilizopo jijini Dodoma lengo likiwa ni kupokea na kujadili taarifa za kampuni zilizowasilisha mipango  ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya madini kama sehemu ya maombi ya leseni za madini.

Sekretarieti ya kikao hicho ikinukuu maelekezo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki pamoja na wajumbe wengine katika kikao hicho.

Read more

GST yaagizwa kuandaa ramani za Madini ngazi za Mikoa, Wilaya

 • Biteko asema wachimbaji sasa kuchimba kwa uhakika

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania  (GST) imetakiwa kuandaa ramani zinazoonyesha madini mbalimbali katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ili kuwapa nafuu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Naibu Waziri Doto Biteko akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming Cheti cha kutambua mchango wake na kukamilika kwa utafiti wa Jiokemia uliofanywa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko   baada ya kupokea taarifa ya Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika nchi nzima kwa ushirikiano kati ya GST na Taasisi ya Jiolojia ya China.

Naibu Waziri Doto, pia, ameitaka taasisi hiyo kuelekeza nguvu katika kuisaidia serikali katika kupata matokeo chanya katika shughuli za madini huku ikiongeza thamani ya kazi kutokana na utafiti huo na kuongeza kuwa, GST inaweza kutumia utafiti huo mkubwa kuandaa ramani za madini katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

Akizungumzia manufaa ya tafiti huo kwa Tanzania, amesema baada ya muda si mrefu watanzania wanaofanya shughuli za uchimbaji watahamia katika uchimbaji wa uhakika na siyo wa kubahatisha kwa kuwa utafiti huo unaonesha mahali sahihi ambapo shughuli hizo zinaweza kufanywa.

Amesema mbali na shughuli za madini, utafiti huo pia unaweza kutumika katika sekta za kilimo, maji na ujenzi wa barabara kwa kuwa unawezesha kutambua aina ya udongo unaofaa kwa shughuli hizo.

Kutokana na umuhimu wa utafiti na kazi iliyofanywa na taasisi hizo mbili, Naibu Waziri Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuitumia taasisi ya GST katika shughuli za kitaalam ikiwemo kupata taarifa za utafiti zinazohusu sekta ya madini na kuongeza kuwa, sekta hiyo inao uwezo mkubwa wa kutekeleza wajibu wake.

Aidha, Naibu Waziri Doto ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya China kutokana na ushirikiano huo iliyoutoa katika kutekeleza utafiti huo ambao umegarimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 4 na Laki Tano.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia ya China, Profesa Sun Xiaoming (kulia) akitoa taarifa ya utafiti huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Mathias Abisai.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jilojia ya China, Profesa Sun Xiaoming amesema kuwa taarifa ya utafiti iliyowasilishwa ni ya nchi nzima ya Tanzania na eneo la Mkoa wa Mbeya.

Amesema utafiti huo umetoa matokeo ya jiokemia ya element 71 nchini kote na element 39 katika mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa utafiti huo utasaidia katika utekelezaji maendeleo ya shughuli za madini, kilimo na mazingira nchini.

Awali, akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mathias Abisai amesema kusudio la ujumbe huo ilikuwa ni kuhakiki kazi iliyofanyika na kuwasilisha ripoti. Ameongeza kuwa, ripoti hiyo itasaidia kwenye tafiti nyingine za madini ikiwemo maji na mazingira.

Ameongeza kuwa, mnamo Mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Jiolojia zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huo wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013 na kukamilishwa mwaka 2018.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokobeth Myumbilwa akileza malengo ya utafiti huo amesema kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia kwa ajili ya kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa zinazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini, upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbalimbali katika  sekta za kilimo  na mazingira.

Read more

Mafunzo kuhusu mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato (GePG) yatolewa kwa wahasibu wa Madini

Na Rhoda James, Morogoro                                                                                                                                                   

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Tume ya Madini kufuatilia madeni yote ya ada ya mwaka (Annual Rent) na kutoa muda kwa wahusika ili walipe ada hizo na endapo watashindwa kulipa katika muda watakaopewa, wapelekwe Mahakamani.

Naibu Waziri wa Madani, Doto Biteko (kushoto) mara baada ya kusaini kitabu cha wangeni katika Ofisi ya Mratibu wa Chuo cha Mazimbu Campus Solomn Maalangu Dkt. Ibrahimu Mjema mkoani Morogoro.

Naibu Waziri Biteko ameyasema hayo Novemba 12, wakati akifungua mafunzo ya Wahasibu wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaohudhuria mafunzo hayo yanayohusu Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato (Goverment E- Payment Gateway – GePG). Mafunzo hayo yanafanyika  katika chuo cha Mazimbu Campus Solomn Mkoani Morogoro.

“Serikali inadai madeni mengi ya ada za mwaka, mfano kuna mtu moja ana leseni 103 na anaendela kuomba leseni nyingine lakini pia huyo mtu anadaiwa pesa nyingi za ada ya mwaka,” amesema Biteko.

Naibu Waziri Biteko amesisitiza kuwa lengo la mfumo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kupunguza mianya ya upotevu wa mapato kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi zote za Serikali.

Pia, Naibu Waziri Biteko ameongeza kuwa, ili kuleta tija na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, Mfumo wa GePG umeunganishwa na taasisi zinazotoa huduma za fedha kama vile Simu Benking za NMB na CRDB pamoja na Kampuni za Simu ambazo zinatoa huduma kupitia matawi, mawakala na mitandao ya simu lengo likiwa ni kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kutumia mfumo huo.

Akifafanua zaidi, Naibu Waziri Biteko amesema kuwa mafunzo hayo yapo kisheria na yanatokana na kifungu cha 44 cha Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 (The Finance Act, 2017) ambapo Wizara iliunganishwa rasmi kwenye mfumo huo mwezi Septemba, 2017.

Naibu Waziri Madini Biteko ameongeza kuwa, mnamo tarehe 4 Septemba, 2017 Serikali ilitoa Waraka wa Hazina Na. 3 kuhusu kutumia mfumo wa Serikali wa Kielektroniki katika Ukusanyaji wa Mapato lengo likiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuhusu kujengwa kwa mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali.

Wahasimu kutoka Wizara ya Madini nchini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko amewapongeza Wahasibu wote kwa kufanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 310 katika mwaka wa fedha 2018/19 na kueleza kuwa, mpaka kufikia tarehe 31 Oktoba, 2018 jumla ya maduhuli yenye thamani ya shilingi bilioni 111 yamekusanywa ambapo ni asilimia 36 ya lengo ambalo wizara iliwekewa  kwa Mwaka wa Fedha wa 2018/19.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume, Prof. Shukrani Manya amesema kuwa, Mafunzo hayo ni muhimu kwa Tume ya Madini na kwamba yataleta fursa mbalimbali kama vile kujifunza na kuboresha utendaji wa wahasibu katika Tume ya Madini.

Mafunzo kama hayo yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo tarehe 28 hadi 31 Agosti, 2017. Kwa mwaka huu,mafunzo haya yameanza leo Novemba 12 na yanatarajia kukamilika tarehe 15 Novemba, 2018.

Read more

Watalaam wa GST wapokea taarifa ya mradi wa jiokemia kutoka kwa watalaam wa China Geological Survey (CGS)

Na Samwel Mtuwa, GST

Watalaam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological Survey of Tanzania-GST) tarehe 10 Oktoba 2018 walikutana na watalaam kutoka Taasisi ya Jiolojia ya China (Geological Survey of China-CGS) kwa ajili ya uwasilishaji na upokeaji wa taarifa ya mradi wa Utafiti wa Jiokemia katika skeli kubwa na skeli ndogo yaani (Geochemical Mapping for High and Low Density) uliofanyika kwa ushirikiano baina ya Serikali ya China na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa GST, Yokbeth Myumbilwa alisema kuwa, Utafiti huo umekusanya taarifa mbalimbali katika upande wa low density na high density  ambapo kwa upande wa low density utafiti ulifanyika katika   Mikoa  ya Mbeya na Songwe na high density ulifanyika kwa nchi nzima .

Akizungumzia juu ya faida zitokanazo na mradi huu wa ushirikiano , Myumbilwa alieleza baadhi ya malengo ya mradi kuwa ni kupata taarifa za utafiti wa jiokemia  kwa ajili ya  kuandaa kanzidata ambayo itaainisha uwepo wa taarifa za jiokemia  za nchini zitakazo ainisha uwepo wa aina mbalimbali za madini, upangaji miji ,pamoja na taarifa hizo kuweza kutumika katika shughuli mbali mbali ndani ya sekta ya killimo  na mazingira.

Alisema kuwa, faida nyingine ni upatikanaji wa taarifa ambazo  zitasaidia pia kuanisha aina mbalimbali za udongo kwa njia ya Ramani yaani (Geochemical Atlas Map of Tanzania).

Mnamo mwaka 2009 serikali ya China na Tanzania kwa kutumia taasisi zake za Geological Survey zilisaini hati ya makubaliano (MoU) kwa lengo la kuanzisha mradi huu wa miaka mitano ambapo kazi rasmi ya mradi ilianza mwaka 2013mpaka 2018.

Akizungumza wakati wa kufunga hafla hiyo, Myumbilwa alishukuru kwa  mafanikio makubwa ya mradi  huo , pamoja ushirikiano mzuri uliokuwepo wakati wa utekelezaji wa mradi toka ulipoanza mwaka 2013.

Katika hafla hiyo ya upokeaji wa taarifa GST iliwakilishwa na watalaam 11  na upande wa China  CGS uliwakilishwa na watalaam Sita Sun Xiaoming ambaye ni mkurugenzi wa CGS, Sun Kai , Wang Huichu , TengXuegian , Li Janjian , Liu Xiaoyangi na Gong Kenghui.

Read more

Wizara ya Madini, Mkandarasi SUMAJKT wajadili maendeleo ujenzi wa vituo vya umahiri

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe Novemba 8, aliongoza kikao cha kujadili Maendeleo ya Ujenzi wa Vituo vya Umahiri vinavyojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri Stanslaus Nyongo na Doto Biteko pamoja na Menejimenti ya Wizara ambapo Mkandarasi SUMAJKT na Washauri Elekezi kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujezi wa vituo hivyo walieleza kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa za ujenzi wa vituo hivyo.

Mkandarasi SUMAJKT anayejega vituo vya umahiri maeneo mbalimbali nchini na Washauri Elekezi Kampuni za Y&P Architects, InterConsult Architects, Sky Architects zinazosimamia ujenzi wa vituo hivyo wakifuatilia kikao hicho baina yao na Wizara.

Vituo vya umahiri vinajengwa maeneo ya mbalimbali nchini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ulio chini ya wizara.

Vituo hivyo vinalenga katika kutoa mafunzo ya jiolojia katika utafiti wa madini, mafunzo ya uchenjuaji wa madini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira hususan kemikali zisizotumia zebaki.

Vilevile, vinalenga katika kutoa mafunzo ya biashara kwa wachimbaji wadogo wa madini, mafunzo ya usalama na afya sehemu za kazi na mafunzo ya namna bora za utunzaji wa mazingira kwenye migodi ya wachimbaji.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Kairuki alisisitiza kuhusu kuzingatiwa kwa ubora wakati wa  ujenzi wa vituo husika na kusisitiza Mkandarasi SUMAJKT kukamilisha ujenzi huo katika muda uliopangwa.

Vituo vya umahiri viko katika hatua mbalimbali za ujenzi na vinajengwa Bariadi, Bukoba, Handeni, Musoma, Songea, Chunya, Mpanda na Chuo Cha Madini Dodoma.

Ujenzi wa vituo hivyo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 11.9 zinazotokana na mkopo wa Benki ya Dunia.

Read more

Ziara ya Waziri wa Madini yaleta tija kwa STAMICO

Na Bibiana Ndumbaro, STAMICO

Ziara ya Waziri wa Madini Angellah Kairuki (Mb) aliyoifanya tarehe 05.11.2018 katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), imeleta tija, baada ya Waziri kuchangia shilingi milioni 24 ili kuongezea nguvu ya kutekeleza mradi Kokoto wa Shirika hilo; uliopo eneo la Ubenazomozi, mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kushoto) wakisalimiana na mwenyeji wao Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylvester Ghuliku wakati wa ziara ya Waziri katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika zilizopo Barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es Salaam.

Kairuki alitoa mchango huo baada ya kuguswa na tatizo la ukosefu wa mitaji ya kutekeleza miradi, kama lilivyobainishwa katika taarifa ya utendaji kazi ya Shirika hilo iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylvester Ghuliku; kwenye kikao cha pamoja baina ya Waziri, Wafanyakazi na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila.

Fedha hizo zitaiwezesha STAMICO kufikia bajeti yake ya Shilingi milioni 54 zinazohitajika kufanya utafiti wa kijiolojia unaolenga kubaini ubora wa mwamba katika eneo la Chigongwe, ambapo awamu ya kwanza ya mradi wa kokoto wa STAMICO itatekelezwa.

Waziri Kairuki aliwataka Wafanyakazi kukuza ubunifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi, huku akiwataka kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuboresha utendaji kazi wa STAMICO wenye tija kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Waziri huyo wa Madini Kairuki na Katibu Mkuu wake Prof. Msanjila, waliipongeza STAMICO kwa kuweka Menejimenti mpya katika Kampuni yake tanzu ya STAMIGOLD kwani imesaidia kujiendesha kwa faida, kuimarisha ulipaji madeni na kumudu gharama za uendeshaji mgodi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Kanali Mhandisi Sylvester Ghuliku alimshukuru Waziri Kairuki kwa ziara hiyo na ushirikiano anaoutoa kwa STAMICO ili kuhakikisha Shirika linakua kwa kasi na kuleta manufaa mapana kwa Taifa na kwa maendeleo ya Watanzania.

Kanali Mhandisi Ghuliku alimhakikikishia Waziri kuwa STAMICO imedhamiria kuleta mabadiliko katika miradi yake kwa kuboresha miundo mbinu ya miradi, mifumo ya uangalizi na ufuatiliaji na kupunguza gharama za uendeshaji migodi ili kuongeza faida na tija kwa Taifa.

Akitoa neno la shukrani, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa STAMICO Meja Luyodrey Masaki amesema kikao hicho cha pamoja na Mhe. Waziri kimekuwa kichocheo cha uwajibikaji kama Shirika na kwa mtu mmoja mmoja na amemuahidi kuwa STAMICO itarekebisha mapungufu yake na kutoa maoni ya maboresho Wizarani, ili kuleta tija kwa Shirika.

Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya STAMICO na Wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipotembelea Shirika la Madini la Taifa, tarehe 5 Novemba 2018 katika ofisi za Makao Makuu ya STAMICO zilizopo barabara ya Umoja wa Mataifa, Upanga jijini Dar es Salaam na kufanya kikao nao.

Meja Masaki alimshukuru Kairuki kwa mchango wake wa Shilingi milioni 24 ambazo zitasadia kutekeleza mradi wa kokoto wa Ubenazomozi, na hivyo kuwezesha kukidhi mahitaji ya kokoto katika miradi ya  miundombinu ya barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege, sambamba na majengo ya biashahara, ofisi na makazi.

Mapema mwezi huu Novemba, Waziri huyo wa Madini aliitembelea STAMICO ikiwa ni ziara yake ya pili kwa mwaka 2018; iliyolenga kufuatilia utendaji kazi wa Shirika, changamoto zake, mbinu utatuzi na mwelekeo wa uendeshaji Shirika kwa kasi itakayoleta matokeo chanya nchini.

Read more

Taarifa kwa Umma-Ushiriki wa GST katika mashindano ya remote sensing kutoka Nchi za SADC trh 29 Oktoba-02 November, 2018

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Remote Sensing yaliyoshirikisha nchi za kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) chini ya udhamini wa taasisi ya Japan Oil,Gas and Metals Extraction Corporation (JOGMEC) ya nchini Japani. JOGMEC ni taasisi ambayo ipo kwenye serikali ya Japan ambapo wameweka kituo cha Remote Sensing nchini Botswana kwa ajili ya mafunzo na mashindano ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC). Mashindano hayo kwa mwaka huu wa 2018 yalishirikisha nchi kumi na tatu ambazo ni Zimbabwe, Tanzania, Msumbiji, Angola, Zambia, Botswana, Malawi, Lesotho, Eswatini, Afrika Kusini, DR. Congo, Madagascar na Nambia.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Wachimbaji Wadogo watakiwa kuhakikisha leseni kutokuwa chanzo cha migogoro

Na Rhoda James, Bukombe

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo nchini kuhakikisha kuwa leseni za uchimbaji Madini zinazotolewa na Wizara kupitia Tume ya Madini ikiwemo mikataba ya ubia wanayongia na Kampuni mbalimbali kutokuwa chanzo cha migogoro nchini.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum Othman (hawapo pichani) katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda.

Naibu Waziri Biteko aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akisuluhisha mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining Ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum Othman ambaye aliilalamikia kampuni hiyo kwa kukiuka mkataba waliojiwekea kati yao.

Akizungumza katika kikao hicho cha usuluhishi, Naibu Waziri Biteko alisema kuwa, wachimbaji wadogo wanapoingia mikataba na kampuni yoyote ile yenye nia ya kuwa na ubia na Mzawa  ni lazima  wazingatie  na kukubaliana juu ya mikataba wanayoingia  kwa kuwa, pindi  taratibu zinapokiukwa zinaichafua nchi.

“Mikataba hii mnayoingia mjue ya kuwa nyinyi mnakuwa ni taswira ya nchi sasa mkikiuka mnakuwa mnaichafua nchi yetu, lazima mzingatie makubaliano mnayojiwekea nyie wote, mwekezaji na mzawa,” alisema Biteko.

Aidha, aliainisha baadhi ya masuala ambayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuingia mikataba na wabia  na kueleza kuwa ni pamoja na kuangalia uhai wa leseni zao, kusajili mikataba yao kwenye Tume ya Madini, kuhakikisha kuwa eneo au biashara wanayoingia haina migogoro, wazawa kujua kuwa wanatakiwa kuwa na asilimia angalau zisizopungua 25 na kuhakikisha kuwa kodi zote za serikali zinalipwa kwa wakati.

Vilevile, Naibu Waziri Biteko alimtaka, Othman ambaye ni mlalamikaji kuhusu ukiukwaji wa mkataba kati yake na Kampuni ya Pamoja Mining Ltd kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria zote ili pande zote mbili ziweze kufanya kazi  kwa tija na bila kukwepa kodi za serikali.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa kwanza kulia mbele) akisikiliza mgogoro uliokuwepo kati ya Kampuni ya Pamoja Mining ltd na Mkazi wa Nyarugusu Salum katika Ofisi ya Halmashauri ya Bukombe. Wengine katika picha ni Wafanyakazi kutoka Ofisi ya Madini Geita na kampuni ya Pamoja Mining Ltd.

Pia, alitumia fursa hiyo kuzitaka Ofisi za Madini kote nchini kuhakikisha kuwa zinaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili matatizo kama hayo yanayojitokeza sasa yasiendele kujitokeza kwani ni wajibu wa Wizara kuhakikisha kuwa migogoro baina ya wachimbaji  na wawekezaji inakwisha.

Naye, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda alimshukuru Naibu Waziri Biteko kwa kusuluhisha mgogoro huo ambao umedumu kwa kipindi kirefu nakueleza kuwa, ofisi hiyo itaendelea kuzingatia na kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa sheria.

Read more

Biteko kutatua mgogoro baina ya Kijiji cha Ngula na mmiliki wa eneo la uchimbaji wa madini ya dhahabu wa Nyati Resource

Na Rhoda James, Geita

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza mgodi wa Nyati Resources ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita kutolipa gawio Serikali ya kijiji cha Ngula kuanzia tarehe 2 Novemba, 2018 ili kutoa nafasi ya uchunguzi kujua ni nani mmiliki halisi wa eneo hilo la mgodi.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akihutubia wananchi wa kijiji cha Ngula na wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa Nyati Resources Ltd (hawapo pichani) katika mkoa wa Geita tarehe 2 Novemba, 2018

Ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 2 hadi 3 Novemba, 2018 iliyolenga  kukagua machimbo ya madini katika Mkoa wa Geita.

Pamoja na ukaguzi huo, Biteko ameeleza kuwa, ametembelea machimbo hayo ili kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina ya Kijiji cha Ngula na mkazi wa kijiji hicho Mindi Masasi.

Akizungumza katika kikao hicho, Biteko ameutaka Mgodi huo wa Nyati Resources ltd kutolipa gawio kwa kijiji hicho kwa kuwa kuna malalamiko kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho ambaye ni Mindi Masasi.

Biteko ameeleza kuwa mgodi huo umeanza uzalishaji tangu Desemba, 2017 na umekuwa ukimlipa Mindi Masasi gawio kwa zaidi ya mwaka kwa kuwa wakati wanaanza uzalishaji wa dhahabu wamemkuta katika ardhi hiyo ambayo amekuwa akiishi tangu mwaka 1954 lakini sasa kijiji kinadai kuwa ardhi hiyo ni mali yao na wao ndio wenye haki ya kulipwa gawio hiyo.

Pamoja na maswali mengi yanayojitokeza, Biteko amesema ni vyema tuachie mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusiana na suala hili “Zaidi ya mwaka Masasi amekuwa akilipwa gawio na mgodi huu, je serikali ya kijiji cha Ngula ilikuwa wapi, mbona serikali ya kijiji haizungumzii eneo lingine isipokuwa eneo la mgodi,” aliuliza Biteko.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngula mara baada ya kukagua Mgodi wa Nyati Resources Ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita.

Wakati huo huo Biteko ameutaka Mgodi wa Nyati Resources ltd kutoa maelezo ni kwa nini tangu mwaka 2017 Desemba walipoanza uzalishaji wa dhahabu wamelipa Mrabaha wa kiasi cha Shilingi 200,000/- tu wakati mapato yao ni zaidi ya  milioni 50.

“Huo ni ukiukwaji wa ulipaji wa kodi za Serikali, haiwezekani tangu mwaka jana hadi leo mmefanikiwa kulipa Mrabaha wa laki mbili tu,” alisema Biteko.

Aliongeza kuwa lazima wazawa kuonesha mfano mzuri wa kulipa kodi ili hata wawekezaji kutoka nje ya nchi wakija waone umuhimu wa kulipa kodi.

Kwa upande wake Meneja wa Mgodi wa Nyati Resource ltd, Christopher Nilla amekiri kuwa kweli kumekuwepo na mapungufu katika ulipaji wa kodi za Serikali lakini na kuahidi kubadilika na kulipa sawasawa na sheria ya madini na kubainisha kuwa  wanamiliki mgodi mwingine ambapo zaidi ya Tsh milioni kumi zimelipwa serikalini.

Read more

Biteko azitaka halmashauri za Wilaya kuwalea wawekezaji wa madini

Nuru Mwasampeta, Pwani

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kushirikiana na kampuni ya Rack Kaloin inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya kaolin wilayani humo kwani imeonesha uzalendo kwa kulipa mirabaha ya serikali inavyopaswa pamojana kuwa na ushirikiano mzuri na jamii inayouzunguka mgodi huo sawasawa na taratibu na sheria ya madini inavyoeleza.

Ametoawito huo tarehe 22 mwezi Oktoba alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani wilayani Kisarawe baada ya kutembelea eneo la machimbo ya mgodi huo na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Adam Ng’imba.

Akielezea dhumuni la ziara hiyo, Biteko alisema ni kukagua shughuli za uchimbaji zinazoendelea pamojana kujiridhisha na suala zima la utunzwaji wa kumbukumbu za uchimbaji nauuzwaji wa madini hayo utakaopelekea Serikali kulipwa kodi stahiki inayotoka na na faida inayopatikana kutokana na uchimbaji na biashara ya madini.

Akizungumzia suala zima la ulipwaji wa mirabaha ya uchimbaji, Biteko alisema mwekezaji anapaswa kulipa kodi hiyo kutokana na kiasi alichokiuza kwenye soko hiyo ikiwa ni pamoja na gharama za usafirishaji kutoka sehemu za machimbo mpaka soko lilipo.

Amesema, awali wawekezaji wa madini walikuwa wakilipa mrabaha kwa gharama ya eneo la machimbo ambapo madini hayo yanaposafirishwa ndipo dhamani yake inaongezeka na kuuzwa kwa gharama ya juu hivyo walikuwa wakiibia Serikali kiasi kikubwa cha pesa.

Aidha, Biteko amekiri kuwa jukumu la kutoa elimu kwa wawekezaji wasiojua taratibu na sheria za kufanya biashara hiyo ni yake baada ya mnunuzi wa madini hayo kubainika kutokuwa na elimu ya kutosha ya kufanya biashara hiyo. “Najua hujui taratibu za kufanya biashara hii, nitakuelimisha kwani hili ni moja kati ya majukumu yangu” alisema.

Akielezea moja ya taratibu anazopaswa kuzifuata mchimbaji au msafirishaji wa madini, Biteko alisema anapaswa kuwa na aidha leseni ya uuzaji wa madini (Dealer licence) au kuwa na leseni ya uchimbaji au zote mbili kwa pamoja.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rack Kaloin alisema wanaendelea vizuri na kazi za kila siku na kwamba watafanya mazungumzo na wanakijiji ili kuona namna watakavyonufaika moja kwa moja kutokana na uchimbaji huo baada ya kupeleka pesa serikali zamita aambazo matokeo yake kwa wanakijiji wanaozunguka mgodi huo hayaonekani.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwambapa amemshukuru Biteko kwa kutembelea Wilaya hiyo na kwa maelekezo aliyoyatoa na kuahidi kuwa halmashauri yake itaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali za sekta ya madini ili waweze kuwa na uzalishaji mzuri na wenye tija kwa wawekezaji na serikali kwa ujumla.

Akikamilisha ziara hiyo Biteko alitoa wito kwa wachimbaji wadogo na wanakisarawe kwa kusema waendelee kushirikiana na ofisi za madini kwani kazi ya Serikali ni kuwafanya wachimbaji hao kukua na kuwa na uchmbaji wenye tija. “Kazi yetu sisi kazi yetu ni kuwalea wao waweze kuchimba kwa kufuata sheria lakini zaidi sana kuwafanya wawe wachimbaji wanaokua kutoka uchimbaji mdogo, wa kati na baadaye kuwa wachimbaji wakubwa.”

Aidha, alitoa wito kwa halmashauri ya Kisarawe kisarawe kuwapa ushirikiano wa kutosha wachimbaji na kwamba wawalee na wao kwani hakuna sababu yoyote ya kuwa na migogoro kila mahali lakini pia wachimbaji wasiwanyonge wala kuwanyonya wanakisarawe isipokuwa wazingatie taratibu zilizowekwa.

Read more

FEMATA watakiwa kuboresha sekta ya Wachimbaji Wadogo Nchini-Kairuki

Na Rhoda James, Dodoma

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameagiza Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA) kuhakikisha kuwa wanakuja na Mikakati ya pamoja ya kuboresha utendaji kazi katika Sekta ya wachimbaji wadogo na kuweka mfumo bora wa kulipa Kodi za Serikali.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki akihutubia Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini mbalimbali (hawapo pichani) jijini Dodoma alipokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa FEMATA jijini Dodoma tarehe 30 Oktoba, 2018.

Waziri Kairuki, ameyasema haya jana tarehe 30 Oktoba, 2018 alipokuwa akifunga Mkutano Mkuu wa Uchanguzi wa Viongozi wa  FEMATA uliofanyika katika Hoteli ya Afrikan Dreams jijini Dodoma.

Kairuki amesema kuwa, Ukilinganisha wachimbaji wakubwa kwa wadogo nchini, wakubwa ni asilimia nne tu wakati wachimbaji wadogo ni asilimia 96 lakini ukitazama mchango wao kwa Pato la Taifa ni kinyume chake.

“Tunataka FEMATA mshiriki kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanachangia kikamilifu katika Pato la Taifa,” alisema Kairuki.

Akizungumza katika Mkutano huo, Kairuki aliwataka wajumbe wote kutumia vyema furasa hiyo katika kujadili na kupanga mikakati itakayotekelezwa na kuimarisha Vyama vya wachimbaji wadogo Kimkoa (REMAS), FEMATA na hatimaye kuimarisha wachimbaji wadogo wa madini nchini.

Aidha, Waziri Kairuki amewapongeza FEMATA kwa kuandaa mkutano huo na kwa kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Madini na kuhaidi kuwa atafanya kazi kwa karibu zaidi nao na nimatumaini yake kuwa ifikapo 2025 Sekta ya Madini itachangia ailimia isiyopungua10 ukilinganisha na mchango wa sasa ambao ni asilimia 4.8 kwa Pato la Taifa.

Akitoa pongezi kwa Uongozi wa FEMATA, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge alieleza kuwa ni matumaini yake kuwa wachimbaji na Wafanyabiashara wa madini wataendelea kulipa kodi zote serikalini kama inavyotakiwa.

Kwa upande wake, Rais wa Wachimbaji wa madini nchini John Bina amesema kuwa, atasimamia kikamilifu ulipaji kodi, uchimbaji salama na endelevu kupitia FEMATA.

Waliohudhuria mkutano huo ni Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Manaibu mawaziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko, Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ikiwa ni pamoja na Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi (OSHA), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki Kuu (BOT) pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji na Wafanyabiashara wa madini.

Read more

Biteko azitaka mamlaka za serikali kufanya kazi kwa pamoja

Na Nuru Mwasampeta,

Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko amezitaka halmashauri za wilaya kufanya kazi na wizara ili kuweza kutatua changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao kabla hazijasababisha madhara makubwa kwa jamii.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa mgodi wa uchimbaji wa madini ya mchanga akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko(wa pili kulia) alipotembelea mgodi huo

Aliyasema hayo mwanzoni mwa wiki alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga alipofika ili kukagua shughuli za uchimbaji wa mchanga unavyoendelea pamoja na kukagua namna ya ulipwaji wa mirabaha ya Serikali inavyofanyika.

Akizungumza katika kikao baina yake na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Hassan Sanga, Biteko alisema “Sisi ni wamoja hivyo tufanye kazi kwa pamoja, tunajifunza pamoja ili tuamue kwa pamoja”.

“Tunatamani mambo mengi yaishie huku chini lakini endapo kuna masuala yanahitaji msukumo wa wizara ninyi mtueleze” alisistiza Biteko.

Aidha, Biteko aliwataka viongozi wa wilaya ya Mkuranga kuhakikisha tozo zinazotozwa na halmashauri hiyo ziwe ni zile zinazokubalika kisheria ili kupunguza migogoro midogomidogo baina ya Serikali na wachimbaji lakini pia kuwasaidia wachimbaji ili waweze kukua na kuongeza kipato chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga alibainisha uwepo wa utoaji wa leseni bila ofisi yake kushirikishwa na hivyo kuwawia ugumu pindi wanapotakiwa kuchukua hatua za kuzuia eneo husika kufanyika shughuli za uchimbaji. “Mchanga unachimbwa kiholela ukiuliza wanasema wanavibali kutoka wizara ya ardhi, madini lakini pia wana vibali kutoka Nemc, tunashindwa kuwachukulia hatua.

Akizungumzia suala hilo Biteko alisema, mmiliki yeyote wa leseni ya madini hatakiwi kuanza kazi pasipo kutoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ambaye atapaswa kukutambulisha katia ngazi zote mpaka katika uongozi wa kijiji leseni yako.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akitembea kuelekea eneo ambako uchimbaji wa mchanga unafanyika.

Aidha aibainisha kuwa maeneo ya jeshi, vyanzo vya maji, maeneo ya hifadhi hayaruhusiwi kutolewa leseni lakini pia aliwataka viongozi hao wa wilaya kusema maeneo wanayodhani hayapaswi kutolewa leseni na kwamba wizara itatii kwa kutokutoa leseni kwa maeneo hayo.

Pia alielezea mamlaka ya wilaya kuwa inauwezo wa kuomba leseni zote zilizoombwa kwa kipindi Fulani ili kujiridhisha kama maeneo hayo yanaweza endeleza shughuli za uchimbaji na kama ni vinginevyo leseni zinafutwa.

Pamoja na hayo, Biteko aliutaka uongozi wa wilaya kuwalea  wachimbaji na kuondokana na urasimu usiokuwa na sababu, “tuwahurumie watu, Urasimu usiokuwa na sababu sisi wizara ya madini tunasema hapana.” Alisema Biteko.

Biteko alitanaibisha kuwa, wawekezaji wanatumia pesa nyingi kuwekeza kwenye uchimbaji na wengine wana mikopo katika mabenki hawalali vizuri hivyo tuwasaidie ili waweze kufanya kazi zao kwa utulivu na kupata kile wanachotarajia.

Read more

Ujenzi wa Mgodi wa mfano Lwamgasa wafikia asilimia 80

Na Asteria Muhozya,

Wizara ya Madini imeanza kukutana na Kamati Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 29 Oktoba hadi Novemba 1, 2018.

Katika kikao cha leo Wizara imewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Akiwasilisha Taarifa kuhusu Ujenzi wa Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa,  Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal amesema hadi kufikia mwezi Septemba,2018, kazi ya ujenzi wa mgodi na usimikaji wa mitambo ya uchenjuaji imekamilika kwa asilimia 80.

Kuhusu mradi wa One Stop Center, eneo la Mirerani, amesema uko kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi  na kuongeza kuwa,   jengo hilo litakapokamilika litakuwa na miundombinu  mbalimbali ikiwemo huduma za Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini, Uhifadhi wa madini kwa usalama  , Kodi na tozo mbalimbali ikiwemo ofisi za TRA, Huduma za kifedha, ikiwemo Benki na Ofisi za Benki kuu, Huduma za tathmini na uthamini madini, Ofisi za Madini na Chumba maalum cha kufanyia minada ya madini.

Read more

Hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb.), akizindua Kamati ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia nchini

Mheshimiwa Stanslaus Nyongo (Mb.), Naibu Waziri, Wizara ya Madini;

Prof. Simon Msanjila, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini;

Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati;

Ndugu Ludovick Utouh, Mwenyekiti Kamati ya TEITI;

Wajumbe wa Kamati ya TEITI;

Sekretarieti ya TEITI;

Waandishi wa Habari;

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote ninapenda kuanza kwa kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutujaalia kukutana siku ya leo katika uzinduzi wa Kamati ya TEITI. Kamati ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia nchini Tanzania kwa kipindi cha Oktoba 2016 – Oktoba 2019. Ninakushuru ndugu Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI kwa kunialika kujumuika nanyi katika tukio hili muhimu ambalo ni kielelezo na nyenzo ya kufanikisha kuboresha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya uziduaji hapa nchini. Kama mnavyofahamu, mwaka 2009 Nchi yetu ilijiunga katika mpango wa kimataifa wa kuhamasisha uwazi na uwajibikaji katika sekta ya Uchimbaji wa Rasilimali (Extractive Industries Transparency Initiative) lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha kwamba mapato yanayotakiwa kulipwa Serikalini kutoka Sekta ya uziduaji yanapatikana na kuwekwa wazi kwa wananchi. Msingi wa falsafa hii ya uwazi na uwajibikaji kwenye Sekta ya uziduaji umejikita kwenye Ibara ya 8 (1) (c) na Ibara 27 (1) & (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Ibara hizi zinazungumzia Serikali kuwajibika kwa wananchi wake na kwamba rasilimali zote za nchi zitatunzwa na wananchi wote kwa manufaa ya wote. Aidha, Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia Tanzania ya mwaka 2015 nayo imeweka msingi imara wa kuhakikisha kunakuwa na uwazi na uwajibikaji kwenye Sekta ya uziduaji Nchini. Hivyo, Kamati hii ninayoizindua leo hii ina umuhimu mkubwa kwa mustakabali ya maendeleo ya Taifa letu iwapo mtatekeleza majukumu yenu kwa weledi, uzalendo na kwa kuipenda nchi yenu. Ni matarajio yangu na matarajio ya kila mwenye kuitakia mema Nchi yetu, mnakwenda kutekeleza wajibu wenu ipasavyo kwa maslahi mapana ya Nchi yenu kwani Taifa limewaamini hivyo msiliangushe.

Ndugu Mwenyekiti na ndugu Wajumbe wa Kamati, Itakumbukwa kuwa, tangu TEITI ianzishwe Mwaka 2009 hii ni Kamati ya tatu. Kamati mbili za awali ziliongozwa na Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mark Bomani. Ninayo faraja kubwa ya kuishuhudia siku hii na kushiriki tukio la leo nikiwa Waziri wa Madini. Ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuniteua mimi kwenye wadhifa huu na kwa kukuteua wewe Bw. Ludovick Utouh Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Mstaafu) kuiongoza Kamati ya tatu ya TEITI. Maamuzi ya Mheshimiwa Rais kumteua Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI ni maamuzi ya kimapinduzi katika kuboresha usimamizi wa rasilimali nchini ilizo nazo katika Sekta ya uziduaji na kuhakikisha kuwa manufaa yanayopatikana kutokana na rasilimali hizi yananufaisha Watanzania wote na kuleta maendeleo kwa nchi. Uteuzi wa Mwenyekiti umezingatia uwezo wake wa uongozi na kubeba dhamana hii kwa kushirikiana na wajumbe kumi na tano kutoka Serikalini, Kampuni za madini, mafuta na gesi asilia na Taasisi za Kiraia. Ni matumaini yangu utaendeleza kazi nzuri ulizokwishafanya huko nyuma katika kuiongoza Kamati hii. Aidha, kwa upande wenu wajumbe wa Kamati hii mlioteuliwa, tunaamini mnao uwezo na weledi wa kuifanya kazi hii. Vile vile tunaamini mna nafasi kubwa ya kuisaidia Serikali katika agenda yake ya kuboresha Sekta hii muhimu kwa kuainisha njia za kuboresha usimamizi wa Sekta ya uzuduaji, kuvutia wawekezaji, kuongeza pato la Taifa na kujenga imani kwa wadau wa sekta hii. Katekelezeni majukumu yenu kwa maslahi ya Nchi yenu.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Hotuba ya Waziri wa Madini Mheshimiwa Angellah J. Kairuki (Mb.) akifungua jukwaa la sekta ya uziduaji Tanzania, lililoandaliwa na hakirasilimali

Waandaaji wa Jukwaa la Sekta ya Uziduaji Tanzania 2018;

Watoa mada kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania;

Wawakilishi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Fedha;

Madhehebu ya Dini (BAKWATA, CCT and TEC);

Wawakilishi wa Mashirika ya Vyama na Asasi za Kijamii;

Washirika wa Kimaendeleo;

Waandishi wa Habari;

Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana.

Habarini za asubuhi na Karibuni katika Jiji la Dodoma.

Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kukutana siku ya leo katika ufunguzi wa Jukwaa la Sekta ya Uziduaji Tanzania ambalo limewaleta pamoja wadau mbalimbali kutoka nyanja zote ndani na nje ya Tanzania, kwa kusudi la kujadili, kujifunza na kushirikishana uzoefu katika utetezi na ushawishi wa michakato ya maamuzi yatokanayo na sekta ya uziduaji ili kuleta maendeleo endelevu yanayotarajiwa na sekta hii kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla. Jukwaa hili limeandaliwa wakati muafaka kwani katika kipindi hiki, tumefanya mageuzi makubwa nchini na tunaendelea na mageuzi mbalimbali lengo ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na hivyo kulazimika kuweka mkazo katika kuihuisha sekta ya uziduaji na ajenda ya viwanda kwa ifikapo mwaka 2025.

Ndugu Washiriki, Usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia ni chachu ya maendeleo ya Tanzania. Mabadiliko ya Sera, Sheria, Taratibu na Kanuni yamefanyika kuinua uzalendo, kurudisha uhuru wa umiliki na usimamizi wa rasilimali za nchi.

Ndugu Washiriki, Nachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuonesha uzalendo katika kusimamia rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania. Hii imejidhihirisha kupitia Serikali kuendesha majadiliano na kampuni za uchimbaji madini ili kuhakikisha Tanzania inanufaika kupitia rasilimali zake lakini pia kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini.

Sekta ya uziduaji nchini inatarajiwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu, hususan kutokana na ongezeko kubwa la uwekezaji. Hivyo, upo umuhimu wa kuendelea kupanua wigo wa majadiliano na kusimamia rasilimali kwani kama ambavyo Mheshimiwa Rais anasisitiza mara kwa mara kuwa uzoefu katika nchi nyingine unaonesha rasilimali hizi zinaweza kugeuka na kuwa laana itakayoharibu na kudunisha matokeo ya maendeleo na kuleta umasikini mkubwa.

Ndugu Washiriki, Ni muhimu kwa Tanzania kuweka zana thabiti ili kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji na usimamizi endelevu wa sekta za madini, mafuta na gesi asilia. Hii inajumuisha kuwepo kwa ufanisi wa ushirikishwaji wa wadau kutoka nyanja mbalimbali zikiwemo ASASI ZA KIRAIA.

Sisi kama Serikali, kupitia Wizara zote mbili ya Madini na ya Nishati, jukumu letu kubwa ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kusimamia utendaji kazi kwenye sekta ya uziduaji kwa kuzingatia kikamilifu utekelezaji wa Sera, Sheria na mahitaji ya udhibiti wa kitaifa na kimataifa. Lakini pia, kuendelea kushirikiana na wadau ili kuweza kuishauri Serikali njia sahihi zitakazoiwezesha Nchi kunufaika na rasilimali hizi. Mbali na hayo, kuwa na jitihada za kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia na makundi maalum yanapata fursa kushiriki kikamilifu katika Sekta ya uziduaji.

>>Soma Zaidi>>

Read more

FEMATA kuimarisha sekta ya madini kupitia kodi

Na Greyson Mwase, Dodoma

Mtendaji Mkuu wa  Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa  Madini Nchini (FEMATA) na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Haroun Kinega amesema kuwa, shirikisho hilo kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Madini limeweka mikakati katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wanakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini kupitia kodi na tozo mbalimbali.

Sehemu ya wajumbe wa meza kuu wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini (FEMATA) na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Haroun Kinega (hayupo pichani).

Kinega ameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba, 2018 katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa FEMATA Nchini uliofanyika jijini Dodoma wenye lengo la kuchagua viongozi wapya pamoja na kujadili changemoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwenye shughuli za uchimbaji wa madini nchini.

Akielezea mikakati ya ongezeko la mapato kutokana na kodi zinazolipwa na wachimbaji wadogo wa madini, Kinega alisema kuwa FEMATA kwa kushirikiana na Tume ya Madini imeweka mikakati ya kuhakikisha maeneo zaidi yanatengwa na kutolewa leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini na kuwataka wachimbaji wadogo wa madini kuunda vikundi, kusajili ili kuomba leseni na uchimbaji wao kuwa rasmi.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya wachimbaji wadogo wa madini nchini wanakuwa rasmi kwa kupatiwa leseni za madini ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali, ninaamini tunaweza kufikia lengo kupitia mikakati tuliyojiwekea.

Wakati huo huo akielezea mikakati ya Serikali katika kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini,  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma,  Jonas Mwano alisema kuwa mbali na Serikali kupitia Wizara ya Madini kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini, elimu imekuwa ikitolewa kwa wachimbaji wadogo kuhusu sheria na kanuni za uchimbaji wa madini pamoja na usalama migodini.

Alisema kuwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa kwa  wachimbaji wadogo wa madini imepunguza kwa kiasi kikubwa migogoro iliyokuwa ikijitokeza kwenye maeneo yao ya uchimbaji wa madini.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa  Madini Nchini (FEMATA), John Bina mbali na kupongeza juhudi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Madini  aliiomba Serikali kuhamasisha wawekezaji kutoka nje kwa ajili ya kujenga mitambo ya kuchenjulia madini nchini na kukuza pato la taifa.

Sehemu ya wawakilishi wa vyama vya wachimbaji wadogo wa madini mikoani wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Nchini (FEMATA), John Bina (hayupo pichani).

Katika uchaguzi huo wa viongozi wa FEMATA nafasi zinazogombewa ni pamoja na Rais, Makamu wa Rais,  Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mweka Hazina, Mweka Hazina Msaidizi, Mwakilishi  wa Wanawake na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Dhahabu.

Nafasi nyingine ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Nishati, Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Viwanda, Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Chumvi, Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Tanzanite, Mwenyekiti wa Kamati ya Madini ya Almas, Mwenyekiti wa Kamati ya Madini Mengine ya Vito na  Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Usuluhishi na Kanuni.

Aidha, Nafasi nyingine ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Mjumbe wa Afya, Mazingira na Usalama Migodini, Mwakilishi wa Wafanyabiashara, Mwakilishi wa Wachimbaji Wasio Rasmi, Mjumbe wa Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Gesi na Mafuta (TEITI) na Bodi ya Wadhamini nafasi tano.

Read more

Naibu Waziri Nyongo afanya ziara katika Migodi ya makaa ya mawe ya Kabulo na Kiwira

Na Greyson Mwase,

Tarehe 19 Oktoba, 2018 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo alifanya ziara katika Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kabulo (Kabulo Coal Mine) uliopo katika eneo la Kabulo lililopo katika wilaya Songwe mkoani Songwe na Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira (Kiwira Coal Mine) iliopo katika Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya. Mara baada ya kufanya ziara katika migodi husika, alizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Akizungumza katika mkutano wa wafanyakazi alisema kuwa, kwa sasa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kutoka Kabulo hadi Kiwira itakayotumika kwa ajili ya usafirishaji wa makaa ya mawe pamoja na kuhakikisha inalipa stahili za wafanyakazi mara baada ya taratibu kukamilika. Katika hatua nyingine, Nyongo aliwataka watumishi kufanya kazi kwa ubunifu na kusisitiza kuwa Wizara ya Madini itahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri.

Wafanyakazi wa Mgodi wa Kiwira walimpongeza Naibu Waziri Nyongo kwa kazi kubwa ya kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini nchini pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Wizara.

Read more

Tanzania, DRC zaanza mazungumzo ujenzi wa kinu/kiwanda cha kuchenjua Colbat

Asteria Muhozya na Rhoda James, Geita 

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeanza kufanya mazungumzo na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili iweze kujenga Kiwanda cha Kuchenjua madini ya Colbat nchini.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na mgeni wake Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu pamoja na ujumbe walioambatana nao wa Mkoa wa Shinyanga wakiangalia namna shughuli mbalimbali za uzalishaji wa madini ya Almasi katika Mgodi wa Almasi Mwadui (WDL) zinavyofanyika.

Hayo yalibainishwa Oktoba 19, mkoani Geita  na Waziri wa Madini wa Tanzania Angellah Kairuki wakati wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya  Waziri wa Madini wa Kongo (DRC), Martin Kabwelulu aliyoifanya nchini kwa mwaliko wa Waziri Kairuki.

Kairuki alisema kuwa, nchi ya Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat duniani ambapo asilimia 70 ya madini hayo duniani yanazalishwa nchini humo.

Aliongeza kuwa, kwa sasa nchi hiyo inayo changamoto ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi ikiwemo ukosefu wa umeme wa kutosheleza kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.

“Tumekubaliana kuendelea na mazungumzo  na Kongo ili shughuli za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini hayo ufanyike nchini  kwa kuwa tumeshaanza kuwekeza kwenye Vinu/viwanda  vya Kuchenjua na kuyeyusha madini mbalimbali. Hivyo, tunataka wayasafirishe makinikia ya Colbat hapa na tuyachenjue hapa,” alisisitiza Kairuki.

Akizungumzia matumizi ya madini hayo, Kairuki alisema kuwa, madini ya Colbat yanatumika kutengeneza betri na vihifadhi nishati (capacitor) ambazo zinahitajika sana hususan, kwenye magari yanayotumia umeme.

Mbali na makubaliano ya ujenzi wa kiwanda hicho, pia Waziri Kairuki alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana masuala kadhaa ikiwemo kuendelea kubadilishana uzoefu wa usimamizi wa sekta ya Madini ili kuweza kunufaisha wananchi hasa wale wanaozunguka maeneo ya migodi.

“Nchi ya Kongo DRC imefurahishwa na hatua za Mkoa wa Geita kwenye usimamizi wa mapato yatokanayo na madini pia mchango wa migodi kwa maendeleo ya wananchi wanaozunguka mgodi,”alisema Kairuki.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Waziri wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Martin Kabwelulu, wakimsikiliza Mtaalam kutoka Mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) wakati akiwaeleza namna shughuli za uchimbaji wa madini hayo zinavyofanyika.

Vilevile, alisema kuwa nchi hizo zimekubaliana kuboresha mahusianao ya kimkakati ambapo Kongo imeahidi kuiunga Mkono Tanzania katika masuala ya Mashtaka dhidi ya makampuni za uwekezaji.

Pia, alisema Kongo imeahidi kukitumia Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu sekta ya madini yanayotolewa kituoni hapo;

“Kongo imepanga kuja kujifunza mfumo mpya wa utoaji wa leseni za madini (cadaster) ambao umebuniwa na kusanifiwa na watanzania,” alisema Kairuki.

Kairuki aliongeza kuwa, nchi hizo zimekubaliana kuendelea kuboresha mifumo ya udhibiti utoroshaji wa madini yanayotoka Kongo na Tanzania kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Aidha, Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa Kongo wenye nia ya kuwekeza nchini kwenye migodi, viwanda vya uchenjuaji, uongezaji thamani madini (ukataji, unga’rishaji).

“Lakini pia tumewakaribisha kutumia bandari yetu kupitisha madini yao pamoja na kukubaliana kuwa na Mining Forum kati ya nchi hizi mbili tu ukiachia Forum nyingine ambazo tumelenga kuziandaa na kushirikisha wadau kutoka nchi mbalimbali,” alisema Kairuki.

Aidha,  alisema nchi hiyo imeahidi kurudi nchini  katika kipindi kifupi kijacho kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu namna Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)  inavyofanya kazi zake za utafiti na maabara.

Kwa upande wake, Waziri wa DRC, Martin Kabwelulu alisema atawatuma Wataalam wake kurudi nchini kwa ajili ya kujifunza mfumo mpya wa utoaji wa leseni za madini (cadaster) wa Tanzania na kuongeza ni mfumo mzuri ambao utaliwezesha taifa hilo kusimamia vema rasilimali madini na kuhakikisha kwamba zinawanuifaisha wananchi wake.

Sehemu ya mitambo mbalimbali katika Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa. Mgodi huo umejengwa na Wizara ya Madini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) kwa lengo la kutoa elimu ya uchimbaji wenye tija kwa wachimbaji wadogo, kutoa huduma na elimu kuhusu uchenjuaji sahihi wa dhahabu. Mgodi huo umejengwa mkoani Geita.

Pia, alisema kuwa nchi hiyo inao ukosefu wa umeme wa kutosha jambo ambalo linafanya nchi hiyo kusafirisha madini hayo nje yakiwa ghafi ikiwemo madini ya Colbat na dhahabu na kuongeza kuwa, Rais wa nchi  hiyo, Joseph Kabila katika ujumbe wake amemweleza kuwa, anataka madini yote ya Kongo yasafirishwe kupitia Tanzania.

“Tunataka tusafirishe madini yetu kupitia bandari ya Tanzania. Lakini pia nimeona njia ya kupitishia madini yetu kupitia reli ya Kati ya Kigoma –Dar es Salaam ni fupi sana,” alisema Kabwelulu.

Akizungumzia mabadiliko ya Sheria ya Madini yaliyofanywa nchini humo hivi karibuni, alisema nchi hiyo iliamua kubadili sheria yake kutokana na kutokunufaika kabisa na rasilimali hiyo hususan kwa wananchi wanaozungukwa na  rasilimali hizo na kuongeza kuwa, sheria ya sasa inapigania zaidi maslahi ya nchi na wananchi wake.

“Nafurahi nimepokelewa vizuri sana Tanzania, nimejifunza mengi kweli hii ni nchi rafiki. Sisi tunao uzoefu wa miaka mingi kwenye sekta hii lakini bado hatujanufaika kabisa,” alisema Kabwelulu.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi alisema kuwa, amemwomba Waziri wa Madini wa Kongo kujenga kiwanda cha Colbat nchini kwa kuwa nchi hiyo iko jirani sana na mkoa huo na kwamba mkoa huo umejipanga kwa mazingira ya uwekezaji mkubwa.

Akiwa nchini, Waziri Kabwelulu alipata fursa ya kukutana na Menejimenti ya Wizara ya Madini na Taasisi zake ambapo pande zote zilibadilishana uzoefu wa namna zinavyosimamia sekta ya madini, ikiwemo masuala ya uchimbaji mdogo wa madini.

Aidha, Waziri Kabwelulu na mwenyeji wake Waziri Kairuki walitembelea Mgodi wa Mfano wa Lwamgasa ambao umejengwa mahsusi kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) unaosimamiwa na wizara. Lengo la mgodi huo ni kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu uchimbaji sahihi  na uchenjuaji bora wa madini dhahabu. Pia, walitembelea migodi ya Wachimbaji wa Kati inayomilikiwa na watanzania ya Buswola  Mining Ltd na Nsangano Gold Mine mkoani Geita kujifunza walikotokea katika uchimbaji mdogo hadi kuwa wa Kati na pia walitembelea mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) mkoani Shinyanga.

Ziara ya Waziri Kabwelulu nchini ililenga katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika masuala ya uendelezaji na usimamizi wa Sekta ya Madini ikiwemo kuimarisha zaidi ushirikiano  uliopo baina  ya hizo mbili, kuangalia fursa za ushirikiano wa kibiashara na kiuwekezaji kupitia rasilimali madini madini, kubadilishana uzoefu kuhusu Mabadiliko ya Sheria  za  Madini yaliyofanywa na nchi hizi mbili hivi karibuni pamoja na kudumisha undugu na urafiki baina ya nchi hizo mbili.

Read more

Serikali yapiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine

Na Greyson Mwase, Songwe

Serikali kupitia Wizara ya Madini imepiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kwa ajili ya kuchenjulia madini ya dhahabu kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na kusisitiza kuwa haitasita kumchukulia hatua za kisheria mchimbaji wa madini atakayekiuka agizo hilo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa New Luika uliopo katika kijiji cha Mbangala wilayani Songwe mkoani Songwe.

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 18 Oktoba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Saza kilichopo wilayani Songwe mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songwe,  Samwel Jeremeah, Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, Afisa Madini anayesimamia wilaya za Songwe na Chunya, Athuman Kwariko, Maafisa Madini kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Ndege Bilagi na Mhandisi Godfrey Nyanda, vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.

Akizungumza na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Madini kupiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kutoka katika mkoa mmoja kwenda mwingine tangu Juni mosi mwaka huu lilikuwa ni kuhakikisha kila mkoa unapata mapato stahiki kupitia ujenzi wa mitambo ya kuchenjua madini kwa kutumia kaboni.

“Kama Serikali tunataka kuhakikisha kila mkoa unajenga mitambo ya kuchenjua madini badala ya kwenda kuchenjulia katika mikoa ya jirani kwa kutumia kaboni na kukosa mapato stahiki,” alifafanua Nyongo.

Alisisitiza kuwa, Serikali haitasita kutaifisha kaboni itakayokamatwa ikisafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ikiwa ni pamoja na kuwachukulia wahusika hatua za kisheria.

Akielezea mikakati ya Wizara ya Madini katika kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini, Nyongo alisema kuwa Wizara imeshaanza kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini na kuwataka kuunda vikundi na kuomba leseni ili waweze kufanya shughuli zao za uchimbaji wa madini kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Saza kilichopo wilayani Songwe mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 18 Oktoba, 2018.

Aliongeza kuwa, Wizara ya Madini imeanza kujenga vituo vya umahiri kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu namna bora ya kubaini, kuchimba na kuchenjua madini na kueleza zaidi kuwa moja ya kituo kinachotarajiwa kujengwa ndani ya kipindi cha miezi sita kitakuwa katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Aidha, Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanalipa mrabaha na kodi mbalimbali zinazotakiwa  Serikalini na  kuwataka maafisa madini nchini kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji wa mapato hayo.

Pia, aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuepuka uchenjuaji wa madini kwa kutumia zebaki kwani ina madhara makubwa katika uharibifu wa mazingira na binadamu.

Akielezea namna bora ya usimamizi wa viwanda vitakavyojengwa kwa ajili ya kuchenjua madini ya dhahabu kwa kutumia kaboni, Nyongo alisema mbali na kuhakikisha wamiliki wanakuwa na leseni za uchenjuaji wa madini, wataalam wa mazingira kutoka Wizara ya Madini watapita na kukagua ili kuhakikisha kuwa viwanda vinajengwa katika mazingira mazuri ambayo hayatakuwa na athari katika makazi ya wananchi.

Awali wakizungumza katika mkutano huo kwa nyakati tofauti wachimbaji wadogo waliwasilisha kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maeneo kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, ushuru na tozo nyingi, pamoja na kutoshirikishwa katika mikataba baina yao na wawekezaji wakubwa wa madini.

Read more

Wachimbaji Madini Songwe waruhusiwa kuendelea na shughuli za uchimbaji madini

Na Greyson Mwase, Songwe

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka wachimbaji wa madini  wanaoendesha shughuli zao za uchimbaji wa madini ya chokaa na ujenzi katika  kijiji cha Nanyala kilichopo katika Wilaya ya Mbozi iliyopo mkoani Songwe kuendelea na shughuli zao wakati wakisubiri  suluhu ya  mgogoro baina yao na kiwanda cha saruji cha Mbeya.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia mbele) na Meneja wa Kiwanda cha chokaa cha Lime Africa kilichopo katika Kata ya Nanyala Wilayani Mbozi Mkoani Songwe, Fredy Msindo (kushoto mbele) pamoja na msafara wakiendelea na ziara katika eneo la kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Songwe yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 17 Oktoba, 2018.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo leo tarehe 17 Oktoba, 2018 alipokuwa akizungumza katika mkutano na wachimbaji wadogo  uliofanyika katika kata ya Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika  mkoa huo  yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, John Palingo, Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, Afisa Madini anayesimamia wilaya za Songwe na Chunya, Athuman Kwariko, Afisa Madini kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Ndege Bilagi, vyombo vya ulinzi na usalama vya wilaya pamoja na waandishi wa habari.

Nyongo alifafanua kuwa, awali maelekezo yalitolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ya kutaka viongozi kutoka katika mikoa ya Mbeya na Songwe kukaa pamoja na kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa ardhi kati ya  wakazi wa Songwe na Mbeya na kiwanda cha kuzalisha saruji nje ya mahakama jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa sasa.

Alielekeza viongozi kutoka katika mikoa husika kuhakikisha wanashughulikia mgogoro wa ardhi kati ya mikoa miwili na kiwanda cha saruji cha Mbeya kwa wakati huku wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uchimbaji madini wakiendelea na shughuli zao kama kawaida katika maeneo husika.

Aliendelea kusema kuwa, jukumu kuu la Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini ni kuhakikisha wanatoa leseni za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuwa leseni ya uchimbaji wa madini ni tofauti na  hati ya ardhi kwa kuwa inahusisha madini yaliyopo chini ya ardhi.

“Ningependa ieleweke kuwa, leseni ya madini inampa mtu kibali cha kuchimba madini yaliyopo chini ya ardhi ambayo ni tofauti na hati ya ardhi, hivyo wachimbaji wa madini wana haki ya kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini wakati suala la mgogoro wa ardhi likiendelea kushughulikiwa na mamlaka husika,” alisisitiza Nyongo.

Akielezea taratibu za kuchimba madini mara baada ya kupata leseni, Naibu Waziri Nyongo alisema mara baada ya mchimbaji kupata leseni ya uchimbaji wa madini anatakiwa kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na baadaye kutambulishwa katika Ofisi ya Kijiji ili kukutanishwa na wananchi na kufanya makubaliano ya ulipaji fidia kabla ya kuanza shughuli rasmi za uchimbaji wa madini.

Alisisitiza kuwa, ni lazima wawekezaji wote katika shughuli za uchimbaji wa madini kuhakikisha kuwa wanajitambulisha na kufanya makubaliano na wananchi kabla ya kuanza rasmi kwa uchimbaji wa madini ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara.

Diwani wa Viti Maalum kutoka Tarafa ya Iyula iliyopo Wilayani Mbozi mkoani Songwe, Messiah Swella akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano huo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka maafisa madini katika mikoa ya Mbeya na Songwe kuendelea na zoezi la kuainisha maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni ili uchimbaji wao uweze kuleta tija kwenye uchumi wa nchi.

Aidha, aliongeza kuwa katika maeneo ambayo ni ya hifadhi au vivutio vya utalii leseni zake zifutwe ili kuhakikisha rasilimali za maliasili zinalindwa na kuongeza pato kwenye uchumi wa taifa.

Wakati huohuo Nyongo aliwataka wachimbaji wa madini kuhakikisha kuwa wanalipa kodi mbalimbali  ili fedha hizo ziweze kutumika katika  uboreshaji wa huduma nyingine za jamii kama vile elimu, afya, miundombunu ya barabara.

Pia, Nyongo aliwataka wachimbaji wa madini kuorodhesha kodi na tozo mbalimbali ambazo wanaona ni nyingi na kuziwasilisha katika Wizara ya Madini, ili Wizara iangalie namna ya kuzipunguza na wapate faida zaidi kwenye uchimbaji wa madini.

Awali wakizungumza katika nyakati tofauti wachimbaji hao walieleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgogoro wa ardhi baina yao na  kiwanda cha saruji cha Mbeya, uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi  ya wachimbaji na ukosefu wa maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa madini.

Read more

Hakuna cha msalia mtume usipotekeleza sheria-Profesa Kikula

Na Rhoda James, Singida

Mwenyekiti wa Tume ya madini, Profesa Idris Kikula amesema kutokujua sheria ya madini si kigezo wala sababu ya kukwepa adhabu ya ukiukwaji wa sheria hiyo na kuwataka wachimbaji wa madini kuzingatia na kufuata sheria na taratibu za kujihusisha na biashara hiyo.

Kamishna wa Tume ya Madini, Athanas Macheyeki, akijadili jambo na wachimbaji pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Kongo na Mpipiti uliopo mkoani Singida

Ameyasema hayo jana tarehe 16 October 2018 mkoani Singida alipokuwa katika  kikao na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi, Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, viongozi wa wachimbaji wadogo pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa Jasi na madini ya dhahabu.

Profesa Kikula ameeleza kuwa, kazi ya tume ni pamoja na kutoa elimu kwa wachimbaji wa madini, Hii ni sababu kubwa ya kuwatembelea siku hii ya leo, “tumewatembelea ili kuwafundisha na kuwakubusha kuhusu sheria zilizopo pamoja na marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017”.

Tunapita ili kutoa elimu katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya kutuza kumbukumbu, mazingira na usalama migodini, utoaji wa tozo mbalimbali kwa mujibu wa sheria ili tutakapokuja tena awamu nyingine na kukuta mmekiuka taratibu sheria ichukue mkondo wake.

Aidha, Profesa Kikula amewataka wachimbaji wadogo, wa kati na hata wakubwa nchini kuhakikisha kuwa wanakaa pamoja na uongozi wa  wilaya au mkoa husika ili kukubaliana juu ya namna ya uwajibikaji katika kutoa huduma kwa jamii (CSR).

“Mikataba hii mnayoingia itasaidia kujua ni kiasi gani mnapata, kiasi gani unatakiwa kulipa kuligana na unachokipata ili Serikali ipate stahiki zake. Alisema Profesa Kikula.

Pamoja na hayo,  Profesa Kikula amewasihi viongozi wa wachimbaji wadogo (REMA) kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu  na wachimbaji wadogo ili kuhakikisha kuwa wachimbaji hao wanajiunga katika vikundi na kuvirasimisha ili Serikali iwatambue na kuwapa huduma wanayostahili kwa wakati.

Kamishna wa Tume ya Madini, Athanas Macheyeki akijadili jambo na wachimbaji pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Kongo na Mpipiti uliopo mkoani Singida

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi, amewataka viongozi wa mkoa, wilaya, kata na hata vijiji kubadilika na kushiriki katika kutatua matatizo ya wananchi kwa karibu.

Aidha, amewataka , watumishi kujishughulisha kwa juhudi na kujituma pasipo kusubiri kuambiwa jambo la kufanya na badala yake wajifunze kufikiri jambo jema linalohitaji kufanyiwa kazi na kutekeleza kwa wakati ili kupunguza changamoto zinazojitokeza.

Akijibu swali la mchimbaji mdogo wa madini(Jina halikufahamika), aliyehoji  juu ya leseni ya utafiti kuchukua muda mrefu pasipo wananchi kupewa maelezo yoyote Kamishna wa Tume ya Madini Abudulkarim Mruma  alifafanua kuwa leseni ya utafiti inatolewa kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza inachukua miaka minne, ya pili miaka mitatu na ya tatu miaka miwili kwa mujibu wa sheria ya madini na baada ya hapo kama mchimbaji hajapata chochote anarudisha eneo hilo kwa Serikali.

Read more

Waziri Kairuki akabidhiwa kikombe cha ushindi, maonesho ya viwanda, Geita

Na Asteria Muhozya,

Wizara ya Madini ilikuwa Mshindi wa Kwanza katika Taasisi za Serikali zilizoshiriki Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu yaliyofanyika Mkoani Geita kuanzia mkoani Geita tarehe 24 – 30 Septemba, 2018.

Maonesho hayo yalifunguliwa kwa niaba ya Waziri wa Madini na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na kufungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Read more

Mwenyekiti Tume ya Madini awaasa wakuu wa wilaya kutatua migogoro sehemu za machimbo

Na. Rhoda James, Manyoni

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameagiza Wakuu wa wilaya inchini kutatua migogoro ya wachimbaji wa  madini inayojitokeza katika maeneo yao ili kuepusha madhara yatokanayo na ucheleweshwaji wa utatuzi wa migogoro hiyo inayopelekea migogoro hiyo kufikishwa katika ngazi za juu.

Mmiliki wa mgodi wa General Business and Equipment Suppliers ltd, Yusufu Kibila akitoa maelezo kwa Kamishna wa Tume, Dkt. Athanas Macheyeki wa kwanza kushoto na Kaimu Afisa Mkazi wa Singida.

Profesa Kikula ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 October, 2018 wakati alipokuwa kwenye ziara yake katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza katika kikao hicho, Profesa Kikula aliwaasa Wakuu wa Wilaya kushirikiana na viongozi wa vijiji, viongozi wa kata kuelewa vyema vyanzo vya migogoro sehemu za machimbo pamoja  na kuitatua.

“Tume ya madini haiwezi kutatua migogoro yote nchi nzima, lazima tushirikiane katika hilo ili kuwasaidia wanachi kupata haki yao kwa wakati” alisema Profesa Kikula.

Profesa Kikula aliongeza kuwa, wapo wenyeviti wa wachimbaji wadogo kila mkoa hivyo fanyeni kazi kwa karibu na hao viongozi wa wachimbaji wadogo ili kubaini changamoto zao na kutatua migogoro inayojitokeza.

Aidha, Profesa Kikula alitoa wito kwa wachimbaji wadogo pamoja na Wakuu wa Wilaya kusoma marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka  2017 na kuielewa ili kuwa na uelewa wa uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Profesa Kikula alisema kuwa ni pamoja na kuangalia usalama wa wachimbaji wadogo, kufuatilia na kujiridhisha na utuzwaji wa kumbukumbu za mapato na tozo mbalimbali, kujiridhisha endapo wachimbaji wanazingatia uchimbaji salama bila kuathiri mazingira pamoja na kufuatilia endapo wachimbaji wanajishughulisha na masuala ya kijamii kama vile kujenga shule, zahanati.

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya madini, Abudulkarim Mruma amewasihi Wakuu wa Wilaya kufatilia taarifa za wachimbaji wadogo ili kujua leseni ya eneo husika inamilikiwa na nani na je ameajiri watumishi wangapi jambo litakalosaidia katika kupunguza na kutatua migogoro itakayojitokeza kwa wakati.

Mjumbe wa Mgodi wa Muhintiri akieleza changamoto wanayoipata kwa Kamishna wa Tume, Athanas Macheyeki ( mwenye shati la blue) wengine ni wachimbaji wadogo pamoja na watumishi kutoka Tume ya madini.

Akizungumzia umuhimu wa utunzwaji wa kumbukumbu kwa wachimbaji wadogo,  Dkt.Athenas Macheyeki Kamishna wa Tume ya madini aliwasisitiza  Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanatuza kumbukumbu za uzalishaji na uuzaji ili kujua kiasi sahihi cha uzalishaji na kilichouzwa ili kwa njia hiyo Serikali ijipatie mapato yanayostahili.

Mkuu wa wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa alimshukuru Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Kikula kwa ujio wao

Na kuahidi kuwa watatekeleza kwa umakini mkubwa suala la kutatua migogoro maeneo ya wachimbaji  kwa kushirikiana na viongozi wa madini waliopo katika maeneo yao pamoja na viongozi wa wachimbaji wenyewe.

Aidha, aliahidi kupitia kwa upya na kuhakikisha marekebisho ya sheria ya madini ya 2017 ameielewa kikamilifu na kuifanyia kazi katika shughuli za kila siku ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake lakini pia serikali inajipatia mapato yake stahiki.

Mwagisa alikamilisha hotuba yake kwa kuahidi kuwa  ataendelea kusimamia na kudhibiti suala la utoroshaji wa madini na kuhakikisha kinachopatikana kinauzwa sehemu maalumu lakini baada ya kumbukumbu kuwekwa sawa na tozo stahiki zimewasilishwa ipasavyo.

Read more

Serikali ipo tayari kusaidia wawekezaji wa madini-Nyongo

Na Greyson Mwase, Sumbawanga

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia wawekezaji kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ili uchimbaji wao ulete manufaa kwa nchi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kulia) kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kabla ya kuanza ziara ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 12 Oktoba, 2018.

Aliyasema hayo leo tarehe 12 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika mgodi wa makaa ya mawe  wa Edenville International (T) Limited uliopo katika  kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na  Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Katibu Tawala Msaidizi – Sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,  Happiness Shayo, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa katika kuhakikisha watafiti na wachimbaji wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kusogeza huduma zake kwa kuhakikisha kuwa inaanzisha ofisi za maafisa madini wakazi katika mikoa yote ambapo mkoa wa Rukwa unatarajiwa kupata ofisi kwa mara ya kwanza.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliushauri uongozi wa mgodi huo kujikita kwenye uzalishaji wa makaa ya mawe ambayo ni bora na kuuza katika nchi za jirani kwa kuwa mahitaji ya makaa ya mawe ni makubwa.

Aliwataka maafisa madini wakazi wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanashirikiana na ofisi za wakuu wa wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika zoezi la usimamizi wa upakiaji wa madini kabla ya kusafirishwa ili kudhibiti mianya ya utoroshwaji wa madini mbalimbali.

Wakati huohuo Naibu Waziri Nyongo aliwataka wachimbaji wa madini nchini kufuata kanuni na sheria za madini katika kuhakikisha kuwa wanalipa kodi stahiki serikalini ili fedha ziweze kuwanufaisha wananchi kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii.

Awali akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, meneja wa mgodi huo Jamhuri Mbamba alisema kuwa,  uzalishaji unazingatia mahitaji ya soko na kusisitiza kuwa kwa sasa mahitaji ni takribani tani 3000 kwa mwezi na kuendelea kusema kuwa mgodi unatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 15,000 za makaa ya mawe kwa mwezi.

Aliendelea kusema kuwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba 2018 jumla ya tani takribani 9941.78 za makaa ya mawe yalioshwa na kuuzwa kwa wateja wa ndani na nje ya nchi.

Meneja wa mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, Jamhuri Mbamba (katikati) akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) katika ziara hiyo.

Akielezea changamoto za mradi Mbamba alisema kuwa, awali lengo kuu la mradi lilikuwa ni uzalishwaji wa umeme lakini mchakato wake umekuwa ukichukua muda mrefu pasipo mafanikio.

Alisema hadi sasa maongezi kati ya kampuni na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yamekuwa yakiendelea kwa kipindi kirefu na kwa sasa kampuni inaandaa zabuni kama ilivyoainishwa hapo awali.

Aliongeza kuwa pia mradi ulilenga ujenzi wa njia ya umeme ya Mbeya hadi Kigoma hadi Nyakanazi ambao haujaanza kujengwa.

Read more

Serikali haitamwonea aibu asiyelipa kodi ya madini-Nyongo

Na Greyson Mwase, Katavi

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini haitamwonea aibu mchimbaji yeyote wa madini atakayekwepa kulipa kodi Serikalini  kwa kuwa ni kinyume na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini kutoka machimbo ya Reef D, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara

Ameyasema hayo leo tarehe 11 Oktoba, 2018 katika  mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli zao katika machimbo ya Reef D, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake  katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,  Salehe Mhando,  Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa, kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wasio waaminifu wanaokwepa kulipa kodi serikalini hali inayokwamisha  upatikanaji wa huduma nyingine muhimu katika jamii kama vile elimu, maji, barabara.

“ Mchimbaji ambaye anakwepa kulipa kodi mbalimbali kama Sheria ya Madini na kanuni zake inavyofafanua ni adui namba moja katika ukuaji wa maendeleo ya nchi, hivyo sisi kama Wizara ya Madini tumejipanga kuchukua hatua za kisheria nia ikiwa ni kutaka kila mwananchi anufaike na rasilimali za madini kupitia uboreshaji wa huduma mbalimbali,”alisema Nyongo.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka maafisa madini wakazi katika mikoa yote kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa maduhuli kwani Sekta ya Madini inatarajiwa mno kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Reef D, yaliyopo katika kata ya Magamba mkoani Katavi akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani)

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaamini kuwa iwapo Sekta ya Madini itasimamiwa kikamilifu, inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye  ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia uimarishaji wa sekta nyingine muhimu.

Aidha, aliwataka maafisa madini nchini kushirikiana na  vyombo vya ulinzi na usalama katika wilaya kwenye zoezi la ukaguzi wa shughuli za madini ili kuongeza tija kwenye  ukaguzi.

Katika mkutano huo mbali na wachimbaji wadogo kumpongeza kwa kazi kubwa anayofanya ya kusikiliza na kutatua changamoto kwenye  shughuli za uchimbaji madini katika mkoa wa Katavi, wachimbaji hao waliwasilisha changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mahitaji ya mikopo katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini, mafunzo kuhusu sheria ya madini na kanuni zake, uchimbaji salama na vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchimbaji wa madini.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo katika eneo hilo, Imso Masumbuko kutoka kikundi cha Kagera Group alisema kuwa wana uhitaji mkubwa wa elimu kuhusu uchimbaji wa madini  salama pamoja na vifaa vya kisasa ili waweze kuzalisha na kulipa kodi zaidi Serikalini.

Masumbuko mbali na kuainisha changamoto hizo aliiomba Wizara ya Madini kuiomba Wizara ya Nishati ili iweze kufikisha umeme katika machimbo hayo  kupitia Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kufanya nao kikao kilicholenga kujadili utendaji kazi.

Alifafanua kuwa, kutokana na ukosefu wa nishati ya umeme katika eneo lao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye uzalishaji wa madini kutokana na matumizi ya dizeli hivyo kupata faida kidogo sana.

Naye Karusum Daudi ambaye ni mchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini iangalie uwezekano wa kuwapatia mikopo ili waweze kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi na kusikiliza kero mbalimbali za watumishi ikiwa ni pamoja na kuzitatua.

Pia Naibu Waziri Nyongo alikutana na wachimbaji wadogo wa madini mjini Mpanda lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini.

Mbali na kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizotatuliwa na Naibu Waziri Nyongo papo hapo  wachimbaji wadogo wa madini walimpongeza Naibu Waziri Nyongo na kumwomba kuendelea na ari ya kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Akizungumza katika kikao hicho, Nyongo alisema Wizara ya Madini haitachoka kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wa madini nchini kwa kuwa inataka wachimbe katika mazingira mazuri na kulipa kodi Serikalini.

Read more

Nyongo aagiza Afisa Madini, Watendaji kusimamia ufungaji na ufunguaji wa madini

Na Greyson Mwase, Katavi

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameagiza  Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Afisa Usalama wa Wilaya, na Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanakuwepo wakati wa ufungaji na ufunguaji wa lakiri (seal)  kwenye madini ya dhahabu ili kudhibiti utoroshwaji wa madini kwenye migodi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi, Mahmood Yass (kushoto) kabla ya kuanza ziara yake katika mgodi huo uliopo katika eneo la Singililwa Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Ameyasema hayo  leo tarehe 09 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika Mgodi Dhahabu  wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa  Wilayani Mpanda mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya ziara yake  katika mkoa huo yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika,  Salehe Mhando,  Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa, ni kosa kubwa la kisheria kwa Afisa Madini Mkazi kufunga au kufungua lakiri (seal) pasipo kushirikisha  Mkuu wa Wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusisitiza kuwa iwapo itagundulika Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria.

Akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini Nchini, Nyongo alisema kuwa ni pamoja na uboreshaji wa Sheria ya Madini iliyolenga kuondoa mianya ya utoroshwaji wa madini nje ya nchi kwa kuzuia usafirishwaji wa madini ghafi nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisalimiana na sehemu ya wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Katavi & Kapufi uliopo katika eneo la Singililwa lililopo Wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Alisisitiza kuwa, Serikali inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi katika ujenzi wa mitambo ya kuchenjulia madini ndani ya nchi  ili kuyaongezea thamani kabla ya kuuzwa nje ya nchi na kuongeza mapato.

Wakati huohuo akizungumza katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika  kijiji cha Kapanda  Wilayani  Mpanda mkoani Katavi yanayomilikiwa na William Mbogo, Naibu Waziri Nyongo alimtaka mmiliki wa leseni kuhakikisha anaandaa mikataba na kusaini pamoja na wachimbaji wadogo wanaoendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara yake haipo tayari kushuhudia migogoro kati ya wawekezaji na wachimbaji wadogo wa madini pasipo suluhu inayotokana na ukiukwaji wa Sheria za Madini na kanuni zake.

Katika hatua nyingine, Nyongo alimtaka mwekezaji huyo kutafuta mwekezaji mkubwa kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za uchimbaji madini katika eneo husika iwapo anakosa uwezo wa kuendeleza kama leseni ya madini inavyomtaka.

Aidha, alimwelekeza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka kuhakikisha anatafuta maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini, ili waweze kuchimba katika mazingira mazuri huku wakifuata sheria na kanuni za madini.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuhakikisha wanalipa mrahaba na kodi mbalimbali Serikalini ili mapato yaweze kutumika kwenye uboreshaji wa sekta nyingine  kama vile afya, elimu, maji na miundombinu.

Awali mbali na pongezi, wakiwasilisha kero mbalimbali wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli za uchimbaji madini katika machimbo ya dhahabu ya Mkwamba yaliyopo katika  kijiji cha Kapanda  Wilayani  Mpanda mkoani Katavi yanayomilikiwa na William Mbogo walieleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitaji midogo, vifaa duni pamoja maeneo rasmi kwa ajili ya uchimbaji madini.

Read more

Kituo kikubwa cha Kimataifa cha Dhahabu kujengwa Geita-Luhumbi

Na Rhoda James, Geita

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi amesema kuwa Kituo kikubwa cha kimataifa cha Dhahabu kinatarajiwa kujengwa Mkoani Geita hivi karibu ambapo pamoja na mambo mengine kitawezesha wachimbaji wadogo kupata elimu kuhusu uchimbaji wenye tija.

Mjiolojio kutoka Wizara ya Madini, Joseph Ngurumwa akiwakilisha mada kwa wachimbaji wadogo katika kikao kilichofanyika mkoani Geita tarehe 28 Septemba, 2018.

Hayo yalibainishwa jana  28 Septemba, 2018 na mkuu huyo wa mkoa  wakati alipokuwa  akiwahutubia  Wachimbaji Wadogo  wa Madini katika katika Clinik ya Maonesho  ya  Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu yanayoendelea  katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Alisema kuwa, bado idadi kubwa ya watumiaji wa madini ya  dhahabu  wanatoka  nje,  hivyo, hawana budi kufahamu  mahali madini hayo yanapotoka   na kuongeza kuwa, ujenzi wa kituo hicho mkoani humo utawezesha kuyatambulisha zaidi madini hayo na mahali yanapotoka.

Aliongeza kuwa, wachimbaji wadogo wamekuwa wakitumia kemikali za sumu katika shughuli zao na kuongeza  kuwa, uwepo ya Kliniki hiyo utawawezesha kupata   majibu kuhusu ni aina gani ya kemikali zinapaswa kutumika katika shughuli za madini ikiwemo  kemikali sahihi zinazopaswa kutumiwa katika shughuli madini na zipi hazipaswi kutumiwa.

Pia, Luhumbi  aliwataka wachimbaji   wadogo wa madini nchini kubadilika  katika masuala  ya utunzaji wa  fedha zao  wanapouza rasilimali hiyo  kwa kuwa wengine wanazichimbia katika mashimo.

“Anzeni kuweka fedha zenu kwenye mabenki, ni sehemu sahihi ya kuweka fedha zenu na mtapata faida nyingi kwa kuweka huko  fedha zenu alisema Luhumbi.

Mjiolojia kutoka Tume ya Madini Geita, Godfrey Keraka akitoa mada kwa wachimbaji wadogo katika viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Vilevile, Luhumbi aliwakumbusha wachimbaji wadogo kuhusu umuhimu wa  kuwa na umoja na hususan wanapopata  maeneo ya kuchimba madini ikiwemo pindi wanapopata dhahabu na kuwaasa kuhusu kuacha ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe kugombea maeneo au madini.

“Ishini kama matajiri, matajiri hawagombanii vitu vidogo vidogo, na nyinyi ni matajiri kwa kuwa nyie ndio mnao uza dhahabu,” alisema Luhumbi.

Pia, Mkuu  huyo wa mkoa alitoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa Kituo cha Taasisi ya Jilojia na Utafiti  wa Madini Tanzania  (GST) kinajengwa mkoani ili kuwafikia wachimbaji wengi  kwa urahisi na kwa wakati.

Kwa upande wake, Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machayeki alieleza kuwa, hakuna mchimbaji na wadau wengine wa madini watakaokosa leseni ikiwa  watakidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu.

Aliongeza kuwa, ili mchimbaji mdogo aweze kupatiwa Leseni, ni lazima awe na Plan ya Local Content, na kuongeza kuwa, Tume ya Madini inaandaa mwongozo huo.

Pia, alifafanua kuwa,  kwa upande wa wachimbaji wa  Wakubwa na wa Kati wanatakiwa kufuata Sheria na utaratibu wa  Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Naye, Mjiolojio kutoka Wizara ya Madini, Joseph Ngurumwa alisema kuwa, wachimbaji wanatakiwa kuelewa kwamba Sera ya madini inahimiza  kuhusu pande   zote yani Serikali  na wachimbaji  kufaidika  kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi akihutubia wachimbaji wadogo katika viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita tarehe 28 Septemba, 2018

Kwa upande wa wachimbaji wadogo, waliiomba serikali iendelee kuwapatia elimu zaidi kuhusu uchimbaji ili kuwawezesha kuwa na  uelewa na hususan masuala ya miamba na mabadiliko yake.

Aidha, wachimbaji hao wadogo waliomba kupata  taarifa za utafiti ikiwezekana  za kuhusu nchi nzima ili  kuwawezesha kufanya shughuli za uchimbaji hata katika mikoa mingine.

Pia, walitoa ombi kwa serikali kuhakikisha wanapata Kituo cha umahiri kwa ajili ya mkoa wa Geita kwa kuwa theluthi ya madini ya dhdhabu nchini inatoka mkoani humo.

Read more

Wizara ya Madini yangaa’ra katika Maonesho ya Madini ya dhahabu Mkoani Geita

Na Rhoda James,

Wizara ya Madini imekuwa mshindi wa kwanza katika taasisi za Serikali zilizoshiriki Maonesho ya kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya dhahabu mkoani Geita yaliyoanza tarehe 24 – 30 Septemba, 2018.

Mjiologia kutoka Wizara ya Madini, Joseph Ngurumwa (mwenye shiti la bluu) akiwa pamoja na Mjiolojia kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Priscus Kaspana.

Maonesho hayo yaliyofana, yaliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan trade).

Maonesho hayo yaliyoshirikisha makampuni 250 kutoka maeneo mbalimbali nchini yalishirikisha wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini.

Aidha, Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka mkoani Geita na yatakuwa yanaandaliwa kwa kushirikiana na taasisi hiyo ya  Tan trade.

Imeelezwa kuwa Maonesho yajayo yataboreshwa zaidi na yatashirikisha mataifa mbalimbali na Wizara ya Madini itashiriki kuyatangaza ili wadau wengi zaidi waweze kushiriki.

Read more

Nafasi za mafunzo kwa ngazi ya cheti TGC

Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinatangaza nafasi za mafunzo ya muda mfupi (Short Course) katika fani ya ukataji na usanifu wa madini ya vito (Lapidary training course) , Utambuzi wa madini ya vito (Intoduction to Gemmology) na  mafunzo katika fani ya usonara (Introduction to jewelry).

Mafunzo hayo yatatolewa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), kilicho chini ya Wizara ya Madini. Kituo kipo Jijini Arusha katika barabara ya Themi karibu na Ofisi ya Madini Arusha.

Sifa za Mwombaji:

 • Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea mwenye kufaulu masomo manne kwa angalau alama D.
 • Mafunzo ni kwa jinsia zote na umri wowote.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Maduka manne ya vito na usonara kufungwa

 • Ni baada ya waziri Kairuki kubaini madudu baada ya ziara ya kushtukiza

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki ameyafungia maduka manne ya vito na usonara yaliyopo katika Mtaa wa Indiragadhi baada ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uuzwaji wa madini hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kwanza kulia akifuatiwa na Waziri wa Nishati mara baada ya kuwasili katika mtaa wa Indiragadhi kwa ziara ya ukaguzi wa maduka ya madini na usonara ili kujiridhisha endapo wafanyabiashara hao wanafuata taratibu za kufanya biashara hiyo.

Hayo yamebainika mara baada ya Kairuki kufanya ziara ya kushtukiza ya kukagua na kujiridhisha endapo wafanyabiashara hao wanafuata taratibu na shaeria za kufanya biashara ya madini Jijini Dar es Salaam na kubaini wengi wao kuzikiuka na kuisababishia Serikali kutokupata mapato halali ya mrabaha kutoka kwa wauzaji wa madini hayo.

Maduka yaliyofungiwa wakati wa ziara hiyo ni Sami Jewellers, New Gold Point, Almasi Jewellers pamoja na Queens Jewellers ambapo wafanyakazi wake hawakutaka kumtaja mmiliki wa maduka hayo yanayodaiwa kuwa ni ya mtu mmoja.

Waziri Kairuki alibainisha kutoridhishwa na wafanyabiashara wa madini hao mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku ya kwanza na hivyo kuagiza maduka hayo kufungwa. “Baada ya kufanya ziara hii na kujionea madudu yanayoendelea nimeelekeza kufungwa kwa maduka manne kutokana na mmiliki wake kutokuzingatia utuzwaji wa kumbukumbu na kufanya biashara hii bila kuwa na leseni kutoka wizara ya Madini kama sheria zinavyoelekeza”. Alisema.

Alikazia kuwa, ili kufanya biashara hii, mfanyabiashara anapaswa kuwa na leseni mbili ambapo moja inatolewa na Wizara ya Madini na nyingine inatolewa na Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji.

Aidha, Waziri Kairuki alibaini kuwa, Wafanyabiashara hao wanakiuka au hawafuati mfumo elekezi wa utunzwaji wa kumbukumbu za mauzo na manunuzi ya madini hayo kutokana na maduka yote aliyoyatembelea kutokufuata utaratibu halali wa kutunza kumbukumbu hizo.

Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki mwenye blauzi ya mistari akimsikiliza mwalimu wa ukataji vito Farai Runyanga (kushoto kwa Waziri) kutoka nchini Zimbambwe aliyefika kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wazawa ili kujishughulisha na kazi hiyo ya kusanifu madini nchini.

Kutokana na kutoridhishwa na ujazwaji wa kumbkumbu hizo Waziri Kairuki aliwaagiza wafanyabiashara hao kuhkikisha wanzingatia namna elekezi ya kutunza taarifa hizo ili kujiweka katika hali salama pindi itakapobainika kuwa madini wanayouziwa ni ya wizi au vinginevyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyeamua kuambatana na Waziri kwenye ziara yake ya siku ya kwanza alisema amesikitishwa sana kuona katika mkoa wake bado kuna watu wanaokiuka sharia na taratibu za nchi na kueleza kuwa wasipotaka kufuata sharia kwa hiari basi sharia zenyewe zitawalazimisha wazifuate.

“Mimi kama Mkuu wa Mkoa huu najisikia vibaya kuwa na wafanyabiashara ambao wanakiuka taratibu na kuwa wajanja wajanja wakati wanafahamu msimamo wa Serikali ya awamu ya tano kuwa ni wajibu wa kila mmoja kufuata sharia na taratibu za ulipwaji wa kodi”. Alisisitiza.

Aidha, Makonda amewataka wafanyabiashara katika mkoa wake kuweka mazingira yao ya biashara vizuri ili kuepuka usumbufu watakaoupata endapo watakiuka taratibu hizo.

Read more

Naibu Waziri Nyongo aagiza maafisa madini kuwasilisha kwake tafsiri sahihi ya mawe yanayokatwa kabla ya kutoa maamuzi ya usafirishwaji wake nje ya nchi

Na Greyson Mwase, Dodoma

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka maafisa madini nchini kuwasilisha kwake haraka maana halisi ya mawe yanayochimbwa na kukatwa kama ni madini ghafi au ni mali ghafi  kabla ya  kutoa maamuzi juu ya usafirishwaji wake nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati mbele) akiendelea na ziara katika machimbo ya mawe yaliyopo katika eneo Itiso Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Aliyasema hayo jana tarehe 06 Oktoba, 2018 mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Mgodi wa Mawe unaomilikiwa na Sisti Mganga uliopo katika eneo la Itiso mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Chamwino yenye lengo la  kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini pamoja na wananchi wanaozunguka migodi.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya  ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, Mbunge wa Jimbo la  Chinolwa, Joel Makanyaga, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Joshua Nduche, vyombo vya  ulinzi na usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.

Alifafanua kuwa Sheria Mpya ya Madini ilitoa zuio la usafirishwaji wa madini ghafi nje ya nchi ili kuzuia mianya ya utoroshwaji wa madini nje ya nchi.

“Kabla ya Sheria hii mpya ya Madini, kulikuwa na utoroshwaji mkubwa wa madini nje ya nchi hali ambayo iliikosesha  Serikali mapato yake, lakini mara baada ya utekelezaji wa Sheria Mpya ya Madini tumeshuhudia ongezeko kubwa la mapato kutokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini,” alisema Nyongo.

Naibu Waziri Nyongo aliendelea kusema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mbali na wachimbaji wa madini hususan  wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri, Serikali inataka kupata mapato stahiki kwa ajili ya uboreshaji wa sekta nyingine muhimu.

Alisema mara baada ya kupokea changamoto ya kuzuiwa kwa usafirishwaji wa mawe yaliyochimbwa na kukatwa na Mgodi wa Mawe unaomilikiwa na Sisti Mganga, aliridhishwa na juhudi zinazofanywa na mgodi huo na kusema kama Serikali inaangalia namna ya kumsaidia mmiliki wa mgodi huo lakini baada ya kujiridhisha kama ni malighafi badala ya madinighafi.

Mmiliki wa Mgodi wa Mawe uliopo katika eneo la Itiso Wilayani Chamwino mkoani Dodoma, Sisti Mganga kushoto akielezea shughuli zinazofanywa na mgodi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto mbele)

“Lazima tuhakikishe Sheria inasimamiwa ipasavyo, iwapo itabainika kuwa mawe yanayochimbwa na kukatwa ni malighafi basi tutatoa uamuzi wa kuyaruhusu kusafirishwa nje ya nchi na Serikali kupata mapato yake,” alisisitiza Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine akizungumza katika nyakati tofauti katika ziara hiyo, Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo nchini wasio rasmi kuunda vikundi na kuomba leseni za uchimbaji madini ili waweze kuchimba kwa kufuata sheria  na kanuni za madini.

Aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imetenga maeneo maalum yaliyofanyiwa utafiti kwa ajili ya kugawiwa kwa wachimbaji wadogo.

Aidha, aliwataka wamiliki wote wa leseni kuendeleza maeneo yao kama Sheria ya Madini inavyowataka  na kusisitiza watakaoshindwa kuendeleza maeneo yao leseni zao zitafutwa na maeneo yao kugawanywa kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Naye Mbunge wa Chilonwa kupitia Chama cha Mapinduzi, Joel Makanyaga akizungumza katika ziara hiyo alimshukuru Naibu Waziri Nyongo kwa kutembelea machimbo hayo na kufafanua kuwa iwapo wachimbaji hao watawezeshwa na Serikali bidhaa za ujenzi zinazotokana na mawe zitaongezeka na kusaidia hususan katika ujenzi wa jiji jipya la Dodoma.

Alisema kuwa mahitaji ya vifaa vya ujenzi ni makubwa katika ujenzi wa jiji la Dodoma na kuendelea kusema kuwa mapato yatokanayo na uchimbaji na ukataji wa mawe yanatarajiwa kuongezeka hivi karibuni.

Awali akiwasilisha changamoto za Mgodi wa Mawe Mkurugenzi wa Mgodi huo, Sisti Mganga alisema kuwa uwepo wa  Sheria ya Madini inayokataza usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi umeathiri utendaji kazi wa kampuni kwani wamerundika mawe mengi wakisubiri maelekezo kutoka Serikalini.

Alisisitiza kuwa mawe yanayochimbwa kukatwa na kung’arishwa katika  machimbo hayo yanajulikana kama malighafi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na barabara na kuiomba Serikali kuruhusu usafirishwaji wa mawe hayo ili waweze kuendesha shughuli za uchimbaji na ukataji wa mawe hayo na kulipa mrabaha na kodi mbalimbali Serikalini.

Aidha Mganga aliiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda kwa ajili ya kuchenjua na kuongeza thamani madini ili kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Read more

Naibu Waziri Nyongo atoa siku mbili kwa mwekezaji kutoa ripoti ya utekelezaji wa mpango wa huduma kwa jamii

Na Greyson Mwase, Dodoma

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa siku mbili kwa kampuni inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika kijiji cha Kwahemu Wilayani Chamwino mkoani Dodoma ya Ruvu Gemstone Mining Co. Limited inayomilikiwa na Kimon Dimitri kuwasilisha ofisini kwake ripoti ya utekelezaji wa mpango wa utoaji wa huduma kwa jamii kwa kipindi cha miaka miwili  kabla ya kutoa maamuzi ya serikali.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akiangalia moja ya mawe yanayochongwa na Mgodi wa Mawe unaomilikiwa na Sisti Mganga katika eneo la Itiso lililopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma katika ziara yake ya siku moja katika machimbo yaliyopo katika Wilaya ya Chamwino yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali kwenye shughuli za uchimbaji madini tarehe 06 Oktoba, 2018.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo jana tarehe 06 Oktoba, 2018   alipokuwa akizungumza na wananchi wa  kijiji cha Kwahemu kilichopo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja  katika Wilaya ya Chamwino  yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini,  kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini pamoja na wananchi wanaozunguka migodi.

Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya  ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, Mbunge wa Jimbo la  Chinolwa, Joel Makanyaga, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Joshua Nduche, vyombo vya  ulinzi na usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa, haiwezekani kampuni inayoendesha shughuli za uchimbaji wa madini ya vito ya Ruvu Gemstone Mining Co. Limited ikaendesha shughuli zake pasipo kunufaisha wananchi wanaozunguka migodi yake.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali kamwe haitamvumilia mwekezaji wa aina yoyote atakayeendesha shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini kwa kukiuka  Sheria Mpya ya Madini  yenye kipengele kinachowataka wawekezaji kuchangia katika uboreshaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vituo vya afya, miundombinu ya barabara na shule.

“Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga katika kuhakikisha watanzania wote wananufaika na uwepo wa rasilimali za madini kupitia kodi, tozo mbalimbali pamoja na mpango wa utoaji wa huduma za jamii,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Moja ya mitambo ya kukata mawe katika Mgodi wa Mawe unaomilikiwa na Sisti Mganga katika eneo la Itiso lililopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma

Alisisitiza kuwa, ni lazima nakala za ripoti zisambazwe kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Diwani na Mbunge ili kubaini  ukweli wa madai ya mwekezaji kuwa amekuwa akichangia katika huduma za jamii tangu alipoanza kuchimba madini ya vito mwaka 1986.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo alimtaka mwekezaji  kuhakikisha anadumisha mahusiano na jamii inayozunguka mgodi  ili kuepusha migogoro inayotokea mara kwa mara.

Awali wakiwasilisha kero kwa Naibu Waziri Nyongo wananchi wa kijiji hicho walimweleza kuwa tangu kuanzishwa kwa mgodi husika hawajaona manufaa ya aina yoyote zaidi ya kunyanyaswa kwa kunyang’anywa ardhi, kupigwa na wakati mwingine kufungwa jela.

Akiwasilisha kero kwa niaba ya wananchi hao, Daudi Kiloka ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kwahemu alisema kuwa awali walikuwa na shamba kubwa lenye ukubwa wa takribani heka 500  chini ya Umoja wa Bega kwa Bega wa kijiji hicho lakini baadaye shamba hilo lilikuja kutwaliwa na mwekezaji huyo.

Aliendelea kusema kuwa, wananchi wamekuwa wakikosa huduma muhimu ikiwa ni pamoja na shule, maji na vituo vya afya  hali inayolazimu wananchi wengi kutumia muda mwingi kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma.

Read more

Tume ya madini yatoa leseni mpya za madini 7879

 • Kampuni nyingi zazidi kujitokeza kwenye uwekezaji wa madini

Na Greyson  Mwase, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa kati ya kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba mwaka huu, Tume ya Madini, imetoa leseni 7879 ambazo maombi yake yaliidhinishwa kupitia kikao cha Tume kilichofanyika tarehe 25 Septemba, 2018 kilicholenga  kujadili taarifa za Kamati za Tume na utendaji kazi katika kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba, 2018.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula (katikati) akitoa ufafanuzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na kushoto ni Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA wa Tume ya Madini, Torece Ngole.

Profesa Kikula ameyasema hayo leo tarehe 04 Oktoba, 2018 kupitia mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za  Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma.

Akielezea kuhusu maombi ya leseni za madini  7879 yaliyoidhinishwa katika kikao cha Tume, Profesa Kikula  alieleza kuwa ni pamoja na  Leseni za Utafutaji wa Madini (Prospecting License – (PL) 263; Leseni Kubwa (Special Mining License – (SML) 03;(ziliidhinishwa ili kupelekwa     kwenye mamlaka husika ambayo ni Baraza la Mawaziri) Leseni za Uchimbaji wa Kati (Mining License – (ML) 14 pamoja na leseni 1 ya Sihia (Transfer) ya uchimbaji wa Kati.

Aliendelea kufafanua kuwa, maombi leseni za  uchimbaji wa kati 14 yaliyopitishwa kuwa ni pamoja na  kampuni za Dangote Industries Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya chokaa katika eneo la Mtwara;  Nazareth Mining Investment Co Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) katika eneo la Ruangwa mkoani Lindi na kampuni ya Sunshine Mining (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini dhahabu katika eneo la Chunya mkoani Mbeya.

Aliendelea kutaja kampuni nyingine kuwa ni pamoja na Said Seif Abdallah kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Masasi mkoani Mtwara; Off Route Technologies (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Ileje mkoani Mbeya; leseni yenye ubia kati ya Shabani Daud Ibrahim, Andrew Bollen, Dunstan M. Mongi na Vedastus Mtesigwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika mkoa wa Geita.

Maombi mengine yaliyopitishwa ni pamoja na leseni yenye ubia kati ya  Jumbo Limited, na Ally Mbarak Mohamed kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya kinywe (graphite) katika eneo la Ruangwa mkoani Lindi, Jacana Resources (Tanzania) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa mchanga bahari (mineral sand) katika eneo la Temeke lililopo jijini Dar es Salaam na P. B. Mining Company kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya  fedha, dhahabu, shaba, zinki na galena katika eneo la Chunya lililopo mkoani Mbeya.

Profesa Kikula alisisitiza kuwa, kikao hicho pia kilipitisha ombi la kubadili umiliki kutoka kwa Mbarouk Saleh Mbarouk kwenda katika kampuni ya M. B. Mining (T) Limited kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Morogoro.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula (kushoto) akielezea takwimu za leseni zilizotolewa na Tume ya Madini tangu kuanzishwa kwake kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dodoma mapema tarehe 04 Oktoba, 2018. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.

Profesa Kikula aliendelea kutaja maombi ya leseni nyingine zilizopitishwa katika kikao hicho kuwa ni pamoja na Leseni za Uchimbaji Mdogo (Primary Mining License – (PML) 6313; Leseni za Uchenjuaji wa Madini (Processing License) 08 na leseni za Biashara ya Madini ambapo leseni kubwa (Dealers License) ni  557; na leseni Ndogo (Broker’s License) 720.

Katika hatua nyingine Profesa Kikula alisema kuwa, Mipango ya Ushirikishwaji wa Utoaji wa Huduma na Bidhaa kwa Wazawa katika Miradi ya Madini (local content plan) 19 ilipitishwa kati ya mipango 26 iliyowasilishwa kutoka katika kampuni mbalimbali za utafutaji na uchimbaji wa kati na mkubwa wa madini.

Alielekeza waombaji leseni za madini kuwasilisha mipango yao kwa wakati ili iweze kupitiwa na kamati husika na kuwezesha leseni kutolewa mapema.

Pia aliwataka waombaji wote wa leseni za madini kufuatilia leseni zao kwenye Ofisi za Madini zilizopo mikoani walikoombea leseni zao na kusisitiza kuwa orodha ya leseni zilizoidhinishwa inapatikana katika tovuti ya Tume.

Wakati huohuo Profesa Kikula alisema kuwa Tume ya Madini imejipanga katika kuhakikisha kila mtanzania ananufaika ipasavyo na rasilimali za madini nchini.

Aliongeza kuwa, Tume imeweka mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwatengea maeneo kwa ajili ya uchimbaji madini na kuwataka kuunda vikundi na kusajiliwa kupitia viongozi wao hivyo kuwezesha upatikanaji wa leseni za madini na kufanya shughuli zao pasipo kikwazo chochote.

“Sisi kama Tume ya Madini tunatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo wa madini na ndio maana tumekuwa tukifanya ziara katika maeneo ya wachimbaji wadogo na  kutatua changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na migogoro; tunataka wafanye kazi katika mazingira salama kabisa,” alisema Profesa Kikula.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akielezea mchango wa Sheria Mpya ya Madini alisema kuwa tangu kuanza kwa utekelezaji wa sheria mpya iliyoweka ongezeko la kutoka asilimia nne hadi sita za mrabaha na tozo la asilimia moja la kodi ya ukaguzi wa madini,  makusanyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni  194 hadi shilingi bilioni 301 kwa mwaka likiwa ni ongezeko la asilimia 55.

Pia, Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA kutoka Tume ya Madini, Torece Ngole akielezea mikakati ya Tume katika kukabiliana na changamoto ya migogoro kwenye uchimbaji wa madini inayosababishwa na wachimbaji wadogo kwa kuvamia maeneo yenye leseni kubwa, alisema kuwa Tume imeshaanza kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kusisitiza kuwa mpaka sasa imeshatenga maeneo 74

Alisisitiza kuwa Tume imekuwa ikiwaelimisha wachimbaji wadogo kuhusu sheria na kanuni za madini na kusisitiza kuunda vikundi ili waweze kupatiwa maeneo na leseni za uchimbaji madini.

Read more

Wadau wa Madini Kimataifa wameona umuhimu wa Tanzania kufanya mabadiliko–Nyongo

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema wadau wa Sekta ya Madini Kimataifa hivi sasa wanaelewa umuhimu wa Tanzania kufanya mabadiliko katika Sekta husika yakiwemo ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yaliyofanyika Mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akimweleza jambo Balozi wa Australia Nchini Alison Charters alipomtembelea Naibu Waziri Nyongo (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma.

Naibu Waziri ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dodoma alipokutana na Balozi wa Australia Nchini, Alison Charters ambaye amemtembelea Naibu Waziri Nyongo kwa lengo la kujadiliana masuala kadhaa katika sekta ya madini ikiwemo kupata mrejesho wa ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Madini kwa nchi za Afrika uliofanyika mwezi Agosti, 2018, nchini Australia, ambapo katika mkutano huo, Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri Nyongo.

Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, awali wadau katika mkutano huo walikuwa na uelewa tofauti lakini mara baada ya kutoa wasilisho kuhusu mabadiliko hayo katika mkutano huo, waliona umuhimu wa Tanzania kufanya mabadiliko hayo kwa maendeleo ya nchi na sekta nzima.

“Mhe. Balozi nashukuru kwa nafasi hiyo isipokuwa nilitamani kupata nafasi zaidi ya kuelezea uzoefu wetu na mabadiliko katika sekta ya madini,” amesisitiza Naibu Waziri.

Ameongeza kuwa, wawekezaji wengi hawana tatizo na mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yaliyofanywa isipokuwa changamoto ipo katika kipengele cha chanzo cha mtaji kutoka katika benki za ndani suala ambalo amesema wizara imelichukua na inaifanyia kazi.

Pia, Naibu waziri amemshukuru Balozi Charters kwa kumwezesha kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya madini wakati akiwa nchini humo, kwani, wadau hao wameonesha nia ya kuisaidia Tanzania katika masuala ya uongezaji thamani madini nchini na mafunzo kwa wataalam wa sekta.

“ Tulizungumza masuala mengi na umuhimu wa sisi kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika hapa nchini. Tunasisitiza suala hili kwa kuwa hivi sasa tumezuia usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi”, amesema Naibu Waziri Nyongo.

Naibu Waziri akifuatilia kikao baina yake na Balozi wa Australia Nchini, Aliston Charters (hayupo pichani).

Kwa upande wake, Balozi Charter amesema nchi hiyo itaona namna bora ya kufanya ili kuweza kuisaidia Tanzania kutoa mafunzo kwa wataalam wa sekta husika lengo likiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kusimamia sekta hiyo vizuri.

“Tunayo bajeti kidogo lakini tunaweza kufanya jambo kwa ajili ya wizara ya madini katika utoaji wa mafunzo. Ikiwezekana hata kuwaleta wataalam wetu kuja kutoa utaalam huo hapa nchini,” amesema Balozi.

Aidha, Balozi huyo ameeleza kuhusu fursa za masomo ambazo zimekuwa zikitolewa nchini Australia zikiwemo nafasi za  mafunzo ya muda mrefu na mfupi na hivyo kuwataka wataalam wa Tanzania  kuomba nafasi hizo pindi zinapojitokeza.

Pia, balozi huyo ametaka kujua majukumu ya Tume ya Madini mara baada ya tume hiyo kuanzishwa ambapo Mwenyekiti wa Tume hiyo ambaye naye amehudhuria kikao hicho, Profesa Idris Kikula amemweleza balozi huyo majukumu yanayosimamiwa na tume hiyo ikiwemo mikakati ya tume katika kutatua changamoto zilizopo katika sekta husika.

Akizungumzia mabadiliko katika sekta ya madini pamoja na masuala ya uwajibikaji kwa kampuni za madini kwa jamii, balozi Charter amesema suala hilo ni la msingi kwani hata katika nchi hiyo masuala hayo yalipewa kipaumbele na kushauri iwapo wizara inaweza kukutana na wadau kwa ajili ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu masuala hayo.

Mbali na mrejesho wa ushiriki wa Tanzania katika mkutano masuala ya madini kwa nchi za Afrika, kikao hicho pia kimejadili masuala ya leseni za madini, Uwajibikaji wa kampuni za madini katika jamii zinazozunguka migodi na kuhusu  kampuni za madini kutumia kampuni za wazawa kutoa huduma katika migodi.

Read more

EoI-Provision of Consultancy Services for Recruitment of Financial Modeling Specialist

PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES FOR RECRUITMENT OF FINANCIAL MODELING SPECIALIST

ADVERTISEMENT

 1. The Government of United Republic of Tanzania has received an additional financing from International Development Association (IDA) for implementation of Sustainable Management of Mineral Resources Project (SMMRP). It is intended that part of this proceeds will be applied to cover eligible payments under the contract for provision of consultancy services for recruitment of financial modeling specialist.
 2. The Consultant among others shall train Government staff and other beneficiary institutions on Financial Modelling of Mining Projects so as to be able to develop cash flows and to make a projection of expected financial benefits of mining projects. The time frame for implementation of this assignment is three (3) calendar months.
 3. The Ministry of Minerals (MoM) now invites eligible consulting firm with qualified staff to indicate their interest in providing the services. Interested consultants should provide information indicating that they have required qualifications and relevant experience to perform the services. The short listing criteria shall consider; the consultant eligibility, the description of similar assignments, experience in similar conditions, availability of appropriate skills among staff etc. Consultants may associate with other firms in the form of joint venture or sub consultancy to enhance their qualifications.

   >>Read More>>

Read more

EoI-Provision of Consultancy Services for Recruitment of Resource Modeling Specialist

PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES FOR RECRUITMENT OF RESOURCE MODELING SPECIALIST

ADVERSTISMENT

 1. The Government of United Republic of Tanzania has received an additional financing from International Development Association (IDA) for implementation of Sustainable Management of Mineral Resources Project (SMMRP). It is intended that part of this proceeds will be applied to cover eligible payments under the contract for provision of consultancy services for recruitment of resource modeling specialist.
 2. The Consultant among others shall train Government staff and other beneficiary institutions on resource estimation modeling so that the Government can administer effectively mining operations and collect appropriate revenues. The time frame for implementation of this assignment is three (3) calendar months.
 3. The Ministry of Minerals (MoM) now invites eligible consulting firm with qualified staff to indicate their interest in providing the services. Interested consultants should provide information indicating that they have required qualifications and relevant experience to perform the services. The short listing criteria shall consider; the consultant eligibility, the description of similar assignments, experience in similar conditions, availability of appropriate skills among staff etc. Consultants may associate with other firms in the form of joint venture or sub consultancy to enhance their qualifications.

>>Read More>>

Read more

EoI-Provision of Consultancy Services to Undertake a Study in Mineral Smuggling

PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES TO UNDERTAKE A STUDY IN MINERAL SMUGGLING

RE-ADVERSTISMENT

 1. The Government of United Republic of Tanzania has received an additional financing from International Development Association (IDA) for implementation of Sustainable Management of Mineral Resources Project (SMMRP). It is intended that part of this proceeds will be applied to cover eligible payments under the contract for provision of consultancy services to undertake a study in Minerals smuggling.

2. The Consultant among others shall research on the minerals smuggling techniques and come out with proposals on how to stop smuggling of minerals for the purpose of enabling the Government to collect its appropriate revenue. The time frame for implementation of this assignment is three (3) calendar months.

3. The Ministry of Minerals (MoM) now invites eligible consulting firm with qualified staff to indicate their interest in providing the services. Interested consultants should provide information indicating that they have required qualifications and relevant experience to perform the services. The short listing criteria shall consider; the consultant eligibility, the description of similar assignments, experience in similar conditions, availability of appropriate skills among staff etc. Consultants may associate with other firms in the form of joint venture or sub consultancy to enhance their qualifications.

>>Read More>>

Read more

Wanajiosayansi waaswa kutathmini mchango wao katika Tanzania ya viwanda

Nuru Mwasampeta na Samwel Mtuwa, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaasa Wanajiosayansi kutathmini mchango wao katika maendeleo ya nchi, hususan katika maendeleo ya Tanzania ya Viwanda.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa wito huo tarehe 27/09/2018 alipokuwa akifungua Warsha ya siku Nne ya Wataalamu wa jiolojia iliyofanyika katika hoteli ya Dodoma jijini Dodoma yenye lengo la kutathmini mchango wa wanajiosayansi katika maendeleo ya viwanda nchini.

Mkutano huo pia unalenga katika kuwaleta pamoja wataalamu hao ili kujadili masuala mbalimbali ya sayansi ya dunia na umuhimu wake kwa jamii.

Akizungumzia umuhimu wa tasnia hiyo, Majaliwa alisema jiolojia ni sayansi inayogusa kila nyanja ya maisha ya binadamu ikiwemo kilimo kitokanacho na udongo utokanao na miamba, maji yapatikanayo ardhini, metali mbalimbali zipatikanazo ardhini kwa ajili ya matumizi katika viwanda ikiwa ni pamoja na vyanzo vya nishati vinavyohusiana moja kwa moja na jiolojia kama vile joto ardhi, makaa yam awe, mafuta na gesi na madini kama vile urani.

Kutokana na umuhimu huo mkubwa wa jiolojia Majaliwa amewataka watanzania kuendelea kutafuta utaalamu huo ili waweze kuchangia katika kuharakisha maendeleo ya nchi yetu.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali za asili nyingi kama vile madini, vito, mafuta gesi asilia, makaa ya mawe . Tanzania ni moja ya nchi chache duniani zilizobarikiwa kuwa na rasilimali hizi kwa wingi hivyo kupelekea kila majadiliano ya mali asili duniani Tanzania kutajwa pia,” alisisitiza.`

Aliongeza kuwa, kutokana na baraka ambazo nchi imejaliwa na Mwenyezi Mungu, nchi inanufaika kutoka na michango mikubwa miwili ya jiosayansi ya kwanza ikiwa ni mchango wake katika sekta ya viwanda, ambapo ili kuweza kufikia Tanzania ya Viwanda tunahitaji malighafi zizalishwe kwa wingi ili zitumike katika viwanda vinavyoanzishwa nchini.

Akizitaja malighafi hizo, Majaliwa  alisema ni kama vile madini ya  kinywe (graphite), jasi, chokaa, kaolini madini ambayo yanahitajika kwa wingikatika kuchochea uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Aidha, Majaliwa aliwataka wanajiolojia kuhakikisha kuwa  wanaonesha ni wapi madini hayo yanapatikana ili kuwawezesha watanzania na wawekezaji kuweza kuyapata na kuyatumia katika viwanda vyao. “Mnatakiwa mtuambie yako wapi na yana kiwango gani ili wazalishaji wa bidhaa za viwandani waweze kupata malighafi hizi kwa urahisi ili kuongeza tija katika viwanda vyetu hapa nchini.” Majaliwa alisisitiza.

Akizungumzia mchango wa pili mkubwa wa jiosayansi, Majaliwa alisema ni katika upatikanaji wa maji ya kutosha nchini. Alieleza kuwa ili kuwa na viwanda vinavyozalisha kwa ufasaha nchini maji lazima yawepo kwani ni bidhaa muhimu katika kuchangia maendeleo ya viwanda nchini.

Majaliwa alitanabahisha kuwa jukumu la wanajiolojia nchini ni kuonesha ni wapi maji yanapatikana ardhini kutokana na ukweli kuwa maji ya ardhini ni mara 5,000 ya maji yanayopatikana katika uso wa dunia.

Kwa kuzingatia kuwa maji yanapatikana popote ardhini aliwataka wataalamu hao kuandaa utaratibu utakaowezesha kuwa na takwimu za uhakika kuhusu kiwango cha maji, mahali yalipo na ujazo wake ili kuweza kuvutia uwekezaji wa viwanda kote nchini.

Aidha, alibainisha mchango mwingine mkubwa wa jiosayansi kuwa ni katika masuala ya nishati ambapo tutapata mchango kutokana na joto ardhi, rasilimali za gesi asilia ambapo gesi asilia pia imeshaanza kutumika katika viwanda vyetu nchini. Alisema, tafiti bado zinahitajika ili ufumbuzi uendelee na gesi yakutosha iweze kugunduliwa ili kutosheleza mahitaji ya sasa na baadaye ili kufikia malengo hayo na kueleza kuwa, jukumu hilo linawahusu wanajiolojia.

Akihitimisha hotuba yake ya ufunguzi, Majaliwa aliwataka wanajiolojia hao kujihoji endapo wanajua jukumu lao katika uboreshaji wa sekta ya madini, na endapo wao ni sehemu ya mabadiliko hayo. “Ni matarajio yangu kuwa kwa kushirikiana na Serikali ambayo tayari imejiimarisha Kisera na kimkakati ili kufikia azma ya viwanda, itakayokuwa tayari kuonesha uzalendo wenu na kuhakikisha mchango wenu katika hili unaonekana,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Angelleh Kairuki alikiri kwamba wizara  yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa wanajiolojia ikiwa ni pamoja na kupokea ushauri wa namna bora ya kuendesha na kuendeleza shughuli za madini nchini.

Aidha, Kairuki alibainisha kuwa wizara inakusudia na itakuwa mstari wa mbele  katika kuanzisha chombo maalumu cha usajili wa Wahandisi  ili kuondoa malalamiko ya watu yanayotokana na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kwa kujifanya ni wataalamu wa miamba na ukweli ikiwa sivyo.

Wizara ya madini kupitia taasisi zake itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanapokea mapendekezo yote yanayotolewa na wataalamu mbalimbali kuhusiana na namna bora ya uendeshaji sekta ya madini hapa nchini na kuyafanyia kazi.

Kutokana na fursa kubwa inayopatikana  katika  sekta ya madini, Kairuki aliwaasa wanajiosayansi kujikita kwenye uwekezaji unaoendana na taaluma yao kutokana na uwepo mkubwa wa rasilimali madini nchini ambayo bado hazijaendelezwa na hivyo kuongeza ufanisi na uwezo wa kiuchumi kwa wanajumuiya hiyo.

Zaidi ya hapo, Waziri Kairuki, alieleza kuwa wizara yake ipo katika mchakato wa kuiwezesha GST kuwa na uwezo wa kukusnya taarifa za kina ambazo zitabaini akiba ya mashapo ya madini mbalimbali yaliyopo nchini.

Uwepo wa taarifa hizo utasaidia kuwavuta na kuwarahisishia wawekezaji pindi wanapotafuta maeneo ya utafiti ili wapate leseni kwenye maeneo ambayo yana taarifa na takwimu za uhakika.

Alibainisha kuwa kasi hiyo itakwenda sambamba na kupitia upya Sera ya madini ya Mwaka 2009 ili iweze kuendana na Marekebisho ya sheria ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 pamoja na kanuni zake za mwaka 2018.

Warsha hii ya wanajiosayansi yenye kauli mbiu isemayo “ Jukumu la wanajiosayansi katika kuendeleza sekta ya viwanda” kwa mwaka huu, hufanyika kila mwaka mara moja.

Read more

Kairuki afanya mazungumzo na Rais wa FEMATA

Na Nuru Mwasampeta, Dodoma

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki leo tarehe 28 Septemba, 2018, amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina ambaye aliambatana na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho hilo, Bwana Haroun Kinega, ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini John W. Bina (Kulia) na kushoto kwa waziri ni Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji wadogo Haroun

Katika kikao hicho, Waziri Kairuki amewashukuru wajumbe hao kwa kumtembelea ofisini kwake na kujadiliana masuala mbalimbali katika sekta ya madini kwa lengo la kuboresha utendaji katika sekta ya madini, uchimbaji na wachimbaji wadogo kwa ujumla.

Aidha, Waziri Kairuki amewataka watanzania wenye mawazo chanya ya kukuza sekta ya madini kutosita kufika na kutoa maoni yao ili Serikali iweze kuyafanyia kazi ili kuboresha sekta hiyo kwa manufaa ya jamii nzima ya watanzania na hivyo kuifanya sekta kuchangia zaidi katika pato la taifa, ajira na kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumzia lengo la kufika wizarani hapo, Rais wa FEMATA, John Bina amesema ni kujadili kuhusu mafanikio, changamoto, fursa za wachimbaji wadogo zilizopo katika sekta husika pamoja na kujadili namna ya kuendeleza sekta ya uchimbaji mdogo wa madini nchini ikiwa ni pamoja na namna ya kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.

Read more

Nyongo autaka Mgodi wa Geita kuwalipa fidia wananchi

Na Rhoda James, Geita

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameutaka Mgodi wa Geita Gold Mine Ltd kuwalipa fidia wananchi waliopata madhara ya nyufa katika katika nyumba zao kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini wa kampuni hiyo.

Wananchi kutoka Mkoa wa Geita na Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo tarehe 26 Septemba, 2018 wakati alipofungua Maonesho ya Kwanza ya Teknolojia ya Uchimbaji na Uwekezaji wa Madini ya Dhahabu mkoani Geita kwa niaba ya Waziri wa Madini, Angellah Kairuki.

Alitoa rai kwa Wachimbaji wadogo wa madini kote nchini kushiriki maonesho hayo yanayoendelea mkoani humo kwa kuwa yatawanufaisha kwa kupata fursa ya kujifunza kuhusu teknolojia mbalimbali na namna bora ya uchimbaji, uchenjuaji, ikiwemo kupata elimu ya kulinda mazingira na kuzalisha kwa tija.

Pia, aliwataka Wakuu wa mikoa yote nchini pamoja na Wakuu wa wilaya zote kujifunza kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi ili kuhakikisha kuwa wananchi wao wanafaidika na rasilimali pamoja na mazao yanayolimwa katika maeneo yao.

“Mkifanya maonesho ya aina hii katika mikoa yenu kulingana na mazao au rasilimali mlizonazo katika mikoa yenu wananchi wenu watafaidika,” alisema Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.

Vilevile, Naibu Waziri Nyongo, aliwataka wananchi wa   mkoa wa Geita na Kagera pamoja na wadau wa madini ya dhahabu kujipanga ili kuhakikisha kuwa maonesho hayo yanafanyika kila mwaka.

Pia, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana na uongozi kutoka Mkoa wa Geita kuhakikisha kuwa wanayatangaza maonesho hayo kwa kiasi kikubwa ili yaweze kufahamika duniani kote hatimaye wadau wa madini waweze  washiriki kwa wingi.

“Wateja wengi wa madini wanatoka nje ya nchi na ni vyema pia wakajua chanjo cha madini hayo kiko wapi,” alisema Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) alipowatembelea katika Viwanja vya CCM Kalangalala mkoani Geita.

Akizungumzia mchango wa Sekta ya madini katika pato la taifa, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa, mchango wa Sekta ya Madini bado ni kidogo na kuongeza kuwa, malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, mchango wake unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

“Mwaka 2016 na 2017 sekta ya madini imechangia kwenye pato la taifa asilimia 4.8 lakini tunatarajia ifikapo 2025 sekta ya madini itachangia zaidi ya asilimia10,” alisema Nyongo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Nyongo ametoa onyo kwa wachimbaji wadogo kuachana na tabia ya kutorosha madini na kueleza kuwa, atakayekamatwa akifanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia, Naibu Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuupongeza Mkoa wa Geita na wadau mbalimbali akiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Bishara Tanzania (TanTrade) pamoja na Wizara ya Madini kwa kuandaa maonesho ya madini ya dhahabu mkoani Geita.

Pia, amewapongeza umoja wa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya dhahabu (GEREMA) kwa kuhakikisha kuwa Maonesho hayo yanafanyika kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel Luhumbi alisema kuwa, ni matarajio yake kuwa maonesho hayo yatakuwa ya kitaifa na hatimaye ya dunia nzima na kuongeza kuwa, anataka maonesho hayo ya madini ya dhahabu kufanyika kila mwaka mkoani kwake.

Pia, alisema alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara ya madini kwa ushirikiano inayotoa kwa wachimbaji wadogo kupitia taasisi za GST na STAMICO.

Read more

Wajumbe wa Bodi Zabuni Madini watakiwa kuepusha hoja za manunuzi

Na Asteria Muhozya, Morogoro

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini kuhakikisha kwamba wizara hiyo haipati hoja kutokana na kukikukwa kwa taratibu za manunuzi baada ya wajumbe hao kupatiwa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi

Pia, wajumbe hao  wametakiwa kuhakikisha wanafamu kwa weledi  Sheria na Kanuni za manunuzi ili  waweze kutoa maamuzi sahihi.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Wizara hiyo  yaliyofanyika katika ofisi za Madini Mkoa Morogoro tarehe 21 Septemba,2018.

Naibu Waziri Nyongo alisema hitaji la kuwapatia mafunzo wajumbe hao linafuatia upya wa wizara hiyo ikiwemo wajumbe wa bodi hiyo ambao wengine wametoka katika sekta mbalimbali hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuzingatia sheria na kanuni  za manunuzi zilizoanishwa.

“Masuala ya manunuzi yanalalamikiwa sana kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi. Lakini pia, manunuzi ya umma yamekuwa na matatizo kutokana na kuwepo Mikataba mibovu kwa hiyo baada ya ninyi kupatiwa mafunzo haya, sitarajii vitu kama hivi kujitokeza.

Pia, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wajumbe wa bodi kuhakikisha kuwa, mafunzo waliyoyapata yanawasaidia kuepukana na vitendo vya rushwa wakati wa kusimamia shughuli za manunuzi ya wizara.

“Ukiiba mali ya umma kuna siku wengine watakuja na watahoji. Siku zote mali ya umma ni ya kuogopa,” alisisitiza Naibu Waziri nyongo.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakiwa wakijadiliana wakati wa mafunzo kuhusu masuala ya manunuzi kwa wizara hiyo

Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo  ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Wizara ya Madini, Issa Nchasi,  alisema kuwa, wakati wa mafunzo wajumbe hao walipata nafasi ya kujifunza kuhusu Sheria, Mikataba na Kanuni za Manunuzi ikiwemo kupata uzoefu wa shughuli za manunuzi na namna zinavyofanyika.

Akizungumzia manufaa ya mafunzo, Nchasi alisema kuwa yamekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa yatawawezesha wajumbe  kutoa maamuzi sahihi ikiwemo kumshauri Afisa Masuhuli kufuata Sheria na Kanuni ili kuepuka ununuzi ambao hauzingatii sheria.

Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wajumbe kuelewa Sheria ili kufanya kazi zao kwa weledi.

Kwa upande wake, Mkufunzi kutoka Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Paschal Komba aliipongeza wizara ya Madini kwa kutoa mafunzo hayo kwa wajumbe wa bodi hiyo na kuelea kuwa, yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na taratibu za ununuzi wa umma.

Mafunzo hayo yalitolewa na Wataalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA).

Read more

Naibu Waziri Biteko atatua mgogoro machimbo ya madini Bunda

 • Atoa miezi miwili kwa mwekezaji kulipa fidia wananchi

Na Greyson Mwase, Bunda

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametatua mgogoro mkubwa wa siku nyingi uliokuwepo kati ya wananchi wa kijiji cha Kunanga kilichopo ndani ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara na kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Lake Victoria kwa kuitaka kampuni  kuhakikisha imelipa fidia kwa wananchi wote ndani ya  kipindi cha miezi miwili.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kunanga kilichopo katika wilaya ya Bunda mkoani Mara. (hawapo pichani)

Naibu Waziri Biteko aliyasema hayo leo tarehe 21 Septemba, 2018 mara baada ya kufanya ziara kwenye machimbo na kusikiliza kero za wachimbaji wadogo kupitia mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya Mara na Geita yenye lengo  la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja kusikiliza na kutatua kero mbalimbali.

Ziara hiyo katika machimbo hayo inatokana na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyoyatoa katika mkoa wa Mara kwenye ziara yake  aliyoifanya kuanzia tarehe 05 hadi 07 Septemba  mwaka huu ya kumtaka Naibu Waziri wa Madini kuhakikisha ametatua mgogoro husika.

Katika ziara hiyo, Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl. Lidia Bupilipili, Rais wa Chama cha Wachimbaji Madini Nchini, John Bina, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mara, Stephan Msseti, Mbunge wa Bunda Vijijini, Boniphace Getere, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya, Watendaji kutoka Wizara ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

Alisema kuwa, baada ya kusikiliza maelezo kutoka pande zote mbili alibaini kuwa wanachi walikuwa na haki ya kulipwa fidia na kumtaka mwekezaji kuhakikisha kuwa anafuata sheria na kanuni za madini kwa kuhakikisha amefanya tathmini na kuwalipa fidia ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Aliendelea kufafanua kuwa, zipo taratibu zinazotakiwa kufuatwa na wawekezaji wote kwenye madini ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa Wakuu wa Wilaya, Vijiji na wananchi na kufanya mazungumzo na kuweka makubaliano ya fidia pamoja na kulipa kabla ya kuanza rasmi shughuli za uchimbaji madini.

“Haiwezekani kamwe mwekezaji anapewa leseni na Ofisi ya Madini anakwenda moja kwa moja kwa wananchi tena akiwa na walinzi na kuanza kuwafukuza bila hata kujitambulisha na kufanya mazungumzo, hii inahatarisha usalama na uhusiano kati ya mwekezaji na wananchi wa sehemu husika,” alisema Naibu Waziri Biteko.

Mkuu Wilaya ya Bunda, Mwl. Lidia Bupilipili akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko alimtaka Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Lake Victoria, Ahmed Magoma na Mkuu wa  Wilaya ya Bunda, Mwl. Lidia Bupilipili kufanya mkutano na wananchi ili kutafuta mustakabali wa fidia na kumpatia taarifa.

Aidha, alimtaka  mwekezaji kuomba kikao na Serikali ya Kijiji kabla ya siku ya Jumatano ya wiki ijayo ya tarehe 26 Septemba mwaka huu na kuendelea kumtaka kuhakikisha anashirikiana na wananchi kwa karibu zaidi na kudumisha mahusiano.

Pia Waziri Biteko alimtaka mwekezaji kuhakikisha analipa deni la Dola za Kimarekani 46,080  Serikalini ndani ya kipindi cha siku 45 tangu alipoandikiwa hati ya makosa kama mojawapo ya uvunjifu wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake.

Wakati huohuo, Naibu Waziri Biteko alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara, Nyaisara Mgaya kuhakikisha eneo lililobaki lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5.12 lililotolewa na mwekezaji linagawanywa na kupewa kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Katika hatua nyingine, akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri Biteko alisikitishwa na kitendo cha wachimbaji wadogo wa madini kutokulipa mrabaha serikalini hali inayoikosesha Serikali mapato yake stahiki.

Alielekeza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mwl. Lidia Bupilipili na Mwenyekiti wa kijiji cha Kunanga, Kisire Marwa kukaa kwa pamoja na kuchunguza kiasi cha fedha zinazodaiwa kulipwa na wachimbaji wadogo wa madini katika serikali ya kijiji na matumizi yake na kisha kutoa taarifa kwa wananchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Lake Victoria, Ahmed Magoma akielezea historia ya mgogoro kati ya kampuni yake na wananchi wa kijiji cha Kunanga kilichopo katika wilaya ya Bunda mkoani Mara kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko. (hayupo pichani)

“Wachimbaji hawa wanadai kuwa  wanalipa fedha katika serikali ya kijiji, kiasi halisi hakijulikani wala matumizi yake, fedha hizi zinatakiwa ziwanufaishe kupitia uboreshaji wa huduma za jamii,” alisema Biteko.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haipo tayari kuona mwekezaji au mchimbaji yeyote ananyanyasika na kufafanua kuwa kila mwananchi ni sehemu ya rasilimali za madini.

Pia, aliwataka wananchi kutii sheria ya madini pamoja na kanuni zake na kuongeza kuwa wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaowekeza kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji madini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Lake Victoria, Ahmed Magoma akizungumza mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri Biteko, aliomba msamaha kwa wananchi wa kijiji cha Kunanga na kueleza kuwa atatekeleza maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano kati yake na wananchi husika ili uchimbaji wa madini ufanyike kwa amani na kila upande uweze kufaidika

Naye Mkuu wa  Wilaya ya Bunda, Mwl. Lidia Bupilipili pamoja na pongezi kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alisema kama serikali watafuatilia kwa karibu mapato na matumizi  ya fedha zinazodaiwa kulipwa katika serikali ya kijiji cha Kunanga na kuchukua hatua kwa waliohusika na ufujaji wa fedha hizo.

Read more

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Mara wakutana kujadili taarifa ya uchunguzi wa Trust Fund

Na Greyson Mwase,

Leo tarehe 20 Septemba, 2018 mjini Musoma mkoani Mara, Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima wamekutana na  Wakuu wa Wilaya, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Mara, Watendaji kutoka Wizara ya Madini kwa ajili ya kujadili taarifa iliyowasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza matumizi ya mfuko wa North Mara Trust Fund kabla ya kutoa maelekezo ya Serikali.

Read more

Mwenyekiti wa Tume ya Madini akutana na Balozi wa India nchini

Na Greyson Mwase, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 13 Septemba, 2018 amekutana na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya jijini Dodoma. Lengo la ziara ya Balozi Arya kwenye Ofisi ya Mwenyekiti wa Tume ya Madini lilikuwa ni kujitambulisha pamoja na kufahamu majukumu ya Tume.

Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula zilizopo jijini Dodoma

Akizungumza katika kikao hicho, Profesa Kikula alieleza kuwa Tume ya Madini imejipanga kusimamia Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 na  kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya madini nchini

Alisema Sheria ya Madini ina  matakwa yake kama vile  local content, utoaji wa huduma kwa jamii kwenye shughuli za uchimbaji madini (corporate social responsibility) na kiapo cha uadilifu kwenye shughuli za uchimbaji madini (integrity pledge)

Alisema kuwa Tume imejipanga pia kutoa leseni haraka iwezekanavyo na kuwasaidia wachimbaji wadogo.

Akizungumzia namna Tume ya Madini ilivyojipanga katika kutatua changamoto ya migogoro kwenye Sekta ya Madini Nchini, Profesa Kikula alisema kuwa Tume inaandaa mpango  wa kutatua migogoro kuanzia katika ngazi ya kijiji, kata, wilaya na taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa migogoro mingi inatatulika katika mamlaka za Vijiji, Kata na Wilaya. Aidha, Profesa Kikula alimwomba Balozi wa India kuendelea kutoa ufadhili kwa wataalam wa Tume ya Madini hususan  katika maeneo ya Uchimbaji wa Madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Usimamizi wa Rasilimali Watu na maeneo  mengine ili  kukuza Sekta ya Madini Nchini.

“ Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, na kama Tume  kwa kushirikiana na  Wizara ya Madini tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na wataalam wenye weledi kwenye usimamizi  wa Sekta ya Madini. Hivyo basi mafunzo  kwa wataalam  tunayapa kipaumbele sana,” alisisitiza Profesa Kikula.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akielezea majukumu ya Tume ya Madini kwa Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (hayupo pichani)

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula alimwomba Balozi wa India kuendelea kutangaza Sekta ya Madini Nchini na kusisitiza kuwa Tanzania ina maeneo mengi yenye madini yaliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Jiolojia na  Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

Alisisitiza kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali.

Wakati huo huo Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya alisema kuwa nchi ya India ipo  tayari kushirikiana na  Tume ya Madini hususan  katika Sekta ya Madini na kusisitiza kuwa wapo tayari kutoa ufadhili kwa watumishi wa Tume.

Aliendelea kusema kuwa nchi ya India imekuwa ikitoa mafunzo ya muda mrefu  hususan katika ngazi za Shahada za Uzamili na za Uzamivu katika vyuo bora na kusisitiza kuwa itaendelea na mpango wake wa kutoa mafunzo hususan kwenye masuala ya madini.

Katika hatua nyingine,  Balozi Arya alimpongeza Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula kwa kuteuliwa kuongoza Tume hiyo pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Tume ya Madini kwenye uboreshaji wa Sekta ya Madini Nchini.

Read more

Serikali yakusudia kuondoa kodi vifaa vya uongezaji thamani madini

Na Asteria Muhozya, Arusha

Serikali imesema inaangalia uwezekano wa kuondoa kodi ya vifaa vya uongezaji thamani madini  ikilenga kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini  kufanyika nchini.

Mmoja wa Wanafunzi wanaofanya mafunzo ya ukataji na unga’rishaji madini ya vito katika Kituo ch Jemolojia Tanzania (TGC).

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akijibu swali la mwanafunzi wa Kituo Cha Jemolojia Tanzania (TGC) Rojer Mpele aliyeiomba Serikali kupitia Naibu Waziri kuangalia namna ya kupunguza kodi ya vifaa hivyo ili  kuwasaidia wanafunzi wanaojifunza ukataji na ung’arishaji madini katika kituo hicho kuweza kujiajiri baada ya kuhitimu .

Nyongo ameongeza kuwa, tayari Serikali imeanza kufanya taratibu za kupeleka maombi  kuhusu jambo hilo katika Mamlaka husika ili liweze kufanyiwa kazi kwani litahamaisha uwekezaji wa viwanda vya uongezaji thamani madini nchini ikiwemo kuongeza wigo wa ajira na mapato kupitia sekta ya madini.

Naibu Waziri Nyongo amekitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujifunza shughuli zinazofanyika kituoni hapo. Kituo cha TGC kipo chini ya Wizara ya Madini, kinatoa mafunzo ya ukataji na ung’arishaji madini ya vito lengo likiwa ni kuongeza thamani madini.

Ameongeza kuwa suala la uongezaji thamani madini nchini ni jambo ambalo  ni  kipaumbele cha serikali kutokana na Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Maboresho yake ya Mwaka 2017 na kwamba tayari serikali imezuia usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi na badala yake inahamasisha shughuli hizo kufanyika hapa hapa nchini kwa kuwa, zitawezesha kuleta ujuzi, ajira, mapato zaidi ya serikali na kuyaongezea thamani madini hayo nchini kabla hayajasafirishwa nje ya nchi.

“Bado Wizara inaweka msisitizo wa shughuli za uongezaji thamani zifanyike hapa nchini. Kwa hiyo napenda kuwaambia ninyi vijana mnajifunza kitu ambacho ni kipaumbele kwa wizara na serikali,” amesisitiza Naibu Waziri.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiangalia moja ya Mashine zinazotumika kufanisi madini ya vito na miamba wakati alipotembelea Kituo cha jemolojia Tanzania (TGC).

Aidha, Naibu Waziri amesema kuwa, serikali kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) unaotekelezwa  chini ya wizara kutokana na mkopo wa Benki ya Dunia, tayari umeagiza vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuanzisha karakana ya shughuli za uongezaji thamani madini katika kituo hicho, karakana hiyo inalenga kutumiwa na wahitimu wa kituo husika ili kwawezesha kujiajiri pindi wanapohitimu mafunzo yao.

“Watakaohitimu hapa watalipia gharama ndogo sana za mashine watakazokuwa wakizitumia kufanya kazi zao katika karakana hiyo. Lakini pia, ili kuboresha shughuli za karakana hiyo, tutaendelea kujifunza kwa nchi nyingine namna wanavyoendesha karakana zao,” ameongeza Nyongo.

Katika jitihada za kuendelea kukiboresha kituo husika, Naibu Waziri Nyongo amemtaka Mratibu wa Kituo hicho, kuandaa  Mpango Mkakati wa namna ya kukiboresha na kukitanua kituo hicho ili kiweze kuwa bora na mfano kwa nchi  nyingine  barani Afrika.

“Imefika wakati ambapo tunataka TGC kuwa chombo ambacho kinatoa ujuzi wa hali ya juu katika uongezaji thamani madini. Lazima tutoe mafunzo kwa vijana wa kitanzania  na tuendelee kuangalia namna ya kuleta ujuzi au kwa kuwapeleka vijana wetu kujifunza kwa wenzetu na baadaye wawe wakufunzi katika kituo hiki.

Vilevile, Naibu Waziri Nyongo amesisitiza kuwa, Serikali kupitia wizara ya Madini itaendelea kusimamia kwa karibu kuhakikisha kuwa inatekeleza na kutimiza malengo ya uanzishwaji wa kituo hicho. “Lazima ifike mahali kituo kitoe mafunzo kwa jinsi ilivyokusudiwa, ameongeza Nyongo.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akipata ufafanuzi kutoka kwa Mjiolojia na Mkufunzi wa Ukataji na Unga’rishaji wa madini ya vito kutoka katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Ester Njiwa, kuhusu namna mashine ya kunga’risha madini inavyofanya kazi wakati alipokitembelea kituo hicho. Mkufunzi huyo aalipata mafunzo kutoka nchini Sri-Lanka.

Kwa upande wake,  Kaimu Mratibu wa Kituo cha TGC, Eric Mpesa amesema kuwa, kituo hicho ni kituo pekee Afrika Mashariki kinachoendeleza taaluma ya uongezaji thamani madini ya vito na miamba.

Pia, amesema kuwa, kituo kinakusudia kutoa mafunzo ya Diploma ya Gem Jewelly technology ambapo mhitimu katika mwaka wa Kwanza atapatiwa cheti cha NTA Level 4, mwaka wa pili NTA Level 5 na mwaka wa tatu NTA Level 6.

“Kwa kuwa mafunzo yanayotolewa katika kituo hiki ni ya muda mrefu na mfupi, taratibu za kukisajili kwenye Baraza la taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) zilifanywa na kwa sasa kituo kimepata usajili wa kudumu wenye Na. REG/SAT/003,” ameongea Mpesa.

Mpesa ameongeza kuwa, wizara iliamua kuwekeza katika Kituo hicho kwa lengo la kutoa mafunzo ya kuongeza thamani madini ya vito kwa wadau na wajasiliamali wa madini hayo hapa nchini.

Ameongeza kuwa, malengo mengine ni pamoja na kukuza na kuendeleza ujuzi na ufahamu wa kutambua madini ya vito, kuongeza thamani kipato na ajira kwa watanzania.

“ Hivi sasa kituo hicho kinatoa mafunzo ya muda mfupi ya ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito na kinaendesha shughuli za uchongaji wa mawe ya miamba kwa kutengeneza  wanyama, ndege, samaki na vitu mbalimbali vya mapambo, amesema Mpesa.

Kituo cha Jemolojia Tanzania (Tanzania Gemological Center -TGC) kilianzishwa mwaka 2003 wakati serikali ikitekeleza mradi wa Maendeleo Sekta ya Madini ( Mineral Sector Development Technical Assistance – MSD TA) ambao ulitekelezwa kati yam waka 1994 na 2005 kwa mkpo kutoka benki ya Dunia. Wakati huo lengo la kuanzissha kituo hicho lilikuwa ni kutekeleza Sera ya Madini ya Mwaka 1997 kuhusu uongezaji thamani madini nchini kwa kuanzia na kutoa mafunzo ya uchongaji wa vinyago vya miamba.

Read more

Profesa Kikula atoa mwezi mmoja utatuzi wa mgogoro wachimbaji madini Winza

Na Greyson Mwase, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ametoa mwezi mmoja kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha mgogoro katika machimbo ya madini aina ya rubi yaliyopo katika kijiji cha Winza kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma unamalizika ili wachimbaji hao waendelee na shughuli zao za uchimbaji madini na kujipatika kipato.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Sarah Komba (kulia) mara baada ya kuwasili kweye Ofisi ya Katibu Tawala huyo.

Profesa Kikula ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea kero za wachimbaji wadogo wa madini katika eneo hilo katika ziara yake katika wilaya ya Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wachimbaji wadogo wa madini.

Katika ziara hiyo Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.

Alimtaka Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto na  Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kushirikiana kwanza kwa kuchukua alama za eneo (coordinates) ili kubaini maeneo yasiyo na leseni na kuwapatia wachimbaji hao ili wafanye uchimbaji bora wenye kufuata sheria na kanuni za madini.

Aliendelea kufafanua kuwa, kwa maeneo yenye leseni wachimbaji wadogo wa madini wanaweza kuangalia namna ya kushirikiana na wamiliki wa leseni kwa kuingia ubia na kujipatia kipato pasipo migogoro isiyo ya lazima.

Profesa Kikula alisisitiza kuwa lengo la Serikali kupitia Tume ya Madini ni kuona wachimbaji wadogo wa madini wanafanya shughuli zao katika mazingira mazuri kwa kufuata kanuni na sheria za madini.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wachimbaji hao kuunda vikundi vidogo na kuomba leseni na kusisitiza kuwa Tume ya Madini ipo tayari  kuwasaidia kwa njia zote kupitia wataalam wake ikiwa ni pamoja na namna ya kuomba leseni za madini, elimu kuhusu kanuni na sheria za madini.

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya kijiji cha Winza kilichopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Wakiwasilisha kero zao kwa Mwenyekiti Kikula kwa nyakati tofauti, wachimbaji hao walisema kuwa wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa muda mrefu pasipokuwa na leseni huku kukiwepo na watu wanaojitokeza na kudai kuwa ni wamiliki halali wa leseni za madini.

Awali akielezea historia ya ugunduzi wa madini aina ya rubi katika eneo hilo, mgunduzi ambaye ni mwenyeji wa kijiji hicho,  Shabani Kigelulye alisema kuwa, kati ya mwaka 2005 na 2006 akiwa shambani kwake katika eneo hilo aligundua mawe aliyohisi kuwa ni madini ya rubi.

Alieleza kuwa, katika harakati za utafiti wa  madini hayo mwaka 2007 alipeleka sampuli za mawe hayo aliyohisi kuwa ni madini ya rubi kwa ndugu wake walioko Dodoma Mjini na Arusha na kuelezwa kuwa yalikuwa ni madini ya rubi.

Aliendelea kueleza kuwa kwa kushirikiana na ndugu zake alipeleka sampuli hizo za mawe kwenye Ofisi za Madini na kushauriwa kuomba leseni na kupata.

Aliongeza kuwa  mwaka 2008 aliingia ubia na  wenzake Roja Sezinga, Johnson Kamara na Perfect Shayo na kuanza uchimbaji wa madini, na kusisitiza kuwa mwaka 2009 wakazi wengi wa kijiji hicho waliingia na kuanza kuchimba kiholela pasipokuwa na leseni hali iliyopelekea mgogoro.

Katika hatua nyingine Profesa Kikula alitembelea eneo lililopangwa kujengwa mtambo wa kuyeyushia shaba na kukuta jengo lililotelekezwa tangu mwaka 2004

Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA), Kulwa Mkalimoto alimweleza Profesa Kikula na timu yake kuwa, kampuni ya Igozomo kutoka China ilipanga kujenga mtambo wa kuyeyushia shaba lakini baadaye walisitisha uwekaji wa mtambo huo baada ya kutoelewana na wazawa.

Jengo lililojengwa kwa ajili ya kusimikwa mtambo wa kuyeyushia shaba na kampuni ya Igozomo ya China lililopo katika kijiji cha Winza wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Profesa Kikula alishauri wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye shughuli za madini nchini kukutana na wenyeviti wa vyama vya wachimbaji madini ambao wanaweza kuwapa taratibu sahihi za uwekezaji nchini hivyo kuepuka kuingia kwenye mikono ya matapeli.

Wakati huohuo akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Sarah Komba, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula alisema kuwa suala ushiriki wa huduma za jamii (corporate social responsibility) kwa makampuni ya madini nchini si la hiari bali ni moja ya sheria.

Aliendelea kufafanua kuwa ni vyema kukawepo  mikataba kati ya wakuu wa wilaya na kampuni za madini kuhusu maeneo yanayohitaji katika uboreshaji wa huduma za jamii na kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na huduma zilizoainishwa kwenye mikataba na kupunguza migogoro.

“Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka  mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wananufaika na rasilimali za madini kupitia ushirikishwaji wananchi kwenye utoaji wa huduma kwenye kampuni za madini (local content) na kupata huduma bora za jamii kutokana na uwekezaji unaofanywa na kampuni za madini,” alisisitiza Profesa Kikula.

Akielezea mikakati ya kumaliza migogoro kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini nchini, Profesa Kikula alisema kuwa Tume ya Madini inaandaa rasimu ya mfumo wa utatuzi wa migogoro  kuanzia kwenye ngazi ya kijiji, kata na wilaya kabla ya kufikia ngazi ya tume.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa, Sarah Komba alimpongeza na kumshukuru Profesa Kikula pamoja na timu yake kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutatua changamoto kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini na kutoa elimu kuhusu sheria na kanuni za madini.

Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega (kushoto) akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Winza yaliyopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Aidha Komba aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kutoa taarifa za wavamizi wasiokuwa na leseni za madini ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akizungumza katika mahojiano maalum na vyombo vya habari aliwataka wananchi wanaogundua madini kwenye maeneo yao kutoa taarifa kwenye ofisi za vijiji na vyama vyama vya wachimbaji madini na kufika kwenye Ofisi za Madini  kwa ajili ya utambuzi wa madini na  kuelekezwa namna ya kuomba leseni.

Alisema kutokana na wagunduzi wengi kuchimba bila kushirikisha uongozi wa kijiji, wilaya na vyama vya wachimbaji madini wamejikuta wakitoa mwanya kwa wajanja kuomba leseni hivyo kuzalisha migogoro isiyokwisha.

Alisema kuwa Serikali kupitia Tume ya  Madini imeweka utaratibu mzuri sana wa kumlinda mgunduzi wa madini tangu anapogundua madini hayo hadi kupata leseni.

Read more

Prof. Kikula aagiza kikundi cha wachimbaji madini kupewa leseni ndani ya mwezi mmoja

Na Greyson Mwase, Dodoma

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amemwagiza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya kuhakikisha wanakipatia kikundi cha wachimbaji wadogo wa madini kijulikanacho  kwa jina la “Hapa Kazi Tu” kinachoendesha shughuli za uchimbaji wa madini aina ya sunstone katika kijiji cha Suguta wilayani Kongwa mkoani Dodoma leseni ya uchimbaji madini ndani ya mwezi mmoja kwa kufuata kanuni na sheria za madini.

Sehemu ya wachimbaji wadogo wa madini wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (hayupo pichani) kwenye machimbo ya Suguta yaliyopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Profesa Kikula alitoa agizo hilo tarehe 05 Septemba, 2018 katika  machimbo ya madini hayo yaliyopo katika kijiji hicho kwenye ziara yake ya siku mbili katika wilaya za Kongwa na Mpwapwa yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji madini zinazofanywa na wachimbaji wadogo, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.

Katika ziara hiyo, Profesa Kikula aliambatana na Makamishna wa Tume, Profesa Abdulkarim Mruma na Haroun Kinega, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma, Nicas Sangaya pamoja na waandishi wa habari.

Mara baada ya kusikiliza kero za wachimbaji wadogo hao Profesa Kikula mbali na kutoa  agizo hilo alimwelekeza Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini mkoani Dodoma (DOREMA),  Kulwa Mkalimoto, kuhakikisha anasaidia kikundi cha wachimbaji wadogo hao katika taratibu zote za usajili wa kikundi  kabla ya kuanza kushirikiana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma katika upatikanaji wa leseni ndani ya mwezi mmoja.

Aidha, Profesa Kikula alimtaka Mwenyekiti huyo kuwasaidia wachimbaji hao katika usajili kwenye vyama vya  wachimbaji madini Tanzania pamoja na utafutaji wa masoko na bei elekezi kwenye masoko ya kimataifa.

“Kutokana na kuwa na mtandao mkubwa na uelewa kwenye masoko na bei elekezi za madini kwenye masoko ya kimataifa, nakuelekeza kama Mwenyekiti wa wachimbaji kuhakikisha unawasaidia wachimbaji hawa hususan kwenye maeneo ya masoko na bei elekezi ili uchimbaji wao uwanufaishe wao na Serikali kupata mapato stahiki,” alisema Profesa Kikula.

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie. Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Madini, Haroun Kinega.

Profesa Kikula alisema Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia uboreshaji wa sheria na kanuni za madini pamoja na utoaji wa elimu kwa wachimbaji wadogo kuhusu sheria na kanuni hizo.

Katika hatua nyingine, Profesa Kikula aliwataka wachimbaji wadogo nchini kuhakikisha kupitia viongozi wao kwenye vyama vya  wachimbaji madini wanashirikiana kwa karibu na viongozi wa vijiji, wilaya na ofisi za madini ili uchimbaji wao ulete tija zaidi kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Awali, wakiwasilisha kero mbalimbali wachimbaji hao walisema kuwa wamekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali kwenye usajili wa kikundi chao hali iliyopelekea ucheleweshwaji wa maombi ya leseni.

Akizungumza kwa niaba ya kikundi hicho, Job Pandila alisema awali waliwasilisha maombi yao kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ajili ya taratibu za usajili lakini kumekuwa na ugumu katika usajili wa kikundi chao kutokana na kutokuwa na uelewa wa namna bora ya kuwasilisha viambatisho kwenye maombi ya usajili wa kikundi.

Pandila aliendelea kusema kuwa uchelewaji wa usajili wa kikundi umepelekea kushindwa kuomba leseni ya madini na kuomba msaada katika usajili wa kikundi pamoja na maombi ya leseni ili waendelee na uchimbaji wa madini na kujipatika kipato.

Awali kabla ya kufika katika kijiji cha Suguta, Profesa Kikula alikutana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie na kuelezwa changamoto mbalimbali kwenye shughuli za uchimbaji madini zilizopo katika wilaya ya Kongwa.

Sehemu ya mgodi wa shaba wa Rays Metal Corporation uliopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembie alisema kumekuwepo na mgogoro kwenye eneo la Suguta lililopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma kutokana na wachimbaji wengi kutokuwa na leseni za uchimbaji madini pamoja na uelewa mdogo wa sheria na kanuni za uchimbaji madini.

Aidha,  Ndejembie alimpongeza Profesa Kikula na timu yake kwa kutembelea wilaya ya Kongwa na kusisitiza kuwa ziara hiyo mbali na kutoa elimu kwa wachimbaji madini, itapunguza migororo isiyo na lazima iliyokuwa ikijitokeza.

Wakati huo huo katika kikao chake na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Profesa Kikula aliwataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini kuandaa utaratibu wa utoaji wa mafunzo kwa wachimbaji madini kuhusu sheria na kanuni za uchimbaji madini.

Katika ziara hiyo Profesa Kikula pamoja na ujumbe wake, walitembelea pia machimbo ya Rays Metal Corporation na Tambi Minerals Resources yaliyopo katika kijiji cha Tambi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Read more

Media Release-Australia’s Kibaran says global opportunity for battery grade graphite is unequivocal

An Australian company set to contribute more than US$1.0 billion to the Tanzanian economy over the next 20 years through local graphite mine projects, says the global market opportunity for battery grade graphite is unequivocal.

Speaking on the second day of the three day Paydirt 2018 Africa Down Under mining conference in Perth, Kibaran Resources Chairman, Mr Robert Pett, said the market opportunity for the commodity was “now” despite a lot of “noise” around the battery component supply chain and forecast supply and demand estimates.

“A raft of high end, credible industry and government agencies have initiated substantial modelling around graphite and the opportunity it presents is quite clear,” Mr Pett said.

“Standout and verifiable conclusions range from the expected presence of one billion electric vehicles on the world’s roads by 2025 under a lithium-ion battery market momentum worth US$290 billion by 2025,” he said.

“Some 47% of the lithium-ion battery market will require a component contribution from spherical graphite and this will generate a 700% increase in natural flake spherical graphite demand in just the next seven years.

“This will stretch global consumption of natural flake spherical graphite from 127,000 tonnes currently per annum to 800,000tpa.”

Cobalt, nickel, lithium and manganese would fulfil the suite of ingredients needed for lithium-ion battery production.

Mr Pett also pointed to the accelerating demand from the energy industry for domestic and industrial application lithium-ion battery storage options.

>>Read More>>

Read more

Naibu Waziri Biteko afanya ziara ya kushtukiza mgodi wa MMG na kubaini madudu

 • Abaini raia wa kigeni 10 wasio na vibali vya kazi waliokuwa wamejificha ndani ya mgodi
 • Atoa wiki moja mikataba ya ajira kwa wafanyakazi

Na Greyson Mwase, Musoma

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 29 Agosti, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza katika Mgodi wa Dhahabu wa MMG unaomilikiwa na kampuni ya Waarmenia uliopo katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Meneja Uendeshaji wa Mgodi wa Dhahabu wa MMG, Sezgey Sazgyyan (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye mgodi huo kwa ajili ya ziara yake tarehe 29 Agosti, 2018.

Mara baada ya kuwasili katika mgodi huo na kupata maelezo ya namna ya uendeshaji wa mgodi huo kutoka kwa Meneja Uendeshaji,  Sezgey Sazgyyan aliendelea na  ukaguzi wa mgodi na kubaini ukiukwaji wa  kanuni za usalama migodini ikiwa ni pamoja na watumishi kufanya  kazi katika mazingira hatarishi pasipokuwa na  vifaa vya usalama mgodini.

Mara baada ya kutoa maelekezo, Naibu Waziri Biteko alifanya kikao na uongozi wa mgodi pamoja na wafanyakazi wa mgodi huo lengo likiwa ni kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuzitatua.

Akitoa maelezo kuhusu idadi ya wataalam wa kigeni na wa kitanzania katika mgodi huo wakati wa uwasilishaji wa  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mgodi huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017 Afisa Utumishi wa mgodi huo,  Rose Masanja alisema mgodi mpaka sasa una wafanyakazi 126 wa kitanzania ambao ni pamoja na vibarua kutoka katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa mgodi na wataalam watatu kutoka nje ya nchi.

Mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Naibu Waziri Biteko alimbana Masanja na kumtaka kutoa taarifa sahihi kuhusu  idadi ya wataalam wa kigeni wanaofanya kazi kwa kuwa taarifa zote anazo kiganjani mwake kabla ya kufanya ziara katika mgodi huo.

Mara baada ya kauli ya Naibu Waziri Biteko, Masanja alieleza kuwa kuna wafanyakazi wa kigeni takribani 10 wasio na vibali vya kazi na wamejificha ndani ya vyumba na kuelekeza kwenye vyumba walivyojificha.

Naibu Waziri Biteko akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicent Anney, Meneja Uendeshaji wa Mgodi huo, Sezgey Sazgyyan  alielekea kwenye vyumba walivyojificha na kufanya msako na kubaini watumishi wa kigeni wasio kuwa na vibali wamejificha kwenye vitanda.

Sehemu ya raia wa kigeni waliokuwa wakifanya kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa MMG pasipokuwa na vibali vya kazi nchini.

Aidha, Biteko alibaini baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo waliokuwa wamefungiwa chooni kwa takribani masaa matatu na uongozi ili kuficha aibu ya kutokuwa na vifaa usalama migodini.

Biteko alimwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicent Anney kuwachukulia hatua za kisheria wafanyakazi hao ambapo bila kusita Mkuu wa Wilaya huyo alielekeza Ofisi ya Wilaya ya Uhamiaji kufika muda huohuo kuwakamata na kuwafikisha kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kutoa maelezo.

Katika hatua nyingine, Biteko alisikiliza kero mbalimbali za watumishi wa mgodi huo ambapo alielezwa kuwa watumishi wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira ya shida ikiwa ni pamoja na kukosa huduma zote muhimu kama maji salama na matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wenzake,  Afisa Usalama wa Mgodi huo,  Stephen Wambura alisema watumishi wa kitanzania wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira yasiyo salama bila kuwa na mikataba ya ajira na pale alipokuwa akiushauri uongozi wa mgodi kutatua changamoto hizo alikuwa akiambulia matusi.

“Mheshimiwa Naibu Waziri, tunashukuru sana kwa kufanya ziara katika mgodi huu kwani tumekuwa tukifanya kazi kama watumwa huku tukikosa huduma muhimu hali inayohatarisha usalama wa afya zetu,” alisema Wambura.

Naye Zuwena Swedi ambaye ni muuguzi wa kituo cha huduma ya kwanza cha mgodi huo aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kutopewa muda wa kutosha kupumzika hasa ikizingatiwa kuwa ni mama wa mtoto mchanga.

Afisa Usalama wa Mgodi wa Dhahabu wa MMG, Stephen Wambura akiwasilisha kero yake mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani).

Wakati huo huo akihitimisha kikao hicho, Naibu Waziri Biteko alitoa wiki moja kwa uongozi wa Mgodi kuhakikisha umesaini mikataba na watumishi.

Alisema kuwa Serikali inawakaribisha wawekezaji kufanya shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini nchini, hivyo wawekezaji wanaowekeza nchini wanatakiwa kufuata sheria na kanuni za utafiti na uchimbaji wa madini.

“Ni lazima wawekezaji wakahakikisha kuwa wanafuata kanuni na sheria za madini ikiwa ni pamoja na kuhakikisha watumishi wa kitanzania wanafanya shughuli za utafutaji na uchimbaji madini katika mazingira yaliyo salama kwa afya na kupata stahiki zao kwa wakati,” alisisitiza Biteko.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha kuwa sekta ya madini inaongeza mchango wake kwenye pato la taifa, serikali imeboresha sheria na kanuni za madini ambazo zitakuwa na manufaa kwa watanzania na wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mara, Vicent Anney akizungumza katika kikao hicho aliwataka watumishi wa mgodi kutoa taarifa zozote za ukiukwaji wa sheria na kanuni za nchi na madini na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ipo tayari kwa ajili ya kuwatetea.

Pamoja na ziara katika mgodi huo, Naibu Waziri Biteko alifanya ziara katika machimbo ya wachimbaji wadogo yaliyopo katika eneo la Ikungwi, Musoma Vijijini  na kuwataka wachimbaji hao kutotumia zebaki katika uchenjuaji wa madini.

Read more

Invitation for Bid-Procurement of LAN and ICT Equipment for Zonal and Residents Mines Offices

 1. The Government of United Republic of Tanzania (hereinafter called “Borrower”) has received financing from the International Development Association (IDA) (hereinafter called “Credit”) towards the cost of Sustainable Management of Mineral Resources Project (SMMRP) and intends to apply part of this Credit to cover eligible payments under contract for procurement of Local Area Network (LAN) and Information Communication Technology (ICT) equipment for Zonal and Residents Mines Offices.
 2.  The Ministry of Minerals (MoM) now invites sealed bids from eligible and qualified bidders for the supply of Local Area Network (LAN) and Information Communication Technology (ICT) equipment for Zonal and Residents Mines Offices as listed below:-
LOT No. DESCRIPTION OF GOODS UNITS QTY
1. LAN equipment Each Various
2. ICT equipment Each Various

The items in this Tender constitute TWO Lots, bidders may quote for ONE or BOTH Lots, bidders must quote for all items and quantity as specified in a particular Lot. Bids not quoting all items and quantities in applied Lot/Lots will be considered non – responsive and rejected for evaluation.

3. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding (NCB) procedures specified under the Public Procurement (Goods, Works, Non Consultant Service and Disposal of Public Assets by Tender) Regulations, 2013 as amended in 2016 and are open to all Bidders as defined in the Regulations.

>>Read More>>

Read more

Invitation for Bid-Supply of Lapidary Machines To Support Women In Value Addition

 1. The United Republic of Tanzania (hereinafter called “Borrower”)has received financing from the International Development Association (IDA) (hereinafter called “Credit”) towards the cost of Sustainable Management of Mineral Resources Project (SMMRP) and intends to apply part of this Credit to cover eligible payments under Contract No.: ME/008/SMMRP/G/64 for supply of Lapidary machines to support women in value addition.
 2. The Ministry of Minerals (MoM) now invites sealed bids from eligible and qualified bidders for the supply of Lapidary equipment and tools as shown below:
Items DESCRIPTION QUANTITY
1. Machines and accessories Various
2. Polishing laps Various
3. Cutting laps Various
4. Polishing compounds Various
5. Wire wrapping tools Various

 

The above items constitute ONEbid,bidders shall quote all items and respective quantities. Bids not quoting all items and quantities will be considered non – responsive and rejected for evaluation.

 1. Bidding will be conducted through the National Competitive Bidding (NCB) procedures specified under the Public Procurement (Amendment) Act 2016 (Goods, Works, Non Consultant Service and Disposal of Public Assets by Tender) amendment Regulations, 2016 –and are open to all Bidders as defined in the Regulations.

Interested eligible bidders may obtain further information from the Ministry of Minerals (MoM) and inspect the bidding documents at the Secretary, Ministerial Tender Board, Ministry of Minerals, Kikuyu Road,P.O. BOX 422,40474 Dodoma, Tanzaniafrom 08:00 to 15:00 hours on (Monday to Friday) inclusive, except on public holidays.

>>Read More>>

Read more

Tanzanite kuwa na hati ya utambulisho Kimataifa

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Serikali imesema inafanya utaratibu wa kuwa na Hati ya Utambulisho wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana katika nchi ya Tanzania pekee katika vilima vya Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushauri na Uchambuzi wa Kazi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akiwasilisha mada kuhusu Muundo na Majukumu ya Wizara ya Madini na Tume ya Madini.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Agosti na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati wa Semina ya mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo imefanyika Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma.

Waziri Kairuki amesema kuwa, serikali inataka kuona kuwa dunia inafahamu kuwa, madini hayo yanapatikana Tanzania pekee na kuhakikisha kwamba yanajulikana zaidi.

Semina ya wabunge imefanyika kufuatia maelekezo ya Kamati hiyo ambayo ilitaka kufahamu kuhusu mwenendo mzima wa Madini ya tanzanite, biashara na udhibiti wa madini hayo baada ya kujengwa kwa Ukuta wa Mirerani unaozunguka migodi ya madini ya tanzanite, Muundo wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na majukumu yao.

Waziri Kairuki amesema kuwa, Wizara imepata fursa ya kuwasilisha kwa Kamati hiyo taarifa za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwemo mikakati ya serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini hayo na mipango madhubuti ambayo serikali inakusudia kuifanya ili kuhakikisha kwamba rasilimali madini inalinufaisha taifa na hatimaye sekta ya madini iweze kufikia asilimia 10 ya machango wake katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025.

Ameongeza ni  kikao ambacho kimekuwa na manufaa kwa upande wa Serikali kwa kuwa imetoa elimu kwa Kamati hiyo kuhusu yale ambayo serikali imefanya na inayokusudia kufanya kuhusuiana na madini  ya tanzanite lakini pia serikali imepata wasaa wa kupokea maoni, mapendekezo na maelekezo kutoka kwa wabunge ambayo yatawezesha kupeleka mbele sekta ya Madini.

Mbali ya tanzanite, Waziri Kairuki amewaeleza wabunge hao kuhusu mkakati wa serikali kuanzisha Mineral Exchange ambapo amesema tayari wizara imeshaandaa timu ya wataalam ili kwenda kujifunza na kufanya utafiti katika nchi nyingine ili suala hilo liweze kufanyika kwa ubora.

Sehemu ya Maafisa Waandamizi wa Wizara na Tume ya Madini wakifuatilia mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Pia, ameeleza kuwa, Wabunge wa Kamati hiyo, wamepata fursa ya kufahamu majukumu ya Wizara baada ya kuundwa kwa Tume ya Madini, majukumu ya tume ya madini na mahusiano ya kiutendaji kati ya Tume na Wizara.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mariam Ditopile, amesema kuwa, kamati imebaini kuwa, Serikali imechukua hatua nyingi za kulinda na kudhibiti madini ya tanzanite ikiwemo  kudhibiti utoroshaji wa madini hayo. “Kama kamati tumeona mnyororo mzima wa thamani ya madini ya tanzanite, awali tulikuwa hatunufaiki kama taifa,” amesema Ditopile.

Awali, akiwasilisha mada kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini ya tanzanite na usimamizi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini ndani ya ukuta, Afisa Madini Mkazi wa Mirerani Mhandisi David Ntalimwa, amezungumzia sababu za kushuka kwa mapato na kueleza kuwa, kunategemea kiwango cha ubora na sifa za madini husika.

Ameongeza kuwa, kutokana na mazingira hayo, kiwango cha thamani ya madini na tozo ya mrabaha kitakuwa tofauti kutegemea na mwezi na uzalishaji uliopo.

Akizungumzia sababu za utoroshaji wa madini ya tanzanite, Mhandisi Ntalimwa amesema kuwa, zinatokana na uwezo mdogo wa kusanifu na kuongeza thamani na kunga’risha madini ya vito na hivyo watu kutamani kuuza tanzanite ghafi.

Pia, amesema utoroshaji wa madini unatokana na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa na serikali ili kujipatia faida kubwa, kuwepo kwa raia wa kigeni nchini wanaofanya biashara ya madini kinyume na sheria kwa kushirikiana na wazawa na kukosekana kwa masoko ya uhakika ya kuuzia madini yanayozalishwa.

Akizungumzia hatua zilizochukuliwa na serikali katika kudhibiti utoroshaji wa madini baada ya kujengwa ukuta amesema kuwa, serikali imeimarisha ulinzi na ukaguzi getini kwa kutumia vikosi vya ulinzi na usalama, kuzuia magari kuingia na kutoka ndani ya ukuta, watu kuingia ndani ya ukuta kwa vitambulisho maalum.

“ Sasa watu wanaingia kwa utaratibu maalum tofauti na walivyozoea awali. Ukuta umeleta utaratibu mzuri na si kero, kama baadhi ya watu wanavyodhani,” amesisitiza Ntalimwa.

Amezitaja hatua nyingine kuwa ni pamoja na kuzuia Mabroker kwenda migodini na badala yake kutakiwa kusubiria madini getini, uthaminishaji madini kufanyika ndani ya ukuta na serikali kujenga jengo lenye ofisi ya ukaguzi, uthaminishaji na ukumbi wa mabroker ndani ya ukuta.

Aidha, pamoja na kushiriki semina hiyo, pia wabunge hao wamepata fursa ya kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Jiolojia na Madini katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania, (GST).

Read more

Wizara ya Madini yakutana na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini

Na Asteria Muhozya,

Kuanzia tarehe 21, 23 na 24 Agosti, Wizara ya Madini ilikutana na  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambapo taarifa  mbalimbali za Utekelezaji wa Majukumu na Miradi zimewasilishwa.

Baadhi ya taarifa zilizowasilishwa katika vikao hivyo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Madini kuanzia mwezi Aprili hadi Julai,2018,
Taarifa kuhusu Uendelezaji na Uwekezaji katika Madini Mkakati na
Taarifa kuhusu Uendelezaji ya Migodi ya Makaa ya Mawe.

Aidha, katika vikao hivyo,  Kamati ilitoa maagizo mbalimbali yanayopaswa kufanyiwa kazi na Wizara ili kuboresha Sekta ya Madini nchini.

* ALICHOKISEMA WAZIRI WA MADINI ANGELLAH KAIRUKI

# Graphite ni madini ambayo tunayapa kipaumbele. Ninawaomba wananchi na ninyi Waheshimiwa Wabunge mtusaidie kuwaambia wananchi wasikwamishe miradi ya uwekezaji.

# Tutakapokuwa katika hatua za uchimbaji wa madini ya Urani, tutakuwa karibu sana na kila hatua itakayofanyika kuhakikisha kwamba hakuna athari zozote za kijamii. Serikali haitaweka maslahi ya kiuchumi mbele kuliko ya kijamii.

# Tutafanya Jukwaa kubwa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2019. Lengo ni kuvutia Wawekezaji na kuwakutanisha wachimbaji na Wabia lakini pia Taasisi za Kifedha.

*ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI,  DOTO BITEKO

# Wachimbaji wetu wanahitaji huduma za umeme, maji na barabara katika maeneo yao. Yapo baadhi ya maeneo ambayo  tayari  Mhe. Waziri  amewasiliana na Mamlaka husika kwa ajili ya masuala hayo.

* ALICHOKISEMA NAIBU WAZIRI WA MADINI STANSLAUS NYONGO

#  Tuna madini mengi ya Kimkakati. Tunaangalia madini ambayo yatasaidia kusukuma mbele Sekta ya Viwanda.

* ALICHOKISEMA KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI, PROF. SIMON MSANJILA

# Kama Wizara tunayo nia ya kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini. Tunaangalia mfumo mzuri wa namna ya kuwasaidia. Tutawashirikisha Waheshimiwa Wabunge kuhusu namna ya kufanya jambo hilo kwa ubora zaidi.

Read more

Serikali kutoa eneo la Buhemba kwa wachimbaji ikiwa itanufaika

Na Asteria Muhozya, Mara

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Wizara italigawa kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini eneo lote la mgodi wa Buhemba linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ikiwa Serikali itanufaika ipasavyo  na makusanyo kutokana na shughuli za wachimbaji hao.

Kauli ya Waziri Kairuki imekuja kufuatia maombi yaliyotolewa na Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mara (MAREMA) kupitia kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Stephano Mseti ambaye alimuomba Waziri Kairuki kulitoa eneo lote la STAMICO kwa wachimbaji hao kwa kuwa wana uhakika wa kuchangia zaidi kodi za serikali ikiwa watamilikishwa eneo husika.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akizungumza jambo wakati wa mkutano na Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mara (MAREMA).

Aidha,  Mseti alimweleza Waziri Kairuki kuwa  wachimbaji katika eneo hilo wamejiandaa kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wanalipa kodi stahiki kwa kuwa, ndani ya mwezi mmoja waliopewa kufanya kazi katika eneo husika, wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 107 kama mrahaba.

Katika hatua nyingine, wakati akisikiliza kero za wachimbaji hao, Waziri Kairuki aliiagiza Tume ya Madini na Wataalam kutoka Wizara hiyo kuchunguza kwa kina suala la migogoro ya migodi  yote iliyopo katika eneo la Buhemba iliyotolewa awali na STAMICO kwa wachimbaji hao  na kukamilisha kazi husika ndani ya kipindi cha wiki 3 ikiwemo  kutoa mapendekezo  aweze kujua hatua za kuchukua.

Akizungumzia mikakati ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo, Waziri Kairuki alieleza kuwa, tayari serikali imeanza kujenga kituo cha umahiri katika mkoa huo ili kuwezesha wachimbaji wadogo  kujifunza uchimbaji bora na kuwataka wachimbaji mkoani humo kukitumia kikamilifu kituo hicho mara baada ya kukamilika kwake.

Akizungumzia muda wa uhai wa leseni, alisema kuwa suala hilo limebainishwa kisheria kuwa ni ndani ya kipindi cha miaka saba na kufafanua kuwa, ipo haki ya kuhuisha  muda wa leseni na hivyo kuwataka wamiliki wote wa leseni kuzingatia muda husika uliowekwa kisheria.

Pia, aliwataka wachimbaji hao kutoa taarifa za kuwepo Maafisa Madini wanaomiliki leseni za uchimbaji madini au wanaomiliki leseni hizo kupitia  kwa kutumia majina tofauti ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Akizungumzia kuhusu suala la migogoro, alisema kuwa Serikali haifurahishwi na migogoro inayotokea katika maeneo ya migodi na hususani ile inayohatarisha maisha na kuongeza kuwa, serikali haipendi kufunga migodi hiyo kutokana na umuhimu wa migodi hiyo kwa pande zote.

Pia, Waziri Kairuki alisisitiza kuhusu suala la uchimbaji salama  migodini na Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii na kuongeza kuwa, suala hilo ni lazima litekelezwe na wamiliki wote wa leseni wakiwemo wachimbaji wadogo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima, alisema Mkoa huo umejipanga kuwa na Gold Exchange ili kuwezesha mkoa huo pia kunufaika na rasilimali hiyo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa MAREMA na Chama cha Wachimbaji Wadogo wa Madini, ( FEMATA).

Aidha, alisisitiza suala la uchimbaji salama wa madini ikiwemo utunzaji wa mazingira na kuwataka wachimbaji hao kubadilika kwa kuhakikisha wanafanya shughuli zao kisasa.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema kuwa, Serikali inawaona wachimbaji wadogo kwa jicho la kipekee na inajua kuwa, ikiwawezesha itapata fedha nyingi kutokana na rasilimali hiyo.

Alisema kuwa, mkoa huo una migogoro mingi ikilinganishwa na mingine na kumshauri Waziri Kairuki kupokea  vizuri malalamiko yote ya wanaolalamika kwani si wote wanalalamika kihalali.

Pia, aliwashauri Maafisa Madini nchini kuhakikisha kuwa, wanapotatua migogoro zawanavishirikisha Vyama vya Wachimbaji katika kutatua migogoro hiyo ikiwemo katika suala la ukusanyaji kodi za serikali.

Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Chama Cha Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, aliiomba  Serikali kuiwezesha Tume ya Madini ili iweze kuwafikia wachimbaji katika ngazi za chini.

Pia, aliwataka wachimbaji kuwa wakweli na kuacha ubifasi, na kueleza kuwa, kuna watu ndani ya umoja huo wananufaika pindi panapokuwa na migogoro na kuongeza kuwa, migogoro katika jamii ya wachimbaji ni mdudu anayekua kila siku.

Awali, akiwasilisha taarifa ya chama hicho, Katibu Mkuu wa MAREMA, Milele Mundeba, alisema Chama hicho kinakusudia uanzishaji wa biashara ya vifaa vya uchimbaji madini.

Mbali na wachimbaji mkutano huo uliofanyika tarehe 16 Agosti, ulihudhuriwa na benki ya CRDB, SIDO, Benki ya Posta Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki ya NMB, FINCA, Shirika la Bima la Taifa ( NHIF),  Mamlaka ya Maji, Musoma (MUWASA), Migodi ya Wachimbaji wa Kati ya CATA Mining, ACACIA na  Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Read more

Serikali kuleta timu jumuishi ya wataalamu utafiti wa madini Muheza

Na Zuena Msuya, Mheza Tanga

Serikali imesema itawaleta wataalam kutoka kituo cha Utafiti wa Miamba(GST), Wizara ya Maliasili  na  Mazingira kwenye eneo walilokuwa wakitumia wachimbaji wadogo kwa shughuli za madini, ambalo pia linadaiwa kuwa liko katika chanzo cha maji, kufanya utafiti na kujiridhisha kama eneo hilo liruhusiwe kuendeleza na shughuli za uchimbaji madini  ama laa.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( mwenye Tshit nyekundu) na Mbunge wa Mheza Balozi Rajab Adad (mbele) wakielekea eneo lililokuwa likitumiwa na wachimbaji wadogo kuchimba madini pia likidaiwa kuwa chanzo cha maji katika hifadhi ya misitu wa asili wa amani, mheza Tanga.

Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika Kata ya Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Mheza mkoani Tanga, wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Naibu Waziri Biteko, alisema kuwa kiu ya serikali ni kuwapatia maeneo ya uchimbaji wachimbaji wadogowadogo ili waweze kubadilisha maisha yao kupitia uchumi wa madini, hii ni kutokana Rais kubadilisha sheria za nchi kwa upande wa madini kutoka kuwanufaisha wageni na sasa kuwanufaisha watanzania.

“Serikali yenu ni sikivu,Mheshimiwa Rais amebadilisha sheria ya madini ili kuwanufaisha watanzania badala ya wageni ,hapa leo tumekuja kuangalia kwa macho ili tufanye uamuzi sahihi …siwezi kumiambia mchimbe sasa hivi ila tutaleta wataalamu wetu wa GST,maliasili na mazingira kwa pamoja ili waje kuona uwezekano wa kupewa eneo la kuchimba ikiwa hapa au kwengine”alisema.

Aidha aliongeza kuwa wananchi lazima wafundishwe kufuata sheria za madini haswa katika kuhama  matumizi ya zebaki katika kuchenjua madini ambayo yana athari kubwa kwenye mazingira na miili ya binadamu kutumia madini ya Sayayi ambayo hayana madhara.

Kwa upande wa wananchi wa eneo hilo, walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

Walisema kuwa kutoka uliopo mwamba unaosadikiwa kuwa na madini na chanzo cha maji ni zaidi ya mita sitini na ilipo hifadhi ya msitu wa asili wa Amani ni zaidi ya mita 3,000 lakini wamekuwa wavumilivu kusubiri hatima ya serikali.

“Mheshimiwa Naibu Waziri uchumi tunao lakini tunakufa maskini…hapa madini yapo lakini serikali imetuzuia kwa hatari ya uharibifu wa mazingira ..sisi tunakuhakikishia hakuna uharibifu wowote wa mazingira  utakaotokea,” alisema Shetwai.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko,( katikati) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sakale, Mheza mkoani Tanga, waliokuwa wakiomba kuruhusiwa kufanya shughuli za uchimbaji madini katika eneo linalodaiwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika Mkoa wa Tanga.

Naye diwani wa kata hiyo Anord Mlowe alisema kuwa wataalamu walikuja kupima mwamba  na baadae ukaanza kutoa madini lakini baadae kukaanza mabishano kati ya watu wa maliasili,maji na mazingira kuhusu usafishaji wa madini kwa kutumia zebaki lakini mkuu wa wilaya  ya Muheza  aliyepita Subira Mgalu alijiridhisha kuwa hakuna madhara lakini serikali ikaweka zuio.

Alimuomba waziri kuwaruhusu ili waweze kuchimba kutoka maeneo yalipo mmwamaba wa madini ni mashamba ya wananchi na sio eneo la hifadhi kutokana wameyarithi kutoka kwa mababu zao.

Akizungumzia eneo hilo,  mbunge wa jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu alimuomba Naibu Waziri , Biteko kuleta wataalamu wa madini kuja kupima ili kuona kama madini hayo yanatoka milimani au yapo kwenye mto ili kuona namna ya kuwasaidia kupewa eneo la uchimbaji.

“Mheshimiwa naibu waziri pale mwamba uko pembeni kutoka chanzo cha maji na wananchi wa Sakale kata ya Mbomole wametunza msitu wa asili wa Amani….hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kutunza msitu bila ya kuathiri  chanzo cha maji” alisema.

Aliongeza “kwa niaba yao tuma wataalamu wako waje ili wakuletee taarifa ili wananchi hawa waweze kuchimba”.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo akisoma taarifa ya zuio la uchimbaji wa madini eneo hilo, alisema lengo ni kulinda mazingira na chanzo cha maji licha ya sheria katika maeneo hayo matatu ya madini, mazingira na maliasili kukinzana jambo ambalo linaleta ugumu kwa watendaji kuwadhibiti wachimbaji hao.

Read more

Serikali yawataka Watanzania kuacha migogoro katika ubia wa uwekezaji

Na Zuena Msuya, Kilimanjaro

Serikali imewataka Watanzania  kuepuka migogoro katika maeno ya migodi hasa inayomilikiwa Kwa ubia na wawekezaji wazawa ili kuondoa taswira mbaya kwa wawekezaji kutoka Matifa mengine yanayokuja nchini kwa lengo la kuwekeza badala yake waungane  kuweka mazingira mazuri na rafiki ya kuvutia wawekezaji hao kuwekeza nchini.

Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko (kulia) akipita katikati ya Mbale za shaba zilizoandaliwa tayari kwa kuchenjuliwa.

Hayo yameelezwa na Naibu  Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa ziara yake mkoani Kilimanjaro  alipotembelea mgodi wa Madini wa Mega unaochimba madini ya shaba .( Mega Copper Company) uliopo katika Kijiji cha Chang`ombe wilayani Mwanga  Mkoani Kilimanjaro, Kwan lengo la kumaliza mgogoro uliopo katika mgodi huo unachimba na kuchenjua madini ya Shaba.

Mgodi huo wa madini ya Shaba unaomilikiwa na Watanzania umekuwa katika migogoro ya kutoelewana wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka 10 sasa, Licha kumepiga hatau katika uchenjuaji  wa shaba na kwamba hausafirishi madini ghafi nje ya nchi  kama serikali ilivyoagiza.

Kwa mantiki hiyo, Biteko alisisitiza kuwa migogoro haipaswi kupewa nafasi na inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania na kuleta taswira mbaya ya Uwekezaji Tanzania katika Mataifa mengine Duniani Kwani kusengskuwa na mgogoro katika mgodi huo wangekuwa wamepiga hatua zaidi kwa manufaa yao na Taifa kwa jumla.

Biteko  alisema “migogoro miongoni ya wabia hasa wazawa haipaswi kufumbiwa macho na mtu yeyote Yule, ambapo alishauri kuwa kama watu, au kikundi wameingia makubaliano ya pamoja katika kuendeleza mgodi au jambo fulani  basi, makubaliano hayo yapelekwe Wizara ya madini  au katika mamlaka husika yasajiliwe kuepusha migogoro.

Aidha aliweka wazi kuwa kutokana na mgogoro, Serikali imetoa Miezi 3 kwa mgodi huo kumaliza tofauti zao na kuendelea na shughuli za uzalishaji, na endapo watashindwa kufanya hivyo, itawaandikia hati ya makosa na kisha kuwanyang’a mgodi huo na kuwapa watu wengine.

“Ninyi wote ni Watanzania tena ni ndugu kwa nini mnagombana? , Mnakuja kuwa Sheria ya madini inaruhusu kuwafungulia hati ya mashitaka na kuwafutia leseni endapo mgogoro huo  hautakwisha na utakuwa na  viashiria vya uvunjivu wa amani na Mkishindwa kuumaliza ndani ya muda uliotolewa Serikali unaingia Kati na kufanya maamuzi,  nawakumbusha  watanzania wote  hasa wanaoishi katika maeneo karibu na migodi kuepuka migogoro ili sekta ya mdini iendeleee kuimarika” alisisitiza Naibu waziri Biteko.

Vilevile alitoa  wito kwa wanatanzania wenye uwezo wa kuongeza thamani  ya madini wafanye hivyo ili kuongeza pato la taifa na mwananchi mmoja mmoja  kuliko kusafirisha  madini ghafi  nje ya nchi kwa kuwa faida kubwa zinapata nchi zinazo nunua madini ghafi hayo na kuyaongeza thamani.

Naibu Waziri wa madini, Dotto Biteko, akizungumza na akina mama wanaofanya kazi katika mgodi wa shaba wa Mega.

Kwa mujibu wa Naibu waziri Biteko  mgogoro ulipo katika mgodi huo kati ya  wabia Watanzania wawili ambao kila mmoja alikuwa na mbao wake kutoka nje, ambao waliingia  makubaliano  ya kuanzisha mradi huo ndani ya miezi sita,  baadae Kuliitokea kutoelewana na kUsababisha   mmoja kati yao kuanza uzalishaji  kabla ya kumshirikisha mwenzie.

Mmoja wa wabia hao ni Ally Nyanza kutoka ambaye  alisema kuwa mgodi huo una ukubwa wa heka 25, ambapo  kwa sasa  wapo kwenye majaribio ya kuchimba na kuchenjua shaba Ambapo wanauwezo wa kuzalisha tani 8-10 za shaba kwa siku.

Alisema Bado wanaendelea na tafiti huku wakiendelea na uzalishaji, soko kubwa la shaba hiyo  liko nchini  China na kutokana na tafiti hizo wamegundua eneo hilo lina  chokaa ambayo hutumika kwenye uzalishaji wa saruji.

Nyanza alismea changamoto kubwa ilikuwa na mgogoro kati yao na uliosabababisha kusimamisha uzalishaji kwa muda mrefu, kwa sasa wanafuata maelekezo ya Naibu waziri kupata muafaka wa kufanya kazi pamoja.

Naye Nassib  Mfinanga  alisema   wamemeridhika na maamuzi ya Naibu Waziri wa Madini na kwamba watakaa kama familia ili tusonge  mbele kwani mgogoro huo umekuwa ukituchelewesha na kutupa hofu kuwekeza bila kuwa na usalama, jambo hili lilikuwa ngumu kwetu.

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aaron Mbogho alisema uwepo wa mgodi huo ni chachu ya maendeleo katika wilaya hiyo tunasuburi wameanza uzalishaji pamoja wazingatie sheriana kanuni za wizara  serikali bado inatamani kuona watoka kwenye uongezajiwathani ya shaba 90% hadi kufikia 100%.

Read more

Ujumbe wa CRDB wafanya ziara Tume ya Madini

Na Greyson Mwase,

Jana tarehe 14 Agosti, 2018  ujumbe kutoka CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi wake Dk. Charles Kimei ulifanya ziara katika Ofisi za Tume ya Madini zilizopo jijini Dodoma lengo likiwa  ni kufahamu majukumu na shughuli za Tume.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akifafanua jambo kwenye kikao kilichoshirikisha ujumbe wake na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya.

Read more

Afrika Kusini yaonesha utayari kuwa na ushirikiano sekta ya madini

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Waziri wa Madini Angellah Kairuki jana tarehe13 Agosti alikutana na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mheshimiwa Thami Mseleku. Katika mkutano huo, Balozi huyo alimueleza Waziri Kairuki kuhusu utayari wa Nchi hiyo ya Afrika Kusini kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta ya madini nchini.

Ujio wa Balozi Thami Mseleku, Makao Makuu ya Wizara ya Madini, unafuatia ziara ya Kamati ya Jamii na Masuala ya usalama ya Bunge ya Jimbo la Gauteng Pretoria- Afrika Kusini ambao walifika nchini mwezi Juni mwaka huu kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa namna sekta ya madini nchini inavyoendeshwa.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Thami Mseleku, wakijadiliana jambo ofisini kwa Waziri Kairuki, jijini Dodoma.

Aidha, wakati wa ziara ya kamati hiyo ya Bunge hilo nchini, ilikubalika kuwa na haja ya kuwa na ushirikiano katika masuala mbalimbali ya namna ya kusimamia sekta ya madini ikiwa ni pamoja na shughuli za uchimbaji madini, kubadilishana uzoefu katika udhibiti wa uchimbaji holela wa madini, usimamizi wa migodi na wachimbaji wadogo wa madini.

Maeneo mengine ni pamoja na namna ya kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini kutoka katika uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

Pia, masuala ya utafiti wa miamba ya uchimbaji madini, mafunzo kwa ajili ya wataalam, kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa sekta ya madini, masuala ya umiliki wa migodi na namna ya kuwawezesha wazawa kumiliki uchumi kupitia sekta ya madini.

Kwa upande wake, Waziri Kairuki alimhakikishia Balozi Thami kuhusu nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kumarisha na kukuza zaidi mahusiano baina ya nchi hizo mbili pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika sekta mbalimbali hususan katika sekta ya madini ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili.

Vilevile, Waziri Kairuki alimueleza Balozi huyo jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini ambapo ameendelea kuwakaribisha zaidi wawekezaji kutoka Afrika Kusini kuwekeza katika sekta ya madini nchini.

Vilevile, Waziri Kairuki alimpa pole Balozi huyo kufuatia kifo cha Mama Winnie Mandela aliyefariki dunia mwezi Aprili mwaka huu.

Read more

Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini

Na Zuena Msuya, Tanga

Serikali imempa muda wa wiki moja nwekezaji  mmiliki wa kampuni ya Amazon Trading (T)Company Limited Abdi Hozza kuhakikisha anailipa serikali kodi ya pango ya uwekezaji kiasi cha dola za Marekani  70,020 sawa na zaidi ya shilingi milioni 140 za kitanzania  anazodaiwa tangu mwaka 2011 katika machimbo ya Kalalani eneo la Umba wilayani Korogwe kutokana na leseni nane za uchimbaji wa madini kuanzialeseni  namba (102-109/2001) anazomiliki.

Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko (aliyesimama) akizungumza na wachimbaji wadogo wa eneo la Kilalani, baada ya kutembelea eneo hilo.

Sambamba na hilo imeiagiza serikali ya wilaya ya Korogwe  kuhakikisha inatenga maeneo ya wachimbaji wadogowadogo wa madini ili kuepusha migogoro iliyodumu kwa muda mrefu hali ambayo imeleta hali ya chuki baina ya mwekezaji na wananchi.

Waziri Biteko alitoa agizo hilo alipotembelea katika machimbo hayo juzi Jumamosi katika vijiji vya Kigwasi na Kalalani kata ya Kalalani wilayani humo.

Biteko alimtaka ndani ya wiki moja mwekezaji huyo kulipa kodi hiyo ya pango anayodaiwa na serikali na amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuwabaini wageni na watu wanaonunua madini  kwa njia za panya.

“Haiwezekani tangu madini yaanze kuchimbwa katika machimbo haya serikali haijapata kodi kutokana na mgodi huu tunakuta sifuri nimewaambia wailipe haraka nataka nikifika Dodoma kuna commitment statement mnalipa lini” alisema.

Aliongeza  “Na yule anayedhani atakuja Kalalani kununua  madini kwa njia ya panya muda huo umekwisha,na tumekwenda kwenye mto tumekuta mnachimba madini,sheria inakataza kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji naomba kuanzia sasa mkaondoe vifaa vyenu kule mtoni”.

Aidha Waziri Biteko, aliongeza kuwa eneo hilo la Kalalani lina leseni za wachimbaji wadogo wa madini ya vito zipatazo 400 lakini leseni zilizohai na zinaendelea kufanya kazi ya uchimbaji ni 70 tu kati ya hizo.

Awali diwani wa kata hiyo Amati Ngerera alimueleza naibu waziri kuwa mwekezaji huyo(Amazon)hana mahusiano mazuri na wa wanakijiji pamoja na wachimbaji wadogowadogo wa hapo kutokana baada ya kupewa leseni na serikali kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo alilitelekeza  kwa muda mrefu bila ya kuendeleza shughuli zozote na wananchi wengi ambao shughuli zao kubwa ni uchimbaji waliokuwa wakiingia eneo hilo walifanyiwa vitendo vya visivyokuwa vya kibinadamu ikiwemo kupigwa risasi,kubakwa na askari aliowaweka kulinda eneo hilo.

Diwani huyo alikwenda mbali zaidi kuwa mwekezaji huyo huwa anatumia eneo hilo kama dhamana ya kukopa fedha kutoka kwenye taasisi za fedha na alimpa mwenzake anaitwa Najim  kuendesha mgodi huo kinyemela bila ya serikali kuwa na taarifa.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko, akikagua Mabaki ya mgodi wa Amazon,ambao umesitisha uchimbaji kwa miaka mingi kutokana na Matatizo mbalimbali.

“Huyu mwekezaji leseni yake ilikwisha tangu mwaka 2001,wananchi wakaomba leseni ya uchimbaji na yeye akaomba ,lakini baadae  akaingia mkataba na mfanyabiashara anayeitwa Najim halafu yeye akajitoa kabisa na huyo Najim hachimbi bali anafanya shughuli zake za biashara ya utalii na huyu Amazon anatumia eneo hili kukopea fedha kwenye taasisi za fedha ”alisema.

Aliongeza “Serikali ya kijiji ilifanya mapendekezo matatu na kuyapeleka katika baraza la madiwani na baadae tukayandika kuyaleta katika ofisi yako,mapendekezo haoy ni eneo hilo litafutwe mwekezaji mwenye sifa ya uwekezaji,nyumba zilizopo eneo la mgodi  zirudishwe serikalini ambazo waasisi wake ni STAMICO na wananchi wakatiwe eneo ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi za uchimbaji”.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwasi, Loronyotu Lakaney alimueleza Naibu Waziri kuwa mbali na mgodi huo kutelekezwa na mwekezaji huyo pia madini yanatorosha kwa njia za panya na  kuuzwa Voi nchini Kenya.

“Mheshimiwa Naibu waziri mbali na mgogoro huo pia wachimbaji wengi wadogowadogo wakishapata madini wanakwenda kuyauza Voi mpakani mwa Kenya na Tanzania upande wa hapa Tanga kutokana hakuna udhibiti  na hakuna minada ya madini inayoendeshwa kama serikali ilivyoagiza”alisema.

Naye mwekezaji huyo alimueleza Naibu waziri kuwa alichelewa kulipa hiyo kodi kutokana Kutokupewa taarifa yoyote ya kuendeleza mgodi wala kudaiwa kodi.

“Mheshimiwa Naibu waziri mimi ni kweli kwa muda mrefu sijapaendeleza hapa baada ya leseni yangu kwisha mwaka 2011 sijapewa leseni nyingine wala sijapata hiyo barua ya kulipa hiyo kodi ya pango”alisema.

Taarifa ya ofisi ya Afisa Madini  Mkazi mkoa wa Tanga amabayo gazeti hili inayo nakala yake  ilishapendekeza kwa kamishna wa madini leseni hizo nane za mwekezaji ziandikiwe hati ya makosa(default notice) na hatimaye zifutwe kwa mujibu wa sheria ya madini mwaka 2010,lakini kwenye mfumo wa flexicadastre leseni hizo zinaonesha zipo hai(active in default) ingawa zilishaisha muda wake tangu Septemba 30,2011.

Read more

Maafisa madini watakiwa kuwa vinara mapambano ya rushwa

Na Greyson Mwase, Morogoro

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka viongozi na maafisa waandamizi walioteuliwa kufanya kazi na Tume ya Madini iliyoanzishwa hivi karibuni kuwa mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya rushwa kwenye maeneo ya kazi.

Kutoka kulia, Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Madini, Jerry Sabi, Mkurugenzi wa Utafiti na Mipango kutoka Tume ya Madini, Julius Moshi na Afisa Madini Mkazi-Ruvuma, Fredy Mahobe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mafunzo hayo.

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo leo tarehe 11 Agosti, 2018 alipokuwa akifunga mafunzo ya siku sita yaliyofanyika mjini Morogoro kwa kushirikisha viongozi na maafisa waandamizi walioteuliwa kufanya kazi na Tume ya Madini.

Alisema kuwa, mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo anatarajia kuona viongozi pamoja na maafisa madini wakazi wa mikoa na maafisa migodi wanakuwa vinara kwenye mapambano dhidi ya rushwa kwenye utoaji wa leseni na migodi.

Katika hatua nyingine, Nyongo aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa ubunifu hususan kwenye ukusanyaji wa maduhuli ili kuvuka lengo lililowekwa na Serikali.

“Ni matarajio yangu kuwa  kuanzia mwezi Septemba, mtaanza kukusanya maduhuli kwa njia ya kieletroniki ili kudhibiti upotevu wa fedha na kufikia lengo lililowekwa na Serikali,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Aliendelea kuwataka viongozi walioteuliwa kusimamia shughuli za madini mikoani kuhakikisha wanatatua migogoro  iliyopo kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji madini badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kutatua kupitia ziara mbalimbali wanazofanya kwenye maeneo hayo.

Awali akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila aliwapongeza viongozi na mafisa waandamizi walioteuliwa kufanya kazi na Tume ya Madini na kuwataka kuhakikisha wanafuata taratibu za makabidhiano ya ofisi kabla ya kuripoti kwenye vituo vipya vya kazi.

Mafunzo hayo yalilenga maeneo tofauti ikiwa ni pamoja na historia ya mabadiliko ya sheria ya madini, sheria ya madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017, muundo wa tume ya madini na mawasiliano ya ndani na nje ya tume.

Kutoka kulia waliokaa mbele, Meneja Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Tume ya Madini, Miriam Mbaga, Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Jerry Sabi, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wa Wizara ya Madini, Issa Nchasi na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira wa Tume ya Madini, Dk. Abrahaman Mwanga wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa madini wa kwenye migodi (MROs)

Maeneo mengine ni pamoja na muundo na mfumo wa mawasiliano wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), taratibu za ofisi na makusanyo na maduhuli ya Serikali kwa njia ya kieletroniki (GEPG), usimamizi na utunzaji wa mali za umma, taratibu za utoaji wa leseni za shughuli za madini na ushirikishwaji wa wananchi/wazawa katika shughuli za madini.

Aidha maeneo mengine ni pamoja na ukaguzi wa madini na biashara, utatuzi wa migogoro katika sekta ya madini, taratibu za uwasilishaji wa taarifa makao makuu ya Tume na kwenye mamlaka nyingine zinazohusika, utunzaji wa siri katika utumishi wa umma, masuala ya utawala na rasilimaliwatu, sheria, kanuni na taratibu za fedha, usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa ndani, maadili katika utumishi wa umma na mfumo wa uwazi wa upimaji utendaji kazi (OPRAS).

Read more

Waziri Kairuki ataka wafanyabiashara wa madini wazaliwe upya

Na Asteria Muhozya, Arusha

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amewataka Wafanyabiashara wa Madini nchini kuzaliwa upya kwa kufuata Sheria, Kanuni na  taratibu kwa kufanya biashara halali ya madini  ili kuziwezesha pande zote yaani Serikali na  Wafanyabishara  kunufaika na rasilimali hiyo.

Sehemu ya wafanyabishara wa madini wa jijini Arusha wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani).

Waziri Kairuki ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wafanyabiashara wa madini  wa jijini Arusha waliohudhuria mkutano huo  ulioratibiwa na Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania, (TAMIDA).

Kairuki alisema zama zimebadilika na hivyo  kuwatahadharisha wale wote wanaofanya vitendo vilivyo kinyume na taratibu na kueleza kuwa,  hawatasalimika na mkono wa sheria kwa kuwa serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba rasilimali madini inawanufaisha watanzania na taifa.

“Nimekuja hapa tubatizane. Naomba tuzaliwe upya. Tushirikiane vizuri. Naahidi kuwa balozi wenu mzuri. Nitatekeleza yale yenye manufaa kwetu sote. Lakini watakaokwenda kinyume, serikali ina macho yanayoona sana na yenye lenzi za hatari,” alisisitiza Kairuki.

Kairuki alisisitiza kuwa, tayari anazo taarifa za kila mfanya biashara wa madini wa jijini Arusha na kuwataka wote wanaokwenda kinyume kujitafakari upya na kuchukua hatua  sahihi kwani anamfahamu kila mmoja.

Alisema, serikali inatambua na kuthamini mchango wa biashara ya madini katika pato la taifa na katika kuzalisha ajira na kuongeza kuwa, itaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara ya madini na kuwataka wale wote waliokuwa wakitenda kinyume ikiwemo kukwepa kodi kujisalimisha kwake ili kuepuka kuingia katika makosa ya uhujumu uchumi.

“Kama unadhani ulikuwa unakwepa kodi, unakwenda kinyume, njoo uniambie. Haitapendeza upate kosa la uhujumu uchumi, kumbukeni kuwa kosa hilo halina dhamana,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Akizungumzia suala la utoaji leseni za usafirishaji madini nje ya nchi, alisema serikali italifanyia haraka suala hilo ili kuleta ufanisi katika biashara ya madini huku akisisitia kuwa, watakaopatiwa leseni hizo ni wale tu watakaokidhi vigezo.

Mmoja wa wafanyabishara madini akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki madini aina ya Ruby na kumweleza kuhusu ukubwa tofauti wa madini hayo na suala zima la uongezaji thamani madini hayo kabla ya kusafirishwa.

Aidha, Waziri Kairuki alitumia fursa hiyo kukaribisha wawekezaji katika sekta ndogo ya Uongezaji thamani madini na kueleza kuwa, serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba shughuli za uongezaji  madini  zinafanyika nchini ikilenga kuongeza  mchango wa madini katika pato la taifa na kuzalisha ajira.

Aliwataka wafanya biashara wa madini wenye nia  kuwekeza katika viwanda vya ukataji na unga’rishaji madini ya vito kufanya hivyo  na kuwasilisha mapendekezo serikalini ili kuna namna bora ya kufanikisha suala husika.

Kairuki aliongeza kuwa, masuala ya uongezaji thamani madini nchini ni moja ya mapendekezo katika Sheria mpya ya madini  na kuelea kuwa, mwongozo wa namna ya shughuli za uongezaji thamani madini zitakavyofanyika utatolewa na serikali baada ya kukamilisha suala hilo.

“ Lakini pia hatukatazi wageni kuwekeza nchini. Isipokuwa tunataka waje kihalali,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Awali, akisoma risala ya wafanyabiashara hao, Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel, alisema, TAMIDA inaunga mkono suala la uongezaji thamani madini kufanyika nchini kwa kuwa shughuli hizo zitasaidia  kuongeza thamani ya madini, fedha za kigeni kuhamisha teknolojia, kupanua wigo wa ajira na kufungua viwanda vingi vya uongezaji thamani na hatimaye kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini barani Afrika.

Vilevile, alisema kuwa, chama hicho kinaunga mkono  kutosafirisha madini ghafi ya Tanzanite nje ya  nchi na kupendekeza kuwa madini ya tanzanite yanayozidi gramu 1  yakatwe  hapa nchini na kwa yale yaliyo  nusu uzito  yaongezwe umbile kisha yaruhusishwe kusafirishwa yakiwa ghafi kwa kuwa bado hakuna ujuzi wa kukata madini  katika kiwango hicho.

“Mhe. Waziri tunapendekeza mchakato  huo ufanyike hivyo  wakati tukiendelea na kupata ujuzi na wataalam katika suala hilo na baada ya muda basi liwekwe zuio,” alisema Mollel.

Sehemu ya wafanyabishara wa madini wa jijini Arusha wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Madini Angellah Kairuki (hayupo pichani).

Pia, alisema Tamida inapendekeza Kamati Pamoja ya kupanga bei elekezi za madini huku ikishirikisha serikali na wadau wa madini na pia kuiomba serikali kuangalia mifumo ya kodi.

Akizungumzia ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite Mirerani, alisema kuwa, Tamida inaunga mkono jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli na kueleza kuwa, ukuta huo umesaidia kulinda rasilimali na udhibiti wa madini hayo.

Mollel aliongeza kuwa, ukuta wa mirerani umezuia uingiaji holela katika migodi hiyo kwa kuwa kila mwingiaji inampasa kuwa na kitambulisho na uwepo wa geti moja tu.

Pia, alisema kuwa, ukuta huo umeongeza Imani kubwa kwa walaji wa madini hayo zikiwemo nchi za Marekani na Ulaya na kuongeza kuwa, “ukuta umedhibiti ajira za watoto migodini na kuondoa wizi wa vifaa  migodini”.

Read more

Waziri Kairuki atembelea eneo la Mpaka wa Namanga

Na Asteria Muhozya,

Waziri wa Madini Angellah Kairuki, akiongozana na Mkuu wa  Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo , Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Longido pamoja na ujumbe aliombata nao wakati wa ziara yake mkoani Arusha, tarehe 9 Agosti,2018, alitembelea eneo la Mpaka wa Namanga, linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Anorld Kisheshi wakati akitoa ufafanuzi wa namna scanner katika eneo hilo zinavyofanya kazi.

Waziri Kairuki alitembelea eneo husika kwa lengo la kukagua na kuangalia namna shughuli za udhibiti wa utoroshaji wa madini  maeneo ya mipakani  zinavyoendelea.

Waziri Kairuki alisema baada ya kufika eneo husika alikuta kuna suala la changamoto ya upungufu wa wafanyakazi na hivyo kuahidi kulifanyia kazi kwa haraka suala hilo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alisema changamoto katika eneo hilo ni upungufu wa wafanyakazi na kuongeza kuwa, tayari Waziri wa madini ameahidi kulifanyia kazi suala husika ili kudhibiti utoroshaji madini katika maeneo ya mipaka.

Aliongeza kuwa, tayari Serikali ya Wilaya imeanza kuweka alama kujua mipaka ya Tanzania katika eneo husika ikiwemo kufuatilia njia za panya ambazo zinaweza kutumika kutorosha madini nje ya nchi.

Naye Mkaguzi wa Migodi, Anold Kisheshi alisema kuwa, serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali kudhibiti utoroshaji wa madini katika maeneo ya mipaka.

Read more

Serikali kutoa Hati ya Makosa kwa wasioendeleza maeneo ya Madini

Na Asteria Muhozya, Longido

Serikali imesema itatoa Hati za Makosa kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji madini ambao hawajaendeleza maeneo yao na endapo hawatatii matakwa ya Sheria, watafutiwa leseni zao na maeneo  yao kupewa wombaji wengine.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki ( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) wakiangalia madini ya Ruby walipotembelea mgodi wa Mundarara Mine uliopo katika kijiji cha Mundarara , Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha, wakati wa ziara ya Waziri Kairuki katika machimbo hayo.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki tarehe 9 Agosti, katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake alipotembelea machimbo ya Ruby katika Kijiji cha Mundarara, Kata ya Mundarara, Wilaya ya Simanjiro mkoani Arusha.

Waziri Kairuki alitembelea migodi inayochimba madini ya Ruby katika eneo la Mundarara ili kuna namna shughuli za uchimbaji  wa madini hayo zinavyofanyika ikiwemo masuala ya afya na usalama migodini, kusikiliza changamoto na migogoro iliyopo katika machimbo hayo.

Alisema kuwa, Serikali inawajali wachimbaji wadogo nchini na kuwataka wenye nia ya kumiliki leseni za madini kufika katika ofisi za madini kwa ajili ya kupata taratibu za uombaji na  taratibu nyingine za umiliki wa leseni na kuongeza kuwa, bado serikali inaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini.

Akizungumzia suala la utoaji ruzuku, Waziri Kairuki alimsema serikali inaangalia mfumo bora ambao inaweza kuutumia katika kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini na kueleza kuwa, ruzuku hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa  vifaa ama  namna nyingine.

Mwekezaji wa mgodi wa madini ya Ruby wa kampuni ya Mundarara Mine, akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki Seal inayotumiwa mgodini hapo kufunga eneo yanapohifadhiwa madini ya Ruby baada ya uzalishaji.

Pia, Waziri Kairuki aliwakumbusha wamiliki wa leseni za madini kuhakikisha wanajitambulisha katika ofisi za vijiji  mahali yalipo maeneo yao kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji madini ili kutambuliwa  na uogozi wa kijiji  jambo ambalo litasaidia kuondoa migogoro.

Vilevile, Waziri Kairuki aliwataka wamiliki wa leseni za madini kuandaa Mpango wa Uwajibikaji kwa jamii na kueleza kuwa,  kwa mujibu wa sheria ya madini, mwekezaji anapaswa kushauriana na wananchi  wa eneo husika, chini ya usimamizi wa Halmashauri kuhusu maeneo ya uwajibikaji katika uwekezaji wake.

Pia, alizungumzia suala la Mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi huku akisisitiza kuwa, endapo kuna shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wananchi katika eneo husika, ni muhimu  jambo husika lifanyike hivyo.

Akitolea ufafanuzi suala la uongeaji thamani madini, alisema kuwa, serikali imekataza kusafirisha madini ghafi nje ya nchi ili yaongezewe thamani nchini na kueleza kuwa, tayari imeandaa mwongozo wa kutafsiri  dhana nzima ya uongezaji thamani madini na baada ya muda mfupi ujao itazungumzia kuhusu jambo hilo.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki asalimiana na baadhi ya kina mama wa Kijiji cha Mundarara mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho ili kuzungumza na wananchi. Wanaofuatilia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (katikati kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe.

Waziri Kairuki alitoa ufafanuzi huo,  baada ya wawekezaji katika machimbo ya Ruby mundarara kuwasilisha ombi la kutaka madini hayo yasifirishwe yakiwa ghafi kutokana na aina ya madini yenyewe.

Pia, Waziri Kairuki alisema kuwa,Wizara kupitia Tume ya Madini itakuwa ikitoa bei elekezi za madini kila mwezi na kusimamia suala la uendeshaji wa minada ya madini nchini.

Aidh, masuala mengine aliyoyasisitiza Waziri Kairuki katika mkutano huo ni pamoja wachimbaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Wachimbaji kutunza kumbukumbu za uzalishaji na kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa za wanaotorosha madini nje ya nchi

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano huo, alimtaka Waziri kupitia wizara yake kutoa ufafanuzi wa Sheria ya madini ili kuwawezesha wachimbaji kuitekeleza kwa mujibu wa kanuni na taratibu zake.

Pia, alimtaka Waziri wa Madini kusaidia kuweka mfumo mzuri wa biashara ya madini hayo na kuongeza kuwa, endapo kutawekwa mazingira mazuri ya biashara ya  madini hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa eneo husika, wilaya na hatimaye taifa.

Afisa Madini akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki maumbile ya miamba katika migodi yanapochimbwa madini ya Ruby katika eneo la Mundarara alipofika ili kusikiliza mgogoro uliopo baina ya wawekezaji wanaofanya shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Awali, akisoma risala ya kijiji, katika mkutano huo, Diwani wa Kata  Mundarara, Alais Mushao aliwasilisha changamoto ya soko la kuuzia madini ya ruby na kumuomba Waziri asaidie kuhakikisha kuwa, wawekezaji wadogo kupewa fursa sawa.

Katika mkutano huo, ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya , Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Ofisi za Madini.

Read more

Serikali yamjia juu mwekezaji mgodi wa CANACO,ulipo Magambazi kukiuka Sheria ya Madini

Na Zuena Msuya, Tanga

Serikali imeiagiza Tume ya Madini Tanzania, kutoa hati ya makosa kwa Kampuni ya Canaco inayomiliki leseni ya Uchimbaji Madini wa Kati  iliyopo katika Kijiji cha Magambazi Wilayani Handeni Mkoani Tanga, na kuzuia mali na mitambo yote iliyopo eneo hilo kutokana kukiuka masharti ya leseni hiyo ya uchimbaji madini ya dhahabu na kwenda kinyume na Sheria ya Madini yam waka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 pamoja na kanuni za mwaka 2018.

Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (katikati) akiwa katika baadhi ya vitendea kazi vya mgodi wa Madini Mali ya kampuni ya Canaco, vilivyozuiliwa kuondolewa eneo hilo hadi pale watakapofuata sheria za uchimbaji madini.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko, wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uchimbaji madini katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, ambapo pamoja na mambo mengine pia aliagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi katika sakata la utoroshwaji wa Carbon zenye madini ambazo ziliibwa usiku kutoka eneo hilo na kupelekwa mkoani Mwanza kwa ajili ya kuyeyushwa ili kupata dhahabu kinyume cha utaratibu.

Waziri Biteko alisema kuwa mwekezaji huyo awali alifika katika Wizara ya Madini na kuomba kibali cha kusafirisha carbon tani 2.23 kwenda mkoani Mwanza katika kiwanda cha JEMA AFRICA LTD  kwa ajili ya kuchenjuliwa lakini wakanyimwa kutokana na matatizo yao ya ndani  lakini baadae wakachukua kibali cha kughushi kutoka Dodoma kwa ajili ya kusafirishia carbon kupeleka Mwanza.

“Hawa watu walikuja ofisini ya madini Handeni  kuomba kibali cha  kusafirisha carbon tani 2.23 kwenda Mwanza kwa ajili ya kuchenjuliwa lakini walinyimwa kutokana na sababu zao za ndani zilikuwepo muombaji kutokuwa mmiliki wa leseni ya Canaco lakini cha kushangaza walitorosha carbon tani 2.23 usiku wa manane na kwenda kuchukua  kibali cha kughushi   kutoka  ofisi ya madini Dodoma kinachoonesha carbon tani 1.5 tu”alisema.

Aliongeza “Baada ya kuichakata carbon tani 1.5 Mwanza  kiasi kingine hakijulikani kilipo mpaka sasa haiwezekani jambo hili lichukue muda katika uchunguzi nakuagiza OCD kadri utakavyoona katika harakati zako za kiuchunguzi hawa watu wakamatwe na nawaomba TAKUKURU nao watusaidie katika kuchunguza wa jambo hili” alisema.

Naibu Waziri,Dotto Biteko (kulia),Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe (Katikati)wakikagua eneo la mgodi wa Madini, katika kijiji cha Magambazi wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mbali na hivyo pia aliumuelekeza Kamishna wa Tume ya Madini Dkt.Athanas Macheyeka kumpa mwekezaji huyo hati ya makosa (default notice) kwa ajili ya kurekebisha makosa waliyonayo kwenye leseni ya uchimbaji wa madini na kama watashindwa  kurekebisha makosa kwa muda uliotajwa na sheria, leseni yao ifutwe wapewe wawekezaji wengine walio makini.

“Sheria ya madini inamtaka mwenye leseni ya madini achimbe siyo atumie mabaki yaliyochimbwa na wachimbaji wengine ayachenjue……kamishna wa tume ya madini kati ya leo na kesho wape ‘default notice’ kwa ajili ya kurekebisha makosa yao na wasipo rekebisha leseni yao ifutwe watafutwe wawekezaji wengine serious” alisema.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe alimuhakikishia Naibu Waziri kutekeleza maagizo aliyoyatoa kwa kuwachukulia hatua kali wawekezaji hao ikiwemo  kuwakamata wahusika.

Alisema kuwa awali baada ya kubaini wizi katika mgodi huo aliunda kamati ya ulinzi na usalama iliyohusisha Afisa madini mkazi,Afisa maendeleo,Afisa misitu na Afisa usalama  ambapo baada ya uchunguzi  kwenye mgodi ,maabara ,makontena pamoja na  kwenda  kwenye maabara za madini Dodoma,Bahi na Mwanza  walibaini carbon hiyo iliibwa na kupelekwa kwatika kiwanda hicho cha JEMA AFRICA LTD.

Katika taarifa ya kamati ya maalum iliyoundwa na Wilaya ya Handeni kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri Biteko alipotembelea mgodi huo mapema mwaka huu  ilibaini  makosa tisa  ambayo ni ukiukwaji  wa sheria,kanuni na utaratibu wa kuingia mkataba usiotambulika kisheria kati ya kampuni ya CANACO na TANZANIA GOLD FIELDS,mgodi kutoendelezwa kwa muda uliopangwa kisheria ndani ya miezi 18,kuchenjua madini bila leseni na utumiaji wa kemikali ya Sayanaidi bila ya kibali cha mkemia mkuu wa serikaiai.

Mambo mengine ni kuwepo kwa udanganyifu wa kampuni ya CANACO na TANZANIA GOLD FIELDS kwa kudai kuwapo katika hatua ya majaribio wakati kuna usimikaji wa mitambo ya uchenjuaji bila kibali cha mkaguzi mkuu wa mgodi,kuendesha shughuli za mgodi bila kuwepo na meneja aliyeteuliwa kisheria,kufanya uchenjuaji wa madini  na marudio ya uchimbaji unaosababisha uharibifu wa mazingira bila ya kuwa na vibali vinavyostahiki,kusimika mtambo wa uchenjuaji wa marudio bila ya kuwa na vibali vya mkaguzi mkuu wa mgodi.

Read more

Maafisa madini watakiwa kufuata sheria, kanuni katika utoaji leseni

Na Greyson Mwase, Morogoro

Maafisa madini nchini wametakiwa kufuata sheria na kanuni katika utoaji wa leseni za madini ili kuondoa changamoto ya migogoro kwenye migodi ya madini.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akielezea taratibu za utoaji wa leseni za madini kwenye mafunzo ya kazi kwa viongozi na maafisa waandamizi wa Tume ya Madini yanayoendelea mjini Morogoro tarehe 08 Agosti, 2018.

Hayo yamesemwa leo tarehe 08 Agosti, 2018 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya alipokuwa akitoa mafunzo juu ya taratibu za utoaji wa leseni za madini kwenye mafunzo ya kazi kwa viongozi na maafisa waandamizi wa Tume ya Madini yanayoendelea mjini Morogoro.

Alisema kuwa, ni vyema taratibu za utoaji wa leseni za  utafutaji wa madini zikafuatwa ambazo ni pamoja na mwombaji kubaini eneo linalomfaa kwa utafiti, kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha Tume ya Madini kwa njia ya mtandao na nakala halisi (hard copies) na ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na kutathiminiwa.

Aliendelea kueleza taratibu nyingine  kuwa ni pamoja na ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni, mmiliki wa leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la utafutaji madini, mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za halmashauri/wilaya kuandaa mpango wa utoaji wa huduma za jamii.

Akielezea taratibu za maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini, Profesa Manya alieleza kuwa ni pamoja na mwombaji kubaini eneo linalomfaa, mwombaji kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi kwa njia ya mtandao na nakala halisi, ombi kupendekezwa na kukubaliwa kupewa leseni, mmiliki wa leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la utafutaji wa madini na mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za halmashauri/wilaya kuandaa mpango wa utoaji wa huduma za jamii.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (hayupo pichani).

Katika hatua nyingine akielezea taratibu za utoaji wa leseni za uchimbaji  wa kati na mkubwa Profesa Manya alitaja kuwa ni pamoja na  mwombaji kubaini eneo la leseni ya utafutaji, kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha Tume ya Madini Makao Makuu kwa njia ya mtandao na nakala halisi (hard copies) na uthibitisho wa uwepo wa mradi wa uchimbaji, upembuzi yakinifu (feasibility Study) na hati ya utunzaji wa mazingira.

Alieleza taratibu nyingine kuwa ni pamoja na ombi kushughulikiwa, kuhakikiwa na kutathminiwa na ombi kupendekezwa kupewa leseni na kuendelea kufafanua kuwa hatua nyingine ni pamoja na ombi la leseni kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri kwa leseni ya uchimbaji mkubwa, (Special Mining Licence), ombi la leseni  kukubaliwa kupewa leseni na mmiliki wa leseni kuomba ridhaa kwa mmiliki halali wa ardhi ya kuingia kwenye eneo la uchimbaji.

“ Mmiliki wa leseni atatakiwa kuomba ridhaa ya uwekezaji kwenye mamlaka ya serikali za mitaa, mmiliki wa leseni kwa kushirikiana na mamlaka za halmashauri/wilaya  kuandaa mpango wa utoaji wa huduma kwa jamii” alisisitiza Profesa Manya.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa leseni za uchenjuaji wa madini, Profesa Manya alisema leseni hutolewa kwa kipindi kisichozidi miaka 10 na Tume ya Madini kwa mtu au kampuni/ushirika katika eneo ambalo lipo nje ya eneo la mmiliki wa leseni ya uchimbaji wa madini.

Aidha,  akielezea leseni za uyeyushaji wa madini, Profesa Manya alisema kuwa leseni hutolewa kwa kipindi  kisichozidi miaka 25 kwa mtu, kampuni au ushirika.

Wakati huo huo akielezea sifa za mwombaji wa leseni, Profesa Manya alieleza kuwa ni pamoja na mwombaji kuwa na umri usio chini ya miaka 18  na mwenye uwezo wa kifedha, kutokuwa na makosa katika umiliki wa leseni ya madini iliyo hai au iliyoisha muda au iliyofutwa ambayo hayakurekebishwa, kutokuwa na makosa yoyote likiwamo la kutokuwa mwaminifu na kampuni husika kuwa na anwani  ya posta na ofisi.

Read more

Viongozi wasiokwenda na kasi ya Tume ya Madini kutenguliwa

Greyson Mwase na Asteria Muhozya, Morogoro

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema kuwa viongozi pamoja na maafisa waandamizi walioteuliwa kufanya kazi katika Tume ya Madini teuzi zao zinaweza kutenguliwa iwapo watafanya kazi kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati waliokaa mbele) Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu waliokaa mbele) Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila ( kushoto waliokaa mbele), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, (wa pili kushoto waliokaa mbele) na , Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga (wa pili kulia waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Tume ya Madini.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 06 Agosti, 2018 wakati wa ufunguzi wa mafunzo  ya kazi kwa viongozi  na maafisa waandamizi wa Tume ya Madini  iliyofanyika mjini Morogoro na kuhudhuriwa na watendaji na watumishi kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. delardus Kilangi.

Alisema kuwa, Serikali imewateua kufanya kufanya kazi na Tume ya Madini  huku ikiwa na matarajio makubwa ikiwa ni pamoja na kuondoa kabisa urasimu kwenye utoaji wa leseni kwa kuhakikisha kuwa wanatoa leseni kwa wakati, kutatua mogogoro ya wachimbaji wadogo na kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini.

Aidha, Waziri Kairuki aliongeza kuwa watendaji wapya wanatakiwa kuwa makini kwenye zoezi zima la utoaji wa leseni kwa kuhakikisha kuwa wanahakiki historia za waombaji wa leseni kwenye uchimbaji madini kabla ya kutoa leseni mpya.

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) kwenye mafunzo hayo.

“Ni vyema mkahakikisha kuwa mnafahamu kwa kina historia za waombaji wa leseni za madini hususan kwenye mapato na matumizi kwa mwaka, ulipiaji wa leseni, ushiriki katika utoaji wa huduma za jamii, uzingatiaji wa kanuni za uhifadhi na mazingira na kuwapatia leseni waombaji  wale tu watakaokidhi vigezo,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Katika hatua nyingine,Waziri Kairuki alitoa onyo kwa watumishi watakaothubutu kuhujumu mfumo wa huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao ujulikanao kama online mining cadastre transactional portal na kuongeza kuwa Wizara haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watakaohujumu mfumo.

Waziri Kairuki aliwataka maafisa madini wa mikoa kuhakikisha wanaainisha maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa madini na kumpatia taarifa mapema na kuhakikisha wanafanya mikutano ya mara kwa mara na wachimbaji wadogo ili kubaini changamoto zao.

Awali akielezea mafunzo hayo, Waziri Kairuki alisema mafunzo hayo ya siku sita yatalenga kutoa elimu kuhusu historia ya mabadiliko ya sheria ya madini, sheria ya madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017, muundo wa tume ya madini na mawasiliano ya ndani na nje ya tume.

Kutoka kushoto, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya, Kamishna wa Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo.

Aliendelea kueleza maeneo mengine kuwa ni pamoja na muundo na mfumo wa mawasiliano wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), taratibu za ofisi na makusanyo na maduhuli ya Serikali kwa njia ya kieletroniki (GEPG), usimamizi na utunzaji wa mali za umma, taratibu za utoaji wa leseni za shughuli za madini na ushirikishwaji wa wananchi/wazawa katika shughuli za madini.

Maeneo mengine ni pamoja na ukaguzi wa madini na biashara, utatuzi wa migogoro katika sekta ya madini, taratibu za uwasilishaji wa taarifa makao makuu ya Tume na kwenye mamlaka nyingine zinazohusika, utunzaji wa siri katika utumishi wa umma, masuala ya utawala na rasilimaliwatu, sheria, kanuni na taratibu za fedha, usimamizi wa mifumo ya udhibiti wa ndani, maadili katika utumishi wa umma na mfumo wa uwazi wa upimaji utendaji kazi (OPRAS).

Alisema kuwa  kwa kuwa tume imepata watumishi wa kutosha inatakiwa kuunda kamati mbalimbali za kisheria na kitendaji kama vile kamati ya maadili, kamati ya ukaguzi, kamati ya ajira za kigeni na baraza la wafanyakazi ili kuifanya tume iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Kaimu Mhasibu Mkuu wa Tume ya Madini, Avodia Lukonge (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkaguzi wa Ndani kutoka Tume ya Madini, Happiness Shirima kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa mafunzo hayo.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza katika mafunzo hayo alimshukuru Waziri Kairuki kwa uteuzi wa watendaji wapya wa Tume ya Madini na kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuyafanyia kazi yote watakayojifunza.

Wakati huohuo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi alisema kuwa mabadiliko ya sheria ya madini yaliyofanyika Tanzania ni hatua ya ushujaa na kuongeza kuwa mataifa mengine yameanza kujifunza.

Alisema kutokana na muhimu wa Sekta ya Madini kwenye mchango wa ukuaji wa uchumi wa nchi ameamua kufika mwenyewe kuja kutoa mafunzo kwa viongozi na maafisa waandamizi wa Tume ya Madini ili waweze kusimamia ipasavyo sekta hiyo kwa kutumia sheria na kanuni za madini.

 

Read more

Leseni za Madini sasa kutolewa kwa Masharti Magumu-Kairuki

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema kuanzia sasa Serikali itaanza kutoa Leseni za madini biashara ya madini kwa masharti magumu huku ikimtaka kila mwombaji  kutoa taarifa za mauzo ya uzalishaji, usafirishaji pamoja na mnyororo mzima wa biashara ya madini ikiwemo fedha zinazoingia nchini kutokana na biashara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya (katikati) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhandisi Tumain Magesa (kulia).

Pia, ameiagiza Tume ya Madini kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kila jambo katika mnyororo huo linasimamiwa kikamilifu na kuongeza kuwa, yeye kama waziri mwenye dhamana atahakikisha anafuatilia kila hatua itakayochukuliwa  na tume hiyo.

“Tume ichukue hatua. Nitakuwa na ninyi. Msiache hata mmoja atakayekwenda kinyume na haya. Nilifanya hivyo katika Sekta ya Utumishi wa Umma hata huku kwenye sekta ya madini, sitashindwa kufanya hivyo,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Waziri kairuki aliyasema hayo jana tarehe 3 Agosti, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara wakati akipokea taarifa ya Kamati Maalum iliyoundwa kuchunguza mnyororo wa madini ya vito nchini.

Kamati hiyo ilifanya kazi yake kwa muda wa siku 30  kuanzia tarehe 26 Aprili, 2018 kwa  jukumu la kuchunguza  mnyororo wa madini ya vito  kuanzia kuzalisha hadi usafirishaji nje ya nchi pamoja na kubaini sababu za utoroshaji wa madini na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuzuia utoroshaji.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akifurahia jambo na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na kusshoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Pia, aliiagiza tume ya madini kuanzia tarehe 4 Agosti, kuhakikisha inapata taarifa za uzalishaji za migodi yote inayozalisha huku akitaka migodi husika ieleze mahali inakouzia madini yao, anayeuziwa madini hayo na kuongeza kuwa, zoezi husika linawajumuisha pia dealers.

Waziri Kairuki alisema, wizara yake imeamua kusimamia suala husika ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli za kuhakikisha kuwa rasilimali madini zinawanufaisha watanzania wote.

“ Lazima watanzania tutambue kuwa madini haya yanamilikiwa na watanzania wote. Tunatakiwa kuyalinda kwa ajii ya maendeleo yetu na kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” alisema Kairuki.

Akizungumzia biashara ya madini ya tanzanite katika ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite mirerani, alisema hakuna serikali inayotaka watu wake wasifanye biashara, hivyo, lengo la ukuta huo ni kuhakikisha kwamba inadhibiti utoroshaji wa madini na kuweka mfumo mzuri ambao utawezesha madini hayo kuzinufaisha  pande zote.

Alisema tayari wizara imeandaa Kanuni za Mirerani (Mirerani Contolled Area) ambazo hivi sasa zinafanyiwa maboresho  baada ya kuwepo changamoto kadhaa katika utekelezaji wake.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini na wabunge wengine wa Mkoa wa Manyara, Kilimanjaro na Arusha.

Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki alisema serikali imebaini  baadhi ya wenye leseni za ‘broker’ kukaribisha wageni kutoka nje kufanya biashara hiyo kinyume na taratibu na  hatimaye kusafirisha madini hayo, hivyo, aliwataka wote wanaofanya hivyo kuacha mara moja na kuwataka watanzania wote wenye taarifa kuhusu suala hilo kutoa taarifa  katika mamlaka zinazohusika.

“Kamati hii imefanya uzalendo na imefanya kazi kubwa sana. Nimeipokea taarifa ya kamati lakini natamani wangenitajia majina ya watoroshaji. Nilitamani sana kuona majina lakini naamini itaniuma sikio,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Pia, aliongeza kuwa serikali itazifuta leseni za  uchimbaji madini kwa wale wote ambao wameshindwa kuyaendeleza maeneo yao na kupewa wengine wenye nia ya dhati ya kuendeleza shughuli za uchimbaji madini nchini.

Akizungumzia mkakati wa serikali katika kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani nchini, alisema kuwa serikali inaendelea kukiimarisha kituo cha TGC kilichopo jijini Arusha, kwa kuongeza wataalam katika masuala ya ukataji na unga’rishaji wa madini ya vito.

“Tayari tumepata walimu  7 kutoka nchini India, lakini bado tunafuatilia wengine kutoka nchini Thailand,”alisema Kairuki.

Akiwasilisha  taarifa ya Kamati kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo,  Mratibu wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Eric Mpesa alisema Kamati husika ilipata fursa ya kutembelea mgodi wa Mundarara mpaka wa Namanga, Uwanja wa ndege wa KIA, Machimbo ya Tanzanite Mirerani, TGC, Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Morogoro na Machimbo ya Epanko, Morogoro

Akiwasilisha mapendekezo ya kamati husika Mpesa alisema kuwa, kamati inapendekeza Serikali kutengeneza mpango wa makazi katika eneo lililozungushiwa ukuta wa Mirerani ikizingatia uwepo wa eneo la uchimbaji, biashara, uanzishwaji wa kituo cha One Stop Centre, huduma za kijamii, maegesho ya vyombo vya usafiri, maeneo ya starehe na maeneo ya utalii.

Pia, alisema serikali ihakikishe kuweka mfumo wa ulinzi katika eneo lililozungushiwa ukuta na pia ilishauri serikali kuongeza wataalam wa Wizara katika maeneo ya migodi ili kurahisisha ufanyaji biashara na kuwezesha kuzuia utoroshaji wa madini ya vito.

Pendekezo lingine ni serikali kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata teknolojia za kisasa pamoja na tafiti za kijiolojia kufanywa na watalaam  kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa malipo ya gharama nafuu yatakayolipwa  baada ya uzalishaji kupatikana.

Pia, Kamati ilipendekeza seriakali kuishawishi mifuko ya jamii isaidie wadau  kuanzisha benki ya Madini itakayowapa wachimbaji na wafanyabiashara mikopo yenye masharti nafuu.

Akizungumzia mcchango wa sekta ya madini, alisema sekta hiyo inachangia fedha za kigeni cha kiasi cha wastani wa dola za Marekani milioni 27.8 kwa mwaka isipokuwa almasi na kati ya hizo, asilimia 27.8 ni madini yaliyosanifiwa na kunga’rishwa na asilimia 71.3 ni madini ghafi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Alexander  Mnyeti alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikichazewa kwa wadau katika migodi kutokulipa kodi stahiki za serikali.

Aliishauri wizara kufuta leseni za wale wote walioohodhi maeneo yao bila kuyafanyia kazi ili kuwezesha leseni husika kutumiwa na wengine wenye nia ya kuendeleza sekta ya madini.

Kuhusu suala la mikataba  ya ajira katika migodi hiyo aliishauri serikali na wadau kukaa pamoja na kujadili suala husika na kulitafutia ufumbuzi.

Kamati iliyoandaa taarifa husika ilikuwa na wajumbe 13 ikiongozwa na Mwenyekiti Sammy Mollel, Makamu Mwenyekiti Hamis Kim, Katibu Adam Rashid pamoja na wajumbe 10 na Sekretarieti.

Wajumbe wa Kamati hiyo walitoka TAMIDA, MAREMA, AREMA, RUVREMA, TAWOMA, BROKER pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Madini na TGC.

Imeandaliwa na:

Asteria Muhozya, Simanjiro

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@madini.go.tz,                                             

Tovuti: madini.go.tz

Read more

Serikali kuweka mbinu za kisasa ulinzi Mirerani

Serikali imesema inajiandaa kuja na mbinu za kisasa zaidi za ukaguzi na ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite, Mirerani  ili kudhibiti utoroshaji wa madini hayo yanayopatikana Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki akisisitiza jambo wakati akizungumza na katika mkutano wa hadhara na wananchi wanaofanya shughuli zao ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, mirerani. Wanaofuatilia mbele ni Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya (kulia) na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumain Magesa.

Hayo  yalisemwa na Waziri wa Madini Angellah Kairuki  tarehe 2 Agosti, 2018 wakati wa mkutano wa hadhara ulishirikisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji na wote wanaofanya shughuli zao za ndani ya ukuta huo.

Alisema, mabadiliko ya ujenzi wa ukuta huo ni chanya ambayo yamelenga kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini ili kuongeza mchango wa sekta husika katika pato la taifa.

Waziri Kairuki alieleza  ili shughuli za uuzaji na ununuzi ziweze kufanyika ndani ya eneo hilo, tayari Serikali imejenga sehemu maalum kwa ajili ya shughuli  hizo na kuongeza, “ baada ya kukamilika jengo hilo kutakuwa na sehemu kwa ajili ya Broker kufanyia shughuli zao hapo hapo ndani ya ukuta.”

Aliongeza, tayari Mkataba wa ujenzi wa Kituo cha kufanyia shughuli zote zinazohusu biashara ya madini ya tanzanite kwa ujumla (One Stop Center) umekwishakabidhiwa na ndani ya muda mfupi ujao, ujenzi wa jengo husika utaanza.

Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara ambao ulijumuisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji, wanunuzi na wanaofanya shughuli mmbalimbali ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mireran wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki, hayupo pichani.

Akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za kuingia na kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya ukuta, Waziri Kairuki alisema taratibu za ukaguzi zinalenga katika kudhibiti utoroshaji madini na hivyo kuwataka wadau wote kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la ukaguzi katika ukuta huo na kuongeza kuwa, aina ya ukaguzi unaofanywa kwa sasa ni wa muda mpaka hapo taratibu maalum za ukaguzi zitakapokuwa tayari.

Akitoa ufafanuzi kuhusu wazawa wenye leseni za uuzaji kulipa ada kwa  kutumia Dola za Marekani, Waziri Kairuki alieleza kuwa, kwa kuwa Kanuni za eneo la Mirerani zimeandaliwa na Waziri mwenye dhamana na sekta, suala hilo litafanyiwa kazi ili kipengele husika kiweze kufanyiwa marekebisho na hivyo kuwawezesha kulipia kwa fedha za Tanzania. Pia, aliongeza kuwa, katika kipindi hiki ambacho mabadiliko hayo hayajafanyika, wahusika watalazimika kuendelea na utaratibu uliopo.

Ili kuongeza kasi ya shughuli ya uthamini wa madini hayo, waziri Kairuki alisema wizara yake itaongeza idadi ya wataalam kutoka mmoja hadi wanne ili kuongeza kasi ya kufanya shughuli husika.

Pia, Waziri Kairuki aliwataka wamiliki wa migodi kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya wafanyakazi katika migodi yao na kuongeza kuwa, suala la maslahi ya watumishi ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na wadau wote katika sekta husika.

Sehemu ya wananchi waliofika katika mkutano wa hadhara ambao ulijumuisha wamiliki wa migodi, wachimbaji, wauzaji, wanunuzi na wanaofanya shughuli mmbalimbali ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Mireran wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki, hayupo pichani.

“Maslahi ya wafanyakazi yanatakiwa kuwa namba moja. Mimi ni Mbunge niliyechaguliwa kupitia umoja wa vyama vya wafanyakazi hivyo suala la maslahi ya wafanyakazi lazima nilisimamie kikamilifu,” alisisitiza Kairuki.

Akizungumzia suala la usafiri ndani ya ukuta, alisema zoezi husika litaendelea kama ilivyo sasa na kutumia fursa hiyo kukaribisha wawekezaji zaidi katika huduma ya kutoa  huduma ya usafiri ndani ya ukuta huo.

Pia, alitumia fursa hiyo kuwataka wadau wote katika eneo hilo kuwa waaminifu na kushirikiana na serikali na hususan ofisi ya Madini katika kutoa taarifa za utoroshaji madini hayo.

Mwisho aliwataka Maafisa Madini  kuendelea kutoa elimu ya Sheria ya Madini pamoja na taratibu zake pia, Mbunge wa eneo husika aendelee kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa ukuta huo ili kuwawezesha wadau wote kuwa na uelewa wa pamoja.

Kwa upande wake, Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya, alisema alimweleza Waziri Kairuki kuwa kero kubwa katika eneo husika ni baina ya wamiliki wa migodi na wafanyakazi na hivyo kumtaka Waziri kuona namna ya kushughulikia suala hilo.

Pia, alipendekeza kuundwa kwa kamati mbili moja ikiwa ya wamiliki na wafanyakazi kwa lengo la kuondoa mvutano uliopo sasa kati ya pande mbili.

Imeandaliwa na:

Asteria Muhozya, Simanjiro

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@madini.go.tz,                                             

Tovuti: madini.go.tz

Read more

Naona fahari uwekezaji wa Mwanga Gems-Kairuki

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema anaona fahari kutokana na uwekezaji wa Kiwanda cha Kuchakata madini ya Kinywe (Graphite) uliofanywa na Kampuni ya wazawa ya GOD Mwanga Gems Ltd iliyopo Kata ya Endiamtu, Wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

Waziri wa Madini Angellah Kairuki (katikati) akipita katika maeneo mbalimbali ya kiwanda cha God Mwanga Gems Ltd kuona namna shughuli mbalimbali za uchakataji wa madini ya Kinywe zinavyofanyika.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 2 Agosti, alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea shughuli zinazofanywa na kiwandani hapo.

Amesema Serikali imekuwa ikihamasisha waombaji wa leseni za madini kuwekeza katika maeneo mbalimbali hivyo, jambo lililofanywa na kiwanda hicho ikiwemo malengo ya kiwanda husika kufungua  viwanda vingine katika mikoa ya Tanga na Manyara ni jambo la kujivunia na fahari kwa Tanzania.

“Nimefurahishwa sana namna kampuni hii inavyofanya kazi. Serikali kupitia wizara yangu imekuwa ikihamasisha uwekezaji. Tuko tayari kuwasimamia na kuwasaidia katika hili. Tunataka kutengeneza ajira zaidi, kukuza uchumi kupitia madini lakini pia serikali kupata kodi,” amesisitiza Kairuki.

Akijibu ombi la kampuni hiyo kupata kibali cha kuuza madini hayo nje, Waziri Kairuki ameahidi kampuni hiyo kuwa mara baada ya taratibu za utoaji vibali kukamilika Wizara kupitia Tume ya Madini itatoa kibali kwa kampuni husika iendelee na taratibu zake za  kuuzwa nje ya nchi madini hayo.

Mmiliki wa kampuni ya God Mwanga Gems Ltd.Godlisten (kulia) Mwanga akimwonesha Waziri wa Madini Angellah Kairuki madini ya Grahite ambayo tayari yamechakatwa.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Kairuki amewataka wenye leseni za madini kutozitumia leseni hizo kuziweka rehani kwa kuwa Sheria ya Madini inakataza jambo hilo badalayake zinatakiwa kutumiwa katika malengo yaliyokusudiwa.

“Wapo baadhi ya wawekezaji wamepewa leseni lakini hawajafanya chochote wengine wanaweka rehani leseni hizi. Nafurahi kuona mzawa mwenzetu amefanya jambo kubwa kama hili, leo nimejionea uhalisia  katika jambo hili,” amesema Waziri Kairuki.

Pia, Waziri Kairuki ameishauri kampuni husika kuendelea kuitumia Maabara ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania (GST) kwa ajili ya shughuli za utafiti na pia kuwatumia wahitimu wa Chuo Cha Madini Dodoma (MRI) katika suala la ajira.

Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki amesema Wizara imewachukulia hatua watumishi 40 kutokana na kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma katika suala zima la usimamizi katika sekta husika.

“Wapo tuliowahamisha vituo vya kazi, wengine tumewasimamisha. Tunachotaka ni kuendana na kasi na huku wakizingatia maadili ya utumishi,” amesema Waziri Kairuki.

Aidha, amesisitiza suala la wawekezaji kuendelea kutoa taarifa za uzalishaji ili  serikali iweze  kupata kodi zake  huku akisisitiza suala la ulipaji kodi  kwa serikali na wenye leseni zao kuzitumia na kuzalisha kwa viwango vinavyohitajika.

Kwa upande, Meneja wa Kiwanda hicho Henry Mbando ameiomba serikali kukisaidia kiwanda hicho kupata kibali kwa ajili ya kuuza madini hayo nje ya nchi ambayo yana masoko katika nchi za Marekani, Kanada, China na ulaya.

Ameongeza kuwa, madini hayo yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali  za viwandani vikiwemo vipuri vya magari, betri za magari na mitambo mengine.

Ameongeza kuwa, soko la madini hayo ni katika nchi za

Akizungumzia idadi ya wafanyakazi waliopo kiwandani hapo amesema kiwanda kina jumla ya watumishi 80 huku waanawake wakiwa 2 na wanaume 78.

Naye, Mmiliki wa kampuni hiyo, Godlisten Mwanga ameishukuru Serikali kwa msamaha wa kodi katika baadhi ya mitambo aliyoinunu kwa ajili ya kiwanda hicho na pia kumshukuru waziri Kairuki kwa kuona umuhimu wa kutembelea kiwanda husika.

Amesema kiwanda hicho kimezalisha tani zaidi ya 2,000 na zilizotayari kwa ajili ya kuuzwa ni tani 200.

Akizungumzia suala la kibali kwa kampuni husika Kamishna wa Madini Mhandisi David Mlabwa amesema kuwa, awali kampuni hiyo ilikuwa haijakidhi vigezo vya kupata kibali lakini baada ya kukidhi viwango hivyo itapatiwa kibali.

Imeandaliwa na:

Asteria Muhozya, Simanjiro

Afisa Habari,

Wizara ya Madini,

Kikuyu Avenue,

P.O Box 422,

40474 Dodoma,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606,

BaruaPepe: info@madini.go.tz,                                             

Tovuti: madini.go.tz

Read more

Watoroshaji Tanzanite kiama kinakuja-Waziri Kairuki

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia  ulinzi  na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda  kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao  kinakuja.

Sehemu ya wachimbaji katika eneo la Lemshuku Wilayani Simanjiro kunakofanyika shughuli za uchimbaji madini ya Green Garnet wakimsikiliza Waziri wa Madini Angellah Kairuki hayupo pichani wakati wa ziara yake katika eneo hilo.

Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini  ya tanzanite ndani ya ukuta wa Mirerani.

Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta unaozunguka migodi  ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini  mengine zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite  unavyoendelea katika migodi husika.

Kairuki aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga  kuangalia namna Sheria ya Madini inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi  na namna migodi husika inavyolipa  kodi  mbalimbali za Serikali  yakiwemo masuala ya usalama sehemu za kazi na  wafanyakazi kwa ujumla.

“Utoroshaji madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,” alisema Kairuki.