Bilionea Lizer aialika tena Serikali Mirerani

Kwa awamu nyingine tena bilionea Saniniu Laizer ameifanya Serikali kufika Mirerani mkoani Manyara yaliko machimbo ya madini ya tanzanite katika hafla ya kukabidhi jiwe lingine la tanzanite lenye uzito wa kilo 6.3317 lililopatikana katikati ya mwezi Juni katika mgodi wake uliopo katika kitalu D ndani ya ukuta unaozunguka machimbo hayo ya madini adhimu duniani. 

Waziri wa Madini Doto Biteko,akiwa na baadhi ya viongozi wa serikali wakikabidhi hundi ya bilioni 4.8 kwa bilionea Saniniu Laizer katika hafla fupi iliyofanyika Mirerani Manyara. Wengine toka kushoto ni Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga,Dkt. Philip Mpango Waziri wa Fedha na Mipango pamoja na naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo

Jiwe hili ni la tatu kupatikana na kuuzwa Serikalini baada ya mawe mengine mawili kununuliwa na serikali katika hafla iliyofanyika tarehe 24 Juni, 2020 mara baada ya mchimbaji huyo kuiarifu Serikali juu ya uwepo wa mawe mawili yenye uzito mkubwa yaliyochimbwa mgodini kwake mnamo tarehe 17 Juni, 2020 yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.

Imeelezwa kwamba ndani ya muda mfupi baada ya Serikali kununua madini hayo kutoka kwa mchimbaji huyo mdogo, mchimbaji huyo alitoa tarifa ya kupatikana kwa jiwe lingine ambapo Serikali imeridhia kununua jiwe hilo na kuifanya Serikali kuwa na mawe matatu ya tanzanite yenye uzito mkubwa kwa uzito wa kufuatana ambapo zito zaidi lina kilo 9.27, kilo 6.33 na kilo 5.103. 

Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika leo tarehe 03 Agosti, 2020, Waziri wa Madini, Doto Biteko aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuacha tabia ya kutorosha madini na kueleza kuwa tabia hiyo haina faida yeyote kwao na zaidi itawasababishia hasara kubwa na kuwapelekea kukamatwa na kushughulikiwa na vyombo vya dola.

Waziri Biteko aliendelea kubainisha kuwa, mnamo tarehe 17 June, 2020 mgodi wa bilionea Laizer ulizalisha kilo 32.872 za tanzanite katika umbali wa mita 1800 chini ya ardhi kwenye mgodi wake uliopo kitalu D uliokuwa na thamani ya shilingi bilioni 8,458,485,970.03 ambapo malipo ya mrabaha na ada ya ukaguzi yalikuwa ni shilingi milioni 507,509,200. 

Akiendelea kuchambua uzalishaji huo, Waziri Biteko alisema ndani ya kilo hizo 32 ndipo yalipopatikana mawe mawili yaliyokuwa na uzito mkubwa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi ambapo kipande kimoja kilikuwa na uzito wa kilo 9.27 na kingine kikiwa na uzito wa kilo 5.103.

Mnamo tarehe 29 Juni, 2020, Serikali iliarifiwa juu ya kupatikana kwa kipande kingine cha tanzanite chenye uzito wa kilo 6.33 kilichopatikana wakati wa zoezi la kusafisha eneo la uzalishaji wa awali yaani ule wa tarehe 17 Juni, 2020 ambapo wachimbaji walikuwa na zoezi la kuondoa miamba iliyokuwa ikikaribia kuanguka ili kuruhusu zoezi la uchorongaji na ulipuaji mwingine kuendelea. Biteko alifafanua.

Biteko amebainisha kuwa, kwa mara nyingine Serikali imeridhia kununua kipande hicho kwa gharama ya shilingi 4,846,537,271.12 kufuatia uthaminishaji uliofanywa na wataalamu wa uthaminishaji madini ambapo shilingi 290,792,236.28 imelipwa kama mrabaha na shilingi 48,465,372.71 imelipwa kama ada ya ukaguzi.  

Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro wakiwa wameshika jiwe la Tanzanite katika hafla ya kiserikali ya kukabidhiwa jiwe toka kwa bilionea Saniniu Laizer

 Akizungumzia faida za ukuta unaozunguka machimbo ya madini hayo ya tanzanite, Waziri Biteko alisema taifa limeshuhudia kuongezeka kwa maduhuli ambapo ndani ya miaka miwili baada ya kujengwa kwa ukuta huo kiasi cha kilo 3,935.43 za tanzanite zenye thamani ya shilingi bilioni 53.141 zilizalishwa na wizara kukusanya mrabaha wa shilingi bilioni 3.9. 

Biteko amebainisha kuwa Serikali imeridhia kununua kipande hicho kwa gharama ya shilingi 4,846,537,271.12 kufuatia uthaminishaji uliofanywa na wataalamu wa madini ambapo shilingi 290,792,236.28 imelipwa kama mrabaha na shilingi 48,465,372.71 imelipwa kama ada ya ukaguzi.

 Akizungumzia kuhusu eneo la kitalu C, Waziri Biteko aliwataka wananchi wa Simanjiro na Tanzania kwa ujumla kutokuvamia eneo hilo kwani Serikali ina taratibu inazozifanya na zitakapokamilika tarifa itatolewa ili kuruhusu shughuli kufanyika sawasawa na maauzi yatakayoagikiwa. 

Aidha aliuhakikishia umma kuwa kamwe eneo hilo halitatolewa kwa wageni ili liweze kunufaisha wazawa na taifa kwa ujumla. “Eneo la kitalu C tutalitoa na wala eneo hilo hatuhitaji mgeni yeyote kuja kuwekeza” Biteko alisisitiza. Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema Sekta ya Madini ni muhimu kwa uchumi wa nchi na kukiri kutambua kazi nzuri zinazofanywa na wachimbaji wa madini katika kukuza uchumi wa nchi.

“Baada ya ujenzi wa ukuta mapato yatokanayo na uchimbaji wa tanzanite yameongezeka mara nne” Waziri Mpango alikiri. Aidha, Waziri Mpango ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais John Magufuli kwa usimamizi madhubuti wa sekta ya madini na kuahidi kuendelea  kumwombea baraka za Mungu kwa mambo mazuri anayoifanyia nchi na wananchi wake.

 Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa namna anavyoisimamia sekta kwa kutoa maelekezo yanavyopelekea mafanikio mazuri yanayoonekana kwenye sekta. Pamoja na hayo Naibu Waziri Nyongo amempongeza mchimbaji Laizer kwa kupata jiwe lingine na kuwaahidi wachimbaji wadogo kuwa serikali yao itawapa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wananufaika na rasilimali madini zilizopo nchini. 

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na viongozi wa Wizara ya Madini katika hafla ya kupokea jiwe la Tanzanite toka kwa bilionea Saniniu Laizer

Zephania Chaula, Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro eneo linalochimba madini ya kipekee ya tanzanite duniani kote akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jiwe hilo alitoa wito kwa watanzania kufika wilayani humo ili kuwekeza katika sekta hiyo. 

Amesema madini yaliyopo wilayani humo yananufaisha nchi nzima na si Simanjiro pekee na kwamba tozo mbalimbali zinazotokana na madini yaliyopo wilayani humo yamechangia katika kuifanya nchi kuingia katika uchumi wa kati. 

 Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo amesema uwepo wa chombo cha ulinzi unawahakikishia uwepo wa ulinzi ulio imara na uimarishaji wa kipato cha taifa. Kama sehemu ya jamii chombo hicho kina kazi ya kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa kikamilifu. 

Jenerali Mabeyo amesema pamoja na kuwepo kwa ukuta bado kunauhitaji wa mifumo bora Zaidi ya kiusalama ili kuweza kudhibiti Zaidi utoroshwaji wa madini maana waswahili husema ‘hakuna ukuta usiokuwa na tundu’ na kuiomba vifaa hivyo vipatikane ili kuzidi kuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali. 

 Naye, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti ameupongeza uamuzi wa kujenga ukuta kuzunguka machimbo hayo uliofanywa na Rais Magufuli na kukiri uamuzi huo umeifanya serikali kukutanishwa na wachimbaji wadogo kwa ukaribu sana.  Umeifanya Serikali kuwa pamoja na wafanyabiashara, kuimarisha usalama kwa wananchi, wachimbaji wadogo pamoja na usalama kwa rasilimali zilizopo nchini.

Amewataka watanzania kuwa na imani na serikali yao. Kwa upande wake mchimbaji Laizer alisema yeye pamoja na wenzake wameridhishwa na bei inayoiuzia Serikali madini kutokana na uwazi katika uthaminishaji na kuelezwa thamani halisi ya madini wanayoyapata.

ReplyForward

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link