Biteko Awataka Wageni Kutokunyanyasa Wazawa Migodini

Na Tito Mselem, Geita

Baadhi ya mitambo ya uzalishaji maadini ya dhahabu katika mgodi wa Nyamahuna

Waziri wa Madini, Doto Biteko amemuagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita Daniel Mapunda kuhakikisha anaukagua kila wiki Mgodi wa Nyamahuna uliopo Wilaya ya Geita Mkoani humo ili kuwafanya Watanzania kushiriki katika uzalishaji wa madini ya dhahabu nchini.

Waziri Biteko alitoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kushitukiza katika mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania Andrew Bole kwa asilimia 95 na asilimia 5 ukimilikiwa na kampuni ya Eagle Brand ya nchini China.

Waziri Biteko alifanya maamuzi ya kutembelea mgodi huo baada ya kusikia malalako kuwa asilimia kubwa ya wanaoshiriki katika shughuli mgodini hapo kuwa ni wachina huku watanzania wakibaki kuwa vibarua.

Aliongeza kuwa nijambo lakusikitisha kuona mtanzania mwenye umiliki wa mgodi kwa asilimia 95 hashirikishwi chochote wala haruhusiwi hata kuingia sehemu za uchenjuaji wa dhahabu huku shughuli zote za uzalishaji zikifanywa na Wachina wenye umiliki wa asilimia tano pekee huku wakifanya kazi zote hata zile zinazoweza kufanywa na watanzania.

ÔÇťSheria ya Madini iliyolekebishwa mwaka 2017 inasema kwamba, kazi zozote zinazoweza kufanywa na Mtanzania, Mgeni hataweza kuzifanya, Mgeni ukimuona hapa maana yake anafanya kazi ambazo Mtanzania hataweza kuzifanya lakini lakushangaza nimeingia kukagua na kukuta kuna mashine yakawaida kabisa ambayo hata Mtanzania akifundishwa anaweza kufanya lakini anaeziendesha ni Mgeni,ÔÇŁ alisema Biteko.

Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) Akitoa onyo la mwisho kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Eagle Brand Tian su Long inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu baada ya kukataa kuwashirikisha watanzania katika shughuli za uzalishaji madini ya dhahabu (kulia) ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita Daniel Mapunda

Aliongeza kuwa lazima ukaguzi ufanyike mara kwa mara na kufuatilia  mashariti ya leseni tuliyompa mmiliki wa mgodi huu ikiwa ni pamoja na mashariti ya wageni katika kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji madini.

Pamoja na hayo, Waziri Biteko aliwataka Watanzania wanaofanya kazi katika mgodi huo kuheshimu sheria za kazi, kushirikiana na kuepuka majungu licha ya kuwalaumu wageni kutofuata sheria kuna mahali pengine baadhi ya watanzania wamekuwa wavivu, na kutofanya kazi kwa bidii, iwapo mtabadilika na kufanya kazi kwa bidii serikali itawalinda na kuwatetea.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Eagle Brand ambae ni raia wa China Tian su Long alisema kuwa mgodi huo unazalisha wastani wa kilo kumi za dhahabu kwa mwezi huku akieleza kuwa wamekuwa wakishirikiana na watanzania pamoja na kutoa mafunzo ya uchimbaji kwa baadhi ya watanzania.

Aidha, Tian su long amemuahidi Waziri Biteko atashirikiana na watanzania huku wakifuata taratibu, kanuni na sheria za nchi.

Wakati huo huo, mmiliki wa leseni ya mgodi huo Andrew Bole alikiri kutokushirikishwa kwa namna yeyote ile juu ya shughuli za mgodi huo na kubainisha kuwa ushirikishwaji umeanza mara baada ya serikali kuingilia ambapo kuna baadhi ya vitu vinavyofanyika katika mgodi huo bado anafichwa mpaka sasa.

akipokea maelekezo hayo,  Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda, alisema kuwa amepokea maagizo ya Waziri Biteko na atahakikisha anafanya ukaguzi kila wiki na kuwasilisha taarifa ofisini huku akiwaeleza wachina hao kuendelea kufuata sheria za nchi zinazosimamia masuala mazima ya uchimbaji wa madini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link