Biteko- Msitumie taaluma yenu vibaya

Issa Mtuwa – DSM

Wanajumuiya ya wana taaluma ya Jiolojia Tanzania (Tanzania Geological Society – TGS) wametahadharishwa na Waziri wa Madini Doto Biteko kuto tumia taaluma yao vibaya kutokana na umuhimu wa taaluma yao katika sekta ya madini. Amesema taaluma ya jiolojia ni mzizi wa sekta ya madini kwani shuguli nyingi za madini chanzo chake ni taarifa za kijiolojia na wao ndio waandaaji. ┬á

Biteko, ameyasema hayo tarehe 27/09/2019 wakati wa kufunga kongamano la wanataaluma ya jiolojia hapa nchini, lililokuwa linafanyika katika ukumbi wa Maktaba mpya ya chuo kikuu cha Dar es salaam kuanzia tarehe 25/09/2019 na kuwakutanisha wana taaluma hiyo kutoka kila kona ya nchi.

Waziri wa Madini Doto Biteko wa tatu kushoto mstari wa kwanza akifuatilia mada kuhusu marekebisho ya sheria ya madini 2017 kwenye kongamano la wataalam wa jiolojia nchini.

Kabla ya kufunga kongamano hilo Biteko alishiriki mjadala wa mada mbalimbali ikiwemo ya marekebisho ya sheria ya madini  ya 2017 ambayo inatajwa kuwa kiini cha mabadiliko katika sekta ya madini.

Amesema taaluma hiyo ni muhimu sana kwa sekta ya madini lakini  wapo baadhi ya wanataaluma wanaitumia vibaya kwa kujinufaisha binafsi. Aliongeza kuwa wapo wanaowadanganya  wawekezaji kwa kuwapa taarifa za zisizo sahihi, ile hali wakifahamu kuwa taarifa wanazozitoa hazina ukweli ili mradi tu anufaike.

ÔÇťWapo baadhi yenu, wasio waaminifu, wanatumia taaluma yao vibaya, ninazo taarifa za baadhi ya wanataaluma wanaotumia vibaya ili kujinufaisha.┬á Tumieni kongamano hili kukatazana mabaya na kuimizana mambo mazuri. Wapo baadhi ya majiolojia wanaofanya kazi katika kampuni binafsi wanaotumia data walizo nazo na kuzipeleka kwa wachimbaji wadogo na kupelekea kuwa chanzo cha migogoro pindi wachimbaji hao wanapovamia kwa nguvu eneo ambalo wameambiwa kuwa kuna madini .ÔÇŁ alisema Biteko.

Awali Biteko amewapongeza wanajumuia hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuisaidia sekta ya madini licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.

Akiwasilisha mada ya marekebisho ya sheria, mkurugenziwa wa huduma za sheria kutoka wizara ya madini Wakili Edwin Igenge, alisema kimsingi sheria ya mwaka 2010 haijabadilishwa kama wanavyo dhania baadhi ya watu isipo kuwa kilichofanyika mwaka 2017 ni marekebisho ambayo ndio yaliyopelekea kuanzishwa kwa Tume ya Madini na kuondoa mamlaka za leseni na udhibiti kutoka kwa Waziri wa Madini na kwenda kwa Tume ya Madini.

Waziri wa Madini Doto Biteko akihutubia kongamano la wana taaluma ya Jiolojia nchini katika ukumbi wa maktaba ya chuo kikuu cha Dar es salaam.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Tume ya Madini Prof. Shukuran Manya ambae pia ni mwanachama wa TGS, akijibu swali la mmoja wa washiriki hao kuhusu ushirikiano wa wazawa na wawekezaji kutoka nje katika uchimbaji wa madini, Prof. Manya alisema marekebisho ya sheria yametoa fursa kwa watanzania weye leseni ya uchimbaji kushirikiana na mwekezaji kutoka nje kwa kufuata masheriti yanayoongoza ushirikiano wao.

Kwa upande wake Rais wa jumuiya hiyo Prof. Abdulkarimu Mruma akiongea kabla ya kumkaribisha waziri wa madini kuongea na wana taaluma hao, alimweleza waziri mambo mengi kuhusu mipango ya jumuiya yao. Aidha, Prof. Mruma aliwasilisha maombi ya kiwanja mjini Dodoma cha kujenga jengo la TGS sambamba na kuanzishwa kwa Bodi ya jumuiya hiyo.

Mkutano huo hufanyika mara moja kila mwaka na kuwakutanisha wana taaluma hao. Kwa mwaka huu jumuiya hiyo inaadhimisha miaka 50 ya uwepo wake.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link