Biteko akutana na Mabalozi watatu ofisini kwake

Na Issa Mtuwa – DSM

Waziri wa Madini Doto Biteko leo tarehe 24/09/2019 amekutana na Mabalozi wa nchi mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti ofisini kwake jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo nao.

Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akiwa na Balozi wa Uingereza Sarah Cooke katikati mara baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Biteko Kulia ni Laura Blizzard mkuu wa idara ya Sera, uchumi na Biashara ubalozi wa Uingereza.

Wa kwanza kuwasili ofisini hapo alikuwa Balozi wa Kenya Dan Kazungu, Biteko na Kazungu wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano katika sekta ya Madini. Baadae alifuata Balozi wa Uingereza Sarah Cooke alie ambatana na Mkuu wa Idara ya Sera, Uchumi na Biashara Laura Blizzard kutoka ubalozi huo.

Mwisho alikuwa Balozi wa Angola Sandro De Oliveria ambae alikuja kujitambulisha kwa Waziri wa Madini na kuomba timu yake kutoka Angola ije Tanzania kuja kuzungumza pamoja na wataalam wa Tanzania kuhusu masuala ya mafuta sekta ambayo inasimamiwa na Wizara ya Nishati. Baada ya mazungumzo Waziri alimuunganisha moja kwa moja na Waziri mwenye dhamana ya Nishati.

Pamoja na mambo mengine Waziri amewaambia mabalozi hao kuwa Tanzania inahitaji sana wawekezaji katika sekta ya madini na kwamba wenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini waende moja kwa moja Wizarani na kuachana na propaganda za baadhi ya watu wasio itakia mema nchi yetu wanao sema sema Tanzania hakuna mazingira rafiki ya uwekezaji.

Ameongeza kuwa, yeye anapenda kuzungumzia mambo halisi (facts) na sio mambo ya kufikirisha (assumption). Amewaomba mabalozi hao kuwaambia watu wao wanaotaka kuja kuwekeza hapa nchini wafike moja kwa moja wizara ya madini na wasikubali kufikia kwenye mikono ya watu nje ya wizara ya madini ili kuepusha uongo na utapeli unaofanywa na watu wasio wema.

Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akiwa na Balozi wa Angola Sandro De Oliveria wakati wa mazungumzo yao ofisini kwa Biteko jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wao kwa nyakati tofauti tofauti wamemshukuru na kumpongeza waziri wa Madini kwa namna anavyo isimamia sekta ya madini ambayo imekuwa na mabadiliko makubwa sana. Balozi wa Kenya na Angola wamesema wanahitaji nchi zao kujifunza Tanzania namna maboresho ya sheria ilivyopelekea mabadiliko makubwa katika sekta ya Madini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal