Archives for Press Release

Taarifa kwa Umma-Uundwaji wa Tume ya Madini kwa Mujibu wa Sheria Na. 7 ya Mwaka 2017

Tume ya Madini iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha 21 cha Sheria ya Marekebisho Anuwai ya Sheria ya Madini Na. 7 ya Mwaka 2017. Mnamo tarehe 17 Aprili, 2018, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, kulingana na Sheria tajwa, aliteua Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Madini. Ili kutekeleza majukumu yake, Tume ilifanya kikao chake cha kwanza tarehe 30 Aprili, 2018 Jijini Dodoma. Pamoja na mambo mengine, Tume iliazimia mambo  yafuatayo:

i) Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini zitakuwa Jijini Dodoma katika Ofisi za Wizara ya Madini;

ii) Kuimarisha usimamizi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya Mwaka 2017 kwa lengo la kuhakikisha kuwa Serikali inamiliki hisa zisizopungua asilimia 16 ya mtaji wa Kampuni zinazomiliki migodi ya kati (MLs) na mikubwa (SMLs), Wazawa wanashirikishwa ipasavyo katika Miradi ya Madini na kunufaisha jamii katika maeneo ya migodi na Taifa kwa ujumla;

iii) Kuwajulisha wamiliki wote wa leseni zote za kuhodhi maeneo (Retention Licences – Jedwali Na. 1) kuwa leseni zao zimefutwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ikisomwa pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2017 na Kanuni ya 21 ya Kanuni za Madini (Haki Madini), 2018 Tangazo la Serikali Na.1/2018 na kwamba maeneo ya leseni hizo yamerudishwa Serikalini bila hakikisho la kupewa tena;

>>Soma Zaidi>>

Read more

Prof. Kikula ateuliwa Mwenyekiti Tume ya Madini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kupitia taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu tarehe 18 Aprili, 2018, ilieleza kuwa, uteuzi wa Prof. Kikula umeanza tarehe 17 Aprili, 2018. Pia, taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais Magufuli pia, amewateua Makamishna wa Tume hiyo ya Madini.

Tume ya Madini ilianzishwa kufuatia kupitishwa kwa Sheria Mpya ijulikanayo kama The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2017 ambayo ilianza kutumika tangu tarehe 7 Julai, 2017. Aidha, Tume ya Madini imeanzishwa baada ya kufanyika Marekebisho makubwa yaliyofanyika katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010.

Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kama ilivyorekebishwa kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 7 ya Mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2017, baadhi ya majukumu ya Tume ya Madini ni kama ifuatavyo;

  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Madini.
  • Kutoa Leseni za Madini.
  • Kufanya Ukaguzi wa Migodi ili kukidhi Matakwa ya Kiusalama.
  • Kutoa Vibali vya Kusafirisha Madini Ndani na Nje ya Nchi.
  • Kusimamia uchimbaji wa Madini na Sekta nzima ya Madini nchini.
  • Utatuzi wa Migogoro inayohusu Madini.

Read more

Taarifa kwa Umma-Matokeo ya mnada wa 3 wa mauzo ya almasi za mgodi wa Williamson Diamonds Limited

Wizara ya Madini inapenda kuutarifu umma kuwa, tarehe 2 hadi 9 Februari, 2018, Mnada wa Tatu (3) wa mauzo ya almasi kutoka Mgodi wa Mwadui unaomilikiwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited ulifanyika mjini Antwerp, nchini Ubelgiji.

Katika mnada huo, jumla ya Karati 54,094.47 ziliuzwa kwa thamani ya Dola za Marekani 13,607,858.72 sawa na shilingi 30.6 Bilioni ambapo jumla ya kampuni 145 zilishiriki katika mnada na kuwasilisha zabuni zao za ununuzi na zabuni 1,019 ziliwasilishwa katika mnada huo.

Kufuatia mauzo ya almasi hizo, Serikali imepata Mrabaha wa (Final Royalty) Dola la Marekani 816,471.52 pamoja na Ada ya ukaguzi (Clearance and Inspection) kiasi cha Dola za Marekani 136,078.59 sawa na shilingi za Kitanzania 2,090,164,095.

Aidha, Mrabaha wa awali (Provisional Royalty) uliolipwa kutokana na uthaminishaji wa awali kabla ya mauzo ni Dola za Marekani 674,941.78, ada ya Clearance na Inspection Dola za Marekani 112,490.30 pamoja na Dola za Marekani 100 kwa ajili ya kibali cha kusafirishia almasi ambapo jumla yake ni Dola za Marekani 787,532.08 sawa na shilingi 1,771,947,000.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Taarifa kwa Umma-Mabadiliko katika sekta ya madini yanayotokana na marekebisho ya sheria ya madini mwaka 2010

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuutarifu umma kuwa, kufuatia kupitishwa kwa Sheria Mpya ijulikanayo kama The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2017 iliyoanza kutumika tarehe 7/7/2017, kumefanyika Marekebisho kadhaa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

Marekebisho makubwa yaliyofanyika katika Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ni pamoja na;

  • Kuanzishwa kwa Tume ya Madini (Mining Commission);
  • Kufutwa kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini (Tanzania Mineral Audit Agency- TMAA);
  • Kuongezeka kwa malipo ya Mrabaha kutoka asilimi 4 (4%) kwa madini ya Metali (mfano dhahabu, shaba, fedha n.k) hadi asilimia 6 (6%);
  • Kuongezeka kwa malipo ya Mrabaha kutoka asilimia 5 (5%) kwa madini ya almasi na vito (mfano Tanzanite, Ruby, Garnets n.k) hadi asilimia 6 (6%).

Aidha, kupitia Marekebisho ya Sheria ya Fedha na Sheria ya Kodi, hivi sasa kila Mtu au Kampuni anayetaka kusafirisha madini nje yatakaguliwa na kuthaminishwa na atalipa ada ya ukaguzi (clearing fees) ambayo ni asilimia 1 (1%) ya thamani ya madini anayosafirisha.

>>Soma Zaidi>>

Read more