Archives for Public Notes

Jarida la Nchi Yetu: Tolea Maalum la Wizara ya Madini, Mei 2019

Uongozi wa Wizara ya Madini unampongeza kwa dhati Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali anayoiongoza, ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ameimarisha na kusisitizia usimamizi wa rasilimali za Taifa hususani madini ili kunufaisha Taifa kwa ujumla.

Katika kipindi cha uongozi wake, Wizara imefanikiwa kufanya marekebisho ya Sheria ya Madini, Miongozo na Kanuni za Sekta ya Madini ili kuhakikisha rasilimali hii inawanufaisha Watanzania na kuongeza mapato ya Serikali na kuongeza ukusanyaji wa maduhuli na hii imeonesha wazi nia ya Wizara ya Madini kutekeleza kwa vitendo maono ya Mhe. Rais kuwa “Rasilimali ya Madini Iwanufaishe Watanzania.”

Tunawiwa kwa namna ulivyosaidia sisi kufika hapa. Hatuna cha kukulipa isipokuwa kukuahidi kazi zaidi na uadilifu zaidi. Na kwa sababu hiyo basi, tunalitoa toleo hili maalum kuwa ni shukrani kwako na tunakuombea afya njema na nguvu zaidi katika kuendelea kuliongoza Taifa letu.

>>Soma Zaidi>>

Read more

Maelezo ya Waziri wa Madini, Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki (Mb.) kuhusu katazo la usafirishaji wa carbon yenye dhahabu kutoka Mkoa mmoja kwenda mwingine aliyoyatoa Bungeni tarehe 14 Juni, 2018

Mheshimiwa Spika, tarehe 4 Juni 2018, Mheshimiwa John Heche (Mb.) aliomba mwongozo wako kuhusu katazo la usafirishaji wa Activated carbon kutoka Mkoa mmoja kwenda Mkoa Mwingine ambapo kufuatia mwongozo huo, Mheshimiwa Spika ulielekeza tutoe maelezo Bungeni kuhusu katazo hilo.

Mheshimiwa Spika, tarehe 1 Juni 2018 wakati nikifanya majumuisho ya hotuba ya bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 nilitangaza katazo la usafirishaji wa Activated carbon zinazotoka katika mitambo ya kuchenjulia dhahabu kutoka nje ya Mkoa ambao una mtambo wa uchenjuaji kupelekwa katika Elusion plant iliyo kwenye Mkoa mwingine ili kufanya uchenjuaji. Hii pia ilitokana na michango mbalimbali ya waheshimiwa wabunge wakati wakijadili hotuba ya bajeti ya Wizara yangu. Katazo hili pamoja na mambo mengine linalenga kudhibiti masuala mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika kinyume cha Sheria na Kanuni kama vile ukwepaji wa kulipa kodi za Serikali, ukwepaji wa kulipa mrabaha kwa Serikali, ukwepaji wa kulipa ushuru wa huduma kwa Halmashauri husika, utoroshaji madini, na matukio ya wizi wa madini wa mara kwa mara unaofanywa na wachimbaji wasio waaminifu kwa kutorosha Carbon na kuzipeleka nchi jirani ambako kumejengwa Elusion plants. Aidha, mabadiliko ya teknolojia hasusan urahisi wa upatikanaji wa teknolojia ya uchenjuaji wa madini yanathibitisha wazi kuwa teknolojia hiyo inaweza kuwekwa kila Mkoa ambako kuna mahitaji ya uchenjuaji.

Mheshimiwa Spika, kufuatia mabadiliko ya teknolojia ya uchenjuaji katika miaka ya 2000, idadi kubwa ya wachimbaji na wachenjuaji wadogo nchini wamekuwa wakitumia Kemikali ya Sayanaidi kwa ajili ya kuchenjua Madini ya dhahabu. Teknolojia hii inahusisha kutumia matenki ya kuozeshea (VAT leaching) na Activated carbon ambazo hufyonza dhahabu kutoka katika udongo uliowekwa katika matenki na kuchanganywa na Kemikali ya Sayanaidi. Dhahabu iliyofyonzwa kwenye Activated carbon huchenjuliwa katika mitambo ya uchenjuaji (Elution plants). Idadi kubwa ya mitambo hii (Elution Plants) imejengwa katika Mikoa ya Mwanza, Geita, Dodoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Songwe, na Singida na hivyo kupelekea wachenjuaji wengi wa dhahabu kusafiri kwenda kwenye Mikoa hiyo kufuata huduma hiyo. Kabla ya katazo hili, ofisi za madini kwenye maeneo husika zimekuwa zikitoa vibali vya usafirishaji wa Carbon zenye dhahabu kutoka eneo moja hadi jingine.

Mheshimiwa Spika, kati ya malengo ya Sera ya Madini ya Mwaka 2009 ni kuimarisha mfumo wa Sheria na udhibiti katika sekta ya madini ili kuhakikisha kuwa Serikali inanufaika na mapato yanayotokana na sekta ya madini. Matukio mengi ya wizi wa Carbon na mengine ya ukiukwaji wa Sheria na kanuni yameripotiwa katika siku za hivi karibuni na Serikali haiwezi kukaa kimya wakati matukio haya yanayoikosesha Serikali mapato yakiendelea.

>>Soma Zaidi>>

Read more
Şanlıurfa araç kiralama Şanlıurfa evden eve nakliyat