Dhahabu Bandia Zakamatwa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga

  • Ni Baada ya Kuanzishwa Operesheni Maalum
  •  Waziri Biteko amwagiza Katibu Mkuu kuwasimamisha Kazi Maafisa Madini waliosaidia kutorosha Madini
  • Ataja mbinu zinatumika kutorosha madini

Na Asteria Muhozya, Mwanza

Madini Feki ya Dhahabu yamekamatwa katika Mikoa ya Shinyanga na Mwanza, huku kilo 4.58 zikikamatwa Mkoa wa  Shinyanga na kilo 6.255 Mkoa wa  Mwanza.

 Akizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara wa Madini na Waandishi Jijini Mwanza Agosti 8, 2019, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema, matokeo ya kukamatwa dhahabu hizo feki   yanatokana na  Operesheni Maalum ambapo  wizara  iliamua  kufuatilia mfumo mzima wa biashara ya madini ya dhahabu  kwa kuunda  Vikosi kazi  mbalimbali katika maeneo  kadhaa ili kubaini  na kudhibiti mianya ya udanganyifu na utoroshaji  wa madini.

Waziri Biteko ameongeza kuwa, baada ya vikosi kazi kuanza majukumu yake, katika vituo vingi  kumekuwa na ongezeko la dhahabu inayouzwa hususan inayozalishwa  kwa kutumia Zebaki.

Akitoa takwimu za mauzo  ya madini ya dhahabu  yaliyochenjuliwa  kwa Zebaki  na kuuzwa katika  Soko la Madini  Geita kuanzia  tarehe  17 Machi,2019 hadi   Agosti 3, 2019, amesema ni gramu 129,115.58 ambapo kati ya hizo, gramu  102,065.58 zimeuzwa kwa kipindi  cha Siku 14 kuanzia  tarehe 20 Julai, 2019 hadi tarehe 3 Agosti,2019 baada ya Operesheni maalum kuanza.

“ Ndugu wana habari, hii ina maana  katika kipindi cha  miezi 4 ni kilo 27  tu zilizouzwa  sokoni ukilinganisha  na kilo 102 zilizouzwa kwa siku 14 baada ya  kikosi kazi kuanza majukumu yake,” amesisitiza Waziri Biteko.

Akitoa takwimu za Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga amesema  kabla ya kuanza  kwa operesheni  kuanzia tarehe 17 Juni, 2019 hadi 30 Juni,2019,  kiasi cha Tsh. 2,559,157,275.19 kilikusanywa  huku ndani ya kipindi cha majuma mawili baada ya operesheni  kuanzia tarehe  17 Julai, 2019 hadi  tarehe 31 Julai kiasi cha Tsh  2,817,602,551.14  kilikusanywa sawa na  ongezeko la Tsh. 258,445,275.95.

Ameongeza kuwa, kwa upande wa leseni  za biashara  kwenye soko la madini  Kahama kulikuwa na  dealers  watano tu  na baada ya operesheni idadi hiyo imeongezeka na kufikia  13, huku maombi ya biashara za madini yakiongezeka  kutoka  31 hadi 48.Sehemu ya Wafanyabiashara wa Madini waliohdhuria mkutano kati yao na Waziri wa Madini.

 “ Wastani wa dhahabu iliyochenjuliwa kwa zebaki na kuuzwa kwenye kituo cha Kakola imefikia  kilo moja  hadi  kilo moja na nusu 1,500 kwa siku. Hii   maana yake ni kuwa kwa mwezi inatakiwa  kuuzwa dhahabu  kati ya  kilo  30 hadi kilo 45. Lakini kabla ya operesheni, kituo hiki hakikuwa na  na taarifa zozote  za mauzo ya dhdhabu na hii inaonesha kulikuwepo na utoroshaji  mkubwa wa madini,”. Amesema Biteko.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Biteko amesema wapo Maafisa Madini wasio waaminifu ambao wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara  katika kutorosha madini hayo nje ya nchi na hivyo kumwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila kuwasimamisha kazi haraka huku akitaka  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  kulifanyia kazi suala hilo.

 “Wale Maafisa ambao wanajua hawawezi kabisa kufanya kazi zenu kwa uaminifu, ni bora waje waniambie niende utumishi niwaombee wapangwe wizara nyingine. Jueni kwamba mmepewa dhamana ya kufanya  kazi ambayo mnayo dhamana ya kulinda madini haya,” amesema Waziri Biteko.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko  amesema pamoja na serikali kuweka mfumo mzuri wa biashara ya madini   nchini kwa wachimbaji na wafanyabiashara, lakini bado  baadhi yao wameendelea kufanya biashara nje ya masoko  kinyume cha  utaratibu na hivyo kuendelea  kutorosha madini huku wakitumia mbinu chafu.


Wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakikata Seal ili kufungua Madini fake yaliyokamatwa.

 Amezitaja mbinu hizo kuwa ni pamoja na kuhifadhi dhahabu kwenye  kwenye soksi wanazokuwa wamevaa  na kuwarahisishia wao  kupita mipakani  bila ya mtu yoyote kujua,  kutumia wenyeji wan chi husika  ili kuvuka mipaka na  kumsaidia kutorosha  dhahabu hiyo, kutumia gari kuficha mizigo kwa  kwa kuweka kwenye  spare tyre, juu ya bonet  huku baadhi ya magari yakiwa yametengenezewa seheu maalum na pindi  wanapofika mipakani  wapo wadau wao  kwa kushirikiana na  watumishi wa serikali  waliopo mipakani  huvusha dhahabu.

Mbinu nyingine ni pamoja na kupitia boti ziendazo nchi za jirani kwa  kuhifadhi  kwenye vitu kama vibakuli na kuweka dhahabu hiyo ambayo  huwekewa vitafunwa  vya aina mbalimbali.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Biteko amewataka watumishi na wafanyabiashara wasiowaaminifu kufuata taratibu zinazotakiwa huku akieleza kuwa, tayari wizara inayo orodha ya wanaotorosha dhahabu hiyo kila wiki, ikiwemo jina la kampuni ya ndege inayosafirisha dhahabu hiyo na nchi zinakopelekwa

Aidha, amechukua fursa hiyo kuvipongeza vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanahi wanaosaidia kutoa taarifa za utoroshaji wa madini hayo.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal