Dola milioni 100 zimelipwa Serikalini na Kampuni ya Uchimbaji Barrick

Na Tito Mselem Dodoma,

Kampuni ya Barrick  imelipa hundi ya Dola za Kimarekani milioni 100 kwa Serikali ya Tanzania kama malipo ya patano kuhusu fidia ya kodi.

Mbele katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Ph i lip Mpango, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi na mbele kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya hundi dola milioni 100 kwa Serikali

Malipo hayo yamefanyika leo 26 Mei, 2020 katika ukumbi wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha jijini Dodoma ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alikabidhiwa hundi hiyo kwa niaba ya Serikali.

Hundi hiyo ya dola za Kimarekani million 100 iliyotolewa ni sehemu ya malipo ya awali ya kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 300 iliyokubaliwa kulipwa kwa Serikali ya Tanzania kama fidia ya Kodi.

Katika hafla ya makabidhiano ya hundi hiyo, viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kirangi, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Gavana wa Benk Kuu, Prof. Florence Luoga, katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na wengine wengi.

Akipokea hundi hiyo Dkt. Mpango amesema tukio hilo ni mwanzo wa safari muhimu  katika utekelezaji wa makubaliano ya mkataba wa msingi baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick yaliyofikiwa tarehe 19, Desemba, 2019 na kusainiwa tarehe 24 Januari 2020 jijini Dar es Salaam.

ÔÇťMakubaliano yaliitaka Kampuni ya Barrick kulipa dola milioni 300 za Kimarekani kwa Serikali ya Tanzania ambapo leo Kampuni hiyo imelipa Dola 100 sawa na bilioni 250 za kitanzania na kubakiza Dola 200 sawa na bilioni 500 za Kitanzania.ÔÇŁ alisema Dkt. Mpango.

Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick zimekubaliana kwamba pande hizi mbili zitashirikiana katika msingi wa mambo yote yanayohusu faida za kiuchumi zinazotokana na madini ya Tanzania katika msingi wa 50 kwa 50 kwa kuzingatia mipango ya uwepo wa madini yanayoendana na kanuni ya usawa wa kiuchumi kama ilinavyoeleza sheria.

Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na kulia ni katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya hundi dola milioni 100 kwa Serikali

Aidha, Dkt mpango, ameishukuru Kampuni ya Barrick kwa kuonesha dhamira ya dhati ya ushirikiano mzuri kwenye muelekeo mpya wa Sekta ya Madini Tanzania ambao umekubalika na pande zote kwa manufaa ya pande zote.

Wakati huo huo, Dkt Mpango ametoa wito kwa makampuni mengine ya madini nchini kufuata mfano mzuri uliooneshwa na kampuni ya Barrick katika huhakikisha kunakuwa na hali ya usawa katika uendeshaji wa shughuli za madini.

Kwa upande wake  Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Dkt. Dennis Mark Brstow ambaye alihudhurilia hafla hiyo kwa njia ya video (Video Conference) ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi wanazozionesha katika kuendeleza Sekta ya Madini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link