Mheshimiwa Spika;

Awali ya yote, napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, aliyetujalia uhai na kutuwezesha kuiona siku ya leo. Kama, Mheshimiwa Spika unavyofahamu, wapo wenzetu ambao tulikuwa nao wakati wa kuzindua Bunge hili, lakini leo hatuko nao. Wametangulia mbele za haki. Hivyo basi, kwa heshima yao naomba tusimame kwa dakika moja kuwakumbuka. Mwenyezi Mungu azipumzishe roho zao mahali pema peponi. Amina.

Mheshimiwa Spika, kabla sijaendelea zaidi, naomba kutambua uwepo wa viongozi mbalimbali kwenye Ukumbi huu. Nimefurahi kuwaona Waheshimiwa Marais wetu Wastaafu wote wapo hapa, pamoja na Makamu wa Rais Wastaafu na pia Mawaziri Wakuu wastaafu, akiwemo Mheshimiwa Lowasa na Mheshimiwa Sumaye. Hii ndiyo Tanzania.

Kwa namna ya pekee, napenda nikushukuru wewe, Mheshimiwa Spika, Job Ndugai, Mbunge wa Kongwa, kwa kunipa kibali cha kuja kulihutubia Bunge hili. Aidha, nawashukuru Naibu Spika, Mheshimiwa Tulia Ackson, pamoja na Wenyeviti wa Bunge, Mheshimiwa Andrew Chenge na Mheshimiwa Najma Giga, kwa ushirikiano wenu. Ahsanteni sana. Hiki ni kielelezo cha uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya mihimili yetu mitatu katika kipindi chote cha miaka mitano iliyopita. 

Nitumie fursa hii pia kueleza kuwa, tangu nimeingia ndani ya Bunge hili leo nimeshuhudia mabadiliko mengi makubwa, tofauti na ilivyokuwa wakati mimi nikiwa Mbunge.  Hivi sasa nimeona hata Waheshimiwa Wabunge wanatumia vifaa vya kisasa kama vile tablets. Enzi zetu, vifaa hivyo, havikuwepo. Hivyo basi, nakupongeza sana Mheshimiwa Spika kwa ubunifu huu; na nawapongeza pia Waheshimiwa Wabunge kwa kuweza kuvitumia vifaa hivi; na hivyo kulifanya Bunge lenu kuwa la kisasa namna hii.

>>Soma Zaidi>>