Hotuba ya Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko (MB.),Waziri wa Madini Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2020/2021.

A. UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba kutokana na taarifa iliyowasilishwa katika Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo imechambua bajeti ya Wizara ya Madini, Bunge lako sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu kwa Mwaka wa 2019/2020 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Madini pamoja na Taasisi zake kwa Mwaka 2020/2021.
  2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha
    kwa mara nyingine kuwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 mbele ya Bunge lako Tukufu.
  3. Mheshimiwa Spika, kipekee napenda nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini kusimamia Sekta ya Madini. Napenda kutoa pongezi kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wake makini na thabiti. Mafanikio hayo yanajidhihirisha katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa ya maendeleo ikiwamo Mradi wa Ufuaji Umeme wa Bonde la Mto Rufiji (Julius Nyerere Hydro power project), ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge Railway), ununuzi wa ndege mpya kufufua Shirika la Ndege Tanzania na miradi mingine kadhaa.
  4. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo ya Kitaifa, nimshukuru tena Mheshimiwa Rais, kwa hatua madhubuti alizochukua yeye binafsi katika kuzilinda rasilimali madini na kuhakikisha kuwa zinawanufaisha wananchi hasa wanyonge na kulinda maslahi ya Taifa. Watanzania watakuwa ni mashahidi wa mafanikio hayo kama ifuatavyo: (i)Uanzishwaji wa Kampuni ya Twiga Minerals Corporation Limited
  5. Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais, Serikali ya Tanzania imeingia ubia na Kampuni ya Barrick Gold Corporation na kuanzisha Kampuni ya Twiga Minerals Corparation Limited. Uwekezaji huu unaipa Serikali umiliki wa hisa asilimia 16 na Kampuni ya Barrick Gold Corporation umiliki wa hisa asimilia 84. Katika makubaliano hayo imekubaliwa pia kwamba kutakuwa na mgawanyo wa manufaa ya kiuchumi ya 50:50 hii ikiwa na maana ya kwamba faida na mapato mengine nje ya uendeshaji kuondolewa itatakiwa kuwekezwa nchini kiasi kisichopungua asilimia 50. Hatua hii itasaidia kulinda maslahi mapana ya nchi na kuongeza udhibiti katika shughuli za uzalishaji madini. Kipekee kabisa nikiri, uthubutu wa namna hii uliwahi kufanyika wakati wa Uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Serikali ilipokuwa na ubia na Kampuni ya Williamson Diamond Limited (WDL). Hakika uongozi wake ni Tunu kwa Taifa. (ii) Uanzishaji na Usimamizi wa Masokonchini.
  6. Mheshimiwa Spika, nashawishika kusema maono ya Mheshimiwa Rais ni baraka kwa Watanzania, kwa dhamira yake tumeweza kuanzisha masoko na vituo vya ununuzi wa madini katika maeneo mbalimbali yenye shughuli za uchimbaji madini nchini. Nikiri kuwa, Masoko haya yamesaidia kutatua changamoto za muda mrefu ambazo zilikuwa zikiikabili Sekta ya Madini hususan wachimbaji wadogo kukosa masoko ya uhakika na bei stahiki ambapo katika kipindi cha kuanzia Machi 2019 hadi Februari 2020 kupitia masoko wachimbaji wadogo wamefanya biashara ya madini yenye thamani ya shilingi 1,088,693,000,153.19 na wameiingizia Serikali mapato kwa kulipa mrabaha na ada ya ukaguzi wa shilingi 78,008,413,233.13. Masoko haya yameleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa Sekta hii kwa kipindi cha Januari hadi Septemba iliongezeka kutoka asilimia 0.9 mwaka 2018 hadi asilimia 12.6 mwaka 2019 kwa kipindi kama hicho. Masoko hayo yameleta manufaa mengine kwa wananchi ikiwemo kuzalisha fursa za ajira na kuongezeka kwa kipato cha wachimbaji wadogo tofauti na hapo awali. Namuomba Mungu azidi kumjalia maono zaidi na zaidi ili Watanzania wazidi kuneemeka. (iii) Uanzishwaji wa Eneo Tengefu la Mirerani.
  7. Mheshimiwa Spika, katika namna isiyokuwa rahisi kuaminika katika macho ya wengi, pale neno la Mungu lilipomjia Mheshimiwa Rais hakutaka kukimbia wito kama ÔÇŁYona mwana wa Amitai, kwenda NinawiÔÇŁ, amekamilisha ujenzi wa Ukuta kuzunguka machimbo ya madini eneo la Mirerani na kuweka vifaa vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa madini ya Tanzanite ambayo ni rasilimali ipatikanayo Tanzania pekee inalindwa. Kufuatia uwekezaji huo, sote tumeshuhudia kuongezeka mara dufu kwa mapato yatokanayo na madini ya Tanzaite katika eneo hilo hususan kutoka kwa wachimbaji wadogo kutoka shilingi 166,094,043 kabla ya kujenga ukuta hadi shilingi 2,150,000,000 baada ya kujengwa kwa ukuta. Kipekee namuomba Mungu azidi kusema nae. (iv)Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Nchini.
  8. Mheshimiwa Spika, kwa azma ileile yakutetea haki za wanyonge, Mheshimiwa Rais alifuta Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio kwa wachimbaji wadogo hii ikiwa ni huruma yake kwa wachimbaji wadogo na mkakati wake wa kuhamasisha uendelezaji wa uchimbaji mdogo nchini. Nitoe rai kwa wachimbaji wadogo kuunga mkono juhudi za Uongozi Shupavu wa Awamu ya Tano kwa kuhakikisha wanatumia fursa hiyo ili kujinufaisha na rasilimali madini ambazo nchi yetu imejaliwa.

>Soma Zaidi>>

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link