Prof. Msanjila Afungua Fursa kwa Kampuni ya AGA Bullion Kuwekeza Kwenye Sekta ya Madini.

Na. Steven Nyamiti-Dodoma

Katibu  Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila leo Novemba 12, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na kampuni ya AGA Bullion kutoka Nchini Uturuki  ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma ambayo imeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya madini Nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo alipokutana na Mkurugenzi Mwamzilishi wa Kampuni ya AGA Bullion iliyofanyika Novemba 12, 2020 Mtumba Jijini Dodoma

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma, Katibu Mkuu Msanjila ameieleza kampuni hiyo uwepo wa Masoko ya Madini yaliyoanzishwa kila mkoa nchini hususan ile yenye uzalishaji mkubwa wa madini ikiwa ni pamoja na mkoa wa Geita, Mwanza, Kahama, Chunya, Arusha na kwingineko ambako AGA Bullion wataweza kuwekea, kununua na kuuza dhahabu kwenye masoko ya nje.

Prof. Msanjila ameitaka kampuni ya AGA Bullion kuwafikia wachimbaji wadogo na wa kati kwa kuwapa uzoefu wa uwekezaji katika sekta ya madini na kupendekeza kutembelea Mgodi wa dhahabu wa Geita na Busolwa, ambao ni mgodi wa kati unaofanya uwekeaji katika uchimbaji wa madini ya dhahabu vizuri nchini.

Ameishauri Uwekezaji unaopangwa kufanywa na kampuni ya AGA Bullion usilenge kwenye biashara ya madini ya dhahabu pekee bali kwenye madini mengine yanayopatikana nchini yakiwemo madini ya Tanzanite yanayopatikana mkoani Manyara, pia kuomba leseni ya uchimbaji ili waweze kuchimba madini nchini.

Prof. Msanjila ameitaka Kampuni ya AGA Bullion kukutana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wakiwemo Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao hutoa huduma na ushauri wa kitaalam kwa wachimbaji wadogo, uchenjuaji dhahabu, kununua na kuuza kutokana na uwepo wa Refinery mkoani Mwanza itakayoanza shughuli mwezi Disemba, 2020. Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kupata taarifa za kitafiti ndani ya nchi, ramani za kijiolojia zinazoonyesha sehemu zenye madini na Tume ya Madini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mwanzilishi wa AGA Bullion, Sarp Tarhanaci amemweleza Prof. Msanjila kuwa Kampuni ya AGA Billion inamiliki viwanda viwili vya usafirishaji wa dhahabu (Refineries) katika nchi za Umoja wa Falme za kiarabu (Dubai) na Uturuki, wanauzoefu katika ununuzi wa dhahabu kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile Ghana, Burkina Faso, Peru, Malaysia na Uturuki.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa kampuni ya AGA Bullion (katikati) akizungumza jambo alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mtumba Jijini Dodoma Novemba 12, 2020

Akizungumza juu ya maelekezo ya kukutana na wadau wengine wa Sekta ya Madini,Tarhanaci amesema tayari kampuni hiyo tarehe 10/11/2020 ilikutana na kufanya mazungumzo na Tanzania Chambers of Mines (TCME), (Chama cha Wachimbaji Wakubwa wa Madini) ambapo imepokea taarifa za uzalishaji na mauzo ya dhahabu, Tarehe 11/11/1010 ilikutana na Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha  wa Benki Kuu ya Tanzania ili kueleza nia yake ya kutaka kutoa huduma ya usafirishaji wa dhahabu, bima na kutafuta masoko ya kimataifa ya dhahabu iliyosafirishwa kwa gharama ya 0.5% hadi 0.8% ya thamani ya madini hayo.

Aidha amesema, kampuni ya AGA Bullion kwa kiasi inayo dhamira ya kufanya biashara ya madini ya dhahabu kutoka wa wachimbaji wadogo, wachimbaji wa kati ikiwemo kuwawezeha kwa kuwapa mitaji ya fedha ili waweze kuzalisha zaidi na kutoa mafunzo kwa wachimbaji, kukutana na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) ili waweze kujadili mambo mbalimbali kwa pamoja.

Aidha amezungumza nia ya kampuni hiyo kusaidia kiwanda vya uongezaji thamani madini ya dhahabu (jewellery industry) kwa kutetengeneza bidhaa zake kama vile pete, hereni na mikufu.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na kamishina wa Madini Muhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi na wadau kutoka AGA Bullion kwa pamoja wamehaidi kuwekeza katika biashara ya madini hususan dhahabu  nchini.

Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Madini waliohudhuria kikao cha Katibu Mkuu Prof. Simon Msanjila na Kampuni ya AGA Bullion iliyofanyika Novemba 12,2020 Mtumba Jijini Dodoma. (Katikati) ni Kamishina wa Madini Muhandisi David Mulabwa na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link