Kiwanda kingine cha uchenjuaji dhahabu chazinduliwa Itumbi, Chunya 

Nuru Mwasampeta na Steven Nyamiti – Itumbi, Chunya

Imeelezwa kwamba, katika kuboresha mazingira na shughuli za wachimbaji wadogo wa madini nchini, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni 4.7 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitatu (3) vya uchenjuaji wa madini ya dhahabu ili kuwasaidia wachimbaji hao kupata mafunzo kwa vitendo katika hatua mbalimbali za upatikanaji wa dhahabu.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Ollal akielezea hatua za ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Itumbi Chunya mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kabla ya kukata utepe na kufanya ukaguzi katika kiwanda hicho iliyofanyika 21 Oktoba, 2020


Mafunzo hayo yatakayokuwa yakitolewa kwa wachimbaji wadogo ni pamoja na elimu ya utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu ili kuwawezesha kufanya uchimbaji wenye tija  na kusaidia kuinua vipato vyao na kuongeza mchango wa sekta kwenye pato la taifa.

Hayo yameelezwa tarehe 21 Oktoba, 2020 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakati wa makabidhiano na uzinduzi wa kiwanda hicho kilichogharimu takribani shilingi bilioni 1.7 mpaka kukamilika kwake.
 
Naibu Waziri Nyongo alitumia fursa hiyo kuishukuru kampuni ya Tan Discovery Mineral Consultancy kwa kukamilisha ujenzi wa viwanda hivyo na kuvikabidhi vikiwa katika ubora kwa mujibu wa makubaliano.
 
Aidha, Nyongo alibainisha kuwa, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lilipewa jukumu la kuhakikisha linasimamia na kuhakikisha ujenzi wa viwanda hivyo vitatu unakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.
 
Ameendelea kusema kuwa, kwa sasa Stamico limeonesha kuwa ni shirika linalojiendesha kwa faida baada ya kuanza kutoa gawio kwa serikali kwa kiasi kisichopungua shilingi bilioni 1 mwaka 2019 na bilioni 1.1 mwaka huu 2020.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Nyongo ameitaka Stamico kuthamini gharama kubwa iliyotumika katika ujenzi wa miradi hii na kuweza kuisimamia ipasavyo ili kuleta matokeo chanya hususani katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kuzalisha kwa tija kwa kutumia vifaa vyenye teknolojia rahisi na bora walivyowekewa na serikali yao.

Aliendelee kuisisitiza Stamico kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa wakazi wa maeneo jirani na kilipo kituo ili waweze kunufaika na matunda ya kuwepo kwa mradi huu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo akitoa salamu za shukrani kwa serikali kwa ujenzi wa viwanda vya kuchenjua dhahabu kwa lengo la kusaidia wachimbaji wadogo, iliyofanyika Oktoba 21, Itumbi Chunya

Naibu waziri, Nyongo ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa Itumbi na maeneo jirani kukitumia kituo hicho kujifunza na kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na shughuli za utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji pamoja na biashara ya madini kwani kituo kimejengwa kwa ajili yao. 
 

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link