Mabadiliko ya Sheria ya Madini Yameongeza Wigo wa Fursa kwa Wazawa

Tito Mselem na Steven Nyamiti, Geita

Imeelezwa kuwa, Mabadiliko  yaliyofanywa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 yameongeza wigo  wa fursa kwa Wazawa kutokana na nafasi za kushiriki katika Uchumi wa Madini.

Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi wa Ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini Terrence Ngole alipokuwa akiwakilisha mada katika semina iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya viwanja vya Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.

Baadhi ya washiriki katika mkutano wa ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini uliyofanyika Septemba 22, 2020 mkoani Geita

Mkutano huo wenye lengo la kujadili  Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini nchini Tanzania hususan Mkoani Geita ambapo unategemea kufanyika kwa siku mbili.

Mkutano huo, ulihudhuriwa na  Wizara ya Madini pamoja na Taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi za Kifedha, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shirika la Bima la Taifa, Tume ya Madini, Kamati ya Ushiriki na Ushirikishwaji katika Uchumi wa Madini wa Mkoa wa Geita, kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Geita pamoja na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML).

Kamishina Ngole amesema, Nchi nyingi za Afrika zina  rasilimali nyingi za Madini lakini baada ya marekebisho ya Sheria kwa upande wa Tanzania kuwekwa kipengele cha Kuwashirikisha Wazawa katika Uchumi wa Madini imesaidia kuongeza wigo wa fursa kwa watanzania zaidi na ilivyokuwa awali ambapo ilitegemewa mapato pekee.

Kabla ya mabadiliko ya Sheria, Kampuni za Migodi zilikuwa zinaagiza bidhaa nje ya nchi hata kama bidhaa hizo zinapatikana nchini, walikuwa wanaagiza mchele, mayai na vingine vingi ambapo baada ya Sheria hii vitu vyote vinavyopatikana nchini lazima vinunuliwe kutoka hapa nchini”, Ngole aliongeza.

Pia, Ngole alisema kuwa hapo awali nafasi nyingi za juu ambazo ndiyo za watoa maamuzi zilikuwa zinashikiliwa na wageni kutoka nje ya Nchi pia, waliolipwa mishahara mikubwa ni wageni kutoka nje ya Nchi.

kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa Mhandisi Gabriel, amezitaka taasisi za kifedha kuangalia namna ya  kuwawezesha Wachimbaji Wadogo na Wafanyabiashara wa Madini kwa kuwapatia Elimu juu ya namna bora ya Uwekezaji katika Sekta hiyo.

Kamati ya ulinzi ya Wilaya katika mkutano wa ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini uliyofanyika Septemba 22, 2020 mkoani Geita

“Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ni Sauti ya wle wasiokuwa na Sauti ndiyo maana tumeona amewasaidia sana wachimbaji wadogo,” amesema  Mhandisi Gabriel.

Naye, Meneja Mwandamizi wa Biashara wa NMB Christopher Mgani, amesema benki ya NMB inakopesha vifaa kwa migodi mbalimbali hivyo ametoa wito kwa wadau wa Madini kote nchini kwenda kukopa vifaa vya uchimbaji.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 22 Septemba, 2020   katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Ukezaji kwenye Sekta ya Madini yenye Kauli mbiu ‘Madini ni Uchumi, 2020 Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Taifa’

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link