Majengo Matatu ya Vituo vya Umahiri Yakabidhiwa kwa Wizara

 

Na Tito Mselem, Simiyu

Naibu Waziri wa Wadini Stanslaus Nyongo akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye amekabidhiwa Jengo la Kituo cha Umahiri Bariadi katika hafla iliyofanyika mkoani Simiyu Septemba 8, 2019.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati)ni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye na kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi wakijadiri jambo

Hadi sasa Vituo Vitatu (3) vya Umahiri vimekabidhiwa kwa Wizara na Mkandarasi SUMA JKT na wizara kuvikabidhi kwa Tume ya Madini baada ya kukamilika kwa asilimia 100.

Vituo hivyo vitatu ya Bukoba, Bariadi, na Mara kati ya Saba vilivyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini vimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.4 kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) huku Kituo cha Simiyu kikigharimu shilingi Bilioni 1.308.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema Lengo la vituo pamoja na mambo mengine vimelenga katika kutoa mafunzo ya kitaalam yanayohusu Madini, Utafiti wa Madini, ambapo piia mafunzo hayo yataonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo wake, Uchimbaji wa Madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji.

Pia, alieleza kuwa, katika majengo hayo kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao usagaji wa mawe na kupima sampuli za madini mbalimbali.

“Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ilifanya utafiti wa kijiolojia na kubaini maeneo saba muhimu ambayo vituo vya umahiri vimejengwa ikiwemo Simiyu,” alisema Nyongo.

Akikabidhi Jengo hilo kwa Ofisi ya Madini Simiyu, Naibu Waziri ametaka litumike kwa kusudio lililowekwa la kuhakikisha wachimbaji wadogo wanafanya shughuli zao kwa ufanisi na hatimaye kuongeza makusanyo ya Serikali.

Aidha, ametoa wito kwa wachimbaji wa madini na wananchi kwa ujumla kukitumia kituo hicho cha Simiyu ili kujifunza na kupata taarifa kuhusiana na shughuli za utafiti na uchimbaji madini kwa kuwa kituo hiki kimejengwa kwa ajili ya wananchi na kwa kodi za wananchi.

Kwa upande upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka aliipongeza Wizara ya Madini kwa ujenzi wa kituo hicho muhimu kitakacho wasaidia wachimbaji wengi wa madini katika Mkoa wa Simiyu.

Naye, Kaimu Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis alisema kuwa   mradi huo umegawanywa katika sehemu kuu tatu ambazo ni kuongeza unufaikaji kutokana na sekta ya Madini kwa Nchi, kukuza uwazi na uwajibikaji katika Sekta ya Madini na Mafunzo na Usimamizi wa Mradi.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (kulia) akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye wakifuatilia jambo wakati wa makabidhiano ya Jengo la Kituo cha Umahiri

“Mradi ulijikita katika kutekeleza kazi mbalimbali zikiwemo ujenzi wa vituo saba vya umahiri, ujenzi wa vituo vya mfano, ukarabati wa ofisi za madini, ununuzi wa vifaa vya ofisi za madini, ununuzi wa samani za ofisi, utafiti wa kijiolojia katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uchimbaji mdogo, na kuongeza ushirikiano na serikali za mitaa zinazofanya shuguli za madini,” Veronica alisema. 

Alisema Serikali iliamua kujenga kituo hicho mkoani humo baada ya utafiti wa kijiolojia uliofanywa na kubaini uwepo wa mashapo ya kutosha katika maeneo ya Nyaranja Meatu na kuwepo na madini ujenzi, na kuongeza kwamba, taarifa za awali za kijiolojia zilionesha utafiti mkubwa wa Madini ya Nickel maeneo ya Dutwa na Ngasamo.

Aliongeza kwamba, Wizara kupitia Mradi imejenga jengo la Taaluma katika Chuo cha Madini (MRI) kwa ajili ya matumizi ya ofisi, madarasa, kumbi za mikutano na ofisi za ushirika wa wachimbaji madini wanawake Tanzania kwa ajili ya kuendeshea shuguli zao.

Ujenzi wa Vituo vya Umahiri na Jengo la Taaluma Chuo Cha Madini Dodoma umegharimu jumla ya shilingi bilioni 11.9 huku vituo saba vya Umahiri vikigharimu shilingi bilioni 7.897.

Kazi za ujenzi kwa baadhi ya majengo zimekamilika  kwa asilimia 100 na mengine yapo katika hatua za ukamilishaji na Mkandarasi anatarajia kukabidhi Majengo hayo hivi karibuni.

 

 

 

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link