Na. Samwel Mtuwa – Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Godfrey Zambi leo Oktoba 5 , 2020 ameipongeza na kuishukuru Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kutoa mrejesho wa Utafiti wa awali unaoonesha uwepo wa Madini mbalimbali Wilayani Liwale Mkoani Lindi.

Wataalam kutoka GST wa kwanza kutoka (kushoto) Solomon Maswi, anayefuata Damas Mushi na Charles Moyes wakiwa katika Mkutano wa Uwasilishaji wa Matokeo ya Utafiti wa Awali katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi

Akizumgumza mapema baada ya kumalizika kwa Uwasilishwaji Mh.Zambi alisema mrejesho huu utasaidia kufahamu juu ya rasilimali Madini zinazopatikana mkoani Lindi ikiwa pamoja na kuongeza fursa za Uwekezaji katika sekta ya Madini.

“Ukweli ni kwamba sekta ya Madini ina mchango mkubwa katika pato la taifa na sisi hapa Lindi tunapopata taarifa Kama hizi tunasikia faraja Sana , nawashukuru Sana wataalam kutoka GST”alisema Mh. Zambi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Mh.Rehema Madenge ameiomba GST kuwasilisha taarifa za Madini katika Wilaya nyingine za Mkoa wa Lindi zinazobainisha uwepo wa Madini.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mbwana Kambangwa alisema kuwa Utafiti huu wa awali utafungua milango ya uwekezaji katika sekta ya Madini ndani ya Wilaya ya Liwale.

Uwasilishwa wa mrejesho wa Utafiti awali umeudhuliwa na watu mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi , Katibu Tawala Mkoa wa Lindi , wakuu wa vyombo vya ulinzi na usala ma mkoani Lindi , Kamanda wa TAKUKURU mkoani Lindi , watumishi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa , pamoja na waandishi wa habari.