Mradi wa Kituo cha Mfano cha Uchenjuaji Dhahabu Kuwanufaisha Wananchi wa Bukombe

Na Tito Mselem

IMEELEZWA kuwa mradi wa kituo cha mfano cha uchenjuaji wa Dhahabu kilichopo katika wilaya ya Bukombe, mkoani Geita unatarajia kuwanufaisha wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu na wananchi wanaozunguka eneo hilo kutokana na mradi huo unatekelezwa katika eneo lao.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akipewa maelezo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa kituo cha mfano cha uchenjuaji wa madini Katente.

Mradi huo uliogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 unatekelezwa katika Kata ya Katente Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe huku kituo hicho kikiwa na wataalamu elekezi (MAGIOLOGIA) kufuatia uwepo wa mitambo ya kisasa ya uchenjuaji Dhahabu kikamilifu pamoja na  vifaa vyote vya uchimbaji wa Dhahabu ili kuwasaidia wachimbaji hao watakaokodi na kuepuka dhana  Duni moko na sululu wanazotumia kwa sasa.

Waziri wa Madini na mbunge wa Jimbo hilo Doto Biteko alisema kuwa mradi huo utakuwa na tija kwakuwa kituo hicho kitatoa fursa za ajira kwa vijana wa maeneo hayo sambamba na kutekeleza miradi mingine ya maendeleo kwa wananchi kama kuchimbia kisima kirefu ili kuwapatia huduma ya maji safi na salama.

Biteko alibainisha hayo juzi alipotembelea mradi huo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha mfano cha uchenjuaji wa Madini ya Dhahabu kinachosimamiwa na STAMICO huku akisema kuwa kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1.6 na kubainisha kuwa kwa vituo hivyo kwa nchi nzima vimejengwa katika Mikoa ya Mbeya wilaya ya chunya, mkoa wa Geita Kata za Katente wilaya ya Bukombe pamoja na lwamgasa mkoani humo.

ÔÇťKatika Wilaya ya Bukombe kwa sasa mradi huu una asilimia 85 na niwahakikishie kufikia Octoba mwaka huu utakuwa umekamilika, kila kitu kitafanyika hapahapa ikiwamo kabon, kitamaliza changamoto za wachimbaji na nimeagiza uongozi wa kituo hiki kujenga kisima kirefu ili wananchi wa maeneo haya wanufaike na mradi wa maji safi na salama hali hiyo itafanya waone mradi wa kituo hiki unatija kwao,ÔÇŁ Alisema Waziri wa Madini Doto Biteko na kuongeza.

ÔÇťRais Magufuli amekusudia kuwasaidia watanzania wanyonge katika nchi yao, zamani wachimbaji wadogo wadogo walikuwa watafiti wa matajiri wakigundua Dhahabu katika maeneo yao anajitokeza tajiri anadai ni eneo lake kwa sasa hakuna utaratibu ho niwaombe mradi huo ni wa wananchi utatumika kubadirisha maisha na kama wachimbaji mtafanya kazi kwa bidii kipindi kijacho Bukombe itabadirika kimaendeleo,ÔÇŁ alisema.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akiongea na wachimbaji wadogo wa dhahabu Katente

Naye Diwani wa Kata ya Katente, Bahati Kayagila akionyesha furaha yake kwa Mheshimiwa Waziri wa Madini alisema kuwa Mradi wa kituo cha mfano cha uchenjuaji kujengwa kwenye kata yake kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hiyo ni kuthamini mchango wa wananchi anaowaongoza na kuiomba serikali ikamirishe mapema mradi huo ili wananchi waweze kunufaika na kuleta maendeleo.

Kwa upande wake meneja wa STAMIKO Lojas Sezinga alisema kuwa Mitambo ya uchenjuaji imelenga kubadirisha maisha ya wachimbaji wadogo na kitatoa huduma za Giologia kwao pamoja na kutoa mafunzo mbalimbali ya upasuaji wa miamba ya mawe kutoka kwa wataalamu wake huku akisea kuwa kutokana na jitihada za Waziri kituo hicho kitakamilika na kufanya kazi na wachimbaji kwa vitendo na kuahidi kuwa kuwanufaisha wao.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link