Naibu Waziri Nyongo Apiga Marufuku Uchomaji Dhahabu Kiholela

Na Tito Mselem, Chunya

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amepiga marufuku uchomaji wa dhahabu kiholela na badala yake amewataka Maafisa Madini nchini kote kutafuta eneo moja kuchomea dhahabu.

Alitoa agizo hilo Septemba 10, 2019 wakati akizungumza na Wachimbaji wadogo, Wafanyabiashara ya dhahabu pamoja na maafisa Madini wa mkoa wa Mbeya.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na wadau wa Madini Wilayani Chunya.

“Naomba nichukue fursa hii kuwaagiza maafisa madini kote nchini kusimamia upatikanaji wa sehemu maalum ya kuchomea dhahabu, hii ni kwa sababu dhahabu inayopatikana kwa zebaki hatuioni bado inapotea,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Pia, Naibu Waziri aliwataka Maafisa madini wote nchini kusajili mialo yote inayoosha dhahabu na kuisimamia ili kuepusha upotevu wa dhahabu inayotokana na zebaki.

“Tumeamua kudhibiti dhahabu zote zinazotokana na zebaki na tumekwishaanza ufuatiliaji maalum, tulianza na Kanda ya Ziwa na sasa tupo nchi nzima,” alisisitiza Naibu Waziri.

Aidha, aliongeza kuwa, katika Sheria Mpya ya Madini imeweka kipengele cha ushiriki wa nchi na wananchi katika biashara ya madini ili wananchi wanufaike, na kusisitiza kuhusu madini yanayo chimbwa nchini ni lazima yaongezewe thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje. Na kuongeza, “sheria imeeleza kuwa wafanyabiashara wote wa madini lazima waweke mahesabu yao wazi”.

Waziri Nyongo alitoa wito kwa wafanyabiashara wote wa madini kuyatumia masoko yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini na wasipofanya hivyo watakamatwa na watafikishwa mahakamani na kutaifishwa madini yao.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mary Prisca Mahundi akizungumza jambo katika kikao hicho. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongi na kulia ni Afisa Madini Chunya,Godson Kamihinda

Aidha, Nyongo aliongeza, wadau wanaotoka nje ya nchi pia wanaweza kufanya biashara kwenye masoko bila ya kubuguziwa na mtu yeyote.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Chunya MaryPrisca Mahundi kwa Juhudi nzuri zinazofanywa na wizara katika kuboresha sekta ya madini hususan suala la kudhibiti utoroshaji wa madini nchini.

“Napenda nichukue fursa hii nikupongeze Naibu Waziri kwa juhudi kubwa mnazozifanya katika kuboresha sekta hii ya madini, miezi mitatu iliyopita tulipata kilo 25.9 za dhahabu zinazotokana na zebaki katika soko letu la Chunya lakini baada ya oparesheni hii maalum mwezi huu tumepata kilo 97.2 za dhahabu zinazotokana na zebaki hayo ni mafanikio makubwa,” alisema

Aidha, Mahundi ameahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri Nyongo ya kuhakikisha kuwa mialo inasajiliwa na kusimamiwa pia kuhakikisha wachimbaji wote wanachomea dhahabu zao sehemu moja.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link