Naibu Waziri Nyongo atoa Siku Saba Madini yote kufikishwa Sokoni, Arusha

Na Nuru Mwasampeta, Arusha

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, ametoa Siku Saba kuanzia tarehe 19 Novemba hadi Novemba 26, 2019 kuhakikisha Wafanyabiashara wote wa Madini waliohifadhi madini majumbani mwao wanayafikisha sokoni kabla Oparesheni ya Kamatakamata haijaanza.

Wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa nchi ambapo Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha walizungumza nao juu ya masuala mbalimbali yanayohusu biashara ya madini.

Pia, body-strong.net Nyongo ametoa kibali kwa wanunuzi wadogo na wakubwa kufanya biashara popote isipokuwa wanatakiwa kuzingatia Sheria na taratibu zinazoongoza Sekta ya Madini na kuongeza kuwa, mfanyabiashara mwenye leseni na vibali halali vya kufanya biashara hiyo asizuiliwe kwa vigezo vya mipaka ya kimikoa.

Hayo, yalielezwa Novemba 18, 2019 eneo lilipo soko la madini la Arusha ambapo Naibu Waziri Nyongo alifika ili kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Waziri wa Madini Doto Biteko ya kuhakikisha biashara zote za madini mkoani Arusha zinafanyika katika masoko ya madini ambapo tarehe 19 Novemba, 2019, ilikuwa mwisho kwa wafanyabiashara wa madini kufanya biashara hiyo nje ya soko.

“Brokers wa Manyara au Arusha anatumia ‘Tin’ namba moja kulipa kodi za serikali na serikali ni moja, tumefungua wigo brokers wa Arusha aruhusiwe kufanya biashara Manyara na wa Manyara aruhusiwe kufanya kazi Arusha, hatutaki biashara icheleweshwe ili wafanyabiashara wailipe serikali chake na kuendelea na biashara,” alisisitiza Nyongo.

Amekumbusha kuwa, wanaofanya biashara nje ya soko oparesheni kamatakamata inaendelea na kuwaeleza kuwa wakiuza madini nje ya soko watambue kuwam wao ni adui wa serikali namba moja. “Ninatoa siku saba kama una madini yasiyo halali nyumbani yatoe uyalete sokoni baada ya siku saba oparesheni inaanza na utakamatwa’’.

“Kwa sasa sisi ni wataalamu wa kuwakamata watoroshaji wa Madini, tunajua jinsi biashara ya madini inavyofanyika hivyo hutakuwa na namna ya kutukwepa,’’ alisema Nyongo.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Nyongo amemwagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Mjiolojia Musa Shanyangi Kuhakikisha anasaini maombi yote ya leseni yaliyowasilishwa kwa miezi ya Julai, Agosti na Septemba ili kuwaruhusu wafanyabiashara hao kuendelea na kazi zao. Amesema, kuchelewesha watu kupata leseni ni kichocheo cha biashara za magendo.

Akihitimisha hotuba yake, Naibu Waziri Nyongo aliwapongeza wafanyabiashara wa madini wa Mkoa wa Arusha kwa kuitikia wito uliotolewa na Waziri Biteko  hali iliyopelekea  kufurika sokoni kuendelea na biashara zao. Alisisitiza kuwa serikali ipo nyuma yao kuhakikisha wanafanya biashara halali na kulipa kodi za serikali.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kizungumza na wafanyabiashara wa madini walipokusanyika kumsiliza mara baada ya kuwasili sokoni hapo kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Madini ya kuwataka wafanyabiashara hao kuhamishia shughuli zao sokoni hapo na si kwingineko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliwataka wafanyabiashara hao wa madini kutokutumia uhuru wao vibaya na kuwaeleza kuwa wakitaka kufurahia kazi yao wafuate taratibu na Sheria zilizowekwa na serikali ili kuwaongoza. “Mna uhuru wa kufanya biashara hivyo mfanye katika maeneo yanayokubalika,” alisititiza Gambo.

Pamoja na hayo, Gambo aliwataka wafanyabiashara hao wa madini kuhakikisha wanaweka uongozi wa soko usiokuwa na itikadi yeyote na kupotosha wengine na kusema, “Msituletee wanaharakati”.

Akikazia suala hilo, Gambo alisema kuwa, yapo makundi ya watu wanaojiita wanaharakati wakijitokeza kwa kofia ya kuongoza vyama vya wachimbaji na badala yake vinawapotosha na kuwapa taarifa zisizo sahihi, katika biashara sokoni hapa achaneni na vyama vya wachimbaji vitawapoteza.

Aliendelea kueleza kwamba vyama hivyo kazi yake ni juu ya vyombo wanavyoviongoza huku akisisitiza kuwa masuala ya serikali yanamalizwa na serikali husika ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni za biashara za madini zinatolewa na serikali na si wanaharakati.

Akihitimisha kuzungumza na wafanyabiashara hiyo, Mkuu wa Mkoa Gamba aliwaeleza maamuzi ya kusogeza huduma za kupata vitambulisho vya utaifa pamoja na Tin namba sokoni hapo ili kuwapunguzia mzunguko wakati wa kuratibu maombi yao ya leseni.

Wakitoa mombi yao kwa serikali, wafanyabiashara wa madini Hussein Idd aliiomba serikali kupeleka wanunuzi wa mawe yasiyo na thamani kubwa sokoni hapo ili na wao waweze kupata mahali pa kuuzia madini yao wakati Mohamed Juma aliitaka serikali kulegeza masharti na kuwapunguzia vikwazo watu kutoka nchi za nje wanapofika na pesa zao ili ziwawezeshe kufanya biashara ya madini nchini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link