Naibu Waziri Stanslaus Nyongo aongoza kikao cha maridhiano na kupokea ombi la mwekezaji

Mwekezaji afurahia utendaji wa Wizara ya Madini Aipongeza Serikali

Nuru Mwasampeta, Nzega

Serikali imeridhia ombi la kupunguza gharama ya ununuzi wa dhahabu unaofanywa na mwekezaji Rashed Shabout Said wa kampuni ya Ashery Construction & Matinje gold Extraction ya uchenjuaji wa marudio ya mchanga wa dhahabu ulioachwa na kampuni ya Resolute iliyofunga shughuli zake za uchimbaji mkubwa wa madini ya dhahabu mwaka 2014.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega ili kusikiliza maombi na kutatua changamoto za wachimbaji na wawaekezaji wadogo wa madini jana tarehe 27Aprili, 2020

Makubaliano hayo yalifikiwa Tarehe 27 Aprili, 2020 wakati wa kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kilicholenga kujadili ombi la mwekezaji Rashed Shabout Said anayechenjua dhahabu kwenye mabaki hayo ya mchanga wa dhahabu ulioachwa na kampuni ya Resolute iliyokuwa ikichimba dhahabu wilayani Nzega, Mkoani Tabora.

Pamoja na Naibu Waziri Nyongo kikao hicho kiliwahusisha Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora Mayingi Makalobela, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula, Mkuu wa Chuo cha Madini kampasi ya Nzega, Nuru Shabani, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nzega pamoja na ujumbe ulioambatana na mwekezaji huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Naibu Waziri Nyongo alisema, kikao kimeridhia ombi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa na mwekezaji ikiwa ni kushusha bei ya kumwuzia dhahabu kiasi kilichopunguzwa kimsaidie kulipia gharama nyingine anazozitumia katika uwekezaji huo.

Nyongo alisema, Rashed aliomba kupunguziwa gharama ya dhahabu anayoinunua serikalini mara baada ya uchenjuaji, kuondolewa gharama za watumishi wanaoshiriki katika kusimamia mchakato mzima wa uchenjuaji wa mchanga huo pamoja na kuondolewa malipo ya mrabaha na kurudishiwa pesa zilizolipwa kama mrabaha kwa awali mbili za uchenjuaji zilizopita.

Nyongo alibainisha kuwa, Wizara kwa kushirikiana na Tume ya madini zimeridhia kupunguza gharama ya kuuza dhahabu kwa mwekezaji huyo na kwamba huduma nyingine na malipo ya mrabaha yatapaswa kulipwa kama kawaida kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya alisema ombi la mwekezaji limepokelewa na kwamba hatua inayofuata ni kwenda kupitia na kurekebisha mkataba ikiwa ni pamoja na kupeleka maoni yaliyofikiwa na kikao hicho kwa mamlaka nyingine ili kumwezesha mwekezaji huyo kufanya kazi yake kwa tija na bila manungÔÇÖuniko.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula wakati wa kikao na wachimbaji wadogo wa madini kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega jana tarehe 27 Aprili, 2020

Akizungumza na waandishi wa habari mwekezaji Rashed, aliishukuru serikali kwa kupokea na kufanyia kazi ombi lake na kukiri hakutegemea kuwa angesaidiwa kwa haraka namna ilivyofanyika na kukiri kwamba hakika Serikali ya Awamu ya Tano inasikiliza na kutatua changamoto za wananchi. ÔÇťNashukuru sana kwa serikali hadi Naibu Waziri kuja kunisikiliza kwakweli Wizara ya madini ni sikivu sana, nashukuru sanaÔÇŁ Rashed alikazia.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa corona Rashed alisema kumekuwa na changamoto ya usafirishaji wa madini kutokana na ndege nyingi za nje kusitisha safari za nje hivyo inakuwa ngumu kwa kuendesha biashara.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link