Ni Rasmi Chuo cha Madini Kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam

* Nyongo – Mabadiliko Yasiondoe Majukumu ya Msingi

* Prof. Anangisye –┬á Msihofu Chuo Kiko┬á Mikono Salama

Asteria Muhozya na Steven Nyamiti, Nzega

Imethibitishwa kuwa sasa Chuo cha Madini kilichokuwa chini ya Wizara ya Madini kitakuwa sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. Hayo yalithibitishwa Agosti 19, 2020 wakati wa Hafla ya Kukabidhi Chuo hicho cha Kampasi ya Dodoma na Nzega Kulelewa kwa muda na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam  katika hafla iliyofanyika katika Kampasi ya Nzega Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora .

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wanaosoma Chuo cha Madini (MRI) katika hafla ya kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika katika Kampasi ya Nzega Agosti 19,2020.

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alisema  kuwa tukio hilo ni moja ya hatua za uboreshaji wa Sekta ya Madini pamoja na kuhakikisha nchi ya Tanzania  inazalisha wataalam wa kutosha  na wenye ujuzi wa hali ya juu katika sekta ya madini kuanzia ngazi ya Astashahada hadi Stashahada ili nchi iweze kusimamia rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia bila kutegemea wataalam kutoka nje.

Alisisitiza kuwa, Serikali  inaamini kuwa,  ulezi wa Chuo  cha Madini kama ilivyoelezwa kwenye mchakato wa awali, kitaendelea  kutoa mafunzo ya mchundo na mafundi sanifu katika sekta ya Madini lengo  likiwa  kukifanya kitengamae hatimaye kiweze kujiendesha.

“Uleaji utakaotolewa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ulenge kukiimarisha Chuo Cha Madini Kitaaluma, kuboresha miundombinu na kuongeza ufanisi┬á wa utendaji kazi,” Alisisitiza Nyongo.

Aliongeza kuwa, Mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa na UDSM yasilenge kuondoa majukumu ya msingi ya Chuo Cha Madini.

“Ni matarajio ya Serikali na Wizara kuwa  Chuo hiki kitafikia viwango vya Kitaaluma vinavyokubaliwa Kitaifa na Kimataifa,” alisema Nyongo.

Akielezea kwamba,  kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kutokuwepo kwa Sheria ya kuanzishwa Chuo Cha Madini; uvamizi  wa maeneo hususan Kampasi ya Nzega na kuongeza kwamba  anaamini  changamoto hizo zitatatuliwa chini ya ulezi huo na kwamba , hafla hiyo  ni matokeo ya utatuzi wa changamoto hizo.

Pia, alizungumzia  hatua mbalimbali ambazo zimechukukiwa  na Serikali, ambazo zimepelekea Sekta ya Madini sasa imeanza kukua kwa kasi kubwa, ambapo Mwaka 2019 iliongoza kwa Ukuaji  kwa asilimia 17.7.

Picha ya pamoja ya kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nzega (kushoto), Viongozi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (katikati) na wafanyakazi wa Wizara ya Madini (kulia) wakisikiliza wakati wa hafla ya kukabidhi Chuo cha Madini (MRI) kulelewa na UDSM katika hafla iliyofanyika Agosti 19, 2020 Kampasi ya Nzega

Alisema kutokana na jitihada hizi sasa  mapato yanayotokana na madini yameongezeka  ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/2019 zilikusanywa Shilingi Bilioni 346 kutoka Shilingi Bilioni 194  Mwaka 2016/17, kwenye Mwaka 2019/2020 zlikusanywa zaidi ya Shilingi Bilioni 470 ambalo  ndiyo lilikuwa lengo la Wizara.

“Malengo kwa Mwaka 2020/2021 ni kukusanya  Shilingi Bilioni 543 , tunaweza kufika Bil 600 lakini pia tuna ndoto ya kukusanya Shilingi Trilioni Moja kwa Mwaka,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Aliongeza kuwa,  Rais Dkt. John Magufuli kwa muda mrefu  amekuwa akisisitiza kuhakikisha rasilimali zetu ikiwemo madini zinasimamiwa kikamilifu ili ziweze kuwanufaisha watanzania ikiwa ni pamoja na kuimarisha Uchumi hatimaye kupunguza utegemezi.

Aliyataja mafanikio mengine tuliyoyapatikana kwenye Sekta ya Madini kuwa Ni pamoja na  kutolewa kwa Leseni 221 za uchenjuaji wa Madini, Leseni 4 za uyeyushaji madini ( smelting) na Leseni 4 za usafishaji madini (refining).

Pia, alisema Wizara imetenga hekta 38.567 kwa ajili ya uchimbaji mdogo na kuwapatia mafunzo wachimbaji wadogo na kuwawezesha kutengeneza maisha yao bila bughudha.

Akizungumza katika hafla hiyo,  Mkuu  wa Wilaya  ya Nzega A. C.P Advera  Bulimba  kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora  alitoa Pongezi kwa  Serikali kuchukua hatua za kuboresha  Chuo hicho na kueleza Serikali ya Mkoa na Wilaya itashirikiana na Chuo kuhakikisha mazingira na mali za Chuo zinalindwa.

“Ni matarajio Chuo kitaongeza Usajili kulingana na mahitaji ya Chuo. Tunawahamasisha wazazi walete watoto wao ili kuboresha Mkoa wetu,”alisema A.C.P Bulimba.

Aliongeza kwamba  Mkoa umefurahia kutokana na hatua hizo zilizochukuliwa kwa kuwa zitauwezesha Mkoa kupata fursa za kimapato kupitia fursa mbalimbali zitakazotolewa na Chuo hicho.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, akieleza jambo katika hafla ya kukabidhi Chuo cha Madini (MRI) kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika Agosti 19, 2020 Kampasi ya Nzega. (Kushoto) ni Prof. William Anangiye Makamu Mkuu wa Chuo Cha Dar es salaam  

Aidha, aliwasisitiza wazazi Mkoani humo kuhakikisha wanapeleka watoto wao ili kupata Elimu zinazotolewa na Chuo hicho  kwa  Lengo la kuboresha Maendeleo ya Mkoa huo.

Naye, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa alizingumza katika halfa hiyo alisema kuwa, wazo la Chuo Cha Madini kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam lilitoka Wizara ya Madini mwezi Januari 2018 ambapo uamuzi ulikusudia kukiwezesha Chuo   cha Madini kuongeza nafasi za udahili, kuendesha kozi zinazoendana na soko la ajira, kuongeza ufanisi katika maeneo  muhimu ya Utafiti,uchapishsji na kuongeza huduma zinazotolewa na Chuo cha Madini.

Akielezea uzoefu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika kuvilea Vyuo vingine alisema kwamba,  uzoefu unaonesha njia ya kulelewa na Taasisi kubwa zenye uzoefu ni bora zaidi katika kuziwezesha taasisi changa kujisimamia zenyewe.

“Chuo cha Ardhi- DSM ambacho kililelewa na UDSM kuanzia Mwaka 1996 mpaka Mwaka 2006 kilipoachwa kijiendeshe chenyewe na Chuo Kikuu cha Mzumbe  wakati huo kikijulikana Kama  Insitute of Development Management ( IDM) kililelewa na UDSM kwa kipindi Cha muda wa miaka 8 na baada ya hapo kiliweza kusimamia na kujiendesha chenyewe na sisi sote ni mashahidi wa mafanikio ya Vyuo hivi viwili,” alisistiza Mhandisi Mulabwa.

Akielezea kuhusu hatua kadhaa zilizochukuliwa ambapo alisema kuwa,  katika hatua za kukamilisha mchakato wa kulelewa, tarehe 20 Februari 2020 ilisainiwa Hati ya Makubaliano  kati ya Wizara ya Madini, Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambayo iliandaa iliandaa utaratibu mzima wa kulelewa.

Pia, alisema kutokana na utaratibu uliowekwa katika Hati ya Makubaliano, mambo mbalimbali yalifanyika ikiwemo kutangazwa kwa Order ya kuanzishwa Chuo  cha Madini katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kuandaliwa kwa muundo wa Taasisi na Muundo wa Utumishi wa Chuo Cha Madini kubainisha Mali zilizopo chini ya Chuo Cha Madini.

” Ni Matumaini yangu kuwa utoaji wa mafunzo wa Chuo cha Madini utakuwa wa kiwango cha juu, udahili wa wanafunzi utaongezea nchini na kutoka nje ya nchi, miundombinu itaboreshwa na kutimiza jitihada za Serikali za kuhakikisha inakuwa na wataalam wazawa watakaofanya shughuli  mbalimbali katika Sekta ya Madini,”” alisema Mhandisi Mulabwa.

Vilevile alisistiza kuwa,  Chuo kitakapoachiwa kitakuwa na mifumo mizuri ya kujiendesha chenyewe

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Prof. William Anangisye alisema kuwa, kwa Chuo Cha Madini kuwa sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam , kinatarajiwa kupata fursa ya kuingia katika wigo mpana zaidi wa kitaaluma.

“Tunafurahi kuwa kwa kupitia mazungumzo ya pamoja kati ya wizara zetu mbili, yaani Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Madini, Sasa tumefikia muafaka kuwa Chuo cha Madini Dodoma kitakuwa sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam baada ya mchakato wake ambao ulianza tangu Mwaka 2018,” alisema Prof. Anangisye.

Aliongeza kwamba, Chuo Kikuu Cha UDSM kimegusa nyanja nyingi  za kitaaluma ikiwemo taaluma ya Madini , ambapo Idara  ya Jiolojia imetoa wataalam wanaoheshimika duniani na imekuwa na mchango mkubwa sana Kitaifa na kuongeza kwamba, jukumu  hilo la kukilea  Chuo Cha Madini  litatupeleka Chuo Cha UDSM kuwa karibu zaidi na Watanzania ambalo ndilo Lengo la chuo.

ÔÇťNapenda niwa hakikishie Makatibu Wakuu wa Wizara zetu mbili kuwa Chuo Kikuu cha Dar┬á Es Salaam kina uzoefu mkubwa wa kukuza taaluma baada ya Kukabidhiwa Vyuo mbalimbali vya Serikali,” alisema Prof. Anangisye.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Madini (MRI) katika hafla ya kukabidhi chuo Chuo cha Madini Kulelewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyofanyika Agosti 19, 2020 katika Kampasi ya Nzega

Prof. Anangisye aliwasisitiza Wafanyakazi na Watumishi sawa Chuo cha Madini kuwa  kuwa wako katika Mikono salama na hivyo hawapaswi kuwa na hofu yoyote ya kuwa sehemu ya chuo hicho.

” Masuala yanayohusu mustakabali wa wafanyakazi na wanafunzi, mali za chuo na mengine mengi, yalijadiliwa kwa kina na umakini mkubwa na Kamati Kuu ya kusimamia Ujumuishaji wa Chuo cha Madini Dodoma kwenye Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. Sisi tunazingatia  yote yaliyopendekezwa na kukubaliwa na tutazingatia wajibu wetu kukiboresha Chuo  cha Madini na kuimarisha viwango vyake vya taaluma,” alisema

Akizungumzia  nafasi ya  Chuo  Kikuu Cha Dar Es Salaam  katika kuendeleza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  John Magufuli katika kuiendeleza Sekta ya Madini Nchini, alisema  moja ya matokeo ya uongozi wake ni kuboresha Sekta ya Madini na kuifanya kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa  nchi yetu, hivyo Chuo hicho  kinachukulia  hatua ya Kukabidhiwa Chuo cha Madini kama  sehemu ya Utekelezaji wa  dhamira ya Serikali ya kukuza Sekta ya Madini.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu  wa Chuo cha Madini Elvanus Kapira alialeza kwamba Menejimenti ya chuo inaamini kwamba kupitia mpango wa kulelewa, Chuo  cha Madini kitaimarika katika nyanja za kielimu, kitafiti, pamoja na huduma za kutoa  ushauri Elekezi huku  changamoto zote zinazokikabili Chuo ambazo zinapelekea kukua kwa  kasi isiyolizisha zitatatuliwa  chini ya mpango wa kulelewa na Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.

Alisema kuwa, menejimenti na wafanyakazi wote wa Chuo  cha Madini wanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote  cha mpango kulelewa ili kufanikisha malengo mahususi ya kuboresha  elimu na huduma zinazotolewa na Chuo  cha Madini kwa masilahi mapana ya Taifa letu.

” Menejimenti ya Chuo cha Madini inaishukuru Wizara ya Madini kwa jitihada ilizochukua kwa ajili ya kukiendeleza Xhuo Cha Dar Es Salaam na pia inaishukuru Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam kwa kuridhi kukilea Chuo hiki,” alisema Kapira.

Pia, Kapira akielezea mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho na kusema pamoja na mafunzo ya muda mrefu , Chuo Cha Madini kinatoa mafunzo ya muda mfupi pamoja na mafunzo Maalum kwa Wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Chuo cha Madini kilianzishwa Mwaka 1982 kwa lengo la kutoa mafunzo ya Ufundi sanifu katika Sekta ya Madini. Chimbuko la kuanzishwa kwake  ni uhitaji uliokuwepo wa wataalm wa kada za ufundi katika miradi ya  utafiti, wa maji, Madini ya Bati na metali nyingine uliojulikana Kama Mineral and Ground Water Exploration Project ( MGWEP) Mkoani Kagera.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link