NMB Yashauriwa kutumia fursa za Kibiashara Sekta ya Madini

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Benki ya NMB imeshauriwa kutumia fursa za Kibiashara zilizopo katika Sekta ya Madini zikiwalenga Wachimbaji Wadogo na wa Kati wanaofanya shughuli hizo katika sekta husika ikiwemo kujifunza namna biashara ya Madini inavyofanyika.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiagana na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Serikali ya Benki ya NMB, Vicky Bishubo na Mkuu wa Idara ya Uhasibu NMB, Michael Mungure.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila wakati wa kikao baina yake na Ujumbe wa Wataalam kutoka Benki hiyo ulioongozwa na Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Serikali ya Benki hiyo, Vicky Bishubo. Kikao hicho kimefanyika Novemba 25, 2019, jijini Dodoma.

Aidha, kauli ya Katibu Mkuu kwa benki hiyo inafuatia juhudi za Serikali kupitia Wizara ya Madini zinazolenga katika kuwapatia elimu Wachimbaji ikiwemo za kutunza kumbukumbu za uzalishaji, kufanya tafiti ili kujua kiasi cha mashapo kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), hayo yote yakilenga katika kuwawezesha wachimbaji hao kukopesheka na Taasisi za Fedha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na Ujumbe kutoka Benki ya NMB pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Madini.

Pia, Prof. Msanjila ameitaka benki hiyo kutumia fursa zilizopo katika masoko ya Madini yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali nchini ili kurahisisha biashara ya Madini na kutolea  mfano wa Soko la Madini Arusha kwamba benki hiyo haina huduma katika soko hilo huku biashara ya Madini sokoni hapo ikifanyika kwa kiasi kikubwa.

Aidha, Prof. Msanjila ameitoa wasiwasi benki hiyo kuwa, hivi sasa biashara za Madini zinafanyika katika mfumo ulio wazi tofauti na ilivyokuwa awali na kuongeza kwamba, ÔÇťkuna biashara nyingi kwenye sekta ya madini. Niwaambie hivi karibuni Serikali ya Qatar itaanza kununua dhahabu moja kwa moja kutoka Geita.ÔÇŁ

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini prof. Simon Msanjila akiongoza kikao baina ya Ujumbe wa Benki ya NMB na Wizara ya Madini.

Katika hatua nyingine, kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 35(j) ya Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015-2020 kuhusu Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa, Prof. Msanjila ameishauri benki hiyo kuangalia namna ya kufanya biashara katika tasnia ya ukataji wa madini, akieleza kwamba, ni miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele na serikali ya kuhakikisha madini yanaongezwa thamani kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

ÔÇťSekta ya madini haijatumiwa vizuri na mabenki ninawakaribisha kwenye sekta hii . Pale Arusha ndo mji pekee wa Ukataji Madini ya Vito. Mwende mkaliangalie hili,ÔÇŁ amesisitiza Prof. Msanjila.

Naye, Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Serikali ya Benki hiyo, Vicky Bishubo  amemshukuru  Prof. Msanjila kwa kueleza fursa zilizopo katika sekta husika na kueleza kwamba, benki hiyo imeyachukua kwa uzito mkubwa yote yaliyoelezwa na iko tayari kuyafanyia kazi.

ÔÇťTumejifunza namna sekta ya Madini inavyofanya kazi kuna uwezekano wa sisi kuandaa mfumo wa kuwasaidia wachimbaji wadogo,ÔÇŁ ameeleza Bishubo.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link