Prof. Mihyo – Sera ni nguzo muhimu katika Sekta ya Madini

Na Issa Mtuwa “WM” Morogoro

Prof. Paschal Mihyo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Sera za Maendeeleo ya Uchumi, Jamii na Mageuzi ya Mfumo wa Uchumi (REPOA) amesema mchango wa Wizara ya Madini kwenye ukuwaji wa uchumi  wa taifa haukwepeki na inawajibu huo kutokana na sekta hiyo kuwa chachu ya ukuwaji  wa uchumi duniani kote.

Amesema Sera ndio kiungo muhimu cha kuifikia hatua hiyo, hivyo ni muhimu sera ya sekta ya madini iguse kila mahali na hilo hufanyika wakati wa uandishi wa sera husika ingawaje kwa sasa kuna tatizo la mvutano kati ya “sera na siasa”.

Mkurugenzi mkuu wa REPOA Dr. Donald Mmari akiongea wakati wa kufunga Mafunzo ya uchambuzi na uandishi wa sera kwa watumishi wa wizara ya madini.

Prof. Mihyo amesema hayo leo tarehe 05/09/2019 wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo yanayohusu uchambuzi na uandishi wa sera kwa watumishi wa wizara ya madini na taasisi zake, mafunzo yanayofanyika katika hotel ya Kingsway mjini Morogoro na yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Madini na REPOA kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway kupitia REPOA.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi watafiti, washauri, na watekelezaji wa sera katika kufanya mapitio na uchambuzi wa sera.

“Mafunzo haya ni muhimu sana na tumelenga kuwafanya watumishi kutambua nafasi zao na nafasi ya sekta hii katika kuchangia ukuwaji wa uchumi wa taifa.” alisisitiza Prof. Mihyo wakati wa mafunzo hayo.

Dkt. Jamal Msami, Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati kutoka REPOA ambaye ni mwezeshaji mwenza wa Prof. Mihyo katika mafunzo hayo, amesema sera ni kiungo muhimu katika kufikia  uchumi wa kati kupitia madini. Kila idara/kitengo kina jukumu la kufanya katika utekelezaji wa majuku yake ambayo hutokana na sera.

Amesema sera inamchango katika kuonyesha namna na mwelekeo wa sekta ya madini katika uchangiaji wa uchumi kwa kuweka mipango sahihi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi amesema sera ndio chombo cha juu cha utekelezaji wa masuala yote yanayofanyika katika wizara. Ameongeza kuwa, mafunzo hayo ni muhimu kwani baada ya mafunzo kutaundwa timu ya wataalum itakayopitia na kuandaa sera ya wizara ambayo pia itapelekea kuwa na muundo mpya wa utumishi utakao kidhi mahitaji halisi na sahihi ya sasa ukizingatia muundo wa wizara unaotumika sasa ni wa mwaka 2002.

Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu Kabigi Nsajigwa akichangia wakati wa mafunzo ya uchambuzi na uandishi wa sera.

Katika mafunzo hayo, mada mbalimbali zimewasilishwa na kugusa masuala ya sera, sheria, uwekezaji, masoko, uchangiaji wa makampuni kwenye shuguli za maendeleo ya jamii (CSR) na ushirikishaji wa wazawa katika masuala ya ajira na manunuzi ya ndani (local content).

Mafunzo hayo ya siku tano, yalianza tarehe 02/09/2019 na kufunguliwaa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila na yatafungwa tarehe 06/09/2019 na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mjini, yakihusisha wataalam wa uchumi, takwimu, jiolojia, uhandisi wa migodi, sheria, mawasiliano na utawala na raslimali watu kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Tanzania Gemmological Centre (TGC) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI)

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal