Prof. Msanjila Asisitiza Kuzingatiwa kwa Mwongozo wa Uendeshaji wa Rush

Na Issa Mtuwa ÔÇô Bariadi Simiyu

Imeelezwa kuwa, migogoro inayojitokeza kwenye Rush (Mlipuko wa Madini) unasababishwa na Kikundi kinachoteuliwa kusimamia uendeshaji wa Rush zinazoanzishwa katika maeneo mbalimbali. 

Hayo yamesemwa Novemba 23, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipotembelea kutatua mgogoro wa Rush ya Bulumbaka ulipo Bariadi mkoani Simiyu ambapo kuna mgogoro kati ya vikundi vya wachimbaji wadogo wa  Mwananyanzala Mine Group, Umoja ni nguvu, Ubunifu & Bulumbaka, Nyamagana Mine Group na Nguvu Moja Mine na mgogoro kati ya wachimbaji wadogo na wamiliki wa mashamba katika mkoa Simiyu wilaya ya Bariadi.

 ÔÇťRush ikitokea kikundi kilichoteuliwa kinatakiwa kizingatie miongozo, nini kifanyeki kwa wakati gani. Mambo yanayo fanyika kwenye mgodi wanaosimamia wamepewa mamlaka ya kusimamia kwa niaba ya Tume ya Madini kwa kuzingatia miongozoÔÇŁ, alisema Prof. Msanjila.

Alisema migogoro inayojitokeza inahusu mvutano wa vikundi vya wachimbaji wadogo wakitaka kila kikundi kiwe msimamizi wa Rush, mgogoro mwingine huibuka kati ya wachimbaji na wamiliki wa  mashamba ambayo madini yameibuliwa na mgogoro mwingine wa mgao unaotokea kati ya wachimbaji na wenye mashamba na mrahaba unaotolewa kwa serikali. Alisistiza muongozo kuzingatiwa kwa kuwa kilakitu kinacholeta mgogoro umetoa maelekezo.

ÔÇťSomeni muongo huu, unaonyesha kila kitu katika hayo mliyoyasema kila kitu kimewekwa wazi na ungefwatwa muongozo huu migogoro isingejitokezaÔÇŁ, aliongeza Prof. Msanjila.

Bwana Majuma Nzige ambae ni mchimbaji alisema chanzo cha mgogoro ni uongozi wa mgodi ambao unaosimamia shuguli mgodini apo. Ameongeza kuwa hata asilimia 30 wanazotozwa wahaoni kitu kinachofanyika huku bwana Webiro Kihatala alisema, pamoja na kuwa na msimamizi, mazingira ya mgodi sio salama kwa maana mazingira ni machafu hakuna vyoo lakini pesa wazotoa.

Kwa upande wa wamiliki wa mashamba, Ngila Machimu, alisema mgogoro wao na washimbaji wadogo wanachimba kwenye mashamba yao bila kupata faida na mazingira yao kwenye mashamba yanakuwa machafu kwa sababu hakuna vyoo.

Akijibu hoja zao kwa ujumla, Prof. Msanjila alisema suluhisho nililolisema ni uzingatiwaji wa muongozo na kutii. Kila kilicholalamikiwa muongozo unatoa suluhisho. Alisisitiza kwamba msimamizi atakae teuliwa hapaswi kuwa mchimbaji katika eneo analosimamia na lazima atoke na ndani ya mkoa wa Simiyu.

ÔÇťNaagiza mchakato wa kumpata msimamizi wa Rush hii, uanze upya na azingatie muongozo katika kutekeleza majukumu. Wakati tukisubiri msimamizi mpya huyu aliyopo ataendelea kusimamia ili kazi ziendeleeÔÇŁ alisema Prof. Msanjila.

 

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link