Profesa Msanjila atoa Kongele Ofisi ya Madini Singida

Na Tito Mselem, Singida

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amewapongeza Watumishi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kwa kuvuka lengo la makusanyo ya Maduhuli ya Serikali baada ya kukusanya kwa asilimia 216.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Simoni Msanjila kulia akiongoza kikao cha watumishi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida, kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Koa wa Singida Chone Malembo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Simon Msanjila akiongoza kikao cha watumishi wa Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Singida, kushoto ni Afisa Madini Mkazi Mkoa wa SWingida Chone Malembo.

Prof. Msanjila alitoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kikazi mkoani humo Mei 9, 2020 baada ya kutembelea Ofisi ya Madini ya Mkoa wa Singida.

“Nimefurahishwa sana na juhudi mnazozifanya watumishi wa ofisi ya Madini Mkoa wa Singida mmedhihirisha wazi kuwa mnaweza kusimamia vyema shughuli za ukusanyaji maduhuli ya Serikali nawapongeza sana kwa kazi nzuri.”

Wakati huo huo, Profesa Msanjila aliwataka watumishi wote wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida kueleza changamoto zao kwa lengo kuboresha shughuli za uzalishaji na ukusanyaji wa maduhuli.

Katika hatua nyingine, Prof. Msanjila alitembelea Soko la Madini la Wilaya ya Shelui, Mgodi ya Nabii Elia na Mgodi wa Sakenke one na kuwataka wachimbaji wa Madini ya dhahabu kuhakikisha wanafuata kanuni, taratibu na sheria za uchimbaji madini kwa mujibu wa sheria.

Alisema pamoja na kuvuka lengo la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali ni wajibu wa kila mchimbaji kufuata Sheria Kanuni na taratibu zinazotolewa na Wizara ya Madini na kueleza kuwa, changamoto nyingine zinazotokea wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ni zakujitakia wenyewe.

‘’Haiwezekani mwende mkachimbe chini ya nguzo ya umeme, kwa  kufanya hivyo mnakuwa mnahatarisha  maisha ya wachimbaji wadogo ambao ndiyo wanaoingia chini kuchimba jambo ambalo  linaweza kuhatarisha maisha ya watu. Tambueni kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini zaidi Maisha ya watu kuliko kitu kingine chochote,” alisema Prof. Msanjila.

 Alisema Serikali iliufunga Mgodi wa SakenkeOne kutokana ukiukwaji wa taratibu za uchimbaji na kuongeza kuwa,  pamoja na wahusika kuomba Mgodi huo ufunguliwe inabidi Tume ya Madini ifanye uchunguzi na kujiridhisha ndipo Mgodi huo utafunguliwa tena. Tena ninawaambia msimlaumu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa yeye hana Mamlaka ya kufungua Mgodi  kwa mujibu wa sheria,” alifafanua Prof. Msanjila.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida wakifuatilia Kikao cka katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila

Akijibu swali la Wachimbaji wa Mchongomani la ukosefu wa  umeme wa uhakika katika Migodi hiyo Profesa Msanjila alisema kwamba, Wizara ya Madini itazungumza na Wizara ya Nishati ili Migodi hiyo iondokane na changamoto ya nishati ya umeme.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula alisema ushirikiano mzuri baina ya Ofisi ya Madini Mkoa na Wachimbaji wadogo wa Sekenke one na Mchongomani pamoja na kamati ya Usalama Wilaya imewezesha kufikia mafanikio hayo

“Kwa kuwa wewe Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini umekuja utatusaidia kutatua changamoto hizo zilizotajwa na wachimbaji hao hususan changamoto ya umeme na nyinginezo ambazo kwa Mamlaka uliyonayo unaweza kuwatatulia kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu za Madini.’’ alisema Luhahula.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo alimweleza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini kwamba changamoto zote za wachimbaji wadogo amekwishaziwasilisha Tume ya Madini.

“Mheshimiwa Katibu Mkuu, Mkoa wa Singida umevuka lengo la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 3,243,231,675.32 sawa na asilimia 216 ambapo Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida ilipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.5,’’ alisema.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida wakifuatilia Kikao cka katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila

Aliongeza kuwa, kuvuka lengo la ukusanyaji huo kumetokana na ushirikano madhubuti wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Wilaya na Mkoa kwa ujumla.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Ushirika wa Uwawakishe Jumanne Masumbuko alimwomba Katibu Mkuu kuwasaidia kuwatatulia Changamoto ya Umeme katika Mgodi wa Mchongomani kwani umume huo hautoshi  kukidhi mashine zilizopo katika Mgodi huo.

Awali, Prof. Msanjila alianza kwa kuwasihi watumishi wa Ofisi ya Madini Mkoa wa Singida, wafanyabiashara na wachimbaji wadogo kuhakikisha wanajilinda dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya korona na kuwataka kuendelea kufuata ushauri wa wataalam ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka mikosanyiko isiyo ya lazima.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link