STAMICO Haiwezi Kufutwa – Kamati ya Bunge

Na Issa Mtuwa, Biharamulo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imesema Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) haliwezi kufutwa tena kutokana na mwenendo wa sasa kuridhisha kutokana na utendaji wake na kubadili mtazamo uliokuwepo awali.

1. Waziri wa Madini aliye tangulia mbele akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma ikiongozwa na mwenyekiti wake Dkt. Raphael Chegeni (wa tatu kulia) kutembelea mgodi wa STAMIGOLD unaomilikiwa na STAMICO.

Kubadili kwa mtazamo huo kunatokana na mwenendo wa awali kutoridhisha katika utendaji wake hali iliyopelekea baadhi ya wabunge kutaka Shirika hilo lifutwe lakini tarehe 17/11/2019 wajumbe wa kamati hiyo walisema kwa sasa shirika hilo haliwezi kufutwa tena kwa sababu juhudi nyingi za makusudi zimefanyika yapo mambo yanayoonekana yanaonekana na kamati imejionea.

“Sisi Wazaramo tuna msemo wetu “seeing is believing”, tukimaanisha kuwa kuona ni kuamini nilichokiona leo kwenye mgodi huu nadiriki kusema nimeona na nimeamini, na kwamba hata yale tuliyokuwa tunayasikia au kuyasoma ni tofauti sana na hiki tulicho kiona hapa,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Zaynabu Vulu.

”Hata mimi nilikuwa mmoja wa wabunge niliokuwa ninataka STAMICO ifutwe lakini leo hapa nafuta kauli yangu na kwamba nimeona na nimeamini kwamba nimeridhishwa na kuna mambo yanafanyika yenye tija,” alisema mjumbe Maftaha Nachuma.

Waziri wa Madini akiwa na watendaji wake wa STAMICO na STAMIGOLD aliwaeleza wajumbe wa kamati kuwa STAMICO ya miaka miwili iliyopita ni tofauti na STAMICO ya sasa na kuongeza, STAMICO ya sasa haizalishi madeni badala yake imekuwa ikilipa madeni, kuzalisha kwa faida na imefanikiwa kupunguza gharama za uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

Aidha, Biteko aliwaeleza wajumbe wa kamati kuhusu Changamoto mbalimbali zinazo isumbua STAMICO ni pamoja ya matumizi ya mafuta ya dizeli kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika mgodini hapo ambapo kwa mwezi wanatumia bilioni 1 wakati wangetumia umeme wa Tanesco  wangekuwa wakitumia umeme kwa gharama ya milioni 300 kwa mwezi na kwamba wangekuwa wanaokoa Tsh milioni 700 kila mwezi.

Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakichangia mjadala ulioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Dkt. Raphael Chegeni sehemu kubwa wameipongeza Wizara na STAMICO kwa mageuzi makubwa na kwamba kazi yao inatia moyo.

3. Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma wakiangalia bwawa linalohifadhi maji sumu (TFS) wakati wa ziara yao kwenye mgodi wa STAMIGOLD.

Hali hiyo ilipelekea wajumbe  kuiuliza STAMICO nini wanataka kamati hiyo iwasaidie ili kufikia malengo yao kama shirika kutokana na mipango yao waliyowaeleza wajumbe hao.

“Ndugu wajumbe kwanza nimefurahishwa kuona mgodi huu ukiendeshwa na watanzania wenyewe na kwamba hili linatia moyo na kujivunia kwamba tuna uwezo wa kuanzisha miradi mingine mikubwa na ikaendeshwa na watanzania wenye, hiki ni kielezo kikubwa, nawapongeza sana”, alisema Mwenyekiti wa Kamati.

Aidha, mwenyekiti wa kamati alisema ni ukweli kwamba Waziri wa Madini Doto Biteko anaitendea haki nafasi aliyopewa na kwamba kuwekuwa na mabadiliko makubwa yanayoonekana kutokana na utendaji wake na hivyo kamati inampongeza na iko tayari kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake huku pia akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwase.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link