Tarehe 24 Julai, 2019, saa 17:33 Mtandao wa Voanews ulichapisha taarifa yenye kichwa cha habari: Chinese Firms to Build Gold Smelter, Refineries in Tanzania, iliyoandikwa na Kampuni kubwa ya habari duniani ya Reuters.

Taarifa hiyo ilitaja chanzo cha habari kuwa ni hotuba ya Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko aliyoitoa tarehe 24 Julai, 2019 Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi ya kupokea na kukabidhiwa dhahabu ya Tanzania iliyokamatwa nchini Kenya.

Sehemu ya taarifa iliyochapishwa na mtandao huo kwa lugha ya Kiingereza kwa tafsiri ya Kiswahili ilimnukuu Waziri Biteko akieleza kwamba;

Tanzania imetoa leseni za ujenzi wa Mitambo ya uchenjuaji madini, moja ya kuchenjulia kwa njia ya kuyeyusha (Smelter) na ya pili ya Mitambo miwili ya kuchenjulia dhahabu kwa njia ya kusafisha (refinery) kwa makampuni ya China kama sehemu ya jitihada za serikali kukusanya mapato kupitia sekta ya madini.

<<Soma Zaidi>>