Tanzania inashiriki katika Mkutano wa  Mwaka kwa Nchi Wanachama wa KIMBERLEY PROCESSING SCHEME, unaofanyika nchini India.

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wapili kushoto), akiwa na Balozi wa Tanzania Nichini India Baraka Luvanda (katikati) pamoja na Maofisa wengine kutoka Tanzania

Ujumbe wa Tanzania  katika mkutano huo  unaongozwa na  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo.
Mkutano huo unahusu nchi wazalishaji wa Madini ya  Almasi  na udhibiti wa biashara ya almasi  duniani.
Aidha, ushiriki  wa Tanzania katika mkutano husika unalenga  katika  kupata uzoefu  kutoka nchi nyingine zinazofanya biashara ya Madini hayo.

Aidha, leo Novemba 20 2019, Naibu Waziri Nyongo ameutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo amekutana na Balozi   wa Tanzania nchini India,  Baraka Luvanda.

Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Kimberley Processeing Scheme wakiwa kwenye Mkutano Nchini India