Kumekuwepo na taarifa za upotoshaji mkubwa ambazo zilichapishwa na Kampuni ya
kuzalisha makaa ya mawe nchini TANCOAL kupitia tovuti ya www.miningreview.com
tarehe 03 Septemba, 2019 na kusambazwa kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Taarifa hizo zinadai kuwa Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kuitoza
TANCOAL tozo ya mrabaha kwenye gharama za usafirishaji wa makaa ya mawe
kutoka mgodini hadi kwa mtumiaji wa mwisho wa ndani na nje ya nchi. Taarifa hiyo
ikaendelea kudai kuwa, tozo ya mrabaha (asilimia tatu) na ada ya ukaguzi (asilimia
moja) inatakiwa kuanza kulipwa mara moja.

Taarifa hiyo ikaendelea kueleza kuwa kampuni ya TANCOAL imelazimishwa kuuza
makaa ya mawe kwa wateja wenye leseni za biashara ya madini hali itakayoongeza
gharama za makaa ya mawe.

Tume ya Madini inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:-

<<soma zaidi>>