Tumuunge Mkono Rais Magufuli Katika Kusimamia Rasilimali Madini

Tito Mselem na Steven Nyamiti, Geita

Watanzania watakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na namna alivyosimamia Sekta ya Madini na hivyo kupelekea Wadau katika Sekta hiyo kunufaika.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela alipotembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza jambo alipotembela Viwanja vya Maonyesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini mkoani Geita Septemba 18, 2020. (Kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel

Vile vile, Mongela amempongeza Rais Magufuli kwa maelekezo aliyoyatoa ya kuanzisha Masoko na kusimamia vizuri rasimali za madini nchini.

“Hatutakuwa tumetenda haki tusipompongeza Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuonesha uzalendo mkubwa katika usimamizi wake makini wa rasilimali hizi muhimu,” alisema Mongela.

Wakati huo huo, Mongela amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 28 Oktoba, 2020 ili kupiga kura na kuchagua viongozi bora watakao ongoza kwa uzalendo.

Inaelezwa kuwa, Mkoa wa Geita umekuwa ukishirikisha mikoa mingine hasa mikoa iliyopo kanda ya ziwa ili kuchangia mawazo ambayo yameweza kusaidia na kuifanya Geita kuwa Kitovu cha Uchumi katika Sekta ya Madini Nchini.

Pamoja na mambo mengine, Mongela amesema elimu haina mwisho hivyo Mkoa wa Mwanza umejifunza mambo mengi katika maonesho hayo na kuwapongeza Wadau wa madini kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika katika maonesho hayo.

“Watu wanasema elimu haina mwisho, hivyo mimi binafsi nimejifunza mambo mengi sana kupitia maonesho haya ambapo siku moja msishangae na sisi Mwanza tukaanzisha maonesho kama haya”, alisema Mongela.

Hivi sasa mapinduzi makubwa yanaonekana katika Sekta ya Madini ambapo mchango wake katika Pato la Taifa umeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza jambo na Kamishina Msaidizi wa Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wazawa katika Uchumi wa Madini (Local content) Terrence Ngole, alipotembelea banda la Wizara ya Madini Septemba 18,2020

“Wadau wote wa Madini wa Mkoa wa Mwanza nitawashauri waje wajionee maonesho haya ili wajifunze namna Mkoa wa Geita ulivyo fanikisha na kugeuka kuwa shule kwa Wadau wa Madini,” aliongeza Mongela.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amewataka wananchi wa Geita kuwa wazalendo na kushirikiana kwa pamoja ili kulinda rasilimali za madini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link