Ukuta wa Magufuli waandika historia mpya

  • Tanzanite zenye Uzito Mkubwa Zachimbwa
  • Mchimbaji Mdogo Laizer apata zaidi ya Bilioni 7

Asteria Muhozya na Tito Mselem, Mirerani

Hatimaye manufaa ya Ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 uliojengwa na Serikali kuzunguka Migodi ya Tanzanite Mirerani, umezidi kuzaa matunda baada ya kuandikwa Historia Mpya kutokana na kuzalishwa kwa Madini ya Tanzanite yenye Uzito Mkubwa kuwahi kutokea katika historia ya uchimbaji wa madini hayo nchini.

Madini hayo yaliyochimbwa na Mchimbaji Mdogo Saniniu Laizer yana Uzito Mkubwa wa jumla ya Kilogramu 14. 130, huku jiwe moja likiwa na uzito wa kilogramu 9.27 na la pili uzito wa kilogramu 5.108. Aidha, jiwe lenye uzito wa kilo 9.27 limetajwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 4.649,470 na jiwe lenye kilo 5.108 lina thamani ya shilingi bilioni 3.375,280 na hivyo yote mawili kuwa na thamani ya shilingi bilioni 7,744,152,703.82.

Kupatikana kwa Tanzanite hizo ambazo zimemfanya Laizer kuwa bilionea zimedhihirisha umadhubuti wa Serikali kuweka usimamizi imara wa kuyalinda madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee huku jitihada za kudhibiti utoroshaji wa madini hayo, ikiwemo manufaa ya Maboresho yaliyofanywa kwenye Sheria ya Madini na Serikali ya Awamu ya Tano yakionekana.

Aidha, kuzalishwa kwa madini hayo kupitia kwa mchimbaji mdogo kumedhihirisha namna ambavyo wachimbaji wadogo wanavyoweza kupata kipato kikubwa cha fedha halali kupitia sekta ya madini huhusan pindi wanapopatiwa fursa kama ambavyo serikali imekuwa  ikihakikisha wachimbaji wadogo wanarasimishwa na kuwekewa mazingira mazuri na bora ili kazi zao kuwa na tija na kufanya biashara ya madini kwa manufaa yao na serikali. Vilevile, dhamira ya serikali kutaka uchimbaji wa madini ya vito kufanywa na wazawa na  kama ambavyo Sheria inavyotaka pamoja na  dhamira ya Rais kutaka uchumi wa Madini urudi kwa Watanzania na kuwanufaishe wananchi wenyewe na taifa.

Akizungumza kwa njia ya simu wakati Serikali ikikakabidhiwa Madini hayo baada ya kuyanunua kutoka kwa Mchimbaji huyo, Rais Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alionesha furaha yake kutokana na kile ambacho kimefanywa na mchimbaji mdogo.  Alitoa pongezi kwa Waziri wa Madini Doto Biteko, mchimbaji huyo, wananchi wa Simajiro na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luogakwa kuhakikisha madini hayo yananunuliwa na Serikali na kusisitiza mchimbaji Laizer kutodhulumiwa hata shilingi. ‘‘nilikuwa naangalia hapa nawafuatilia, nimefurahi sana,’’ alisema Rais Magufuli.

Naye, Waziri wa Madini anaelezea ndoto ya Rais Magufuli ambayo wengi waliiona haiwezekani sasa imewezekana na tukio la Laizer kuzalisha madini ya uzito mkubwa ni kielelezo kwamba wachimbaji wanaweza na ndoto za Rais Magufuli kuhusu Sekta ya Madini zinatekelezeka na kuyaeleza madini hayo kuwa tangu yaanze kuchimbwa hapa nchini, tanzanite ya uzito huo haijawahi kuzalishwa.

“Ninawapongeza sana wananchi wa Simanjiro, mengi yalisemwa hawawezi na kwamba wanaoweza ni wageni tu, leo wametuvisha nguo. Tangu kuanza kuchimbwa kwa tanzanite, haijatokea ya uzito na ukubwa huu. Tumefanikiwa sana katika Sekta ya Madini mapato yameongezeka sana, mpaka leo tumekusanya shilingi Bilioni 520 sawa na asilimia 111,’’anasema Waziri Biteko.

Akijibu ombi la wachimbaji kupatiwa eneo la Kitalu C ili wachimbe kama ambavyo lilivyowasilishwa na Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Madini Tanzania, John Bina, Waziri Biteko anawataka wachimbaji kutovamia kitalu hicho wakati serikali ikiweka mazingira ya namna eneo hilo litakavyofanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa, Rais Magufuli ametengeneza mabilioni kutokana na namna anavyosimamia Sekta ya Madini na kuongeza kwamba, tangu uhuru tanzanite ya kiwango hicho haikuwa kuzalishwa nchini na kueleza kuwa, Serikali itamkabidhi mchimbaji Laizer fedha zake zote.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo anasema Serikali imepata kodi mbalimbali kupitia shughuli za uchimbaji madini unaofanywa na Laizer, huku katika kipindi chake cha uchimbaji akiwa amezalisha kilo 108.

‘’Naendelea kumhsukuru Rais Magufuli kutokana na namna maelekezo yake anayotupatia ya kusimamia sekta ya madini, Rais wetu ni Game changer na mimi huwa namwita kimoyomoyo, record breaker,’’ anasema Naibu Waziri.

Awali, akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Simajiro Mhandisi Zephania Chaula, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo alisema tanzanite hizo zimeonesha matunda ya udhibiti wa rasilimali madini unaofanywa na Rais Magufuli huku tangu kujengwa kwa ukuta huo mapato ya Tanzanite yameongezeka tofauti na ilivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri Biteko tanzanite hizo zimepatikana kwenye eneo la umbali wa  zaidi ya mita 1,800.

Tukio Serikali kukabidhiwa madini hayo lilfanyika tarehe 24 Juni, 2020 katika eneo la Mirerani ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya tanzanite, Wilayani Simanjiro , Mkoa wa Manyara.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link