Wachimbaji watakiwa kuongeza matumizi ya teknolojia

Asteria Muhozya, Boaz Mazigo na Greyson Mwase, Geita

Wachimbaji wa Madini nchini wametakiwa kuongeza matumizi ya Teknolojia katika shughuli zao ili kuwaongezea mapato ikiwemo kuachana na matumizi ya Zebaki.

Aidha, wametakiwa kuvitumia vituo vya Mfano vinavyojengwa na Wizara ya Madini maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vya Itumbi, Kantente na Lwamgasa ili kuwawezesha kupata elimu bora ya uchimbaji  wenye tija.

Hayo yalibainishwa Septemba 29, 2019 na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akifunga Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu.

Waziri Biteko ametaka maonesho hayo yaliyofanyika mkoani Geita kuwa chachu ya kutambua na kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini ikiwemo kuzitumia fursa zinazopatikana kwenye sekta husika.

Akizungumzia manufaa ya uwepo wa masoko nchini, amesema kwamba ni suala ambalo kama nchi ilichelewa kulitekeleza kutokana na matokeo makubwa ambayo yameonekana katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake na akaupongeza Mkoa wa Geita kutokana na kuwa mfano bora.

‘’ Kama kuna mtu wa kupongezwa katika hili ni Rais Dkt. John Magufuli. Uanzishwaji wa masoko ulikuwa wa kusuasua lakini baada ya kutoa agizo alipokuwa Mkoani Mbeya, lilitekelezwa katika maeneo mengi na mafanikio yake yanayonekana,’’ alisisitiza Biteko.

Aliongeza masoko ya madini yamekuwa ni mfano pekee duniani huku Tanzania ikitajwa kuwa kinara jambo ambalo linapelekea nchi nyingi kufika kujifunza na nyingine kutaka kujifunza nchini na hususan katika Soko la Geita na akatumi fursa hiyo kuwasisitiza wachimbaji na wadau wa madini kuendelea kuyatumia masoko hayo.

‘’Wana Geita tembeeni vifua mbele mna kiongozi mchapa kazi na anayesimamia vema rasilimali madini. Halmashauri wekeni mazingira mazuri kuwezesha masoko ya madini kufanya kazi zake vizuri,’’ amesema Biteko.

Pia, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu suala la udhibiti wa utoroshaji madini kwa kuwafichua wale wote wanaofanya vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Biteko alizungumzia manufaa ya mabadiliko ya Sheria na namna yalivyowezesha kuweka mazingira mazuri ya ajira katika migodi mikubwa ikiwemo Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) na kueleza kuwa, asilimia 97 ya wafanyakazi katika mgodi huo ni watanzania.

Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (Wanne kushoto) na Viongozi wa Chama Mkoa wa Geita wakijiandaa kutoa zawadi kwa Washindi wa Maonesho ya Uwekezaji Geita

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robart Gabriel amesema maonesho hayo yamekuwa na manufaa yakiwemo Mabenki yaliyoshiriki kuongeza idadi ya wateja, wachimbaji kupata mikopo, mawasiliano ya kibiashara na kampuni za kigeni kushiriki maonesho hayo hali ambayo inapelekea kuwepo mapinduzi ya kiuchumi.

Akizungumzia maandalizi ya maonesho mengine amesema tayari mkoa huo umetenga kiasi cha hekari 100 kwa ajili ya eneo Maalum la maonesho ambapo kwa mwaka ujao mkoa umejipanga kuandaa maonesho ngazi ya Kimataifa. Ufafanuzi huo unafuatia hoja iliyotolewa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ambaye ameutaka mkoa huo kutanua wigo wa maonesho hayo ili yafanyike katika ngazi ya kimataifa.

Akizungumzia hali ya uzalishaji katika masoko ya madini Mhandisi Gabrie amesema kuwa, mpaka kufikia tarehe ya 28 Septemba jioni, kilo 490 za dhahabu zilikuwa zimezalishwa katika soko la madini na kueleza kuwa, lengo ni kufikia kilo 500 ifikapo mwishoni mwa mwezi.

Kuhusu mipango ya baadaye ya kuendelea kuujenga mkoa wa Geita, amesema kuwa mkoa huo umelenga kuyatumia mapato yanayotokana na sekta ya madini kuhakikisha kuwa unaanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameendelea kusisitiza wachimbaji kujiandaa na kuachana na matumizi ya zebaki ifikapo mwaka 2024 kutokana nan chi kusaini Mkataba wa kuachana na matumizi ya Zebaki ifikapo mwaka 2030.

Amesema kwa kipindi hiki ambacho wachimbaji wanaendelea kutumia zebaki katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu wanapaswa kuzingatia matumizi sahihi na  na salama  yasiyokuwa na madhara wakati serikali ikiendelea kutafuta njia mbadala  katika shughuli hizo.

Pia, Naibu Waziri Nyongo amesisitiza kuhusu kutobugudhiwa kwa wachimbaji wanaopeleka madini yao katika masoko ya madini na kutaka vyombo vya ulinzi na usalama vinavyothibiti vitendo vya utoroshaji madini kutowabugudhi wale wote wanaotumia masoko hayo kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

Akizungumzia maeneo ya wachimbaji, amesema tayari wizara imekwisha tenga maeneo maalum kwa ajli ya wachimbaji wadogo wa madini na kueleza kuwa, wizara iko katika hatua ya kuyagawa maeneo hayo ambapo Wakuu wa Mikoa na Maafisa Madini watakuwa wahusika na wasimamizi wakuu katika kusimamia zoezi hilo.

Majibu hayo ya Naibu Waziri yanafuatia ombi lililotolwa na Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Geita (GEREMA) ambaye ameomba wachimbaji kupatiwa maeneo ya kuchimba.

Akisoma taarifa ya Maonesho hayo, MWenyekiti wa Kamati ya maandalizi Chacha Wambura amesema kuwa, yalishirikisha waoneshaji zaidi ya 280 ambapo pia yaliambatana na masuala mbalimbali yakiwemo makangamano ambapo wachimbaji na wadau wengine walipata fusa ya kuelimishwa.

Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yalikuwa na kaulimbiu ‘’Madini ni Chachu ya  Ukuaji wa Uchumi wa  Viwanda, Tuwekeze kwenye Teknolojia  Bora ya Uzalishaji  na Tuyatumie  Masoko ya Madini’’ yalianza tarehe 20 Septemba, 2019 na kufunguliwa rasmi tarehe 23, 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link