Wadau wa Madini Washauriwa Kuungana ili Kuzalisha Kwa Tija

Tito Mselem na Steven Nyamiti, Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko amewashauri Wadau wa Madini wa Mkoa wa Geita kuungana na kutengeneza Kampuni ya pamoja ili kuongeza tija katika shughuli zao.

Waziri wa Madini Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Madini alipotembelea katika Maonyesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Septemba 21,2020 Geita

Ushauri huo, ameutoa mara baada ya kutembelea Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.

Wakati huo huo, Waziri Biteko ametoa pongezi kwa waandaji wa Maonesho hayo ambayo mwaka huu zaidi ya kampuni 420 zinashiriki.

Vilevile, Waziri Biteko ametoa Wito kwa taasisi za Kibenki kuendelea kuwalea Wachimbaji Wadogo na Wafanyabiashara ya Madini kwa kuwapa mafunzo pamoja na mikopo ili wazalishe kwa faida.

Naye, Mkurugenzi wa Mikopo kwa Wajasiliamali Wadogo wa NBC Elibariki Masuke, amesema Benki ya NBC Mkoa wa Geita imetoa mkupo wa zaidi ya Shilingi bilioni 4.4 kwa Wadau wa Sekta ya Madini mkoani humo ili kuwaongezea uwezo katika shughuli zao.

Hayo aliyasema mbele ya Waziri Biteko alipotembelea banda la la benki ya NBC katika Maonesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Imeelezwa kuwa, wanufaika wa mikopo hiyo ni pamoja na Wachimbaji Wadogo, Wafanyabiashara ya Madini na Wachenjuaji wa Madini wa Mkoa wa Geita.

“Sisi kama Benki ya NBC tumeanza kutoa mafunzo kwa Wadau wa Madini hususan Wachimbaji Wadogo wa dhahabu na Wafanyabiashara ya dhahabu ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kuwekeza katika Sekta ya Madini”, alisema Masuke.

Waziri wa Madini Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni katika banda la benki ya CRDB alipotembelea katika Maonyesho ya Tatu ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Septemba 21, 2020 Geita

Pamoja na mambo mengine, Masuke amesema Banki ya NBC imekuwa Mdau Mkubwa kwenye Sekta ya Madini  ambapo mpaka sasa kuna taratibu zinawekwa sawa ili mikopo mikubwa zaidi ianze kutolewa kwa Wadau wa Sekta ya Madini kote nchini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link