Waziri Biteko Aipongeza FEMATA, Ataka Ushirikiano Zaidi

Tito Mselem- Tanga

Waziri wa Madini Doto Biteko amelipongeza Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji wa Madini Nchini (FEMATA) kutokana na namna linavyofanya kazi na kutaka ushirikiano zaidi ili Sekta ya Madini izidi kukua na kuheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Waziri Biteko aliyasema hayo wakati aliposhiriki katika Mkutano wa Sita (6) wa Shirikisho hilo uliofanyika Jijini Tanga Agosti 31, 2019.

Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akihutubia Mkutano wa 6 wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa Madini (FEMATA) uliofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort uliopo Jijini Tanga

ÔÇťTunaichukulia FEMATA kama nyenzo muhimu katika kuendeleza sekta ya uchimbaji mdogo nchini, hivyo basi naomba niwakumbushe na nitoe wito kwa viongozi na wawakilishi wa FEMATA kuwa, muda wowote muwe huru kutushirikisha katika kuandaa mipango yenu ili mwisho wa siku tuwe na mtazamo mmoja,ÔÇŁ alisema Waziri Biteko.

 Waziri Biteko aliongeza kwamba, ushirikiano wa FEMATA na Wizara ya Madini ni muhimu katika kuhakikisha ndoto ya Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli inafikiwa ya kuhakikisha wachimbaji wadogo wanawezeshwa ili waweze kukua na kuwa wachimbaji wa kati au wakubwa na hatimaye waweze kuongeza mchango kwenye pato la Taifa.

Aidha, Waziri Biteko aliwataka wanachama wa Shirikisho hilo kuwa na utaratibu wa kupitia masuala ya sheria za madini pomoja na kanuni zake ili wazifahamu vizuri.

ÔÇťNitafurahi sana kama kwenye mkutano huu mkipata wasaa wa kupitia Sheria ya Madini na Marekebisho yake, Kanuni za Madini, sheria mbalimbali za Kodi na pia masuala mbalimbali ya usimamizi kama vile masharti ya leseni zenu,ÔÇŁ alisema.

Pia, Waziri Biteko aliwataka wachimbaji wadogo kutoa ushirikano kwa Maafisa wa Wizara ya Madini pindi watakapoanza kutoa elimu kwa wachimbaji madini maeneo mbalimbali ya uchimbaji.

ÔÇťSisi kama Wizara, tutaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwawezesha wachimbaji wadogo kama vile kuwapatia maeneo ya kuchimba na muda sio mrefu Maafisa wangu kutoka Wizarani na Taasisi zake wataanza kutoa elimu mbalimbali kwa Wachimbaji wadogo naomba muwape ushirikiano,ÔÇŁ alisema Waziri Biteko.

Kwa upande wake, Rais wa FEMATA John Bina alimpongeza Waziri wa Madini kwa ushirikano mzuri anaowapa wachimbaji wadogo hususan katika suala la kuwarasimisha maeneo ya uchimbaji madini na kuwapatia elimu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchimbaji endelevu wa madini.

Pia, Bina alimpongeza Waziri Biteko kwa ujenzi wa Vituo vya Mfano ambavyo vitasaidia katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa kazi za uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo nchini.

Viongozi wa Mkutano wa FEMATA wakiwa katika maombi ya ufunguzi wa Mkutano

Mbali na wanachama wa FEMATA, viongozi mbalimbali walishiriki mkutano huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella, Rais wa FEMATA John Bina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji Haroun Kanega na wengine wengi.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link