Waziri Biteko Ataka Mialo Yote Kusajiliwa

Na.Steven Nyamiti, Nyarugusu Geita

Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wamiliki wote wa Mialo kuisajili ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi za Madini yaliyochenjuliwa na kudhibiti utoroshaji unaofanywa na watu wasio waaminifu.

Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza na Wachimbaji wa wadogo wa Nyarugusu Geita alipotembelea eneo hilo Desemba 31, 2020

Ameongeza kuwa, Wizara ya Madini imeanzisha utaratibu huo mpya wa kusajili Mialo ya kuoshea mchanga wa madini ya Dhahabu kupitia ofisi za Madini za Mikoa hivyo kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za madini yanayopatikana katika mualo husika.

Waziri Biteko ameyasema hayo leo Desemba 31, 2020 ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara ya kikazi Mkoani Geita ambapo ametembelea na kuzungumza na wachimbaji wadogo wa eneo la Nyarugusu.

Biteko amefafanua kuwa, utoroshaji mkubwa wa Dhahabu unafanyika zaidi kwenye Dhahabu inayozalishwa kwenye Mialo na kuwatakia wachimbaji kuacha tabia hiyo.

Aidha Biteko amewapongeza wachimbaji wa eneo hilo kwa kufuata taratibu zote za kufanya biashara ya madini na kusema “Serikali itawaunga mkono wachimbaji wa Nyarugusu, ninawapongeza sana Nyarugusu kwa kufuata utaratibu wa kuuza dhahabu.”

Ameongeza kuwa, Serikali inawathamini Wachimbaji wa Madini ndio maana imeweka utaratibu mzuri wa kusajili Mialo. “Raisi wetu ana nia njema na ninyi, anataka uchumi wa madini ubaki mikononi mwenu naomba mpendane. Alishauri Biteko.”

Katika hatua nyingine Waziri Biteko amepinga wauzaji wa dhahabu kuulizwa maswali ilikotoka dhahabu husika wanapofika sokoni na badala yake ipimwe uzito na kufanyiwa mahesabu na sio kuuliza ilikotoka.

Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa Mkoa wa Geita, mpaka sasa kwa Mkoa wa Geita pekee imesajili Mialo 800 na 300 tayari imesajiliwa kwa eneo la Nyarugusu.

Akikazia juu ya agizo hilo, Biteko amesema Serikali itawachukulia hatua Kali wote watakao kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa na Wizara ya Madini hususani kwenye uendeshaji wa Mialo.

Picha ya Mchimbaji mdogo wa Madini akiendelea na shughuli katika eneo la Mialo la Nyarugusu Geita panapofanyika shughuli za Uchimbaji Madini Desemba 31,2020

“Kuna utaratibu tunauandaa hata mawe wanunue watu wenye Mialo iliyosajiliwa.

Katika ziara hiyo Waziri Biteko aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Fadhil Juma, Mbunge wa Jimbo la Busanda Tumaini Magesa, Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Geita na Wadau wengine wa Sekta ya Madini.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link