Waziri wa madini akabidhiwa jengo la kituo cha umahiri Kagera

Na Tito Mselem, Kagera

Waziri wa Madini Doto Biteko amekabidhiwa jengo la ghorofa tatu lenye thamani ya shilingi bilioni 1.81 ambalo litatumika kama Kituo cha Umahiri mkoani Kagera.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya jengo hilo, Waziri Biteko ameipongeza SUMA JKT kwa kazi nzuri iliyofanywa ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamilika ndani ya muda uliopangwa.

Baada ya makabidhiano, Waziri Biteko amelikabidhi jengo hilo kwa Tume ya Madini na kuwataka litunzwe   ili lisaidie kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wachimbaji wadogo ili wachimbe kwa tija.

Jengo la umahiri lililojengwa na SUMA JKT na kukabidhiwa kwa Waziri wa Madini Doto Biteko

“Lengo kuu la kujenga kituo hiki cha umahiri hapa Kagera ni kuwasaidia wachimbaji wa madini kupata elimu ya namna bora ya kufanya utafiti wa madini, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani wa madini na kuyajua masoko. Hivyo, nitoe wito kwa wachimbaji wote kukitumia kituo hiki ili kuongeza tija katika uzalishaji na wakuze kipato chao,” aliongeza Biteko.

Pia, kituo hicho kinatarajiwa kutoa huduma  nyingine zikiwemo  za upimaji wa madini, kuhifadhi madini na kutoa huduma za uombaji wa leseni kupitia mfumo wa Tume ya Madini.

Aidha, Waziri Biteko amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti kuhakisha sekta ya madini inasimamiwa vizuri mkoani humo ili iwanufaishe wananchi na kutaka Kagera iwe moja kati ya Mikoa inayo changia pato kubwa la nchi kupitia sekta ya madini.

Katika hafla hiyo, Waziri Biteko amesisitiza kwa mikoa iliyoko mipakani kuondoa vikwazo kwa wasafirishaji wa madini ambao wanasafirisha sampuli za madini kutoka nchi nyingine na kuleta katika maabara zilizopo nchini.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatamani tupate cheti cha kusafirisha Tin hata leo ili tuanze kusafirisha madini hayo nje ya nchi maana tumechelewa, pia, Rais wetu anatamani uchumi wa madini umilikiwe na watanzania wenyewe”, alisema Biteko.

Hata hivyo, Waziri Biteko amesema Wizara ya Madini ikishirikiana na Tume ya Madini imefuta zaidi ya leseni 12,000 za uchimbaji mdogo ambazo haziendelezwi kati ya hizo 156 ni za  Mkoa wa Kagera,  na kueleza zitatolewa kwa wenye nia ya dhati ya kuchimba.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Marco Gaguti aliahidi kutekeleza maagizo ya Waziri Biteko na kuitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kagera kuimalisha ulinzi hususan maeneo ya mipakani ili kuepusha utoroshwaji wa madini nchini.

Meneja wa SUMA JKT wa Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa akielezea namna bora ya matumizi ya jengo hilo mbele ya Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti na Katibu Tawala wa Mkoa wa kagera Profesa Faustin Kamzora

“Kagera imeanza kuonesha mafanikio mazuri kwenye sekta ya madini tofauti na kipindi cha nyuma ambapo tulikuwa tunapata maduhuli kiasi cha shilingi milioni 70 kwa mwaka na sasa tunakusanya zaidi ya bilioni 2.7, hayo ni mafanikio makubwa na tutaendelea kuimalisha usimamizi ili madini yaongeze pato kwa nchi na kuleta tija kwa wachimbaji wadogo,” alisema Gaguti.

Gaguti aliongeza kuwa,  mkoa huo una  changamoto ya mitaji kwa wachimbaji wadogo ambao hawana uwezo wa kutosha kwenye uzalishaji wa madini ya Tin, ambapo wanazalisha tani 3 mpaka 4 kwa mwezi na kueleza kuwa, kuna uwezekano wa kuchimba tani 20 kwa mwezi.

“katika maonesha ya teknolojia ya madini yaliyofanyika Mkoani Geita, nilipata fursa ya kuongea na wadau mbalimbali wa madini na kuahidiwa kusaidiwa kupata elimu na upatikanaji wa mitataji kwa wachimbaji wetu ili waongeze uzalishaji,” alisema Gaguti.

Kituo cha Umahiri Kagera ni moja kati ya Vituo 7 vya Umahiri pamoja na Jengo la Taaluma la Chuo cha Madini Dodoma vinajengwa katika mikoa mbalimbali nchini kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP). Vituo hivyo vilivyojengwa na SUMA JKT, vimegharimu kiasi cha shilingi Bil 11.9 ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Maeneo mengine ambayo vituo hivyo vimejengwa na vingine vikiendelea kukamilishwa ni pamoja na Handeni- Tanga, Bariadi –Simiyu, Chunya- Mbeya, Mpanda- Katavi, Songea na Mara.

Aidha, sehemu ya Jengo la Taaluma la Chuo Cha Madini (MRI) inatarajiwa kutumiwa na Wanawake wachimbaji ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha kupata mafunzo ya uchimbaji kama ilivyo kwa vituo vingine.

 

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Français Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film érotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno caché Porno de qualité HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secrétaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vidéo Amateur Vidéo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link