Wizara ya Madini Yatoa Mafunzo Elekezi kwa Waajiriwa Wapya

Na Issa Mtuwa – Dodoma

Wizara ya Madini, imeandaa na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi walioajiliwa hivi karibuni kwenye Utumishi wa Umma kwa ajili ya kuwafahamisha kuhusu namna Serikali na Wizara ya Madini inavyotekeleza majukumu yake.

Picha ya pamoja kwa Viongozi wa Idara na Vitengo pamoja na Watumishi wapya kwenye Mafunzo Elekezi iliyofanyika Septemba 23 Mji wa Kiserikali Wizara ya Madini Mtumba

 Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Idara ya Utawala na Rasilimali Watu yanafanyika na kutolewa na wataalam mbalimbali kutoka ndani ya Wizara, Chuo cha Utumishi Umma na Ofisi ya Usalama Serikali (GSO) kuanzia leo tarehe 23 Septemba hadi tarehe 25 Septemba, 2020. 

Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu, Issa Nchasi amesema mafunzo yanayotolewa  ni muhimu kwa watumishi hao ili waelewe namna ya kutekeleza majukumu yao kama watumishi wa Umma .

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mwenyikiti wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Raslimali watu Wizara ya Madini Kabigi Nsajigwa, amesema serikalini kuna mambo mengi, hivyo ni vyema wayafahamu kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.

Ameongeza kuwa, katika mafunzo hayo wafanyakazi hao watafamishwa kuhusu majukumu ya wizara kupitia mada zitakazo tolewa na wakuu wa idara na vitengo, maadili ya utumishi wa umma, na namna ya kuwahudumia wateja, na masuala ya kuzingatia  katika kutunza siri na utii kazini.

Idara na vitengo vya wizara vilivyowasilisha mada juu ya majukumu yao ni; Idara ya Sera na Mipango,Idara ya Madini, Idara ya Rasilimali Watu na Utawala,  Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Mawasilino Serikali, Kitengo cha Huduma  za Sheria, Kitengo cha TEHAMA, Idara ya Fedha na Kitengo cha Manunuzi.

Kwa upande wake, Kamishna wa Madini (Idara ya Madini), Mha. David Mulabwa, amesema majukumu yake ni mengi na ametaja moja wapo kuwa ni; Kutoa mchango katika kuanda na kupitia sera, mikakati na sheria kuhusiana namasuala ya utafutaji na uchimbaji wa madini na kufuatilia utekelezaji wake.

 Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Martius Abisai alisema kitengo chake kinajukumu la kumshauri Afisa Masuhuli kuhusu: Udhibiti wa mifumo ya ndani ya Wizara na matumizi bora ya raslimali za Wizara ya Madini.

Mkuu wa Ktengo cha Mawasilino Serikali, Asteria Muhozya amesema kitengo chake kina jukumu kubwa la kuhakikisha inakuwa daraja baina ya Wizara na wadau wa ndani na nje wa wizara ikienda sambamba na utoaji wa taarifa na elimu juu ya sheria, sera, kanuni mbalimbali zinazosimamia sekta pamoja na kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali yanayofanywa na wizara ili umma wa watanzania ujue.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Augustine Olal, amesema idara yake inaratibu kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na  kusimamia masuala ya sera inayosimamia Sekta ya Madini kuratibu na kusimamia maandalizi ya bajeti ya wizara.

Picha ya pamoja kwa Viongozi wa Idara na Vitengo walioshiriki Mafunzo kwa watumishi wapya iliyofanyika Septemba 23 Mji wa Kiserikali Wizara ya Madini Mtumba

Amesema, uandaji wa sera hutegemea mahitaji ya wakati uliopo ambapo serikali ikibaini mapungufu kwenye sera iliyopo idara hiyo itahusika katika kuboresha na kuzalisha sera sera mpya.

Wafanyakazi wapya na waliohamia ni; Steven Nyamiti, kitengo cha Mawasiliano,  Dohaha Yanda, Iddi Shebila, Selemani Malunde, Desdelius Kalinda, Primatus John na Emanuel Dato wote wa idara ya Utawala na Nickson Emmanuel kitengo cha Uhasibu TGC Arusha.

About the Author

You may also like these

gaziantep escort
Porno Gratuit Porno Fran├žais Adulte XXX Brazzers Porn College Girls Film ├ęrotique Hard Porn Inceste Famille Porno Japonais Asiatique Jeunes Filles Porno Latin Brown Femmes Porn Mobile Porn Russe Porn Stars Porno Arabe Turc Porno cach├ę Porno de qualit├ę HD Porno Gratuit Porno Mature de Milf Porno Noir Regarder Porn Relations Lesbiennes Secr├ętaire de Bureau Porn Sexe en Groupe Sexe Gay Sexe Oral Vid├ęo Amateur Vid├ęo Anal

porno Seks hikayeleri Seks hikayeleri porno izle dubai escorts bordell berlin short link