Tarehe : Sept. 4, 2024
Uongezaji thamani madini ni miongoni mwa kipaumbele kikubwa kwa Wizara ya Madini na Sera yetu ya Madini ya Mwaka 2009 na Sheria ya Madini imeelekeza kuhakikisha madini yanaongezwa thamani ndani ya nchi ili kuongeza manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Mnyororo wa uongezaji thamani madini unafaidisha watu wengi ndani ya nchi ikiwa ni pamoja na kutoa ajira, kukuza teknolojia na kuongeza mapato kwa Serikali. Mikakati tuliyonayo ni kuhakikisha tunakuwa na wataalamu wabobezi ndani ya nchi wanaoendana na teknolojia za kisasa za uongezaji thamani madini na pia kuendelea kufanya mabadiliko ya Sheria ili kuzuia usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi. Kwa sasa tumeanza na madini mkakati ambapo maelekezo ya Serikali ni kuhakisha leseni kubwa za uchimbaji madini mkakati zinazotolewa zitazingatia kuhakikisha madini hayo yanaongezewa thamani ndani ya nchi. Hivyo, niwapongeze tena TWiMMI kwa kuandaa mafunzo yanayoendana na Sera yetu ya Madini na malengo ya Serikali yetu.
by: madini
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshiriki Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Madini Afrika …
by: madini on: Oct. 7, 2022, 11:20 a.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
The Ministry of Minerals informs the public and mining sector stakeholders that Tanzania, in collab…
by: madini on: Jan. 24, 2024, 7:59 p.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.