[Latest Updates]: Sekta ya Madini imepiga hatua kubwa - Dkt. Kiruswa

Tarehe : April 30, 2025, 7:40 p.m.
left

- Aipa Tano Tume ya Madini ukusanyaji maduhuli

NAIBU Waziri wa Madini, Mhe.  Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa, chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Sekta ya Madini imepiga hatua kubwa.

Dkt. Kiruswa ameyasema hayo leo Aprili 30, 2025 wakati akifunga Kikao cha Manejimenti ya Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma.

Amesema, kutokana na usimamizi mzuri wa Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mbibo mafanikio makubwa yamepatikana katika Sekta ya Madini yaliyopelekea mchango wake kufikia asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa.

Katika hatua nyingine, amewapongeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kwa kasi ya ukusanyaji wa maduhuli na kuwataka kuimarisha ushirikiano kati yao na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika Sekta ya Madini na kutatua kero za wadau wa madini. 

"Nitumie nafasi hii kuwakumbusha  umuhimu wa kushirikiana kutekeleza mikakati ya Usimamizi wa Sekta ya Madini ili sote kwa pamoja tuweze kufurahia ushindi wa kufikia malengo tuliyojiwekea,"amesema Dkt. Kiruswa na kuongeza,

*Nitoe rai kwenu kuongeza ushirikiano, mshikamano na upendo katika utendaji wa kazi ili tujenge nguzo imara itakayoendelea kutoa matokeo bora kwa Wizara yetu na kwa manufaa ya Taifa letu," amesema.

Aidha, amewapongeza Menejimenti na Watumishi wa Tume kwa juhudi za ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025  ambapo kuanzia kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Aprili 29, 2025 Tume imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 862.64 ikiwa ni asilimia  86.53 ya lengo la mwaka 2024/2025.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals