[Latest Updates]: Kilogramu 6.93 za Dhahabu Zakamatwa Zikitoroshwa Chunya

Tarehe : Oct. 28, 2023, 5:54 p.m.
left

# Yenye thamani ya shilingi milioni 961 za kitanzania

# Takribani leseni 964 za wachimbaji wadogo zinafanya kazi

# Wastani wa Kg 250 za dhahabu uzalishwa kwa mwezi wilayani Chunya

Na.Wizara ya Madini - Chunya.

Madini yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 961 yenye  uzito wa kilogramu 6.93  yakamatwa wilaya ya Chunya , Mkoani Mbeya  yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 28, 2023 na  Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde  akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya katika machimbo ya dhahabu wilayani Chunya.

 Mhe.Mavunde amesema dhahabu iliyokamatwa ina thamani zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 961ambapo kama ingetoroshwa Serikali ingekosa mapato ya zaidi mioni 60 .

Akizungumza na wafanyabiashara wa Madini katika soko la madini Mbeya Mhe.Mavunde amewataka  wafanyabiara wote wa madini kutojihusisha na njama zozote za utoroshaji madini kwani kufanya hivyo kunakosesha mapato  nchini na kudumaza juhudi za kuleta maendeleo.

Aidha, Mhe .Mavunde amefafanua  kuwa Serikali kupitia Wizara ya  Madini ina mikakati mbalimbali ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa  madini  nchini kwa kuwapatia mitambo ya  uchorongaji , kuwajengea mazingira wezeshi ya kupata mikopo  yenye riba nafuu pamoja na kufanya utafiti wa kina ili kufanya uchimbaji bila kubahatisha.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka Mayeka amesema kuwa mazingira ya uchimbaji madini wilayani Chunya yanaendelea kuhimarishwa hisipokuwa changamoto kubwa ni utoroshaji madini na wizi wa Carbon katika mialo ya uchenjuaji madini.

Awali, akitoa taarifa kuhusu Sekta ya Madini Wilayani Chunya , Afisa Madini Mkazi Sabahi Nyansiri amesema mpaka sasa vituo vidogo 24 vya ununuzi wa dhahabu vimefunguliwa ili kusogeza huduma ya ununuzi na uuzaji kwa wachimbaji wadogo wasio na uwezo wa kufika katika soko kuu pamoja na wale wenye kiasi kidogo cha dhahabu.

Akielezea kuhusu mikakati  kuwaendeleza wachimbaji wadogo Chunya Sabahi ameeleza kuwa kwasasa wapo na mkakati wa kurasimisha na kuboresha mfumo mzima wa uchimbaji mdogo kwa kuwatengea maeneo ya uchimbaji mdogo katika maeneo ya Godima , Isenyela na Itumbi.

Mkakati mwingine ni kufanya utafiti wa kijiolojia wa kuonesha mashapo ya miamba katika maeneo ya Itumbi, Mbigwa, Godima na Isenyela.

Katika ziara hiyo Mhe.Mavunde amekagua machimbo ya wachimbaji wadogo wa  Itumbi na kufanya  mkutano kwa lengo la  kujua  changamoto zinazowakabili.

Mnamo Oktoba 26 , 2023 ilitolewa taarifa kuhusu  kukamatwa kwa kilogramu 6.93 za madini ya dhahabu yakisafirishwa kuuzwa nje ya nchi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals