[Latest Updates]: Tanzania Yaanza Maandalizi Ushiriki Mining Indaba 2024

Tarehe : Oct. 8, 2023, 9:17 a.m.
left

Dar Es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Madini  kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta ya Madini imeanza maandalizi ya kushiriki Maonesho Makubwa ya Madini Barani Afrika ya Mining Indaba.

Maonesho hayo yatakayofanyika mwezi Februari 2024,  katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini yatashirikisha wafanyabiashara, watoa huduma, taasisi mbalimbali za kisekta pamoja na wakuu wa kampuni kubwa za  uchimbaji madini duniani.

Akizungumza wakati akiwasilisha mpango wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo kwa Waziri wa Madini kwa  niaba ya Sekretarieti ya maandalizi, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi Mhandisi Philbert Rweyemamu amesema ni moja ya maonesho 
ambayo huwakutanisha  wawekezaji wapatao angalau 900, taasisi za sekta zipatazo angalau 40 na watendaji wa kampuni wapato 1000.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema ushiriki watanzania Katika Maonesho hayo unatarajia kuiweka Tanzania kwenye ramani ya Afrika na dunia nzima huku ukileta sauti moja kwa wadau kuielewa Tanzania. 

Kwa upande wake, Katibu  Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesema dhamira ya Wizara  ni kuweka ushiriki wa pamoja katika banda moja la wizara, taasisi na wadau ili kufanya ushiriki wenye tija zaidi kwa Tanzania .

Tanzania inatarajia kutumia maonesho ya Mining Indaba kuvutia mitaji, uwekezaji, kujifunza, kuleta teknolojia bora za uchimbaji, kujenga mahusiano ya kibiashara, kuimarisha ushirikiano pamoja na mambo mengine. 

Kampuni zinazotarajia kudhamini ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo ni pamoja na Anglo Gold Ashanti, Barrick Gold, Shanta Gold, Mantra Tanzania, Tembo Nickel, TRX Gold, Petra Diamond na City Engineering Ltd.
 
#TanzaniaItakuwepo#
#MiningIndaba2024#

 VISION 2030: Madini ni Maisha na Utajiri

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals