[Latest Updates]: Michezo yaleta Mshikamano na Afya kwa Watumishi Madini

Tarehe : Oct. 20, 2025, 2:06 p.m.
left

Wizara ya Madini leo Oktoba 18, 2025, imeshiriki Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin jijini Dodoma, likiwakutanisha watumishi kutoka taasisi zote za Wizara. Bonanza hilo limekuwa sehemu ya utaratibu wa kila robo mwaka ulioanzishwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, kwa lengo la kujenga mshikamano, afya bora, na kuimarisha ari ya watumishi kuweza kuitumikia Serikali ipasavyo.

Akizungumza katika bonanza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba amesema michezo ni nguzo muhimu ya kuimarisha umoja, afya za watumishi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza  ili  waweze  kuishi maisha marefu na hatimaye  kuongeza ufanisi kazini na kutimiza malengo  iliyowekewa Wizara na Serikali.

Aidha, amewahimiza watumishi wote kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura ili, kuchagua viongozi bora wenye dira ya kuweza kuisimamia  Sekta ya Madini kwa maendeleo ya sekta na  maendeleo kwa taifa kwa ujumla kwa kusikiliza sera na kuwahamasisha wengine na hatimaye kuwachagua viongozi wanaofaa.

 Pia, amezitaka taasisi zote chini ya wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa tija na matokeo, ili kuiheshimisha Sekta mbele ya watanzania na jumuiya ya kimataifa, kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa ushauri, tafiti na mitambo na  kuendelea kuhamasiaha uwekezaji nchini kwa kutoa taarifa za uwazi na uwajibikaji kwa kampuni za madini.

‘’Niendelee kuwapongeza sana taasisi zote, Tume ya madini kuendelea kutuheshimisha kwenye makusanyo, STAMICO kuendelea kuwaelea wachimbaji wadogo, kuwapata ushauri na mitambo na kuwa nao karibu, GST kuendelea kuwasaidia wachimbaji wakubwa,  wa kati   na wadogo kwenye masuala ya kijiolojia, TEITI kuendelea kutoa taarifa kwa uwazi kwenye sekta ya Madini ili wananchi wafahamu mwelekeo na imechangia kitu gani na kikubwa zaidi  kuwavutia wawekezaji kuhusu wazi na usimamizi wa  rasilimali madini,’’ amesema Eng. Samamba.

Bonanza hilo limehusisha taasisi zifuatazo; Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST),  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI)

Aidha, limehusisha jogging ya pamoja, michezo ya mbio za mita 100 kwa wanaume na wanawake, mpira wa miguu ambapo timu ya Tume ya Madini na STAMICO zimeifunga  timu ya Wizara na GST kwa magoli 4-1, mpira wapete kwa timu ya GST na TEITI zimeishinda timu ya Wizara  na STAMICO kwa vikapu 17-14,  mchezo wa kamba wanawake imeshinda timu ya Wizara .

Michezo mengine imehusisha kukimbia na mayai kwa wanawake na wanaume na mpira wa kikapu.  Katika michezo hiyo, Eng. Samamba ametoa medali na makombe kwa timu zilizoshinda pamoja na mshindi mmoja mmoja. Aidha, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janeth Lekashingo ametoa kikombe maalum kwa mchezaji bora Eng. Samamba ikiwa ni maalum kutokana na kuhamasisha michezo kwa watumishi wa wizara na taasisi kushiriki katika michezo.

Akizungumza Dkt. Lekashingo amesema,’’ tunakushuru Katibu Mkuu kwa kuendelea kuhamasisha michezo miongoni mwa watumishi wawizara, na hili linatupa ushindi katika nyanja zote.

"Ndugu mgeni rasmi tumeanza bonaza hili saa 12 asubuhi kwa Jogging ya pamoja ikiwa ni ishara ya kuamsha miili na kuongeza ari ya michezo,’’ amesema Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Bi. Beatrice Matemu.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Features Images
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals