[Latest Updates]: Geita Kinara Uzalishaji Dhahabu

Tarehe : Sept. 27, 2023, 8:10 a.m.
left

• 2017- 2023  Kiasi cha kilogram 111,533.93 zimezalishwa

• Leseni 803 za uchimbaji mdogo zatolewa

Mkoa wa Geita umetajwa kuwa  kinara wa uzalishaji wa Madini ya dhahabu yanayochimbwa maeneo mbalimbali katika mikoa ya kimadini ambayo Madini mkoa wa Geita na Madini Mbogwe ikilinganishwa na mikoa mingine.

Hayo yamesemwa Septemba 26, 2023 na Kaimu Mkuu wa Geita Grace Kingalame ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale wakati akihairisha semina kuhusu fursa za kijamii na kiuchumi zinazopatikana mkoani Geita.

Akizungumza kuhusu  shughuli za Madini zinazofanyika katika Mkoa wa Geita , Kingalame alisema shughuli za Madini zimegawanyika katika makundi manne ambayo ni Utafiti wa Madini, Uchimbaji, Uchenjuaji na uuzaji yaani biashara za Madini.

Mkoa wa Geita  kwasasa una leseni mbalimbali  zikiwemo  leseni kubwa 2 za uchimbaji, leseni za utafiti 127, leseni za uchimbaji mdogo 803, uchimbaji wa kati 8 , leseni za biashara kubwa (Dealers) 47 na biashara ndogo  (Brokers) leseni 33, leseni za uchakataji 33 na mitambo ya kuchenjulia madini leseni 265.

Takwimu za uzalishaji wa dhahabu kutoka Tume ya Madini mkoani Geita  zinaonesha kuanzia mwaka 2017 mpaka 2023 kiasi cha kilogram 111,585.56 zimezalishwa.

Kwa kipindi cha miaka saba mwenendo wa uzalishaji wa madini ya dhahabu ulikuwa kama ifuatavyo mwaka  2017/18 kiasi cha kilogram 18,483, 2018/19 20,008 kg, 2019/20 14,251.65 kg , 2020/21 23,931.33 kg.

Aidha, mwaka 2021/2022 kiasi cha   kilogram 16,274.12 zilizalishwa  na mwaka 2022 /23  kilogram 18,585.56 zilizalishwa.

Mkoa wa Geita una migodi mikubwa miwili ambayo ni Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na Mgodi wa Buckreef .

Mkoa wa Geita una wilaya tano ambazo ni Wilaya ya Geita , Bukombe, Mbogwe, Nyang'wale na Chato.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals