Tarehe : Nov. 26, 2018, 9:23 a.m.
Na Rhoda James, Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko ameutaka Mgodi wa MMC kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vya Mtukule na Mangae Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro waliopisha mgodi huo kufanya shughuli za uchimbaji lakini hawakuwahi kulipwa fidia zao.
Wafanyakazi wa Mgodi wa MMC wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) wakati alipofanya kikao kati yao ili kujua utendaji kazi wao katika mgodi wa MMC uliopo mkoani Morogoro.[/caption]
Naibu Waziri Doto Biteko alitoa agizo hilo Desemba 10, 2018 alipotembelea Mgodi wa MMC kwa lengo la kukagua shughuli zinazoendelea mgodini hapo pamoja na kwamba mgodi husika uliagizwa kusimamisha shughuli hizo hadi hapo utakapowalipa fidia wananchi wanaodai haki zao.
Biteko alieleza kuwa, tangu Mgodi huu uanze kazi umekuwa ukiendelea na shughuli za uchimbaji pasipo kuwalipa fidia wananchi wanaouzunguka na hivyo, kuuagiza kuwalipa kwanza wananchi ndipo uendelee na shughuli zake.
“Lipeni kwanza fidia na kama uwekezaji wenu ni halali mtaendelea. MMC hakikisheni wananchi wote wanalipwa haki zao na siyo shilingi Laki Tano niliyoambiwa kwamba wamelipwa,” alisisitiza Biteko.
Vilevile, Naibu Waziri Biteko alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally kufanya uchambuzi ili kujua wananchi wenye haki ya kulipwa ikiwemo kujua ikiwa ardhi hiyo inamilikiwa na wananchi hao ama mgodi, kujua kiasi cha fidia ambacho kila mmoja anatakiwa kulipwa. “Kama uwekezaji ni wa haki, wananchi wapishe uwekezaji huo,” aliongeza Biteko.
Aliongeza kuwa, maendeleo hayawezi kupatikana ikiwa mgodi na wananchi hawaelewani na hivyo kutoa wito kwa wawekezaji kupitia hatua mbalimbali kabla ya kuwekeza ikiwemo kujitambulisha katika ngazi za Serikali ya Kijiji hadi ya Wilaya.
“Na ili Mgodi upate adhabu ni lazima shughuli zake za uchimbaji zisimame hadi hapo watakapokuwa wamewalipa wananchi fidia yao, alisema Naibu Madini Biteko.
Pia, alimtaka Mkuu huyo wa Wilaya kushirikiana na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Tanzania (TARURA) kulifanyia kazi tatizo la barabara linalowakabili wananchi hao kufuatia hatua ya mgodi huo kubadili matumizi ya barabara iliyokuwa ikitumiwa awali na wananchi hao. Tunataka tuondoe ubabaishaji na uongouongo kwenye Sekta ya Madini,” aliongeza
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally (kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko wakikagua uwekezaji uliofanywa na Mgodi wa MMC mkoani Morogoro.[/caption]
Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Madini Biteko ametoa wito kwa Watanzania wote hususan wachimbaji wadogo kuhakikisha kuwa Serikali inatambua mikataba yao wanayoingia na wawekezaji
Biteko alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa watanzania hawanyonywi na vile vile wawekezaji hawaingii mikataba ambayo sio sahihi jambo litasaidia serikali kutolaumiwa.
“Sisi watanzania tusiwaingize wawekezaji kwenye migogoro. Madhara yanasababisha nchi ya Tanzania kuonekana kwamba inawanyanyasa wawekezaji.Fuateni sheria zilizopo,” alisema Biteko.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mwalimu Mohamed Utally alihaidi kuwa atayafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa atayasimamia kuhakikisha kuwa kila mwananchi analipwa haki yake.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.