[Latest Updates]: Waziri Mavunde Aongoza Kikao Kutatua Mgogoro Mgodi Ililika - Nyarugusu

Tarehe : Feb. 20, 2026, 10:45 a.m.
left

 Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Februari 20, 2026 ameongoza kikao cha kutatua Mgogoro kati ya Wachimbaji Wadogo wa duara No 15 na Uongozi wa Mgodi wa ILILIKA uliopo Nyarugusu Mkoani Geita. 

Baada ya kusikiliza pande zote mbili kupitia wawakilishi wao, Waziri Mavunde  amesema ili kufikia muafaka wa mgogoro huo na kuhakikisha haki inapatikana, ameelekeza kupimwa kwa sampuli ya mawe yanayolalamikiwa na pia kutaka uwepo wa mashahidi wengi zaidi wa pande zote ili kupata taarifa sahihi kisha kuendeleza kikao hicho ili haki ipatikane pale inapostahili.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhan Lwamo, Afisa Madini Mkazi Geita Mkoa Wa Geita  Samweli Shoo,  Msimamizi wa Mgodi wa Ililika Bi. Salma Mipawa pamoja na wachimbaji waki wakilishwa na Bw. Geofrey Mushi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals