[Latest Updates]: Serikali Kujenga Maabara ya Kisasa ya Upimaji wa Sampuli za Madini Nchini

Tarehe : April 25, 2024, 11:52 a.m.
left

Waziri Mavunde aitaka GST kuwa sehemu ya kwanza ya taarifa sahihi za maabara

Maabara kuwekwa vifaa na mitambo ya kisasa

Watumishi GST kujengewa uwezo zaidi

Maabara za Kanda kujengwa ili kusogeza huduma karibu kwa wachimbaji

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema  kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluh Hassan imejipanga katika mwaka wa Fedha 2024/25 kuanza ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa na yenye vifaa vya kisasa itakayojengwa katika eneo la Kizota jijini Dodoma ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Sekta ya Madini nchini na matarajio ya wadau kwa ujumla.

Ujenzi huo wa maabara kubwa na ya kisasa utakwenda sambamba na ujenzi wa maabara za kanda na kuwajengea uwezo watumishi wa GST ili kuendana na kasi kubwa ya maendeleo ya Teknolojia duniani.

Mhe. Mavunde aliyasema hayo jana Aprili 24, 2024 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja cha kujadili namna bora ya utendaji kazi kilichowakutanisha  Watumishi wote wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

“Jukumu letu la kimsingi ni kuhakikisha kwamba taasisi hii inatoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya madini hapa nchini Tanzania.

Aliongeza kwamba, taarifa za maabara kutoka GST zinapaswa kuwa za uhakika na sahihi kwa wachimbaji jukumu ambalo kama  ambalo kama serikali haliwezi kulikwepa.

*Tumedhamiria kuhakikisha tunajenga maabara kubwa, ya kisasa na tegemeo katika utoaji wa huduma ndani na nje ya mipaka Tanzania,"alisema Mavunde.

Pia, Waziri Mavunde aliongeza kuwa  GST ina mchango mkubwa katika ukuaji wa Sekta ya Madini huku akisisitiza kwamba GST ni Moyo wa Sekta ya Madini nchini, kutokana na umuhimu huo Serikali imeendelea kuiwezesha zaidi GST ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi unaotarajiwa.

Mavunde alitumia fursa hiyo kuwataka watumishi wote kujituma na kufanya kazi kwa weledi katika kutekeleza majukumu ya GST na kusisitiza kwamba hatakuwa tayari kumvumilia mtu yoyote ambaye hatakuwa tayari kuchapa kazi kwa bidii ili kufikia maono na matarajio ya Wizara na wadau kwa ujumla.

Pia, alisema umoja na mshikamano ndiyo kitaisaidia taasisi hiyo kusonga mbele  na kuwataka watumishi wote kufanya kazi kama timu moja na kuongeza, "kwa umoja wetu utasaidia kufikia malengo tuliyojiwekea ya kufanya utafiti wa kina wa asilimia angalau 50 ifikapo mwaka 2030.

Akitoa maelezo ya awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini  Kheri Abdul Mahimbali aliwaahidi watumishi wa GST  kushughulikia changamoto mbalimbali za kiutumishi walizonazo ili kuboresha mazingira yao ya kufanya kazi.

Akitoa salamu za shukrani, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba aliishukuru Serikali kwa kuipa kipaumbele Taasisi ya GST na kuahidi kusimamia utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa ili kuongeza na kuboresha ufanisi wa taasisi.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals