[Latest Updates]: Katibu Mkuu Madini Atoa Miezi Miwili Mgodi Stamigold Kuanzisha Migodi Mipya

Tarehe : Nov. 22, 2020, 11:51 a.m.
left

Na Issa Mtuwa – Kagera Stamigold

Wizara ya Madini imetoa kipindi cha miezi miwili kwa Mgodi wa STAMIGOLD kuwasilisha Mpango wa kuanzisha Migodi Mipya.

Kauli hiyo kwa STAMIGOLD ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inafuatia kuonyesha uwezo wa kuanzisha na kuendesha migodi mipya.

Hayo yamesemwa Novemba 21, 2020 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila alipotembelea mgodi huo wa STAMIGOLD unaomilikiwa na Serikali kupitia STAMICO kwa lengo la kuona maendeleo ya uendeshaji wa shuguli za mgodi huo.

Baada ya kufika mgodini hapo, Meneja Mkuu wa Stamigold Mhandisi Kilasha Shamika alitoa taarifa ya uendeshaji   wa mgodi  pamoja na changamoto zinazojitokeza wakati  wa uendeshaji wa mgodi.

“Leo ninatoa agizo ndani ya miezi miwilikuanzia Desemba na Januari 2021  mwishoninataka nipatiwe taarifa hiyo inayoonesha mpango wa kuanzisha Migodi Mipya,” alisisitiza Prof. Msanjila.

Baada ya kufika mgodini hapo, Meneja Mkuu wa STAMIGOLD Mhandisi Kilasha Shamika alitoa taarifa ya uendeshaji wa mgodi pamoja na changamoto zake zinazojitokeza wakati wa uendeshaji wa mgodi.

Mhandisi Shamika alimueleza Katibu Mkuu kuwa uendeshaji wa shuguli za mgodi zinaendelea vizuri  na hadi hivi sasa mgodi unajiendesha kwa fedha zake.

Ameongeza kuwa kutokana na uzalisha wanaoufanya, hawapati faida kubwa lakini kiasi hicho kinawapa nafasi ya kupunguza madeni ya zamani ambapo mgodi teyari umeshalipa shilingi bilioni kumi (Bil. 10) kati ya jumla bilioni 39 wanazodaiwa.

“Kutokana na uendeshaji wa mgodi, mgodi kwa sasa hauzalishi madeni mapya. Mgodi unatekeleza maagizo mbalimbali yaliyotolewa na viongozi katika utoaji wa motisha kwa wafanyakazi”, alisema Mhandisi Shamika.

Aliongeza kuwa katika kutekeleza kwa maagizo hayo, Mgodi umeanza kutowa mikataba ya miaka miwili miwili ambayo inawapa utulivu kazini. Pamoja na hilo, wafanyakazi wametafutiwa fursa ya kupata mkopo kutoka kwenye benki mbalimbali na uanzishwaji wa chama cha wafanyakazi.

Akizungumzia kuhusu changamoto Mhandisi Shamika alisema, suala la ukosefu wa umeme ni tatizo na kueleza kwamba . gharama za mafuta zimekuwa kubwa ambapo  kila mwezi hutumika bilioni 1.2, wakati endapo wengetumia umeme gharama yake ingekuwa Shilingi milioni 300 kwa mwezi na hivyo kuokoa kati ya shilingi milioni 700 au 800 kwa mwezi.  

Alisema changamoto nyingine ni mtaji kwa ajili ya kuanzia miradi mingene kama mradi wa Visusi.

Katika hatua nyingine, Prof. Msanjila alitoa pongezi kwa STAMIGOLD kwa kazi nzuri wanayoifanya mgodini hapo.

Aliongeza kwa kuanza kuendesha mgodi kwa gharama zao, kutengeneza faida japo ni kidogo, kulipa madeni ya zamani, kutoendelea kuzalisha madeni mapya na kutengeneza mazingira ya utulivu kwa wafanyakazi.

“Nimefurahi sanaa kwa haya yote mliyoyasema kwenye taarifa yenu. Nimefurahi ingawaje mna  changamoto kadhaa” alisema Prof. Msanjila.

Akizungumzia changamoto zilizosemwa Prof. Msanjila alikiri suala gharama za mafuta ni tatizo na kuahidi kulifuatilia suala hilo kwenye mamlaka zinazotakiwa kuleta umeme mgodini.

Kuhusu mtaji alisema, Mgodi una asset ni pamoja la lesseni za uchimbaji ambayo ni sehemu ya mtaji.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals